Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Jumatatu

0
0

Wanajeshi wa Nigeria Wagoma Kwenda Vitani Kukabiliana na Boko Haram

0
0
Wanajeshi wa Nigeria wagoma kwenda vitani kukabiliana na Boko Haram
Kikosi kimoja cha majeshi ya Nigeria kimefyatua risasi angani kupinga amri ya kwenda mstari wa mbele kukabiliana na wanamgombo wa Boko Haramu.

Vyombo vya habari vya nchi hivyo vimeripoti kuwa askari alikataa kupanda ndege ambayo ilikuwa iwahamishe kutoka Maiduguri katika mji mkuu wa jimbo la Borno kwenda katika mji wa Marte karibu na nchi jirani ya Niger.

Hali hiyo hakutarajiwa lakini ndivyo ilivyotokea katika jeshi la Nigeria siku ya jumapili, ambapo wanajeshi wa kikosi kimoja walipoonyesha kukataa kwenda mstari wa mbele kukabiliana na Boko haramu.

Mwandishi wa BBC anasema kumekuwepo na hali ya kutotii amri miongoni mwa wanajeshi kwa miaka nane sasa.

Kundi la Boko haramu limekuwa liikiendesha vitendo vya utekaji mauaji na hata vitendo vya ubakaji na ukatili.

Kumekuwa na maswali mengi kutoka miongoni mwa raia kufuatia kundi hilo kuendelea na vitendo vya kikatili huku majeshi Nigeria yakidai yanalidhibiti.

Kamishna Mkuu TRA Aagiza Ukaguzi Saa 24 Mipakani

0
0
Kamishna Mkuu TRA Aagiza Ukaguzi Saa 24 Mipakani
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Charles Kichere, ameagiza maofisa wake kufanya ukaguzi wa saa 24 katika maeneo yote ya mpakani ili kutokomeza biashara ya magendo.

Vilevile, amesema chombo chochote cha moto kitakachohusishwa na ubebaji wa bidhaa za magendo kitataifishwa kwa mujibu wa sheria.

Kichere alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na maofisa kutoka TRA, Uhamiaji, Jeshi la Polisi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alipotembelea mipaka ya Tarakea, Rombo na Holili kuangalia utendaji katika mipaka hiyo. 

"Ningependa kuona kila ofisa aliyeko hapa anafanya kazi kwa bidii akijua ya kuwa mapato yanayokusanywa hapa siyo kwa ajili ya TRA tu, ndiyo yanayopelekea kupatikana kwa mishahara ya watumishi wa umma, huduma za afya, shule pamoja na bararaba za kisasa," alisema Kichere.

Aliongeza kuwa kufumbia macho suala la magendo ni kinyume cha maadili na kunaikosesha serikali mapato kwa kuwa bidhaa hizo zinaingizwa bila kulipiwa kodi na kuuzwa kwa bei ya chini na kusababisha bidhaa halali kukosa soko.

"Tuwatumie vyema wananchi wanaoishi mipakani ili wawe mabalozi wazuri wa kulinda kodi zao pamoja na kuwataja wale wote wanaohusika kwa njia moja ama nyingine kupitisha magendo lakini pia tuwe makini kwani baadhi yao wanatumiwa na watu wasio na nia nzuri," alisema.

Kichere pia alitoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa kwa TRA wanapoona watu wanapitisha bidhaa katika njia zisizo rasmi na kuwataka kuwa wazalendo na kutumia bidhaa zinazopatikana nchini.

"Najua kati yenu kuna maofisa ambao siyo waadilifu na ndiyo wanaotumika kutoa taarifa na kushirikiana na wafanyabiashara za magendo, watu hao sitawafumbia macho nitawafukuza kazi na kutaifisha mali zote walizochuma," alisema.

Kichere aliahidi kushirikiana na wakuu wa taasisi zilizopo mpakani kuwachukulia hatua maofisa wote watakaojihusisha au kushirikaina na wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kodi.

Salma Kikwete Aonya Wasioandikisha Watoto

0
0
Salma Kikwete Aonya Wasioandikisha Watoto
MKE wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Salma Kikwete, ameshauri serikali kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao hawawaandikishi watoto wao wanapozaliwa kupata vyeti kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mama Salma alitoa ombi hilo mwishoni mwa wiki, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu barani Afrika, ambayo kitaifa yalifanyika katika Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama, Kibiti mkoani Pwani.

Sherehe hizo zilizoadhimishwa kwa mara ya kwanza barani Afrika, ziliambatana na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi 200 wa shule hiyo, vilivyotolewa na Wakala wa Usajili na Udhamini (Rita).

Salma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), alisema kutomsajili mtoto ni kumnyima haki ya msingi na kuinyima serikali taarifa muhimu za maendeleo, na kwamba wazazi ambao watoto wao hawakupata huduma hiyo wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

“Kama hawatawapeleka watoto wao kusajiliwa nafikiri ni vyema kuchukua hatua kali zinazostahili ili kumsaidia mtoto asije akapata matatizo baadaye, kwa kuwa utambulisho wa mtoto ni haki yao na hawastahili kunyimwa kwa kuwa hahitaji kulipia zaidi ya mzazi au mlezi kumpeleka mtoto kituo cha kuandikisha,” alisema Salma.



Alisema mzazi anaweza kumsajili mtoto na kupata vyeti katika ofisi za watendaji kata na vituo vya tiba, ambavyo ni rahisi kwa wananchi kufika, na kuwataka watu kuitikia wito na watoto wao kupata vyeti.

“Huduma imepelekwa kwenye maeneo wanayoishi halafu ni ya bure, hakuna sababu ya mzazi kushindwa kumwandikisha mtoto wake na akifanya hivyo anamnyima haki ya msingi,” alisema.

Mama Salma ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema kuwa matumani ni kuwa Watanzania wote watapata huduma ya kusajiliwa kwenye matukio muhimu ya maisha yake, na hivyo kuwa na matukio halisi kwa kadri ya mpango kazi.



Alisema changamoto kubwa ni wananchi kufikia huduma ya usajili kwa kuwa hutembea umbali mrefu kutoka vijijini hadi wilayani na kwamba ndicho kikwazo kikubwa katika usajili wa matukio hayo muhimu.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Rita, Emmy Hudson, alisema usajili wa matukio muhimu ya binadamu husaidia nchi kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

Alisema wameamua kutumia maadhimisho ya siku hiyo kutoa vyeti kama njia ya kuhamasisha wananchi umuhimu wa kuwa navyo na kwamba mwendelezo wa juhudi mbalimbali za kuboresha mifumo ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa nchi za Afrika.



Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Rita, Prof. Khamis Dihenga, alisema wameshusha huduma za usajili wa matukio muhimu ya binadamu hadi ngazi ya kata na kwa kupitia mfumo maalum kila mtoto anayezaliwa anaandikishwa wakati huo huo na kupewa cheti na wameshaifikia mikoa 11.

Alisema Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ilibainisha kuwa asilimia 13 ya Watanzania ndiyo wenye vyeti vya kuzaliwa na kwamba kwa kasi ya Rita wamefikia asilimia 25, lengo likiwa kila Mtanzania kusajiliwa.

“Tunataka kila mtoto anayezaliwa kupata cheti kabla ya kutoka hospitalini, tunataka ifike mahali Mkuu wa Wilaya au ofisa yeyote anaweza kuangalia taarifa za watu wake kupitia kanzi data, itasaidia kupanga shughuli za maendeleo na kupeleka huduma kwenye maeneo husika,” alisema.

Naye Mkuu wa shule hiyo, Mwajuma Mbuguni, alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 337 wa kidato cha kwanza hadi cha sita, ambao wanalipiwa ada kwa asilimia 100 na wahisani mbalimbali ikiwamo taasisi ya Wama na wanatoka maeneo yote ya nchi.

Alisema kati ya wanafunzi hao, 30 pekee ndiyo wanalipiwa ada na wazazi wao na sifa zinazotumika kuwachagua ni walio na wazazi, lakini wanatoka familia duni, mazingira hatarishi na yatima.



Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa shule, maendeleo ya kitaaluma ni mazuri kwa kuwa matokeo ya kidato cha nne kati ya wanafunzi 85, saba walipata daraja la kwanza, 32 daraja la pili, 27 daraja la tatu na 17 daraja la nne huku mmoja akipata sifuri.

Aidha, matokeo ya kidato cha sita wanafunzi 10 walipata daraja la kwanza, 23 daraja la pili, 18 daraja la tatu na kushika nafasi ya 26 kimkoa na kitaifa nafasi ya 117 kati ya shule 543.

Mbuguni alisema kati ya wanafunzi 44 wameendelea na masomo katika vyuo vikuu mbalimbali nchini na saba wataenda kusoma stashahada.

Ronaldo Hali Tete Alazwa Hospitali

0
0
 Ronaldo Hali Tete Alazwa Hospitali
Nyota wazamani wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo amelazwa hospitali ya Ibiza kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 ameripoti kupitia mtandao wake wa twitter kuwa amefikishwa hospitalini hapo siku ya Ijumaa na kutarajia kupata ruksa leo siku ya Jumatatu.



Ronaldo amefunga jumla ya mabao 62 akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil yakiwemo magoli mawili aliyoifunga Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2002.

Nyota huyo wazamani wa klabu za Real Madrid, Barcelona, Inter Milan pamoja na AC Milan amewashukuru mashabiki zake kwa kumtakia afya njema.

Ronaldo ameshinda mataji mawili ya La Liga akiwa na Real na Uefa Cup akiwa na Inter.

Amekuwa sehemu ya kikosi cha Brazil ambacho kimetwaa taji la kombe la dunia mwaka 1994 na kuiwezesha timu hiyo kufika fainali mwaka 1998.

Lakini pia amewahi kutwaa taji la Ballon d’Or mara mbili mwaka 1997 na 2002.

Makamba "Nawashangaa Wanaoshangaa Mtatiro Kuhamia CCM..Lowassa na Sumaye Je?

0
0

Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba amesema wanaoshangaa hatua ya Julius Mtatiro kutoka CUF, kuingia CCM wanapaswa kujiuliza kama walishangaa wakati mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye walipohamia upinzani.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo

NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara

FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

AY Apata Mtoto wa Kwanza wa Kiume

0
0
AY Apata Mtoto wa Kwanza wa Kiume
Mke wa msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Ambwene Yessayah aka AY aitwaye, Remy siku ya jana amejifungua mtoto wa kwanza wa kiume huko Dallas -Texas nchini Marekani.


Jumatatu hii rapa huyo ameutaarifu umma kwamba mke wake huyo amepata mtoto wa kiume aitwaye Aviel ikiwa ni miezi 6 toka wawili hao waingie kwenye maisha ya ndoa.


“Mungu ni mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na My Beautiful Wife #Remy tarehe 12.08.2018 Medical City Healthcare Dallas -Texas tumepata mtoto wa kiume AVIEL maana yake GOD IS MY FATHER…. 3.9Kgs & 27 inches…Welcome to the World AVIEL YESSAYAH 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿,” aliandika rapa huyo kupitia instagram yake.


Baada ya Ndoa ya Kwanza Kuota Mbawa Mafufu Kuoa Tena Agost 25

0
0
Baada ya Ndoa ya Kwanza Kuota Mbawa Mafufu Kuoa Tena Agost 25
UBUYU ukufikie kuwa, harusi ya mwigizaji mkongwe wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu inatarajiwa kuruka hewani ‘live’ itakapofungwa jijini Dar, Agosti 25, mwaka huu.

Taarifa iliyolifikia Ijumaa Wikienda ilieleza kuwa, shughuli hiyo itarushwa kupitia Televisheni ya Wasafi ikiwa ni sehemu ya kuonesha umuhimu wa ndoa hiyo ambapo Mafufu anaoa kwa mara ya pili baada ya ndoa yake ya kwanza kuota mbawa.

Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mafufu alisema kuwa, ameamua kufanya hivyo kwa sababu yupo tayari kufanyiwa mahojiano yoyote na waandishi wa habari hata kama yatakakuwa yanamhusu yeye na mwanamke wake wa zamani atayajibu ili kila mtu ajue kilichotokea awali.


“Unajua nilipotaka kuoa niliongea na Mungu kupitia njia ya sala na hata sasa siku yangu hii itakuwa ikionekana hatua kwa hatua kwenye televisheni na nipo tayari kuulizwa chochote kinachohusiana na ndoa yangu mpya na hata ile ya zamani.

Mafufu aliongeza kuwa, kikubwa anamshukuru Mungu kwani anatarajia kufunga ndoa na mwanamke ambaye anamjua vizuri tangu wakiwa watoto wadogo na hadi familia zinajuana vyema.

Asilimia 70 ya Migogoro ya CUF Imechangiwa na Mtatiro, Bora Ameondoka- Kambaya

0
0
Asilimia 70 ya Migogoro ya CUF Imechangiwa na  Mtatiro, Bora Ameondoka- Kambaya
Mkurugenzi wa habari, uenezi na uhusiano wa umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ndani ya chama hicho imechangiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la uongozi chama hicho, Julius Mtatiro.

Kambaya amesema hayo  ikiwa ni siku moja baada ya Mtatiro kujiengua CUF na kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mtatiro ambaye alikuwa upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, alitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM  Agosti 11, 2018.

Kambaya amesema Mtatiro alipokuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu alisababisha chama hicho kugawanyika kwa kutosikiliza maoni ya wajumbe wa mkutano huo na kuamua kuuendesha kibabe.

Ameongeza kuwa Mtatiro alipokuwa Naibu Katibu mkuu alikiingiza chama hicho katika mgogoro uliosababisha Hamad Rashid kufukuzwa uanachama baada ya kuhoji ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh300milioni katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.

“Hakuna kitu ambacho Mtatiro amekifanya kwenye chama hiki, kubwa zaidi amesababisha migogoro. Wanasiasa wapambanaji hawakimbii  migogoro ndani ya vyama vyao bali wanakaa humo humo mpaka migogoro itakapokwisha” amedai Kambaya.

Kambaya ambaye  yupo upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa; “Tazama Sophia Simba hakukimbia CCM sambamba na Nape Nnauye (mbunge wa Mtama-CCM). Hata Mnyika (John-Mbunge wa Kibamba-Chadema) hakukimbia chama hicho.”

Lowassa Akanusha Madai ya Kutaka Kuhamia CCM...." Sina Huo Mpango, Msinigombanishe na Rais"

0
0
Lowassa Akanusha Madai ya Kutaka Kuhamia CCM...." Sina Huo Mpango, Msinigombanishe na Rais"
Hatimaye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amejibu mapigo ya taarifa zilizokuwa zimesambaa kuwa anawatanguliza watu CCM ili baadaye  ahamie.

Akizungumza mwishoni  mwa wiki iliyopita katika jimbo la Monduli, Lowassa alikanusha vikali taarifa hizo akidai kuwa wanaoeneza taarifa hizo ni waongo na wambea.

Mbunge huyo wa zamani wa Monduli ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani alimjibu aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga akimtaka aweke wazi sababu zilizomfanya ahame  kwakuwa ni haki yake ya kikatiba bila kutumia jina lake kwa uongo.

“Waambieni waache umbea na uongo. Anasema uongo kwa kinywa chake. Mimi nimtangulize kwani mimi sina miguu?” alisema Lowassa huku akisisitiza kuwa hana mpango huo.

“Wanasema eti mimi nimekubaliana na Magufuli kuwahamisha wabunge kwenda CCM. Acheni kunichonganisha na Rais, mimi sina mpango wowote na [Rais] Magufuli,” alisema.

Aliongeza kuwa kinachofanywa na wanaohama ni haki yao na wanapaswa kuwaeleza ukweli wananchi kuwa ni shida zao binafsi. Aidha, alimvaa Kalanga akidai kuwa alikuwa na mikopo ambayo imelipwa na kumfanya ahame.

Lowassa ambaye alikuwa mbunge wa Monduli kwa miaka 20, aliwataka wananchi hao ‘kumtoa tongotongo’ kwenye uchaguzi wa Ubunge wa marudio akiahidi kuwa angerejea hapo kwa ajili ya kufanya kampeni za ubunge.

Aliwataka wananchi wa eneo hilo kupuuzia taarifa kuwa hakuna maendeleo ambayo yanafanyika Monduli akiwataka kukumbuka maendeleo ambayo waliyashuhudia alipokuwa mbunge.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliwahakikishia wana Monduli kuwa bado yuko imara kwenye kambi ya upinzani na kuwataka kutoyumba huku akitolea mfano Nigeria ambako wanasiasa takribani 600 wamehama vyama vyao. Alisema suala la kuhama vyama ni la kawaida kwa wanasiasa  hivyo lisiwashtue bali liwafanye wawe imara zaidi.

Joto la uchaguzi wa Ubunge Monduli limeanza kupanda baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Julius Kalanga kujiuzulu na kujiunga na CCM kisha kuchukua fomu ya kugombea tena.

Chadema ambao watakuwa na kibarua cha kutetea jimbo hilo wako katika hatua za kuwachuja walioomba kugombea akiwemo Freddy ambaye ni mtoto wa Lowassa.

Nape Nnauye: Zitto Unajua Nakuheshimu Sana Huo Uongo Unaoutunga ni kwa Faida ya Nani?

0
0
Nape Nnauye: Zitto Unajua Nakuheshimu Sana Huo Uongo Unaoutunga ni kwa Faida ya Nani?
KUFUATIA Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuweka mtandaoni matokeo ya awali ya Ubunge wa Jimbo la Buyungu, Kakonko mkoani Kigoma akisema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshindwa katika kata 12 kati ya 13, kada wa CCM, Nape Nnauye ameibuka na kumjibu hoja yake huku akisema anamuheshimu hivyo aache uongo.

Jokate Aapa Kupambana na Wazazi, Walezi Wasiowapeleka Watoto Shule

0
0
Jokate Aapa Kupambana na Wazazi, Walezi Wasiowapeleka Watoto Shule
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo amesema atawachukulia hatua za kisheria wazazi au walezi wasiowapeleka watoto shule.

Alisema hayo juzi alipofanya ziara katika shule za msingi Chazige A na B alikokutana na wananchi na kusikiliza kero zao.

Jokate alisema mzazi au mlezi asiyempeleka shule mtoto hasa wa kike hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo kupelekwa mahakamani.

Alisema wataendelea na kampeni ya “Tokomeza Ziro” yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu na miundombinu ya shule, madarasa na vyoo.

Naye ofisa elimu msingi wilayani Kisarawe, Shomari Bane alisema: “Kampeni imetusaidia, wanafunzi kuanzia mwaka jana ufaulu darasa la saba uliongezeka na walifanya vizuri.

Pia, Jokate alimuagiza mganga mkuu na madaktari wilayani Kisarawe kutoa dawa zilizopo hospitalini kwa wagonjwa na kama hazipo, watoe mbadala ili wananchi wasipate usumbufu.

Polisi Mkoani Kigoma Imekamata Silaha ya Kivita Aina ya AK47

0
0
Polisi Mkoani Kigoma Imekamata Silaha ya Kivita Aina ya AK47
Polisi mkoani Kigoma imekamata silaha ya kivita aina ya AK47 katika tukio la ujambazi ambalo lilisababisha vifo vya watu wanne.

Katika tukio hilo lililotokea Ijumaa iliyopita, polisi waliwaua watu watatu walipokuwa katika msako wa kuwasaka watuhumiwa wa ujambazi waliomuua Lukas Luchapa (38), saa tano usiku katika Kijiji cha Kigina, Kibondo.

Mbali ya kuwa na silaha hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno alisema jana katika tukio hilo walikamata pia risasi 69 na magazine tatu kwamba bunduki hiyo ina usajili wa Burundi.

Alisema watu hao walimuua Luchapa kwa kutumia silaha hiyo walipomvamia akiwa ametoka kunywa pombe.

Alisema awali, walitaka kuweka magogo barabarani kuzuia magari kabla ya mtu huyo akiwa ameonekana kama amepotea njia kutokea na kuanza kumshambulia kwa risasi za kichwani na mguuni.

“Tulipata taarifa hizo kwa kushirikiana na wananchi wa kijijini na tulifuatilia na kugundua walikuwa watu kama saba,” alisema Kamanda Ottieno.

Alisema askari wake walianza kuwasaka watu hao na kukutana nao katika msitu ulio karibu na kijiji hicho na kuanza majibizano ya risasi.

Alidai kwamba mmoja wa watuhumiwa hao aliuawa alipokuwa akijaribu kuwashambulia polisi kwa risasi.

Kamanda Ottieno alisema msako unaendelea kuwatafuta watu wanne waliokimbia kwa kuwasiliana na nchi jirani ya Burundi.

“Niwaombe wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kutoa taarifa pale wanapomuona mtu mgeni na kumtilia shaka kijijini,” alisema Ottieno.

Hii Hapa Orodha ya Walioteuliwa na Rais Magufuli leo

0
0
Hii Hapa Orodha ya Uteuzi Alioufanya Rais Magufuli leo
Leo August 13, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amefanya teuzi mbalimbali siku ya leo na kufanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Msafiri Simeoni wa Kwimba amepelekwa Chato, Senyi Simon amepelekwa Kwimba

Wafuatao ni baadhi ya walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji

Halmashauri ya Misenyi Mkurugenzi ni Innocent Mbandwa

Jiji la Mbeya Mkurugenzi ni James Kasusura

Halmashauri ya Malinyi Mkurugenzi ni Mussa Elias Mnyeti

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ni Maulid Madeni

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke ni Lusibilo Mwakabili

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo ni Beatrice Kwai

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni ni Mwilabu Nyabusu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa mkoani Dodoma ni Mustapha Yusuph

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi ni Tatu Seleman Kikwete

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko ni Masumbuko Stephano

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Katavi ni Ramadhan Mohamed

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Butiama ni Mugalane Alphonce

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kyela ni Lucy Mganga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombelo ni Eng. Stephan Kaliwa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa ni Asailiwe Lucas

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe ni Esther Chaula

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru ni Emmanuel Mkongo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Simiyu ni Michael John

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi ni Justice Laurenc

Breaking: Mbunge Mwingine CUF Ajiunga na CCM Apokelewa Lumumba

0
0
Mbunge wa CUF Aliyehamia CCM Apokelewa Lumumba
Mbunge wa Liwale kupitia CUF, Zubeir Kachauka aliyejivua ubunge wake na uanachama wake na kujiunga na CCM hivi karibuni  leo amepokelewa katika ofisi za Makao Makuu ya Chama cha CCM na Katbu Mkuu wa Chama hicho, Dk Bashiru Ally

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:


FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.


NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Young Dee Autema Uongozi Wake...Adai Kwasasa Ana Kampuni yake

0
0

Paka Rapper Young Dee kwa mara ya kwanza amesema kuwa amefungua Kampuni yake mwenyewe ambayo itasimamia kazi zake za sanaa na ameachana na Habari za kuwapa watu wengine wasimamie kazi zake za muziki.

Exclusive Young Dee ameongeza kuwa Wiki ijayo ataachia wimbo wake mwenyewe na kwa mara ya kwanza hiyo itakuwa ndio itakuwa kazi ya kwanza kutoka kwenye Kampuni hiyo ambayo ataitambulisha rasmi kwa mashabiki zake.

Kauli ya Kubenea Kuhusu kujiunga CCM

0
0

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amefunguka kuhusu taarifa zinazodai yuko mbioni kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Tangu mwaka jana, wimbi la viongozi, wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM lilipoanza, Kubenea amekuwa akihusishwa na mpango wa kuihama  Chadema na kujiunga na chama tawala. 

Juzi aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akitetea uamuzi wa viongozi wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM. 

Ujumbe huo wa mbunge huyo anayefahamika kwa kutoa habari nyingi za msingi wa makatazo na machukio dhidi ya watu walio mafisadi nchini akiwa mwandishi wa habari, ulisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua mjadala kutokana na kuhusishwa kwake kwa muda mrefu kujiunga na chama tawala. 

Ujumbe huo ulisomeka: "Si wote wanaohama wamenunuliwa, ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya waliohama wamenunuliwa. Kuna wengine wamehama kutokana na kuwapo migogoro, chuki na ubaguzi katika maeneo waliyokuwapo." 

Alipotafutwa na Nipashe jana, Kubenea alikiri kuuandika na kueleza kuwa kuhamia CCM kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, kulimsukuma kuandika ujumbe huo. 

"Ujumbe huo ni kweli ni wa kwangu," Kubenea alisema, "niliandika baada ya Julius Mtatiro kutangaza kuhama CUF na kujiunga na CCM.  

"Inawezekana hakunuliwa, lakini inawezekana njaa ndiyo imempeleka huko kwa sababu kwanza ukumbuke chama chake kina mgogoro mkubwa, pia upande aliokuwa yeye, hakuna ruzuku. Kwa hiyo, hawakuwa na pesa ya kujiendesha na ndiyo maana akaona ahame tu. 

"Nasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao mimi nawafahamu, walihama na hawakununuliwa isipokuwa walishindwa kuvumilia baada ya kukutana na watu ambao walitofautiana nao kimawazo, yaani mawazo yao yalikinzana, wao badala ya kuvumilia walishindwa." 

KUHAMIA CCMAlipoulizwa na Nipashe kuhusu kama naye ni miongoni mwa wanaodaiwa wako kwenye foleni ya kujiunga na CCM, Kubenea alisema hana mpango wa kukihama chama chake kwa sasa. 

"Mimi sina kabisa mpango wa kuhama chama changu (Chadema), hicho nilichoandika yalikuwa ni maoni yangu tu baada ya Mtatiro kuhama na si vinginevyo, watu wasahau kabisa na wasifikirie kwamba mimi naweza kuhama," Kubenea alisema na kueleza zaidi: 

"Unajua vyama vya siasa siyo madhehebu ya dini, misikiti au makanisa kusema watu wasipishane mitazamo, vyama vyote vya siasa watu wanapishana mawazo na mitazamo. 

"Na hiyo sioni kama ni sababu kubwa ya kukufanya eti uhame, kwani huko unakokwenda wenyewe hawatofautiani? Mbona kila chama watu wanatofautiana?" 

Kubenea alichaguliwa kuwa Mbunge wa Ubungo baada ya kushinda uchaguzi wa Oktoba 25, 2015. Ni mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd na katika kutekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari, alifahamika kwa kuandika habari za kufichua ufisadi. 

Januari 5, 2008, alivamiwa ofisini kwake na kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.

Chris Brown Apagawa na Umbo la Rihanna Akiwa na Bikini, Ataka Asipunguze Mwili

0
0

Baada ya mwanamuziki kutoka Marekani Rihanna kuliambia jarida la VOGUE mipango yake ya kurudi gym kwa ajili ya kupunguza mwili, mpenzi wake wa zamani ambae pia ni mwanamziki maarufu duniani, Chris Brown ameonekana kusikitiswa na kauli aliyosema Rihanna kwamba atarudi gym kupunguza mwili kwani Breezy anapenda muonekano wa mwili wa mwanadada huyo, jinsi alivyoongezeka mwili na jinsi anavyopendeza akivaa bikini, alisema rafiki wa karibu na Chris Brown kupitia HollywoodLife. - #regrann
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images