Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Taarifa za Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono Kulishwa Sumu

$
0
0
 Nimrod Mkono amekoswakoswa kuuawa nchini Uingereza alikokuwa amekwenda kikazi. Aliwekewa sumu ambayo ilipaswa iharibu kabisa figo zake ndani ya saa 72. Uongozi wa bunge umethibitisha na ripoti ya madaktari wa London inaonesha hivyo. Mkono mwenyewe anasema alionywa kuwa usalama wake uko mashakani na akatakiwa asifikie katika hoteli ambayo ujumbe wa viongozi wa Tanzania utafikia. Mkono anasema alipofika London aliamua kwenda katika nyumba yake binafsi, lakini baadaye alianza kutoka jasho, kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu kwa saa 6. Ikumbukwe kuwa Mkono na kampuni yake ya Mkono & Advocates ndiyo iliyokuwa inatetea upande wa TANESCO na Serikali katika kesi dhidi ya IPTL. Inasemekana Mkono anatafutwa kuuawa kwa sababu inaonekana ana taarifa nyingi mno kuhusu sakata la IPTL na ESCROW, na serikali inamtuhumu kuwa yeye ndiye aliyevujisha nyaraka zote hadi umma wa watanzania kugundua kuwa zaidi ya bilioni 321 mali ya umma zimeibiwa katika sakata hilo.

Mchumba wa Agness Masogange Aibuka na Kusema Haya Kuhusu Kusalitiwa

$
0
0
STORI: Musa Mateja
MCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ aitwaye Evance Kom juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa msichana huyo amemsaliti baada ya kuvunja makubaliano yao.
Akizungumza na gazeti hili Jumatatu hii, alisema hana tena mpango wa kuoana na Agnes kwani kitendo chake cha kuamua kuhamia Afrika Kusini kimeonyesha wazi hawawezi kuishi tena pamoja.Akisimulia, Evance alisema hapo awali walikubaliana kuwa pamoja kiasi kwamba hadi kufikia kumvalisha pete, wazazi wa pande zote mbili walikwishajua na kubariki uhusiano wao.

“Wakati anapanga mipango yake ya kuhamia Afrika Kusini, hakuwahi kuniambia hata mara moja, alikuja kuniambia eti tuhamie huko siku chache tu kabla hajaondoka, nisingeweza kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya huko wakati hapa Bongo nina miradi yangu kibao,” alisema.

Alisema kutokana na kitendo hicho cha kuhamia huko, pia mchumba wake huyo alikuwa amejiingiza kwenye mambo yasiyofaa ambayo wazazi wake wasingeweza tena kumsapoti kama angehitaji kuendelea na nia yake ya kumuoa.

“Nilimpenda sana Agnes na yeye alinipenda lakini alichokiamua ni kizuri kwake, ila kwangu ni kama amenisaliti maana kajiingiza kwenye mambo yasiyofaa hivyo kwa sasa amebaki kama rafiki yangu wa kawaida tu,” alisema.

Ray: Chuchu Ndio Kila Kitu Kwangu, Johari na Mainda Tupa Kule

$
0
0
Stori: Musa Mateja
LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu.

Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.

“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’.

Kikao Cha Dharula: Kitimoto kwa Wabunge wa CCM Wanaopigia Kelele Escrow

$
0
0
Kikao kinaongozwa na Wasira na Lukuvi, 

Wabunge wa ccm wale wanaopiga kelele kuhusu Wizi huu wamewekwa mtu kati,

Kinafanyikia Ikulu ya Dodoma kwa siri kubwa, hata magari yao yote yameigizwa ndani kabisa, kwa hapa nje lipo Gari la Lembeli aina ya Range Rover Namba T382 lililokosa nafasi ndani. kikao hiki kimeitishwa kwa meseji tu hii ni baada ya jioni kutangazwa kuwa kimeahirishwa,

Sababu za usiri huu ni pale tulipowaanika jana katika kikao chao cha shinikizo kwa Werema ajiuzuru, Zigo limemdondokea Godfrey Zambi kuwa ndie aliyevujisha siri ile kwakuwa aligoma kuzima simu na alikuwa akichati fb wakati kikao kikiendelea, hivyo kikao cha sasa hivi katupwanje.

Kikao hiki kwa sasa kimembana Ndugai kwamadai anaihujumu serikali, 

Ndugai amezila kuendelea na Bunge amesema yeye sasa hata ongoza vikao, bora awe pembeni kuepusha msongamano!

Ccm imegawanyika makundi matatu, lile linaloshinikiza waliohusika na wizi huu wote wapigwe chini lakini,ukifuatilia kundi hili linavizia vyeo vya uwazili, na tayari kampenzi za kuwania vyeo hivyo zimeanza. 

Kundi la pili hili ni wanafiki wa kati wasio na msimamo, lenyewe linataka wafukuzwe wachache (maswi,tibaijuka,mhongo na werema) hili linasema linanusuru serikali isianguke.

Kundi la mwisho ni la wezi wenyewe, hili linafanya kila njia ripoti hii isisomwe bungeni, hili linaongozwa na Pinda na Werema.

UPDATES.22/11/2014

Ndege ya serikali ipo hapa Dodoma imekuja alfajiri hii 5-H CCM.. Aina ya folker F28 haijajulikana imemleta au imekuja kumchukua Nani, ila taarifa za awali zinasema Bilali alikuwa aje leo.

Hali ya mambo ni ngumu kama vile nchi ipo vitani...!

Kinana tayari ameletwa na Ndege mida hii,

Mrejesho wa Kikao Cha jana usiku

Imeamriwa popote alipo Spika Makinda aje, Ndugai out hadi sakata lipite, afanye awezavyo Pinda apone,.. Wachangiaji wakali wasipate nafasi iitwe briefing ya wabunge wote watapike nyongo nje ya waandishi ili siku ya mjadala kuwe na hewa safi.Kama ni kuondoka waondoke mawaziri ila sio waziri mkuu.

Inatakiwa njia ya kumuangukia au kumdhibiti Mh. Mengi wa IPP,

Leo agenda kuhusu Mengi itajadiliwa kwa kina katika kikao cha baadae. Ifahamike kuwa Vyombo vya habari vya Bwana Mengi vimekuwa vinalielezea jambo hili kwa uwazi na uhuru mkubwa kiasi cha umma kulielewa.

Unapoufurahia Ujuzi wa Mpenzi Wako, Hujiulizi Kautoa Wapi?

$
0
0
Kwetu tunaamini mchawi aliyekubuhu, ni yule aliyeuwa watu wengi zaidi. Au hata ukimuona dereva anakimbiza gari barabarani unaamini ana uzoefu wa udereva wa mda mrefu na atakuwa ameshawahi kuendesha magari mbali mbali.
Sasa linapokuja swala la mahusiano, ninaona watu wanalalamika kuhusu ujuzi wa wenzi wao. Ingekuwa mimi, endapo mwenzi wangu angekuwa na kiwango kidogo cha ujuzi kwenye maswala ya chumbani, lingekuwa jambo la furaha na kheri. 
Pale unapotaka mpenzi wako awe na ujuzi wa PhD katika maswala ya chumbani, wewe unataka awe amejifunzia wapi? Kama unataka mjuzi, nenda kachukue Changu doa ambaye anajua michezo yote...
Dada zetu waliofunzwa wakatulia, na kaka zetu au wadogo zetu waliofunzwa wakatulia technically watakuwa na ujuzi mdogo na over the time katika maisha yao ya mahusiano (ndoa) wataweza kujifunza na kuimprove.
Ukimpata yule anayekupeleka puta, inabidi ukae chini na ujiulize atakuwa amewapitia au amepitiwa na wangapi mpaka akapata utaaalam huo?

NB: Sio wote wenye utaalam wa chumbani wanahistoria ndeefu (mbaya) ya kwenye mahusiano...

Maskini Kijana Sande Aliyekuwa na kilo 250, Amefariki Dunia, Mashirika ya ndege Yachangia Kifo Chake

$
0
0
Kijana Sande Mrema aliyekuwa na tatizo la kuwa na kilo nyingi zilizokuwa zikifikia 250 na umri wa miaka 25 aliyekuwa eneo la karakana katika moja ya Hoteli alipokuwa akiishi wakati akisubiri kupatikana kwa Ndege amefariki dunia usiku wa saa nne kuamkia leo jijini Dar es salaam.

Sande amefariki dunia wakati bado taratibu za kuona ni namna gani atakavyoweza kupatiwa ndege kwaajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini india zilikuwa zikifanyika miongoni mwa wanandugu.

Sande Mrema alishindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.

R.I.P Sande.

Hivi Ndivyo Whatsapp Imevunja Ndoa ya Wawili Hawa

$
0
0
Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message aliyomtumia yeye hakuijibu.

Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa miaka miwili tangu ifungwe.

Umeona Video Nzima ya Jinsi Mfanyakazi wa Ndani Anavyomtesa Huyu Mtoto na Kumpa Kipigo

$
0
0
Kama kutakuwa na list ya watu wasio kuwa na huruma hata kidogo ama kwa lugha nyingine tunaweza kusema katili basi bila shaka huyu dada wa kazi kwenye top 10 atashika nafasi ya kwanza…
Hii inawahusu sana wakina mama ambao uwaachia watoto wao Dada wa nyumbani (HOUSE GIRL) pengine kutokana na majukumu ya kikazi au inapotokea safari ya ghafla… hii video itakuonesha tukio zima na tabiwa kama hii wapo baadhi ya Madada wanazo ivyo umakini mkubwa unatakiwa.

Kama Ulipitwa Kuangalia Wema Sepetu 'In My Shoes' Season Two Basi Hii Hapa Nimekuletea

$
0
0
Ule msimu wa pili wa Reality show ya Wema Sepetu In my shoes umeishaanza na hii ndio episode ya kwanza iliyo muhusisha Diamond ndani yake…



Video Hii Hapa:

Mchezaji Adebayor Adai Mamaake ni Mchawi, Amfukuza Nyumbani

$
0
0

Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.

Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.
Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.

Hatimaye Diamond Aongelea Kuhusu Kuachana na Wema na Mahusiano yake na Zari Boss Lady

$
0
0
Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:

Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“

Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“

B 12 :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?...”

Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “

B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“

Diamond :- “… Sijui…“

B 12  :- “...Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“

Diamond : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:

Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…“

Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.


Mwenzangu Embu Angalia Hii Kitu Jinsi Wenye Nchi Wanavyogawana Mabilioni ya Fedha Huku Hospitalini Hakuna Dawa

$
0
0

Picha Hapo Juu ikionyesha Mgawanyo wa Fedha.....

Mwee....Hapana sio kila siku ni jumapili .siku nyingine ni ijumaa wakishindwa tutaingia mtaani kudai haki zetu .pamoja na ukawa tunaweza sio kitu ,ushenzi kama huu unatakiwa ukomeshwe ili tufike tnako taka kwenda watu wachache wanagawana hela ya kusambaza madawa nchi nzima huu ni uonevu wa wanyoge hatukubali..

Hili Sakata la ESKROW ni matata matupu.
1. Ziara ya Jaji Mkuu kwenda kumtembelea Mh. Rais (nini ulikuwa mjadala)?
2. Maamuzi ya kusema Sakata hili lisijadiliwe Bungeni liko Mahakamani... Je linatokana na Ziara?
3. Waziri Mkuu kutaka Busara itumike. Ipi? labda angetoa ufafanuzi...
4. Wabunge kutoridhishwa na mwenendo wa Sakata na na namna Serikali inavyotaka kulifunika funika.
Spika uamuzi wako utaliokoa Taifa au kulididimiza. Ni wazi kabisa ukumbuke hapo ulipo utakachokifanya kitadhihirisha umoja wa uovu au weledi wako kupingana na maovu..

Jokate: Mimi Sio Malaya Jamani

$
0
0
MWANAMITINDO na mtangazaji kiwango Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa sababu kubwa inayomfanya awe karibu zaidi na wanaume ni marafiki zake wa kike kuwa nje ya nchi .

Akizungumza na mwanahabari wetu, Jokate alisema amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuwa kampani yake kubwa ni wanaume hadi wengine kumuona ni malaya wakati si kweli .

“Watu wengi wanasema mimi malaya kwa sababu ya ukaribu wangu na wanaume lakini ukweli ni kwamba kampani yangu ya kike kubwa ipo nje ya nchi , sina jinsi, ” alisema Jokate.

Ukweli Kuhusu Safari ya Jaji Mkuu Washington DC, Maafisa Wake na Francis Nyalali

$
0
0
Tumefanya uchunguzi hapa DSM na huko Washington DC kufuatilia hicho kinachoitwa semina ya majaji
iliyofanyika USA ambayo ilijaza na maafisa wakuu wa mahakama. uchunguzi wetu ulianzia ubalozi wa marekani 
hapa dsm eneo la Drive inn kupata ukweli juu ya semina ya majaji hao lakini ktk kitengo chao cha habari kwa
Bw. MOORE akatuambia hakuna kitu kama hicho kuhusu mualiko wowote unaousiana na semina ya majaji au wanasheria uliopita ubalozi huo.

Tukatoka hapo tukawasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo washington DC kupata maelezo yeyote kuhusiana na semina yeyote ya majaji inayoendelea huko ofisa wa ubalozi alisita kwanza lakini baadaye walituambia kuwa hawawezi kushea information kama hizo na sisi kwahiyo tuwasiliane na wausika. Tukaenda kwenye website ya mahakama kuu ya marekani kuona kama kuna tangazo lolote kuhusu semina hakuna kitu kama hicho tumekuta matukio mengine lakini hakuna issue ya semina. Tumewasiliana na wahusika akiwemo jaji mmojawapo kwy ule msafara simu zao zinaita hazipokelewi.

Conclusion yetu

Kulingana na uchunguzi wetu tumeitimisha kuwa jaji mkuu pamoja na maofisa wa mahakama walikwenda Washington DC kwa ajili ya kitu kimoja tu nacho ni kujadili suala zima la issue ya acount ya Escrow na mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuhusiana na uwepo wa semina unless watoe picha zinazoonesha semina hiyo ambayo wahusika walidai walikwenda kuhudhuria na siyo kuonana na JK.

Swali kubwa ambalo inabidi watanzania tujiulize hivi ni kweli mahakama zetu ni huru ?? kwa mujibu wa uchunguzi wetu ni kuna muingiliano wa hali ya juu kati ya mahakama na executive kwa maana ya ikulu. Tunajiuliza kama jaji
mkuu na maofisa wa ngazi ya juu wa mahakama wanaweza kufunga safari kwenda kuonana na Rais kwa ajili kujaribu kupotosha nchi na kulinda mafisadi. Je Rais anapokuwa nyumbani ni mara ngapi jaji mkuu na maofisa wake wanakwenda ikulu kujadili na mkuu wa nchi kuhusu mienendo ya kesi mbali mbali na maswala ya ushahidi?? 

Hii inatupelekea kuamini kabisa maneno aliyoongea aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania Francis Nyalali kuwa mahakama za Tanzania si huru na zitakuwa huru tu endapo ikulu itakapoacha kuitisha na kuyajadili mafaili ya watuhumiwa ikulu.

Kitendo cha ofisa wa ngazi ya juu wa ikulu Bw.Ombeni Sefue cha kutoa tamko la kutojadiliwa issue ya ESCROW bungeni na kujigeuza messenger wa mahakama na kulitishia bunge kuwa linaingilia amri ya mahakama ni kosa la wazi na linathibitisha jinsi ikulu inapoingilia wazi uhuru siyo wa bunge bali na mahakama zetu.

By  Politiki/Jamii Forums

Ripoti ya CAG Yavuja, Baadhi ya Kurasa Zinazodaiwa Kuchomolewa Zawekwa Wazi

$
0
0
Ripoti ya CAG YavujaBaadhi ya kurasa zinazodaiwa kuchomolewa zawekwa wazi na ripoti nzima yadaiwa itawekwa hewani endapo kutatokea kuchakachua

Kimsingi, ripoti nzima ipo na itawekwa hewani endapo michezo inayochezwa itaendelea!

Nimesikitishwa na taarifa za kuanza kunyofolewa kurasa za ripoti hii; bahati nzuri kuna watu wanayo original copy na imeshasambaa sana hivyo ni vema wahusika wakaacha wabunge waifanye kazi yao kwa kadiri inavyostahili.

Hatungependa kuingilia sana lakini tunaona kama tunalazimishwa kufanya hivyo.

DOKEZO:

Hizi chini ni baadhi ya kurasa zinazodaiwa kunyofolewa...


Source:Jamii Forums

Maneno ya Meneja wa Wema Sepetu Kadinda Kuhusu Kumwachanisha na Diamond na Wema

$
0
0
Kama macho yako hayakosi Magazeti ya kila siku au kusoma mitandao mbalimbali ni lazima utakua umekutana na stori kwamba Wema Sepetu na Diamond Platnumz wameachana.
Diamond Platnumz alihojiwa kwenye XXL ya CloudsFM November 21 2014 lakini hakuweka wazi kabisa nini kinaendelea lakini maelezo yake yanaweza yakawa na ishara ya jibu linakoelekea.

Moja kati ya alivyovisema ni kwamba hata yeye alishangaa kuhusu ile zawadi ya gari aina ya BMW aliyozawadiwa Wema kwenye birthday yake huku meneja wake Martin akikaririwa na vyombo vya habari kwamba ni marafiki walijichanga kumnunulia Wema.

Baada ya hayo kuna baadhi ya stori zimekua zikitambaa kwamba Martin Kadinda ndio amehusika kuwaachanisha Diamond na Wema Sepetu ambapo aliamua kujibu kwa kuandika hivi kwenye instagram >>> ‘Siwezagi kujibizana.. Ila i gat people who can do that…. Namleta kwenu bingwa wa kutusi watu… Mimi nimemwachanisha wema na chibu ahahahahahaa ahahhahahaha ahahahahaha walaaahi naona raha.. We Nasri that powerful couple ambayo haijawahi kutokea tz na haitakuja kutokea iachanishwe na mimi fundi makoti?? Team kadinda mpeni what he deserve…..’




Sakata la Mtoto Aliye Teswa na House Girl, Waajiri Tujifunze Kitu Muhimu Hapa

$
0
0
Dah kwa alieoona clip hii ataamini kuwa baadhi ya wanawake wana roho za kikatili. Na sijui huyo msichana ningemfanya nn katika nafasi ya yule baba. Maana.. Na vile naskia habari tofauti wengine wanasema mtoto ameshaaga dunia , wengine wanasema yupo mahututi amepata tatizo la uti wa mgongo. Mungu asimame tu!

Yote sawa, hiki sio kigezo cha kunyanyasa wafanyakazi kwa sababu sio wote wenye roho katili hivi. Wengine wanaanza ukatili baada ya kukatiliwa na mabosi wao. Kuishi vizuri na hawa watu ni muhimu sana. Wao pia ni binadamu.
Ila pia haya ndio maisha ya watoto wengi wanaolelewa na kina mama wa kambo, ni basi tu wengi wao hawajakamatwa na cameras.
Wanaume wanaopenda kuzaa zaa , mtu unakuta anazaa pengine na kuoa pengine, mnaweka damu zenu zisizo na hatia katika ukatili huu. Istoshe suala la uzazi wa mpango limerahisishwa sana.
Ni ushauri tu kwa wanaume, waoe walipozalisha au wazae BAADA TU ya ndoa. Sababu hii ni hulka ya mwanamke ambayo haiwez badilika, hata akupendeje huyo mwanamke, atakunyanyasia mwanao hivi.
Na wazazi waliooana ni vema kudumisha familia kakamavu , lasivyo kutengana kwa Baba na mama huchangia hali.. Hii kwa kiasi kikubwa.
Nia yangu kuu ni , tujue kuwa maamuzi yetu ya sasa yanaashiria kitu mbeleni katika maisha yetu.Tusiwe wachoyo kwa kujifikiria tu na furaha za nafsi zetu, tujali hata wa pembeni yetu pamoja na damu zetu. Tunaweza sambaza upendo kwa kutenda kwa busara leo hii na kila mtu akaishi kwa.furaha na amani.

By Leah-Buzuka Derefa

Kucha za Bandia zile za Kubandika na Gundi Samsababishia Mauti Bibi Harusi

$
0
0

“Sijui walitumia gundi ya aina gani
kumbandikia kucha mwanangu, mpaka sasa sielewi, mtoto mwenyewe ndiyo huyo huyo mmoja wa kike niliyekuwa nikimtegemea na ndiyo kwanza ndoa yake bado change kabisa hata mwezi mmoja haina, huu ni mtihani mkubwa kwangu na kwa mumewe ambaye wamefunga naye ndoa wiki tatu zilizopita, inauma sana lakini
tunamwachia Mungu.”

Ni maneno ya mama mzazi wa Sophia Komba aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es Salaam, baada ya kupata kidonda kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto alipokuwa akibandua kucha za bandia alizobandikwa siku ya harusi yake na kusababisha apatwe na tetenasi.
Sophia hadi kifo kinamkuta alikuwa na umri wa miaka 28, Oktoba 15 alifunga ndoa na Richard Mmary katika harusi ya aina yake iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wakisimulia namna walivyomuuguza Sophia kwa takriban wiki moja na
nusu, mume wa marehemu anasema
wiki moja baada ya sherehe ya harusi yao, Sophia aliamua kwenda tena salon kwa ajili ya kutengeneza nywele na kutoa kucha alizobandikwa siku ya harusi yao.
“Ilikuwa siku ya Jumamosi jioni,
Sophia aliniaga anaenda saluni, alirudi baada ya saa mbili kupita lakini alikuwa akilalamika kuwa kidole kinamuuma sana, nikamuuliza amefanya nini akanijibu kuwa alikuwa anabandua kucha, lakini bahati mbaya kucha moja inaonekana ilibandikwa vibaya walipokuwa wanaibandua ilibanduka na ngozi ya pembeni ya kidole na ikamuachia kidonda.
“Sikujali sana nikajua ni kidonda cha
kawaida tu, nikaenda kwenye duka la dawa nikamnunulia spiriti
nikamsafisha lile eneo, lakini
kilichonishangaza alikuwa akilalamikia maumivu makali,” anasema.
Mama yake Sophia, Victoria Haule
anasema kuwa anaamini kuwa kifo cha mwanaye kimetokana na kucha bandia ambayo ilimsababishia apatwe na
tetenasi.
“Tulipoona maumivu yanamzidia,
tulimpeleka Hospitali ya Sinza, daktari alipomfanyia vipimo alitutaka tumpeleke Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi, kwa kuwa alibaini kuwa Sophia ana tetenasi iliyosababishwa na kile kidonda.
Binafsi niliamini kucha ile ndiyo
tatizo, kwa kuwa ilifikia hatua mkono
mzima ukawa umevimba na
kubadirika rangi na kuwa mweusi sana kama damu imevilia,” anasimulia mama yake Sophia.
Kwa maelezo ya ndugu hao wa
marehemu, Sophia alifariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu na kwa
mujibu wa daktari kifo chake
kilisababishwa na tetenasi.
Mabibi harusi wengi hivi sasa na hata wanawake kwa wasichana
wanapendelea sana kubandika kucha bandia wakilenga kuboresha
mwonekano wa vidole vyao. Wengi
hupenda kuwa na kucha ndefu ambazo huzipaka rangi na hivyo kuvutia pindi mtu azionapo.

Breaking: JAJA Ajiondoa Rasmi Yanga, EMERSON Achukua Nafasi Yake

$
0
0
MSHAMBULIAJI Genilson Santana Santos ‘Jaja’ amejiondoa Yanga SC
akiwa likizo nchini mwao, Brazil na sasa nafasi yake itazibwa na
kiungo mkabaji, Emerson Oliveira Neves Roque, Jaja amesema ana matatizo ya kifamilia yanayomzuia kurejea
Tanzania kufanya kazi.
Emerson mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Rio de Janeiro,
anakuja Yanga SC akitokea klabu ya Bonsucesso ya mjini humo, ambayo imewahi kucheza Ligi ya Serie B
mara mbili, ingawa kwa sasa inacheza ligi ya jimbo la Rio.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumanne kwa ajili
ya kufanyiwa majaribio na akifuzu atafanyiwa vipimo vya afya, kabla
ya kusajiliwa. Wazi mchezaji huyo ana nafasi ya kusajiliwa Yanga SC
kwa kuwa analetwa na kocha Maximo.

Jibu la Diamond la Kwanini Ametumia Tena Wazungu Kwenye Video Mpya ‘Ntampata Wapi’

$
0
0
Baada ya Diamond kuachia video ya ‘Ntampata wapi’ iliyofanyika Afrika Kusini, amekutana tena na maswali aliyokutana nayo kipindi alipoachia video ya ‘Mdogo mdogo’, ya kwanini amewatumia zaidi wazungu kwenye video ya wimbo wake wenye ladha ya Kiafrika. 

Hili ndio jibu la Platnumz baada ya kuulizwa swali hilo kwenye kipindi cha Power Jamz kupitia East Africa Radio:

Kuna kitu kimoja, waache ubaguzi inategemea na script ya nyimbo inavyozungumza, script inataka kitu gani, script yangu ya mdogo mdogo ilikuwa inazungumza kwamba mapenzi hayachagui, ndio maana kulikuwa na familia ya kizungu mimi familia ya kiafrika, mimi namtaka demu wa kizungu lakini wazazi wake hawataki, kwahiyo ndo maana mwisho tukaandika mapenzi hayachagui”.

Na naamini hicho kitu ndo kilisababisha kufanya hata Marekani ikashinda tuzo, video ya Aye haikushinda ikashinda video ya Mdogo mdogo kama video ya Afrika kwasbaabu concept yenyewe ilikuwa inazungumza vizuri, wazungu wenyewe wameona kama aah hii kweli lakini tuache maswala ya kibaguzi”.
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images