Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Imejulikana Diamond Hakupewa Kibali cha Kuvaa Nguo za Jeshi Fiesta

$
0
0
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kuwa mwanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu ‘Diamond Platinumz’, aliyetinga na sare za jeshi jukwaani kwenye tamasha la Fiesta, hakuwa na kibali cha kuvaa nguo hizo.

Jeshi hilo ambalo bado linaendelea na uchunguzi, limesema kwa kawaida JWTZ haiwezi kutoa nguo au vifaa vyake kwa ajili ya maonesho ya wanamuziki au shughuli nyingine yoyote zaidi ya matumizi ya jeshi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Ofisa Mnadhimu wa Mkoa wa Polisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi (SSP), Boniventure Mushongi.

Alisema hakuna kibali kinachotolewa na jeshi lolote kwa nguo au vifaa vyake kutumika na watu wasio wanajeshi.

“Jeshi haliwezi kutoa kibali cha nguo zake kutumika jukwaani, hata hao wasanii wanaoonekana kuvaa nguo za jeshi majukwaani wanakiuka sheria,” alisema SSP Mushongi.

Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini jeshi la Polisi lilishindwa kuchukua hatua siku ya tukio, SSP Mushongi alisema kwa hali ilivyokuwa, isingekuwa rahisi kufanya hivyo na huenda zingetokea fujo.

“Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa weledi. Lingeweza kumchukulia hatua siku ile ile aliyopanda jukwaani na mavazi yale, ila haikuona madhara kwa wakati huo shughuli zinaendelea.. endapo hali ile ingetokea mikoani huko, msanii huyo angechukuliwa hatua hapo hapo,” alisema.

SSP Mushongi, aliongeza kuwa hatua ya wasanii nchini kupenda kuvaa mavazi ya majeshi ni ukiukwaji wa sheria na elimu zaidi inahitajika.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema wanenguaji wa mwanamuziki huyo, wamekamatwa na kuhojiwa na Polisi wa kituo hicho cha Oysterbay, kwa tuhuma za kuvaa sare za JWTZ.

Wengine walioshikiliwa ni pamoja na meneja wake Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ambaye ameshaachiwa baada ya kuhojiwa.

Hata hivyo, awali vyanzo mbalimbali vya habari vilivyoifikia Tanzania Daima, vilieleza kuwa, Babu Tale alijisalimisha Polisi Oysterbay juzi majira ya jioni na baada ya kuhojiwa, aliswekwa mahabusu. Babu Tale alipoulizwa alipo Diamond, alisema amesafiri nje ya nchi mara baada ya onyesho la Fiesta.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi (ACP), Camillus Wambura, alisema bado hajapata taarifa ya kukamatwa kwa meneja huyo pamoja na wanenguaji hao, kwani shauri hilo l ipo kwenye uchunguzi chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa.

T.I Aimwagia Sifa Tena Tanzania Kwenye Interview Yake Radioni Huko Marekani

$
0
0
Clifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya nguvu katika jukwaa la Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 2014 katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyokutana nayo Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya New York Marekani na kituo maarufu cha redio Power 105.1 kwenye show ya Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000.
T.I amelinganisha idadi hiyo kubwa aliyokutana nayo Tanzania kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho anakiona kabisa sio rahisi na ndio maana hii ya Leaders imekua kubwa kwake.
Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa kwa T.I kama alichukua tahadhari kwa kufanya utafiti kabla ya kwenda Afrika na kusema hakuwa na hofu yoyote alipokuja Tanzania, zaidi alikuwa akifikiria tu kuhusu mpenzi wake, hata hivyo hakukutana na Ebola wala kuona hata dalili za uwepo wake na kusisitiza kwamba mara nyingi Ebola imekua ikiwapata Wanaowahudumia wagonjwa’
Kwenye sentensi nyingine rapper huyu mwenye umri wa miaka 34 alisifia jinsi alivyopokelewa vizuri na kusema Tanzania ni watu wazuri hivyo akamwambia Dj Envy kwamba ataenjoy sana kwenye safari yake ya Afrika December mwaka huu.

Mike Sonko Aja na Mpya..Sasa Unaweza Weka Tangazo la Biashara Kichwani Kwake

$
0
0
The Nairobi senator’s head has become some sort of phenomenon thanks to his hair do’s with writings on them. From ‘Uhuruto Is Innocent’, ‘Rais Usiende ICC’, ‘Muthama Respect Wife’, I have a feeling there are more to come.

Someone is now of the view that Sonko should use his big head for advertising and probably make more money. Applications are now open for anyone willing to place an ad.

Miss Tanzania Namba 3 Afunguka Kuhusu Ushindi wa Sitti Mtemvu Wenye Utata

$
0
0
Na Hamida Hassan na Imelda Mtema
Gumzo mtaani kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti Abbas Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la Miss Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi, maneno yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine wakasema eti ana mtoto.

Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni Jihan Dimachk.

Kwenye fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss Tanzania Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii iliyofanyika kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar.

Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey, nashukuru kuwafahamu, karibuni.
Ijumaa: Tuanze na matokeo ya kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe ulistahili kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?

Jihan: Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa nikiamini nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain (haikuwa sawa ila siwezi kuelezea).
Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo? hebu fafanua kauli yako.

Jihan: Sipendi kuwa muongeaji sana, naheshimu maamuzi ya majaji na Kamati ya Miss Tanzania lakini ukweli uliopo moyoni mwangu ni kwamba nilijiamini na ndiyo maana niliingia kwenye kinyang’anyiro nikijua ushindi ni haki yangu.

Ijumaa: Wapo wanaosema ulikuwa na kila kigezo cha kuwa Miss Tanzania 2014 lakini umetoswa kutokana na rangi yako ukihisiwa wewe si Mtanzania, unaliongeleaje hili?
Jihan: Sipendi kabisa kusikia maneno hayo, mimi ni Mtanzania, nimezaliwa Mwanza, mama yangu ni Msukuma na baba yangu Mlebanon. Tangu naingia kwenye shindano hili waandaaji walinihoji, wakafuatilia hilo na kutambua ni Mtanzania, ingekuwa tofauti sidhani kama ningeruhusiwa kushiriki.
 Ijumaa: Kwa mfano ikitokea Sitti akavuliwa taji kutokana na haya yanayozungumzwa, uko tayari uvishwe wewe?

Jihan: Siwezi kulijibu swali hilo kwani haijatokea. Endapo itatokea na waandaaji wakanifuata kuniambia hivyo, hapo ndiyo nitakuwa na la kuzungumza.
Ijumaa: Unamuongeleaje Sitti Mtemvu?
Jihan: Kwa sababu ndiye aliyevishwa taji, naheshimu ushindi wake, namkubali kuwa ni mrembo na siwezi kupingana na maamuzi yaliyotolewa.

Ijumaa: Umechukua nafasi ya tatu ambayo nayo si haba, una mipango gani ya baadaye?
Jihan: Nina mambo mengi ya kufanya. Nina ndoto za kuwasaidia wanawake na watoto lakini pia nahisi nina jukumu la kusaidia katika suala la elimu nchini, nitajipanga kufanikisha hayo.
Ijumaa: Kwa nini elimu?

Jihan: Nimekuwa nikikutana na watu wengi ambao elimu imekuwa kikwazo kwenye maisha yao, nikawa nimejiapiza kuhakikisha nawasaidia kadiri nitakavyoweza.
Ijumaa: Asante sana Jihan, tunakutakia mafanikio katika yale unayopanga kuyafanya.
 Jihan: Nashukuru sana.
~Credits:GPL

Mgombea Udiwani 2015 Anaswa Kitandani Akiwa na Mwanafunzi Guest House

$
0
0
HILI nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la  mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, Ijumaa ‘kubwa’ lina mkanda wote.

Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.

WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema  alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo.

USHUSHUSHU 
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno  (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.

MBALI NA UJUMBE
Ikadaiwa kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye mazuri siku za usoni.

BINTI ATII AMRI YA WAZAZI
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.

NI KAMA WALISEMA
“Mtu gani mama?”
Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”
Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”
Mama: “Anaitwa nani?”


Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli?  (kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku moja.” 
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”

MTEGO
Ikadaiwa kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda wakutane huko gesti ili  wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo, mzee akashindwa kujiongeza. 
Binti akiwa na mzazi wake na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo alishafika zamani gani na kumsubiri.

Baada ya muda, binti alituma meseji kwa mama yake akisema mambo tayari, wapo ‘weupe pee’ (hawana nguo). Ndipo mama huyo akachukua timu yake na kuvamia gesti hiyo kwa ajili ya kulianzisha.

OFM YAKATIZA MITAANI, YAKUMBANA NA KASHESHE
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ilikuwa ikikatiza mitaani kusaka matukio kwani ni ada yake, ndipo walipoibukia eneo lenye gesti hiyo na kukumbana na kasheshe hilo la nguvu.
 “Hawa wazee ndiyo wale ambao wanaharibu watoto wa watu huku yeye wanawe wakisoma vizuri na hakuna anaowaharibia masomo yao,” alisikika akichonga mama huyo.
Akaendelea: “Jamani nawaomba njooni na makamera yenu yote hapa.”

OFM YAPATA NGUVU
Kufuatia maneno ya mama, OFM walipata nguvu na kuanza kupiga picha za kumwaga kwa ajili ya kumbukumbu.

MGOMBEA ASEMA NENO
Huku akiwa amekaa kwa tafakuri ya kina, mzee Beno alisema ameumbuka na kuitaka familia ya mwanafunzi huyo kumalizana kifamilia nje ya gesti hiyo huku akiwaomba OFM chondechonde wasiitoe habari gazetini.

Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitamboni, mwanamke huyo alisema hawajamalizana chochote hivyo OFM inaendelea kufuatilia sakata hilo.
~Credits:GPL

Raisi Jakaya Kikwete Afunguka ya Moyoni ..Asema Kazi ya Urasi ni Ngumu Anatamani Muda wake Uishe

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru kufanya mambo yake, ikiwamo kilimo, huku akiamini atapatikana Rais bora kuiongoza vizuri zaidi Tanzania kuliko yeye.

Rais Kikwete alisema hayo Beijing alipokuwa akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha mataifa yao nchini China.

Kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Wageni wa Serikali ya China ya Diaoyutai, Rais Kikwete katika shughuli yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku sita kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Xi Jinping.

“Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu, nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha,” alisema Rais Kikwete kwenye mkutano huo baada ya naibu balozi wa Nigeria, Sola Onadipe kuelezea kushangazwa na kauli yake ya kutamani muda wake wa uongozi ufike ili apumzike.

“Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano au miaka 10 ni wa kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha kulibadilisha.

“Pili, kazi hii ya urais ni ngumu sana. Kwa hakika nawaonea gere sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi,” alisema Rais Kikwete.

“Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka 10, anaingia mtu mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya.”

Rais Kikwete alisema mfumo huo unamridhisha na hakuna kinachomshawishi abakie madarakani zaidi ya muda wa kikatiba.

“Nina hakika, nchi yetu itapata kiongozi mwingine, bora kuliko hata mimi, kuongoza vizuri nchi yetu,” alisema Rais Kikwete ambaye aligombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995, lakini akashindwa kwenye kura ya maoni ndani ya CCM.

Awali Balozi Onadipe alisema kuwa lingekuwa jambo la maana kwa Afrika kama viongozi wengine wangekuwa na mawazo ya namna hiyo ya kuheshimu Katiba za nchi zao na kung’atuka kwenye uongozi muda wao unapowadia.

Rais Kikwete pia alisema siyo busara kwa kiongozi kuwasikiliza wale wanaoshauri wakisema kuwa akiondoka madarakani nchi itavurugika.

Taarifa Kuhusu Madaktari Watanzania Waliokwenda Kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

$
0
0
Unaposikia ugonjwa wa ebola, ni sawa na kusikia sauti ya mauti. Ugonjwa huu ambao unaliandama eneo la Afrika Magharibi umesababisha vifo vya maelfu ya watu na hata kuuingiza ulimwengu kwenye wasiwasi mkubwa.

Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kwa kugusana tu, kwa kuwa virusi vinavyoeneza maradhi haya huishi katika majimaji ya mwilini yakiwamo mate, damu na hata jasho.

Pamoja na hatari ya ebola, lakini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa maagizo ya Rais Jakaya Kikwete, ilituma timu ya madaktari bingwa watano kwenda katika nchi zilizoathirika na ebola ili kusaidia.

Madaktari hao ni Justin Maeda ambaye ni mganga mkuu wa Hospitali ya Mvomero, mkoani Morogoro, Theopili Malibicha kutoka Hospitali ya Mkoa wa Lindi, Godbles Lucas, wizarani, Erild Temba kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Saasita Ramadhan kutoka Chunya, Mbeya.

Madaktari wote hawatakwenda eneo moja. Dk Maeda, Malibicha na Lucas wataenda Liberia, wakati Temba na Ramadhan wakienda Sierra Leone.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja anasema madaktari hao wamekwenda katika nchi hizo ili kusaidia kutoa huduma za afya na kupata ujuzi.

“Kitendo cha madaktari hawa kwenda katika nchi zenye ebola si cha kutisha kama wengi wanavyodhani kwani ni sawa na askari anayekwenda vitani,” anasema.

Anasema mwanajeshi hupata mafunzo akijua siku yeyote anaweza kupata wajibu wa kwenda kupigana kwenye vita ambako kuna kufa au kupona.
Credits:Mwananchi

Maswali 7 Ya Godbless Lema Kwa Polisi-Mauaji ya Mtuhumiwa wa Mabomu Arusha

$
0
0
1.Tobo la risasi katika hiyo picha Linaonekana tumboni. Je hapo ndipo lilipo ---- la kulia? kwanini wadanganje..?? what are they hiding?.

2.Nani mwenye uwezo wa kuthibitisha makosa ya mtuhumiwa na kukiri kwake kuhusika namatukio ya ugaidi?.

3. Hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma kwa maana ya mgongoni si tumboni.

4. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo"halafu umsafirishe bila kumfunga pingu?.

5.Kwa jinsi ambavyo nguvu kubwa ilitumika na Polisi wenyewe na hata Serikali nachama tawala kupotosha juu ya tukio lile la milipuko kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, na kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete aligomea wito wa Chadema na makundi mbalimbali ya kijamii wa kumtaka aunde tume ya kijaji (Judiciary commission) kuchunguza mauaji yale, kwa nini tuwaamini polisi kuhusu taarifa namaelezo yao kuwa mtuhumiwa alitoroka akiwa chini ya ulinzi kisha akauawa?.

6. Tukumbuke kuanzia mwanzo jeshi la Polisi na hata Rais hawakuonyesha nia njema katika hili leo hii tuwaamini walikuwa wana nia njema ya kumfikisha mtuhumiwa kwenye mikono ya sheria?.

7. Kifo cha mtuhumiwa katika"Mazingira tata" mikononi mwa watuhumiwa wengine (Maana hata polisi walituhumiwa kuhusika) lazima kitaacha maswali mengi bila majibuTunahitaji jeshi linalotoa huduma (PoliceService). nitakuwa wa mwisho kuamini tukio hili....... (Godbless Lema).

Diamond Platnumz’ Asalimisha Nguo Zake za Kijeshi Kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay

$
0
0
Dar es Salaam. Mwanamuziki Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amesalimisha nguo zake za kijeshi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Diamond alisema kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo (Oysterbay) akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu.

“Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,” alisema nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland.

Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa dhamana yoyote.

Nafikiria Kuachana na Yule Mpenzi Wangu Asiyeniomba Hela

$
0
0
Juzi kati hapa nilileta uzi kuwa nimepata mtoto wa chuo na huu ni mwezi wa tatu hajaomba cha vocha wala hela yoyote.

sasa kama mjuavyo vyuo vimefunguliwa wiki hii na hajapata chumba bado nikamshauri akae kwangu kwa sababu ni karibu na chuoni kwao.

so jumatatu akahamia wakati tunashughulikia masuala ya hostel

nilimuacha nyumbani nikaenda kwenye mihangaiko yangu kurudi nyumbani nyumba imepekuliwa kuanzia uvunguni mpaka kwenye dari document zangu zote kasoma japo ziko salama .

wiki mbili zilizopita alipekenyua laptop yangu picha nilizopiga na mademu zangu wa miaka nenda rudi nikamkuta anazicheki.

nikienda choooni anakaa mlango wa choo sijui anasikilizia nini.

nilimkuta ameshika simu yangu na kalamu na karatasi ananakili baadhi ya namba kumuuuliza anachekacheka
sasa huyu ni mpenzi au FBI.

nafikiria kumuacha lakini its too late ananijua kuliko hata mama yangu mzazi maana hadi mikataba ya kazini kwangu juu ya mshahara na kila kitu ninachomiliki anakijua kupitia udukuzi wake
Nishaurini jamani

By mdukuzi via JF

Mwigizaji Mainda Amwagiwa Sifa Kede Kede Baada ya Kubadilika na Kushinda Mapepo ya Bongo Movies

$
0
0
Tupate Umbea wa Instagram Kidogo ....
Mwanadada mwigizaji wa Tasnia ya Bongo Movies Mainda Amepewa Sifa kwa Kubadilika na Kuacha mambo ya Skendo kama Wenzake wa Huko Bongo Movies ....Akanti Maarufu ya Michambo huko instagram ya Mrekebishatabia Imeandika Haya Yafuatayo:

"We mtoto @ maindasmallbaby ni mrembo unayejitambua leo naomba nikupe hongera kwa kushinda yale mapepo ya "bongomovie" na globalpublishers umekuwa mtoto mzuri hadi raha. Watu wanabadilika jaman msiendelee kumjudge kwa yaliyotokea. Ni kiumbe mpya kwasasahivi, Mainda wasaidie na wenzako jinsi ya kujitambua na kumfuata Mola. Ila usiache sanaa, wewe ni mwigazaji mzuri na unakubalika nchini. Natamani tukuone zaidi kwa game.. Speed yako nzuri unafaa kuwa mama mchungaji!!! wavute na akina Ray waje kanisani kwa Mungu hakuna linaloshindikana!! ....Byeeee, weekend njema wapenzi!!"

Skylight Band Wajitamba Kuwa Wao Ndio Wamechangia Kushuka Kwa Umaarufu wa Machozi Band

$
0
0
Mwanadada Aneth Kushaba Ambae ni Maneja na Mwimbaji wa Band ya Skylight amesikika akijitamba kuwa Band hiyo ya Skylight ndio imechangia kuipoteza Band inayomilikiwa na Lady Jay Dee inayojulikana kama Machozi Band ...Anath Amejitamba kwa kusema kuwa walichukua wanamuziki wawili ambao walikuwa ni nguzo ya machozi band na kuanzia hapo mambo kwa machozi band yakaanza kwenda mrama na kupotea katika ramani ya muziki Bongo.

Je Unakubaliana na Hilo ? Skylight Band na Machozi Band ipo Bora kwa sasa?

Mwanamuziki Ali Kiba Akanusha Vikali Kuwa Aliandaa Watu Kumzomea Diamond Fiesta

$
0
0
Mwanamuziki Ali Kiba a.k.a The King is Back  Amekanusha Vikali Uvumi ulio enea mitandaoni na magazetini kuwa eti alikodisha watu kwa ajili ya kumshangilia yeye na pia kumzomea Diamond Platnumz...Ali Kiba Amesema hawezi fanya kitu kama hicho kamwe kwa sababu hakina faida yoyote katika mziki wake ...Ali kiba pia Amewashukuru sana mashabiki kwa jinsi walivyompokea siku hiyo kwa kusema kuwa kitendo hicho cha kupokelewa vizuri kimempa matumaini mapya kimuziki.

Salama Jabir Akanusha Kutoka Kimapenzi na Mtangazaji Josh Murunga

$
0
0
Na hiki ndicho alichokisema mwanadada Salama Jabir kupitia fan page yake insta, makubwa haya blog: Wapendwa naombeni twende sawa hapa kidogo,,,ile picha ya masinema ya mabusu,,nothing is serious ni katika vijimambo tu vya location,,and the lucky guy happened to be a brother Mr Josiah "Josh"Murunga ambaye ni producer na director wa MkasiTv! Who is married! so nothing serious!..its just a brother and sister love(bloodline)..Nafahamu wengi mnahamu ya kumjua Hubby ake,,,basi Inshallah siku ikifika mtamjua!

Diamond, Davido Wabwagwa na Sauti Sol kwenye Tuzo za MTV Europe Music

$
0
0
Usione kimya sana leo ni kwamba diamond kapigwa chini kwenye best african act ya Europe music award(Ema) wameshinda sauti sol ambao sasa watashindana na jamaa wa asia hapo tarehe 9 november huko glasgow.

Congratulatory messages have been flowing in for Sauti Sol after they scooped the MTV Europe Awards fending off competition from Tanzania's Diamond , Mafikizolo from South Africa and Naija's Davido.

Diamond who was the favourite of the category was among the first artists who sent a congratulatory message to Sauri Sol. This is a good gesture coming form the Tanzanian who has scooped most regional awards in 2014.

Sauti Sol took Diamond's online marketing machine head on and managed to rally Kenyans online to each cast a vote. The Number One singer posted on his Facebook page.

Miss Tanzania 2014 Kufungwa Miaka Mitatu Endapo Atabainika Alighushi Vyeti

$
0
0
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) wamesema endapo mrembo wa Taifa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti Mtemvu, atabainika kudanganya umri wake kwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, atakabiliwa na kifungo cha kwenda jela kwa muda usiopungua miaka mitatu, imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Rita, Josephat Kimaro, alisema adhabu hiyo imewekwa kwa wale watakaofanya makosa ya kutoa taarifa za uongo ili waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa au kifo.

Kimaro alisema kwamba adhabu hiyo humpata mkosaji hapo hapo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa taarifa zake na kulinganisha na zile alizoziwasilisha Rita ili kupatiwa cheti kipya.

"Kifungu namba 28 (3) cha sheria ya kuandikisha vizazi na vifo kimeweka adhabu kwa makosa ya kutoa habari za uongo na adhabu hiyo hutolewa hapo kwa hapo," alisema Kimaro.

Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (sura ya 108) toleo la mwaka 2002, ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili, na pia kosa la jinai kughushi.

Alisema kwa sasa suala la Sitti limepelekwa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo (Philip Saliboko) na mara baada ya kukamilika taarifa zake zitatolewa hadharani ili jamii ifahamu ukweli.

"Huo mkanganyiko tumeshaupokea na tunaufanyia kazi, tutafanya kazi hii kwa kuzingatia na kufuata sheria na miongozo," Kimaro alisema.
"Rita imebaini kuwapo na udanganyifu wa aina hiyo ambao unafanywa na waombaji kwa kutuma maombi mapya baada ya kutakiwa kupeleka vyeti ili wapate ajira, kujiunga na vyuo au kusafiri nje ya nchi.

~Chanzo: Gazeti la Nipashe

Breaking News: Mwimbaji Chid Benz Akamatwa na Madawa ya Kulevya Airport

$
0
0
Kuna Taarifa kuwa Msanii Chid Benzi amekamatwa na Madawa ya kulevya Airport Dar es Salaam ambapo alikuwa anaelekea Mbeya Kufanya Show ya Instagram..Amekamatwa na Kete Kumi na nne za madawa ya kulevya , pia na Bangi Misokoto miwili ambazo zilikuwa katika mfuko wake wa Shati .

Chid alikuwa ameongoza na Mwanamuziki Sheta ambae yeye aliruhusiwa kuendelea na safari
Baada ya kuhojiwa inasemekana Chid Alijitetea kwa kusema ni kwa ajili ya matumizi yake Binafsi , Chid kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi...


UKAWA kufanya Mkutano Jangwani siku ya Jumapili

$
0
0
Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unawatangazia Wananchi wote wazalendo wapenda nchi yao kuhudhuria katika Mkutano Mkubwa wa aina yake wenye lengo la kuizika CCM siku ya Jumapili katika viwanja vya JANGWANI kuanzia saa 8:00 Mchana. 

Njoo ushuhudie tukio muhimu la kihistoria ambapo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda UKAWA watakavyosaini Makubaliano ya pamoja ya ushirikiano ktk Chaguzi zote zijazo kuelekea 2015.

Mkutano utarushwa live na kituo cha ITV.

Njoo ujionee namna madalali wa nchi hii watakavyoumbuliwa na katiba yao feki kusasambuliwa!

Mpe taarifa hii na mwenzako.

UKAWA TUMAINI LETU!

Chupuchupu Kubakwa, Kusingizia Nina Ukimwi ilinisaidia

$
0
0
Habar ya humu wadada na wakaka... Wakubwa na wadogo kwa ujumla..
Nimekumbuka hili tukio lililonitokea kitambo kidogo japo si sana lakini bado nakumbuka na ningependa kushare na ninyi hapa..najua jf ina watu wengi na wa umri mbalimbali tunaweza kusaidiana kinamna moja ama nyingine"..

Nakumbuka siku ya tukio nilipokea simu namba mpya na jamaa alijitambulisha kama "Michael", sikumfahamu awali ila aliniomba niwe mpole nitamfahamu polepole na jioni yake aliniomba tule dinner wote sikubisha!".. Jioni ya saa moja niliweka mambo yangu vizur na kujiandaa mpaka saa mbili Tayar kulikuwa Giza,nikajivalia kigauni cha usiku kilichoacha sehemu kubwa ya mapaja yangu wazi!.nilichukua pikipiki mpaka sehemu husika (jina sipakumbuki vizuri), baada ya kushuka kwel nilimuona lkn bado sikumfahamu..tulikaa sehemu kuna kagiza taa kwa mbali hatukuongea sana akaniuliza ntakula nn nikamwambia..chakula kikaletwa tukala tukashiba akaniambia hakai mbali na pale tulipo ivo twende kwake aliniandalia kinywaji..nikakubali tukaenda. Kiukwel hapakuwa mbali kama kupanga basi alijipanga vyema...
Tulipofika aliniwekea Bia mbili za Safari baridi..sikuwa na mzuka sana siku hiyo na ivo alitegemea ningelewa mpaka nisijiweze lkn haikuwa ivo kwan zile bia zilinifanya niwe na nguvu zaid..baada ya mda kwenda ilitimu saa nne nikamuomba kuondoka ndo tatizo lilipoanzia hapo...akataka tufanye mapenzi tena kwa lazima nikagoma...tulibishana na kuvutana akaona namzid nguvu huku mda unazid kwenda...mungu anisamehe maana nilipata wazo la kumcoma kisu nikimbie lkn alilock mlango na ufunguo akautupa chini ya uvungu..baada ya mda nilisikia anaongea na simu aliporud akaniambia si najifanya mjanja sitaki kumpa papuchi basi nitaitoa kwa lazima..mara nilisikia group la wanaume weng kwa nnje wakigonga wafunguliwe hapo pombe yote ilipotea kichwan nikajikuta nasmile huku nawaza cha kufanya..nilimvuta taratibu nikamuigizia uwoya haoni ndani...nilimbembeleza kama motto kwa sauti ya kimahaba sana huku machozi yakinitoka..nilisingizia ukimwi huku namuangalia usoni kama kwel vile..alinyong'on yea akaniamni.aliwatoa wale wanaume akanirudisha nilipokuwa nakaa saa tano akinishukuru njia nzima.nilifika na kulala tu...

Wanaume nawaheshimu lkn sijui nawaonaje..bado weng wenu mnatakiwa kujifunza mengi juu ya mwanamke...ni kiumbe adimu hlf mapenzi sio amri ni hisia .kwa wale wapenda ofa na kukutana na mastrangers angalieni sana yasijetokea puani.
Usikuni mwema.

Rais Barack Obama Alipomkumbatia ''Mgonjwa wa Ebola''

$
0
0
Nurse Nina Pham aliekuwa kapata maabukizi ya Ebola baada ya kusibitika Dawa imemsaidia na sasa amepona Ugonjwa huo alipoenda kumtembelea Rais Ikulu.(Sasa kama vipimo vimepepesa macho Obama shauli yako)
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live


Latest Images