Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Rose Muhando Adaiwa Kutumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
HUKU mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano linateremka nayo.

Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za kupokea fedha za shoo halafu hatokei tu!

WATOA MADAI
Hivi karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo za Injili.

“Sisi tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.
“Huwa anafika hatua anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo maana mtu anaweza kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa kutoka ndani kwake.

“Kwa hiyo jamani, si suala la kumwandika tu kwamba anaingia mitini na fedha za watu bali mumsaidie Rose kama kweli mnampenda, sisi wenyewe tunamwombea kwa Mungu kila siku,” alisema mama mmoja kati ya hao waliofika lakini bila kutaja majina yao.

MADAI SUGU
Madai ya kwamba, Rose anatumia madawa ni ya siku nyingi, wengi wamekuwa wakisema wana uhakika, wengine wanasema wanasikiasikia tu lakini hawana uhakika.

Magazeti ya Global (Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Jumatano, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi) yameshapokea madai hayo kwa muda mrefu lakini kilichokuwa kikifanyika ni kuendelea kumchunguza msanii huyo kuhusu madai hayo.

RISASI LAINGIA KAZINI KUCHUNGUZA
Kufuatia madai ya akina mama hao waliojitambulisha ni waumini wa kutoka katika kanisa moja la kilokole jijini Dar, gazeti hili liliamua kuingia kazini kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli au uongo wa madai hayo.

WATU WA KARIBU NA ROSE
Mtu wa kwanza kumtafuta ambaye gazeti hili liliamini kwamba anaweza kujua chochote kuhusu madai hayo ni mratibu wa Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka kwenye baadhi ya mikoa, Alex Msama.
Msama: “Mimi siwezi kusema ni kweli kwani sijawahi kumwona akitumia wala sijui kama ameathirika.”

Risasi Jumatano likamsaka Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania (Chawaita), Stela Joel: “Mimi sijui, kama unasema kuna watu wamekuja ofisini kwenu na kutoa madai hayo, basi wamwombee. Lakini tutachunguza.”

MCHUNGAJI
Risasi Jumatano pia lilibahatika kuzungumza na mchungaji mmoja (jina tunalo) ambaye alisema ameshawahi kusikia taarifa hizo akamuuliza Rose lakini alimkatalia kuwa si madai ya kweli.

“Ila ninachojua mimi ni kwamba, Rose amekuwa akitumia dawa f’lani (akazitaja jina). Hizi ni dawa zinazopatikana kwa njia ya sindano. Mara nyingi mtu akiwa hajiwezi kwa maana ya kushindwa kufanya kazi anachomwa hizi zinampa nguvu.

“Niliwahi kusikia kwamba, kuna daktari mmoja katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (akamtaja jina). Huyu ndiye aliyekuwa akimchoma sindano zenye dawa hizo Rose pale mwili unapokuwa dhaifu.

“Ila madhara yake sasa, dawa ikiwa imekwisha mwilini, mtu anakuwa mlegevu, anahisi kizunguzungu au kulalalala, kutokwa jasho jingi na kuhisi anaumwa kiasi kwamba ukimwona unaweza kusema ni teja. Ni dawa ghali sana kwa dozi moja, nadhani ni shilingi laki sita,” alisema mchungaji huyo.
Akaongeza: “Nasikia Rose amefika mahali huwa anajichoma mwenyewe akipata dozi. Kwa hiyo kwa suala la kubwia unga nadhani alilikanusha.”

ROSE MWENYEWE SASA
Risasi Jumatano, juzi lilimpigia simu Rose lakini hakupokea hata baada ya kurudia kumpigia mara kadhaa. Likamtumia meseji na kumsomea mashitaka yote, akajibu:

“Samahani sana nawaomba mnipumzishe kuniandika...najua ni nani na kwa nini ananitenda hivyo, ni kwa sababu anataka kunitumia kwa faida yake na ni mtu hatari sana kwangu na kwa taifa zima.
“Mtu huyo anafanya haya ili kuniziba mdomo kwani najua siri zake nyingi na nzito, nashindwa kusema ataniua.”

Hata hivyo, Rose alipotakiwa kumtaja kwa jina mtu huyo ambaye Risasi Jumatano halimjui, alikataa katakata akisema anaogopa!

Ray C Aifuta Kesi ya Mwanamuziki Chid Benz

$
0
0
Wakati nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe.

Akiongea na Gpl, Ray C alisema ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai.

“Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na wala sitaki kesi naye, lakini kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika tiba ya Methadone,” alisema.

Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya.

“Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja. Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu,” yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni.

Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi

Wanamziki wengine wa Bongo Fleva Muige mfano wa Insp Haroun, hongera kwa kutimiza miaka 10 ya ndoa

$
0
0
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’ au ‘Babu’ anatarajiwa kufanya shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya ndoa yake, itakayofanyika Octoba 25 katika ukumbi wa Mpoafrika Devis Corner, Temeke Dar es Salaam.

Kiingilio katika shoo hiyo iliyopewa jina la ‘Usiku wa Wakongwe’ kitakuwa sh 5,000 na itaanza saa mbili usiku na kuendelea ambapo atasindikizwa na wakongwe kibao.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Inspector alisema kuwa, anaomba mashabiki wa muziki wake wamwagike kwa wingi katika ukumbi huo kwa lengo la kupata burudani ilikwenda shule.

Alisema atasindikizwa na Luten Karama, TID Mnyama, Scorpion Giirlz (Isabela), LWP & Mabaga Flesh, Young Tuso & Drama Boy na Kimbiza Dj’s.

Inspector alisema kuwa siku hiyo atafanya shoo kubwa ambayo hajafanya kwa muda mrefu hivyo wapenzi wa kazi zake wanatakiwa kumwagika kwa wingi.

Mkongwe huyo alishawahi kutamba na ngoma zake kama Asali wa Moyo, Sharubu za Babu, Mungu ndio anapanga na nyingine nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Rais aipasua kichwa Ukawa 2015

$
0
0
Baada ya vyama vinne vya upinzani nchini kusaini makubaliano ya kushirikiana pamoja na kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zote zijazo, umoja huo sasa unakabiliwa na kazi ngumu ya kuweka sawa mambo, ikiwa ni pamoja na mchakato wa kumpata mgombea urais, kabla ya filimbi ya uchaguzi kupulizwa.

Vyama hivyo vitalazimika kufanya uamuzi katika sera tofauti za vyama vyao, kukabiliana na Sheria ya Uchaguzi, taratibu za kupata wagombea wa kuanzia ngazi ya chini hadi urais na jinsi ya kuendesha kampeni zao kabla ya kuwaendea wananchi kuwaeleza kuwa wameshajizatiti kukabiliana na chama tawala, ambacho kina mtandao karibu nchi mzima uliojengwa kwa miaka mingi.

Vyama hivyo vimeibuka na nguvu mpya baada ya kuunganishwa na hoja ya kutetea Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilielezewa kuwa ilitokana na maoni ya wananchi na hivyo kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupambana na wajumbe wa CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Vyama hivyo, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD vilisusia mchakato wa Katiba kwa kile vilichodai kuwa ni kutoridhishwa na mambo yalivyokuwa yakiendeshwa na sasa umoja wao umekwenda mbali zaidi kutaka kushirikiana kwenye chaguzi.

Kutekeleza hilo, Jumapili iliyopita wenyeviti wa vyama hivyo, Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF), Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Dk Emmanuel Makaidi (NLD) walisaini makubaliano ya ushirikiano huo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Jangwani.

Moja ya kazi ngumu inayoukabili umoja huo ni jinsi ya kumpata mgombea wa urais atakayetoa upinzani mkubwa zaidi kwa mgombea wa chama tawala na kuendelea kupunguza kura za CCM baada ya mafanikio ya mwaka 2010 ya kupunguza asilimia 20 za kura alizopata RaisJakaya Kikwete mwaka 2005.

Exclusive : Diamond Kupewa PHD Chuo Kikuu cha Mlimani, Sasa Ataanza Kuitwa Doctor Nassib.

$
0
0

TANGAZO NDUGU ZANGU: Ifikapo Tarehe 8 Novemba Saa 10 jioni,Kijana mwenzetu ambaye sisi tunamdharau na wengine wapuuzi kabisa kwa kufeli kwao maisha wana wivu na wanathubutu kumzomea atakuwa anatunukiwa Shahada ya Uzamivu(Phd) na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kuthamini mchango wake kwenye jamii…Honorary Phd hata Raisi wetu anayo…Alongside DIAMOND mwingine atakayepewa Shahada hii ya Heshima kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence Kazaura ambaye amewahi kuwa VC wa UDSM miaka ya nyuma!! Ningependa kuwakaribisha wale Wazomeaji woooteee wenye sauti mbaha kabisa waweze kufika kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA Vimemfikisha hapa.. SHKAMOO DR.NASIBU ABDUL au Pengine DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka swaga DR.PLATNUMZ BABY! Sky is never the limit!Hongera kwa Mameneja waliomfikisha DIAMOND hapo alipo

Hatimae Chid Benz amepata dhamana.

$
0
0
Taarifa ambazo zimetoka muda mfupi uliopita zinasema kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ asubuhi ya leo October 29 amepata dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa.
Chid Benz alipandishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana October 28 na kusomewa mashtaka matatu yaliyokuwa yakimkabili ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Leo asubuhi amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya,kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tena October 11 mwaka huu 2014.

Ajali Mbaya Yatokea Arusha , Lori Lagongana Uso kwa Uso na Kifodi na Kuua

$
0
0


Watu 9 wamekufa na wengine 2 wamejeruhiwa baada ya basi dogo la abiria Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori mafuta katika eneo la Usa River, Arusha 

Wema Sepetu Sasa Ajuta Kuwa Maarufu, Asema Umaarufu Unamtesa

$
0
0
‘BEAUTIFUL Onyinye’, WEMA Isaack Sepetu ‘Madame’ ametoa ya moyoni na kufichua kwamba maisha yake ya umaarufu anayoishi yanamtesa kwa asilimia 40.

Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa filamu alisema anafurahia maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na kuandikwa na vyombo vya habari mara kwa mara.

“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.

“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi sana, kuna wakati mtu anaweza kukuandika habari inayokufanya ushindwe hata kutoka nje na kubaki ndani tu,”alisema.

Wema alisema kuna wakati huwa anatamani asingekuwa maarufu kwani akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida lakini hupokelewa kama habari kubwa na kuongelewa sana.

“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.

Haya yamechangia Laveda kutoka mapema Big Brother

$
0
0
WASHIRIKI wa Big Brother Afrika wanaotokea ukanda wa Afrika Mashariki wapo katika wakati mgumu baada ya wengi wao akiwamo Laveda wa Tanzania kutoka katika wiki za mwanzoni za mashindano hayo.

Juzi Jumapili tulimshuhudia Laveda na Alusa wa Kenya wakitoka katika mashindano hayo kwa mkupuo licha ya wiki iliyopita Esther wa Uganda na Sabina na Kenya na kuaga.

Kufuatia sakata hilo, hivi sasa Afrika Mashariki imebakiwa na washiriki wanne akiwamo Frankie na Arthur kutoka Rwanda, Idris toka Tanzania na Ellah wa Uganda.

Kinachoonekana nchi nyingine kuungana na kupiga kura dhidi ya washiriki wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, kosa walilolifanya Idris na Laveda kupendekeza Frankie kutoka Rwanda aingie kwenye kinyang’anyiro, limesababisha nchi hiyo wiki hii kumpigia kura Ellah kutoka Uganda na kumwacha Laveda akirudi nyumbani.

Laveda amekuwa mshiriki aliyepigiwa kura na nchi moja pekee, huku akiambulia kura chache zaidi akifuatiwa na Alusa kutoka Kenya ambaye naye kura zake hazikutosha.

Hapa bado kuna shaka iwapo Watanzania waliamua kutompigia kura za kutosha Laveda kutokana na kilichotokea katika sherehe fupi iliyofanyika wikiendi iliyopita au kuna sababu nyingine.

Hata hivyo, Laveda wiki iliyopita aliongoza kwa kupigiwa kura 11 na washiriki wenzake, wakimtaka aingie kwenye kinyang’anyiro cha kupigiwa kura.

Huenda pia hali hii iliwakatisha tamaa Watanzania na nchi nyingine kutompigia kura.

Laveda amekuwa na uraibu wa kupuliza tarumbeta mara kwa mara anapokuwa katika jumba hilo, jambo hilo lilikuwa linawakera washiriki wenzake na hata baadhi ya watazamaji.

Licha ya kwamba alianza mchezo vizuri wiki ya kwanza na kuwavutia Waafrika wengi, Laveda alitibua mwishoni baada ya kudaiwa na washiriki wenzake kwamba ni rahisi kwa mwanaume yeyote kumpata iwapo atamhitaji.

Mpaka anaondoka katika jumba hilo, Laveda alikuwa ameingia katika uhusiano wa kimapenzi na mshiriki Permithias kutoka Namibia na kuonekana mara kadhaa wakibusiana, jambo lililozidi kumweka mrembo huyu matatani.

Kibadeni: Phiri, Matola watimuliwe Simba, Uwezo Wao Umefikia Mwisho

$
0
0
 KOCHA wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni, amesema kuwa uongozi wa klabu ya Simba umekosea kuwasimamisha wachezaji Shaaban Kisiga, Amri Kiemba na Haroun Chanongo kwani tatizo lipo kwenye benchi la ufundi.

“Tatizo la Simba ni benchi la ufundi, tatizo si Chanongo wala Kiemba au hata Kisiga kama wanavyoona viongozi. Uongozi wa klabu ni mzuri, lakini wanatakiwa kujua kuwa hakuna jipya kwenye benchi la ufundi na ndiyo maana timu inafanya vibaya,” alisema Kibadeni.

“Kuwasimamisha wachezaji hao ndiyo kuiweka timu pabaya zaidi, inakuaje Simba ina wachezaji wazuri wa timu za taifa lakini wanapokuwa kwenye klabu wanashindwa kucheza vizuri?

“Nafikiri ni muda sasa timu ipewe makocha wazawa ukizingatia kuwa kuna wengi wamehitimu na wengine wameonyesha kufanya kazi inavyotakiwa kama Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Minziro wa JKT Ruvu.

“Uwezo wa Phiri na Matola umefika mwisho kwenye kuiokoa Simba, ubunifu wa ziada unahitajika ambao kwasasa hawana.

“Tatizo la viongozi wanaweza kuwa wanamtetea Phiri na mshauri wake ambaye ni Matola badala ya kuwatimua.”

Kibadeni ambaye pia ni mwanachama wa Simba,, aliongeza: “Mambo mengi yamebadilika, wakati Phiri akipata mafanikio na Simba pale awali, alikuwa na viongozi wanaomsaidia kwenye mambo ya nje ya uwanja huku ya ndani ya uwanja akiyafanya mwenyewe.”

Kibadeni ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake binafsi katika eneo la Chanika, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Unamkataa Mtu Halafu Unamtangaza Chuo Kizima au Ofisi Yote Hadi Walinzi Wanajua

$
0
0
Kuna watu wa ajabu sana.
Anatokea mtu anaweza kuwa mwanamke au mwanaume kuomba mahusioni ya kimapenzi kwa mwingine.

Sana sana kwenye jumuia mfano chuo,maofisini na ata kwenye viwanda mahali ambapo watu wanakutana mara kwa mara.

Mtu amekutungoza umemkataa au amekukuta tayar una mtu unaishi nae kuna sababu gan kumtangaza kwa watu wote kua fulan nimemkataa.

Kinachokufanya kila mtu
kumwambie kua umekataa mtu fulani nini?
Ili uonekana unatafutwa sana na watu au mzuri sana.

Ukimkataa mtu na yeye akikuelewa basi hakuna sababu yakutangaza chuo kizima au ofisi yote adi walinzi wajue.

Wenye tabia hii acheni Mara moja.

Baada ya Kumkimbia Mumewe, Aunt Ezekiel Adungwa Mimba na Mume wa Mtu

$
0
0
Ama kweli kuolewa kunazidi kuwa kama fashion. Mnamo mwaka 2012 Aunt Ezekiel aliolewa 
kwa mbwembwe zote na kijana Sunday Del Monte na baadae kwenda kuishia nae huko Dubai.
Sunday wakati huo pesa ilikua si tatizo kwake na hata kukubali kuolewa na kijana yule ilikua ni
kufata pesa zake.

japo baadae aliwekwa kizuizini kutokana na kuishi huko Dubai Kinyume na sheria na hadi sasa 
nasikia bado yuko nyuma ya Nondo akisubiria mwisho wa hatma yake. Baada ya sakata hilo aunt
Ezekiel aliamua Kuamua kurudi Bongo na kuendelea kula bata kama kawa kama dawa

Hivi sasa Mwigizaji huyo mashuhuri kapachikwa Mimba na inaedaiwa kuwa mimba hiyo ni ya mume 
wa mume wa mtu. Habari za mimba hiyo alikua hataki zijulikane na alikua akijificha ficha sema ndio 
wambea tukazinyaka.......Alikua anasema anatamani kupata mtoto sasa aliyokua anatamani yametimia.

Happy birthday Mama Kijacho, Picha hiyo jana kwenye birthday nadhani unaona mwenyewe

Je ni Kweli Lady Jay Dee Anampiga Dongo Gadner kwenye Tangazo la Radio la Mgahawa Mpya

$
0
0
Mdau mmoja Huko Jamii Forums Amefunguka Hivi kuhusu Tangazo la Mgahawa Mpya wa MOG ambalo amelifanya Lady Jady linalorushwa Radio Mbali Mbali:

"Naamini wengi wamesikia tangazo jipya la mgahawa wa Jaydee unaokwenda kwa jina jipya la MOG na kikolombwezo cha LIFE IS TOUGH na mwishowe anamalizia na YAHAYA UNAISHI WAPIII
Wenye kujua mafumbo wanajua anamaanisha nini!!! Jaydee ni mtu wa nongwa sana na anapenda visasi kapitiliza, ukigombana naye hakuachi mpaka akutungie wimbo wa vijembe kafanya hivyo kwa wengi tu wakiwemo Ruge, Mwana FA, na sasa vijembe vyote ni kwa mtalaka wake, sio kwenye mitandao kwenye vyombo vya habari na sasa kwenye matangazo yake

Mkiwa wanandoa hakuna mmoja anaweza kujvunia mafanikio bila ya mwenza wako, hata ile tu kuhisi kuwa nyumbani nina mke au mume ananisubiri hata kama hana kazi inakupa nguvu ya kufanya kazi kwa utulivu na amani

Huyu mtalaka wake alikuwa ni mme wa mtu mwenye ndoa halali na mtoto juu, kwa kutumia influence yake wakati huo ya vijisenti na umaarufu akampoka asiye nguvu mume....akumbuke mtenda hutendwa.....

Aukubali ukweli, we are living in the world of impermanence...! Nothing last forever, yeye si wa kwanza kusuffer broken heart na hatakuwa wa mwisho... It happens always and ever... Na katika maisha huwezi kupata kila kitu ni ukweli mchungu! Vijembe na mafumbo havitabadili ukweli wala kumpunguzia maumivu" By Mshana jr

Bifu kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba ni Miradi ya Watu

$
0
0
Baada ya kuanzisha mashindano ya mbio kati ya farasi(Dimond) na kobe(kiba) na kutaka kuiaminisha dunia kuwa kobe ana mbio kushinda farasi, hatimaye ile miradi iliyotangazwa kwa nderemo na vifijo imeanza miradi hiyo yote inaonekana ilibuniwa kwa ustadi kabisa kwa kumtumia kiba na mtu aliyepo juu katika game ili kusudi pesa zipatikane kwa watu hao.

Miradi hiyo ni pamoja na Tshirt zilizoandikwa Kiba ni mfalme wa muziki, Dimond mwisho Tandale mjini kote kiba, Cd zilizoandikwa Kiba V Dimond, kwa mtu yeyote mwenye akili atagundua kumbe lile zomeazomea na mambo ya ajabu kama Dimond eti alisema mbeya hamna hoteli ya yeye kulala ilikuwa ni mipango ya watu wachache ya kutengeneza hela, laiti ingekuwa siasa ungesema ni siasa za maji taka, Kumbe hili bifu la kupikwa lilianzishwa ili watu fulani wapate hela na kwa uhunguzi wangu hawa watu wanajiita Team kiba.

Imani yangu ni kwamba mashabiki wa Kiba wapo tena wastaarabu lakini hizi hype zilizoanzishwa za Kiba V Dimond ni kwaajili ya manufaa ya watu wachhache ambao kwa maslahi yao wanataka kumchafua "Chibu Dangote" ili waje kutuuzia Tshirt na Cd zao uchwara ,kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuvaa Tshirt imeandika Dimond mwisho Tandale!!!

Tussuport muziki mzuri...

Ukweli Kuhusu Diamond Kupewa Udoctor na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

$
0
0
Jana kuliendea uvumi katika mitandao ya Kijamii kuwa Diamond atatunukiwa Udaktari na chuo kikuu cha Dar es Salaam kutoka na mafanikio yake kimuziki ...
Habari hiyo si ya kweli ..Haya hapa chini na majibizano kati ya Profesa Mgaya na mmoja wa viongozi wa Diamond...


Aliyejilipua kwa risasi Arusha Aibua Mambo Mazito..Kumbe Sababu ni Vimada

$
0
0
SAKATA la Mkurugenzi wa Kampuni ya Kitalii ya DAGT, Timoth Mroki, kujiua kwa kujilipua kwa risasi, limeibua mambo mapya kutokana na kuelezwa kuwa wivu wa kimapenzi.
Habari zilizopatikana jijini hapa, zinasema kuwa Mroki (36), alikuwa na vimada wawili ambao ni wake za watu na kuwa kabla ya kujilipua kwa risasi na kupoteza maisha, alitoa taarifa kwa wanawake hao (majina yanahifadhiwa).
Imeelezwa kuwa Mroki alikuwa akitoka na wanawake hao kila mmoja kwa muda wake, lakini baadaye siri hiyo ilianza kuvuja na hatimaye vimada kufahamiana, ikiwa ni pamoja na mkewe kuanza kupenyezewa taarifa hizo.
Mroki, ambaye pia ni Meneja wa Operesheni na Masoko wa Kampuni ya Tanzania Bush Camp, alijiua kwa kujipiga risasi Oktoba 25, mwaka huu, saa 1:00, baada ya kubaini kuwa vimada wake hao wamefahamiana.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu zimesema kuwa, vimada hao baada ya kufahamiana, walikutana na kufanya mazungumzo kisha kupiga picha pamoja na kumrushia kupitia simu ya mkononi.
Kugundulika kwa siri hiyo, kulizusha taharuki kwa Mroki, hivyo kusababisha kuyumba kwa uhusiano baina yake na vimada hao, akiwemo mmoja ambaye pia ni mshirika wake kibiashara.
“Hawa wanawake wana siri nzito kuhusiana na kifo hiki kwa sababu kabla ya kufanya uamuzi, aliwasiliana nao…kikubwa awali walikuwa hawafahamiani ila baadaye walikutana na kuungana kuwa kitu kimoja.
“Haifahamiki ni kwa vipi walijenga urafiki, ila watu wa karibu wanasema walijipanga kumkomoa ili afilisike kwa kuwa kila mmoja alikuwa na malengo yake,” alisema mtoa habari wetu.
Kuungana kwa wanawake hao kumlichanganya Mroki, ambaye tayari uhusiano wake nyumbani pia ulianza kuwa tete baada ya mkewe kuhisi kuna mambo yanafanyika kinyume cha utaratibu.
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa miongoni mwa wanawake hao, yupo aliyejenga uswahiba na mke wa marehemu huku uhusiano wa kimapenzi ukifichwa chini ya mwamvuli wa biashara.
Chanzo chetu kimesema kuwa, kutokana na ukaribu huo, familia hizo zimekuwa na kawaida ya kutembeleana, ikiwa ni pamoja na watoto kukaa kwa siku kadhaa nyumbani kwa kimada mmoja.
Imeelezwa kuwa kutokana na kugundulika kwa siri hiyo, Mroki alichukua uamuzi wa kujimaliza ili kukwepa aibu mbele ya familia.
“Kugonga gari si sababu ya Mroki kujiua, ni kutokana na kutingwa na mambo mengi kichwani, hasa baada ya siri ya kimapenzi kuanza kubainika,” aliongeza mmoja wa rafiki wa marehemu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema Mroki alijiua kwa kujipiga risasi kifuani kwa kutumia bastola aina ya KEL –TEC yenye namba HCB21.
Katika taarifa yake, Kamanda Sabas alisema kabla ya tukio hilo, Mroki alikuwa na gari namba T222CMX, aina ya Isuzu Double Cabin, iliyokuwa ikitokea Mbauda kwenda katikati ya jiji.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na msongamano wa magari, Mroki alitanua barabara kukwepa foleni huku akiwa katika mwendo kasi.
Alipofika maeneo ya Shams, aligongana na gari la mizigo, mali ya Kampuni ya Gupta, lenye namba T548 BRL.
Taarifa ilisema pamoja na kusababisha ajali hiyo, Mroki aliendelea na safari yake ndipo madereva wa bodaboda walipoamua kumfukuza na kumkamata eneo la kona ya Nairobi Ngarenaro.
Mroki aliporejea eneo la tukio na kuulizwa sababu za kusababisha ajali na kuendelea na safari, alitoa bastola na kufyatua risasi mbili hewani na ya tatu kumpiga kifuani.

Msiba Bongo Movies:Muigizaji Mzee Manento Amefariki Dunia.

$
0
0
Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.

Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani

Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina. 

Wema na Aunty Husagana! Wadendeka Laivu..Diamond Akasirika Aondoka na Wapambe Wake

$
0
0
Stori: Musa Mateja na Imelda Mtema
Ni sheedah! Pamoja na kukanusha kwa kutumia nguvu kubwa, nyuma ya ushosti wa mastaa grade one wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Aunty Ezekiel kuna siri nzito ikidaiwa kwamba wawili hao husagana.

TUKIO BICHI 
Madai hayo ya muda mrefu huku wenyewe wakisisitiza si ya kweli, yameibuka upya juzikati baada ya warembo hao kuonesha mahaba niue au nikongorowe kisha ‘kudendeka’ hadharani na kusababisha mwandani wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukasirika na kuondoka eneo la tukio akiambatana na timu yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).

ILIKUWAJE? Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri usiku wa kuamkia Oktoba 28, mwaka huu ndani ya Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar ambapo Aunty alikuwa akisherehekea siku ya yake ya kuzaliwa ‘bethidei’.

WEMA ATOKEA DUBAI 
Shughuli hiyo ilitawaliwa na matukio baada ya Wema kuwasili ukumbini hapo akitokea nchini China kupitia Dubai alikokwenda hivi karibuni kwa biashara binafsi ikidaiwa kwamba amerejea na mkwanja wa kutosha.

Wema alitinga ukumbini hapo saa 7:15 usiku na kuwakuta wadau wakiendelea na sherehe hiyo ambapo mara tu baada ya kufika alikumbatiana kimahaba na  Aunty zoezi lililochukua dakika kadhaa wakiwa wamenasiana huku wakifunika nyuso zao kwa zile nywele nyingi za Wema hivyo kilichoendelea humo ndani hakikujulikana. Walipojifunua kwenye nywele ndipo ikabaini kwamba kumbe walikuwa ‘wakidendeka’ bila kujali wingi wa kamera.

WASHUTUMIWA 
“Mungu wangu, leo mambo hadharani. Mbona ni sheedah? Yaani wanadendeka hadharani! Kwa vyovyote vile Wema na Aunty husagana,” alisikika mmoja wa waalikwa.

Mmoja wa waigizaji chipukizi alidakia: “Yaani utadhani wapenzi kabisa maana kila mmoja anaonesha hisia za kumisiana. Hawaogopi kuambiwa wanasagana? Haya bwana, yetu macho maana leo tutaona mengi. Vitendo kama hivi ni vya kulaaniwa vikali na kuwakumbusha kwamba wao ni kioo cha jamii.”

DIAMOND AKASIRIKA, AONDOKA 
Kufuatia  hali hiyo, Diamond alionekana kukasirika na kushindwa kuvumilia hivyo aliamua kuwaacha wajinafasi kwa kuondoka ukumbini akiwa ameambatana na timu yake. Waalikwa waliokuwa ndani ya ukumbi huo waliendelea kupigwa butwaa na kitendo hicho hasa Diamond alipoamua kusepa huku nyuma Wema na Aunty wakibaki huru na kuendelea kufanyiana mambo ya kimahaba mara nyingine wakati wakilishana keki kwa staili ya njiwa.

AMANI LAMVAA AUNTY 
Baada ya kuona hali hiyo, paparazi wa Amani aliyekuwa ukumbini hapo alimvaa Aunty na kumuuliza kwa nini ameamua kuonesha hali hiyo mbele ya kadamnasi ambapo alijibu hakuna mambo ya usagaji. Alisema hali hiyo ilitokea tu maana yeye na Wema ni marafiki ambao wameshapitiliza hivyo wamejikuta wakiwa kwenye hali hiyo bila wao kuona kama ni tatizo. “Kwani nani asiyejua kama mimi na Wema ni marafiki, suala la kukisiana ni jambo la kawaida kwetu.
GPL

Gazeti Lamchafua Wolper na Uwoya eti Wanatuma Picha za Utupu Kwa Ali Kiba , Wolper Akasirika na Kusema Haya

$
0
0
Gazeti Moja la Udaku leo limemchefua Mrembo Mwigizaji Jack Wolper Baada ya Kuandika  Wolper, Uwoya Wamgombea Ali Kiba Wamtumia Picha za Utupu Kumtega...

Jisomee Hapa :

Kama wewe ni Mshabiki wa Wolper Embu Toa Ushauri wako Hapo ni nini Afanye Dada Jack Wolper kuhusiana na Gazeti Hilo Kumchafua.

Martin Kadinda Amuanika Mpenzi Wake Anayetarajia Kufunga Nae Ndoa

$
0
0
Na Imelda Mtema
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ambaye siku za nyuma alikuwa na mpango wa kufunga naye ndoa mapema mwaka huu lakini kukatokea tofauti kidogo wakahairisha zoezi hilo.

Akizunguza na  mwandishi wa habari hivi karibuni, Kadinda  aliweka wazi kuwa huyo ndio mke wake mtarajiwa na Mungu akipenda watafunga naye ndoa mwakani.  “ Ni kweli ni mpenzi wangu nampenda sana na Mungu akipenda ndiye mke wangu ambaye nitafunga naye ndoa mapema tu mwakani na Mungu atusimamie katika hilo,” alisema Kadinda.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images