Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Tamko la Serekali Kuhusu Wizi Unaofanywa na Makampuni ya Simu Tanzania Kwa Wateja Wao

$
0
0
Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, jana katika kikao cha Bunge Dodoma Serikali imesema inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi na kutoa tamko namna ambavyo imejipanga kukabiliana na wizi wa aina hiyo.

Akitoa tamko hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema Serikali itaanzisha kituo maalum cha kushughulikia malalamiko hayo CCC, kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.

Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali ilivyojipanga kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji alisema;

Wizi huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW.. ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano elfu tatu lakini kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa Tabora elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke malalamiko yao, gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai malalamiko ya elfu tatu..”

Hivi serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama Watanzania wamekuwa wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina fund katika wizi huu..?”- Khatib Said Haji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema;

"Napenda nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika kudhibiti wizi huo.. Licha ya utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika makampuni ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia wateja wake, lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga simu muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati unasubiri kulalamika pia unakatwa..

"Kwa hiyo Serikali inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake sio kufuatilia tu mapato lakini ubora wa mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya wakati mwingine yanachelewa wakati mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa hiyo huna haja kusafiri kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu tano. Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..”- January Makamba.

Kila utakapopiga kulalamika utapewa namba maalum ya lalamiko lako, na lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia lalamiko lako na yenyewe itakuwa sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa..”- January Makamba.

Aibu:Picha za Jack wa Maisha Plus Akioga Bafuni Zavuja

$
0
0

Stori: Imelda Mtema
Msanii wa filamu ambaye sasa amejichimbia Dubai akisaka maisha, Jacqueline Dustan amevujisha picha zinazomuonesha akioga bafuni huku akionekana yuko bwii,  jambo ambalo ni kinyume na maadili.

Picha hizo zinamuonesha msanii huyo akiwa kwenye sinki lenye mapovu na nyingine zikimuonesha hadi sehemu zake muhimu.

Katika kutaka kupata sababu ya mwanadada huyo kuziachia picha hizo ambazo Ijumaa imezipata kutoka kwa rafiki yake wa karibu (jina tunalihifadhi) ikidaiwa kuwa aliyempiga ni bwana wake, mwandishi wetu alimtafuta kupitia simu yake ya kiganjani na alipopatikana alisema: Cha ajabu kipi hapo, nilikuwa naoga kwa raha zangu nikamuita mtu akanifotoa, tatizo liko wapi?”
GPL

Dewji Bilionea Namba Moja, Rostam Aziz Anamfuatia

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (39), ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba moja nchini kwa sasa, akifuatiwa na Rostam Aziz (49).

Kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Ventures Afrika lililotolewa jana, wafanyabiashara hao ndiyo Watanzania pekee waliongia kwenye orodha ya mabilionea 55 barani Afrika.

Dewji, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM, ni mfanyabishara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa Dola 2 bilioni Marekani (Sh3 trilioni).

Nafasi hiyo inamfanya kijana huyo kutambulika kama tajiri namba moja nchini kwa sasa na siyo tena Rostam.

Katika orodha hiyo Dewji amemwacha Rostam kwa nafasi 16. Rostam anashika nafasi ya 40 akiwa na utajiri wa Dola 1.2 bilioni za Marekani.

Mwaka jana, Rostam alitajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania. Hiyo ilikuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la Marekani la Forbes. Rostam alikamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.6 trilioni).

Katika orodha hiyo, yumo pia Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma kuwa mmoja wa mabilionea wa Tanzania na Afrika.

Hata hivyo, ripoti ya jarida hilo ya mwaka 2011, ilimtaja Bakhresa kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni) akifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.

Mengi alishikilia nafasi ya pili Tanzania na 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 za Marekani (Sh861 bilioni).

Forbes ilionyesha kuwa Bakhresa alifungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika. Wote walikuwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni). Jarida hilo limemtaja pia tajiri kijana wa Nigeria mwenye umri sawa na Dewji, Igho Sanomi kuwa anashika nafasi ya 30 akimiliki Dola 1.3 bilioni.

Aunty Ezekiel na Odama Watimuliwa Bongo Movie

$
0
0
Hamida Hassan na Gladness Mallya

UPEPO mbaya unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozama katika kikao kilichofanyika juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.

“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama wenye msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.

Baada ya habari hizo kutua katika rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:

Devotha: Mimi ndiyo kwanza nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.

Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.

Lulu Michael 'Masharobaro Hawana Nafasi Kwangu Kwenye Mapenzi, Kwa Sababu Hawafikirii Maisha Kabisa'

$
0
0

Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.

“Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa, hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,” alisema Lulu.

Zitto Amwambia Mbowe Anavyofanya ni Utoto

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kitendo alichofanya Freeman Mbowe cha kumsimanga wakati wa mikutano yake ya hadhara mkoani Kigoma kuwa amemsaidia sana ni cha kitoto.

Zitto amesema “nimeshangazwa na tabia ya Mbowe ya kunisimanga, tena kunisimanga nyumbani kwetu. Hata hivyo nimepuuza kwa maana kwa vyovyote vile aliongea bila kufikiri. Anasema nilitaka kusaliti chama, aseme kwa ushahidi maana kutamka tu hakuna maana hata kidogo.”

"Kiongozi mkubwa kama Mbowe anapaswa kujadili masuala ya Taifa na namna ya kutatua changamoto , sio kubaki kusema na kusimanga watu. Mbinu hiyo hailisaidii Taifa," Amesema Zitto.

“Mimi nina rekodi ya kujivunia … nimeibadilisha Kigoma na kusimamia ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Nimewezesha wakulima kuwa na hifadhiya jamii, bimna ya afya. Je, yeye kafanya nini Hai?” aliuliza Zitto.

Zitto aliendelea kusema "Nimeibua hoja za maana Bungeni zikiwemo ya kubadili sheria kwa manufaa ya nchi. Yeye kafanya nini Bungeni kwa manufaa ya nchi tangu aingie?Ametoa hoja gani binafsi? Ametunga sheria gani binafsi?

Dr. Slaa anasa Mawasiliano ya siri kuhusu utafiti uliofanywa na TWAWEZA

$
0
0
Dar es Salaam. Utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza kuhusu maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa nchini, umeibua madai mapya ambayo yanauhusisha na jitihada za kukisaidia chama tawala CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa Dar es Salaam juzi, inaonyesha kuwa kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika sasa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angeshinda urais kwa asilimia 13, akifuatiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa asilimia 12, huku Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa akiibuka na asilimia kumi na moja.

Mbali na wanasiasa hao, wengine waliotajwa katika ripoti hiyo na asilimia zao kwenye mabano ni Profesa Ibrahim Lipumba (6%), Dk John Magufuli (3%), Freeman Mbowe (3%), Samuel Sitta (4%), Bernard Membe (5%) na Zitto Kabwe (1%).

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa iwapo vyama vyote vya upinzani vitaungana na kumchagua mgombea mmoja wa urais, Dk Slaa angeongoza kwa asilimia 41, akifuatiwa na Profesa Lipumba (14%), Mbowe (11%) na Zitto Kabwe (6%). Wengine ni Tundu Lissu, Maalim Seif Sharif Hamad, James Mbatia na Augustine Mrema ambao kila mmoja aliambulia asilimia moja.

Dk Slaa

Akizungumzia utafiti huo jana, Dk Slaa alisema chama chake kinautilia shaka kwani licha ya kuonyesha kwamba umefanywa na taasisi ya Twaweza, taarifa alizonazo zinaeleza kuwa matokeo yake yameandaliwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana.

Dk Slaa alisema Dk Bana anafahamika kuwa na uhusiano na CCM na kwamba pia anafanya kazi na taasisi nyingine ya utafiti ya Redet jambo linaloonyesha kuwa utafiti huo umeandaliwa kwa manufaa ya CCM.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti jana, madai hayo yalikanushwa na Mkurugenzi wa Twaweza anayemaliza muda wake, Rakesh Rajani na Dk Bana.

Dk Slaa alisema kuwa amepata taarifa alizoziita za kutisha kuwa mmoja wa viongozi nchini (hakumtaja jina) alituma baruapepe kwenda kwa kiongozi mwingine akimwambia kuwa bosi wake atafurahi kwa kuwa kazi aliyowatuma wameimaliza.

“Taarifa hii imetushtua na tunaendelea kuifanyia kazi,” alisema Dk Slaa. Alisema alisoma ripoti ya Twaweza siku tano kabla ya uzinduzi na kwamba alibaini kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi waliohojiwa walikuwa ni wazee.

“Tunataka kujua jambo hili lilifanyika kwa makusudi au lilikuwa na maana gani?”

Katibu Mkuu huyo aliikosoa ripoti hiyo kuwa iliwezaje kutabiri mambo kabla hayajatokea kwa kueleza kuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ungeungana na kumsimamisha mgombea mmoja wa urais.

“Ukitazama taarifa imetolewa lini na maswali yaliulizwa lini utashangaa. Kwa nini unaweka mkokoteni mbele ya punda?” alihoji Dk Slaa. Hata hivyo Twaweza katika ripoti yake inaeleza bayana kwamba iliuliza swali kuhusu mgombea mmoja wa upinzani ikiwa vyama hivyo vitaungana.

“Wakati tunafanya utafiti huu vyama vinavyounda Ukawa vilikuwa havijasaini makubaliano ya kuwa na mgombea mmoja lakini kwa sababu tulishaona dalili na kusikia tetesi, basi tuliamua kuuliza swali hili. Kwa hiyo kwa kuwa sasa tayari vyama hivyo vimeshasaini makubaliano, utafiti mwingine unaweza kuwa na matokeo tofauti kabisa,” alisema Mwasilishaji wa Utafiti huo, Elvis Mushi juzi.

Rakesh atoa ufafanuzi

Akizungumzia tuhuma za kumtumia Dk Bana kufanya utafiti huo, Rakesh alisema siyo za ukweli kwa kuwa matokeo yanaonyesha kuwa walioshinda ni wananchi asilimia 33 ambao hawajaamua kumpigia kura mgombea wa chama chochote.

“Siwezi kusema kama Dk Bana anatumiwa na CCM, lakini ninachojua ni kuwa tulimwalika kushiriki kama mchangia mada kama watu wengine walivyofanya,” alisema.

Kuhusu kundi la wananchi ambao hawajaamua mtu wa kumpigia kura, Rakesh alisema ni vyema hata kama mtu angesema CCM haifai kutokana na matokeo hayo kwa kuwa wagombea wote wamepata chini ya asilimia 15.

Alisema watu wanaoisoma ripoti hiyo kwa kuangalia majina ya watu maarufu wanafanya makosa kwa sababu mwanafunzi hawezi kushangilia kwa kupata maksi ndogo.

“Hivi wewe ukipata mtihani mmoja asilimia 13 na mwingine 33, upi utakuwa umefaulu?” alimhoji mwandishi na kuongeza: “Asilimia 33 ndiyo unakuwa umefaulu.”

Alisema Twaweza imefanya tafiti za Sauti za Wananchi mara 24 na kwamba wamekuwa wakifanya kwa uadilifu wa hali ya juu. Alifafanua kuwa Watanzania wanafurahi pale matokeo ya utafiti yanapokuwa mazuri kwao, lakini hukasirika yanapokuwa kinyume.

Dk Bana ajitetea

Kadhalika, Dk Bana alikanusha tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa dhidi yake akisema hajawahi kuwa na uhusiano na Twaweza huku akidai kuwa hata yeye mwenyewe anatamani CCM itoke madarakani miaka mitano tu, ili wananchi wapate uongozi tofauti.

“Kwa kweli ningekuwa na simu ya Dk Slaa ningempigia. Chadema na Ukawa wakijipanga wanaweza kuchukua nchi maana wana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya habari na makundi ya jamii.

“Kosa walilolifanya ni kumtimua Zitto Kabwe, ni kama vile Barcelona bila (Lionel) Messi. CCM sasa hivi imechokwa wananchi wanataka kuona uongozi tofauti,” alisema Dk Bana.

Alisema kitendo cha Chadema kumhusisha na CCM kitakwamisha mpango wake wa kujiunga na chama hicho ili agombee ubunge katika Jimbo la Bukoba Vijijini... “Ingawa familia yangu haipendi niingie kwenye siasa, bado naendelea kufikiri, lakini kwa mambo haya (Chadema) watanikubali kweli?” alihoji.

Breaking News: Jengo la Machinga Complex Linaungua Moto

$
0
0
Jengo la Machinga Complex lililoko Maeneo ya Karume ilala Linaungua Moto ..Chanzo cha moto bado hakijajulikana ..Habari zaidi na picha zitawajia Baadae

Kampuni ya PAP Yakanusha Kumilikiwa na Familia ya Rais Kikwete, Yataja Wamiliki Wake Halali

$
0
0
KAMPUNI ya Pan Africa Power Resources (PAP) imesema haina mahusiano ya kiumiliki na familia ya Rais Jakaya Kikwete, kama umma unavyoaminishwa kwa kuwekewa taarifa sizizo za kweli kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Taarifa ya kupinga tuhuma hizo ilitolewa jana na Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Kampuni ya IPTL inayomilikiwa na PAP, Joseph Makandege, alipozungumza na waandishi wa habari.

Hivi karibuni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, aitwaye Miraji alisikitishwa na tuhuma hizo zinazotolewa dhidi yake kuhusishwa na umiliki wa kampuni ya PAP kwamba yeye na dada yake, Salama wanamiliki asilimia 50 za PAP kupitia Simba Trust, wakati si kweli.

Akizungumzia jambo hilo, Makandege alisema PAP inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbidher Sing Seth na Simba Trust, ambayo nayo inamiliki asilimia 50.

Kwa mujibu wa Makandege alisema majina ya wamiliki wa Simba Trust ni Settler Clive Anthony Cooke, Pamela Sethi na Hardeep Kaur Chaggar.

Alisema hakuna sehemu yoyote inayoonesha kuwa kuna majina yatokanayo na familia ya Rais Kikwete, wakiwemo watoto wake, ambao ni Salama na Miraji Kikwete, hivyo huo ni mwendelezo wa upotoshaji wa uongo unaofanywa na wanasiasa na baadhi ya watu juu ya IPTL.

“Taarifa zinazosambazwa katika mitandao zina lengo la kuichafua familia ya Rais Kikwete na IPTL na ndio maana tumeona tufafanue ukweli halisi wa jambo hili ili umma uelewe,”alisema.

Makandege alisema PAP/IPTL haipendi kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na sakata la ESCROW linaloendelea bungeni kwa kuwa wanasubiri ripoti ya serikali.

“Tunasubiri ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),”alisema.

Hivyo, Makandege aliwataka Watanzania kuwa makini na taarifa zinazosambazwa katika mitandao kwa kuwa hazielezi ukweli wa jambo hilo

Picha Jinsi Jengo la Machinga Complex Linavyoungua Moto

$
0
0

Jengo la wafanyabiashara ndogondogo (Machinga Complex) lililopo jijini Dar Es Salaam linawaka moto muda huu..Juhudi za kuuzima zinaendelea

Watoto Watatu Wliofungiwa Ndani na Baba yao Kwa Miaka Saba Wazungumza Lugha Isiofahamika

$
0
0
Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.
Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.
Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.
Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.
Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.

Jibu la Serikali lililosubiriwa Baada ya Vipimo vya Ebola Kuhusu yule Binti wa Miaka 17 Aliefariki Sengerema

$
0
0
October 18 2014 Wizara ya Afya ndio ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhusu kuwepo kwa mtu aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola kutokea wilaya ya Sengerema ambapo alikua ni binti wa miaka 17 mkazi wa kijiji cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema.
Alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili ambapo alilazwa kwenye Kituo cha Afya Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba 2014 kabla ya kuhamishiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema October 17 na kufariki duniani siku hiyohiyo saa 3.30 usiku.

Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo ndani ya siku ya 21 zilizopita ambapo alizikwa kama mgonjwa wa Ebola na hakukuwa na ndugu wala yeyote asiehusika isipokua Watu maalum waliokua wamevalia mavazi ya kujikinga.

Baada ya hapo Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilichukuliwa ili ithibitike ni ugonjwa gani umemuua sababu serikali iliahidi kutoa majibu hayo.

 ‘Hili swala la Ebola ni taarifa iliyotolewa bila kupitia kwenye mamlaka husika yani ilikua ni uvumi na huyo mtu aliezungumza kwamba kuna Ebola labda alikua anaona kuna dalili flani zimetokea akawa na wasiwasi lakini nikuhakikishie hatuna Ebola kwenye wilaya ya Sengerema’
‘Yule binti wa miaka 17 alieumwa mpaka akafariki alikua ana ugonjwa wa ini ambapo Wataalamu wanatuambia upande wa Afya kwamba mgonjwa wa Ini anapofikia hatua flani anaweza kupata dalili flani ambazo mtu anaweza kufikiria ni Ebola, tulijitahidi kuhakikisha kwamba hizo sampuli zimepelekwa kwenye Maabara Dar es salaam na taarifa tulizozipata ni kwamba hakuna kabisa dalili za ugonjwa wa Ebola kwa yule mgonjwa ambae alifariki‘ Mkuu wa wilaya Sengerema

Majibu ya Shilole kwa Shabiki Aliyekosoa Nyimbo za Bongo Kuchezwa Sana Jumba la Big Brother Africa

$
0
0
Dj Tass kutoka Tanzania usiku wa November 14 2014 aliiwakilisha Tanzania baada ya kupewa mwaliko wa kwenda kuwarusha  washiriki kwenye jumba la shindano la Big Brother Africa 2014 ambapo sehemu kubwa ya hits alizozicheza ni nyimbo za bongofleva.

Miongoni mwa watu walioangalia burudani hiyo ni Shilole ambaye aliisifia burudani ya Dj Tass kupitia Instagram na kuandika ‘@djtass kaka wew ni ny**o coz umejua kuipenda nchi yako na hizo ngoma zako kali!!@bigbrother africa oyooooooo

Baada ya Shilole kuandika hayo alitokea mmoja wa followers wake ambae aliandika ‘kaitangaza nchi yetu vizuri ila bba it’s all about Africa kwahiyo kwa upande mwingine kawaboa nchi zingine na hata housemates wengine walikua hawachezi maana hawaelewi, kwaio angepiga nyimbo ili wote wafurai,sio sisi tu na idris‘
Shilole hakuchukua time na akaamua kumjibu shabiki huyo kwa kumuandikia comment hii >>> ‘Utakuwa hauna shukran we dada masna asingepiga pia nyimbo zetu pia ungechamba kama si kuha*****! Dj kapiga nyimbo za nchi zote zilizipo pale, hivi lini mtaacha ushamba wa kukoment ××××× kwani lazima ukoment! Mnaboa, nina wasiwasi wewe utakua sio Mtanzania

ISABELA Amchana Mama Wema Sepetu kwa Kuingilia Mapenzi ya Mwanae

$
0
0
MSANII wa Filamu na Muziki Bongo, Isabela Mpanda amemvaa mama wa msanii mwenzake, Wema Sepetu, Miriam Sepetu na kumtaka aache kuingilia mapenzi ya mwanaye kwani mapenzi hayaingiliwi.

Akistorisha na gazeti hili, Isabela alisema siku zote unaopenda ni moyo siyo mwili kwa hiyo mama Wema kama anataka mwanaye aachane kabisa na Diamond basi amtoe moyo uliompa nafasi mwanaume huyo.

Mama Wema kama mzazi anatakiwa akae kimya, amuache mwanaye moyo wake ufanye utakavyo maana kutoa maneno na kufanya sherehe kwa sababu ya mwanaye ameachana na Diamond siyo sawa, akumbuke kwamba Diamond naye ana wazazi, hivi mama yake anajisikiaje jamani?” alihoji Isabela.

Mchungaji Afa Maji baada ya kujaribu kutembea Juu ya Maji kama Yesu

$
0
0
Mchungaji kutoka Nigeria, Frank Kabele (35) amesombwa na maji katika mto mmoja nchini hiyo na kufariki alipojaribu kutembea juu ya maji kama Yesu.

Frank Kabele aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani.

Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya mchungaji huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi na kufariki dunia

Haturuhusu Wafungwa Kufanya Tendo la Ndoa Ndani ya Gerezani

$
0
0
SERIKALI imesema Tanzania haina sheria ya kuwaruhusu wafungwa kukutana faragha na wenzao wao.

Hii ni mara ya tatu kwa serikali kutoa majibu hayo, kutokana na maswali ya wabunge ambapo mara kadhaa swali hilo limekuwa likiulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Salum Msabaha (Chadema).

Hata hivyo, jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alikiri kwa Tanzania kutokuwa na sheria hiyo na akajibu kuwa ujauzito ambao huwapata wafungwa wanawake, unatokana na wafungwa hao kuupata nje ya Magereza.

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF) ambaye alitaka kujua ni kwa namna gani wafungwa wanawake wanapata ujauzito wanapokuwa ndani ya magereza yao.

Pia, alihoji kama magerezani kuna usiri, ni kwa namna gani mahabusi ambao ni mashekhe kutoka Zanzibar wanafanyiwa vitendo vya ulawiti gerezani.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alisema jeshi la Magereza lina utaratibu wa kutenganisha wafungwa wa kiume na wa kike kwani kila watu hutunzwa kwa sehemu zao na hulindwa na watu wa jinsia zao.

Kuhusu tuhuma za kulawitiwa kwa mashekhe wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe, alisema sakata la Shekhe Salum Ali Salum linafanyiwa kazi na kwamba kiongozi huyo ameshafanyiwa uchunguzi wa awali katika Hospitali ya Amana.

“Jambo hilo lipo mikononi mwetu, tumempeleka Hospitali ya Amana na kesho (leo) tutampeleka Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, lakini tunachunguza pia tabia ya kiongozi huyo na mwenendo wake kabla ya kuingia gerezani,” alisema Chikawe.

Hata hivyo, Chikawe alisema kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa watuhumiwa hao, kwani tangu mwanzo hakuwa ameripoti vitendo hivyo, lakini alipofika mara ya nne gerezani ndipo akaripoti kufanyiwa vitendo hivyo na mmoja wa polisi.

Mauaji Yanayotokea Kiteto yanadhihirisha Tanzania Haina Serikali

$
0
0
Mapigano bado yanaendelea kati ya wafugaji wakimasai na wakulima eneo la Matui, chanzo kugombea maeneo ya kilimo na ufugaji, naomba serikali ichukue hatua maana hali ni mbaya sana, hamna hata polisi mmoja aliyeenda kutuliza gasia hizo, watu wengi wameshaanza kuyahama makazi yao kunusuru maisha yao, na inasemekana kuna kundi kubwa la wamasai kutoka Mererani na Simanjiro wamejipanga kwenda kuwasaidia wenzao. 

Raia wamfunga majumba yao na wamekusanyika katika kituo kidogo cha polisi Matui kwajili ya usalama wao.

Kajala: Natamani Kupatana na Wema Sepetu

$
0
0
SIKU chache baada ya mtangazaji Penniel Mungilwa ‘ VJ Penny ’ kupatana na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu , mwigizaji Kajala Masanja ‘ Kay’ naye ameibuka na kuweka bayana kuwa hata yeye yupo radhi na anatamani kupatana na Wema ambaye wameogelea kwenye bifu miezi kadhaa sasa .

Kajala alifunguka hayo mara baada ya paparazi wetu kumuuliza kuhusiana na mtazamo wake juu ya Wema na Penny kupatana ndipo aliposema amefurahi mno na hata watu wengine watakuwa wamejifunza kitu kutokana na kupatana kwao. 

Akizidi kushusha ‘ vesi ’ mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi , Kajala alisema anaamini siku zote bifu zinarudisha nyuma maendeleo hivyo Wema kupatana na Penny ni jambo la busara kwani ni moja ya chachu ya kufanya mambo mengine yaendelee kwani hata yeye hapendezwi na mabifu . Wema Sepetu akipozi .

“Hata mimi natamani kupatana na Wema . Mabifu ni mambo ya kitoto sana, kwa kweli nimefurahi sana kuona Penny na Wema wamepatana kwani ni marafiki wa siku nyingi sana na wanastahili ifike sehemu vitu viishe na maisha yaendelee kama kawaida , ” alisema Kajala .

Alipoulizwa Kajala kama kweli yupo tayari kupatana na Wema na uwezekano huo upo, Kajala alisema muda wowote wanaweza kukaa na kumaliza tofauti zao. “Hata mimi siku si nyingi tutaweka mambo sawa kwa sababu bifu hazijengi , hazina maana hata kidogo ni kufanya mambo yasiende mbele tu , inabidi tubadilike ,” alisema Kajala .

Wema na Kajala walikuwa mashosti wa damu lakini mwaka jana mwishoni waligombana huku chanzo kikitajwa kuwa ni kugombea mwanaume ambaye alifahamika kwa jina la CK.

Geez Mabovu Ameacha Deni kwa Vituo vya Redio, Kucheza Nyimbo zake Sasa Hazililipi

$
0
0
Geez Mabovu amefariki katika kipindi ambacho kwa asilimia kubwa alikuwa amepotea kwenye masikio ya wengi. Na mara nyingi sababu za kupotea kwenye masikio ya watu ni kutochezwa kwa nyimbo za msanii katika vituo vya redio.

Kwahiyo haimaanishi kuwa kupotea kwa msanii kwenye masikio ya watu kunatokana na ukimya wake mwenyewe bali ni kutopata nafasi ya nyimbo zake kuchezwa kwenye vituo vya redio zaidi hata kwenye TV.

Mara ya mwisho kukutana na Geez Mabovu na kuongea naye ilikuwa January 7 mwaka huu pale Msasani Club kwenye kilinge. Nilizungumza naye kwa kirefu na alikuwa mengi ya kueleza kutokana na kupotea kwake. Pamoja na wengi kutomsikia, Geez alikuwa akiendelea na harakati zake za kuachia ngoma.

Sauti yake nzito na uandishi wa akili ulikuwa bado uko vile vile. Siku za hivi karibuni afya yake ilikuwa imedhoofika kiasi pengine ni kutokana na kunywa sana pombe kali. Lakini hiyo haikuwa imeathiri uwezo wake wa pekee katika kuandika na kuchana.

Geez uliyemsikia kwenye ngoma zilizohit kama ‘Mtoto wa Kiume’ ‘Mimi’ na zingine ndiye yule yule aliyesikika kwenye wimbo wa hivi karibuni ‘U Can’t Stop Me Now’ aliomshirikisha Joh Makini na Nisher.

Huu ni miongoni mwa nyimbo za hip hop zilizotoka miaka miwili iliyopita na bora kabisa. Bahati mbaya wimbo huu haukupata nafasi na mashabiki wengi wa hip hop hawakupewa haki ya kuusikiliza. Pengine ulikuwa na nafasi kubwa ya kumrejesha tena kwenye chart. Iwapo wimbo mkali kama huo ulinyimwa nafasi, msanii arekodi wimbo wa aina gani ili apewe fursa? Hatuoni kama kuna tatizo sehemu? Tatizo ambalo linatakiwa kurekebishwa.

Redio hazikuutendea haki wimbo huo. Redio hazikumtendea haki Geez Mabovu. Redio zina deni kubwa kwa Geez Mabovu. Bahati mbaya deni hilo haliwezi kulipwa sasa. “Tulipofanya hii ngoma kwa Majani nikamwambia ‘Geez hii ngoma kali’ lakini mimi ndiye niliyekuwa namcheck sababu nilikuwa naiona ile ngoma,” amesema Joh Makini.

“Nilikuwa nahisi kuna matatizo yanamsumbua au labda ni life au stress whatever. Nilikuwa nikiuangalia huo muziki niliofanya na yeye na nikiulinganisha na muziki wa hip hop uliopo kwenye mainstream, nilikuwa naona muziki mkubwa sana ndio maana nilikuwa namuambia niachie huu muziki uwe wangu ili niupush wewe uwe kama umeshirikishwa.”

Haisadii tena kucheza nyimbo zake sasa hivi labda kama lengo ni kumuenzi, lakini si kwa kumsaidia yeye kuishi. Geez hatuko naye tena. Geez hahitaji tena show.

Redio hazikitakiwi kukumbuka kucheza nyimbo za wasanii wenye vipaji kama hawa wakifariki, haiwasaidii, inawaletea huzuni tu ndugu na mashabiki wake.
Sikumbuki ni lini katika miaka mitano iliyopita Geez Mabovu alitajwa kutumbuiza kwenye show yoyote kubwa. Mtu kama huyu ambaye anatagemea muziki anaishi vipi? Roma aliandika jambo la msingi na lenye ukweli kuwa hakuna watu wenye stress kama wasanii.

Kuna vipaji vingi vinapuuzwa sasa. Tunasubiri vipotee kabisa ndio tuanze kucheza nyimbo zao? “Wasanii kama Geez Mabovu tunao wengi sana hapa ‪Tanzania lakini hatujifunzi kwa mifano,” anasema Roma.

“Kuna vipaji havipaswi kupuuziwa hata kidogo jamani vipeni support, hundred please. Hatatokea msanii kama ‪ Afande Sele‬, mi nakwambia hadi leo ni mkali sana huyu mtu. Hakuna rapper‬ kama ‪Jos Mtambo‬ asikwambie mtu. Yule ‎Enika‬ yule ni anaimba jamani acha tu. Hawa vijana wa ‪‎Tamaduni Music‬ ni new ‪‎faces‬ zinazokuja vizuri sana wapewe ‪‎support ‎Joslin‬, MB Dog, hawa watu ni ‪Almasi‬ jamani. Tuna wasanii wakali kibao mi nakwambia ‪‎Dojo na Kaya ni ‎ny**o. Wataimba wote ila mtu kama ‪ Rama Dee‬ ni hadithi nyingine ujue,” anasisitiza.

“Wito wangu tafadhali tuwasapoti na tuzidi kuwasapoti vijana wetu wenye vipaji,” Roma anatoa ushauri. “Najua wapo wenye matatizo lakini tusiikate tamaa tuzidi kuwaonyesha njia bora ya mafanikio.”

Nilizungumza na Joh Makini ambaye ameshawahi kufanya ngoma zaidi ya tatu na Geez Mabovu na wana historia ndefu naye. Joh anaamini kuwa hakitatokea kizazi cha muziki wa hip hop bora kama chao na hivyo kukipuuza ni kosa kubwa. “Hofu yangu ni kwamba industry ya hiphop itachukua muda sana kupata generation kama hii. Na pengine inaweza isitokee tena,” anasema Joh.

“Hicho kipaji cha Geez Mabovu, Ngwair, Langa, Joh Makini, Nako 2 Nako, Fid Q, Mapacha, sidhani katika miaka miwili ijayo tutakuwa na kizazi kama hicho. Tukiwa nacho pia tutakuwa tumebarikiwa,” anasisitiza rapper huyo ambaye yeye na wenzake Weusi waliamua kuahirisha show yao ya Mbeya wiki hii kwa heshima ya Geez.

Ngwair, Langa na Geez Mabovu wamefariki katika kipindi ambacho vyombo vya habari vilikuwa vimewapa mgongo. Kosa hili litaendelea kutokea kama tutashindwa kuvienzi vipaji vilivyopo sasa.

Badala ya kuanza kulaumiana katika kipindi ambacho maji yameshamwagika na hatuwezi tena kuyazoa, tujifunze kutokana na makosa na tuvipe nafasi vipaji vinavyostahili kupewa.

Credits:BONGO5.com

Moja ya Sababu za Wanawake Kudundwa na Wanaume Wao

$
0
0
Jana jioni nilipotoka kazini nikapitiliza nyumbani, nipo na mchumba wangu kama mwezi hapa alikuja kunitembelea. 

Nilipofika nikamkuta anaangalia tamthilia, nikavua nguo nikaenda kuoga.

Ukweli njaa ilikuwa imenibana kishenzi.

Nilivyotoka bafuni nikaambiwa, baby leo zamu yako kupika, nikadhani nimesikia vibaya, nikamuuliza tena na kupewa jibu lile lile. 

Nikavaa nguo nikaenda zangu pub nikaagiza chakula nikala(sio kwamba kupika siwezi ila kupangiwa ratiba).
Nilivyorudi nyumbani nikapitiliza moja kwa moja kulala. 

Baada ya muda akaanza kunifokea na kuniambia nilikuwa kwa malaya wangu na nimekula huko.

Nilipatwa na hasira nikamtandika vibao. Asubuhi tumeamka ananiambia anataka kuondoka, nikampa nauli na kumtakia safari njema. 

Nikamwambia ‘umepoteza maksi zaidi ya nusu'.
Mpaka sasa hajaondoka na anaomba tuyamalize.

Wadada, hata kama umesoma kiasi gani mambo ya haki sawa na kupangiana ratiba hayapo dunia hii. Nitapika siku nikijisikia na sio uanze kunipangia ratiba ya kupika.

Ugomvi mwingine mnautafuta bila sababu za msingi. 

Bora hata angeniambia naomba tusaidiane kupika leo.
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images