Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live

Rita:Madudu ya kina Sitti Mkiendelea Kuyafumbia Macho Tutegemee Aibu Zaidi

$
0
0
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), bila shaka mko vizuri mnaendelea kusimamia jukumu zito katika taifa letu.Usajili, Ufilisi na Udhamini siyo kazi ndogo. Ni kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu maana matokeo ya ufanisi wenu ndiyo majibu ya shughuli nyingi katika nchi.

Watu wakitaka kusafiri, kutambulika katika maeneo mbalimbali nyinyi lazima mhusike kutatua.
Mkitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea na majukumu yangu kama kawaida.  Nimewakumbuka leo kupitia barua hii ili niweze kuwafikishia yaliyoko katika akili yangu ndogo.

Madhumuni ya barua hii kwanza kabisa ni kutaka kuwauliza, hivi mmewahi kuwaza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa watu kufanya madudu ya kufoji vyeti kama anavyodaiwa kufanya mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu?Kwa kuanzia eneo hilo, ni vyema basi chombo chenu kikafanya tathmini upya katika kuhakiki taarifa mbalimbali na kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti mtu kufanya udanganyifu wa aina yoyote.

Msisubiri hadi yatokee ya kutokea ndiyo muanze kuchukua hatua.
Kupitia suala la Sitti ni dhahiri inaonesha kuna walakini kwenye ofisi yenu. Haiwezekani nyaraka nyingine za mtu huyohuyo mmoja zioneshe kwamba amezaliwa mwaka 1989 huku mwenyewe akidai kuwa amezaliwa mwaka 1991.

Kinachonisikitisha zaidi mhusika anadai eti cheti chake cha kuzaliwa kilipotea na akadai kuwa mmempatia kingine kipya Septemba 9, mwaka huu.Alipoulizwa kwamba alitoa taarifa katika kituo gani cha polisi juu ya upotevu wa cheti chake hakuwa na jibu la kueleweka, mlimpaje?

Wakati umri wa mrembo huyo ukiendelea kuwa gumzo kwa takriban mwezi mzima, RITA mliendelea kuziba mdomo katika kung’amua umri halisi wa binti huyo licha ya wadau mbalimbali kuhoji juu ya hilo. Mtendaji Mkuu wa RITA, Jumamosi iliyopita alikaririwa katika chombo cha habari akisema bado wanaendelea kumchunguza miss huyo. Hadi lini?

Labda sina uzoefu juu ya mambo ya uchunguzi lakini kweli mfumo mlionao si rafiki kiasi cha suala hilo kuchunguzwa kwa zaidi ya wiki tatu? Nafikiri kuna haja ya kwenda mbele zaidi ya hapo. Dunia ya leo kila kitu kinakwenda katika mfumo ‘data base’ kwenye kompyuta.

Kwa nchi za wenzetu ni rahisi tu mtu kupata taarifa zake, tena hakuna kificho ndiyo maana utata wa Sitti ulipokuwa ukiendelea, watu ‘wali-google’ tu na kupata taarifa zote za Sitti kule Texas, Marekani na kila kitu kikawekwa hadharani. Kuanzia leseni ya udereva hadi hati ya kusafiria.

Ni wakati sasa umefika tubadilike, tutengeneze mfumo wa kuweka wazi data. Isichukue muda mrefu kubaini taarifa za mtu hususan katika suala la utaifa kama la Miss Tanzania ambaye anatakiwa akaiwakilishe nchi katika mashindano ya urembo ya dunia.
Wasalaam,
Erick Evarist.

Wema Sepetu Afunguka 'Walio na Mipango ya Kuzaa Hongereni... Mimi Sina ... Im Done"

$
0
0
Katika page yake ya instagram, super star wema sepetu aka mama ubaya amewataka wote wanaompigia kelele kuhusu kuzaa mtoto wamkome, kwani hana mpango huo kwa sasa. Hiki ndicho alicho kipost:

Okay... Lets get things straight here.... See dat doggie up there... Y'all see her....? Dat is my bebi.... since i dont have a bebi... Huyo ndo mtoto wng... Basi sasa nitapopost afu nisikie kuzaa nakublock fasta... Mshaniona sizai basi ndo mjue sizai... Akha...!! Zaa zaa... If u have a child im happy for u... Nd wish u da best... I dont... Ndo mungu alivyonipangia... So please hey.... Watakaozaa all da best... Walio na mipango ya kuzaa hongereni... Mimi sina ... Im done... Vanilla ndo bebi wangu kipenzi na nampenda kuliko.... Na wale wa subhannah llah pia nisiwaone... This is getting too personal sasa...

Chid Benz Atoa Wimbo Mpya Usikilize Hapa, Kawachana Wote Wanaomsema Vibaya

$
0
0
Huu ni wimbo mpya wa Chid Benz kautoa leo ikiwa ni siku chache tu toka atoke lupango ambapo alikua kashikiriwa kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya uwanja wa ndege wakati akitaka kusafiri. Wimbo huu umewalenga watu wote wanaomhukumu kwamba alikua au anatumia madawa ya kulevya.

Unaweza kuusikiliza wimbo huu hapa chini:

Idris ageuka kipenzi cha Afrika, wengi watabiri anaweza kushinda!

$
0
0
Wazungu wanasema ni vizuri kutumaini mema na kujiandaa kwa mabaya. Kama mambo yataenda vile ambavyo yanaenda sasa, huenda Idris akarudi na $300,000 za Big Brother Africa.

Mpiga picha huyo amegeuka kuwa si tu kipenzi cha wasichana, bali cha mashabiki wengi wa shindano hilo. Kikubwa anachopendewa ni ule uwezo wa kuweza kuwa rafiki wa kila housemate.

Wakati shindano likiendelea, jina la Idris limekuwa likiongoza kwa kutrend zaidi kwenye Twitter kuliko washiriki wenzake. Hizi ni baadhi ya tweets za hivi karibuni zinazomhusu:

Top six I for-see for now: Idris, Tayo, Sheila, Sammy, Macky2 and Trezegah

I’m saying it again!! Idris is gonna take this thing

If Idris continues with this altitude, he will win without breaking a sweat

Idris looking all hot and sexy…and the way he bites his lower lip tho

Idris is a hotshot his got both talent and a swag

Idris looking on point!!!! You know he gotta dress the part his hoh

Mastaa wa Kike Wafunguka Kuhusu Viungo Nyeti vya Bandia

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
MASTAA wa kike wa fani mbalimbali nchini, wamezungumzia matumizi ya nyeti bandia, baadhi wakizipongeza kuwa zinawasaidia kuondokana na ‘stress’ za wanaume huku wengine wakiziponda kuwa hazina ‘ladha’.

Baadhi ya wasanii hao walisema kuwa ingawa wanazifahamu na hata kuwajua wanaotumia wao wanaamini wanaotumia ni wale ambao hupenda kufanya tendo kila siku wakiwa na wenza wao, hivyo wanaposafiri au kusigana kidogo, ndipo wanapolazimika kuzitumia.

Mastaa waliozungumza na gazeti hili kuhusu nyeti hizo, lakini wakikana kuwahi kutumia ni pamoja na Lulu Semagongo, Isabela Mpanda, Baby Madaha, Tamrina Poshi ‘Amanda’ na Vai wa Ukweli ambaye alisema yeye anapojisikia karaha ya mapenzi, hupenda kunywa pombe, hata kama ni asubuhi.

Mlemavu wa Macho Aelezea Jinsi Alivyochukua Kichapo Kwenye Vurugu za Mdahalo wa Katiba

$
0
0
Amoni aliekuwa mbunge wa bunge maalumu la katiba ambae ni mlemavu wa macho ametoa taarifa kwa vyombo vya habari na kuandika kwenye ukurasa wake wa wakijamii kuwa amepigwa na kupasuka na vijana wa ukawa na wakati wanampiga walikuwa wakimwambia kuwa “koma na acha kuitetea CCM’‘ kwa kweli nasikitika sana,mimi sioni,lakini nilikuwa na pigwa na mikono na kurushiwa kiti hadi pale ndugu yangu Makonda aliponiona nakuamua kuja kunisaidia,sina lakusema ila najua MUNGU ANAWAONA NA ANAWAJUA NA YEYE ATA WAPIGA HAPA HAPA DUNIANI KAMA WALIVYONIPIGA MIMI NAKUNIPASUA KICHWANI AMBAE SIJAWAHI KUWAPIGA,”

Aina ya Simu Kumi Zinazoongoza Kwa Ubora Duniani Kwa Sasa Hizi Hapa

$
0
0
10 best mobile phones in the world today

10.Google Nexus 5

09. Samsung Galaxy s5

08.Sony Xperia Z3

07.Nokia Lumia 1520

06.Sony Xperia Z3 Compact

05.Iphone 6 plus

04.Samsung Galaxy Note 4

03.LG G3

02.IpHONE 6

01.HTC one M8

Kigogo wa Madawa ya Kulevya wa Kike, Akamatwa na Madawa ya Kulevya

$
0
0
Hawa wadada wa mjini kujifanya wanauza nguo na simu kumbe uongo tu mwingine akamatwa....

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’ mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.

Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.

Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.

“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.

Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.

“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.

Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.

Kiongozi Mwingine wa Dini ya Kiislam Auawa Nchi Kenya kwa Risasi

$
0
0
Watu wasiojulikani kwenye mji wa pwani nchini Kenya ,Mombasa wamemuua kwa kumpiga risasi kiongozi mashuhuri na mwenye msimamo wa wastani wa dini ya kislamu.
Sheikh Salim Bakari Mwarangi ambaye ni mwanaharakati wa kampeni dhidi ya itikadi kali alipigwa risasi wakati alipokuwa akirudi nyumbani kutoka msikitini jumanne usiku.
Viongozi sita wa dini ya kiislamu badhi yao wenye itikadi kali na wale walio na misimamo ya wastani wameuawa mjini Mombasa tangu mwaka 2012.
Eneo la pwani ya kenya lenye waislamu wengi limekumbwa na misururu ya mashambuli ya mabomu yanoyoaminika kutekelezwa na watu walio na uhusiano na kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia.

Kama Ulimmiss Rehema Chalamila aka Ray C, Hii inaweza Kuwa Habari Njema Kwako.

$
0
0
“Ray C The Singer is Back,” ameandika muimbaji huyo kwenye Instagram. “Napenda kuwajulisha mashabiki kuwa kuanzia sasa muda wowote,saa yoyote,dakika yoyote,siku yoyote kuanzia sasa Single yangu mpya MshumMshum/Walimwengu itaanza kusikika kwenye simu zenu plus kwa wale wapenzi wa mitandao Kama Mimi ya Facebook,Twitter,Instagram,Google,YouTube,blogs na websites mbalimbali mtaweza…..Kwa mashabiki wangu wa ndani na nje ya nchi mlichokuwa mkisubiri tayari kishamalizwa!!!!Kazi kwenu………Stay Tuned for more info……Love u guys…mmmmwaaaaah!i miss my beautiful voice too……I jst can’t wait to sing live for u guys!

Follow Udaku Specially Blog on Instagram Kupata Udaku wa Chini ya Kapeti

$
0
0
Usipitwe na Stori Kubwa za Kimjini Mjini na Udaku wa Chini ya Kapeti , Tufuate INSTAGRAM Kwa Kubonyeza Link Ifuatayo na Ikifunguka Bonyeza Kitufye cha Follow chini ya Profile Picha:
>>>>> @Udakuspecially

Taarifa ya TCRA kwa wamiliki wa blogu Tanzania

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY


ISO 9001:2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA INAPENDA KUWATANGAZIA WAMILIKI WOTE WA MITANDAO YA KIJAMII “BLOGERS” KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO TAREHE 11.11.2014 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM.

MKUTANO HUO UTAJADILI MATUMIZI YA BLOGS KIPINDI CHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WABUNGE NA RAIS KAMA ILIVYOAINISWA KWENYE RASIMU YA MWONGOZO WA MAUDHUI KWA AJILI YA KAMPENI ZA UCHAGUZI MWAKA 2015.

TAFADHALI MNAOMBWA KUFIKA BILA KUKOSA.

Imetolewana
MkurugenziMkuu
MamlakayaMawasiliano Tanzania
S.L.P. 474
DAR ES SALAAM

Rais Uhuru Kenyata wa Kenya awa Raisi wa Kwanza Kupanda Daladala Kutoka Ofisini Kwenda Mjini

$
0
0

Rais uhuru Kenyata ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa nchini Kenya kutokana na matukio mengi anayoyafanya, mengi yakiwa yale ambay ni mara chache sana kumuona rais akifanya. Mfano ni kama lile tukio la kutoka ikulu akiwa hana bila ya walinzi, kucheza mziki katika matamasha mbalimbali na lile la kusimamisha msafara wake kisa tu anunue karanga.

Jipya alilolifanya siku ya jana ni pale alipoamua kutumia usafiri wa Matatu au kwetu tunaita Daladala kwenda mjini. Inasemekana Rais Kenyata ndio rais wa kwanza ktumia usafiri huo akiwa madarakani, marais wote waliopita hawajawahi kuutumia wakiwa madarakani. Kikubwa kingine alichosema na kimeungwa mkono na vijana wengi ni kuruhusu Daladala kuchorwa Graffit jambo ambalo limekua likizuiliwa na uongozi nchini humo kwa mda sasa. Rais Kenyata alisema ” To be frank why are we interfering with graffiti on Matatu? Let us promote our young people – Uhuru Kenyatta ”


Paul Makonda: Vurugu za Mdahalo zilizima Ndoto Zangu

$
0
0
 Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda amesema alitamani kuzungumza siku ya mdahalo ulioandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere Foundation lakini vurugu zikazima ndoto yake.

Makonda ambaye anatuhumiwa kuwa ndiye aliyepanga vurugu hizo zilizosababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba kushambuliwa, alikana na kudai kuwa hata yeye alitamani kukisikia kile kilichopangwa kuzungumzwa na wasemaji wakuu wa mdahalo huo ili ajibu hoja zao katika mkutano huo.

Akizungumza jana katika ofisi za gazeti hili, Makonda alisema aliingia ukumbini akiwa na nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa madai kuwa ingeweza kumsaidia kuainisha yale ambayo yangejadiliwa na ikibidi achangie hoja kwa kutetea au kutoa ufafanuzi wa kile kilichoandikwa ndani ya Katiba hiyo.

“Nasikitika kwa sababu malengo yangu hayakutimia kutokana na vurugu zile. Lengo langu lilikuwa; nipate nafasi ya kuzungumza ili nitoe hoja zangu na kufafanua uzuri wa Katiba Inayopendekezwa,” alisema.

Hata hivyo, alisema yaliyosemwa na Jaji Warioba kabla ya mdahalo kuvunjika, yalimpa fursa ya kujua ni vifungu vipi vina kasoro na vipi viko sahihi.

“Kwa maelezo ya Jaji Warioba, asilimia 90 ya maoni yaliyokuwamo katika Rasimu waliyoipendekeza ndiyo yaliyomo katika Katiba hii Inayopendekezwa,” alisema Makonda.

Tuhuma zinazomwandama

Kada huyo wa CCM, akizungumzia tuhuma kuwa alishiriki kumpiga Jaji Warioba, alisema kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho na hakuna mtu yeyote anayeweza kuthubutu kumpiga mzee huyo.

Alisema tuhuma zinazozidi kumwandama sasa ni mwendelezo wa zile zilizokuwa zikiwatuhumu awali, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

“Mimi ni kama napokea kijiti kutoka kwa hawa watangulizi wangu, walishatuhumiwa sana kuwa walikuwa wakitumwa kuanzisha vurugu na mambo mengine mengi, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyethibitisha hili, binafsi naona huu ni mchezo tu wa kisiasa wa watu kutaka kutafuta huruma kutoka kwa watu wengine,” alisema Makonda.

Alisema hata malumbano yanayoendelea hivi sasa kuhusiana na Katiba hiyo mpya, hayaihusu Tume ya Warioba bali ni baina ya vyama vya siasa vinavyotaka kujitafutia umaarufu kila kimoja kwa mtindo wake.

Alipoulizwa ni kwa nini UVCCM iliamua kutoa tamko linaloashiria kuanza kwa mapambano ya kuhakikisha Katiba hiyo inapita kwa kupigiwa kura ya ndiyo na Watanzania wote, Makonda alisema: “Mimi kama msemaji wa UVCCM, hatukuwahi kutoa tamko kama hilo, hii ni propaganda tu ya wapinzani wetu.” Makonda alisema daima huwa anaamini katika ukweli na siku zote hupenda kusimamia kile anachokiona kina masilahi kwa umma wa Watanzania.

JK apiga marufuku kampeni, Ukawa wanasa waraka mzito

$
0
0
Wakati Rais Jakaya Kikwete akipiga marufuku vyama vya siasa na asasi za kiraia kufanya mapema kampeni za kuhamasisha wananchi kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umenasa waraka wa mkakati wa kutumia Sh2.5 bilioni za umma kuipigia debe katiba hiyo.

Pamoja na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa Dodoma, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein jana hiyohiyo, aliwataka Wazanzibari kuipitisha Katiba Inayopendekezwa bila kufanya makosa.

Nyuma ya kauli hizo za marais, Ukawa umesema umeandaliwa mkakati kabambe wa kuvitumia vyombo vya habari kwa fedha za umma kutoka Ikulu kuwashawishi wananchi kupigia kura ya ‘ndiyo’ katiba hiyo.

Kauli ya Rais Kikwete

“Kwa sababu hiyo naomba Watanzania wenzangu tuzingatie mamlaka ya Sheria ya Kura ya Maoni ambayo imeelekeza vizuri lini kura ya maoni itafanyika na lini kampeni zitafanyika, lini wadau watatoa elimu naomba tuwe na subira. Tukizingatia sheria hii hakuna ugomvi.”

Aliongeza hadi Tume itakapotoa maelekezo ya utekelezaji, wakati wa kampeni na kutoa elimu kwa umma bado na kwamba sheria ipo na imezipanga siku maalumu za kufanya hivyo.

Alisema licha ya sheria kuruhusu kampeni kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kura za maoni kupigwa, kwa mamlaka yake akiwa kiongozi wa nchi, kura na kampeni vitafanyika ndani ya siku 30 tu.

“Kampeni zitaanza tarehe 30 Machi na kumalizika tarehe 29 Aprili ikiwa ni siku moja kabla ya kupiga kura ya maoni. Muda huo ndiyo utakuwa wa kufanya hivyo,” alisema Kikwete.

 Waraka wa wapinzani

Jana, viongozi wa Ukawa walieleza kunasa waraka wa mkakati unaofanywa na Ikulu kutaka kuidhinisha fedha za umma Sh2.5 bilioni kwa ajili malipo kwa vyombo vya habari vitakavyotumika kushawishi wananchi kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa.

Tuhuma hizo ziliibuliwa jana kwa nyakati tofauti na Katibu Mwenza wa Ukawa, Dk Willibrod Slaa katika mkutano uliohusisha viongozi wenzake wa Ukawa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee katika moja ya mikutano yake Kanda ya Ziwa.

Viongozi wengine waliokuwapo kwenye mkutano wa Ukawa ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dk Slaa alisema mpango huo unaratibiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu.

Alisema Rweyemamu amepeleka dokezo hilo kwa Katibu wa Rais akitaka kuidhinishiwa kiasi hicho cha fedha ili kampeni za kushawishi wananchi zianze kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kazi ya kuelimisha umma itafanywa na kamati mbili zitakazoundwa na tume hiyo.

Alisema kabla ya kupiga kura ya maoni, Tume itaunda kamati mbili, moja itakuwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa kundi litakalopiga kura ya ‘ndiyo’ na ya pili kwa ajili ya elimu kwa kundi la ‘hapana’.

“Gharama za kamati hizo mbili zitakazoundwa maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa makundi hayo zitatolewa na NEC,” alisema Jaji Lubuva.
“Katika matangazo hayo kuna orodha ya wasomi 20 baadhi kutoka vyuo vikuu watakaokuwa wakishiriki kwenye mahojiano ambao kazi yao ni kueleza umuhimu kwa wananchi kuipigia kura ya ‘ndiyo’ Katiba Inayopendekezwa,” lilisema dokezo hilo huku likiwataja kwa majina baadhi ya wasomi hao.

Katika dokezo hilo, yametajwa majina ya watangazaji tisa wa televisheni ambao wataandaa vipindi kwa ajili ya `kuipigia debe’ Katiba Inayopendekezwa.

Lilisema kutakuwa na vituo vya redio 22 zikiwamo za kanda na mikoa ambazo zitafikisha ujumbe huo ili kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa.

“Umuhimu wa mpango huu ni kuiepusha Serikali na aibu ambayo inaweza kutokea endapo wananchi wataamua kuikataa Katiba Inayopendekezwa katika kura ya maoni,” Slaa alisoma sehemu ya dokezo hilo ambalo gazeti hili limeliona.

Alisema dokezo hilo linapendekeza kuwashirikisha wasanii wa kizazi kipya, makundi maalumu katika jamii, ngoma na vikundi vya utamaduni asili na magazeti yakiwamo ya udaku.

“Kundi la wahariri linaandaliwa kwa ajili kusaidia kuitangaza Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya magazeti, bajeti itajulikana baada ya kukamilisha mazungumzo na wahariri hao,” alisema Slaa akirejea dokezo hilo.

Alisema huo ni ufisadi wa fedha za walipakodi kutumika kupitisha Katiba ambayo haina manufaa kwa wananchi, bali kwa wanachama wa CCM.

“Hizi si fedha za Rais Kikwete, ni fedha za walipakodi wa nchi hii. Ikulu kutumia fedha hizi kwa ajili ya kushawishi wananchi ni ufisadi,” alisema.

Akizungumzia hilo, Mbatia alisema wakati Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikikosa Sh8 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa dawa, Sh2.5 bilioni zinatumika kupitisha Katiba yenye manufaa kwa wanaCCM na si wananchi.





Ukijaliwa Kuwa Msichana Mzuri na Mrembo Usidhani Kamwe Utatetemesha Kila Mwanaume

$
0
0
Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna wanaume na akili zao kichwani,urembo wako hauwasumbui kama bichwa lako ni kanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utashangaa no one is paying attention,watu utakaowapata ni walewale kanyaboya wenzako, na hawana futuretabaki unaliwa bure kila siku unatoa macho.

Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana,madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata mwingine kisa wewe ni mzuri, la hasha Mwanaume akijitoa mhanga kukupenda kwa uzuri wako mheshimu,maana viumbe wa kike wakiwa wazuri ni shida na matatizo hakuna mtu anataka,sasa ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako,maana hicho ndo kinakudanganya sana kwamba we ni mrembo.

Watch out drama zina mwisho, leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa usidhani wanaume hawaumii, tunaumia
sema hatusemi tu,machozi yetu kama ya samaki.

Mama Ajifungua Mtoto Kisha Amdumbukiza Chooni, Majirani Wasikia Akilia na Kumuokoa

$
0
0
Tukio hili la kusikitisha limetokea Mkoani Iringa ambapo mwanamke mmoja alijifungua mtoto na kisha kumdumbukiza katika tundu la choo. Mtoto huyo alizaliwa nyumbani sio hospitali baadae siku ya tarehe 04/11/2014 mama huyo alimdumbumiza kichanga hiko jinsia ya Kiume chooni.

Mama huyo alietambulika kwa jina la Magdalena inasemekana lengo kuu la kufanya kitendo hiko cha kikatili ni kuficha ukweli kwa mume wake aliekua safarini kuwa amezaa. kwani tabia yake imekua ni kutoka na wanaume wengine pindi mumewe akiwa hayupo na this time alinasa. ili kujinasua akaamua kudumbukiza mtoto chooni na yeye abaki kuwa mwanamke kwema mbele ya macho ya mumewe.

Mtoto huyo alidumbukizwa chooni jion/usiku wa tarehe 04 na kuokolewa asubuhi yake tarehe 05/11/2014 (leo) baada ya majirani kusikia sauti za kilio cha mtoto mchanga. Mtoto huyo yuko hospitalin kwa sasa huku mama yake akishikiliwa na polisi mwa mahojiano zaidi. 

INASIKITISHA KWA KWELI.
Follow us on Instagram: Udakuspecially

Muongozaji Wa Video Tanzania Nisher Atoa Ujumbe Huu Kwa Wanaomkosoa Mitandaoni

$
0
0
Nisher ni miongoni mwa waongozaji/mtayarishaji wa video aliyepitia changamoto nyingi mpaka kueleweka na wafuatiliaji wa kazi za bongo fleva.Kupitia Instagram yake Nisher ameandika haya maneno kwa wanaomkosoa kila mara kwa kuandika waraka tofauti kuhusu yeye na kazi zake.
Nisher Ametengeneza video kama Nasry-Nini. Ben Pol Ft Joh Makini-Unanichora, Nikki Wa Pili Ft Joh Makini Na G Nako-Nje Ya Box..

Follow me on Instagram: Udakuspecially

Hasheem Thabit Akataa offer ya Kucheza Ulaya, Aamua Kurudi Tena D-League

$
0
0
Mtanzania anayepeperusha bendera ya nchi yake kwenye Nba, Hasheem Thabeet amerudi kwenye D-League baada ya kusajiliwa na Grand Rapids Drive.

Kabla ya kwenda D-League kwa mara ya pili, Hasheem alikataa kwenda kwenye timu za Ulaya ambazo zilionyesha nia ya kumsajili.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Detroit Pistons, "Hasheem anaweza kurudi kwenye NBA Muda wowote na uwezekano bado upo" alinukuliwa Andrew Loomis.


Gardner G Habash ‘Kapteini’ Adaiwa Kumpandisha Lady Jay Dee Kortini

$
0
0
Na Musa Mateja
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.

Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.

Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.

“Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali.

“Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane kiroho safi lakini Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani anaogopa ule usemi kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria.”

Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, kitendo cha Jaydee kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.

Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na kuamua kukimbilia mahakamani. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: “Kaka kusema kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata wapi dah.”

Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aitwaye Wakazi.
GPL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live




Latest Images