Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live

Mourinho Amkataa Martial Mbele ya Waandishi wa Habari

$
0
0
Mourinho amkataa Martial mbele ya waandishi wa habari
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho usiku wa kuamkia leo alifanya Press baada ya mchezo wao dhidi ya klabu yake ya zamani Real Madrid huko Miami nchini Marekani katika mfululizo wa michezo ya kirafiki inayoendelea kwa vilabu mbali mbali.



Manchester United imecheza tayari michezo mitano ya kirafiki, huku baadhi ya michezo hiyo ikicheza na klabu mbili za kimarekani ambazo ni Club America Phenex ambapo matokeo yalikuwa sare ya 1-1,mchezo mwingine ni baina ya San Jose matokeo yalikuwa suluhu ya bila kufungana na mchezo mwingine ulikuwa baina ya AC Milan ambapo matokeo yake yalikuwa sare ya 1-1 lakini baada ya kuingia kwenye penati manchester walishinda kwa penati 9-8.



Mchezo mwingine ulikuwa dhidi ya wapinzani wao wakubwa Liverpool na katika mchezo huo United alipoteza kwa kipigo cha goli 4-1,lakini mchezo wa jana usiku United walileta matumaini kwa mashabiki wao kwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Real Madrid.

Baada ya mchezo huo Mourinho aliongea mengi sana akianza kwa kuwasifia vijana wake kwani wamepata ushindi dhidi ya timu kubwa na Mourinho kudai kwamba bado kikosi chake hakijakamilika hivyo wachezaji wote wakijumuika na wenzao atakuwa na matumaini zaidi.

lakini alipoulizwa swali kuhusiana na mchezaji wake ambaye majuzi aliondoka kwenye kambi ya timu kwenda kwao Ufaransa kwa ajili ya kuungana na mke wake wakati anajifungua mtoto wao wapili Anthon Martial.

Mourinho alisema “Anthony Martial? Ni bora kwa [afisa wa vyombo vya habari] Karen Shotbolt kujibu kama anataka kujibu, “Mourinho alisema. Shotbolt kisha akajibu:” Tuko hapa kuzungumza kuhusu mchezo na sio kuhusu Martial”



Alipoulizwa na mwandishi mwingine endapo kama Martial ataungana na wenzake kwa maana ya kurudi katika mazoezi Manchester, Mourinho alisema: “Sijui.”



Wakati huo huo, Phil Jones, Marcus Rashford na Romelu Lukaku wameamua kusitisha likizo zao ili kuja kuungana nasi katika mafunzo kabla ya msimu kuanza, Mourinho alisema.

Wachezaji hao watatu, ambao wote waliotajwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia, watarudi siku tatu zijazo mapema tofauti na ilivyopangwa ili kujiweka tayari kwa mchezo wa kwanza wa United dhidi ya Leicester City, Agosti 10.


Makampuni Yanayotoa Huduma za Internet Yaagizwa Kufungia Tovuti za Picha Chafu ‘Pornography’ Ifikapo Mwezi Septemba 2018

$
0
0
Makampuni yanayotoa huduma za Internet yaagizwa kufungia tovuti za picha chafu ‘Pornography’ ifikapo mwezi Septemba 2018
Kwa kile kinachoonekana ni kulinda maadili ya wananchi nchini Uganda, Serikali ya nchi hiyo kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo (UCC) imeyatangazia makampuni yanayojihusisha na utoaji wa huduma ya Internet (Internet Service Providers- ISPs) na Mitandao ya simu kufungia tovuti zinazorusha picha chafu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCC, Godfrey Mutabazi amesema kuwa nchini Uganda kuna tovuti 17 ndani ya nchi hiyo ambazo zinatoa huduma hiyo huku tovuti 10 za kimataifa zikiwa zinaongoza kutazamwa ambapo amedai kuwa ameshaagiza makampuni yote tajwa yafungie mitandao hiyo kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

“Mamlaka yetu imebaini kuwa kuna tovuti nyingi nchini zinazoonesha picha chafu, hii ni kutokana na Kamati yetu ya Kudhibiti Masuala ya Ngono Mtandaoni. Kamati hiyo pia imebaini kuwa kuna tovuti za ngono ambazo zinaonesha mubashara kiyu ambacho kinavunja sheria moja moja ya nchi ya kifungu namba 13 cha sheria ya mwaka 2014 inayokataza masuala ya picha chafu.“amesema Robert Mutabazi kwenye mahojiano yake na UBC.

Sakata hilo la kubaini tovuti zinazoonesha picha chafu lilianza mwaka 2016 baada ya nchi hiyo kununua kifaa maalumu (Pornography-Detecting Machine) cha kubaini tovuti zinazorusha Ponografia nchini humo.

Mutabazi amesema kuwa makampuni ambayo yatakiuka agizo hilo hadi kufikia mwezi Septemba 2018 yatatozwa faini.

Hayo yote yanajiri ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu taifa hilo lipitishe sheria ya kutoza kodi kwa watumiaji wote wa mitandao ya kijamii.

Mastaa Watoa Ya Moyoni Kuhusu Uteuzi wa Joketi

$
0
0
Mastaa Watoa Ya Moyoni Kuhusu Joketi
BAADA ya wikiendi iliyopita nyota njema kumuwakia mwanamitindo na msanii maarufu nchini Jokate Mwegelo kutokana na Rais Dk John Pombe Magufuli kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, mastaa mbalimbali wameibuka na kutoa neno juu ya nafasi aliyopata mrembo huyo. Mastaa wengi wameonekana kufurahia uteuzi huo ambapo baadhi yao waliamua kutoa yao ya moyoni huku wakimpongeza kama yanavyosomeka hapa chini;

ILLUMINATA POSHI ‘DOTNATA’

Jokate nafasi aliyopewa ataiweza vizuri kwa sababu alishakuwa kiongozi wa vijana CCM namuombea Mungu amsaidie sana najua atakutana na changamoto nyingi kwa kuwa hakuzoea kuletewa kesi na watu wazima, lakini kwa sababu ni msomi na muelewa atafanya kazi vizuri sana ili aweze kumwakilisha vyema rais wetu aliyemteua.

Tunajua wanawake wengi kwa sasa tunaweza zaidi kwa kujiamini siyo mambo ya kizamani. Nawaomba Watanzania wamwangalie kwa jicho la sasa ya nyuma waache. Kila mtu ana rekodi ya maisha yake, hii ni bahati kubwa sana kwa binti mdogo kama huyu kuwa mkuu wa wilaya.

Mungu alishamchagua kuwa kiongozi. Kikubwa wanawake wote tumpongeze binti yetu na dada walio sawa naye kwa umri wamsapoti na wafuate nyayo zake. Hakuibuka tu kuwa kiongozi bali amesukwa kwanza na mkuu wa nchi akaona anafaa.

JIMMY MAFUFU

Ni baraka kwetu kama tasnia na haya ni maombi, sisi waigizaji watumishi wa Mungu tumekuwa tukimsihi Mungu kutuinulia wasanii miongoni mwetu watakaoingia katika nafasi za uongozi, kitu kizuri ni kwamba Jokate ni mtu makini hivyo hatutegemei aibu kutoka kwake.
Tokeo la picha la salma jabu
SALMA JABU ‘NISHA’

Ni kitu kizuri nampongeza Rais Magufuli na wasaidizi wake na Jokate Mwegelo pia, anastahili sana ukuu wa wilaya ana sifa zote na Mwenyezi Mungu amjaalie aje afike mbali zaidi.

FAIZA ALLY

Anastahili na nimefurahi sana nimependa maamuzi ya rais pia kama mwanamke najivunia sana kuona mwanamke mwenzangu mwenye cheo na madaraka ya juu.

TUNDA SEBASTIAN

Kwanza kabisa nampongeza sana ni hatua kubwa ambayo kila mwenye akili timamu lazima asikie wivu!

ISABELA MPANDA

Mimi nimefurahi sana pia kujiheshimu kwake kumemfanya rais amteue.

ZENA ABDALLAH ‘JIKE SHUPA’

Nimependa maana Jokate hana mambo ya mjini, mambo yake ni kimyakimya yaani kwa sasa huwezi kumjua mpenzi wake siyo kama sisi wakina Jike Shupa ukimpata mpenzi mpya dunia nzima itajua, nampongeza sana Jokate kwa kweli.
Tokeo la picha la dr cheni
MAHSEIN AWADH ‘DK. CHENI’

Nimefarijika sana tena sana Jokate kupata ukuu wa wilaya. Rais Magufuli ameamua kutupa nafasi vijana na hatutamuangusha.

ISABELA FRANCIS ‘VAI WA UKWELI’

Mungu ambariki Jokate na namshauri afanye kazi vizuri pia abadilike kidogo maana ameshakuwa kiongozi sasa siyo kama alivyokuwa zamani.

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’

Ni jambo jema, kwanza Jokate ni mtu ambaye amejishirikisha sana katika mambo ya kijamii, ukiachana na kuwa kijana machachari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pia amekuwa akijihusisha na mambo yanayohusu vijana, ni mbunifu pia hivyo ana haki ya kuwa kiongozi kwa sababu amezaliwa kama kiongozi kwani kuna vitu amevifanya ambavyo hakuna mtu mwingine amewahi kuvifanya, kifupi ni msichana anayejielewa, atakuwa ni mmoja kati ya viongozi bora kabisa naamini atafika mbali, nimefurahi sana.
Tokeo la picha la sauda mwilima
SAUDA MWILIMA

Kwa kweli ni jambo la kupongezwa sana kwa hatua hiyo maana ameonyesha mfano mzuri kwa vijana kwa juhudi zake za upambanaji wa kazi na kujitoa kwa jamii pia kujijengea heshima katika jamii.

MARY MAWIGI

Nampongeza sana Jokate, juhudi na malengo yake yamempa heshima ya kufika hapo alipo, namtakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yake pia tunamshukuru rais wetu kwa kuamini katika tasnia.

Mfuko wa Pensheni wa PSSSF Waanza Rasmi Leo

$
0
0
Mfuko wa Pensheni wa PSSSF Waanza Rasmi Leo
Tarehe 31 Januari, 2018 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).



Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inaunganisha Mifuko ya Pensheni minne ambayo ni Mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF na kuunda Mfuko mmoja kwa ajili ya Watumishi wa Umma unaojulikana kama Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma.



Mara baada ya kupitishwa na Bunge tarehe 8 Februari, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alitia saini Sheria hiyo na hivyo kuifanya kuwa sehemu ya Sheria za nchi.



Baada ya kukamilika kwa hatua hizo muhimu, hatua inayokuwa inasubiriwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF.



Kwa mujibu wa Sheria, Waziri mwenye dhamana ya Hifadhi ya Jamii ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza tarehe baada ya kuridhika kuwa maandalizi yote ya msingi yanayohusu utekelezaji wa Sheria hiyo yamekamilika.



Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha kuwa Serikali imekamikisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma( PSSSF) unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake.



Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF.



Hatua hii inamaana kwamba Mfuko wa PSSSF utaanza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 1 Agosti, 2018, hivyo kuanzia tarehe hiyo wafanyakazi wote watakaoajiriwa katika sekta ya umma watasajiliwa katika Mfuko wa PSSSF na wale watakaoajiriwa katika sekta binafsi watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF.



Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na Mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.



Vivyo hivyo, rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa itahamishiwa katika Mfuko mpya wa PSSSF.



Watumishi wote wa mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa Mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa Mfuko huu.

Kabla ya kufikia hatua ya kutangaza tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF, Serikali ilipaswa kuhakikisha kwamba imekamilisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji ili kuhakikisha kwamba huduma kwa wanachama haziathiri kwa namna yeyote ile.



Serikali kwa kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko imeandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu Sheria na Kanuni za PSSSF ili kuhakikisha kwamba wanachama na wadau wote wa Sekta wanakuwa na uelewa sahihi wa Sheria hizi na mabadiliko yaliyofanyika.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO*

Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Aliowateua......Asema Ilimlazimu Kukaa na Majina yao Miezi Minne Akiwachuja

$
0
0
Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Aliowateua......Asema Ilimlazimu Kukaa na Majina yao Miezi Minne Akiwachuja
Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni Mungu ndiye amewachagua.

“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.

“Tanzania ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa Rais.

“Hata Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.

“Wengine wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila (David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.

“Alipokuwa huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema.

Hii ndio perfomance ya Sanchez katika michezo ya kirafiki Marekani

$
0
0
Hii ndio perfomance ya Sanchez katika michezo ya kirafiki Marekani
Mchezaji wa Manchester United, Alexis Sanchez usiku wa jana alisaidia klabu yake kushinda mechi ya kirafiki jumla mabao 2 – 1 dhidi na Real Madrid huko Miami nchini Marekani.

Raia huyo wa Chile alisaidia klabu yake kushinda mchezo huo kwani aliifungia goli dakika ya 1`8 na kutoa assist kwa Hererra dakika ya 27 ingawa goli la Madrid lilipatikana kupitia Benzema dakika ya 45,hivyo hadi mwisho wa mchezo Mancester United 2-1 Madrid.

Sanchez ameonyesha kiwango kikubwa mno kwenye mchezo huo dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa barani Ulaya klabu ya Real Madrid baada ya kufunga bao la kwanza na lamapema.

Shangwe Zatanda Kumkaribisha Bembe DRC

$
0
0
Shangwe Zatanda Kumkaribisha Bembe DRC
Kiongozi wa upinzani nchini Kongo, Jean Pierre Bemba amerudi nyumbani leo, baada ya kukaa kwa takribani muongo mmoja akiwa kifungoni na nje ya nchi ya Kongo.

Bemba alifutiwa mashataka hivi karibuni na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, aidha ameonesha wazi nia yake ya kugombea Urais nchini Demokrasia ya Kongo. Alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2006 dhidi ya Rais wa sasa Joseph Kabila ambaye muda wake umeisha tangu mwaka 2016, jambo ambalo bado linaleta maswali mengi kama ataogombea tena.

Kurudi kwa Bemba kunaonekana kusisimua upya na kutikisa siasa za Demokrasia ya Kongo, chama tawala tayari wametoa tamko kuwa Bemba hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais nchini humo, kutokana na alikua mshitakiwa wa mahakama ya makosa ya jinai ICC.

Image caption
Mmoja wa wafuasi wa Jean Pierre Bemba
Vyama vimebakiwa na wiki moja ya kuwasilisha majina ya wagombea wao, na tayari chama cha Bemba kimeshamchagua kuwa Mgombea wao wa Urais, amesema kuwa atamuunga mkono mgombea yoyote kutoka upinzani.

Kwa upande wafuasi wa Rais kabila wanasema Bemba hatakiwi kugombea kwani anakiukuka Utaratibu wa katiba.

Kwa upande wa Kabila mwenyewe bado hajazungumza chochote juu ya kurudi kwa Bemba.

Makamu huyo wa Rais wa zamani amekua Ulaya kwa miaka 12 huku miaka 10 akiwa akitumikia kifungo kutokana na ukikukwaji wa haki za binaadamu ulifanywa na wafuasi wake katika nchi jirani Jamhuri ya Afrika ya kati, ambapo hivi karibuni alifutiwa mashtaka na ICC jambo lilomfanya aweze kurudi kwake nyumbani.

Jeshi la Polisi Lasema Mbwa Aliyedaiwa Kupotea Alikuwa Kwenye Mafunzo

$
0
0
Mbwa wa kazi maalum za Bandari ya Dar es Salaam anayedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, alikuwa kwenye mafunzo bwalo la Polisi.

 Hayo yameelezwa leo Agosti Mosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa katika mkutano na wanahabari. Amezungumza hayo huku ukumbini hapo kukiwa na mbwa wawili wa polisi, akiwamo anayedaiwa kutoweka.

Amesema kulikuwa na mkanganyiko na hakuna mbwa aliyepotea.

“Tunataka kuwaambia kuwa mbwa huyo alikuwa kwenye mafunzo ya bwalo la Polisi na mbwa aliyekuwa hayupo siyo hobi,” amesema Mwakalukwa na kuongeza:

“Mbwa wote wapo hakuna hata mmoja aliyetoweka huwa wanaenda kwenye kazi na kurudi.”

 Julai mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alimpa saa saba Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro kuhakikisha mbwa huyo anarudi bandarini baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Picha: Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Harusi ya Zabibu Kiba na Abdi Banda

$
0
0
Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Harusi ya Zabibu Kiba na Abdi Banda
MCHEZAJI wa timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na aliyewahi kuzichezea Simba SC ya Dar es Salaam  na Coastal Union ya Tanga, Abdi Banda, alfajiri ya leo Agosti 1, 2018 amefunga ndoa na Zabibu Kiba, ambaye ni dada wa mkali wa Bongo Fleva Ali Kiba kwenye msikiti wa Ahmad al maseeid uliopo Tabata jijini Dar es Salaam.


Mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ (kulia),  akiwa na Abdi Banda na mke wake Zabibu Kiba.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

$
0
0


TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo

NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

"Hata Wakisema Ninadanga Hainiharibii Kitu" Irene

$
0
0
Video queen irene amefunguka na kusema kuwa anashngaa sana watu wanamsema kuwa amekuwa akidanga na kutembea na wanaume tofauti ili kuendesha maisha yake.irene anasema kuwa pamoja na kwamba wanamsema anadanga lakini kwake haimuharibii kitu kwa sababu kwake ina faida.

Irene anaeonekana kama anamjibu mtu aliyempa dongo hilo la kudanga anasema kuwa kama wao wanaona kudanga ni kazi rahisi basi na wao waende wakadange ili wanufaike kama anavyopata yeye.

Hata wakisema kuwa mimi nina danga kwangu hainiharibii kitu, eeh so ninadanga okay so wats up.sijui wengine wanachukuliaje kudanga lakini mimi nina enjoy na ninapenda tu. na yeye kama anaona ni rahisi kudanga akadange.

Pretty Kindy "Nikimtaka Mwanaume Hawezi Kunikataa"

$
0
0

Mwanadada pretty kindy amefunguka na kusema kuwa yeye ni msichana mzuri sana kiasi kwamba hakuna hata mwanaume anayetaka kumfuata na akamkataa kutokana na uzuri wake.

Akiulizwa maneno yake kuhusu  kauli yake aliyowahi kuisema kuwa anampenda sana Diamond , Pretty kindy anasema kuwa kwa sasa hawezi kulizungumzia hilo kwa sababu watu wamekuwa wakimtafisri vibaya lakini kwa upande wake akimtaka mwanaume hawezi kumkataa.

mimi ni mwanamke na siwezi nikamkata mwanamke na akaniktaa hata siku moja, lakini maswala ya diamond siwezi kuyaongelea kwa sababu yalishaleta mkanganyiko sana, alafu mimi ni mwanamke mzuri sana sidhani kama ninaweza nikamkata mwanaume na akanikataa.

labda niwe simtaki au ninamjokes lakini kama ni serious hawezi kuktaa, alafu mimi nikiwa serious siweiz kwenda in public kwa sababu mapenzi sio matangazo.

Zari “Mimi Sio Level Zenu, Msiniringanishe na Vinuka Mkojo”

$
0
0

Baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amekuja juu na kumwaga povu zito siku ya jana na kuomba asilinganishwe na vinuka mkojo.

Povu hili la Zari limekuja siku chache baada ya kupishana Kauli na wasanii mbali mbali kutoka Bongo Movie ambao walitakiwa kwenda nchini South Africa kwa ajili ya birthday ya mtoto wa Diamond, Tiffah.

Zari aliwaambia wasanii kama Wema Sepetu, Aunty Ezekiel, Maimatha na kamati nzima ya Zamaradi kuwa hataki waende South Africa kwenye birthday ya Mtoto wake kwani watachafua nyumba yake.

Siku ya jana pia Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Zari aliwamwagia povu hili watu ambao hawakuwataja majina lakini hakutaka kulinganishwa nao.

Ati sijui A or B, mimi sio level zenu I worked hard for my name, Am not a social climber. Hatuuzi sura tu, tunapambana na  msiniringanishe na vinuka mkojo vwenu, mxiuuu.”.

Hakuna Anayeweza Kuninunua Kama Kununuliwa Ingekuwa Wakati wa Tegeta Escrow-- Kafulila

$
0
0
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila amekanusha uvumi wa madai ya baadhi ya wanasiasa wanaodai uteuzi aliofanya Rais John Magufuli kwa Wakuu wa wizara, Mikoa na Wilaya hivi karibuni ni wa kisiasa na sehemu ya malipo kwa kuwa amewapa nafasi waliotoka upinzani.

Kafulila amekanusha uvumi huo wakati akizungumza katika mahojiano maalum na www.eatv.tv, ambapo amesema taarifa za  wanasiasa wanaosema serikali ya CCM imekuwa ikinunua wanasiasa kutoka upinzani kwa ahadi ya kuwapa madaraka ikiwemo katibu tawala, ukuu wa mkoa na wilaya, hazina ukweli wowote na kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumnunua na kama nikununuliwa ingekuwa wakati wa sakata akaunti ya Tegeta Escrow.

Kafulila ameeleza kuwa hawezi kununuliwa kwa gharama yoyote kwani hakuna wakati watu waligawana fedha kama kwenye sakata la Tegeta Escrow, hivyo huo ndio ulikuwa muda wa yeye kununuliwa na sio sasa.

Amesema jambo kubwa lililomuondoa CHADEMA kwenda CCM ni kukubaliana na yale ambayo yanafanywa na Rais Dkt. John Magufuli katika utendaji wa serikali, usimamizi wa rasilimali, vita dhidi ya ufisadi na katika mambo makubwa ya kimkakati ya namna gani ya kuisogeza Tanzania mbele isiwe tu katika sura ya Afrika Mashariki.

Amesema " hayo ndio mambo makubwa ambayo nilikuwa nikiyapigia kilele ndani ya bunge na katika siasa ndiyo hata ambayo Mh.. rais anafanyanyia kazi kwa hiyo nisingeweza kuendelea kuwa mnafiki wa kupinga wakati yanayofanyika ni yale ambayo nilisema yafanyiwe kazi hilo ni jambo muhimu sana".

Akizungumzia hatma yake kwenye siasa baada ya kuteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa wa Songwe Kafulila amefafanua kuwa kila jambo lina nafasi yake na kamwe hawezi kuchanganya suala la utendaji na siasa.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya utumishi atatelekeza majukumu yake ndani ya sheria, hivyo jambo pekee ambalo watanzania wanatakiwa kutarajia ni utekelezaji wa kiwango cha juu kabisa wa maendeleo kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa uma ambayo pamoja na mambo mengine inamtaka mtumishi wa uma kufanya kazi kwa kutoa huduma bora, kutii serikali, bidii ya kazi, kufanya kazi bila upendeleo na kuheshimu sheria.

Ameongeza kuwa "Safari yangu katika siasa ni jambo ambalo siwezi kulijadili sasa kwa sasa mimi ni mtendaji, jambo pekee naweza nikalisema kwa hakika kabisa ni suala la utendaji, tunahitaji pia watu ambao wanajua namna gani ambavyo serikali inafanya kazi sio tu kwamba unakuwa mwanasiasa miaka yote tunahitaji pia kujua namna ya kufanya utendaji"

Kafulila amesema kuwa kwa miaka yote akiwa kwenye siasa amekuwa akikosoa, sasa ni wakati wake wa kutenda yale ambayo amekuwa akikosoa.

Aidha licha ya David Kafulila kushindwa kutetea kiti chake cha Ubunge katika jimbo la Kigoma kusini kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi lakini jina lake limebaki kwenye historia ya Tanzania kuwa miongoni mwa wabunge walioisaidia serikali kuibua ufisadi wa kutisha wa shilingi bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Vitisho Vyamfanya Meya Ilala Kupitia CUF Omary Kumbilamoto Kujiuzulu

$
0
0
Vitisho Vyamfanya Meya Ilala Kupitia CUF Omary Kumbilamoto  Kujiuzulu
Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto (CUF) amejiuzulu nyadhfa zake asubuhi hii huku akidai sababu kubwa ya yeye kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na migogoro iliyopo ndani ya chama chake.

Kumbilamoto ameeleza hayo wakati alipokua anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi Agosti mosi, 2018 na kusema sababu kubwa ya yeye kufanya hivyo, ni kutokana na kutishwa na viongozi wa chama hicho, pindi anapokuwa anaungana na viongozi wa serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

"Kuanzia leo najiuzulu nafasi yangu ya udiwani wa kata ya Vingunguti pamoja na ya unaibu Meya wa Ilala, hivyo sasa mimi ni mtu huru. Nitaelekea kufanya mambo yangu ya kilimo lakini hapo baadae nitawaambia wananchi wangu ni chama gani ambacho nitajiunga nacho", amesema Kumbilamoto.

Pamoja na hayo, Kumbilamoto ameendelea kwa kusema "nina mpongeza Rais Magufuli kwa kuweza kurudisha watumishi wa umma katika mstari unaohitajika, ambapo mambo hayo sisi tulikuwa wasafiri tulikuwa tunayaona kwa wenzetu lakini hivi sasa Rais Magufuli ameweza kuyarudisha na nchini kwetu".

Akizungumza na www.eatv.tv Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Ilala, Bakari Shingo amesema wamesikia taarifa za kujiuzulu diwani wao huku akisikitika juu ya madai yaliyomfanya kung'atuka ndani ya CUF.

"Siku zote migogoro ndani ya chama ni jambo la kawaida ila ninachoamini ameafuata upepo tu wa kisiasa. Mimi nasema waache waondoke na upinzani hautaweza kufa. Kila diwani anayetaka kuondoka na aondoke sisi tutaendelea kubaki kwenye msimamo wetu na taifa kiujumla", amesema Shingo.

Wakati vuguvugu la kisiasa likiwa linaendelea hasa katika upande wa upinzani kuhama vyama vyao na kuenda kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika ujenzi wa taifa, wachambuzi mbalimbali wa siasa, wamesema suala hilo ni jambo la kawaida kutokea kwa madai hiyo ni haki ya kila mtu kuchagua chaguo sahihi.

Baada ya Zito Kutakiwa Kujisalimisha Polisi ACT-Wazalendo Wamvaa Kangi Lugola

$
0
0
Baada ya Zito Kutakiwa Kujisalimisha Polisi ACT-Wazalendo Wamvaa Kangi Lugola
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kuendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa agizo lililotolewa na Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola halina nguvu kisheria.

Jana Lugola alimtaka Zitto kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi kwa kile kilichoelezwa alitoa maneno ya kichochezi wakati wa mkutano wa hadhara kati yake na Mbunge wa Kilwa Kusini(CUF), Seluiman Bungara 'bwege'.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho,Ado Shaibu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti Mosi 2018 wakati akizungumza na wanahabari.

Amesema wanasheria wa chama wamelipitia kwa undani tamko hilo la Lugola na kujiridhisha kuwa lina makosa na halina nguvu kisheria.

"Wanasheria wa chama wamejiridhisha pasipo shaka na kugundua kuwa Lugola amekurupuka kutoa tamko lile.Lugola katumia siasa kutoa tamko lile na siyo kufuata sheria.

“Zitto akiitwa kisheria ataenda kuripoti polisi na hatuna sababu ya kuogopa.Zitto ni kiongozi mbunge akiitikia wito huu wa Lugola atakuwa hajiheshimu, "amesema Shaibu.

Shaibu amesema hakuna kosa lolote ambalo Zitto amelitenda katika mkutano ule, lakini Lugola amekuwa na makeke katika kutoa matamko yake.

“Yaani tumetesti mitambo mara moja tu, pale Kilwa kwa kumpandisha jukwaani Zitto imekuwa nongwa watu wanalipuka? Hatuwezi kuvumilia hali hii,"amesema.

Watetezi Haki Za Binadamu Walaani Mnyeti Kumtupa Selo Wakili

$
0
0
Watetezi Haki Za Binadamu Walaani Mnyeti Kumtupa Selo Wakili
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umelaani kitendo cha kushikiliwa kwa Wakili Menrad D’Souza na wateja wake kwa amri ya Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti juzi Julai 30, mwaka huu.

Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema kitendo hicho ni ukandamizaji wa haki na uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti Mosi, Jijini Dar es Salaam Olengurumwa amesema kuwa hawakufurahishwa na kitendo hicho hivyo wanalaani kwa nguvu zote na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa katiba.

“Wakili huyo alifungiwa katika chumba kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa Manyara juzi, kutokana na madai ya kushinikiza wakili na wateja wake waweze kuwasiliana na wakurugenzi wa wateja hao ili wakubali kuongeza kiasi cha fidia kwa wakulima katika mgogoro wa mbegu kati yao na wateja wa wakili D’Souza.

“THRDC kama mwavuli wa watetezi wa haki za binadamu inatambua kuwa mawakili ni watetezi wa haki za binadamu na wanafanya kazi zao za utetezi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na nchi,” amesema.

Kutokana na hilo, ameshauri kwamba ikitokea kuna wakili viongozi anadhani amekiuka maadili ya kazi yake basi atoe taarifa kwa chama cha mawakili au mahakama.

Pia kwa mawakili amewasihi  kupitia vyama vyao wasimame kwa umoja na kulinda Uhuru wa kazi ya mawakili na utawala wa sheria hapa nchini.

Sambamba na hilo, Mratibu huyo amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuacha kutumia madaraka yao chini ya kifungu cha 15 na 17 cha sheria ya Tawala za Mkkoa ya mwaka 1996 kwa kutoa amri ya kuwakamata watu na kuwaweka vizuizini bila sababu za msingi za kisheria kwani vitendo hivyo vimekuwa vokijirudia mara kwa mara.

Yanga Yaomba Msahada kwa Wanachama Wake Kuchangia Timu

$
0
0
Yanga Yaomba Msahada kwa Wanachama Wake Kuchangia Timu
Baada ya hali kiuchumi kuwa ngumu ndani Yanga, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, ametangaza kuomba wanachama mashabiki wa timu hiyo kuichangia fedha.

Kaaya ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ambaye alijiuzulu kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya kiafya, amewaomba wanayanga wajitoe ili kuisaidia timu wakati huu wa mpito.

Kaimu huyo amesema kinachofanyika hivi sasa ni kuandaa namba maalum ambazo wanayanga wataweza kuzitumia kwa ajili ya kuichangia fedha ili kuikwamua klabu hiyo na hali ngumu inayopitia kwa sasa.

Yanga imeamua kufikia maamuzi hayo ili kuweza kupata fedha walau za kuweza kujikimu wakati timu ikiwa kambini kwa ajili ya msimu ujao na mashindano mengine ikiwemo ya kimataifa.

Wakati uongozi ukitangaza kuandaa namba hizo za kuchagia, kikosi cha timu hiyi sasa kipo katika maandalizi ya msimu mpya na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa siku za usoni jijini Dar es Salaam.

Halima Mdee Matatizoni Tena, Akamatwa na Polisi

$
0
0

Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Halima Mdee (Mb) pamoja na viongozi wengine, wanachama na CHADEMA Jimbo la Kawe takriban 13, wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Kawe. 

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amesema Mbunge huyo amekamatwa eneo la Tanganyika Parkers alipokua akizungumza na wananchi wa jimbo lake waliomsimamisha kutaka kumuelezea kero zao. 

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema bado hana taarifa zozote za kushikiliwa kwa Mbunge huyo. 

Zitto Kabwe Awekwa Kati na Polisi

$
0
0

Jeshi la Polisi limefungua jalada la uchunguzi dhidi ya kauli zilizotolewa na mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe.


Akizungumza leo Jumatano Agosti Mosi, 2018 msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa amesema kwa sasa uchunguzi unafanyika kuhusiana na tuhuma zinazomkabili mbunge huyo ambaye pia ni kiongozi wa ACT.


Mwakalukwa ameeleza hayo ikiwa imepita siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani,  Kangi Lugola kumtaka kiongozi huyo kujisalimisha polisi  kwa maelezo kuwa ametoa kauli za uchochezi.


Lugola amesema Zitto ametoa kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi wa Serikali wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini, mkoani Lindi.


Katika mkutano huo Zitto alialikwa na mbunge wa jimbo hilo, Seleman Bungara maarufu Bwege.


Mwakalukwa amesema kufuatia agizo hilo la Lugola tayari wamefungua jadala kuchunguza jambo hilo, kwamba uchunguzi ukikamilika na iwapo itaonekana mbunge huyo anahitajika, watamuita polisi.


Amesema polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria, kwamba Zitto akihitajika ataripoti kwa kamanda wa polisi mkoani Lindi.


Jana, Zitto alijibu kauli ya Lugola ya kumtaka aripoti polisi akibainisha kuwa atakwenda ikiwa atapewa wito wa kisheria.


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Zitto amesema, “waziri hana hayo mamlaka. Kama polisi wananitaka watoe wito wa kisheria nitakwenda.”


“Naendelea na kampeni za ubunge wa Buyungu ambapo tunamuunga mgombea wa Chadema na madiwani wa ACT- Wazalendo kwenye kata kadhaa. Nashauri waziri ampate kwanza yule mbwa wa polisi bandari.“
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live




Latest Images