Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

"Kipimo cha Msanii ni Tuzo"- Joh Makini

$
0
0
Rapa kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka na kudai, kutokuwepo kwa tuzo nchini kumesababisha kuwatia ulemavu wasanii wengi kwa kutokufanya vizuri kwenye 'game'.


Akizungumza na www.eatv.tv hii leo Joh Makini amesema tuzo ilikuwa inampa hamasa msanii kwa kuendelee kuumiza kichwa, juu ya kutoa ngoma kali kusudi aweze kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha tuzo.

"Tuzo ni kitu cha msingi na kipimo tosha kwa msanii kuwa ana uwezo kiasi gani ila kwa sisi Weusi, tunajua nini tunafanya na tunaamini ni wakali ndio maana huwa tunafanya vitu vingi ambavyo vinawashangaza watu", amesema Joh Makini.

Aidha, Joh Makini amesema msanii ni mfano wa mwanafunzi ambaye yupo shuleni kwa lengo la kusoma kwa bidii na kuweza kushika nafasi ya kwanza au pili, kusudi mtu huyo apate zawadi fulani au sifa nzuri nyumbani kwao au kwa majama zake kwa kile alichokifanya.

Mbali na hilo, Joh Makini amesema sababu kubwa ya wasanii wa hiphop kushindwa kufanya vizuri, ni kutokana na mipaka waliyojiwekea wakati sanaa wanayoitumikia haipo hivyo, huku akimtolea mfano 'role model' wake Jay Z kuwa kila siku anabadilika na kuwa mpya kutokana na mahitaji ya mashabiki zake wanavyotaka na soko kiujumla.

EATV

Diamond Athibitisha Kushusha Mjengo Mwingine Afrika Ya Kusini

$
0
0
Staa wa muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vyema hivi sasa na ngoma  yake ya ‘Jibebe’ (I Like It) ameweka wazi kuwa ana mpango wa kuongeza Mjengo mwingine nchini Afrika ya kusini.

Diamond ambaye tayari anamiliki nyumba moja nchini Sauzi ambayo inatajwa kuwa na thamani Dola za kimarekani 500,000 $ ambazo ni sawa na shilingi 1,143,700,000 za Kitanzania.
Diamond amethibitisha taarifa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

Still in love with my first South Africa house…. adding the new house in here before end of the year”.

Diamond tayari ana mijengo kadhaa nchini lakini pia nyumba yake ya South Africa ndiyo anayoishi mama watoto wake Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady pamoja na watoto wake.

Wasanii wa Bongo Waaswa Kuacha Unafiki na Uoga..."Mbona Lissu Hamkumpost?"

$
0
0

Moja ya wanasiasa nchini, Peter msigwa amewaomba wasanii wa Tanzania kuacha kuwa wanafiki na waoga katika kutetea mambo ambayo yanakuwa na mnufaa kwa jamii hasa pale wanapoamua kufanya kwa ajili ya jamii.

Akiandika katika ukurasa wake, Peter msigwa anasema kuwa  ameona katika mitandao ya kijamii wasanii baadhi yao wakiungana na wasanii wa Uganda katika kampeni yao ya kuishinikiza serikali kumuachia mwanasiasa aliwahi kuwa msanii nchini humu Bob wine.

“Nimeona baadhi ya wasanii Tanzania wanaandika FREE BOBI WINE , jambo ambalo ni zuri lakini alipoonewa Sugu,Lissu ,Mawazzo ,Saanane,Azori  hapa Tanzania wamekaa kimya , Injustice  to one is injustice to all” Tuache unafiki  na UWOGA , Museveni Free BOBI wine, Magufuli FREE DEMEOCRACY.

Yanga Yaichezesha Samba Mtibwa Sugar, Mashabiki Wafurahishwa na Kiwango

$
0
0
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwenye mchezo huo wa kwanza kwa timu zote mbili msimu huu wa mwaka 2018/19 umeonekana kuwa wenye kasi na ufundi wa hali ya juu kwa pande zote.

Yanga imefanikiwa kupata mabao yake kupitia kwa Heritier Makambo dakika ya 31 na Kelvin Yondani akiandika la pili kupitia mkwaju wa penati dakika ya 40 wakati la Mtibwa Sugar likifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 73.

Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani wameonekana kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao katika mchezo huo.

Michezo mingine iliyopigwa leo Stand United imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon,JKT Tanzania ikitoka sare ya 0-0 mbele ya KMC.

Mbowe: Waliomuua Akwilina Wanajulikana, Lakini Wanataka Sisi Ndo Tufungwe

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amesema Tanzania inapitia kipindi kigumu cha viongozi wa kiserikali kutoheshimu sheria na katiba.

Akizungumza na wandishi Leo Makao Makuu ya Chama hicho, Mbowe amesema kumekuepo na uvunjifu wa sheria kwenye kesi inayomkabili yeye na viongozi wengine wandamizi wa Chama hicho huku wakiwa wananyimwa haki zao za msingi.

" Tunaheshimu mahakama zetu lakini kinachofanyika Hivi Sasa sio haki kwetu, hii ni kesi ambayo inawahusisha wabunge ambao wanapaswa kuwepo katika majimbo yao lakini kesi imekua ikipelekwa pelekwa tu muda mwingine hadi usiku.

" Mawakili wetu walipeleka maombi ya kutaka kesi yetu ipelekwe mahakama kuu kutoka kisutu lakini hakimu amekataa na kulazimisha tuingie kwenye shtaka jambo ambalo Wakili Mtobesya amekataa kukubaliana nalo na kuamua kujitoa mbaya zaidi Hakimu ametaka kesi iendelee kesho," Amesema Mbowe.

Mbowe amesema ubabe unaotumika na dola katika kuwakandamiza wapinzani katika kesi yao, uonevu wanaofanyiwa katika chaguzi zinazoendelea, utishwaji wa viongozi wao kutoka kwa viongozi ambao wanasaidiwa na Polisi utapelekea kutokea kile kinachoendelea nchini Uganda.

" Tunaheshimu mahakama lakini inawezekana mahakimu na majaji kutumika kwa kufanya kazi kwa maelekezo, na hii lazima tuzungumze ili Dunia na watanzania waelewe kwamba hatuoni haki ikitendeka kwa kesi yetu inayosikilizwa na hakimu Mashauri na ndio maana hata tulipoomba ajitoe ameendelea kukataa.

“Waliomuua Akwilina wapo, lakini tunatengenezewa kesi sisi ili tufungwe, tunasema hatuogopi kwenda jela, lakini tunataka tufungwe pale ambapo tuna haki ya kufungwa. Waue wengine, wapige risasi wengine, waumize wengine, walioonewa ndiyo wanakuwa washutumiwa?” amesema Mbowe

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 24

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 24

Irene Uwoya Awaonya Wanaopiga Picha za Nusu Uchi

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amefunguka na kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia 'skendo' za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu na si TCRA pekee.

Uwoya ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kna  eNewz ya EATV, na kusema wanaofanya na vitendo hivyo wanajidhalilisha wao wenyewe bila ya kujijua.

"Mimi nadhani kuna kitu watu hawajui au hawakitambui, kuwa kuna tofauti ya kutaka kuwa 'star' na kufanya kitu ambacho unakipenda ambacho kitakupelekea kuwa 'star' moja kwa moja", amesema Uwoya.

Pamoja na hayo, Uwoya ameendelea kwa kusema "mimi nawashauri watanzania kama kuna mtu anataka kuwa muigizaji basi afuate misingi iliyowekwa nasio kupiga picha za nusu utupu kwa kuwa haitoweza kumfanya mtu kuwa star na badala yake inakushusha. Wanaopiga picha za nusu utupu wanajidhalilisha kiukweli maana hata Mungu hapendi".

Kauli hiyo ya Irene Uwoya imekuja baada ya kupita takribani siku 36 tokea alipopigwa onyo na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), kuhusiana na kuchapisha picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii na kusisitiziwa kuwa endapo atarudia kufanya hivyo adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha ya Polisi Akinywa Bia Baa Yamponza Mwandishi wa Gazeti la Uhuru

$
0
0
Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, Constantine Mathias, amehojiwa na polisi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza jana Agosti 23 Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki alisema Mathias alikamatwa, akahojiwa kisha akaachiwa.

Imeelezwa kuwa Mathias alisambaza picha kwenye mtandao wa kijamii wa facebook inayomuonyesha askari polisi akinywa bia akiwa na sare za kazi.

Picha anazodaiwa kusambaza ni za askari polisi PC Neto Mahenge wa kituo cha polisi Mwamapalala.

"Anahojiwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na madai ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. Nimeagiza achukuliwe maelezo na kuachiwa kwa dhamana akikamilisha taratibu na mahitaji ya kisheria," alisema Kamanda Nsimeki.

Vigogo KCU Kizimbani Kwa Uhujumu Uchumi

$
0
0

Vigogo watatu wa zamani wa Chama Kikuu cha Ushirika, Mkoa wa Kagera KCU 1990 LTD wamesomewa mashitaka matano likiwamo la uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya milioni 124.

Wakili Mwandamizi wa Serikali Athuman Matuma aliieleza mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Kagera jana kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti mwaka 2011.

Washitakiwa hao ni Mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya KCU, John Binunshu, aliyekuwa Meneja Mkuu KCU, Vedastus Ngaiza na aliyekuwa mhasibu, Bestina Rwebangira.

Aliyataja mashtaka hayo kuwa ni kula njama matumizi mabaya ya ofisi, kughushi, matumizi mabaya ya madaraka na kuhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh124 milioni.

Watuhumiwa walisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi John Kapokolo  na wamenyimwa dhamana hadi Jumatatu kesi yao itakapotajwa tena.

Video: Samaritha Aliyeonekana Kwa Mganga Kafunguka Yote

$
0
0

Ni headlines za mfanyabiashara kutokea mkoani Arusha, Samiratha ambae kipindi cha nyuma alioneka kwa mganga wa kienyeji akifanyiwa dawa kasha video yake kusambaa katika mitandao ya kijamii huku story zikidai mumewe ndokavujisha video hiyo baada ya kugombana sasa kupitia Ayo TV Samiratha kafunguka yote

Bonyeza PLAY kutazama FULL STORY

Mbwana Samatta Hataki Utani Safari ya Europa League, Leo Kapiga Hat-Trick

$
0
0
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa August 23 2018 amerudi kwenye headlines baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Brondby If ya Denmark.

Huo ulikuwa ni mchezo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2018/2019, Samatta akicheza game hiyo kwa dakika zote 90 na amefanikiwa kuifungia KRC Genk hat-trick katika ushindi wa magoli 5-2, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 38, 55 na 70 mengine yakifungwa na Leandro Trossard dakika ya 45 na 90.

Magoli ya Brondby IF yalifungwa na Hjortur Hermannsson dakika ya 47 na Kamil Wilczek dakika ya 51, leo ndio kwa mara ya kwanza Mbwana Samatta anafunga hat-trick akiwa na KRC Genk lakini ameanza vizuri katika msimu wa 2018/2019 akiichezea KRC Genk katika mashindano tofauti ya Ligi na kuwania kufuzu hatua ya makundi ya UEFA Europa League.

Mbwana Samatta sasa akiichezea KRC Genk katika game zake nne mfululizo zilizopita amefunga jumla ya magoli 7, ambapo amecheza dakika 281 na kufunga jumla ya magoli saba ambapo ni wastani wa kufunga goli moja kila baada ya dakika 40, huu ni muendelezo mzuri kwa Samatta hususani akiwa msimu wake wa tatu na Genk na inawezekana akavivutia vilabu vikubwa zaidi kuhitaji saini yake.

'Nipo Tayari Kubeba Mimba ya Staa Yoyote Bongo Kwa Milion 20' Sabby Angel

$
0
0
BAADA ya Mtangazaji wa Redio, Loveness Malinzi ‘Diva thebawse’ kudai kuwa ana tatizo la kizazi na hivyo anahangaika kubeba mimba, staa wa Filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameibuka na kudai kuwa yupo tayari kumbebea staa yeyote mimba ila kwa dau kuanzia milioni ishirini.

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, Sabby aliyewahi kudaiwa kubanjuka kimapenzi na mastaa kadhaa akiwemo Alikiba alisema kuwa, anajua kuwa wapo mastaa wa kiume walio na wapenzi wao wenye matatizo kwenye kizazi kwa hiyo yupo tayari kuwabebea mimba.

“Sitafuti kiki ila nimeeleza kitu ambacho nimekuwa nakifikiria muda mrefu baada ya kuona watu wengi wakiwemo mastaa hapa Tanzania kuwa na tatizo katika kizazi, mara mimba zinatoka na wengine kushindwa tu kubeba kwa sababu mbalimbali na ndiyo maana nikaamua kuongea hivi,” alisema Sabby na kuongeza;

“Zipo njia za kitalaamu unapandikiza mwisho wa siku unakuwa na mtoto wako ila kwangu kwa sharti moja tutasaini mkataba ambao sio chini ya milioni ishirini ili kupandikiza hizo mbegu kwa kuwa si unajua uzazi unachakaza sometimes kwa hiyo lazima nipate hela za kujitengeneza,” alimaliza Sabby.

STORI: SHAMUMA AWADHI

Kutana na Sharifu Seif Mohammed wa Bagamoyo, Kijana Aliyezaliwa Katika Koo za Masharifu

$
0
0
KUTANA NA SHARIFU SEIF MOHAMMED WA BAGAMOYO, KIJANA ALIEZALIWA KATIKA KOO ZA MASHARIFU

SASA AMEKUWA GUMZO DUNIANI KOTE KUTOKANA NA DUWA NA TIBA MBALIMBALI ANAZOTOA,

SHARIFU SEIF MOHAMMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA

Sharifu seif Mohammed ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Tanzania na duniani kote,

ANATIBU KWA KUTUMIA KITABU CHA QUR'AN, DAWA ZA ASILI, NJIWA NA MAJINI

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

JE? Umeachwa na UMPENDAE Awe MME/MKE au MPENZI na Bado Unampenda? Mpigie Simu SHARIFU sasa Hivi Ujionee miujiza yake, Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA/ MAHUSIANO yako ndani ya saa 72 tu.
Hata kama mpenzi wako anaishi na mtu mwingine anauwezo wa hali ya juu ya Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) na kumrejesha kwako,
Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone SHARIFU SEIFU MOHAMMED Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi, SHARIFU SEIF MOHAMMED Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza tatizo lako, ANATAFSIRI NDOTO, ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, ANATOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI, ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI ZINAZOENDANA NA NYOTA YAKO, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU KAMA VILE MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, TATIZO LA UZAZI KWA KINA MAMA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE POTEA, ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE,

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu, Hutoa Jini MALI kwa wale Wanao hitaji Utajiri Bila Masharti,

Kwa mawasiliano na ushauri zaidi:
Mobile + 255 654 836970
WhatsApp +255 756 033670

Ushauri: Ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa wakati

Trump awaonya wamarekani..... " Mkiniondoa Madarakani Mtakuwa Masikini"

$
0
0
Trump awaonya wamarekani..... " Mkiniondoa Madarakani Mtakuwa Masikini"
Rais wa Marekani Donald Trump amejibu uvumi kuwa anaweza kuondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa kuonya kuwa uchumi utaharibika

Wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Fox & Friends alisema masoko yataporomoka na "kila mtu atakuwa maskini".

Alikuwa akizungumza baada ya Michael Cohen, wakili wake wa zamani kukiri kuvunja sheria za uchaguzi na kusema alishauriwa kufanya hivyo na Trump.

Si kawaida kwa Trump kuzungumzia suala la kutolewa mamlakani.

Waandishi wa habari wanasema haiwezekani kuwa wapinzani wa Trump watajaribu kumuondoa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye kabla ya uchaguzi wa kati ya muhula wa mwezi Novemba.

Sijui ni kwa njia gani mtamtoa madarakani mtu ambaye amefanya kazi nzuri," Trump alikiambia kipindi cha Fox and Friends.

"Ninawaambia hivi, ikiwa nitaondolewa nafikiri masoko yataporomoka, nafikiri kila mtu atakuwa maskini."

Trump alitetea malipo kwa wanawake wawili na kusema hakuwa anawajua wakati huo.

Matamshi yake yanaenda kinyume na taarifa zilizotolewa mapema na Cohen ambapo alisema kuwa Rais Trump aliimuagiza kufanya malipo hayo.

Mwezi Julai Cohen alitoa kanda ya sauti yake na Trump wakizungumzia moja ya malipo hayo kabla ya uchaguzi

Cohen anasem alifanya malipo hayo kwa wanawake wawili wakati wa kampeni ya urais ya mwaka 2016.

Wanawawe hao wawili wanatajwa kuwa manyota wa filamu za ngono Stormy Daniels na Karen McDougal, wote walidai walikuwa na uhusiano na Trump

Lakini Trump alisisitiza kuwa malipo hayo hayakukiuka sheria za uchaguzi.

Alisema malipo hayo yalitoka kwake mwenyewe na sio kutoka kwa kampeni lakini hakufahamua kuyahusu hadi baadaye.

Waziri Mkuu wa Australia Malcom Turnbull Atimuliwa

$
0
0
Waziri Mkuu wa Australia Malcom Turnbull Atimuliwa
Scott Morrison anatarajiwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya Malcom Turnbull kutimuliwa kwa lazima na chama chake maafisa wamethibitisha.

Turnbull alikuwa kwenye shinikizo kubwa kuanzia kuorodheswha chini katika kura za kutafuta maoni, uchaguzi unaowadia, na kugeukiwa na wabunge wa kihafidhina.

Morrison ambaye ndiye mweka hazina wa sasa alishinda kura 45 kati ya 50 ya ndani dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amaesema kinara wa chama cha kiliberali Nola Maroni.

Turnbull hakuwania katika ushindani huo wa uongozi.

Alikubali kuandaa kura baada ya idadi kubwa ya wabunge katika chama chake kusaini barua kutaka uchaguzi ufanyike.

Turnbull alikuwa akipuuzia wito wa kumtaka ajiuzulu wakati tuhuma za uongozi zikiididimiza serikali yake.


Jana Alhamisi , aliwaambia waandishi habari, kuwa raia nchini Australia 'watashangazwa mno kwa wanachokishuhudia'.

Waziri wa mambo ya nje Julie Bishop pia ni miongoni mwa waliogombea nafasi hiyo, lakini hakufanikiwa katika duru ya mwisho.

Bwana Turnbull na Bi Bishop hawakuzungumza na waandishi habari moja kwa moja baada ya kura hiyo.

Calisah Kuja na Vidonge vya Kung'alisha Ngozi

$
0
0
Calisah Kuja na Vidonge vya Kung'alisha Ngozi
BAADA ya ‘kutrend’ na ishu ya kuwapa mimba wanawake 25, mwanamitindo maarufu Bongo, Calisah Abdulhamid, ameibuka na ishu nyingine kuwa yupo mbioni kufungua duka la vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake.

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, Calisah ambaye amehusishwa mara kibao kubadili ngozi yake na kuwa mweupe, alisema weupe wake umetokana na AC za magari na si vinginevyo kama watu wanavyoeneza.

“Hapana sijawahi badili rangi ya mwili wangu, mimi ndo nipo hivihivi tangu zamani, kubadili ngozi kwanza ni mambo ya kike ambayo sijawahi kufanya hivyo, hizi ni AC tu za magari halafu mimi ni mtu ambaye naamini sana kwenye muonekano wa kiume ndiyo mana hata nafanya mazoezi, kwa hiyo sijawahi kufanya hivyo kwa sababu hata familia yangu ni ya watu weupe,” alisema Calisah na kuongeza;

“Kwanza nipo mbioni kufungua duka la dawa za vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake ambapo Bongo hii hakuna, mimi ndiyo nimeagiza pekee na nitakuwa naziuza ofisini kwangu,” alimaliza.

Baba Kortini Kwa Kumbaka Mtoto wake wa Miaka 12

$
0
0
Baba Kortini Kwa Kumbaka Mtoto wake wa Miaka 12
Mkazi wa Stendimpya, Mugumu, Nyamhura Werema (35)amepandishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka(12)

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa polisi, Paskael Nkenyenge amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka huu.

“Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” amesema

Amesema Upelelezi haujakamilika na mshitakiwa amekana shitaka. Mshtakiwa amenyimwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba mwaka huu.

Wabunge 19 CHADEMA Kulinda Kura Dodoma

$
0
0
Wabunge 19 CHADEMA Kulinda Kura Dodoma
Viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema watawatumia wabunge 19 wa chama hicho kulinda kura katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kizota katika jiji la Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Iddy Kizota alisema watawatumia wabunge wa Chadema kulinda kura za mgombea kutokana na kuwapo kwa hujuma za kuwapiga mawakala na kuwaondoa vituoni kwa lengo la kubadilisha matokeo.

Hata hivyo Kizota alisema kulikuwepo na njama kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa na Ofisi Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu kwa kutaka kumkwamisha mgombea wa Chadema kwa kumwekea vikwazo visivyokuwa na sababu.

“Unaweza kujiuliza msimamizi wa uchaguzi anakuwa na visingizio kibao kwa kudai kuwa ofisi ya kata haina daftari ya orodha ya wapiga kura, mara hakuna risiti kwa kwa ajili ya kumpatia mgombea pamoja na mambo kadha wa kadha,” alisema Mrefu.

Amlisema kutokana na kuwapo dalili za hujuma ambazo zinafanywa na viongozi wa chama tawala kwa kushirikiana na watumishi wa serikali wamejipanga kuhakikisha wanalinda na kusimamia sheria, kanuni na misingi yote ya uchaguzi.

Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu alipoulizwa juu malalamiko ya wanayoelezwa na wanachama wa Chadema alisema yeye siyo msemaji wa uchaguzi ingawa ni Ofasa Mtendaji kata.

Pamoja na kudai kuwa siyo msemaji alieleza kuwa vyama vilivyochukua fomu na kurejesha ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, UDPD na NLD.

Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Kizota kupitia Chadema, Omar Bangababo amesema amejitosa kuwania nafasi hiyo ili kupambana na changamoto ambazo mtangulizi wake ameshindwa kuzitatua kutokana na kukosa msimamo kwa wananchi walio mchagua.

Wakili Afunguka Kilichomwondoa Katika Kesi ya Mbowe na Wenzake

$
0
0
Wakili Afunguka Kilichomwondoa Katika Kesi ya Mbowe na Wenzake
Wakili Jeremiah Mtobesya amejitoa kuwawakilisha katika kesi viongozi tisa wa Chadema, akiwamo mwenyekiti Freeman Mbowe akisema anaona haki haitatendeka.

Mtobesya alijiondoa katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Alifikia uamuzi huo baada ya Mahakama kutoa uamuzi wa kutupilia mbali maombi ya wateja wake ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112/2018 iahirishwe ili kusubiri kusikilizwa maombi na rufani iliyopo Mahakama ya Rufaa.

Washtakiwa wamewasilisha katika Mahakama ya Rufaa maombi wakitaka kesi ya msingi iliyopo Kisutu isitishwe usikilizwaji hadi rufaa ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupilia mbali maombi ya marejeo namba 126/2018 itakaposikilizwa na uamuzi kutolewa.

Katika Mahakama Kuu, washtakiwa waliiomba irejee mwenendo wa kesi na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Jana, baada ya Hakimu Mashauri kuyatupilia mbali maombi ya washtakiwa aliamuru wasomewe maelezo ya awali ya kesi inayowakabili.

Wakili Mtobesya alieleza kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na uamuzi ulitolewa.

Alisema hakubaliani na ombi la upande wa mashtaka la kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Wakili Mtobesya aliieleza Mahakama kuwa anajiondoa katika kesi kwa sababu anaona kwa namna mwenendo wa kesi unavyokwenda haki haitatendeka.

Kwa kauli hiyo, Mtobesya alibeba begi lake na kuondoka ndani ya ukumbi namba moja wa Mahakama ambako kesi ilikuwa ikiendeshwa.

Aliwaacha washtakiwa wakiwa hawana wakili mahakamani kwa kuwa wakili mwingine anayewawakilisha, Peter Kibatala hakuwapo.

Hakimu Mashauri aliwaeleza washtakiwa kwa kuwa hawakuwa na wakili mwingine mahakamani, anaahirisha kesi hadi Agosti 27 watakaposomewa maelezo ya awali.

Sababu za maombi kutupwa

Hakimu Mashauri katika uamuzi wa kutupilia mbali maombi ya washtakiwa, alisema kifungu cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai kilichotumika kuwasilisha maombi hayo, hakiipi Mahakama mamlaka ya kuahirisha kesi kusubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa.

Alisema hata kama kifungu hicho kingekuwa kinaipa Mahakama mamlaka ya kufanya hivyo, basi isingefanya hivyo kwa sababu ilishatoa uamuzi mara kadhaa kutokana na maombi mbalimbali ya utetezi na kuyatupilia mbali, hivyo haiwezi kula matapishi yake.

Baada ya uamuzi kutolewa, wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi alisema kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, na kwa kuwa uamuzi umeshatolewa aliiomba Mahakama iridhie washtakiwa wasomewe maelezo ya awali. Ombi hilo lilipingwa na Mtobesya.

Hakimu Mashauri alisema ni kweli kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa kusubiri uamuzi ambao alishautoa, hivyo haoni haja ya kuahirisha kusomwa kwa maelezo ya awali.

Alisema usomaji wa maelezo hayo hauhitaji maandalizi, hivyo aliamuru upande wa mashtaka kuwasomea washtakiwa hao.

Wakili Kibatala alipowasilisha maombi awali, alidai Mahakama hiyo ina mamlaka ya kuiahirisha kesi ya jinai namba 112/2018 kwa kipindi kisichozidi siku 15 iwapo mshtakiwa atakuwa ndani na kisichozidi siku 30 iwapo mshtakiwa au washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana.

Wakili Nchimbi alidai kuwa maombi hayo ya utetezi yanakosa baraka za kisheria na hata miguu ya kisheria ya kusimama mbele ya Mahakama hiyo.

Aliiomba Mahakama itupilie mbali maombi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kwa sababu yanakosa msingi wa kisheria.

Alidai maombi ya upande wa utetezi yanalenga kuchelewesha kesi na hakuna kipya kilichowasilishwa mahakamani. Mbali na Mbowe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai ni naibu katibu mkuu wa Chadema –Zanzibar, Salum Mwalimu na naibu katibu mkuu –Bara, John Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Kibamba.

Wengine ni wabunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Esther Matiko (Tarime Mjini) na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Februari Mosi na Februari 16 jijini Dar es Salaam.

Mashabiki Man U Wamtaka Mtendaji wa Klabu Atimuliwe

$
0
0
Mashabiki Man U Wamtaka Mtendaji wa Klabu Atimuliwe
MASHABIKI wa Manchester United wamelipia bango kubwa litakalokuwa linapepea hewani wakati wa mchezo kati ya timu yao dhidi ya Burnley likitaka Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, aondoke kwenye klabu hiyo.



Tukio hilo litatokea Jumamosi ya wiki ijayo kwenye Dimba la Turf Moor, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England baina ya timu hizo.

Tukio hilo limekuja baada ya kocha Jose Mourinho, kulalamika mara kwa mara kuwa bosi huyo alishindwa kutoa fedha za kutosha za usajili.



Inaaminika kuwa bango hilo litakuwa limeandikwa ‘Ed Out – LUHG’, ikiwa ni ishara ya kwanza kuwa bosi huyo hatakiwi na mashabiki. LUHG ikiwakilisha Love United, Hate Glazers, yaani Ipende United, Wachukie Glazers (wamiliki wa klabu)



Mashabiki wa timu hii walikuwa wa kwanza kutumia mbinu ya mabango kumuondoa aliyekuwa kocha wao, David Moyes.



Lakini pia Arsenal waliwahi kutumia njia hiyo pia wakati wa vuguvugu la kuondolewa kwa kocha, Arsene Wenger.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images