Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Lady Jay Dee 'Niacheni Niishi Maisha yangu Bila Stresi, Mimi Sio Yesu au Bikira Maria

$
0
0
Wakati kukiwa na maneno mengi juu ya madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na mtangazaji  maarufu Bongo wa Redio E-FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’, supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee amefunguka kuwa naye si mkamilifu kwani siyo Yesu wala Bikira Maria. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wikiendi iliyopita Jide aliamua kuvunja ukimya kufuatia maswali ya mashabiki wake lukuki waliotaka afunguke kinachoendelea katika maisha yake. “Watu wanategemea niwe kama Yesu au Bikira Maria? Siwezi, mimi ni mwanadamu tu. Hakuna aliye mkamilifu. Niacheni niishi maisha yangu bila stresi. Mwingine yeyote pia aishi maisha yake. Kila mmoja anatakiwa awe huru,” aliandika Jide.

Msanii Linex Katapeliwa Sh.11 millions, Steve Nyerere Ahusishwa kwa Utapeli

$
0
0
Linex msanii wa bongo fleva anaetamba kwa sasa na wimbo wa wema kwa ubaya amedai kutapeliwa shiling 11 milion na jamaa ambaye anaitwa Minyamihela ambaye Steve Nyerere alimuunganisha na Linex na huyo Minyamihela ili aweze kumnunulia gari.

Baada ya kupewa gar Linex alilitumia kwa muda wa siku mbili ndipo huyo Minyamihela kuja kulichukua akimuahid atampatia gari jingine, lakini toka huo mwezi wa kwanza hadi leo Linex hajapewa gari lake na wala jamaa(Minyamihela) hajarudisha hizo pesa na kibaya zaidi jamaa hapokei simu ya Linex. 

Linex anaomba ushauri afanyaje?

Joyce Kiria Amwagia Sifa Mumewe Asema Anafaa Kuwa Mbunge wa Mwanga 2015

$
0
0
'Siku zote Taifa lolote lile linaanzia kwenye ngazi ya Familia... Baba au Mama ndani ya Familia akiwa anawajibika vyema kwa Familia yake ni wazi kwamba Familia husika itakuwa na furaha na Amani pamoja na Maendeleo yenye tija kwa wanafamilia... kadhalika watu hao wakipewa jukumu la kuongoza jamii ni wazi kwamba jamii itafaidika na ule uwajibikaji wao kwa kupata huduma bora na kwa wakati.....

Kwa sababu hiyo na mtazamo huo, Mume wangu Henry Kilewo ni Mume na baba bora katika Familia yetu, anatekeleza majukumu yake kama baba na kama Mume vizuri kabisa... ninaimani wananchi wa Mwanga mkimchagua 2015 kuwa Mbunge wenu hakika hamtajuta....

Kwa sasa yupo jimboni kwake Mwanga katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa... anaamini katika kuweka msingi mzuri, yaani timu atakayokuja kushirikiana nayo wakati ukifika, ili ile kazi ya kuwaletea Maendeleo Wana Mwanga iwe rahisi zaidi... Nami ninamuunga mkono Mume wangu kipenzi katika Ndoto yake hiyo ya kuongoza Jimbo la Mwanga kuanzia 2015... All the best my Love Henry...' Joyce Kiria

Tickets za The All White Party Zinapatikana Sehemu Hizi

$
0
0
Kiingilio ni VIP Tsh. 20,000 na 10,000 Tikets kuanzia leo zinapatikana at:- ..........1. Samaki Samaki Mliman City 2. Samaki Samaki Mjini 3. City Sports Lounge Mjini 4. Clouds Media Mikochen.....VIP tikets zipo chache so wahi.mapema please!.....kuingia ni kwa Tikets tu please usije kuniulizia Mlangoni....kama unanijua sana nitafute sasa kabla.ya Jumamosi lakini PLEASE USIJE KUNITAFUTA MLANGONI......DRESS CODE:- White + Gold + Light Blue......usiku wa kiama U know I loooove it!-Lemutuz

Pombe si Chai, Binti wa Kiarabu Amwaga Radhi Hadharani.. Midume Yatoka Udenda

$
0
0
POMBE si chai! Binti mrembo mwenye asili ya Kiarabu ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akifanya vioja baada ya kulewa chakari na kusababisha midume kumtolea udenda, Ijumaa Wikienda lilimpiga chabo.

Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye onesho la Kundi la Mashauzi Classic ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo lilikuwa likitambulisha albam yake mpya ya Sura Surambi, Sura Siyo Roho.

Awali binti huyo alionekana ukumbini humo akiwa mpole na mwenye sura ya soni huku akipata kilaji polepole kabla ya kumkolea na kuwa staa wa kubinuka kihasarahasara na kumwaga ‘lazi’ mbele ya kadamnasi huku akiacha sehemu ya maungo yake nyeti kweupe.

“Jamani pombe mwanaharamu. Muone yule binti wa Kiarabu, kaja mpole lakini hebu ona vituko utadhani kuna skruu imefunguka kichwani,” alisema mmoja wa mashuhuda.Katika hali iliyoonekana kuzidi kuelemewa na kilaji, binti huyo alianza kuwavaa wanamuziki stejini na kuwakumbatia kisha kuinua mguu na kurusha mateke ya kinyumenyume kama mwanasoka, Cristino Ronaldo wa Real Madrid.

Vioja vya binti huyo havikuishia hapo kwani aliwavaa wanaume na kuwakatikia vilivyo.
Wakati tukio hilo likiendelea, jamaa mmoja alimfuata akidai ni mkewe ambapo alimfokea mwanahabari wetu akimtisha kwamba endapo akiziona picha gazetini atamfanya lolote akafie jela Segerea.

GPL

Imegundulika Kumbe Mastaa wa Kike Bongo Hujiuza Kupitia Mitandao ya Kijamii

$
0
0
MWANADADA mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameibuka na kueleza kwamba mastaa wamegundua njia mpya ya kujiuza ambayo ni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akistorisha na gazeti hili, Aunt Lulu alisema mastaa wengi wa kike wanajiuza kwenye mitandao ambapo mapedeshee waliopo mikoa mbalimbali wakishaziona picha zao huwa wanawatafuta kwa udi na uvumba ambapo wanawapigia simu na kuwatumia fedha na tiketi za ndege ya kwenda na kurudi.

“Yaani mastaa wa kike hatulali unakuta pedeshee anakutumia tiketi ya ndege unamfuata mkoani ukienda usiku asubuhi umesharudi Dar unaendelea na mambo yako ndiyo maana unawaona wasanii wengi wa kike wana fedha lakini kazi wanazozifanya huzioni,” alisema Aunt Lulu.
GPL

Wema Sepetu Akubali Matokeo ya Kuachana na Diamond..Soma Ujumbe Alioandika

$
0
0
This is what she wrote on her instagram page:

'Wen one door closes, dont stress..!, dont think...!God has another one with a Brighter and Nicer future jus around da corner waiting for u to Open IT...!!! Take it from ME...!!!'

Mabibi na Mabwana ile Single Mpya ya Vanessa Mdee na Barnaba Ndio Hii Imetoka

$
0
0
Kwanza watu walianza kuitamani baada ya mfululizo wa picha kuendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na imeingia kwenye Top10 ya cover za single mpya Tanzania zilizoongelewa sana.
Barnaba na Vanessa ni marafiki wa muda mrefu lakini hawajawahi kusikika kwenye single moja, ibonyeze brand new hapa chini alafu usiache kutoa maoni yako.

Unapomkamata Mpenzi wako na Mchepuko Nani wa Kum-Face?

$
0
0
Inapotokea umemkamata mpenzi wako na mchepuko live nani wa kum-face kati ya mchepuko na mpenzi wako?

Mara nyingi naona asilimia kubwa ya wengi huwa wana attack mchepuko wakisahau mchepukaji ni jitu zima na akili zake ambalo halijawekewa risasi kichwani na kulazimishwa lichepuke.

Nini maoni yako?

Wapinzani Wamsulubu Mwakyembe Bungeni

$
0
0
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) bila kufuata taratibu.

Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake na Shirika la Reli Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.

Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji na Uwezeshaji, Pauline Gekul alitoa madai hayo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).

Gekul alisema taratibu hazikufuatwa kwa kuwa haieleweki ni lini Serikali, wakala au Wizara ya Uchukuzi ilitangaza zabuni ya mradi wa treni kutoka Stesheni hadi Pugu kupitia JNIA.

“Pia haijulikani ni lini Serikali ilifanya upembuzi yakinifu kuhusu mradi huo wa reli kwa kufuata taratibu kama zinavyoainishwa na Sheria ya PPP ya mwaka 2010 ambayo inafanyiwa marekebisho hivi sasa,” alisema Gekul na kuongeza: “Haijulikani ni kampuni ngapi ambazo ziliomba tenda ya ukandarasi wa treni na kwamba M/s Shumoja ilishinda tenda hiyo kwa vigezo gani.”

Alisema kwa kifupi ni wazi kuwa Dk Mwakyembe na wizara yake walikiuka vifungu vya Sheria ya PPP. Alivitaja vifungu hivyo kuwa ni 4(1) na (2) vinavyomtaka waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.

Rita Sasa Yampeleka Polisi ‘Miss Tanzania’

$
0
0
Kashfa ya aliyekuwa Miss Tanzania, Sitti Mtemvu imechukua sura mpya baada ya Wakala wa Uzazi, Vifo na Ufilisi (Rita) kusema kuwa wamekamilisha upekuzi wa taarifa alizotumia kuombea cheti cha kuzaliwa na vielelezo hivyo vimelekwa polisi vikafanyiwe kazi.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, Ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja masoko na mawasiliano, Josephat Kimaro walisema upekuzi wa nyaraka zilizotumiwa na Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari umekamilika.

“Kazi yetu (Rita) tumeimaliza na upekuzi wa taarifa za Sitti umekamilika na kinachofuata sasa ni kupeleka nyaraka hizo kwenye mamlaka inayohusika ambayo ni polisi, wao ndio wataamua nini cha kufanya,” alisema Kimaro.

Alisema Rita haiwezi kumhukumu moja kwa moja mrembo huyo kuwa alighushi nyaraka na kudanganya ili apate cheti hicho cha kuzaliwa kilichotolewa na Rita Septemba na badala yake wanapeleka vielelezo walivyonavyo polisi ili nao wavifanyie kazi.

“Sisi (Rita) jukumu letu lilikuwa ni upekuzi wa nyaraka, kazi ambayo imefanywa kwa ustadi mkubwa na jopo la wanasheria wetu na hadi sasa imekamilika na kinachofuata ni kuzipeleka nyaraka hizo polisi ambao wao ndiyo wenye jukumu la uchunguzi na kumchukulia hatua Sitti au la,” alisema.

Wakati huohuo, Saliboko akieleza kuwa bado wana changamoto ya baadhi ya watu kudanganya taarifa zao ili wapate vyeti vya kuzaliwa na kusisitiza kuwa wanaandaa mfumo maalumu ili kukomesha udanganyifu huo.

“Tukibaini mtu ametumia udanganyifu ili kupata cheti, kwanza huwa tunamfutia cheti chake na taratibu nyingine za kisheria zinafuata. Tunafanya hivyo kwa watu wote wanaokuja kuomba vyeti kwetu na siyo kwa Miss Tanzania peke yake japo hili la Sitti tunaiachia mamlaka husika ifanye kazi yake,” alisema.

Sitti Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya umri wake na nyaraka zake mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri ambao umepitiliza ule unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania, huku cheti chake kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika kuvua taji hilo.

Wakamatwa kwa Kumvua Nguo mwanamke Hadharani Kenya

$
0
0
Polisi mjini Nairobi wamewakamata watu 100 katika msako baada ya mwanamke mwingine kuvuliwa nguo katika mtaa wa mabanda wa Kayole mjini Nairobi.
Inadaiwa mwanamke huyo alikuwa amevalia nguo zisizo za heshima.
Naibu kamanda wa polisi mjini Nairobi Moses Ombati, amaenukuliwa akisema wengi wa waliokamatwa walikuwa wanaume walevi.
Bwana Ombati aliongeza kusema kwamba, mwanamke huyo alishambuliwa katika mtaa wa Kayole Jumatatu jioni na kwamba polisi wanaendelea na msako.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake waliandamana katika barabara za katikati mwa mji kulaani kitendo cha kumvua nguo mwanamke mwingine mapema mwezi huu mjini Nairobi.
Wanawake hao waliandamana kufuatia wito kwenye mitandao ya kijamii chini ya kauli mbiu #MyDressMyChoice yaani vazi langu uamuzi wangu au nitavaa nitakachojiamulia mwenyewe.
Waandamanaji hao wakiwemo wanawake mashuhuri, wanasiasa na wanaharakati waliandamana hadi katika kituo cha mabasi ambako mwanamke wa kwanza alidaiwa kuvuliwa mavazi yake kwa madai alikuwa amevalia 'Mini Skirt'

Makubwa..Kama una Macho Mazima Embu Niambie nini Kinaendelea Hapo Katika Hii Picha

$
0
0
Makubwa..Kama una Macho Mazima Embu Niambie nini Kinaendelea Hapo Katika Hii Picha
Wengi Najua Mtakosa..Hahaha

Kinachoendelea Kuhusu Kesi ya Mauaji ya Mwigizaji Lulu Michael

$
0
0
Stori: Musa Mateja
KESI ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi za mauaji mahakamani, Risasi Mchanganyiko limetonywa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa tena Februari mwakani kutokana na mlolongo mkubwa wa kesi za mauaji zilizopo Mahakama Kuu ya Tanzania.

Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya kamati ya majaji wanaoshughulikia kesi hiyo, kimenyetisha kuwa kesi ya Lulu itakuwa ngumu kusikilizwa wakati huu kwani mbali na wingi wa kesi mahakamani hapo, lakini pia majaji na mawakili watakwenda likizo.

“Ujue kesi ya Lulu ilikuwa miongoni mwa ambazo zingesomwa kabla ya mwaka huu kuisha, ila kulingana na vikao vya majaji inaonyesha wazi kabisa mwaka huu itakuwa ngumu hata Januari haitawezekana kwani wana kesi kama tatu za mauaji na baada ya hapo watakwenda likizo sambamba na mawakili kwani nao ndiyo kipindi chao cha likizo,” kilisema chanzo chetu.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, Aprili 7, 2012  maeneo ya Vatican-Sinza jijini Dar.Kifo cha Kanumba kilichotokea nyumbani kwake, kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
GPL

Ali Kiba Kumbuka Majivuno na Maringo Ndivyo Vilivyokupoteza

$
0
0
Kwako
staa uliyerudi kivingine na wimbo wa Mwana, Ali Kiba. Vipi uko poa? Bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na harakati zako za kimuziki.Ukitaka kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya namshukuru Mungu maisha yanasonga. Naendelea na majukumu ya kila siku likiwemo hili la kukuandikia barua.

Pasipo kupepesa macho, pamoja na salamu, dhumuni la kukuandikia barua hii ni kwamba kuna kitu kimenigusa nataka kukukumbusha maana akili ya mwanadamu siku zote imeumbwa kusahau.

Ni rahisi sana mtu kula msoto mkubwa lakini ndani ya dakika chache tu pale unapopata mafanikio, unasahau.Nakumbuka kabla ya kuachia nyimbo za Kimasomaso na Mwana ambazo zinaendelea kufanya vizuri hadi sasa, ulikuwa kimya. Najua unaweza usikubaliane na mimi lakini ukimya ule ulitokana na kujisahau baada ya kuwa na mafanikio makubwa.

Kipindi kile ulifanikiwa kuiteka Bongo, kila mmoja alikuwa akikutambua wewe kama namba moja hususan pale ulipofanikiwa kuwa msanii pekee kutoka Tanzania na kwenda kufanya kolabo maalum iliyoandaliwa na legendary wa muziki kutoka Marekani, R. Kelly.

Kiba ulikuwa Kiba kweli. Kipindi hicho ukitaja Diamond, kila mtu anakuuliza ndiyo nani. Hakuna aliyemjua. Kila mmoja alikujua wewe kwamba ndiyo kioo cha Tanzania katika anga za kimataifa, uwezo wako uliheshimika.
Hapo ndipo zilipoanza pozi, majivuno kama siyo maringo. Ukawa unapanga bei yoyote ya shoo hata ya kukomoa ili mradi anayeandaa shoo ashindwe kufanya kazi na wewe.

Pia hapo ndipo ulipokuwa ukitoa ushirikiano hafifu kwa mashabiki wako kwa kujitenga na vyombo vya habari.Ulijisahau ukaona jina ulilolitengeneza linaweza kuendelea kuwepo hata kama usipozungumza lolote kwa mashabiki wako kupitia vyombo vya habari.

Hata hao waandishi waliokuwa wakitaka kufanya mahojiano na wewe kwa faida yako nao ulikuwa ukiwaletea pozi.Mashabiki wakaanza kukumiss katika kazi zako. Wakawa wanakosa habari zako mpya kiasi cha kukuweka kando na kumpa sapoti bwa’mdogo ambaye sasa anakimbiza kinoma, Nasibu Abdul ‘Diamond’ (wakati huo wewe ulimuona wa kawaida sana).

Kaugonjwa ka kujisahau naona tayari kameanza kukunyemelea. Nimetonywa kwamba umeanza tena. Pozi zimeanza, ‘vurugu’ za vyombo vya habari zimeanza kukata.Nahisi zile shoo kadhaa ulizopiga zimeanza kukusahaulisha hata ile mipango yako ya kutoa video za nyimbo zako mpya tena sizisikii. Nikwambie tu, ulipata bahati Watanzania walikupokea kwa mara nyingine maana ipo mifano ya wasanii wengi waliowika wakapotea lakini kila walipotaka kurudi walichemka.

Itumie fursa ya kurudi na kukubalika upya kama fundisho kwako, usikubali kukaa mbali na mashabiki wako. Wape kazi mpya, wape habari zako kila siku ili waendelee kukupa sapoti wasije wakakusahau ukarudi kule ulikokuwa.Kwa leo ni hayo tu, asante kwa kunisoma.

Wasalaam
Erick Evarist

Chameleone 'Diamond ni Msanii Mchanga Siwezi Kamwe Kumuomba Collabo'

$
0
0
Chameleone amesema kuwa application ya Mziiki ambayo Diamond ni balozi wake wa Tanzania ipo kwenye mazungumzo naye ili kumfanya balozi wake wa Uganda na hivyo ilimuomba afanye wimbo na Diamond kama anthem ya Afrika Mashariki.“Lakini we talked about business na hatujamalizana nao. Lakini sio eti mimi nimempigia (Diamond) kumuomba tufanye collabo na kitu kama hicho,” amesema Chameleone. “Wale wa Mziiki app ndo wanahitaji mimi na yeye tufanye kazi ya anthem ya Mziiki app. Wanajaribu kuunganisha yeye na mimi tufanye collaboration lakini sio eti mimi nimemu whatsapp na nimemuomba collaboration , that’s not right,” amesisitiza hitmaker huyo wa Valu Valu.

Am not at a level of asking for a collaboration from any artist in that manner. Sio kwamba sina heshima yake (Diamond) au kitu kama hicho lakini that’s not the truth, haiwezi kuwa hivyo. I have been doing music for the past 14 years, right? So I am not an upcoming artist.

Hali yazidi Kuwa Tete Escrow, Hapatoshi Dodoma

$
0
0
IKIWA ni siku chache tu baada ya kutolewa kwa taarifa za kukabidhiwa kwa ripoti ya ukaguzi wa akaunti ya ESCROW, uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), kwa spika na kamati ya mahesabu ya serikali PAC, mengi yameibuka.


Hali hiyo inatokana na kuwepo kwa mgawanyiko wa wabunge kuhusu na jambo hilo huku kila upande ukiwa na mtazamo wake tofauti juu ya jambo hilo, ambalo wabunge wengi wanaamini linapikwa na halizungumzwi ukweli.


Taarifa kutoka Dodoma zinasema kwamba wabunge wengi wameshitushwa na kuvuja kwa taarifa kuwa kamati ya PAC imelivalia njuga suala hilo, baada ya kushindwana kuafikiana mgao wa malipo kutoka kwa wamiliki wa kampuni ya IPTL/PAP ili kulizuia kulimaliza katika Kamati lisifike bungeni mapema mwaka huu.


Taarifa hizo zinasema kamati ya PAC iliwatumia mwanasheria aliyefahamika kwa jina la Albert Msando ambaye ni msaidizi wa kisheria wa Zitto Kabwe na Beatus Malima kujadili juu ya malipo watakayolipwa PAC ili kuidhibiti ripoti hiyo na namna ambavyo PAC ingetoa hukumu ya awali.

Vithibitisho ambavyo baadhi ya waandishi wameonyeshwa na baadhi ya wabunge hao, vinaonyesha mijadala iliyokuwa ikiendelea bungeni kuwa mingi ni ya kupikwa na ya kimkakati inayotokana na hasira za kutokupatiwa malipo waliyoomba PAP na hivyo kulitaka bunge lipigie mhuri kitu ambacho ni mgogoro unaotawali na maslahi binafsi.


Haijafahamika mara moja kwamba ni kiasi gani kimeombwa na kamati ya PAC kwa PAP ili walifunge jambo hilo, mlakini baadhi ya wabunge hao wamesema wapo tayari kuweka wazi kila kitu ili kila mtu avune alichopanda.


‘’Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda, kama wanataka kutugeuza wabunge wote ni ‘Rubber stamp’ tuhalalishe hukumu inayotokana na hasira zao za kunyimwa mgao, basi wamegonga mwamba’’. 
Alisema mmoja wa wabunge hao anayetokea chama kimoja cha upinzani akijibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe aliyenukuliwa na gazeti moja hivi karibuni.


Hivi karibuni Filikunjombe, alisema katika gazeti hilo, kwamba kila mtu atavuna alichopanda katika sakata hilo, baada ya kupokea ripoti ya CAG kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai.

Akizungumza kwa kujiamini, mbunge mwingine ambaye pia ameomba ahifadhiwe jina lake kwa sasa anasema ’’Hata Kamati yenyewe ya PAC imegawanyika vipande vipande, wakubwa wao wamevuta mzigo wa kutosha na wenzao wanawaburuza, halafu kazi nzima ya kamati inapelekeshwa kutoa sifa kwa watu wawili tu ambao ni Zitto na Filikunjombe, huu ni upuuzi’’.


Mbunge huyo alisema sisi sote ni wanasiasa, unafikiri nani atakuwa tayari kufanya kazi, halafu sifa ziwaendee watu wawili tu kwamba wao ndio wanaakili sana na wana uchungu sana na nchi.
‘’Hebu jiulize kamati ina wajumbe zaidi ya 20 lakini kila kitu zitto na deo wanajiweka kimbelembele, sasa na safari hii wanapoumbuliwa kwa madili yao ya rushwa wakae kimbelembele hivyo hivyo’’. Alisema mbunge huyo.


Hata hivyo, taarifa kutoka kwenye ripoti iliyovuja ya CAG haionyeshi kwamba kuna tatizo kwenye ukaguzi walioufanya wa akaunti ya ESCROW, badala yake umeibua madai mapya ambayo sio msingi wa uchunguzi walioagizwa kufanya.


Itakakumbukwa kwamba akaunti ya ESCROW ilifunguliwa rasmi Julai, 5 2006, wakati ripoti ya CAG inaonyesha mapungufu ya kuanzia Januar 2002 mpaka Desemba 2006 huku ripoti yenyewe ilipaswa kujikita kati ya 2006 mpaka 2013 ilipofungwa.


‘’Hatupaswi kuwaadhibu watu kwa sababu tu tunawachukia, au kwa sababu tunachuki na tofauti nao binafsi ama za kisiasa, sisi kama bunge ni lazima tufanye kazi zetu kwa kudhibiti hisia zetu, wanachokifanya kina Zitto, David Kafulila na Deo, ni chuki binafsi na si uzalendo kama wanavyotaka iwe, kama ni wazalendo wasingefanya kama haya wanayofanya’’. alisema mbunge huyo.


Alisema mbunge huyo, wabunge hao baada ya kuona ripoti ya CAG haiwatii hatiani serikali na wanaowachukia wao, wanalazimisha kusema kuwa kuna hasara ya bilioni 321. Waache kuwafanya wabunge watoto wadogo kwa kuwa kila kitu tunakijua.


Wakati hayo yakiendelea, jana asubuhi Mbunge wa Mtera-CCM, Livingstone Lusinde aliiomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job Ndugai kuhusiana na kubana kwa ratiba katika suala la akaunti ya ESCROW huku jambo hilo likiwa na hamasa kubwa kwa watanzania.
“Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Kamati ya Uongozi ya Bunge iongeze siku au muda katika kujadili suala hili, kwa kuwa ni jambo kubwa linalohitaji kujadiliwa zaidi, tuna mengi tunayoyajua, makando kando ya wanaotuhumiwa na wanaotuhumu pia, kwa kuwa waswahili wana msemo mmoja ukimuona anayelia sana ujue ndio mchawi mwenyewe,’’alisema.


Alisema wabunge wanaolia sana kuhusiana na jambo hilo, wenyewe wana makando makando katika suala hilo kutokana na kuhusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo, ambalo anaamini kujadiliwa kwa muda mrefu zaidi ndio jambo litakaloweka haki kwa kila mtu.
Hivyo, aliiomba Bunge iongeze siku zaidi kujaidli suala hilo, ambapo Naibu Spika Ndugai alisema atawasiliana na Kamati ya Uongozi ya bunge kuhusiana na mwongozo huo wa Lusinde ili ufanyiwe kazi kwa kuwa jambo hilo lina umuhimu mkubwa kwa taifa.

Moja ya Sababu ya Kenya kuwa Juu ya Tanzania Kiuchumi

$
0
0
Leo katika taarifa ya habari saa 1 jioni ya kituo cha televisheni cha K24 cha Kenya imeonesha mchakato wa usajili na uandikaji namba mpya za magari nchini humo, uandishi wa vibao vya namba za magari unaofanywa na wafungwa wa gereza nchini humo.

Uandishi wa vibao vya namba za magari ni mradi endelevu tena wenye kuingiza fedha nyingi mno. Kwa hapa kwetu,mradi mara ya kwanza ilipewa kampuni binafsi. Inasemekana kampuni hiyo ina ubia na Waziri Mkuu wa zamani,ambaye ni fisadi mjanja sana. Ameificha miradi yake ya kifisadi kwenye majina na makampuni yaliyochini ya watu tofauti tofauti.

Hapa nchini,makampuni yenye kuzaa faida yamechukuliwa na viongozi mafisadi,mfano,makampuni ya mawasiliano yalichotwa hisa za umma kupewa wageni kwa niaba ya mafisadi wazawa walio ndani ya Serekali, angalia TTCL,ATCL, aidha, inasemekana tiGO ilipokuwa chini ya MIC ltd serikali ilikuwa na hisa % 17 ambazo zilichotwa kinamna na spika mmoja wa zamani wa bunge la JMT.

Huko Kenya kampuni ya simu ya umma ndiyo inashikilia na kutamba katika nyanja ya mawasiliano nchini humo.

Kwa mfumo huu, Kenya itendelea kututimulia vumbi.

Sakata la Tegeta Escrow Lilivyoanza Mpaka watu Kuitana Tumbili na Mwizi

$
0
0
Kashfa ya Tegeta Escrow iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.Kuibuliwa kwa kashfa hiyo, kulisababisha Kafulila kuingia kwenye malumbano makali yaliyowafikisha katika kutoleana maneno ya dharau na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni.

Maneno hayo ya dharau yalihusisha Jaji Werema kumwita Kafulila kuwa ni tumbili na Kafulila kumwita Jaji Werema mwizi.Baadhi ya wabunge wamekuwa wakishinikiza wakitaka ripoti hiyo pamoja na ile ya uchunguzi uliofanyw a na Takukuru ziwasilishwe bungeni ili zikajadiliwe na wabunge ili ukweli ujulikane.

Tayari nchi wahisani zimetangaza kuikatia misaada serikali ya zaidi ya Sh. trilioni 1 kutokana na kashfa hiyo.Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa kutokana na kutoelewana kuhusu gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na kampuni ya kufua umeme ya IPTL na kuuzwa Tanesco.

Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID), katika uamuzi wake wa Februari 2014, ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa
kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa uamuzi huo, ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali, lakini badala yake fedha hizo zilitoweka ghafla kwenye akaunti hiyo.

KILICHOMO KATIKA RIPOTI YA CAG
Matokeo ya ukaguzi uliofanywa na CAG kuhusiana na kuchotwa kwa Sh. bilioni 306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yameiweka matatani Ofisi ya Mwananasheria Mkuu wa Serikali (AG), huku yakizitambua fedha hizo kuwa ni za umma.

Vyanzo vyetu mbalimbali vimebainisha kuwa Ofisi ya AG inadaiwa kuingia matatani, baada ya ripoti ya ukaguzi huo iliyovuja, kubaini kwamba, inahusika moja kwa moja katika kuisababishia serikali hasara ya jumla ya Sh. bilioni 321 katika kashfa hiyo.

Pia Wizara ya Nishati na Madini, nayo pia inatajwa na ripoti hiyo kuhusika katika kuisababishia serikali hasara hiyo.

Vilevile, Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) nayo pia imeingia matatani, baada ya kuhusishwa na ripoti hiyo kwa tuhuma za kulikosesha shirika hilo kiasi hicho cha fedha.

Ofisi ya AG inahusishwa na kashfa hiyo, baada ya ripoti hiyo kueleza kuwa ilivunja sheria makusudi kwa kuelekeza kuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye gharama za uendeshaji (capacity charges), ambazo Tanesco walilipishwa na IPTL, isilipwe.

Maelekezo hayo ya ofisi ya AG yanadaiwa kusababisha serikali kupoteza mapato ya Sh. bilioni 21.

Mwanamke Aliye mnyoa Nywele Kwa Kisu Mwanamke Mwenzake Arusha Yamkuta Makubwa..

$
0
0
Haya jamani majibu si mnakumbuka haya dada alimuabisha mwanamke mwenzie hatimae sasa mwanaume huyooo kamchukua kimada chezea wanaume wewe...



Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images