Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Mkongo wa Wolper: Namtaka "LULU" Kwa Gharama Yoyote

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima , inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC ) , Mwami Rajabu ‘ Mkongo ’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘ kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘ Lulu’ kwa gharama yoyote.

Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo. 

“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper , Husna mara Wema , si kweli , hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi ( Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu, ” alisema Mwami bila soni.

Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake. “Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana, ” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea .

Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar , hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea .

Wasanii Waliopotelea "Majuu" Kuna Faida Yoyote b na Mbona Hatuwasikii Tena ?

$
0
0
Kuna kumbukumbu za vijana mbalimbali ambao kutokana na maisha yalivyowaendea hapa nyumbani waliamua kutorokea ughaibuni.
Niwengi sana watu waliotorokea nnje.

Kwa kumbukumbu zangu nawakumbuka vijana au wasanii wetu kadhaa wa mmuziki wa kizazi kipya kama Balozi Dola soul, Solo Thang, Mad Ice,  Stiggo, footballer Renatus Njohole na weengi wengine.

Vijana hawa wengi wao wakiwa huko hupata wanawake wa kizungu na kuanzisha maisha ya kifamilia ili kuweka uwepesi wa wao kuishi nchi ya ugenini.
Bahati mbaya watoto wanaozaliwa katika mahusiano haya huwa hawajui nchi alikotoka baba na mara chache hata wanawake zao hawa huwa hawataki kabisa kuja Afrika.
hii hupelekea kizazi kupotelea ughaibuni na vijana wetu kuwa kama wao ndio walioolewa huko Ulaya!!

Maoni yangu ni kwamba vijana tuwe wavumilivu na tukubali kupambana na maisha yetu hapa Afrika na kukataa kuolewa na wazungu ulaya na Marekani huku tukiachia familia zetu hali ya sintofahamu kuhusu kijana wao aliye ulaya ambae hawana faida nae wala undugu na kizazi anachoanzisha ulaya kikiwa hakina faida yeyote nyumbani!!!

Tena Kwenda huko Ulaya kunaua Vipaji , Wengi Wakishaenda Huko Hatuwasikii tena ndio Kwishney..

Ebola Tena Marekani ..Daktari Aliyekuwa Akimtibu Yule Mgonjwa wa Ebola Aliyefariki nae Akutwa na Virusi Hivyo

$
0
0
Mfanyakazi aliyemtibu mgonjwa wa Ebola Thomas Eric Duncan nchini Marekani kabla hajafariki ameripotiwa kukutwa na virusi vya Ebola kutokana na utafiti wa afya aliofanyiwa ambapo kwa sasa amewekwa kwenye kitengo maalumu huku ikisemekana pamoja na kuvaa mavazi ya kumkinga kuambukizwa virusi, haikusaidia chochote.

Duncan ambaye alipata virusi hivyo vya Ebola alipokuwa mjini Liberia alifariki Jumatano ambapo mlipuko huu wa virusi vya Ebola kutoka nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone imethibitishwa kuwa na waathirika 8300 na vifo vya kukaribia 4033.
Hospitali imethibitisha kuwa njia za kujikinga na maambukizi hayo ya Ebola zinafatwa kwa uangalizi mkubwa na wafanyakazi wote ambao wanafanya kwenye kituo hicho cha afya cha Texas Health Presbyterian ambapo mkuu wa kituo hicho Dr. Tom Frieden amesema kuna uwezekano mfanyakazi huyo hakufata njia zote husika za kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu wa kituo hicho cha afya alikiambia chombo cha habari cha Marekani CBS kwamba watafanya uchunguzi ili kujua ni jinsi gani muhudumu huyo wa afya alipata virusi hivyo vya Ebola na kwamba wote ambao walimuhudumia Duncan watafanyiwa uchunguzi ili kujua kama na wao wamepata virusi hivyo vya Ebola.

Mchekeshaji Kansiime Kutoka Uganda Umuonyesha Mpenzi Wake

$
0
0
Ni mchekeshaji wa Uganda ambae tumekutana na video zake fupifupi nyingi sana kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, facebook na hata tumekua tukirushiana Whatsapp.
Kwenye upande wake wa pili kama binadamu, Kansiime amepost picha ya yeye na mpenzi wake wakiwa wanasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao na kusema 

Kwenye mahojiano ya hivi karibuni niliulizwa utapigana kwa ajili ya Mwanaume wako? hmmm nikacheka, aliyenihoji hakuwa anajua kama hata naweza kuingia vitani kwa ajili tu ya Ojok wangu, ni mwaka mmoja sasa toka tuchague kuwa pamoja na natarajia kufurahia miaka mingine mingi

Udaku Specially Blog Yafikisha Miaka Miwili ..Udaku Team Ina haya ya Kusema Kwako

$
0
0
Udaku Team
Team ya Udaku Specially Blog Inapenda kutoa shukrani za Dhati Kwa Watembelea wa Blog hii Kwa Kutufikisha hapa tulipo leo Ambapo Blog inatimiza Miaka Miwili rasmi Toka ianzishwe mwaka 2012 October

Katika miaka hiyo miwili tumepitia mengi sana kufikia sasa blog inatembelewa na watu zaidi ya 200,000 kwa siku na toka ianzishwe imefikisha visitors zaidi ya Millioni 48  na kwa sasa ni moja ya blog maarufu hapa Tanzania...Asante Sana Kwa Kuwa Nasi Muda Wote huo..Keep it Locked

Waziri Mh. Lazaro Nyalandu Afungukia Madai ya Kutoka Kimapenzi na Aunt Ezekiel

$
0
0
Juzi gazeti moja la habari za mastaa nchini liliandika kuwa ndoa ya Mh. Lazaro Nyalandu ambaye ni mbunge na waziri wa maliasili na utalii nchini na Faraja Kota ambaye ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 2004 inatikisika kisa kikidaiwa ni star wa filamu nchini Aunty Ezekiel kudaiwa kutoka na mh. Nyalandu mara baada ya kukutana nchini Marekani katikati ya mwezi September mwaka huu.

Aunty Ezekiel hakuzungumzia suala hilo mpaka sasa, hata hivyo Nyalandu amezungumzia suala hilo mbele ya waandishi wa habari baada ya magazeti kuandika habari ya yeye kudaiwa kuwa wapenzi na Aunty ikidaiwa ni ufujaji wa pesa za walipa kodi kwa alichokifanya kwenda kutanua na Aunty nchini Marekani. 
  
kwa mujibu wa Mtanzania, Nyalandu alijibu madai hayo kwa kusema kuwa hakutanua na Aunty na wala sio wapenzi bali alienda Marekani alipoalikwa kama mgeni rasmi wa tamasha la Utamaduni na Utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ikiwamo kuwatangaza wasanii kimataifa.Alisema tamasha hilo liliendeshwa na blog ya Vijimambo 13 September mwaka huu.

Alisema Aunty aliongozana na msaniii wa Bongo Fleva Cassim Mganga na safari yao iliratibiwa na waandaaji hao kwa ushirikiano na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na sio yeye aliyempeleka Aunty nchini humo bali alisema wabaya wake kisiasa wakiwemo baadhi ya watendaji wa wizara yake na baadhi ya viongozi wa serikali ndiyo humchafua kwenye media kutokana na kutopenda utendaji wake kazi mzuri wa kutotaka kushrikiana na majangili.

Mimi na Aunty tulionana siku moja tu tena usiku wa tukio ambalo lilifanyika 13 September 2014 kwenye kilele cha sherehe ya utalii na baada ya hapo sikuwahi kuonana naye tena” Alisema Nyalandu n a kuongeza:

Baada ya sherehe ya utalii Jumatatu nilisafiri kwenda California kuzindua kampuni ya utalii ya Tanzania Safari And Tourism inayomilikiwa na balozi wa heshima Ahmed Issa na sikurudi tena Washington, DC mpaka siku niliyoondioka

Aliingia ndani zaidi kukana madai ya kutoka na star huyo wa filamu kwa kusema “Sikuwahi kutanua na msanii huyu kama ilivyodaiwa lakini sishangai kwani mambo haya yamekuwa yakifanywa na genge la watu ambao miongoni mwao ni viongozi wa serikali na waliomo kwenye wizara yangu”

Huyo Aunty nimezoea kumuona au kumsikia kwa kupitia vyombo vya habari lakini kwa mtazamo wa watu hawa wanataka kumfanya kiongozi atakapofika kwenye mkutano wowote ule na kumkuta mdada maarufu basi akimbie”. Alisema Nyalandu ambaye mkewe Faraja Kota aliyetwaa taji la Miss Tanzania hiyo ni msomi pia huku akiwa hana skendo za ajabu ajabu kama baadhi ya mamiss wengine

Nyalandu alisema kuwa tayari amewatambua watu hao na kwamba yeye ataendelea na msimamo wake wa kulinda maslahi ya taifa hususani katika nafasi yake hiyo

Diamond Platnumz Afunguka Kiundani Juu ya Tetesi za Kuwa na Ugomvi na Ali kiba

$
0
0
Diamond na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa za mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao, Team Diamond v/s Team Alikiba, ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo Nasib Abdul amedai kuwa haipo.

Platnumz ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka juu ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa inazungumzwa baina yake na muimbaji huyo wa ‘Mwana’.

Nimekua nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana, kwenye mitandao katika nini, sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm 

Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.

Tangia mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo ilikua sijui kwa Belle 9, ilitoka kwa Belle 9 ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja sijui kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa Richard Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda unafanya vizuri hivyo vitu vinakua vinatokea, so ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa na upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si tatizo ni vitu ambavyo vitakuwepo tu kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika kazi inayofanana hivyo vitu vitatokea yaani watu watashindanisha, unaweza hata ukashindanishwa na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.

Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”

Diamond amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na tatizo na yeye anaamini angeweza kumfata na kumwambia sababu amefahamiana nae kabla hajakuwa mwanamuziki.

Sasa hivi yaani karibia mwaka wa tano, Mi tangia nianze kufanya muziki sijawahi kudrop kila siku nazidi kupanda juu…so hivyo vitu lazima vitatokea lazima nivikubali, inawezekana we unasema we unasema we hauna tatizo lakini mwenzio akawa anahisi wewe una tatizo nae, lakini naamini kama angekuwa anahisi kama mimi nina matatizo na yeye angenifata akaniambia kwa sababu mimi sijajuana na Ali kwenye muziki, nimejuana na Ali kabla sijakuwa mwanamuziki, nimemjua Ali kupitia dada yangu Queen Darleen so alikuwa an uwezo wa kunifata akaniambia personally kwamba bana umefanya hichi na hichi na hichi”.

Diamond amemaliza kwa kusema kuwaomba media na mashabiki wasifanye ionekane kama wana beef binafsi bali wazishindanishe kazi ili kukuza muziki wa Tanzania.

Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.

Mwanamke Kalio Bwana, Kama Sura Hata Mbuzi Anayo

$
0
0
Nimekutana na hii Mahali:

"Mwanamke mwenye kalio halali na njaa hapa town hata awe na sura mbaya vipi
Hakuna mwanaume atakayegeuka nyuma kumuangalia mwanamke mwenye sura nzuri
Siku zote wanaume wanageuka nyuma kuangalia mwanamke mwenye kalio la kutosha.

Wanaohongwa magari na nyumba wengi ni wenye makalio makubwa, wenye makalio kama wamepigwa pasi wanaishia kuhongwa vocha tu.

Achana na Wezere Bana......KALIO KWANZA, Sura peleka kwa mzee wako"

Je ya Kweli Hayo?

Usiruhusu Mumeo Afanyiwe Masaji na Mwanamke Mwenzio

$
0
0
Inabidi sasa wanawake tuanze kuwapa somo wenyewe manake inaonekana hamfundishani kabisa. Sababu kila kukicha Mambo ni yale yale.

Wanawake mmekuwa na tabia mume akikueleza anajisikia vibaya,mwili unamuuma haraka unamwambia nenda hospitali au unakwenda kumnunulia panadol apunguze maumivu, Mnakosea kabisa.

Kumbe daktari au nesi au mtabibu ni wewe mwenyewe, hebu nikupe siri moja wala usiniulize mchaichai nitaupata wapi, kwani uko mwingi sokoni na kwenye maduka ya dawa za asili. Chukua nazi zako, zikune halafu chuja taratibu mpaka upate tui zito, pika mafuta ya nazi, ule muda ambao tui lako liko jikoni chukua majani ya mchaichai changanya kwenye tui hilo wakati linachemka changanya na mdalasini pamoja na hiriki, acha tui lichemke mpaka ligande. Likishaganda unatoa mafuta mazuri yanayonukia kisha chuja na uweke kwenye chupa safi.

Muinue mumeo kamuogeshe, ikiwezekana hata kumbeba mbebe, mwanaume si mzito hata akiwa na uzito wa tani tano huwezi kushindwa kumbeba,mbona mkiwa kwenye mahaba uzito huuoni? Mume anafanyiwa kila linalowezekana ilimradi liwe halali kwa Mwenyezi Mungu. Mwanaume ni bahati, hawapatikani kilahisi. Hakikisha mume unamshikilia asikuponyoke. Siku hizi wanaume tumekua adimu hadi tunagombaniwa, walio na moyo mwepesi wanajichoma visu wengine wanakunywa sumu, unabaki unajiuliza kwani anayo ya dhahabu? Mwanaume ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na siri ya tungi aijuaye kata.

Sasa mbebe mumeo kisha kamuogeshe na baada ya hapo mkaushe kwa taulo laini siyo kwa kanga na usimsugue, taulo lina manyoya yake ambayo ni malaini na ni maalum kwa ajili ya kufutia maji, kanga inasugua ngozi si salama sana pia kwa sababu inatoa rangi.

Baada ya kukausha maji chukua mafuta yako umpake mwili mzima kisha fanya masaji taratibu, baadhi ya wanawake wanawapeleka waume zao kwenye vituo vya masaji wakafanyiwe masaji ya mwili, hivi kwa nini mumeo akashikweshikwe na mwanamke mwenzako wakati ufundi wewe unao?
Kama huna ndiyo huu nakupa.

Mpapase taratibu mumeo huku unamfanyia masaji, fika mpaka kwenye milima ya gorani, teremka taratibu kwenye bonde la Sinai, hapo sasa utakapofika kwenye bonde hilo sidhani kama maumivu yatakuwepo, lazima atataka chakula cha usiku hata kama itakuwa mchana atataka cha usiku tu Mlishe usimnyime chakula. Mimi nawasaidia Mahusiano yasiwashinde. Unashangaa mwenzio anadumu kwenye mahusiano unaanza kusema kaenda kwa mganga kumbe hujui anayo mfanyia Mpenzie. Chukua hatua. 

Watakucheka watu ukiachwa, Mara Nyingi Huko Kwenye Vituo vya masaje Mwanaume akiwa anafanyiwa hiyo masaje na Mwanamke ikilolea atataka na papucha ..Shauri Zenu 

Kizungumkuti:Utata Kura za Wajumbe wa Bunge la Katiba Waliokwenda Hijja

$
0
0
Utata umezidi kugubika kura mbili zilizowezesha kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa ambayo wiki iliyopita ilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mjini Dodoma.

Utata huo unatokana na kura za wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) upande wa visiwani, wajumbe waliokuwa Hijja, Saudi Arabia na zile za baadhi ya wajumbe wanaodaiwa kuhamishwa kinyemela kutoka Bara kwenda Zanzibar au kinyume chake.



Utata Saudia

Chanzo chetu kutoka Dodoma kilisema: “Kuna utata maana hakuna uhakika iwapo kweli mahujaji ambao ni wajumbe wa Bunge la Katiba walipiga kura maana kuna barua ilitoka ubalozini Saudi Arabia ikisema hilo lisingewezekana.”

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Ubalozi wa Tanzania Riyadh, uliandika barua kwa Bunge Maalumu la Katiba ukieleza kwamba usingeweza kuratibu upigaji kura kutokana na mazingira halisi ya ibada ya Hijja.

Miongoni mwa sababu zilizotolewa na ofisi ya ubalozi huo ni kwamba mtu yeyote ambaye si hujaji hakuwa anaruhusiwa kuingia katika maeneo ya Hijja na Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa imetoa vitambulisho maalumu kwa mahujaji tu.

Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alikiri kupokea barua kutoka Ubalozi wa Tanzania uliopo Riyadh, ukieleza kwamba mazingira yasingeruhusu wajumbe hao wanane kupiga kura, lakini akasema walitumia njia nyingine kufanikisha kazi hiyo.

“Tulipokea barua hiyo kweli na pengine niseme tu siyo moja, zilikuwa barua kama tatu au nne hivi, maana hata hapa foreign (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) Dar es Salaam walituandikia kuhusu ugumu wanaouona, lakini baada ya kuona hivyo tuliamua kutumia njia zetu wenyewe.

“Tulimtuma ofisa wetu kwenda Saudi Arabia na tulimkatia tiketi na kusema kweli wakati wote alikuwa akiwasiliana nasi, nakumbuka mtu wa kwanza kupiga kura alikuwa Raza (Mohamed, Mwakilishi wa Uzini) ambaye alikuwa Dubai na baada ya hapo alikwenda walikokuwa mahujaji wengine na walifanikisha vizuri sana,” alisema.

Wajumbe wengine waliokuwa Uarabuni kwa mujibu wa orodha iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta ni pamoja na Dk Abdallah Kigoda, Sheikh Mussa Kundecha, Hamza Mustapha Njozi, Dk Maua Daftari, Shawana Bukheti Hassan, Asha Mtwangi, Amina Andrew Clement na Riziki Lulida.

Laana za Ngoma za Vigodoro Bado Zaendelea Wamama Watu Wazima Washindana Kuvua Nguo

$
0
0



MAADILI YA MTANZANIA YANAPOROMOKO.
WANAWAKE watu wazima'Miji Mama' mwishoni mwa wiki iliyopita ilimwaga radhi hadharani eneo la Msamvu Magodolo jirani na kiwanda cha Komoa.

Miji Mama hiyo ambayo baadhi ya wake za watu walifanya uchafu huo kwenye sherehe ya kumtoa mtoto wa rafiki yao'Arobaini'.
Wanawake hao wambao wana kikundi cha kusaidia kwenye shida na raha walifanya sindano hilo la kuvua nguo 

PICHA:Trafiki Apokea Kichapo Ubungo Mataa

$
0
0
Dah Mwezi huu ni mwezi mgumu sana kwa hawa ndugu zetu wa usalama barabarani..Achiliambali wale ndugu zetu waliofukuzwa kazi..Leo hii majira ya mchana hapa mjini Dar es salaam, eneo la BUNGO mataa, Raia wenye hasira walianza kumshushia kichapo askali mmoja wa barabarani kwa kudaiwa kusababisha ajali....

Pichani ni Askali alipewa kichapo kidogo na kukimbilia kwenye bajaji ili ajisalimishe...jamani jamani ile kauli ya WAPIGWE TUU naona inatekelezwa sasa upande wao....hehehehhee natania tu:

Wanawake Wenye Hips na Shida Wanazokabiliana Nazo Kila Siku

$
0
0
Wanawake wengi wenye hips , ni wanawake ambao si kwa mwanaume tu hata kwa wanawake wenzie husifia kuwa fulani kajaliwa, ki maumbile, ni kweli wana mvuto wa pekee, humwagiwa sifa nyingi za urembo, lakini pia kwa upande mwingine wa shillingi ni matatizo tupu.

Sifa:

1. Huwatesa sana wakina baba wanapokuwa katika vyombo vya usafiri kama daladala, treni, meli na ngalawa, mababa wengi hujawa na hisia kali za mahaba kiasi kwamba hupata mfadhaiko.

2. Hawana haraka sana kwani mwendo wao, hutembea kwa maringo, hata daladala likisimamia mbali hawawezi kukimbia kuwahi.

3. Hutongozwa wanaume watano kwa siku, hata wanaume wasiposema kitu angalau ukonyeza.

4. Ni wasikivu sana wakati wa kudate maana wengi ni warefu hupenda sana kukuinamia kusikia zaidi uliongealo.
Matatizo.


1. Kwa kuwa huwa wanavutia sana ni rahisi kurubuniwa kwani mwanamke yeye duniani hawezi kutongozwa watu elfu 2000 asimpende mmojawapo.

2. Hawana raha kwani ukodolewa sana macho na watu, si wanawake wala wanaume.

3. Upata magonjwa sana asa fungus kwani sehemu zao za siri hazipati hewa ya kutosha kufatana na kubanana kwa nyama na msuguano kila watembeapo.

4. Wana gharama sana kuwatunza kwa sababu hawatakiwi kutembea kwa muda mrefu kuogopa msuguana hivyo umuoapo ni lazima ughalimike usafiri au unatakiwa kumunulia skin taiti kila mara kwa kuwa zinahariibika muda mfupi sehemu ya mapaja.

Matamshi ya Chris Brown Kuhusu Ugonjwa wa Ebola yanakera

$
0
0
Mwimbaji mashuhuri duniani ,Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.
''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown.
Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikimye.
Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.
Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema.
Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.
Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.

Habari ya kufukuzwa kwa askari polisi wa usalama barabarani wiki iliyopita imepata attention ya kimataifa.

$
0
0
Hii ni habari iliyoandikwa kwenye website ya BBC.

When is it OK to kiss a colleague? Two Tanzanian police officers, whose kiss was widely shared on social media, have prompted a discussion about just that – and both have also lost their jobs.

A relationship with a colleague can throw up any number of complications, but the two young police officers in the picture may not have thought it would end their careers. The photograph – taken in Kagera, north west Tanzania – shows the pair kissing whilst dressed in their work uniforms, and was considered grounds for dismissal. Residents of the country have taken to social media to voice their dismay.

The image was uploaded to the internet by a third officer, who also took the photo, and drawn to the attention of the authorities at the Kagera police force. Henry Mwaibambe, the regional police commander, spoke to the BBC about the steps taken, and defends his department’s decision. “We followed all disciplinary procedures to make sure that they were given a chance to defend themselves,” he says. “The officer looking at the case was convinced there was compelling evidence against them, and that they had breached police code of conduct. That’s why they lost their jobs.” In this case it wasn’t the kiss itself that led to their dismissal, but the fact that that it happened in public, whilst in uniform, and was subsequently posted online. Indeed, the officer behind the camera also lost his job over the incident.

The story was picked up by the local press last week, and news of the punishment has surprised many on social media. Most believed the response was disproportionate. “They should have been reprimanded, sacking them is extreme, huuh!” posted one on Facebook. “I once saw a pic of former US President the late Reagan kissing his wife in the Oval Office… and nobody called for his impeachment,” said another. “Police couple kissing taken more serious than bribery,” wrote a third on Twitter.

Masoud George, a lawyer at the Tanzania Legal and Human Rights Center says that as severe as the punishment seems, the decision is unlikely to be illegal. “It is according to their code of conduct, so from a legal point of view we can’t say their dismissal was unfair.”

Reporting by Sam Judah.

Hussein Machozi Asema Wimbo Wake wa Mdogo Mdogo Aliurekodi Kabla ya Diamond Kurekodi Wake, Akana Kuwa na Beef Nae

$
0
0
Week iliyopita Mtandao Maarufu wa Kenya unaitwa Ghafla ulitoa wimbo ambao unaitwa Mdogo mdogo wa Hussein Machozi Ambao kidogo Umefanana na ule wa Diamond wa Mdogo mdogo Kimahadhi ...
Hussein Machozi Ameibuka na Kusema Haya:

Yeah kuna wimbo upo masikioni mwa watu sasa hivi ambao haukupangwa kutoka hivi karibuni ila nashangaa kuukuta mitandaoni yaani umevuja”.

Hit maker huyo wa ‘Kwa Ajili Yako’ amesema kuwa wimbo huo ameurekodi miaka miwili iliyopita, na si kama ambavyo watu wanadhani kuwa huenda ameutoa kumjibu Diamond.

Wimbo umerekodiwa miaka miwili nyuma na sikuwa najua kama Diamond nae ana wimbo kama huo. Wakati naufikiria kuutoa ndio nikasikia Diamond ametoa wakwake nae ameuita mdogo mdogo. Nilijaribu sana kubadilisha jina ila haikuwezekana kulingana na maana nzima ya wimbo, mimi nikauacha nikasema wacha niutulize hadi ya bwana Diamond ipite nami nitautoa wangu, ila nimeukuta kwenye mitandao sina jinsi.”

Kuhusu nani anayehusika kuuvujisha na hatua zozote alizochukua:

Nadhani ni producer maana hakuna aliyewahi kua nao huu wimbo zaidi ya mimi na producer Toti. Sijachukua hatua zozote zaidi ya kumuuliza na alivyokataa basi nikawa sina jinsi tena maana tayari watu wanao sasa huu wimbo siwezi waambia rudisheni au uacheni, nimeuacha uende tu.”

Kuhusu sababu anazohizi zimefanya wimbo wake upambanishwe na mdogo mdogo ya Diamond, je ni kweli ana beef nae?:

Hapana mimi sinaga beef na mtu kwa kweli beef labda kikazi tu, mimi naona sio mbaya maana sisi ni wanamuziki na hiyo ni kazi yetu na wao pia wamefanya kazi yao ambayo wanaona inawafaidisha wao, angekuwa mtu mwingine au wimbo ni wa kawaida tu wasingeweza kumuweka hapo na Diamond au kumuandika kivyovyote. So wameona mimi nastahili na pia inastahili ni kali namaanisha ndio maana wameiweka hapo, mimi naona ni sawa tu”.

Shirika la Ndege la Fast Jet Lalamikiwa Kuwa ni Kimeo, Wateja Walalamika

$
0
0
Stori: Ojuku Abraham
SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.

“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.

Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air Tanzania.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.

“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.

Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.

“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia kuwaambia wafanyakazi wa ndege kuwa waniangalizie vitu vyangu pale nilipokaa, lakini jambo la ajabu eti wakadai hawakuviona, wakati mimi nilikuwa msafiri wa mwisho kushuka kwenye ndege, ina maana hakukuwa na mwingine baada ya mimi kushuka ambaye ningeweza kusema l ndiye aliyechukua vile vitu,” alisema Shomari ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na Radio One, kwa sasa anafanya kazi Sauti ya Amerika (Voa) jijini Washington, Marekani.

Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.

Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi za Fast Jet zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutaka maelezo ya uongozi kuhusu tuhuma hizo, lakini walinzi walimzuia kuingia ndani na kutakiwa kuchukua anuani ya barua pepe ya msemaji wake, kwa maelezo kwamba ndiye angeweza kumsaidia kwa mambo ya kihabari.

Mwandishi aliandika madai yote na kuyatuma kwenye anuani hiyo akitaka kuonana na uongozi kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa, lakini afisa uhusiano aliyejibu ujumbe huo, Lucy Mbogoro, baadaye alilitaka gazeti hili kuandika maswali hayo na kuyatuma, sambamba na nakala ya sura ya mbele ya gazeti.
Lakini hata baada ya kutuma maswali hayo kama ilivyotakiwa, Fasjet wameshindwa kutoa majibu na Lucy alipopigiwa simu na kuulizwa, alidai anayehusika na majibu hayo ametingwa na kazi.

Hata hivyo, gazeti hili bado linafuatilia kwa karibu ili kupata majibu ya maswali hayo.
GPL


Diamond Platnumz Apata Aibu Nyingine, Dodoma Napo Pamnukia Afanya Show na Muziki wa Kigodoro

$
0
0
Stori: Richard Bukos, Dodoma
KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.

Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.


Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.

Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.

Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.

Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.

Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.

“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka betri mpya kwenye maiki?

Wagonjwa wa Akili walala Wodi Moja na Wagonjwa wa Kawaida

$
0
0

Hospitali kongwe ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, inakabiliwa na upungufu wa wodi za kulaza wagonjwa na kulazimika kuwachanganya wagonjwa wenye matatizo ya akili na wale wenye  maradhi mengine.

Muuguzi wa hospitali hiyo, Bahati Kuguru, alisema hospitali hiyo ni miongoni mwa zile zinazofanya kazi katika mazingira magumu hasa ya kutokuwa na wodi maalum za kulaza wagonjwa hali inayohatarisha usalama wa wagonjwa na wauguzi.

 “Serikali iangalie namna ya kunusuru hali hii haraka iwezekanavyo kwa sababu wagonjwa wenye matatizo ya akili kitabibu wanahitaji kulazwa wodi maalum peke yao, vinginevyo wanaweza kuleta madhara kwa wagonjwa wengine na wauguzi pia,” alisema Kuguru.

Pia alisema chumba cha kuhifadhia wagonjwa  cha hospitali hiyo ni kidogo na hakina majokofu jambo linalosababisha ndugu kulazimishwa kuchukua miili ya ndugu zao muda mfupi baada ya kufariki dunia.

Aliongeza kuwa ingawa serikali inazitambua changamoto zilizoko, bado haijashirikiana na hospitali hiyo katika kuboresha mazingira halisi badala yake miundombinu yake inazidi kuchakaa.

“Tunaomba serikali ichukue maamuzi magumu katika kutatua suala hili, kwanza itupatie gari ya usafiri itakayotumika kutoa huduma ndani na nje ya hospitali pale inapobidi pamoja na kujenga majengo yatakayojitegemea kutokana na tatizo la wagonjwa,” alisema Kaguru.

Mgonjwa wa matatizo ya akili aliyelazwa katika wodi ya wananwake katika hospitali hiyo, Roida Mwangaya, alisema serikali iboreshe hospitali hiyo kwa sababu ni kitovu cha wakazi wa ndani na nje ya eneo hilo.

“Ipatikane wodi  maalumu za kulaza wanawake, watoto, wanaume pamoja na kitengo maalum cha kuwalaza na kuwalea wagonjwa wa matatizo ya akili,” alisema Mwangaya.

CHANZO: NIPASHE

Familia ya Mwal Nyerere yasusia Maadhimisho ya Nyerere Day-Tabora

$
0
0
Mmoja wa watoto wa Mwal. anasema hakuna dhamira ya dhati ya kumuenzi Mwal. Nyerere, kwani siku ya maadhimisho watu wanazihusisha na uzimaji wa Mwenge.
"Tumeamua kumuenzi hapa hapa Nyumbani" Alisema

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images