Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Kampuni ya Apple afunguka na kudai anajivunia kuwa Shoga

$
0
0
Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza jinsia yake akisema kuwa ''anajivunia kuwa shoga''..
Bwana Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu wanaong'ang'ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg.
Amekuwa wazi kuhusu jinsia yake,lakini pia amejaribu kuweka maisha yake katika faragha hadi sasa alisema.

Wiki hii Bwana Cook alitoa changamoto kwa jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia zinaheshimiwa.
''Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine'',alisema bwana Cook.
''Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao ,ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha''aliongezea.
Bwana Cook amesema amekuwa wazi kuhusu jinsia yake na watu wengi wakiwemo wafanyikazi wenzake katika kampuni ya Apple,lakini hilo halikuwa chaguo rahisi kutangaza hadharani kuhusu jinsia yake.





Bunge lachomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais agoma kuachia madaraka

$
0
0
Mbali na maafa makubwa yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na majengo ya bunge kuchomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais aliye madarakani amegoma kuachia madaraka yake.
Blaise Compaore rais wa Burkina Faso aliyekaa madarakani kwa miaka 27 anatajwa kuwa mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi na bado anasisitiza kuwa ana miezi 12 zaidi ya kuendelea kuwepo madarakani kabla ya kukabidhi madaraka kwa rais ajaye.
Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya machafuko hayo.
Chanzo cha machafuko hayo kinatajwa kuwa ni kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangemfanya Blaise Compaore kubakia madarakani kwa kipindi kingine zaidi.

Taarifa zinasema jeshi limelazimika kuongoza nchi hiyo ili kurejesha utulivu.

Wema Sepetu Ammwaga Diamond..Wakutana Kwenye Sherehe Wachuniana Kama Hawajuani

$
0
0
Na Musa mateja
Safari hii ndiyo basi tena! Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.


KUMBE NI MUDA MREFU TU
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.

SAFARI YA CHINA
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man.

KAMA MBWAI, IWE MBWAI 
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’ hivyo akampuuza na kwenda zake China!

AHADI HEWA?
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati Madam alimuomba Dangote au Chibu ampe fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo alikubali lakini siku zikawa zinayoyoma bila dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu mwenyewe hawezi kumsaidia?

ANAMTUMIA KIBIASHARA?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali hiyo, Wema alijiongeza na kuanza kukubaliana na makelele mengi kuwa jamaa huyo anamtumia kibiashara huku yeye akilamba shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya Bongo.

UBAHILI WAMPONZA DIAMOND
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.

“Wewe unamuonaje Wema? Yule mtoto bei mbaya bwana. Matunzo yake si mchezo. Sasa Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia Madam kwenye bomba,” kilisema chanzo hicho.

BMW LATAJWA
Chanzo hicho kilitiririka: “Unalikumbuka lile BMW (gari) alilodaiwa Wema kapewa na Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua Diamond alikuwa Marekani, sasa aliporudi akataka kujua BMW imetoka wapi maana yeye alitoa Murano, hapo ndipo moto ukawaka na wakawa hawaivani tena.”

BETHIDEI  YA DIAMOND
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku ya bethidei ya Diamond ambapo jamaa huyo alizawadiwa BMW X6 na uongozi wake wa Wasafi, Wema alikwenda kwenye shughuli tu ili kuonekana kwenye kamera.

Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye shughuli hiyo Diamond ndiye aliyekuwa akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu tofauti na Wema aliyekuwa anafuata tu maelekezo ‘kishingo upande’ kwani ndani yake hakuna mapenzi tena.

UKIMYA WAPITA
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile kulipita ukimya fulani huku kila mmoja akiishi kwake tofauti na awali ambapo Diamond alikuwa akijinasibu kuwa huwa analala nyumbani kwa baby (Wema), Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.

DRAMA KWENYE BETHIDEI  YA AUNTY EZEKIEL
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni shosti wa Wema, Aunty Ezekiel, Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini kwenye Mgahawa wa Rodizio uliopo Masaki jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa safarini.

Wakati shughuli ikiendelea, Diamond alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake lakini ghafla alipoibuka Wema upepo ukabadilika.

Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini hata kabla ya kwenda nyumbani, alimpita Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha akaanza kuzunguka kwenye meza kusalimiana na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika upande aliokuwa ameketi Diamond na timu yake, aliwaruka na kwenda moja kwa moja kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.


MINONG’ONO KILA KONA
Ishu hiyo iliibua minong’ono kila kona ya ukumbi huo na kuthibitisha zile tetesi kwamba hawapo kwenye uhusiano mzuri.Wakati Wema akifanya yake na Aunty, Diamond alipishana naye kama hawajuani na kukimbilia kwenye gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua.

‘HUYU DEMU SIYO’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini Diamond na ‘kruu’ yake waliacha sherehe wakitaka kutimua, mmoja wa memba wa timu yake ya Wasafi alisikika akisema ‘huyu demu siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’.

WEMA VIPI?
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake ukumbini na kumfanya Diamond achomoke bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya kina na kusema hakujua nini kilimkimbiza ila yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya Aunt na si kingine.

DIAMOND ANASEMA?
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya kutoka nduki baada ya Wema kuingia ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu amwache kwa maana kwamba ampotezee na kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia hilo hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya kiganjani haikupokelewa muda wote alipopigiwa.

TUMETOKA MBALI
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. 
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kisha kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ huku cha Wema kikiwa kwa yule kigogo wake, Clement.

Baby Madaha Atilia Shaka Afya ya Mkongo wa Jack Wolper

$
0
0
Msanii wa filamu na muziki, Baby Joseph Madaha amesema ana wasiwasi na afya ya mwanaume Mkongo anayefahamika kwa jina la Mwani aliyewahi kuwa mpenzi wa Jacqueline Wolper.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Baby Madaha alisema, hofu yake hiyo inatokana na namna mwanaume huyo anavyotapanya pesa huku akitangaza dau kubwa ili kuwapata mastaa wa kike.

“Kimsingi mimi nina wasiwasi na afya yake, asije akawa anataka kutumaliza. Mimi simhitaji hata kama ana mamilioni yake. Hofu yangu ni hii tabia yake ya kutaka kutupitia sisi mastaa, wanaokubali kuwa naye eti kisa ana mkwanja nawaonea huruma,” alisema Baby Madaha
GPL

Wanawake na Ushamba wa Kubofya Simu, Mnatia Aibu

$
0
0
Siku hizi sijui ndio swagger au vipi unakuta kila msichana yupo bize na kubofya simu.

Huu mimi naona ni ushamba wa hali ya juu, yani wewe unadhani ukiwa bize na simu ndio usista duu au?sana sana unaonyesha jinsi ulivyo mpweke na haujiamini kinga yako ni simu.

Ebu fikiria unamkuta demu unamsalimia halafu kenyewe kanajifanya ka-cute kanakutazamaa huku kanabofya then kanashtuka eti ah unanisalimia? nitakukata ngumi mbili ufe.

Hivi nani aliwadanganya ukiwa bize na insta au wosapu ndio utaonekana classic washamba nyie?

Ndio maana siku hizi mnakuwa na makengeza kwa sababu ya ushamba wa kuchungulia jicho moja kwenye screen ya simu jicho lingine ndio linaaangalia mambo mengine chunguza vimacho vyao masista duu vimepinda karibia wote.

Acheni huu ushamba wengine tuna mikono mwepesi hatukawii kunasa makofi mtu.

Halima Mdee Amsambaratisha Magufuli

$
0
0
Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee jana alitikisa Jimboni Chato kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara kuwahi kuhutubiwa jimboni hapo miaka ya karibuni.

Awali Mdee alilakiwa na umati mkubwa wa watu wakiwa na msururu mrefu wa magari,pikipiki,baiskeli huku akina mama wakiwa kandokando ya barabara wakipunga matawi ya miti.

Ujumbe mkubwa wa Halima Mdee kwa wanaChato ni kuikataa Katiba Haramu ya CCM na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Halima Mdee maarufu kama Tanzanian Iron Lady alipokea kadi 200 za watu walioamua kujitoa CCM na kujiunga Chadema.Huku mamia ya wananchi wengine ambao hawakuwa na chama wakijiunga pia Chadema.

Ikumbukwe jimbo la Chato linaongozwa na mbunge wa CCM John Pombe Magufuli ambaye ni waziri wa Ujenzi.

Ni simulizi hapa Chato kuanzia jana mpaka asubuhi hii kumzungumzia Halima Mdee na Chadema!

UKAWA Umewafanya Watu Wengi Wasijue Mengi Yaliyomo Kwenye Rasimu

$
0
0
Warioba wakati anawasilisha Taarifa ya Tume Bungeni ali-base sana kwenye Muundo wa Muungano kuliko vitu vingine! Hata takwimu, hatukusikia kuhusu Haki za Binadamu wangapi walisema nini, ila tu kwenye Muungano ndio tulipewa takwimu na Warioba! Ni Warioba ndiye aliyefanya mchakato wa Katiba mpya uonekane kuwa ulilenga tu kubadili Muundo wa Muungano! Kwa bahati mbaya walijitoleza watu waliodaka mrengo wa Warioba na kuufanya ndio main agenda, si wengine bali ni wale waliojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA}! Kiuhalisia huu Umoja ni kwa ajili ya kutetea Muundo wa Serikali 3 tu basi na sio Umoja wa Kutetea Katiba as a whole.

UKAWA mara nyingi wamekuwa wakisisitiza muundo wa Serikali tu bila kuelezea mengine! Wanapodai kuwa maoni ya "Wananchi Walio Wengi" yametupwa mara nyingi yanalenga juu ya Serikali 3, mengine ni ya ziada tu! Na hii imekuwa ni main topic na kwa bahati mbaya vyombo vya habari vingi vimekuwa taken away na msimamo huo.

Matokeo yake ni kwamba mambo mengine mengi yaliyomo kwenye Rasimu watu hawatayajua na tunaweza ikifika Aprili, 2015 tukajikuta tunapiga kura juu ya Muundo wa Muungano, only that.

Ni wakati sasa wa kubadili mtazamo wa kiu-UKAWA na kuangalia kila kitu kilichomo kwenye Rasimu na kufanya maamuzi sahihi! Tuachane na wenye maslahi binafsi juu ya Muundo wa Muungano.
Tujadili zaidi.

Wabunge Tisa Wajiuzulu Kumpinga Shy-Rose

$
0
0
Mgogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (Eala) umechukua sura mpya baada ya wabunge tisa, wakiwamo makamishna watano na wenyeviti wanne wa kamati za Bunge hilo, kuwasilisha barua za kujiuzulu nafasi zao hizo, ikiwa ni matokeo ya sakata linalomhusisha mbunge mwenzao kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji (pichani).

Kutokana na hali hiyo, Bunge hilo ambalo lilikutana kwa wiki mbili huko Kigali, Rwanda liliahirishwa jana kwa muda usiojulikana, muda mfupi baada ya kushindwa kufanya uamuzi wa kumwadhibu Bhanji ambaye anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu.

Mgogoro huo ulisababisha Eala kwa wiki mbili, kushindwa kufanya lolote lililokuwa limepangwa kwenye kalenda yake, kwani kila lilipokutana, wabunge walitoa hoja liahirishwe hadi pale suala la nidhamu dhidi ya Bhanji litakapotolewa uamuzi.

Mbunge huyo anatuhumiwa kutoa maneno yasiyokuwa na staha kwa wenzake, kuwakashifu na kuwatukana baadhi ya viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa ziara ya ujumbe wa Eala katika nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), Ubelgiji.

Zijue sababu za Benjamin Mkapa kumuunga mkono Lowassa

$
0
0
Ikiwa Dunia imesimama kwa mshutuko wa kumpoteza kiongozi shupavu Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Satta kilichotokea London mapema wiki hii, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekaririwa na kituo cha lunginga CITIZEN nchini Kenya kwa njia ya simu akihojiwa maswali mbali mbali baada ya kifo cha Satta, Katika mahojiano yake siku sita OKELLO kupata tafakuri ya Zaidi ya masaa 30 hadi sasa na kudhubutu kusema Lowassa ameungwa Mkono na Mkapa kwa maslahi ya Taifa , chama na Serikali. Zijue sababu za Mkapa kumuunga mkono Lowassa katika Tafsiri ya mahojiano yake na kituo tajwa.

1. EDWARD LOWASSA ANAUZIKA KWA WANANCHI

Rais Mkapa aliangazia wasifu wa Lowassa bila shaka na kukiri ndie anaeuzika akiangalia utendaji na uchapakazi wa Lowassa na ndioa maana alinukuliwa aisema,"Chama kama chama lazima muwe na mtu anayeuzika na kukubalika katika jamii kwa utendaji wake, haiba yake, wasifu wake (ndani ya Chama na Serikali) lakini vile vile ushawishi wake.." ambae bila shaka ni Lowassa.

2. VIJANA WAJITOKEZE ILA NI WAKATI WA LOWASSA.
Hapa Mheshimiwa rais Mstaafu alionyesha kuwa chama kina kuza demokrasia pia na hivyo hazina ya vijana haipaswi kupuuzwa ila huu ni wa kati wa Lowassa na ndio maana hakusita kumtaja Lowassa pale alipo jitokeza 1995 na sasa ni wakati wake. Hivyo alisema "...Haya mambo ya umri na kadhalika sisi hatukutazama wakati huo ila si dhambi vijana KUJITOKEZA manake hata wakati wangu Rais wa sasa Mhe. Kikwete na kina Lowassa walijitokeza na LEO unaona Kikwete ndiye Rais" akimaanisha vijana wajitokeze ila Lowassa ndie Rais AJAYE.

3. AKIRI LOWASSA HAKUNA WA KUMZUIA NDANI YA CHAMA

"...nikuhakikishie hata kama mimi Benjamin Mkapa siko na Kikwete mwisho wa siku wanachama ndio watakaosema wewe hutaki ila sisi tuachie huyo huyo...Na hayo yalijitokeza mwaka 2005 watu walimtaka Mhe Kikwete sasa mimi kuwa Mwenyekiti wa Chama hakunipi Mandate ya kushindana na walio wengi na mliona alishinda kwa asilimia kubwa kweli kweli.." HIVYO ni wazi hata Rais Jakaya hayuko kwa ajili ya kumzuia Lowassa bali kutimiza Demokrasia.

4. AONYA MAKUNDI YA URAIS NDANI YA CHAMA YANAYOMCHAFUA BILA SABABU

Mheshimiwa Mkapa alirejea kauli ya Edward Lowassa February 7 ,2008 alipoonya wanasiasa kupakaziana siasa chafu hivyo nae alionya kwa kusema "Hivyo CCM Ina taratibu zake na wanajua nani anafaa manake siasa hizi...tuhuma zingine za kipuuzi kweli kweli...sasa mkiendekeza tuhuma mwishowe mnakuta mnabaki bila chama na kwenye siasa mkianza kushutumiana hakuna wa kusimama"

5. LOWASSA NI TUMAINI LA WENGI NA CHAGUO LA WENGI

Amekishauri chama kuwa Lowassa ni tumaini la wengi hivyo cha kama chama wao watawekeza kwake na ndipo alipo yanena haya "Hakuna chama duniani ambacho kinaona kabisa fulani atatusaidia halafu kimwache -hakuna. Manake huko ni kukiua Chama...Naamini ndivyo ilivyo hata mpaka sasa tafiti zimefanyika na naamini wamesikia watu wakisema wanamtaka nani…wakati wangu mimi mgombea alikuwa amesha tungiwa nyimbo na watu mbali mbali wenye mapenzi nae. Hivyo labda hata sasa yawezekana kuwa hivyo…washwahili walisema nyota njema huonekana asubuhi"

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA ,….SAFARI YA MATUMAINI KUELEKEA 2015.

Unaambiwa Davido Alivuta Dolla 40,000 Fiesta...'Loading..'

$
0
0
Kwa mujibu wa MwanaFa akiwa kwenye kipindi Choice fm ni kuwa Davido alilipwa Dolla 40,000 kupiga show Fiesta.

Fa alihoji kwa nini waandaaji wasiwalipe dolla 10,000 wasanii wanne wa Bongo wapige show kali kuliko kuzipoteza kwa show mbovu ya Davido?

Je wadau wa Fiesta ni kweli kuwa show ya Davido haikuwa na thamani hiyo au ni kujikweza tu kwa Fa na wenzake?

Mtangazi Gadner G. Habash Aikimbia Times FM ..Aajiriwa Na Redio Mpya Dar

$
0
0
Mtangazaji  mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga  na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7  cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho kipya.

“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema Kanky.

Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fm na baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole.
Asante,

Meneja Uhusiano.

Kanky Mwaigomole.

Lowassa Aliangukia Kanisa Katoliki: Asema Maneno ya Sitta Bungeni Yapuuzwe

$
0
0
Wakati Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (MBK) ikitarajia kuingia katika hatua ya kura ya maoni mwakani, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ameibuka na kuliomba radhi Kanisa Katoliki kufuatia mgongano iliyojitokeza kati ya kanisa hilo na baadhi ya viongozi serikali na wa Bunge hilo.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, aliomba msamaha huo wakati akitoa salamu zake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge, mkoani Morogoro.

Alisema Kanisa Katoliki lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na mshikamano nchini, hivyo mambo yaliyojitokeza yanapaswa kusamehewa.

“Najua hivi karibuni tumewaudhi, lakini mimi naomba mtusamehe bure tu, kama vile mzazi anavyomsamehe mtoto wake anapokosea,” alisema Lowassa na kuongeza kuwa Kanisa Katoliki ni muhimu katika maendeleo ya nchi.

Ingawa Lowassa hakueleza kwa undani tofauti zilizojitokeza kati ya Kanisa hilo na baadhi ya viongozi wa serikali, lakini wakati BMK likiendelea, taasisi za dini zilisambaza waraka uliosainiwa na viongozi wake ukilikosoa Bunge hilo kwa mambo mbalimbali ikiwamo kuendelea kujadili rasimu bila maridhiano kutokana na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia.

Kadhalika, viongozi wa madhahebu hayo ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT) na Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walilikosoa BMK kwa kupuuza maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Waraka huo ulisababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kujiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi na wa hovyo hovyo.

Sitta ambaye alitoa kauli hiyo Oktoba Mosi mwaka huu, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa waraka wa maaskofu una lugha ya Ukawa, ingawa maaskofu kwa upande wao waliueleza kuwa ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.

Baada ya Uvumi wa Kuwa na Ujauzito wa Diamond,Meninah Kayazungumza Haya

$
0
0
Meninah ambaye ni zao kutoka Bongo Star Search miezi michache iliyopita ameripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond Platnumz huku mwenyewe akikana mara kadhaa kila anapopata nafasi ya kulizungumza hili.
Kupitia kisehemu cha You heard kwenye kipindi cha XXL Soudy Brown amekuja na stori inayohusu hali inayosemekana anayo kwa sasa Meninah kwa kile kinachosemwa ana ujauzito wa Diamond Platnumz.

Meninah ameanza kwa kusema>>’Hapana sina ujauzito,siko na Diamond pia sina mimba sina ujauzito kwani hizo habari unazitoa wapi?mimi sina mimba wala ujauzito,siko nae na sifatilii haya mambo’
Alipoulizwa na Soudy Brown kuhusu kutajwa na Diamond kama wife material Meninah amesema ‘Hapana hakuna kitu kama hicho naweza kuwa wife lakini sijawa tayari kuwa wife material.
Bonyeza play kumsikiliza Meninah akiongea na Soudy Brown.
SIKILIZA HAPA.   

Wema Sepetu: Kissing on the lips kwa girls to girls is very very okay, I kiss my mama, I kiss my sister kwenye lips

$
0
0
Baada ya picha inayomuonesha Wema Sepetu akibusiana na Aunt Ezekiel kwenye Lips kuleta hisia tofauti kutokana na kitendo hicho kutozoeleka kufanywa na watu wa jinsia moja, Wema amesema “Yes I kissed her”, na kusema kuwa hufanya hivyo hata kwa watu wengine wa jinsia yake ambao yuko nao karibu.

It is not only her, I Kiss my daughter, I kiss my sister, I kiss just people who are close to me”.Amesema kupitia Power Jams ya EA Radio.

Mpenzi huyo wa Diamond ameendelea kujitetea kwa kitendo hicho kwa kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa wasichana waliokaribu kubusiana kwenye lips na kuongeza kuwa hubusiana hata na mama yake na dada yake kwenye lips.

Kissing on the lips kwa girls to girls is very very okay, it is not okay kwa men to girls or men to men, kwa girls to girls kama you guys are like really close and you are attached, because I kiss my mama, I Kiss my sister kwenye lips“.

Binti Amefariki Akiwa Bangkok Wakati Akifanyiwa Upasuaji wa Kutengeneza Makalio

$
0
0
Binti wa Kinigeria (23) amefariki akiwa Bangkok wakati akifanyiwa upasuaji wa kutengeneza makalio ktk upasuaji uliomgharimu takribani Sh. Milioni 5.
- Alifanyiwa upasuaji na kurudi nyumbani Nigeria alikoanza kuugua tokana na Kuoza kwa ile sehemu aliyofanyiwa upasuaji kuongeza makalio, kisha akarudi kutibiwa upya huko Bankok lakini kwa bahati mbaya alivyokuwa anatibiwa upya akafariki....

A 23 year old Nigerian girl Joy Willaims died in Bangkok on Oct 23 during a buttock augmentation surgery. Joy flew to Bangkok on Oct 14, to visit the SP clinic for £2,000 buttock augmentation surgery. 

A few days later her wounds became infected and she returned to have corrective surgery to remove the silicon implants. She died in the operating table during the corrective surgery. 

The deceased brother Anietie who spoke to Dailymail from his home in Lagos says the family were not aware Joy travelled to Bangkok: 

“We don't really know what went wrong, we only know what is in reports in the media. She was a very nice and caring person.She brought joy to people's lives.She was a beautiful girl, loved by everybody. We will miss her so much.'
He added that the family is still making preparations to bring Miss Williams's body home and that his brother was planning to fly to Thailand and return to London with it.

The doctor who carried out the procedure, Sompob Sansiri, has been arrested. Thai officials are still investigating the cause of her death.

Miss Williams, who was born in Lagos, settled in Thamesmead with her mother Christie in 2007 and had been to Thailand twice before choosing to visit for surgery. 


May her soul rest in perfect peace. 

RASMI: Sitti Mtemvu sasa kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014

$
0
0
WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu, taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.

FikraPevu imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.

Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
FikraPevu imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18.

Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.

Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, ameiambia FikraPevu leo Alhamisi Oktoba 31, 2014 kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa.

Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa...

Wema: Kipindi Cha in My Shoes on Air Next Week, Diamond Atakuwepo.

$
0
0
Kipindi cha maisha na hustle za Wema Sepetu 'In
My Shoes' msimu wa pili kinaanza tena wiki ijayo
na kwenye interview niliyofanya naye Wema
amesema haya mapya
1] Maboresho mengi zaidi, mwanzo ulikuwa
mgumu sana, sasa nitaonyesha kila kitu kwa
upana zaidi.
2] Safari zake za njee zitaonekana.
3] Anavyotengeneza pesa na dili anazofanya
vitaonekana
4] Mpenzi wake Diamond ataonekana kwenye
show "Episode ya kwanza atakuwepo na
zinazokuja".
Show ya Wema ambaye ni Miss Tz 2006
itarushwa Ijumaa saa tatu na nusu usiku kabla ya
Friday Nite Live

Mbinu Mpya za Wanawake wa Siku Hizi Wanao Saka Ndoa Kwa Nguvu

$
0
0
Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja
anaifua
anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi
anaondoka...
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa
usiku,asubuhi
anaianika nyuma ya mlango anaondoka...
Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza
anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni
zangu
mezani'
Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya
kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels
anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka
na
flat shoes kwenda chuo..
Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na
vitu
kadha wa kadha,na ole wako uvihamishe
alipoacha,kesi zinaanza...Hao ndo Wanawake
wa
kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi
mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia
taratibu..
Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa
ina
perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa
hereni
na 'Foundation'... My Brother,huna haja ya
kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....Kifuatacho
utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamani
nilijua
ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed
Calls,Siku
hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu jua
imekula kwako,inawindwa ndoa...

Baada ya Kutoka Jela Chid Benz Azumgumza Kuhusu Sakata la Kumpiga Ray C

$
0
0
Rapper Chidi Benz ambae alishikiliwa na Polisi mwezi huu baada ya kukutwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akisafiri kwenda Mbeya, ameachiwa kwa dhamana na sasa yuko mtaani.
Mtangazaji wa So so Fresh ya Clouds FM Dj Fetty Ijumaa ya October 31 2014 alirusha Exclusive interview na Chidi Benz ambae  moja ya vitu alivyozungumza ni ishu ya kumpiga mwimbaji Rehema Chalamila a.k.a Ray C

Soudy Brown ambae ni producer wa show hiyo alianza kwa kumuuliza Chidi…… ‘Ray C anasema ametupa kesi aliyokuwa amekufungulia’ Chidi akajibu >>> ‘Thanks kama ametupa hiyo kesi lakini sidhani kama kesi ilikua bado ipo kwa sababu mara ya mwisho nilimwambia points kadhaa ambazo zilikua ni za msingi, nilimtumia msg kwenye simu yake…. pls tuachane na huu ujinga, sanasana watu watakua wanatuona wale Wateja labda wamezinguana‘
‘Unasema nini Ray C wakati mimi ni mtu nimekuandikia miziki, nimerekodi na wewe…. mtu ulikua unaniambia unanipenda unasema Chidi jamani naomba nishoot video na wewe najua siwezi kukulipa, wewe kaka yangu kabila moja…. mtu nimekusaidia tumefanya vitu vingi, inawezekana vipi nije kukubadilikia na kuwa adui yako? ni kitu wewe umefanya unachokijua wewe lakini dunia haijui, watu hawajui mambo yetu…. hiyo ni mambo binafsi'
‘Hizo ni ishu zetu, kama unasema mimi ni kaka yako si mimi umeniudhi kaka yako kinyumbani….. so wewe umekuja kuchukua ukaleta kwenye media ukasema nimekupiga lakini mimi najua ulichokifanya na nilikukanya kwa mara ya kwanza ukaomba msamaha alafu mara ya pili ukafanya tena, nikakufata kwako kweli…… ‘
‘Mi najua Ray C yuko kwenye kuacha madawa anakunywa zile Methodone, najua madawa sio kitu kizuri…. mimi pia nilitumia kwa hiyo huwezi kuwa sawa kwa harakaharaka, unakua unapona taratibutaratibu, so najua alipitiwa tu….. point nyingine nilimwambia sidhani kama mimi ndio mtu mbaya sana kwako Ray C’
‘Nilimwambia kama ni kunikamata na kunipeleka jela nahisi kuna watu Ray C inatakiwa uwakamate na uwafunge jela hao ndio wamekuharibia sehemu kubwa ya maisha yako, hakuna kibaya nilichokufanyia mimi’ – Chidi Benz


MSIKILIZE HAPA:

Source:Millard Ayo

Mambo Manne Aliyoyasema Chidi Benz, Jinsi Alivyokamatwa Airport na Dawa za Kulevya

$
0
0
Imekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.
Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.

Kuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay>>> ‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake… tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji, tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’

Kuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema>>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’

‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.

MSIKILIZE HAPA: ~Millard ayo
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images