Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

Lukuvi Apiga ‘stop’ Nyumba Kuwekewa X

0
0

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amepiga marufuku uwekaji wa alama ya ‘X’ kwenye makazi ya wananchi waliojenga katika maeneo ambayo hayajarasimishwa kote nchini. 

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wadau wa ardhi waliokutana kujadili mpango mji wa miaka 20 wa Jiji la Dar es Salaam. 

Alisisitiza kuwa hakuna mwananchi atakayevunjiwa nyumba yake kwa sababu amejenga katika eneo ambalo halijarasimishwa, kwa sababu Serikali imewapa fursa ya kurasimisha maeneo hayo. 

Pia alizipiga marufuku kampuni zinazojihusisha na urasimishaji wa maeneo kuwachangisha fedha wananchi kutokana na kubaini kuwapo kwa kasoro kadhaa wakati wa zoezi hilo maeneo ya jijini Dar es Salaam. 

“Zoezi hili tulilianza tukaona lina kasoro, Dar es Salaam kuna watu walianza kutoza wananchi Sh 500,000 hadi Sh 400,000 ili kupima kiwanja kimoja cha maskini aliyejenga kwenye eneo lisilo rasmi. 

“Lakini baada ya kuchunguza nimegundua gharama halisi hazizidi Sh 250,000, kwa hiyo nimetoa agizo kwamba katika urasmishaji wowote hapa Tanzania, mwananchi asichangie zaidi ya Sh 250,000 ili kupimiwa kiwanja chake hiyo ni gharama ya juu. 

“Kampuni hizi zishindane kwa sababu tenda zitatangazwa na wilaya ili kila mtu anayetaka kupata kazi lazima atoe bei isiyozidi Sh 250,000 na iwe marufuku kwa kampuni kuchangisha fedha za wananchi katika sehemu ambayo inarasimishwa. 

“Dar es Salaam yako makampuni matatu yamechukua fedha, wananchi wamechangisha kwenye akaunti zao na wametoroka hawakufanya kazi, hawa tunawakamata. 

Alisema wakati wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo mbalimbali wananchi wenyewe watafungua akaunti zao za mitaa ambazo watazisimamia. 

Aliwaonya viongozi wa mitaa kujihusisha na fedha hizo na kwamba, malipo yatafanyika baada ya kazi hiyo kuthibitishwa na maofisa wa wilaya. 

Alisema gharama zitakazotumika kurasimisha zitakapokubaliwa ndipo wananchi watatoa fedha kuzilipa kampuni zitakazopewa kazi hiyo. 

“Najua watendaji na wapimaji wa Serikali ni wachache, ndiyo maana tumeweza kusajili kampuni nyingi za upimaji, kwa hiyo ni marufuku kwa kampuni binafsi kwenda kuomba kazi huko mitaani, lazima waanzie wilayani na isimamiwe na wilaya. Na iwe kiungo kati ya wale warasimishwaji na warasmishaji. 

“Narudia, ni marufuku kwa kampuni kuchukua fedha za wananchi na kuingiza kwenye akaunti zao. Lakini iwe tena ni marufuku kwa madiwani na wenyeviti wa mitaa kwa sababu baadhi yao wamekuwa wanachukua fedha kwa makampuni wakidanganya kuwa wao ndio wanatoa kazi za urasimishaji na upimaji. 

“Matokeo yake wanataka kuhongwa fedha na gharama hizo zinaingia kwenye gharama za watu wanaotaka kurasimishiwa. Kazi hazitatolewa na mwenyekiti wa mtaa wala diwani, zitatolewa wilayani kwa hiyo kampuni zisiende kwenye mitaa kuhonga madiwani au wenyeviti wa mitaa ili wapate kazi ya urasimishaji,” alisema. 

Waziri Lukuvi aliwataka watendaji wote wa ardhi wa wilaya zote nchini kuhakikisha wanasimamia zoezi la urasimishwaji na uhamasishaji na kwamba, migogoro yoyote itakayotokea watawajibika. 

“Isitokee mtu tena akaweka X kwenye nyumba za wananchi kama ilivyojitokeza Babati jana (juzi), katika maeneo ambayo watu wamejenga kiholela isipokuwa kwa watu waliojenga kwenye maeneo yaliyo kwenye hifadhi zilizopo kwa mujibu wa sheria, kama vile hifadhi ya barabara, hifadhi ya misitu iliyosajiliwa au iliyotangazwa kwenye gazeti la Serikali,” alisema Waziri Lukuvi. 

Waziri Lukuvi alizitaka wilaya zote kuhakikisha zinaainisha maeneo yote ambayo hayajarasimishwa ili kupanga utaratibu wa zoezi hilo ili wananchi wapate barabara, hati miliki za maeneo hayo kulingana na nyumba walizozijenga. 

“Barabara watazipata kwa kukubaliana wenyewe ni nani achangie ardhi yake ili barabara iweze kupita na kila mwananchi atachanga fedha kuhakikisha nyumba yake inapimwa kwa gharama zake,” alisema Lukuvi. 

Waislamu wenye msimamo mkali wahukumiwa kunyongwa

0
0

Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo Waislam 75 wenye msimamo mkali wakiwemo viongozi wa kikundi kilichopigwa marufuku cha Muslim Brotherhood hukumu inayoelezwa ni kubwa kutolewa mara moja kwa watu wengi nchini humo. 

Hata hivyo sheria nchini Misri zinataka Mufti Mkuu aridhie au kukataa kutekelezwa kwa hukumu hiyo na pia waliohukumiwa wana haki ya kukata riufaa. 

Waliotiwa hatiani ni miongoni mwa washitakiwa 713 waliofunguliwa mashitaka ya madi ya kuwauwa askari polisi  katika mapambano baina ya vikosi vya usalama na  wafuasi wa aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani mwaka 2013. 

Wanachana waandamizi wa Muslim Brotherhood, Mohamed El-Baltagui, Issa Aryan na Safwat Hijazi walikuwepo mahakamani wakati hukumu ikitolewa  wakati wengine 31  wamehukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.

Naibu Waziri Aweso amtumbua mhandisi wa maji Tanga

0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amelazimika kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji. 

Naibu Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa watendaji wa serikali. 

Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao. 

Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu hayo. 

“Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

0
0

TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo 

NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593 

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

Manara amkumbusha Kessy jinsi alivyoondoka Simba

0
0

July 27 2018 club ya Yanga ilitoa list ya wachezaji itakaowatumia msimu wa 2018/2019 hiyo ni baada ya siku moja dirisha la usajili la Ligi Kuu kufungwa, Yanga walitoa list hiyo na kutaja majina ya wachezaji wanne walioachana nao. 

Kati ya hao yupo Hassan Kessy ambaye awali iliripotiwa kuwa amepata timu nchini Zambia, ila kumbe Yanga na Hassan Kessy indaiwa kuwa hawakufikia makubaliano na hatimae wakaja kumpa taarifa za kutomsajili dakika za mwisho. 

Baada ya taarifa hizo kutoka unajua Kessy aliwahi kucheza Simba pia lakini inadaiwa hakuondoka vizuri hivyo afisa habari wa Simba SC Haji Manara akaandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram kuhusiana na malalamiko ya beki huyo. 

“Baadhi ya Binaadam hujisahau sana..huwa wanakosa utu na hisani…kila siku nasema hivi Vilabu vina mila zake na mifumo yake lazma uviheshimu..Dogo uliondoka kwetu kwa kejeli sana.ukaongea kila aina ya maudhi hukutosheka” 

“Ukashuka kwenye basi mkiwa na kombe pale Msimbazi ukatubeza mno..cc hatukukujibu..leo kiko wapi?mwenzio Ajibu kahama kimya kimya….Huyo ndio Mungu na hizi ndio Simba na Yanga!! 
But cc tunaendelea kukutakia kheri huko uendako,"

Wema Sepetu Amekaa Jirani Sana na Jela!

0
0

WEMA Sepetu alihukumiwa Ijumaa, ama kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini. Alikutwa na hatia ya kumiliki na kutumia dawa za kulevya.

Hukumu aliyopewa Wema yenye kumpa chaguo la kulipa faini ni nafuu kubwa kwake na hutakosea ukisema ni upendeleo mkubwa. Watu wengi wanakutwa na hatia ya mara moja wananyimwa kulipa faini na kuamriwa kwenda jela, ila yeye si mara ya kwanza bado kapewa fursa ya kulipa faini iliyo ndani ya uwezo wake.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu', aliachiwa kutoka jela Mei mwaka huu, alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano. Sugu alikutwa na hatia ya kuzungumza maneno yenye kumfedhehesha Rais. Katika hukumu yake hakupewa chaguo la faini ingawa lilikuwa kosa la kwanza.

Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, Januari mwaka jana alikutwa na hatia ya kufanya vurugu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, wakati wa uchaguzi wa baraza la madiwani. Lijualikali alihukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini. Hata hivyo, Lijualikali alishinda rufaa yake Mahakama Kuu.

Julai 23, 2008, fundi wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID', alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, kwa kosa la kumjeruhi mtu katika ugomvi wa klabu akiwa amelewa. TID hakupewa fursa ya kulipa faini japokuwa lilikuwa kosa lake la kwanza.

Wema aliwahi kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kesi ikiwa kugombana na kuharibu gari la aliyekuwa boyfriend wake, staa wa Bongo Movie, marehemu Steven Kanumba. Hata hivyo, kesi iliisha baada Kanumba kuomba kutoendelea na kesi.

Juni 9, 2011, Wema alihukumiwa kwenye Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni, kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini Sh40,000 kwa kosa la kumtusi mwanamuziki na prodyuza wa Sharobaro Records, Raheem Nanji 'Bob Junior'. Wema alilipa faini.

Hivyo, Wema ni mzoefu wa matukio ya jinai, ila ana bahati, kwani hajapewa adhabu ya jela moja kwa moja kama wengine wengi. Hakimu wa juzi (Ijumaa) angeamua kuzingatia rekodi zake za nyuma, angeweza kumnyima fursa ya rufaa. Ni ushauri kwake kujichunga. Tayari ana rekodi chafu na siku nyingine si rahisi kupewa dirisha la rufaa. Atatupwa jela. Si kila siku ni Ijumaa.

Ndimi Luqman Maloto

Kujiuzulu Kwa Waitara na Jokate Kupewa Ukuu wa Wilaya

0
0

Je, ni kweli Waitara ameondoka Chadema kisa alizuiwa kugombea uenyekiti? Hii ni mpya. Ila kama Chadema wanaweza kumharasi mwanachama wao anayetaka kugombea uenyekiti, huo ni utoto, ni utovu wa demokrasia.

Angeachwa tu agombee halafu tuone kama Chadema wangeweza kumwondoa Mbowe ili Waitara aongoze chama chao. Kweli Mbowe abadilishwe kwa Waitara? Kwa maoni yangu Waitara hatoshi hata uenyekiti wa Shilawadu, itawezekana vipi uenyekiti Chadema?

KUHUSU JOKATE

Tanzania hakuna sheria yenye kumdhibiti Rais kufanya uteuzi kwenye ofisi za umma. Hivyo, humteua amtakaye kwa pendezo lake. Nini Jokate, angetaka hata Gigy Money angeweza kupewa ukuu wa mkoa.

Pongezi kwa Jokate na wote walioteuliwa ukuu wa wilaya, mkoa na ukatibu wa wizara. Wajibu mkuu kwa walioteuliwa ni kufanya kazi kwa bidii, wakifuata sheria na utu ili kumlindia hadhi aliyewateua. Wakiboronga, wanaobeza uteuzi hivi sasa wataongezewa cha kuongea.

Tafadhalini; msiingie ofisini kwa sifa na mbwembwe. Uongozi ni kivuli cha mpito, maisha ni safari ndefu. Hakikisheni mnatunza pumzi ili ziwafae safarini baada ya vijiti mlivyopokea kupokelewa na wengine.

Ndimi Luqman MALOTO

Usajili Wamkera Mourinho

0
0

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameonesha kutofurahishwa na utendaji wa bodi pamoja na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo juu ya usajili uliofanywa kuelekea msimu mpya wa mashindano. 

Mourinho amefunguka kuwa angependa akamilishiwe usajili wa wachezaji wake anaowahitaji ili kuimarisha kikosi kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 10 mwaka huu kwa ligi kuu ya Uingereza (EPL) pekee. 

 “Inawezekana nikafanya usajili wa mchezaji mmoja na akawa ni huyo pekee, nilitoa listi ya wachezaji watano ninaowahitaji kwa klabu yangu na nasubiri kuona kama itawezekana“. Amesema Mourinho. 

Kocha huyo pia ameonesha kutofurahishwa na matokeo ya timu yake katika michezo ya kirafiki iliyocheza mpaka sasa, huku akilaumu kutokuwepo kwa wachezaji wake tegemeo ambao bado wapo likizo tangu michuano ya kombe la dunia ilipomalizika. 

Man United imefanya usajili wa wachezaji watatu pekee mpaka sasa ambao ni , Diogo Dalot kutoka Fc Porto, Fred aliyesajiliwa kutokea Shaktar na mlinda mlango Lee Grant. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Man United kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Liverpool usiku wa jana katika mfululizo wa michezo ya kirafiki ya, International Club Championship (ICC) inayoendelea barani Asia na Marekani. 

Matokeo ya michezo mingine ya kirafiki iliyochezwa usiku wa jana ni pamoja na Manchester City kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Bayern Munich, Barcelona ikiifunga Tottenham Hortspur kwa mikwaju ya penalti 5-3, Chelsea ikiifunga Inter Milan kwa penalti 5-4 huku Juventus ikishinda kwa penalti 4-2 dhidi ya Benfica.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, nasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

0
0

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:

GUMBA POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.

NTINJE:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0754741788, 0715741788, 0783741788

-DR MAGISE 

Uteuzi wa Jokate, Flaviana Matata asema ‘Inahuzunisha

0
0

Baada ya mwanamitindo na Miss Tanzania namba mbili 2006 Jokate Mwegelo kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani maneno yamekuwa mengi kuhusiana na nafasi hiyo na Jokate kama hataiweza au hatoiweza.

Wapo wanaokosoa na wapo wanaounga mkono uteuzi huo, baada ya uteuzi huo moja kati ya watu ambao wametoa mawazo yao ni Uncle Fafi na mwanamitindo wa Tanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani Flaviana Matata.

Zitto Afunguka Kuondoka Kwa Waitara Chadema na Kujiunga CCM

0
0

Baada ya Mbunge wa Ukonga (Chadema) Mwita Waitara kutangaza kurudi CCM, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe  ametoa neno kuhusu hatua hiyo. Anaripoti Regina Kelvin

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Zitto amemhoji Mwita kwa kuandika kuwa, amerudije CCM wakati viongozi waandamizi wa Chadema wana kesi mahakani  huku Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yuko hospitalini takribani mwaka kwa majeraha ya risasi kutokana na jaribio la kuuawa.

“Mbunge mwenzio yupo hospitali mwaka sasa kwa majeraha ya risasi kufuatia jaribio la kumwua. Viongozi wa Chama chako Karibu wote Ngazi ya Taifa wana kesi inayohatarisha kuwaweka jela. Watu wanauwawa na kupotea kila siku. Halafu unajiunga na hao wanaosababisha hayo? Kweli Mwita?” amehoji Zitto.

Waitara ametangaza uamuzi wa kurudi CCM mchana wa leo jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari baada ya kukaribishwa rasmi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Hunphrey Polepole.

Kuhusu Kufariki Kwa Mchezaji wa Yanga Kamusoko

0
0

Mapema leo katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa zilizodai kuwa kiungo msambuliaji wa klabu ya Yanga, mzimbabwe Thabani Kamusoko amefariki kutokana na ajali iliyohusisha gari aina ya Noah.

www.eatv.tv iliutafuta uongozi wa Yanga, ambapo kupitia Afisa habari wake Dismas Ten amekanusha taarifa na kudai kuwa ni za uzushi na tayari wamesharipoti kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake na kusema kuwa mchezaji wao yuko salama akiwa tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

“Taarifa hii ni uzushi, mtu huyu amekuwa akifanya hivi mara nyingi kuwazushia watu mbalimbali vifo, alifanya hivyo kwa baadhi ya wachezaji pia kama vile Mrisho Ngasa na Hassan Kessy na vingozi mbalimbali wa Serikali na leo ameandika hivi kwa Kamusoko”, amesema Ten.

Yanga itakuwa dimbani leo ikimenyana na Gor Mahia ya Kenya, katika mchezo wa wamarejeano kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam.

Mugabe agoma kumuunga mkono Rais kwenye uchaguzi mkuu

0
0

Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefanya mazungumzo ya kushtukiza na vyombo vya habari wakati ambapo taifa hilo linafanya uchaguzi siku ya Juatatu. 

Mugabe amesema hatamuunga mkono Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa, baada ya kushinikizwa kuondoka madarakani na ''chama nilichokuanzisha''. 

''Siwezi kuwapigia kura walionitesa,'' alisema .''Nitafanya uamuzi wangu miongoni mwa wagombea wengine 22''. 

Raia wa Zimbabwe watapiga kura Jumatatu, kura za kwanza tangu Mugabe alipoondolewa madarakani mwezi Novemba. 

Akizungumza akiwa nyumbani kwake, mjini Harare, siku ya Jumapili, Mugabe alisema kuwa ''alifukuzwa'' ikiwa ni sehemu ya mapinduzi ya kijeshi na kuwa aliamua kuondoka madarakani ''kuepuka mogoro''. 

Alisema sasa anamtakia kila la heri Kiongozi wa chama cha upinzani , MDC, Nelson Chamisa , katika kura za siku ya Jumatatu. 

''Anaonekana kufanya vizuri, na kama atachaguliwa namtakia kila la heri'', Alisema bwana Mugabe. 

Alipoulizwa na BBC kama atapenda kuona Bwana Chamisa akishika madaraka nchini Zimbabwe,Mugabe alieleza kuwa Chamisa ni mgombea pekee mwenye uwezo. 

Mugabe alisema:''Nina matumaini kuwa uamuzi wa kupiga kura kesho, utatamatisha utawala wa kijeshi na kuturejesha katika utawala wa kikatiba. 

''Acha kesho sauti za watu ziseme kuwa hatutakuwa na kipindi ambacho jeshi linakuwa na uwezo wa kumuweka mtu madarakani''. 

Mugabe pia alikana kuwa, alipokuwa Rais, alikuwa na mipango ya kukabidhi madaraka kwa mkewe Grace, akisema kuwa ilikuwa ''Upuuzi mtupu'', na kusema kuwa waziri wa zamani wa ulinzi Sydney Sekeramayi angechukua nafasi yake. 

Bwana Mugabe alisema,tangu aliposhinikizwa kuondoka madarakani mwaka jana,''Watu wa Zimbabwe hawajawa huru''. 

Zaidi ya watu milioni tano nchini humo wanajiandaa kwenda kupiga kura kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38 bila Mugabe kuwa madarakani. 

Kura za maoni juma lililopita MDC na Zanu-PF zilikaribiana kwa alama 11 kwa 3, huku 20% ya wapiga kura wakiwa hawajaamua.

Tetemeko laua watu 14, watalii wasimulia

0
0

Watu 14 wamepoteza maisha baada ya tetemeko kupiga eneo maarufu la utalii nchini Indonesia 

Tetemeko la ukubwa wa 6.4 lilitokea kisiwa la Lombok siku ya Jumapili 

Kisiwa hicho huwavutia watalii kutoka duniani kote kutokana na fukwe zake za kuvutia na maeneo ya kutembea, eneo hilo liko umbali wa kilometa 40 mashariki mwa Bali. 

Zaidi ya watu 160 wamejeruhiwa na maelfu ya makazi yameharibiwa, maafisa wameeleza. 

Mtalii raia wa Malaysia aliyekua akitembea kuelekea mlima Rinjani ni miongoni mwa waliopoteza maisha. 

Utafiti wa wataalamu wa Jiolojia nchini Marekani ulisema tetemeko lilipiga umbali wa kilometa 50 Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Mataram. 

Kisha likafuatiwa na matetemeko madogo zaidi ya 60, kubwa likirekodiwa kuwa na ukubwa wa 5.7. 

Sutopo Purwo Nugroho, Msemaji wa taasisi ya kukabiliana na majanga, amesema kuwa madhara mengi hujitokeza pale watu wanapoangukiwa na vifuri au mawe 

''Sasa tunachokitazama na kuwaokoa watu.Baadhi ya waliojeruhiwa bado wanapata matibabu kwenye vituo vya afya'', alieleza 

''Tetemeko lilikuwa na nguvu....watalii waliingiwa na hofu na kuanza kuondoka hotelini'',Lalu Muhammad Iqbal afisa kutoka wizara ya mambo ya nje aliiambia BBC. 

''Matetemeko yalikuwa na nguvu ''niliona mawimbi kwenye bwawa la kuogelea hotelini, tulikimbia nje ya hoteli''. 

''Dakika 30 baadae kulikuwa na tetemeko la kwanza.Watu waliingiwa na hofu kwa kuwa nyumba nyingi zimetengenezwa kwa mbao na bamboo, lakini watalii walikuwa na hofu zaidi. 

Watalii wa UK , Katherine and Alexis Bouvier, ambao walilkuwa kwenye fungate wameiambia BBC: ''tuliamshwa na tetemeko la ardhi majira ya saa sita usiku, ilikua inaogopesha''. 

maporomoko ya ardhi yamekata mfumo wa usambazaji maji na umeme katika baadhi ya nyumba, walieleza. 

''Tumepishana na magari kadhaa ya maji tulipokuwa tukielekea kusuni.Walituambia kuwa udongo wa saruji ulikuwa unadondoka kutoka sehemu ya dari na nyufa zikaanza kujitokeza kwenye majengo''. 

Hifadhi ya mlima Rinjani,imefungwa kutokana na maporomoko ya ardhi.

Habari Zilizopo Katika Magazewti ya Leo Jumatatu ya July 30

0
0

Habari Zilizopo Katika Magazewti ya Leo Jumatatu ya July 30

Kutana na Sharifu Seif Mohammed Mtaalam wa Tiba za Asili Tanzania

0
0

Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.



Sharifu seif Mohammed ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)



Sharifu seif Mohammed ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..) Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?

Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio? Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo.. Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.

Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?

Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim khatibu Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi.. Sharifu seif Mohammed Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..

Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..

ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..

MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..

Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti.. Kwa mawasiliano na ushauri zaidi



Mobile + 255 654 836970

WhatsApp +255 756 033670

Sumaye Alilia Demokrasia, Asema Chaguzi Ndogo Zinagharimu Pesa Nyingi za Maendeleo

0
0
Waziri  Mkuu mstaafu, Fedrick Sumaye, ameweka kile alichokieleza njama za kufuta upinzani nchini na kutahadharisha kuwa kufanya hivyo ni kuondoa sauti, uhuru wa watu na kwamba jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa taifa.

Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, alieleza hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa marudio wa udiwani Kata ya Makorola jijini Tanga.

Alisema kufuta upinzani ni kukataa demokrasia, hivyo kuwafanya watu wakose mahali pa kusemea kero zao, jambo alilolifananisha na bomu ambalo alidai linaweza kuleta madhara makubwa litakapo kuja kulipuka.

Aliwataka Watanzania watambue kuwa kufutika upinzani nchini ni kusababisha mapambano na kuondoa amani iliyopo kwa kuwa kushindana kwa vyama ndiyo nguzo ya amani.

“Watanzania msishabikie kuua upinzani maana yake mnashabikia kuua demokrasia na kuondoa sauti za watu, maendeleo na uhuru wa watu kuongea matatizo yao,” alisema Sumaye.

Alisema sababu ya kufanyika chaguzi ndogo kila mara ni dalili za kukosekana kwa demokrasia ya kweli na kwamba mabilioni ya fedha yanayotumika kwenye uchaguzi huo yangetumika kuondoa kero mbalimbali za kijamii.

Alieleza athari nyingine ya kuua upinzani ni kuzalisha vibaraka wengi na kudumaza maendeleo na kuvishauri vyombo vya dola kutoingilia masuala ya uchaguzi huo badala yake kazi hiyo iachwe kwenye ushindani wa vyama vya siasa.

Alimwombea kura mgombea wa kata hiyo anayeungwa mkono na Ukawa, Zainab Ashiraf, ambaye alisema kumchagua kuwa diwani pamoja na mambo mengine, ni kukataa ukandamizwaji wa demokrasia nchini.

Mkutano huo uliofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Wilaya ya Tanga, Richard Abel, ulihudhuriwa na vyama vinavyounda Ukawa ambao ni mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe na Jonatha Bahweje ambaye ni katibu wa Chadema Mkoa Tanga.

Wengine waliohudhuria na kupewa nafasi ya kuzungumza ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF, Amour Abal-hasan; Kamishna wa NCCR- Mageuzi, Ramadhan Manyeko na Mbunge Viti Maalum Chadema, Yosephar Komba.

Maskini: Mwanamke Mjamzito Aliwa na Mamba Akiogelea Ziwa Tanganyika

0
0

Mkazi  wa Kijiji cha Msamba, Kata ya Ninde, wilayani hapa Magreth Ndasi (18), ameuawa kwa kuliwa na mamba wakati akiogelea katika Ziwa Tanganyika.

Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu Joseph Ndasi, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita (Julai 27) majira ya saa 12:30 jioni baada ya Magreth aliyekuwa pia ni mjamzito kwenda kuoga katika ziwa hilo.

Alisema alipofika katika ziwa hilo aliingia ndani ya maji na kuanza kuoga ndipo alipovamiwa na mamba huyo ambaye alimkamata mguu na kuondoka naye kuelekea katika kina kirefu cha maji.

“Wakati alipokuwa anavutwa na mamba huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo walipojitokeza wananchi kutaka kumsaidia,” alisema.

Alisema baada ya mamba huyo kuona kundi la watu likiwa linaingia ndani ya maji, alimzamisha Magreth na kumkalia juu huku akifoka kuwatisha watu waliokwenda kumuokoa.

Aidha, wananchi walioshuhudia tukio hilo, walisema watu wenye silaha za jadi walipofika karibu na mamba huyo ili kumshambulia, alimwachia mwanamke huyo ambaye tayari alikuwa ameshakufa na kukimbia.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha kwenda kuogelea ziwani hasa nyakati za jioni.

Mbowe Atoa Msimamo Wake juu ya CHADEMA

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameagiza uongozi wa chama hicho kila wilaya kujenga ofisi ifikapo mwaka 2020 na kuondokana na adha ya kupanga.


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la ofisi ya Chama hicho Wilayani Tarime.

Mbowe amesema hayo leo Jumapili Julai 29, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Chadema wilayani Tarime mkoani Mara, ambapo amesisitiza kuwa mpango ujenzi wa ofisi hizo ulicheleweshwa na huu haukuwa muda wake.

“Mpango wa ujenzi wa hili jengo umecheleweshwa na huu haukuwa muda wake lakini nawapongeza  viongozi walioona njozi ya kuanzisha ujenzi huu ambao uko hatua ya renta ili kuunga mkono ujenzi huu Mimi naanza na Shilingi milioni mbili kila mbunge mkoani Mara achangie milioni moja," amesema Mbowe.

Mbowe  ametoa maagizo hayo wilayani humo ambapo amekwenda kwaajili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Turwa ambao umefanyika leo.

Rais Magufuli Awatumia Salamu Waislamu

0
0
Rais Dkt. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeir bin Ally kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Ulamaa katika Mkoa huo Sheikh Salum Hassani Fereji.

Salamu hizo za Dkt. Magufuli amezitoa leo Julai 30, 2018 na kusema kwamba anamkumbuka Sheikh Fereji kwa ucha Mungu wake, ukarimu, upendo kwa wananchi na namna alivyokuwa akiunga mkono juhudi za kudumisha amani na kusukuma mbele maendeleo.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha Sheikh Fereji, nilipokuwa nikienda Mwanza alikuwa miongoni mwa viongozi wa dini waliokuja kunipokea na amekuwa akifanya kazi ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi makubwa na nchi yake, pole sana Mufti wa Tanzania na nakuomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia yake, Waislamu wote wa Mkoa wa Mwanza na nchi nzima pamoja na wote walioguswa na msiba huu", amesema Rais Magufuli.

Sheikh Salum Hassani Fereji alifariki usiku wa kuamkia Julai 28, 2018 katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.

Maiti ya Sheikh Salum Hassani Fereji ilisaliwa Julai 29, 2018 katika msikiti wa Raudhwa uliopo mtaa wa Lumumba jijini Mwanza na kuzikwa siku hiyo hiyo ambapo viongozi wa dini akiwamo Mufti wa Tanzania Aboubakary Zubeir walihudhuria katika mazishi hayo pamoja na viongozi wa serikali.
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images