Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

Mwanaume Anae Jua Kupetipeti Vs Mwanaume Mtundu Kitandani

$
0
0
Leo nina swali dogo tu kwa ladies. Assume una wanaume wawili mmoja ni mzee wa kupetipeti, yaani utabembelezwa, maneno matamu yakukufanya ujihisi wewe mzuri kuliko malkia cleopatra, utapewa kila ukitakacho mtoto wa kike, utasikilizwa, utaheshimiwa, utaachiwa uhuru nk. Lakini mkiingia uwanjana jamaa anaishia kukupakaza jasho tu, in short jamaaa ni lazy sana kwa bed. Lakini Kwa upande mwingine una jemba nyingine ambayo kupetipeti kumeipitia kushoto kubembeleza hajui, bahiri, maneno matamu hana. Ila ukija kwa bed anapiga mzigo balaaaa, unahisi utamu mpaka mboni ya jicho inavibrate.

Sasa inafikia wakati inabidi ubaki na mmoja tu. Kwa wewe mdada ungempa kibuti nani na kumpa shavu nani? Kati ya jamaaa hizi mbili

Kuchapiwa Mke Wanaume Saa Nyingine Mnajitafutia..Soma Hapa

$
0
0

WIFE....Honey plz lets come and help
me in the garden to clean these
flowers??
MME.......Are you mad ,do I look like a
gardener?
WIFE.....Ok sory babie,...but
sweetheart please go and fix that
door to the bathroom,Junior broke it
last night??
MME.....I hate your nosense
requests,,do I look like a Carpenter??
..
At night MME came back from town
and found that the garden is clean
and the door if fixed well..he was
surprised and decided to ask his wife..
..
MME.....Honey I can see the garden is
clean and the Door is well fixed,who
fixed the door for you??
WIFE.....Its our neighbour ofcourse..

MME.....Woow thats great,,did he fixed
it for you free of charge?
WIFE........NO he gave me two options
to choose...He said I must give him
BREAD OR SE..X..
MME.....I hope you gave him BREAD??
WIFE....What???....Do I look like
BAKERY???

MME Fainted....

Mama Mwenye Nyumba Ananitega Sana.

$
0
0

Nilipohamishiwa kanda ya ziwa kikazi toka Dar. nilimtafuta dalali ili anisaidie kunitafutia nyumba, kweli alipata nyumba ya mama mmoja hivi ambaye kiutamaduni ni mtani wangu na yy huwa ananiita mtani.

Sasa kwanza hana mume, mumewe alifariki mwaka jana mwezi wa 4 na ana watoto wakubwa tu wengine wapo vyuoni na mmoja anafanya kazi dar.

Toka mwezi huu uanze ameanza kunionyeshea tabia fulani fulani, kila nikitoka kazini anakuja ndani mwangu anakaa na wakati mwingine kumbe anakuja amefunga kanga tu.

Jana nimetoka kazini nikapita Hotelini kula nikakaa hadi saa 2 usiku nimerudi home aliposikia nafungua mpango tu huyo akaja na chakula nikamwambia nimeshiba nishakula, akanilazimisha kuwa chukua ule, nikapokea nikakiweka mezani then akakaa, akaniambia niwashe TV nikawasha.

Nikaenda kuoga kurudi naingia chumbani na yy huyo kafika akaniambia ngoja nikupake mafuta nikasema hapana sipaki mafuta usiku, aise si akakaa kitandani!! kumbe hakuwa na nguo ya ndani akabenua kanga mapaja hayo nje nje kweli nilipata mfadhaiko muda huo nikamwambia naenda sebuleni kuangalia kipindi fulani hivi cha ITV-KIPIMA JOTO, Akasema njoo kwanza nikarudi akaanza kunishika shika masikioni, nikamwambia nooo!! sipo tyr akauliza kwa nini? nikamwambia leo sijisikii kufanya hicho unachotaka, akaniuliza ina maana mi mbaya? nikasema hapana ila leo sina hamu kabisa ki ukweli nilikuwa na hamu sana ila nikimwangalia huyu mama ni mtu mzima sana ni above 50 na mimi mwenyewe ndo nipo above 27 nikasema hapana.

Akaniambia njoo angalau mara moja tu tux nikampa moyo kuwa subiri kesho yaani leo. Sasa ndugu zangu leo nitamdanganyaje tena?

Huyu mama sitaki kux naye coz ni kama mama yangu, pia, watoto wake japo wapo hostel chuoni kwao hapa hapa nahofia wakija jua kuwa namx mama yao na tunaheshimiana sana.

wazo la kuhama limenijia usiku ws leo sana.

Nifanyeje

Beyonce Afunguka Kuhusu Upasuaji Aliofanyiwa

$
0
0
Ifahamu hii siri nyingine kutoka kwa staa Beyonce ambaye amefunguka na kusema kuwa alifanyiwa upasuaji kipindi cha kujifungua watoto wake mapacha Rumi na Sir na amelithibitisha hilo katika jarida la Vogue hii ni baada ya kuzungumzia muonekano wake kipindi baada ya kujifungua.

Beyonce amefunguka na kusema kuwa kipindi cha ujauzito wa watoto wake mapacha aliongezeka uzito na kufikia hadi kilo 98 hali ambayo ilimfanya ashindwe kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na kuishiwa nguvu na hali hiyo ilionyesha kuhatarisha maisha ya watoto wake na hivyo ilibidi afanyiwe upasuaji unaofahamika kama (Cesarian Section).

“Nilikuwa na kilo 98 siku ambayo nilijifungua watoto wangu Rumi na Sir, na nilikuwa katika chumba cha mapumziko kwa mwezi mmoja kutokana na tatizo la toksemia, hali yangu pamoja na watoto haikuwa nzuri kwahiyo nilifanyiwa upasuaji wa haraka unaojulikana kama C-Section na tulikaa NICU kwa wiki kadhaa”



Beyonce alifunguka zaidi na kusema kuwa baada ya watoto hao kuzaliwa walibidi wawe chini ya uangalizi wa madaktari na hivyo walipelekwa chumba maalumu cha uangalizi na walikaa kwa wiki kadhaa, pia  anamshukuru sana mume wake Jay Z kwa kuwa rafiki wa karibu na baba bora kutokana na kuonyesha ushirikiano katika kipindi hicho kigumu.

Huu ndio Ugonjwa Unaomsababisha Wema Asizae Mwenyewe Afunguka A-Z

$
0
0
Huu ndio Ugonjwa Unaomsababisha Wema Asizae Mwenyewe Afunguka A-Z
KWELI; usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Ishu ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutokuzaa imepindishwapindishwa weee, kumbe ana gonjwa linalomzuia kunasa ujauzito.

Nani kasema? Ni Wema mwenyewe ndiye aliyefunguka hivi karibuni mbele ya ‘mshika kalamu’ wa Risasi alipokuwa akifanya naye Exclusive Interview nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam.

“Karibu uketi.” Hivi ndivyo safari ya mahojiano kati ya mwandishi wetu na miss huyo ilivyoanza na kuwafikisha katika kuzungumzia suala la mrembo huyo kutokuzaa mpaka sasa.



HAYA HAPA MAHOJIANO

Risasi: Pole na kuumwa maana leo ndiyo tunaonana.

Wema: Asante sana, niliumwa siyo mchezo.

Risasi: Ndiyo hiyo ishu ya kukatwa utumbo?

Swali hili lilizingatia habari zilizozagaa mitandaoni kwamba mrembo huyo alikwenda nchini India kufanyiwa oparesheni ya kukatwa utumbo ili kupunguza mwili na kujenga muonekano mzuri.

Wema: (Mshangao) kukatwa utumbo tena? Unajua mimi sijakatwa utumbo kama watu wanavyosema; ningekatwa nisingekuwa hivi.



Risasi: Nini sasa kilikuwa kikisumbua maana kuna wakati ulikwenda India kwa matibabu?

Wema: Unajua mimi nilikuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa tumbo langu la uzazi lililosababisha nisiweze kuzaa kwa muda wote huu.

Risasi: Pole sana; tatizo lililokuwa linasababisha usizae! Ni tatizo gani hilo?

Wema: Ngoja niweke wazi leo watu wajue, mimi nina ugonjwa ambao unasababisha mayai yangu ya uzazi kutoboka na kushindwa kupevusha mbegu za uzazi.


KIPINDI CHA KULITAZAMA GONJWA HILO

Mara baada ya Wema kufichua siri tatizo linalomzuia kuzaa na kwamba walioligundua ni madaktari wa nchini India ambako alifanyiwa upasuaji Risasi lilitaka kujua ugonjwa huo unaitwaje.

Kwa sababu Wema mwenyewe alishindwa kufafanua undani wa ugonjwa wake, dalili zake, visababishi, tiba na kinga yake, Risasi liliuweka kuwa ‘asaimenti’ ya kuifanyia kazi kupitia madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.



TUENDELEE NA MAZUNGUMZO

Wikienda: Kwa hiyo video uliyokuwa ukionekana uko hospitali hapa Bongo ilikuwa ni nini?

Wema: Unajua baada ya oparesheni ya India niliporudi nikapata tatizo la kushindwa kupumua vizuri na kingine nikapata maambukizi ya bakteria kwenye kidonda na presha ikawa inashuka.

Risasi: Oooh! Kwa hiyo baada ya upasuaji huko India tatizo la mji wa uzazi limeisha?

Wema: Naendelea na matibabu lakini tatizo limeanza kupungua nafikiri baada ya mwaka nitakuwa mzima kabisa.



ISHU YA KANSA YAIBUKA

Risasi: Risasi linakuombea heri ugonjwa huo uweze kuisha na kukurejeshea furaha.

Wema: Nashukuru ila kiukweli hali ilikuwa mbaya sana, maana madaktari wa India waliponifanyia vipimo walisema kama ningechelewa kuutibu ugonjwa uliokuwa unanisumbua ungeweza kubadilika na kuwa kansa na hivyo kuhatarisha maisha yangu.

Risasi: Duh, kwa hiyo baada ya oparesheni kufanikiwa wamekuhakikishia kuwa hatari hiyo haipo?

Wema: Yeah; hakuna kitisho hicho tena, hali imerudi kawaida kabisa.



DAKTARI AUTAJA UGONJWA WA WEMA

“Kama Wema ameeleza kuwa amekuwa na tatizo kwenye via vyake vya uzazi na kwamba mayai yamekuwa yakishambuliwa na virusi kiasi cha kushindwa kupevuka basi ni kweli lakini nimsahihishe tu kwamba huwa mayai hayatoboki bali huweka vimbe ndogondogo nyingi kwenye yai,” anasema Dokta Godfrey Chale daktari maarufu wa Muhimbili.

Anaendelea kueleza: “Tatizo hilo kitaalamu huitwa Polycysitic Appearing Cyst na ugonjwa huitwa Polycystic Ovarian Disease (PCOD). “Uvimbe wa aina hii unakuwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogovidogo na siyo matobo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

Tokeo la picha la Polycystic Ovarian Disease (PCOD)

“Dalili kubwa ni mwanamke kukosa hedhi, kukosa hamu ya tendo la ndoa, huwa na homoni nyingi za kiume kuliko za kike na wengine kuota ndevu au vinyweleo vingi mwilini na mara nyingi huwakumba wanawake wanene.

“Lakini mwanamke pia anaweza kuwa na uvimbe unaojulikana kitaalamu kama Follicular Cyst. Hii hutokea wakati ovulation (uchavushaji wa yai) isipotokea au baada ya kiungo kiitwacho corpus luteum (kondo la uzazi) kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutokupachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.



“Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana, uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation.“Maumivu haya yanayojulikana kama mittelschmer huonekana kwa wanawake kwa kiwango cha robo moja wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote.

“Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. “Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndiyo unaojulikana kama ovarian cyst.



“Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake.Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. “Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya ya mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum,” alisema Dk. Chale.



TIBA YA PCOD NI NINI?

Akizungumzia tiba ya Dk Chale alisema: “Mwanamke mwenye vivimbe kwenye mayai yake hutibiwa kwa dawa kwa muda mrefu na mara nyingi hutumia dawa za kisukari aina ya Matfoam.  Endapo matumizi ya dawa yatashindwa kuondoa tatizo basi hatua ya kufanyiwa upasuaji huchukuliwa kwa lengo la kuviondoa vivimbe hivyo kwenye mfuko wa uzazi.

Tokeo la picha la WEMA

WEMA ANAWEZA KUZAA?

Kwa mujibu wa daktari huyo, mgonjwa yeyote anapopewa matibabu sahihi na yeye kuzingatia ushauri wa kitalaam atakaopewa basi uwezekano wa kuweza kuzaa upo kwa kiwango kikubwa, lakini kama tatizo halijatibiwa mwanamke hata atembee na wanaume mia ni nadra sana kupata ujauzito. “Kama Wema amefanyiwa upasuaji na anazingatia ushauri wa madaktari wake atapona kabisa na ataweza kupata ujauzito bila wasiwasi,” alisema Dokta Chale.



Tatizo la Wema kutokuzaa limekuwa likipata nafasi kubwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari huku kukiwepo na taarifa kinzani kuhusu mrembo huyo aliyepita kwa wanaume wengi kutofanikiwa kuzaa. Miaka miwili iliyopita katika mahojiano yake na redio moja jijini Dar, Wema aliwahi kukaririwa akisem: “Maneno ya mimi kutokuzaa yananiumiza sana, lakini Mungu hajapenda na sina la kufanya.”



Baada ya miss huyo kusikika akisema maneno hayo, msanii mwenzake wa filamu Riyama Ally alimfariji kwa maneno haya: “Naomba hapa unisikie kwa makini; Nabii Ibrahim alimzaa Nabii Ismail (Isaka) akiwa mzee.”

TFF Yaungana na Makonda Katika Maandalizi wa AFCONU17

$
0
0
TFF Yaungana na Makonda Katika Maandalizi wa AFCONU17
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), kupitia kwa Rais wake Wallace Karia, limethibitisha kupata ushirikiano kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika maandalizi ya michuano ya kuwania kufuzu AFCON U17 mwaka 2019 kwa vijana kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Rais wa TFF Wallace Karia (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia).

Karia amebainisha hilo leo kwenye mkutano wa pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, TFF na wanahabari, ambapo amesema taratibu zote za mapokezi ya timu kutoka mataifa 12 zinaratibiwa kwa pamoja na ofisi ya mkoa pamoja na shirikisho na kila kitu kipo sawa.

''Kwa upande wetu maandalizi ya michuano hiyo itakayoanza Agosti 11 kwa kushirikisha timu 12, yameshakamilika ila tu tuishukuru serikali ya mkoa wa Dar es salaam kwa ushirikiano wanaotupatia kwenye mapokezi na usalama wa timu'' - amesema.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, amesema wamejipanga kama mkoa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa mafanikio ili kurejesha imani kwa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na kusaidia kuendelea kupewa fursa ya kuandaa mashindano mengine.

Michuano hiyo ya vijana ambapo Tanzania tayari imefuzu fainali za mwakani kwa kigezo cha kuwa mwenyeji, inaanza Agosti 11 na kumalizika Agosti 26. Timu zitakuwa kwenye makundi mawili na zitacheza kwa mfumo wa ligi na baadae robo fainali, nusu na fainali. Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Ukanda wa CECAFA kwenye AFCON U17 ya 2019

PICHA: Rais Magufuli Akutana Na Viongozi Wa Jumuiya Ya Kikristo Tanzania (CCT) Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi  Alinikisya Cheyo, aliyeongoza ujumbe wa viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
PICHA: Rais Magufuli Akutana Na Viongozi Wa Jumuiya Ya Kikristo Tanzania (CCT) Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  Dkt. Frederick Shayowakati ujumbe wa viongozi wakuu  wa Jumuiya hiyo  ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa watika mazungumzo  na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania,  Alinikisya Cheyo, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Shoo, Makamu wa Pili wa Mwenyekiti  Dkt Jacob Chimeleje na Katibu Mkuu wa CCT  Canon Moses Matonya ujumbe huo viongozi wapya wa jumuiya hiyo ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.

Nilitamani sana nimwambie Nikki wa Pili aache muziki – Joh Makini

$
0
0
Nilitamani sana nimwambie Nikki wa Pili aache muziki – Joh Makini
Leo ni siku ya kuzaliwa ya rapa kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ambapo mashabiki pamoja na ndugu zake wa karibu wametumia mitandao ya kijamii kumtakia heri na baraka katika maisha yake.


Joh Makini ambaye ni kaka wa rapa huyo akiwa katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, amefunguka namna alivyotamani kumkataza mdogo wake huyo kufanya muziki kutoka na changamoto ambazo alikutana nazo.

“Nilikuwa naambiwa na watu kuwa mdogo wangu 9Nikki wa Pili) anachana na sikuzingatia na hata wakati anarekodi GoodBoy sikuwepo, kuna kipindi nilikuwa natamani nimwambie asifanye muziki kutokana na changamoto na mazingira ambayo tulikuwa tunapitia ila nilikuwa nashindwa sababu alikuwa ananiprove wrong kwenye kazi zake,” alisema Joh Makini.

Mapema ya leo hii Nikki alianza kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kwenda kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia katika shule za msingi.

“Asubuhi nilienda shule kupeleka vitabu na mapokezi ya shule yalikuwa makubwa kwani nilienda toka wiki iliyopita kuomba nafasi na walikubali na leo ikiwa ni siku ya kumbukizi yangu ya kuzaliwa nikaona niende kupelea vitabu,” alisema Nikki.

Roma na Stamina Wamejifungia Wenyewe, Wanatafuta Kiki – BASATA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limekanusa taarifa ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii kwamba wimbo mpya ‘Parapanda’ wa Roma na Stamina umefungiwa.


Taarifa hizo zilianza kuzagaa mara baada ya wawili hao kuitwa na Baraza hilo kwaajili ya kikao cha kujadiliana mambo mbalimbali kusuhu kanuni mpya za baraza hilo zilizotangazwa mapema jana.

Muda mchache baada ya kikao hicho Roma na Stamina alionekana wakilalamika kupitia mitandao ya kijamii kwamba waliitwa kwaajili ya wimbo wao mpya huku wakidai umeonekana una matatizo.

Mapema jana Katibu wa Baraza la Sanaa, Godfrey Mngereza, aliimbia Bongo5 kwamba wawili hao hawakuijwa kwaajili ya wimbo wao.

Akizungumza na mtandao wa Mwananchi Digital, Mngereza alisema “Labda kama wameamua kujifungia wenyewe ili kuufanya wimbo wao ujulikane na watu, lakini sisi hata hatujauona na kuupitia kama taratibu zetu zinavyotaka na mnajua tukifungia wimbo huwa tunatangaza sasa labda Roma awaonyeshe wapi tumesema hivyo,” amesema Mngereza.

Hata hivyo, katibu huyo alikiri kuwa jana wasanii hao wawili kufika katika ofisi za Basata kwa ajili ya kushiriki jukwaa la wasanii ambalo hufanyika kila siku ya Jumatatu katika ukumbi wao uliopo Ilala Gereji huku mada kuu kwa siku hiyo ilikuwa kuhusu kanuni mpya za sanaa zilizoanza kutumika Julai mwaka huu.

Katika jukwaa hilo anasema mmoja wa waandishi aliuliza swali kuhusu matumizi ya picha za waasisi wa mbalimbali wa nchi hii katika sanaa, ambapo Mngereza anadai alimjibu kuwa msanii anapaswa kupata kibali kutoka kwa familia au Serikali.

“Huenda majibu haya labda ndiyo yalimfanya Roma akaondoka pale na tafsiri yake na kuandika hicho alichokiandika, lakini kiukweli hatujamfungia wala kumuita kumuhoji kuhusiana na wimbo hiyo,” amesema Katibu huyo.

Source: Mwananchi

Ongeza Uume, Nguvu na Hamu ya Tendo la Ndoa Hata Kwa Wenye Kisukari na Pressure

$
0
0

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limezidi kuongezeka kwa kasi duniani kote na limekuwa chanzo kikubwa cha ndoa nyingi na mahusiano kukosa uaminifu kutokana na wengi kutoka nje ya ndoa ili kupata mtu atakayemtosheleza na kumfikisha kileleni. Pia udogo wa maumbile ni tatizo kubwa na limekuwa likiwakosesha wanaume wengi uwezo wa kujiamini katika tendo na kusababisha tendo hilo kutokufanyika kwa usahihi. Hili pia huchangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa ( MAHUSIANO) kutafuta mbadala wake.
BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.

Kwa kutumia mimea tiba na matunda bila kemikali sasa
@markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 5.5 hadi 6 @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo ×3. @150,000/=
BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA KIAFYA NA ZIMETHIBITISHWA
NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO).
KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
WEB:www.markbeauty.org
Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0767447444 na
0714335378
UTAPATA HUDUMA
NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
#OngezaUume
#NguvuZaKiume
#HandsomeUpOg
#BidhaaTz

Wakala wa Pogba Afanya Maamuzi Magumu

$
0
0
Ajenti wa mcheza soka wa Manchester United, Mino Raiola, anafanya juhudi za kumwondoa mchezaji huyo katika timu hiyo ya Uingereza ili aende kuchezea timu ya Barcelona.

Raiola amekuwa akifanya juhudi hizo kwa muda wa miaka miwili tangu Pogba alipohama timu ya Juventus na kujiunga na United kwa Paundi mil. 89 (Sh. bil. 263).

Mchezaji huyo hivi sasa amerejea Uingereza akitokea kwao Ufaransa baada ya kutwaa Kombe la Dunia  nchini Urusi.

Hata hivyo, United wamesisitiza jana (Jumatatu) kwamba hawamuuzi mchezaji huyo na wamekataa ofa ya Barcelona ya Paundi mil. 44.6 (Sh. bilioni 132) na kupewa pia wachezaji  Yerry Mina na Andre Gomes.

Kwa vile msimu wa ligi kuu unaanza Ijumaa wiki hii kwa United kucheza nyumbani dhidi ya Leicester, huenda mpango huo ukafanyika wakati wa dirisha dogo.

BASATA Wafunguka ‘Roma na Stamina ni Watu Waajabu’ (Video)

$
0
0
Bazara la Sanaa Taifa (BASATA) limefunguka kukanusha taarifa ambazo zimeenezwa na Roma na Stamina kwamba waliitwa na kuhojiwa na baraza hilo kwaajili ya wimbo wao mpya uitwao Parapanda. Katibu Mkuu wa Basata Godfrey Mngereza amedai wasani hao waliitwa na baraza hilo kwaajili ya kuelekezwa mambo kadhaa kuhusu kazi zao kwa kuwa wao ndio walezi wa wasanii wote. VIDEO:

Tundu Lissu "Habari ya Mujini Nimetoka Hospitalini Nipo Kwangu'

$
0
0
Hello Friends of Me!!!

Good afternoon to y'all. Kwa mara nyingine nawaleteeni habari njema.

Alfajiri ya tarehe 6 January ya mwaka huu, niliondoka Nairobi Hospital na kusafiri hadi Leuven, Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu zaidi. Jana tarehe 6 Agosti ilikuwa mwezi wa saba kamili tangu niletwe hapa Ubelgiji kwa ajili hiyo.

Leo tarehe 7 Agosti ni miezi 11 to the day niliposhambuliwa na watu wanaojulikana sana kama 'watu wasiojulikana.'

Tarehe 7 September mwaka jana sikulala nyumbani kwangu. Tarehe 7 Agosti ya leo, miezi 11 kamili baadae, nimeamkia nyumbani kwangu.

Tarehe 7 September iliyopita wote mlikuwa na hofu kubwa kama ningemaliza siku hiyo, au siku chache zilizofuata, nikiwa hai. Miezi 11 kamili baadae, Professor Dr. Wilhelmus Jan Mertsemakers, daktari wangu tangu nilipokuja University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya kitabibu ya kuendelea kukaa hospitali.

Prof. Mertsemakers amesema nitaendelea na uponyaji nikiwa nyumbani kwangu. Nitatembelewa na homecare nurses kila siku nyumbani kuniangalia naendeleaje. Na nitarudi hospitali kumwona kila baada ya wiki mbili.

Bado nina lichuma kubwa kwenye paja liko kama antenna ya TV za mwaka '47. Na Prof. Mertsemakers amesema nitakaa nalo kwa si chini ya miezi sita. Lakini habari ya mujini ndio hiyo: nimetoka hospitalini.

Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuniuguza na kuniponya. Na chochote mtakachokula au kunywa siku ya leo mnibakishie. Siko mbali.

Tundu Lissu,
Brussels, Belgium.

Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Akamatwa na Polisi Kwa Kujiunga na Kikundi cha Ukabaji

$
0
0

DODOMA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Itega, Mohamed Ramadhani(18) kwa kujiunga na kikundi cha uhalifu cha 'Kamchape' ambacho kinajihusisha na ukabaji
-
Kamanda wa Polisi, Gilles Muroto amesema kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu ambapo kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye
-
Aidha, Kamanda Muroto amesema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini alikamatwa tena, alipobainika kuwa amehusika katika kuvunja nyumba ya mtu na kuwafunga kamba wenye nyumba ili wawaibie
-
Kwa upande wake mtuhumiwa huyo amedai chanzo cha yeye kujihusisha na matukio hayo ya uhalifu ni kutokana na hali ngumu ya maisha ndio imemfanya kutenda hayo
-
Wengine waliokamatwa ambao wanaunda kundi hilo la Kamchape lililopo Kizota ni Abdul Mchangala(18), Mashaka Idd(17), Salum Mohamed(24) na Hamis Kikweli(40)

Stamina wa Rostam aonyesha Barua ya Kuitwa Basata Jana Kujadili Wimbo wa Parapanda..Kupinga Kauli ya Basata

$
0
0

Baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kudai kwamba Roma Mkatoliki na Stamina hawakuitwa na baraza hilo Jana kwaajili ya wimbo wao mpya ‘Parapanda’ na kudaiwa wanatafuta kiki, Stamina ameamua kuweka wazi kila kitu baada ya sakata hilo kuonekana kuchukua sura mpya.

Stamina Ameandika Hivi Kupitia Ukurasa wake wa Instagram  -

" Sisi kama ROSTAM Tunaamini kile tunachokifanya na hatujawahi kufanya mziki kwa mlengo huo wa kiki ,Mwenye uelewa ukisoma hiyo barua utaelewa kama tunatafuta kiki au kweli tuliitwa kwa ajili ya wimbo wa parapanda.
Hata hvyo tunawashukuru BASATA kwa kuthibitisha mbele ya umma leo kua nyimbo haijafungiwa.
Pia Tunashukuru mashabiki kwa kuendelea kuSupport mziki wetu, naomba tuendelee kuuchagua wimbo wetu kwenye media mbalimbali

#Hatuongeitena
#achagomaliendelee

Asante

Barua ya Basata iliyopostiwa na Stamina kwenye Instagram:

Mambo Sita Usiyoyafahamu Kuhusu Alikiba na Coastal: Mkataba, Namba ya Jezi, Mchezo wake Wakwanza na Muziki (Video)

$
0
0




1. Alikiba anatarajia kurikodi video yake mpya.
Wakati tulipomtembelea Alikiba kwenye mazoezi yake alitudokeza kuwa muda simrefu anatarajia kurikodi video mpya licha yakushindwa kutaja jina la wimbo wenyewe.

2. Jina la Alikiba limepelekwa kwenyeshirikisho la soka nchini Tanzania TFF tayari kwa kutumiwa na Coastal

Bongo5 imefanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Coastal Union kupitia kwa msemaji wake, Hafidh Athumani Kido ambaye amethibitisha kuwa jina la mchezaji wao mpya Alikiba limefikishwa TFF kwaajili ya kutumiwa kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.

3. Mkataba wa Alikiba ndani ya klabu ya Coastal Union

Uongozi wa Coastal Union umeshindwa kuweka hadharani mkataba wa mchezaji huyo ukidai kuwa swala hilo ni landani ya uongozi na meneja hivyo hawawezi kuliweka wazi. Kwamujibu wa vyanzo vyetu vya ndani msanii huyo ataitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja wa mwaka 2018/19 huku akiwa amejitolea kutokana kucheza bure kutokana na mapenzi yake katika soka.

4. Alikiba kuanza kucheza kwenye mchezo wakwanza wa ligi

Ofisa habari huyo wa Coastal, Kido amesema kuwa Alikiba atakuwa kwenye mchezo wao wa ufunguzi utakao pigwa tarehe 22 ya mwezi huu kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

5. Alikiba atacheza kwenye mechi za Simba na Yanga

”Alikiba lazima atacheza kwenye mechi za Simba na Yanga kwasababu wanaocheza nao ni binadamu,” amesema Hafidh Athumani Kido Ofisa habari wa Coastal.

6. Namba ya jezi atakayovaa Alikiba ndani ya Coastal Union

Kido amesema kuwa Alikiba hajawahi kucheza mpira kwenye ligi kuu na hivyo watu wasubiri kuona uwezo utakao onyeshwa na msanii huyo huku akitarajiwa kuvaa jezi namba 15 kutokana na mazungumzi baina yake na klabu.

Alikiba ataweza kuisaidia Coastal Union licha ya uchezaji ndani ya uwanja lakini pia ataweza kuibeba klabu hiyo kupitia umaarufu wa staa huyo wa muziki nchini na bara zima la Afrika.

Klabu ya Coastal Union imepanda rasmi ligi kuu mwaka huu baada ya kuiyaga michuano hiyo msimu wa mwaka 2015/16.

Ofa ya Kuinunua Arsenal yakubaliwa

$
0
0
Wamiliki wa Arsenal Stan Kroenke na Alisher Usmanov
NA ELBOGAST MYALUKO
Mmiliki wa asilimia 30 ya hisa ndani ya klabu ya Arsenal Alisher Usmanov amekubali ofa ya Paundi milioni 600 zaidi ya shilingi trilioni 1 aliyotoa tajiri Stan Kroenke, ambaye ni mmiliki mwenza wa Arsenal kwaajili ya kununua asilimia hizo 30 Alisher Usmanov.

 Mapema leo Agosti 7, 2018 Alisher Usmanov alitangaza kuziweka sokoni hisa zake huku  Kroenke anayemilikia asilimia 67 ya hisa akitangaza nia ya kutaka kuzinunua asilimia 30 ili aimiliki moja kwa moja klabu hiyo kupitia kampuni yake ya KSE.

Usmanov amesema kuwa amevutiwa na mpango wa KSE ambao ni kuifanya Arsenal kuwa ya ushindani zaidi na kutwaa mataji kama EPL na ligi ya mabingwa Ulaya sambamba na kuwekeza kwenye timu ya wanawake na timu za vijana hivyo yupo tayari kumuuzia  Kroenke ili alitekeleze hilo.

Pamoja na matajiri hao kuonekana kukaribia kukubaliana lakini mashabiki wa timu hiyo ambao nao ni moja ya wamiliki wa hisa 'Arsenal Supporters Trust' (AST), wamepinga vikali hatua ya timu hiyo kumilikiwa na mtu mmoja wakiamini kuwa utakuwa ndio mwisho wa wanachama hao kumiliki hisa ndani ya timu yao.

Kroenke mwenyewe amesema kuimiliki Arsenal peke yake kutasaidia utekelezaji wa mambo kwa wepesi kwani hakutakuwa na pingamizi na klabu pia itakuwa na uwezo wa kununua wachezaji wakubwa na wenye ushindani kwani hatapenda kuona biashara ya kampuni yake KSE inafeli.

EATV

Nampenda Mtoto wa Mjomba wa Kiume..Nashindwa Kuvumilia

$
0
0
Jamani mie nimeshindwa ngoja niseme tu leo ...Mie ni msichana wa miaka 22 niko chuo UDSM mwaka wa pili , Wazazi wangu wanaishi Mwanza...

Hapa dar huwa nafikia kwa mjomba wangu hasa week end huwa natoka hostel nakuja kwa mjomba..Mjomba wangu ana mtoto wa kiume wa miaka 28 nimetokea kumpenda jinsi alivyo mpole na Mstaarabu sana , huwa kila mara anakuja kunitembelea Hostel na akija nakuwa happy sana, Huwa nawadanganya Marafiki zangu kuwa ni Boyfriend wangu..

Nampenda sana mpaka siku hizi nimeanza kumtega ili nilale nae ila naona kama bado hajashtukia, Juzi aliingia chumbani kwangu nikajifanya taulo limedondoka ila akatoka haraka na kufunga mlango...Mie nilidhani nae atapagawa na umbo langu ila laaa ...Nifanyaje ? Je kutembea na mtoto wa Mjomba ni Vibaya?

A Lady With a Big List of Men Sio Kigezo Hafai Kuwa Mke Mwema!!!!!! Sometimes We are All Victims of Fate!

$
0
0
Lets have a HEALTHY CONVERSATION! Tuchallangiane kwa logics na points! Matusi ni ya makuli kule bandarini. Haipendezi unabinya binya keypad afu mitusi kibao!

Leo nimeamua kabisa nidedicate siku hii ya leo kukabiliana na jamii yetu ambayo ni very JUDGMENTAL and CONDEMNING by nature kujaribu kuwaelewesheni viumbe wagumu kuelewa, wepesi kusahau kuwa sometimes A SISTER GOTTA DO WHAT SHE HAS TO DO!!!!!!!!!!!!!

Sio mara 1 au 2 watu tumekuwa wepesi kuhukumu, kushadadia, na kuleta upambe nuksi kuwa Mwanamke flani hafai hafai hata kwa mbolea kuolewa coz She has THE LIST (Hii ni THE LIST kwa herufi kubwa manake kuna uwezekano inaweza kuwa NEVER ENDING! au she IS NOT SURE au SHE STOPPED COUNTING A LONGTIME AGO!) UWE ME AU KE YOU GOT NO RIGHT TO SAY SHIT ABOUT THE SISTER NO MATTER HOW CLEAN YOU ARE (TO BE PRECISE YOU WISH YOU ARE)!!!!!!

Mtu kuwa na wanaume wengi sio kigezo cha kumconvict directly kuwa She is a bad person na mtu kuwa na list ndogo sio kigezo cha usafi smts ni lack of opportunity tooo! Mtu kuwa na wanaume wengi au kidogo sometimes ni matokeo ya mambo yafatayo ambayo YAKO NJE YA UWEZO WA KIBINADAMU WA MTU!!!!!!!!!!!!

1. KUZALIWA KICHUNA WA HAJA/ FLAWLESS BEAUTY!!!!!!!!! Mtoto mcute of the cutest, kijungu kijungu, rangi ya carolite ama black beauty, hips hips kama Wema Sepetu! Automatically utapata opportunity kwa watu wa vijijini wataita challanges zisizo na kikomo kutoka kwa MAPEDESHEEE! You jst name your price (Every body has a price) watailipia ili wakatishe japo mara moja katikati ya miguu yako. To whom much is given much is expected! Vishawishi vinakuwa TOO MUCH! Beyond reasonable zone ambayo binri wa kawaida angevishinda! So its logical ku expect from What Wema et al walivojaaliwa na Bwana at the age of 24 na vishawishi wanavopata eti mimi Lara et al nimhukumu kwa TUVISHAWISHI TWANGU kutongozwa na wachovu wenzangu kuwa flani HAJATULIA! COME ON!!!!!!!!!! Hata mimi Lara ningejaliwa vile NISINGETULIA!!!!!!!!! Labda nina kijilist coz wakawaida sanaa anitake nani? Tuhukumu watu kwa kubase Majaliwa yao na uzito wa misalaba yao! Wema katongozwa na wanaume 100, kakubali 20, Lara anaume 10, kakubali 2 sasa hamuoni %wise NGOMA DROO!!!!!!!!

2. KUZALIWA NA BLACK FATE/ MISFORTUNE NA WANAUME!!!!!!!!!! Kuna watu wamezaliwa na bahati zao ati! Mwanaume wa kwanza anafungua njia huyo huyo ana muoa!Jst her lack! Au umezaliwa maeneo full of quality men! Kila mtu potential husband. Sasa huwezi kutuhukumu sisi wengine wenye BLACK FATE! Mtu una intentions nzuri kabisaaa, wala huna tamaa! Ila kila unaepata MAGUMASHI!!!!!!! Sasa kupambana na THE LIST ndo ukubali ku settle for less au uendelee kuwa victim wa THE LIST and AGE!!!!!!!! Whatever pressure gets to you first either way life has ----ed us!!!!!! Its PURELY NOT OUR FAULT!!!!!!!!!!! Na utakuta tunasali sanaa tu! Basi tu ndo vile haijaandikwa! Cause you are SIMPLY LUCKY you got no damn right to judge us, simply because we were not as lucky as you are! HAVE MERCY PEOPLE!!!!!!!! Remember KARMA IS A BI.TCH, your luck may change.

3. EXPOSURE AND INTELLIGENCY! Kuzaliwa mwanamke ukawa very SMART kichwani, afu ukapata EXPOSURE believe it or not ITS A CURSE!!!!!!!!!!!!! No man (Maybe very few tena wanaweza kuwa wameoa) will ever be GOOD ENOUGH (as good enough toka rohoni kwako) for you! Hata ukiolewa kudumu pia ni mashaka sanaaa au umpate mwanaume verty stu.pid au smater than you! Sababu tayari wewe ni Strong Character na umezaliwa na nyota ya Jua! Kama Oprah (specifically fate yako ni kurule, accomplish and kuconquer ambayo ni nyota ya kiume!). Its not your fault that you aint stupid, lakini ki Africa a Womans Place is in the Kitchen Sink! Automatically utajikuta na THE LIST OF LISTS not because you are a Bad Person or something, ni kuwa you are too gifted, you can see right through men, you can smell foul play from a mile, you cant know things are wrong and do nothing, you cant just take shit! Unajikuta una list coz unatafuta stronger character mwenzio. Sasa sisi kina Lara tumezaliwa na nyota ya mwezi, mwanaume anaweza kuwa anakuonea live live wala hushtuki! What you dont know cant kill you! Au hata ukijua you jst find it in you kumsamehe no matter how grave is the offence. You feel happy n nothin is missing! Mtu wa nyota ya mwezi haruhusiwi kumhukumu mtu wa nyota ya jua!

4. MAZINGIRA NA MALEZI! Mtu huchagui uzaliwe wapi? Unajikuta tu umezaliwa iwe kwa Baa medi au kwa bosi wa bandari ndo ushazaliwa! We just have to live our life the way its given to us. Sasa kama umezaliwa sehemu ambapo Sex is a means of life, na kwa kukosa muongozo mzuri ukajikuta ushavuruga vuruga, not because you are a bad evil person ila ni tu kwamba you were not lucky kufundishwa morals at the right time. I know ukija kujua may be at 19yrs wakati THE LIST ishafika 30 men, its not too late! A sisr cant change her past but can surely change her future! Au ugumu wa maisha ulikufanya ufanye things you are not proud of, its not your fault! Shit happens because it just does! Sasa unakuta jitu limelelewa kwenye sofa za cashmere, limesoma kibwenyenye halafu la kwanza kuhukumu. Kama ndo yeye angpitia hayo maisha angekuwa amesha Rest In Peace siku nyingi! Kabla hujamuhukumu mtu jiulize je wewe ungepewa maisha yale ungekuwa Msafi?

All im sayin is WITH THE LIST OR WITHOUT THE LIST It doesnt make you a Bad person or a better person!!!!!!!! ITS JUST A LIST! A sister shouldnt be judged by her past but WHO SHE REALY IS!!!!!!!!!!!

laRA

Diamond Amsambaratisha Mganga wa Diamond..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 8

$
0
0

Diamond Amsambaratisha Mganga wa Diamond..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 8
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images