Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Kipande cha wimbo mpya wa Dimond platnumz chavunja rekodi

0
0
Teaser ya wimbo wa msanii kinara katika muziki wa Bongo "Dimond platnumz" imevunja rekodi ya kupakuliwa katika mitandao mara nyingi zaidi, kipande hicho ni cha sekunde 21 kinachoonyesha kuwa hiyo nyimbo itakuwa bora kabisa endapo itatotelewa mwaka huu au ujao...hebu iangalie halafu utoe maneno yako bila unafki wala ushabiki...mi naanza kusema hili litakuwa BONGE LA HIT ....

Johari: Sitaki Kusikia Habari za Chuchu

0
0
STAA wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘ Johari’ amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia habari za mwigizaji, Chuchu Hans ambaye wamekuwa wakitifuana mara kwa mara wakidaiwa kugombea penzi la Vincent Kigosi ‘ Ray ’ .

Akikitemea cheche kinasa sauti cha paparazi wetu baada ya kuulizwa kuhusiana na hatma ya malumbano yao ya mara kwa mara na Chuchu, Johari alisema hataki kumzungumzia mwanadada huyo kwani anampaisha bure . 

“Nimeamua nikae kimya kabisa wala sitaki kuzozana na mtu nitajishushia hadhi kwa mashabiki wangu bure , siwezi kuwa namnufaisha mtu kwa kumpandisha daraja kupitia mgongo wangu kutokana na malumbano, ” alisema Johari.

Mchungaji wa Sinza Akamatwa na Madawa ya Kulevya

0
0
Stori: MAKONGORO OGING’ na Haruni Sanchawa               
KIMENUKA! Vigogo wa madawa ya kulevya wakiwemo viongozi wa dini sasa wanaanza kupukutika kutoka kwenye mstari wa siri huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi kufuatia oparesheni kali inayofanywa na Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulenya Tanzania kuwanasa kila kukicha, Uwazi  lina mchoro kamili.

Hivi karibuni kikosi hicho kimemkamata askofu (mwangalizi mkuu wa kanisa) aliyetambulika kwa jina la Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria ambaye ana kanisa la kiroho maeneo ya Sinza jijini Dar.
Jina la kanisa hilo limedhibitiwa na vyombo husika kwa sababu ya uchunguzi zaidi na uhalali wake wa kuwepo nchini.

SIKU YA TUKIO
Vyanzo vyetu makini ndani ya kikosi kazi vinaeleza kwamba, mchungaji huyo alikamatwa Oktoba 31, mwaka huu saa kumi usiku Tegeta wilayani Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroine kilo 35.

KAMA UNGEINGIA SOKONI
 Habari za ndani kutoka kwenye oparesheni hiyo zinasema kuwa, endapo unga huo ungeingia sokoni na kununuliwa, basi mtumishi huyo wa Mungu angevuna kitita cha zaidi ya shilingi bilioni mbili.

NYUMBA ALIYONASIWA YA PROFESA
Mchungaji huyo ambaye serikali imeanza kazi ya kulichunguza kanisa lake, alidakwa na mzigo huo haramu kwenye makazi aliyopanga ambayo ni nyumba ya profesa mmoja wa chuo kikuu, Mbezi jijini Dar es Salaam.

WASHIRIKA NAO WADAKWA
Kwa mujibu wa chanzo, kamatakamata ya mchungaji huyo pia iliwakumba watuhumiwa wengine ambao ni Walyat Khan raia wa Pakistani, Chuksi Sylvester Agbazuo na Tony Olafor wote raia wa Nigeria na inadaiwa kwamba walikuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali na kutoroka.

HABARI NYETI
Habari za siri ambazo Uwazi ilizinasa zinadai kuwa,  watumishi wa Mungu waliokuwa kwenye orodha ya kunaswa walikuwa wengi lakini  wamekimbilia nje ya nchi na kikosi hicho kimeshawasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kuwasaka na kuwatia nguvuni.

MAJINA MAPYA MEZAN KWA NZOWA
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa amekabidhiwa majina ya vigogo wakiwemo viongozi wa dini ambao ni sugu katika biashara hiyo. Mbali na majina hayo,  pia amepewa ratiba zao za safari za kibiashara hivyo kilichobaki ni kuwafuatilia na kuwakamata na ushahidi ili kuhakikisha kwamba hawawezi kupona mahakamani.

MTANDAO HATARI
Habari zaidi zinadai kuwa, siku za hivi karibuni, Kamanda  Nzowa amekuwa akifumua mtandao wa watu wazito katika biashara hiyo na imebainika kuwa vigogo hao wana mtandao mkubwa serikalini ikiwemo wizara ya mambo ya ndani ambao wanawalinda kwa kupewa mamilioni ya pesa kwa ajili ya usimamizi wa upitishwaji wa biashara hiyo haramu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar.

“Unajua zamani viongozi hao serikalini walikuwa wakimsumbua Kamanda Nzowa ili awaachie watuhumiwa waliokamatwa na unga bila mafanikio, lakini sasa wameshamsoma kiasi kwamba hata wakikamatwa hawampigii simu tena,” kilisema chanzo kingine.

WATOTO WA VIGOGO
Habari nyingine zinadai kuwa, Kamanda Nzowa pia ana majina ya watoto wa vigogo wa serikali wanaojihusisha na biashara hiyo na anayafanyia kazi.

KUMBUKUMBU
Kukamatwa kwa askofu huyo kumekuja baada ya kukamatwa kwa vigogo ambao ni viongozi wa dini katika makanisa ya kilokole.

Januari 11, mwaka huu, Askofu Moris Charles alidaiwa kukamatwa na polisi maeneo ya Chinga Mbili mkoani Lindi akiwa na kilo 210 za madawa ya kulevya aina ya heroine yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4, kesi yake bado inaendelea mahakamani mkoani humo.

Juni 8, 2011 polisi walifanikiwa kumkamata Mchungaji Kapupu Denis Okechuku wa kanisa la kilokole lililopo Kinondoni Biafra akiwa na kilo 81 za cocaine, kesi yao bado ipo Mahakama ya Kisutu, Dar.

KAMANDA NZOWA
Uwazi lilipomtafuta Kamanda Nzowa ofisini kwake juzi, alisema kuna watu wanne waliokamatwa Tegeta wakiwa na kilo 35 za madawa ya kulevya aina ya heroin na kuna wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.

“Kwa sasa nisingependa kuzungumzia sakata hilo kutokana na sababu za kiupelelezi kwani kuna wengine tunawatafuta na nitahakikisha wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, nawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao,” alisema Nzowa.

Ally Keissy ‘Alianzisha’ Tena Bungeni Kuhusu Suala ya Kikwete Kutibiwa Marekani

0
0
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy almanusura azue kizaazaa kwa mara nyingine na wabunge wa Zanzibar alipohoji sababu ya wabunge hao kuzungumzia suala la Rais Jakaya Kikwete kwenda kutibiwa Marekani akisema wenyewe wamekuwa wakienda kutibiwa India.

Mbunge huyo amekuwa akiingia katika mgogoro na wabunge wa Zanzibar kuhusu masuala mbalimbali. Kwanza ilikuwa katika Bunge la Bajeti lililopita, alipochangia Bajeti ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akihoji mchango wa Zanzibar katika wizara hiyo na mwisho ilikuwa katika Bunge la Katiba alipokuwa akichangia suala la Muungano.

Jana, Kessy alisema hayo wakati Naibu Spika, Job Ndugai alipokuwa akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge walioiomba baada ya kipindi cha maswali na majibu kitendo ambacho kiliwafanya wabunge karibu wote wa upinzani kusimama wengine wakitaka atolewe nje.

Wakati Ndugai akiendelea kusikiliza miongozo hiyo, Kessy alisimama na kupewa nafasi kisha kusema: “Hao wanapiga kelele kwa nini Rais amekwenda kutibiwa Marekani mbona wao wamekwenda kutibiwa India? Tena nawafahamu wabunge kama sita hasa wa CUF, sasa Rais kaenda kutibiwa Marekani mnahoji, je, mlitaka akatibiwe Zanzibar?

Kauli hiyo iliamsha hasira za wabunge wa upande wa upinzani ambao walisimama wakitaka Keissy achukuliwe hatua za kinidhamu.

Rais Kikwete yuko Marekani baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume kwenye Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland ambako taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana, ilisema hali yake inaendelea kuimarika na alianza kufanya mazoezi ya kutembea tangu juzi.

Baada ya wabunge wa upinzani kusimama akiwamo David Kafulila (Kigoma Kusini - NCCR Mageuzi), David Silinde (Mbozi Magharibi - Chadema) na wengine wakitaka Kessy atimuliwe, Ndugai aliwaomba kuwa watulivu huku Kessy akiamua kutoka kwenye Ukumbi wa Bunge.

Wakati Kessy akitoka, Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji alinyanyuka na kuonekana kumfuata lakini alizuiwa na walinzi pamoja na Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage na kumrudisha huku Keissy akisindikizwa na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba na mmoja wa walinzi wa Bunge.

Interpol Yawasaka Wachina 30 kwa Ujangili wa Tembo

0
0
Siku tano baada ya Serikali kukanusha vikali ripoti ya Shirika la Kimataifa la Mazingira (EIA) iliyoihusisha China na utoroshaji wa meno ya tembo nchini wakati wa ziara ya Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping mwaka jana, Shirika la Polisi la Kimataifa (Intepol), Tawi la Tanzania limesema linawatafuta raia zaidi ya 30 wa China ambao wanatuhumiwa kusafirisha meno ya tembo na kufanya uharamia wa kimazingira katika hifadhi za Taifa nchini.

Kauli ya Interpol inakuja huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu kashfa hiyo iliyosambaa wiki iliyopita kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa ambayo hata hivyo, Serikali imekanusha kupitia Ikulu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maliasili na Utalii huku ubalozi wa China nchini nao ukitoa tamko la kukanusha taarifa hizo.

Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav Babile alisema jana kuwa raia hao wa China wanatafutwa popote walipo duniani na hivyo watakapopatikana watakamatwa.

“Tunawatafuta popote duniani kwa usafirishaji wa meno ya tembo na uharamia wa mazingira, wakipatikana watachukuliwa hatua,” alisema Kamishna Babile.

Alisema majina na idadi kamili ya Wachina wanaotafutwa ipo na endapo kuna umuhimu wa kutajwa, yatatangazwa.

Mpaka sasa, mtandao wa Interpol umeweka majina ya raia wawili wa China, Mingzhi Zhang na Deng Jiyun ambao wanasakwa kwa tuhuma za kusafirisha meno ya tembo.

Wanadiplomasia kutokaguliwa

Wakati ripoti hiyo ilidai meno hayo yalisafirishwa kwa ndege ya Rais wa China kupitia maofisa wa kidiplomasia wa nchi hiyo ambao hawakaguliwi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema maofisa wataendelea kutokaguliwa kwa kuwa Serikali haiwezi kubadili sheria za kimataifa za maofisa hao kupata kinga ya kutokaguliwa wanapokuwa kwenye msafara wa Rais.

“Kwa ninavyojua, ukaguzi wa mizigo kwa misafara ya kidiplomasia unazingatia na kutawaliwa na sheria za kimataifa kwa hiyo Tanzania haiwezi kubadili tu kama Taifa,” alisema Balozi Sefue.

Hata hivyo, alisema ni vyema kama Wizara ya Mambo ya Nje ingezungumzia suala hilo la sheria za kutokaguliwa kwa mizigo ya maofisa wa msafara wa Rais.

“Ni sheria za kimataifa kwa hiyo ipo, mizigo ambayo inakidhi vigezo vya kimataifa vya kutofanyiwa ukaguzi na ipo ambayo haina vigezo hivyo,” alisema Sefue.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Katibu Mkuu wake, Michael Haule hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo lakini ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema: “Kwa kawaida mizigo ya wanadiplomasia hao hukaguliwa ila wao wenyewe ndiyo hawakaguliwi, hilo ndilo jambo msilolielewa, ingekuwa wamebeba kitu kingeonekana tu.”

Mtoto Aliyefaulu la Saba Nusura Atolewe Kafara

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limemtia mbaroni mganga mmoja wa jadi anayedaiwa kuteka watoto kwa njia za kishirikina kwa ajili ya kutolewa kafara.

Mbali na mganga huyo, pia wamemtia mbaroni mwanamke mmoja, anayedaiwa kusuka mipango ya kutekwa nyara kwa watoto na kuwahifadhi kwa mganga huyo.

Mganga huyo ambaye anadaiwa ni mwenyeji wa mkoani Mbeya, alikutwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, akiwa tayari amepumbazwa tayari kumpeleka Mbozi mkoani Mbeya. Mtoto huyo aliyemaliza darasa la saba mapema mwaka huu Shule ya Msingi Majengo katika Manispaa ya Moshi ni miongoni mwa waliofaulu katika mtihani wa Taifa.

Kwa mujibu wa habari hizo, mganga huyo (jina tunalo), anadaiwa kushirikiana na mwanamke mmoja, mkazi wa TPC kula njama za kumteka mtoto huyo. “Huyo mwanamke ndiye alishirikiana na huyo mganga kumteka mtoto kwa lengo la kumpeleka Mbozi, mkoani Mbeya na ajabu ni kwamba naye alikuwa akishiriki kumtafuta,” imedokezwa.

Kulingana na chanzo hicho, kiini cha kugundulika kwa mpango huo ni baada ya mwanamke huyo kwenda na rafiki yake kwa mganga, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kusafiri.

“Walipeleka chakula kwa huyo mganga na walipoingia ndani ndipo rafiki yake akamuuliza mbona huyu mtoto, ndiye anayetafutwa,” alidokeza mmoja wa ndugu wa mtoto na kuongeza:

“Huyo mwanamke ndiyo akamwambia naomba unyamaze kwa sababu huyu mtoto anasafiri kwenda Mbozi na mganga na wazazi wake hawatakaa wamwone tena na ndiyo maana nimeleta na hili begi.”

Hata hivyo, rafiki huyo aliamua kuvujisha siri hiyo kwa ndugu wa mtoto huyo kuwa amefichwa nyumbani kwa mganga huyo na ndipo ndugu walipomfuata kwa mganga.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kituo cha kati cha polisi mjini Moshi, Prosper Swai ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo, alisema mwanaye alitoweka Novemba 2 na baada ya kutoonekana alitoa taarifa kituo cha Polisi cha TPC na kwa uongozi wa kijiji na juhudi za kumtafuta hazikuzaa matunda.

Swai alisema baada ya siku tano, alipata taarifa kwa mtu mmoja kuwa mwanae amehifadhiwa nyumbani kwa mganga na alipelekwa na mwanamke huyo.

Baada ya kupata taarifa hizo, akiwa na polisi na uongozi wa kijiji, walivamia nyumba ya mganga huyo na kumkuta mtoto akiwa amelala chini kwenye mfuko wa mbolea akiwa hajitambui.

Alifafanua kuwa baada ya kumpata mtoto huyo, alimkagua na kumkuta na hirizi kubwa kiunoni hali iliyomfanya aogope kuwa mwanae huyo aliibwa kwa lengo la kutolewa kafara.

Swai alisema matukio ya wizi wa watoto katika eneo la TPC na maeneo ya jirani yamekithiri na katika kipindi cha mwezi mmoja, watoto wanne wamepotea katika mazingira hayo.

Alisema wawili kati yao ni wakazi wa Kijiji cha Langasani na walikutwa wamekatwa viungo na kutupwa msituni wakati mtoto mwingine ni wa Kijiji cha Chekereni ambaye bado hajapatikana.

Mtoto mwingine ni wa Kijiji cha Mbugani alitoweka juzi baada ya baba yake kumtuma kwenda kukagua tanuru la matofali na hadi jana mchana alikuwa hajapatikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alikiri kumshikilia mganga huyo na watu wengine wanaodaiwa kuhusika kumpeleka mtoto huyo kwa mganga huyo na kuwa atatoa taarifa baada ya kukusanya taarifa zaidi.

Siti Mtemvu Kuburuzwa Mahakamani Kwa Udanganyifu

0
0
Huku akiwa ametangaza kuvua taji la urembo la Taifa 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti Mtemvu, anadaiwa kuandaliwa hati ya mashtaka kuhusiana na tuhuma za kudanganya umri wake ili kutimiza sifa za kushiriki shindano hilo ambalo fainali zake kitaifa zilifanyika Oktoba 11, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari NIPASHE ilizozipata jijini jana zinadai kuwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) tayari wameshabaini kwamba Sitti alipata cheti kipya kwa njia ya udanganyifu na sasa wanaendelea kuchunguza ili kuwabaini wale waliohusika katika kukipata cheti hicho ili wote waweze kushtakiwa pamoja.

Chanzo chetu kiliendelea kueleza kwamba taasisi hiyo imechukizwa na sakata hilo na inataka kuchukua hatua zinazostahili ili iwe fundisho kwa wote ambao wanania ya kufanya kosa la aina hiyo.

"Imebainika kuwa watu wengi wanatoa taarifa zisizo sahihi ili kupata vyeti vipya vya kuzaliwa kwa lengo la kuwasaidia katika kupata ajira, nafasi za masomo au kurahisisha mambo yao mengine, sasa hatutaki taasisi yetu iendelee kuchafuliwa jina, kuna tamko litatolewa hivi karibuni, hatutakaa kimya," kiliongeza chanzo chetu.

WANASHERIA WALONGA
Alex Mgongolwa, wa jijini aliliambia gazeti hili kuwa kosa la kughushi limegawanyika katika sehemu mbili na kila moja lina adhabu yake tofauti.

Mgongolwa alisema kuwa kosa la kwanza la kughushi nyaraka adhabu yake ni miaka saba jela kama ilivyoainishwa katika kifungu cha kanuni cha adhabu namba 333.

Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, alisema katika kifungu cha 337 endapo mtu atapatikana na hatia ya kutumia hati iliyoghushiwa, hukumu yake itakuwa ni kwenda jela kwa muda wa miaka mitatu.

"Kama mtuhumiwa atakuwa amekutwa na hati hiyo ya kughushi na alishiriki pia katika kuitengeneza atakumbana na adhabu zote mbili," alisema mwanasheria huyo maarufu na mwanachama wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wanachama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Katibu Mkuu wa zamani wa Simba na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Sheria wa TFF, Evodius Mtawala, alisema kuwa kifungu cha 339 kinaeleza kwamba mtu atakayebainika amedanganya kwa kughushi atatakiwa kwenda jela kwa muda wa miaka saba.

"Ila kifungu cha 338 ambacho kinaeleza makosa ya kughushi wosia, hati za ardhi, hukumu ya mahakama, hundi, nyaraka za benki, fedha au malipo yoyote, adhabu yake ni kifungo cha maisha," alisema Mtawala.

Naye Wakili, Damas Ndumbaro, alisema kuwa kwanza mtu atakayebainika na kosa hilo anatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja na hukumu yake itatolewa ya kwenda jela na haina faini.

"Uthibitisho ukishapatikana mtu huyo anafikishwa mahakamani moja kwa moja," Ndumbaro aliongeza.Kifungu namba 28 (3) cha Sheria ya Kuandikisha Vizazi na Vifo ya Rita kimeweka wazi kuwa atakayebainika ametoa taarifa za uongo ili kupata cheti cha kuzaliwa adhabu yake ni kwenda jela kwa muda usiopungua miaka mitatu. 

Cheti ambacho Rita inakifanyia uchunguzi ni kile kilichotolewa Septemba 9, mwaka huu chenye namba 1000580309 ambacho kinataja jina la baba wa Sitti ni Abbas Mtemvu Zuberi (Mbunge-Temeke) na mama yake ni Mariam Nassor Juma ambaye ni diwani wa Temeke, jijini Dar es Salaam.

Cheti hicho kinaonesha Sitti amezaliwa Mei 31, 1991.Moja ya taarifa za awali zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii siku moja baada ya mrembo huyo kushinda taji ni hati ya kusafiria inayoonesha ilitolewa Februari 15, 2007 na muda wake wa kutumika mwisho ukiwa ni Februari 14, 2017, huku zikitaja tarehe ya kuzaliwa Sitti ni Mei 31, 1989.

CHANZO:NIPASHE

Kwa Maoni yako Nani zaidi kati ya Wema au Zari?

0
0

Diamond na Zari Week hii Wamekuwa Katika Midomo ya Watu kila kona .... Je kwa Mtazamo wako kati ya Zari na Wema Nani Zaidi? Je urafiki huu mpya wa Diamond na Zari ni zaidi ya wapenzi au ni mazungumzo tu?

Mizaa Mingine Bana....Ona Rais Wetu na Docta Wake Wanavyoongea

0
0
Hahah..Mizaa mingine bana...This Made my Day....

Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi ya Filbert Bayi

0
0
Moto mkubwa umeteketeza majengo ya Shule ya msingi Filbert Bayi na kisha kusambaa na kuteketeza mabweni yote ya Wanafunzi pamoja na madarasa.
Mwenyekiti wa shule hiyo Filbert Bayi amesema moto huo ulianza saa nane usiku katika bweni la wanafunzi wa kike na kisha kusambaa shule nzima kutokana na gari za zimamoto kuchelewa kufika mapema.

Hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa wala kudhurika kutokana na moto huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna mwandamizi wa Polisi Litrichi Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili juu ya chanzo cha moto huo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bonyeza play kusikiliza taarifa iliyoripotiwa na televisheni ya TBC 1 kuhusu ajali hiyo.

Taarifa Kuhusu Comments za Anonymous kwenye Blog hii

0
0
Kutokana na Muongozo wa TCRA ambao umetolewa leo kwa bloggers kuhusu wakati huu tunapoelekea kwenye wa Mchakato wa Changuzi mbali mbali, blog hii imeonelea kufunga sehemu ya Comment za watu wasiyojulikana (Anonymous) ili kuepusha comments za uchochezi zinazoandikwa na watu wasioweza kutambulika haraka..Hivyo basi kuanzia sasa utaweza kutoa comment yako kwa kupitia Facebook Comment Box ambayo ipo chini mwisho wa Habari .
Asanteni 
Blog Admin

Samson Mwigamba 'atimuliwa' uongozi ACT-Tanzania; Kitila Mkumbo Apewa Karipio Kali

0
0
Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba amesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili,kuvunja katiba na ubadhirifu ndani ya chama hicho.

Taarifa kutoka kwa waasisi wa chama hicho ambao ni Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona zinasema mbali na Mwigamba pia chama hicho kimetoa karipio kali kwa viongozi waandamizi wa chama hicho Professor Kitila Mkumbo na Habib Mchange kwa tuhuma mbalimbali.

Ikumbukwe Samson Mwigamba,Prof Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe walitimuliwa uongozi ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu kwa tuhuma kama hizi na kusababisha kukimbilia chama cha ACT Tanzania.

Source:Mtanzania Jumatano

Updates zaidi....

Waasisi wa ACT Tanzania Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona waliwaambia waandishi wa habari jana kuwa waliwakaribisha Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ndani ya chama hicho kwa nia njema kumbe ni wasaliti na walaghai wakubwa.

Alisema kwanza kina Mwigamba wanajivika uasisi wa ACT huku wakijua si kweli. Pia kina Mwigamba wanatuhumiwa kwenda ofisi ya Msajili kubadili nembo ya chama kinyume cha utaratibu. Pia wanatuhumiwa kusajili katiba nyingine kinyume na Katiba waliyoandaa waasisi na kupatia chama usajili.

Nyakarungu amesema tayari Waasisi halali wa ACT wameshamwandikia barua msajili wa vyama kumuelezea juu ya uasi unaofanywa na kina Mwigamba na Kitila

Kwanini Zitto Kabwe Bado Anavaa Magwanda ya CHADEMA?

0
0
Nimemwona mh. Zitto katika Taarifa ya habari ya clouds TV kavalia magwanda ya people .

RAI
Huyu mbunge anajipambanua waziwazi kuwa ni mpinzani wa CHADEMA na wapambe wake wakijinadi kuwa siku yoyote atajiunga na ACT Tanzania. Kwanini yeye Zitto anaendelea kuinadi CHADEMA kwa kuvalia magwanda?

Nawashauri uongozi wa juu umsamehe Zitto kwani bado anaipenda CHADEMA kwani ACT-Tanzania imekosa mwelekeo.

Wadau Wamtaka Sitti Mtemvu Kuvua Mataji Mengine ya Miss Chang'ombe na Miss Temeke 2014

0
0
Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na maneno ya watu kuhusu umri wake. Wadau wamemtaka pia avue mataji mengine mawili ambayo ni Miss Chang'ombe 2014 na Miss Temeke 2014 kwakuwa kote alidanganya.

Kwa upande wako, unaunga mkono jambo hilo au aendelee kubaki nayo hayo mataji mawili?

Mdau Adai EATV Nayo Imepoteza Mvuto..Bora Ingebaki kuwa Channel 5 Kama Zamani

0
0
Mimi ni mfuatiliaji wa hii channel ya vijana lakini naona saizi wanatuwekea bongo movies tu kila siku ni bora wange iacha itwe chanel 5 kuliko EATV na wakati hao wakenya na waganda hawana hata matangazo kwa hiyo chanel.

Hebu fikiria zamani kulikuwa na vipindi kama Afro beat ya Ben na Maimartha, Planet bongo ya Salama, Friday night ya Ssebo, In da house na Jukbox ya Kitenge(O timer) . Hivi ni baadhi ya vipindi bomba lakini saizi hawana jipya hata comedy yenyewe utumbo mtupu. 

Ni hayo tu.

Sitaki maswali sijajianda
~Mdau

Meninah Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutoa Mimba ya Diamond Platnumz

0
0
Mwanamuziki Hot Sexy hapa Bongo, Meninah Atick ameifungukia ishu ya kuchoropoa mimba ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusema hajawahi kubeba mimba ya staa huyo na wala katika maisha yake hajawahi kufanya kitendo hicho.

“Jamani mimi ni mdogo, kwanza kwa nini watu wanapenda kunibebesha vitu vikubwa, mimi sijawahi kubeba wala kuchoropoa mimba katika maisha yangu,” alisema msichana huyo.

Meninah alienda mbele zaidi na kusema maneno hayo yanaweza kuwapandisha hasira wapenzi wa Diamond na kumjengea nao chuki, wakati ukweli ni kwamba hajawahi kutoka na msanii huyo mwenye historia ya kutoka na wasichana wengi.
GPL

TCRA Yawataka Wamiliki wa Blogs Tanzania Kuzitumia Vizuri Wakati wa Uchaguzi

0
0
WAMILIKI wa Blogs nchini wametakiwa kuzitumia vyema blog zao katika kuripoti habari na matukio mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wabunge na urais.

Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma leo alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Blogs hizo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Profesa Nkoma alisisitiza kwamba wakati wa uchaguzi wamiliki wa Blogs wanatakiwa kutoa fursa sawa kwa kila upande pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.

Aidha katika mkutao huo, wamiliki wa Blogs walikubaliana kuendeleza mchakato wa kuwa na umoja wao uliosajiliwa kisheria ambapo walichagua viongozi wa muda watakaosimamia mchakato huo. 

Uongozi wa muda uliopitishwa na wamiliki hao ni kama ifuatavyo:

1.Joachim Mushi - Mwenyekiti

2. Francis Godwin - Makamu Mwenyekiti

3. Khadija Kalili - Katibu

4. Shamim Mwasha - Mjumbe

5. Othman Maulid - Mjumbe

6. William Malecela 'Lemutuz'- Mjumbe

7.Henry Mdimu - Mjumbe

TCRA imeahidi kutoa ushirikiano katika mchakato huo wa kusajili umoja wa wamiliki wa Blogs na kutoa elimu katika masuala mbalimbali yatakayosaidia jamii.

Baada ya Wema na Penny Kumaliza Tofauti zao Sasa Waanza Kushirikiana Kwenye Kazi

0
0
Baada ya staa wa filamu Wema Sepetu na mtangazaji wa radio VJ Penny weekend iliyopita kumaliza tofauti zao zilizowatenganisha kwa muda mrefu, hatimaye sasa wameanza kuwa karibu.


Kupatanishwa kwao kulikofanywa na rafiki yao Junaithar aliyewaalika kwenye dinner ya birthday yake usiku wa Jumamosi, haukuishia hapo bali sasa wamerudisha ukaribu kiasi cha kuanza kutembeleana.

Kupitia Instagram Wema ameshare picha hii mpya akiwa na Penny nyumbani kwake na kuandika:

“And the Saga continues… I must say I am a Happy Soul…. So at peace…. Kajisemea shem lake na nanukuu ” kwenye vitu flani vya PROJECT…..” @vjpenny04 @jumalokole2

Penny naye alii-repost.

Lakini ukaribu wao wa sasa unaonekana pia unahusisha kazi, kupitia akaunti ya mtu ambaye Wema amemtag kwenye picha hiyo @jumalokole2, naye alipost picha hizo alizopiga nao, na kuandika caption zinazoashiria walikuwa wanarekodi kipindi.

jumalokole2: “Watu makini tukifanya yetu new Project @wemasepetu @vjpenny04…..” na nyingine aliandika “Kwenye vitu flani vya PROJECT…..! “

Mtoto wa Rais Kikwete Awacharukia Wale Wanao Msema Anamiliki Simba Trust Australia

0
0
Mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Miraji Kikwete usiku wa Nov 11 2014 ameeleza kuhusu ishu inayosambazwa kwamba anamiliki kampuni ya Simba Trust iliyopo Australia akishirikiana na dada yake.
Kufuatia tuhuma hizo Miraji alipost maandishi akikanusha hiyo ishu akisisitiza kwa hashtag >>>  #Ieleweke hivi ningekuwa napokea milioni 100 kwa siku wallahi ningeshukuru kwa mola ila siwezi kuchukua fedha kinyume na haki ninayo stahili’
‘Katika jambo lililonishangaza ni hizi tuhuma za kuwa ninamiliki kampuni ya Simba trust ya Australia mimi na dada yangu Salama, naona sasas mmeishiwa hoja na kuanza kuzusha mambo, sijawahi kufika Australia na sina kampuni ninayomiliki na dada yangu, lakushangaza kwanini PAP wanilipe pesa bila sababu maalum

Sina pesa nyingi kiasi hicho, kidogo ninachokipata ni kwa jasho langu, sijawahi na sitodiriki kupokea pesa ambazo si haki yangu kupata, acheni kupandikiza chuki zisizo na ukweli wowote, atakaethibitisha basi na aonyeshe hilo kwa vielelezo na ushahidi, chuki hazijengi, kweli umeishiwa hoja na mambo ya msingi ya kujadili

Download Wimbo Mpya wa Izzo B Feat G.Nako-Haina Kufeli

0
0
Msanii Mkali Kwenye Hip Hop Izzo Bizness Ametoa Wimbo Mkali Mwingine Kama Kawaida yake Ambao Amemshirikisha mkali mwingine wa Hip Hop G.nako Unaweza Download Wimbo Huo Hapa chini, Unaweza Kununua Ama Kudownload Bure..Chaguo ni Lako
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images