Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

Maisha ya Instagram ni Zaidi ya Maigizo..Watu Wanajua Kula Raha Asikwambie Mtu Jionee Mwenyewe

0
0
Instagram ni zaidi ya uionavyo, watu wanajua kula raha asikwambie Mtu jionee mwenyewe...maisha mazuri hadi unashawishika kutaka kujua zaidi wanafanya nini...ntajaribu kuwatafuta hawa watupe siri ya mafanikio yao.

 1. Vera Sidika anapenda clubs yaani mdada yeye ni full ku party. What I like from her she has a talent ni mchoraji balaa anaonekana msomi pia alisema karudi shule big up @queenveebossette naomba tuongee zaidi kuhusu vipaji vyako naamini watu watabaki vinywa wazi.. 

2. Starlisha huyu naye ni mrembo wa instagram yeye anapenda kula sehemu nzuri, kupiga picha akiendesha magari mazuri na selfie za kumwaga. Mungu ni mkubwa kapunguza mabifu, sikuhizi yeye ni mshauri na mhamasishaji wa masuala mbali mbali ya maendeleo, hii inampa heshima safi sana @chaggabarbie naomba nijue siri ya utulivu wako, inapendeza sana. 

3. Huddah kama hayuko airport, hotelini basi swimming pool @huddahthebosschick unapenda kuogelea we mtoto, umekaa kibiashara tu mara photo shoot, lebel yako ya mavazi iko hewan na mengine atleast unaonekana unafanya kazi. Hizo bikini ukiziweka sokoni utauza sana. Hongera 

4. Masogange, picha nyingi yuko kitandani, kama sio kitandani bafuni kama sio nje ya nyumba then anarudi kitandani anajipiga mapicha weee hadi analala. Hongera nawe @officialagnes Mungu kakupendelea sana. 

Kuna wengine humu nashindwa kuwaelezea kwakweli...sitaki kujua sana maisha binafsi ya mtu ila natamani kujifunza au tujifunze kupitia hao "mastaa" Hakuna asiyependa kupiga mapicha all the time kalala, anaogelea, kwenye mahoteli makubwa na maboti anaenjoy maisha kama mnaweza kupiga mapicha hayo jamani tuonesheni na kazi zenu nasi tutamani kufikia huko??..

-Mrekebishatabia

Uhaba wa Wanaume: Msichana Mrembo Aamua "Kujioa Yeye Mwenyewe" Baada ya Kukosa Mume.

0
0
Uvumilivu wa kusubiri mwanaume wa kuja kumpigia goti na kumuuliza ‘will you marry me?’, umemshinda mwanamke mmoja wa Uingereza, aliyeamua kuchukua uamuzi wa kujichumbia na kujioa mwenyewe!

Grace Gelder ambaye ni ‘mme na mke’ alijichumbia November, 2013 na baadae kujioa March, 2014 na kuamua kufanya sherehe ya harusi yake iliyohudhuriwa na wageni 50.



Na ule wakati wa ile hatua ya ‘you may now kiss the bride’ ulipowadia, Grace alijibusu kwenye kioo.
Mwanamke huyo alisema baada ya kuwa single kwa miaka 6 aliamua ku-fall in love na ‘yeye mwenyewe’ baada ya kuona hapati mtu wa kumpenda.

Mwanamke huyo alisema kuwa pia wimbo wa Björk song Isobel ambao una mstari unaosema ‘My name’s Isobel, married to myself’, nao ulimuhamasisha kutimiza azimio lake.

1.Sasa mie nashangaa, hivi wanaume wa kuoa wameisha ulimwengu huu??? 
2.Je, ndio kusema wanaume domo zege ndo wanazid ongezeka duniani kila kuchao?
3.Je, ndio kusema mabinti wa kileo ndo wanazidi kuchuja /kukosa mvuto wa kuolewa?
4.Je, ni kitu gani mabinti warembo wanakosea mpaka kufikia hatua hii ya kujioa mwenyewe?

Ukitaka kuoa Sinza, Magomeni na Kinondoni Sio Sehemu Nzuri za Kuchagua Mchumba

0
0
Kuna wakati wakina dada wengi wanapata shida kuolewa kutokana na maeneo wanayotoka, utafiti nilioufanya maeneo niliyoyataja ni nadra sana kupata mke bora ambaye hajashawishika, kuna kipindi ndogo wangu alitaka mchumba, alihangaika sana kupata mwenza kwani wanawake wengi wenye mvuto hukaa maeneo hatarishi ambayo ni Sinza, Magomeni, na Kinondoni, kuna siku tulipata mchumba maeneo ya kinondoni shamba.

Tunaanza kuchumbia tu tulipewa orodha ya wanawake hatari sana naye akiwemo. 

Kwa ufupi wakazi wa Kinondoni shamba wengi wanajuana kwa majina na tabia, kwa kuwa wasichana wengi wamesoma Oysterbay, Mbuyuni, Sekondari kisutu, Kambangwa , Kinondoni musilim.

Hivyo kitabia karibu wanafanana, ukienda magomeni vile vile, tumeamia Bunju tu tukapata mchumba aliyetulia.

Sehemu za wake waliotulia ni Mwenge, Kijitonyama, Kimara, Mbezi juu, mbezi chini , unajua ni kwa nini? wengi wanaishi kwao..Unakubaliana na Mimi Au Unakataa?

Mkapa, Karume Wakacha Uzinduzi wa Katiba

0
0
Japokuwa jana niliangalia kwa muda mfupi Mchakato wa makabidhiano ya katiba ya CCM iliyooandaliwa na Sitta, Chenge,wabunge wengi wa CCM (ukiwaacha Lugola na Filikunjombe walioiasi) na mawakala wao, nilishtushwa kutowaona Mabalozi wa nchi wafadhili wa serikali ya CCM, wajumbe wote wa Tume ya Katiba na Maraisi Wastaafu Mh Benjamin Mkapa na Aman Abeid Karume. Je, tatizo ni mimi sikuwaona au ni kweli hawakuwepo? Na kama ni kweli hawakuwepo;

Je, ndo tuamini kuwa watu wote hawa muhimu wamesusia katiba ya CCM?

Je, huu siyo uthibithisho wa taarifa kuwa mabalozi hawa walimwambia JK haiafiki katiba hiyo? 

Je, hii haimaanishi kuwa katiba ya fisadi Chenge na mbabaishaji Samwel Sitta inapingwa vikali hata ndani ya ccm yenyewe? 
Ninatafakari tu kwa sauti wala sina ugomvi na mtu ye yote. 

Nawasilisha, 
By Aweda 

Lady Jay Dee na Mwanamuziki Ay Laivu Wanaswa

0
0
Stori: Andrew Carlos
KABANG! Mwanadada asiyechuja kwenye muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo   ‘Jide’ mwishoni mwa wiki iliyopita alibambwa ‘laivu’ kwa mara ya kwanza katika kipindi kirefu akiwa ‘very close’ na mwanamuziki mwenzake, Ambwene Yessaya ‘AY’ wakiteta jambo.

Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa High Spirit uliopo Jengo la IT Plaza, Posta jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa huduma mpya ya mtandao wa Airtel huku mastaa mbalimbali na waandishi wa habari wakijumuika pamoja kuanzia  saa 1:00 usiku.

Mapema kabla ya uzinduzi huo, AY aliyekuwa amepiga pamba nyeusi alikuwa wa kwanza kutinga ukumbini hapo akiwa ameongozana na Mtangazaji wa Show ya Mkasi kupitia EATV, Salama Jabir.Wakiwa wanapiga stori za hapa na pale, mara Jide naye alitinga ukumbini hapo ambapo jicho lake lilitua kwa AY na kusogea karibu kwenda kusalimiana naye.

Wakiwa katika maongezi Jide na AY, mshereheshaji aliyekuwa akiendesha uzinduzi huo, Ephraim Kibonde aliwataka wakae mbele ikiwa ni kusaidia kuendesha shughuli ya ufunguzi wa huduma hiyo kama majaji.

Katika uzinduzi huo, waandishi na wahudhuriaji walikuwa wakishindana kuimba na kupewa zawadi kama head phones, simu aina ya Samsung Galaxy III pamoja na spika ndogo kutoka kampuni kubwa ya kutengeneza bidhaa za muziki iitwayo Beats.

Jide alionekana kukubali wito huo wa kukaa na AY ambapo aliamua kuwatema wenzake aliokuwa ameongozana nao hapo ukumbini na kwenda kukaa mbele na AY, vivyo hivyo kwa AY naye aliwatema akina Salama na mshikaji wake na kwenda mbele

Katika hali nyingine ya kuduwaza, Jide akiwa na AY huku wakionekana wako ‘dipu’ kwa mazungumzo kabla ya kuanza kuwajaji waimbaji, alionekana kukolea na kinywaji alichokuwa anakunywa bila kutumia glasi (kupiga tarumbeta) mwanzo mwisho.

Mara kwa mara wawili hao walikuwa bize wakiteta kwa sauti ya chini kwa takribani nusu saa
GPL

Udaku:Johari na Chuchu Hans Nusura Wazichape Tena Laivu Laivu

0
0
Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema
Mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans  ambao wamekuwa katika bifu kwa muda mrefu kutokana na uhusiano wa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’, hivi karibuni nusu wazichape kwa mara nyingine baada ya kurushiana matusi mazito ya nguoni.

Tukio  hilo lilijiri juzikati katika hoteli moja iliyopo Sinza jijini Dar.
Chanzo cha uhakika kilichokuwa eneo la tukio kinavujisha kwamba, Ray alifika katika hoteli hiyo akiwa katika teksi na aliandamana na Chuchu.

Inadaiwa Ray alifika hotelini hapo kwa ajili ya kuonana na mkurugenzi mwenza wa kampuni yao ya RJ, Johari, ambaye kwa wakati huo alikuwa akisimamia kambi ya projekti yao mpya.

Baada ya Ray kushuka kwenye teksi na kuingia ndani ya hoteli hiyo huku Chuchu naye akishuka kwenye na kusimama nje akimwangalia mwandani wake anavyomsogelea Johari ambaye siku za nyuma alikuwa ndiye mwandani wake.

Kitendo cha Chuchu kutokeza kuonesha alikuwa ameandamana na mkali huyo wa filamu kilimchukiza Johari ambaye kwa sauti iliyosikika vyema, alimuuliza Ray kwa nini alikwenda akiwa ameongozana na ‘malaya’ wake.

“Matusi yale yalimkera sana Chuchu, naye aliamua kumrudishia hali iliyosababisha kutokea kwa tafrani kubwa kwani watu walianza kujazana na kuwazuia wasichapane,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya habari hii kutua mezani, mapaparazi wetu waliingia kazini ili kuujua ukweli, mtu wa kwanza kuzungumza naye ni Johari ambaye siku za nyuma aliwahi kuzichapa na mpinzani wake huyo wakati akilitetea penzi lake lililokuwa likiyumba.

Johari alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mwigizaji huyo alikwenda kambini kwake kufanya fujo ambazo hata hivyo alishindwa kufafanua.

Kwa upande wake, Chuchu alipoulizwa alisema: “Nimemvumilia sana Johari, amekuwa akinitukana kila kukicha nanyamaza, sasa nimechoka na kibaya zaidi siku hiyo alinitukania mama yangu, nimekuwa nikimvumilia kwa sababu alikuwa akinitukana mimi, sasa kumuingiza mama kwenye ugomvi wetu siwezi kumvumilia kamwe,” alisema Chuchu.
GPL

Wema Akacha Kumpa Zawadi Diamond, Wengi Wasema Ameshindwa Kujibu Mapigo ya Murano

0
0
Na Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu ameshindwa kujibu mapigo ya mwandani wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kutompa zawadi yoyote katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar.

Kutokana na msanii Diamond kumpa zawadi ya gari aina ya Nisani Morano mwandani wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa japo hakuwepo na kumuachia mama yake amkabidhi, mashabiki wengi walikuwa na kiu ya kutaka kujua ni kipi ambacho Wema angemzawadia mpenzi wake katika siku hiyo ili kudhihirisha upendo wake ikiwemo kwa mashabiki kama alivyofanya Diamond.

Mpaka shughuli inaisha watu mbalimbali walijitokeza kutoa zawadi zao huku wengine wakimmwagia noti pamoja na menejimenti yake kumzawadia gari aina ya BMW X6 lakini mwanadada huyo alishindwa kuonyesha makeke yake mpaka mwisho wa shughuli na kubaki akijilaumu;

“Hee halafu sijui kwa nini mpaka shughuli imeisha eti sijatoka kumpa zawadi baby wangu, sasa mbona hakuna aliyenikumbusha?” alisema Wema mwisho wa shughuli hiyo.

Kajala yamkuta Baada ya Kuweka picha simu Ambayo Bado Haijatoka sokoni Akidai Anayo

0
0
Kupitia mtandao maarufu wa picha wa kijamii, mwanadada Kajala amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuweka picha ya simu aina ya samsung galaxy note 4 kwenye account yake kuwa anamiliki simu hiyo ilihali simu yenyewe ikiwa bado hata haijaanzwa kuuzwa sehemu yoyote duniani. Kupitia picha hiyo kajala aliambulia maneno kadhaa ya kashfa toka kwa watu mbalimbali wengi wao wakimtaka aache maisha ya kuigiza.



Baadhi ya maoni hayo ni:-


"Hahahaha watu ndo wanatoa pre order october 16 ndo ina launched we umeitoa wap wakat bado haijaanzwa kuuzwa!dah!kwel sasa naanza kumin maisha yako ni ya kuigiza nakufata mkumbo mumy...pole"

"Duh ... Simu aijatoka hiyo Pre Order imeanza USA & UK tarehe 19/09 lkn retail stores wanaanza kuuza tarehe 17/10 , hiyo pre order kwa watu ambao awataki kumiss ikitoka wanalipia kabisa ikitoka unaenda kuchukua , sasa hiyo umenunua wapi mwenzetu..."

"KAJALA ACHA UONGO HII CM LABDA MCHINA ORIGINAL HAIJATOKA MPKA KWA ORDER LOO MWANAMKE MZIMA MPKA LEO UNARINGISHIA CM PAULA NAE AFANYE NINI"

Wewe unaonaje kuhusu jambo hili la mastaa nchini kuishi maisha ya kuigiza kwa ajili ya kuonekana wapo juu kwa mashabiki wao?


Nimejaribu Ku Google nikapata haya:
"Oct. 17 2014 is shaping up to be a very important day for Samsung, especially in light of its disappointing earnings call. The company will release its next-generation Galaxy Note 4 phablet across the globe and the device is the first in Samsung's successful Galaxy Note smartphone lineup to take on Apple's first entry in the category with its 5.5-inch iPhone 6 Plus"

Kama Haya Ninayosikia Ni Kweli Basi Wema Sepetu Atavunja Rekodi Tanzania

0
0
Kumekuwa na tetesi kuhusu muigizaji na mwanamitindo wema sepetu, kutaka kufunga ndoa na mwanamuziki nguli wa bongo fleva diamond, kwa mujibu wa mama yake wema amefunguka na kusema kama diamond atataka kumwoa mwanawe itamghalimu kutoa tsh milion100 kama mahali ya mwanawe uyo, kama alivyohojiwa na blog moja hapa dar,wachunguzi wa mambo ya ndoa tunaona kama wema sepetu atatolewa pesa hizo na diamond kama mahali basi atavunja rekodi kuwa mwanamke pekee tanzania kuolewa kwa pesa nyingi ,lakini we ma mwenyewe amedai yuko tayali kuolewa na diamond hata bure

Picha za Mtangazaji Gadner Akiwa Katika Mapozi Tata na Mrembo Coco Beach

0
0

LICHA ya kutothibitishwa juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa ndoa yake na mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ amenaswa na kabinti akiwa kwenye pozi tata za kimahaba hivyo baadhi ya watu kuhoji anasaliti ndoa?

Tukio hilo lililojaa viulizo kibao bila majibu  lilijiri Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar kulipokuwa tamasha la wazi la kuibua vipaji vya wasaniii mbalimbali.

Awali, vijana mbalimbali walipanda katika onesho hilo na kuonesha vipaji huku binti huyo jina halikupatikana mara moja, alionekana na rafiki yake ambapo wote walikuwa ni washiriki katika onesho hilo.
~Global Publishers

Msanii Irene Uwoya Ajitokeza na Kuongelea Mahusiano Yake ya Kimapenzi na Msanii Msami

0
0
~By Rosary Robert-Udakuspecially
Hatimae Mwigizaji wa Bongo Movies Mrembo Irene Uwoya Amejitokeza na Kuongelea Mahusiano yake na Msanii Msami wa Soundtrack .

Irene Uwoya Amesema kuwa Hana Mahusiano yoyote ya Kimapenzi na Msami , Ameongeza kusema kuwa kwa wale mliosikia Tetesi ya Mimi kuwa Penzini na Msami basi ilikuwa si kweli bali tulikuwa tunacheza Movie iitwayo "Kisoda" Ambayo itatoka Hivi Karibuni.

Wolper Amlipua Pedeshee Mkongo 'Kwangu Huyo Mkongo Siyo Hadhi Yangu, ni Mshamba na Limbukeni

0
0
~Stori: Erick Evarist
MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu na kumwambia aache kumfuatafuata

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkongo huyo ambaye anajitapa kuwa ameshatembea na baadhi ya mastaa Bongo akiwemo Wolper, alikaririwa katika gazeti hilihili akidai ametembea na Wolper kisha kumwaga na sasa anammendea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema anamshangaa mwanaume huyo amekuwa akimfuatafuata na kumzungumzia katika vyombo vya habari wakati hana hadhi ya kuwa na mtu kama yeye

Kwangu mimi huyo mwanaume siyo hadhi yangu, ni mshamba, limbukeni asiyeweza kuniweka mjini…kifupi nimwambie akome kunizungumzia mimi siyo taipu yake, atafute wa saizi yake,” alisema Wolper na kuongeza:

Nilikutana naye Nairobi aliposema ana shida ya kikazi ndiyo akaanza kuleta mambo ya kunitongoza, nilipomfuatilia nikaona si mtu mzuri, hazimo kidogo. Huwezi kuwa mwanaume ambaye unaropokaropoka hovyo, mimi nina mtu wangu namuheshimu, akome kunizungumzia.

January Makamba 'Ili Tanzania Ipige Hatua Kimaendeleo Inahitaji Kiongozi Anayefanya Maamuzi Kidikteta'

0
0
Dar es Salaam. Iko dhana kuwa ili Tanzania ipige hatua kimaendeleo inahitaji kiongozi anayethubutu kufanya uamuzi mgumu hasa kuwawajibisha viongozi wabadhirifu na wazembe, lakini Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba amekwenda mbali zaidi; anasema dawa ni kufanya uamuzi wa kidikteta.

Makamba alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumamosi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, ametoa kauli hiyo wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi huo huku tayari watu mbalimbali, hasa kutoka chama tawala cha CCM wakiwa wameshaanza kujinadi.

“Moja ya vitu vitakavyozuia rushwa ni adhabu kali ambayo itaonekana. Kwa nini madikteta wanawaua watu hadharani? Wanachojaribu kukionyesha ni kwamba kama siku moja mtu akijaribu kuwapindua atapelekwa uwanjani na kupigwa risasi hadharani. Lengo ni kuwatia watu hofu,” alisema.

Alisema, “Moja ya namna ya kupambana na rushwa ni kuwatia watu hofu, kwamba ukikamatwa yatakayokukuta ni kama yanayowakuta wenzako.”

Alisema ili kupambana na rushwa ni lazima kuwekwe mbinu za kivita na kwamba kama hilo lisipofanyika ni sawa na kupoteza muda.

“Serikali itakuwa inakusanya mapato na kupanga mambo yake, lakini asilimia 50 ya mambo hayo yanarudi mikononi mwa watu,” alisema.

Makamba alisema mmomonyoko wa maadili ni moja ya sababu inayofanya nchi ichelewe kupata maendeleo.

“Kuna wizi na ubadhilifu mkubwa siyo tu kwa viongozi wa kisiasa, hasa kwa watendaji na watumishi wa kada za kati na chini. Watu wanawatizama wabunge na waziri pekee wakati wapo wahasibu wa wizara na halmashauri,” alisema.

Kuwa Makini na Matapeli, Ona huyu Anavyotaka Kujipatia Hela ya Bure Kwa Kigezo cha Kumtafutia Kazi

0
0
Kale kautapeli ka Kutumia Watu message na kuahidi kukutafutia Kazi kwa malipo kidogo kameanza Tena Safari hii wameamia Kwenye Whats app ..Ona hii Message Katumiwa Jamaa yangu Hapa ..Jisomee Hapo Kwenye Picha Juu....Wandugu Tuwe Makini na Message Kama Hizo ..Si za kweli ukutuma tu Hela Imekula Kwako...Akili ki Mkichwa

Kivuli Chamuumbua Mdada aliyefanyia Photoshop Picha ili Awe na Mahispi Makubwa

0
0
Mbio za Kuwa na makalio Makubwa na Mahips kwa wadada siku hizi zimeshika kasi kubwa kiasi wengine wakipiga picha basi lazima waongeze makalio yao ama mahipsi kwa kutumia photoshop kisha kuzipost kwenye mitandao kama instagram na facebook ili kuvutia mashabiki wao.. Hili tumeliona hasa kwa wadada maarufu hapa bongo...Ona huyo hapo juu alichofanya , kivuli chake kinamuonesha ni mwembaba sana , pia kasahau kumtengeneza na huyo mtoto kwa pembeni mpaka miguu yake imepinda kutokana na ukubwa wa hips Lol,,,.
~Regina Iwole -Udaku team

Lemutuz Atangaza Ajira ,HouseGirl na Personal Assinstant ..Changamkia Fursa

0
0
Mzee Mzima William Malecella a.k.a Mzee wa Bebies Hapa Mjini Ametangaza Ajira ..Jisomee Mwenyewe na Kama Upo Intrested Basi Changamkia fursaaa,

BIG BROTHER AFRICA: Mshiriki wa Kiume (Idris) Toka Tanzania Anakera

0
0
Kwa wale ambao wamekuwa wafwatiliaji wa BBA 2014 mtakubaliana na mimi kwamba kijana wetu toka Arusha na anayeiwakilisha Tanzania ndani ya jumba hilo ANABOA. Kijana kawa mzururaji tu na kukaa na wadada muda wote. Siyo mbunifu wa kitu chochote kama washiriki wenzake ambao wameonekana wakionesha juhudi binafsi na vipaji mbalimbali. 

Binafsi nimevunjika Moyo kumpigia kura. Hajanishawishi maana sipigi hura kwa kuangalia utanzania.Hapana. Napiga kura nikizingatia ubunifu na juhudi binafsi. 

Je wewe unamuoengeleaje Idris?! Lavida anafanya vizuri mpaka sasa. Aibu kwa Idris!

Mwanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Dar (TIA) Ajichoma Kisu Baada ya Kusalitiwa na Boyfriend

0
0
Mwanafunzi wa chuo cha uhasibu dar (TIA) ajichoma kisu baada ya kusalitiwa na boyfriend wake...nyie wanaume kuwenu na roho ya huruma mnapendwa lkn hampendeki had ajiue hivi ndo uamini??...sio sirii niliwah fikia this stage lkn saiv hata chozi langu hutoliona"
~Mrekebisha Tabia


'Sina Uhusiano Wa Kimapenzi Na Master Jay'– Shaa

0
0
Shaa ambaye ni mwimbaji maarufu wa vibao vya Sugua Gaga na Subira  amekana kuwa na uhusuiano na producer maarufu wa muziki wa kizazi kipya Master J.

Akizungumza na jarida moja linalotoka kila mwezi Shaa amesema kuwa ameshangazwa na media kuandika ni wapenzi wakati yeye na master Jay wapo kikazi zaidi.

Hata hivyo wakati Shaa akiyasema hayo inadaiwa tayari familia ya Master J inamtambua kama mkwe wao na ameshatambulishwa.

TCRA Yaipiga Faini ya Milioni 1 Kituo cha Redio cha Times Fm Radio kwa kukiuka Maadili

0
0
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo kali kwa kituo cha Redio cha Times Fm, pamoja na faini ya kulipa kiasi cha Sh milioni 1, kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na mamlaka hiyo.

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margareth Munyagi, alisema ‘ Times Fm’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kukiuka taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo, kwa kutangaza hewani maneno yanayokiuka maadili ya utangazaji.

Munyagi alisema kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua tatu’ kilichorushwa saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichorushwa mchana wa Agosti 29 mwaka huu, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono bila kuzingatia muda huo ambao watoto wengi wanaweza kusikiliza

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo zilikuwa zikitangazwa, si muda muafaka kwa kuwa vipindi hivyo pia vingewezwa kusikilizwa na watoto na kwamba muda wa dondoo kama hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao.

Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri.

Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live




Latest Images