Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Al-Shabaab Wavamia Basi na Kuua Watu 28, Nairobi

0
0
Takriban watu 28 wameuawa na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab waliovamia basi la abiria jijini Nairobi, Kenya.

Tukio hilo limetokea alfajiri leo saa 11:30 kwenye eneo la Mandera.

Kamishna Msaidizi wa kaunti ya Mandera East, Elvis Korir alisema taarifa za awali zimedai kuwa wanamgambo hao takriban 100 waliisimamisha basi hiyo na kuamuru watu wote watoke nje.

Anadai kuwa abiria hao waliwekwa kwenye makundi mawili ya Wasomali na wasio wasomali. Alisema kundi la wasio wasomali walimiminiwa risasi.

Abiria 59 walikuwa wamepanda basi hilo.

Chanzo: Daily Nation

Picha za Diamond Akimla Denda Zari the Boss Lady Zavuja Mitandaoni

0
0
Duu Yameongelewa Mengi Wengine wakisema ni wapenzi wengine wakikataa na kusema ni Project ya mziki wanafanya pamoja ..Ila hii Picha inaelezea Yote ..Unachoona Ndio Hicho Kubali ama kataaa..
New Couple in Town !!
Wapi Team Wema???
Mupo Hapo

Mwigulu Nchemba Acharuka Asema Walio iba Fedha za Escrow Wakamatwe na Kufilisiwa Mali zao

0
0
Mwigulu Nchemba alitoa msimamo mkali kuhusu sakata hilo la escrow na kwamba ametaka hatua zichukuliwe kwa wahusika wote.

Katika kikao hicho inaelezwa kwamba Nchemba alionyesha msimamo wake waziwazi kuwa sakata hilo ni hujuma  na kwamba haiwezekani walioiba fedha hizo wakaachiwa tu hivihivi.

Ndani ya kikao hicho imeelezwa kuwa Mwigulu alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.

Alisema haiwezekani watu wakawajibika tu kwa kujiuzulu kwa kuwa huko ni kutoa tu likizo mtu akale mabilioni yake, hivyo wachukuliwe hatua ipasavyo na kufilisiwa.

“CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe,” alisema Mwigulu.

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe, zifilisiwe na fedha zirudishwe kwa wananchi.

Pia aliagiza mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha irudi serikalini.

Habari za uhakika kutoka kikao hicho zinaeleza kuwa Mwigulu aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri Mkuu na kusema kuwa kujiuzulu siyo adhabu stahiki kwa wizi mkubwa kama huo.

Mwigulu alisema: “Tazama wanafunzi, watoto wa maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna, maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia maskini?”

Kwa mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 bilioni Mwigulu akatoa agizo:

Nimemwagiza Kamishna wa Kodi amfukuze kazi yule mtumishi wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe na wahusika wakamatwe.

Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga maskini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini,” Mwigulu alisisitiza.

Ni aibu India na Kenya Kuipiku Tanzania kwa Uuzaji Madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania Pekee

0
0
Taarifa kwamba nchi za Kenya na India zimeipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha madini ya Tanzanite yanayopatikana hapa nchini pekee na kuyauza katika soko la dunia ni jambo ambalo siyo rahisi kuliamini.

Nasema siyo rahisi kuamini kwa sababu haingii akilini hata kidogo, mtu ambaye halimi mahindi anaibuka kinara wa kuuza sokoni mahindi yako anayoyaiba shambani kwako.

Ni heri kama angekuwa anakuja kununua kwa njia ya kawaida na wewe ukanufaika.

Nilimsoma kwa makini Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja hivi karibuni kupitia baadhi ya magazeti nchini akisema kwamba kwa mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Mwaka jana pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 100 milioni (Sh173 bilioni), dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni), zilizouzwa na Tanzania.

Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza Tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola 300 milioni za Marekani(Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India.

Mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka Marekani, aliwahi kuwauliza viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini iwapo kuna migodi ya Tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata Tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya Tanzanite inayopatikana Mirerani, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi na kwamba Serikali imeanza kuchukua hatua.

Kama nilivyosema awali, hili ni jambo la kushangaza sana. Ninajiuliza; hivi haya madini nani anayeyatorosha kwenda nchi za nje? Ni wazi kuwa watu wachache waliopewa jukumu la kusimamia sekta ya madini, wamekuwa wakishirikiana na watu wa nje kutorosha madini hayo.

Tumejua wizi wa madini haya kwa sababu tu yanapatikana pekee Tanzania. Tujiulize wizi huu wa madini yetu ukoje katika madini mengine ambayo pia yanapatikana katika nchi nyingine?

Kwa hakika, raslimali za nchi hii zinaliwa na watu wengine, huku Watanzania wakibaki mikono mitupu.

Wanaume Tunarogwa Sana na Hawa Wanawake Zetu

0
0
Katika Uchunguzi Wangu nimegundua Wateja wengi wa waganga wa Kienyeji ni wanawake ,hii inatoka na kuwa ushindani wa namba umekuwa mkubwa sana matokeo yake wakina dada na wakina mama wamemua kutafuta plan B nayo si nyingine ni kutuchawia, tunarogwa sana,  tunalishwa vitu vya ajabu.

Wateja wakubwa wa waganga ni hawa wanawake unadhani wanafuata nini huko kwa Waganga?

Pinda, Werema na Muhongo wataka zigo la Escrow abebeshwe Kikwete!

0
0
Dodoma kumekucha. Naomba kwa ufupi niwafahamishe kinachojiri maeneo haya (nimepiga kambi huku).

MOSI:
Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa anataka PM Pinda atoke kwa sababu mbili, moja ili njia ya kupata Urais iwe nyeupe lakini pili ili asiwe PM peke yake aliyewahi kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa. Watu wake Edward wanahangaika sana kushawishi watu ili azma hii itimie.

PILI:
Membe naye anataka PM ang'oke kwa sababu kuu mbili, moja ili njia ya Urais iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM japo kwa muda tu ili nyota ing'are zaidi.

TATU:
Wassira naye anatakaPinda aanguke ili njia iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM.
Mwandosya naye anataka PM adondoke kwa matumaini ya kupata uPM kutokana na utu uzima.

Sitta naye vivyo hivyo.

NNE:
Mawaziri walioondolewa huko nyuma wakiongozwa na Kagasheki, Nchimbi na Maige nao wanaomba Serikali idondoke kwa sababu wanaamini Pinda aliwatosa ili apone yeye na sasa wanataka na yeye awajibike kwa udhaifu wake. Yupo mtu kama Mwigulu ambaye anautaka Uwaziri kamili kwa udi na uvumba na anataka Serikali ianguke ili Baraza la Mawaziri lisukwe upya awe Waziri kamili.

Kambi za Urais za wazee zimeungana kutaka Pinda ang'oke!

TANO:
Kwa upande mwingine hii ni vita ya watu wa Mara: Maswi, Muhongo, Werema na Mkono. 

Upande mwingine ni vita ya baina ya vizazi; kizazi cha vijana na kizazi cha wazee.

Tazama Vijana walioshikilia bango suala hili ni wabunge vijana: Zitto, Kafulila, Filikunjombe, Serukamba, Mpina, Bulaya, Kigwangalla n.k.

Wanaotetea ni watu wazima: Pinda, Muhongo, Werema na wengine.

Lakini pia kwa Upande mwingine ni vita ya pesa: Kila upande umekula na ujanja ni kuwahi kupaka matope wengine!

SITA:
Kamati ya PAC imeandika ripoti nzito zaidi ya ripoti ya CAG ambayo ni laini mno (nimebahatika kuziona walau zote mbili). PAC, chini ya Zitto na Filikunjombe wanaweza kuwa wamefanikisha kufanya ripoti yao iwe vizuri hivyo kwa sababu wamewahoji watu na kupata taarifa za ziada (ambazo zitaibua mjadala mzito sana Bungeni).

SABA:
Pinda anapigana kufa na kupona ili apone. Pinda akianguka hapa Urais ndio kwisha. Hata hivyo, Pinda hata asipotoka uPM atakuwa tayari amechafuka na udhaifu wake umebainika. Ijapokuwa Wabunge wanaweza kumponya tu Pinda kwa sababu ya kumsaidia Kikwete lakini tayari ana doa!

Hata hivyo, katika harakati za kupona Pinda, Werema na Muhongo wamekuwa wanawaambia wabunge kwamba kulikuwa na agizo la Rais la pesa kulipwa. Yaani Pinda yuko tayari kumuingiza Rais kwenye tope kulinda vyeo vyao!

Kikwete inabidi afanye maamuzi ya Kiurais, watu aliowaamini hawana hiyana kumtosa. Akimaliza Urais ndio hatari zaidi (mtakumbuka kauli yangu 2016/2017)

Aibu: Msanii wa Bongo Movies Afumwa Makaburini Akivunja Nazi ili awe Maarufu Kama Wema Sepetu

0
0
Ulozi! Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’ amenaswa makaburini akiwanga katika kile kinachodaiwa kuwa ni kutekeleza masharti ya ‘sangoma’ ili ajipatie umaarufu na kuwafikia mastaa kama Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Massawe na Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Makaburi ya Ufi yaliyopo maeneo ya Ubungo-Kisiwani jijini Dar, mishale ya saa nne usiku.


Habari zilidai kwamba msanii huyo alifumwa akivunja nazi na kuzungumza maneno yasiyoeleweka.
Awali, ilidaiwa kwamba, Fetty ambaye anaonekana kwenye Filamu ya House of Death akiwa na mwigizaji Kulwa Kikumba ’Dude’ alitinga kwenye makaburi hayo akiwa ameshika kimfuko huku akiangaza huku na huku kisha akatoa nazi na kuivunja huku akinuiza maneno bila kujua kuna mtu alikuwa akimpiga picha.

Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Fetty na kumuuliza juu ya madai hayo, alianza kujikanyaga kabla ya kufunguka kuwa hapendi mambo ya kishirikina ila alilazimika kufanya hivyo kutokana na masharti aliyopewa na mganga wake kutokana na matatizo yake ya kimaisha yanayomsumbua pamoja na ndoto yake ya kuwa msanii mkubwa.

Pinda - Mjadala Escrow Umeongezwa Chumvi, Watanzania Msiamini Mambo ya Uzushi

0
0
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa nyingi za mjadala wa akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za umeme kati ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambao unaendelea bungeni, umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili.

Kauli hiyo ya Pinda aliitoa kanisa kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika wakati wa kumsimika Dk Jackson Chilongani kuwa Askofu wa Sita wa dayosisi hiyo.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya aliitaka Serikali kutoa taarifa juu ya akaunti ya Escrow ili wananchi wajue kilichotokea ili ijulikane ukweli upi na uvumi upi kwani iko hatari ya kutengeneza taifa lenye kuamini uvumi.

Dk Chimeledya alisema Watanzania sasa wanaishi kwenye hali ya sintofahamu kwani hawajui yupi anasema ukweli na yupi ni `mzushi’. Alisema ni lazima Serikali itoe maelezo kwa wananchi juu ya kashfa hiyo ili wajue kilichotokea kwani ipo hatari ya kutengeneza taifa linaloishi kwa kuamini uvumi.

“Hatutakiwi kuishi kwenye taifa linaloamini uvumi… taifa halitapiga hatua kwa taarifa za kusikia tu bila kujua ukweli uko wapi, nini kimetokea na hatua gani imechukuliwa,” alisema

Lundenga Awaka Kisa Kuulizwa Kuhusu Sitti Mtemvu

0
0
Stori: Musa Mateja
MKURUGENZI wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga amewaka kinomanoma baada ya kuulizwa habari za mrembo wake aliyejivua taji hivi karibuni, Sitti Mtemvu

Lundenga alibwatuka maneno makali baada ya paparazi wetu kumuuliza juu ya uwepo wa taarifa kwamba shindano hilo linaweza kufungiwa kutokana na kashfa mbalimbali zinazolitafuna sambamba na ufafanuzi wa zawadi ambayo alipewa Sitti kama anaweza kuirejesha kwa mrembo namba mbili aliyechukua nafasi yake.

“Sikiliza nyinyi nawaheshimu sana sababu najua mpo makini, tusivunjiane heshima hizo habari zisizokuwa na kichwa wala miguu waachieni wanaokurupuka kuandika mambo ya uongo, wapuuzi sana wale,” alisema Lundenga na kukata simu na hata alipopigiwa tena, hakupokea.

Download Wimbo Mpya wa Lady Jay Dee Feat. Dabo -Forever

0
0
Download Wimbo Mpya wa Lady Jay Dee Feat. Dabo -Forever

U Heard ya leo Kuhusu Nay wa Mitego na Kala Jeremiah Kuchuniana Baada ya Nay Kumdis Kala Kwenye Wimbo

0
0
Kama umepitwa na U Heard kwenye XXL ya leo nimekuwekea hapa, zimesikika taarifa kuhusu Kala Jeremiah na Ney wa Mitego.
Baada ya tetesi nyingi kuenea mtaani kuhusu wasanii wawili ambao walikuwa hawaongei karibu miezi mitano kisa kikidaiwa ni mambo ya nyimbo zao.
Mwezi wa sita msanii Kala Jeremiah aliachia nyimbo ya ‘Simu ya Mwisho’ alichomshirikisha Ney wa Mitego, haukupita muda mrefu Ney akaaichia Mr. Ney ambapo ndani yake alimtaja Kala Jeremiah kuwa kapotea kwenye game na huo ukawa mwisho wa wasanii hao kuwasiliana kama ilivyokuwa zamani.
Wakali hawa wamekutana Ubungo kwenye studio ya mtengeneza Video, Pablo na maongezi yao yalikuwa poa, kama watu ambao hawana tofauti yoyote.
U Heard nimekuwekea hapa, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.


Muhongo Ahusishwa Wizi Nyaraka za Escrow Bungeni

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, ametajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mmoja kati ya vijana wawili wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuiba kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge ripoti ya ukaguzi wa hesabu za zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa kifisadi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ukaguzi huo ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).Wakati Waziri Muhongo akitajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mtuhumiwa huyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye jana ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuongoza Bunge tangu lianze Novemba 4, mwaka huu, anadaiwa kutajwa kuwamo katika orodha ya vigogo waliovuna fedha hizo, huku yeye akipata mgawo wa Dola za Marekani milioni moja.

Aliyemtaja Waziri Muhongo kuwa na uhusiano wa karibu na kijana huyo, ni Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.

Mnyika alimtaja Waziri Muhongo, wakati akichangia mjadala kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2014, bungeni jana.

Muswada huo uliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni, Ijumaa wiki iliyopita.

”Mheshimiwa Spika, ni muhimu ofisi yako ifuatilie. Kwa sababu mtuhumiwa yule ana uhusiano wa karibu sana na Prof. Sospeter Muhongo, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa kwenye kashfa tunazozijadili,” alisema Mnyika.

Aliongeza: “Sasa nasema haya mapema ili isifikie hatua tukatumiwa kisingizio cha mambo kuwa mahakamani kushindwa kuwataja kwa majina wahusika. Polisi wafanye uchunguzi, wachukue hatua.”

Mnyika alisema uharamia kwenye suala IPTL wa muda mrefu umezidi mipaka.

Alisema taarifa alizonazo ni kwamba, polisi wanamshauri Spika wa Bunge kwa sababu wanataka haraka haraka wamkimbize mtuhumiwa huyo mahakamani ili baada ya hapo alieleze Bunge kuwa kishapelekwa mahakamani, hivyo hakuna sababu ya kutaja jina wala suala lake kujadiliwa.

Mnyika alisema tangu siku waliyowapa polisi taarifa, mpaka leo wamekuwa wakisitasita wakishindwa kutaja jina la mtuhumiwa, huku wakisingizia uchunguzi.
Hata hivyo, alisema upande wa serikali wanapokutana nao kwenye korido wamekuwa wakiwaambia kuwa mhusika anafahamika, ikiwa ni pamoja na watu wote ambao amekuwa akiwasiliana nao.

“Mheshimiwa Spika, ukiendelea kuyakinga mambo haya kwa kisingizio cha mambo kuwa polisi, halafu baadaye polisi wakaenda mahakamani, ukaja kuyakinga hapa kwa kisingizio cha kwamba mambo yako mahakamani, maana yake Mheshimiwa Spika na wewe utahesabika kwamba, hizo mbinu za hao maharamia waliopora ripoti ndani ya ofisi yako pengine na ofisi yako inahusika,” alisema Mnyika.

Mwimbaji Baby Madaha Adaiwa Kuambukizwa Gonjwa Baya

0
0
MSANII wa Bongo Fleva, Baby Madaha anadaiwa kuambukizwa gonjwa hatari la zinaa ambalo halikutajwa jina lakini likielezwa kuwa linampa wakati mgumu kisaikolojia. Chanzo kimoja kimeiambia show bize kuwa, nyota huyo amekuwa akitumia dawa za kusafisha haja ndogo kwa muda mrefu lakini bila mafanikio.

Show bize ilimsaka Baby Madaha mwenyewe ambapo aling’aka kwa ukali.
“Hizo habari nani kakupa wewe? Hayo si moja ya maisha ya wanadamu kwani kipi kibaya hapo? Oke, sawa naumwa na hao wanaume wanaotaka nikatibiwe wanajua mimi naumwa nini? Magonjwa ya zinaa si yana dawa?” alihoji.

Hata hivyo, mrembo huyo alisema yeye ana tatizo la haja ndogo kuwa chafu lakini si ugonjwa wa zinaa.

Issue ya Madawa ya Kulevya, Chonji Hali Tete

0
0
HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.

Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.

Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike.

“Tunachunguza mali zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya na siyo kwa Chonji peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa wanafilisiwa,” alisema Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne walikamatwa usiku wa manane Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni Mtaa wa Kondoa jijini Dar  na inadaiwa walikuwa  na mzigo wa unga uliokuwa ukifungwa katika vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na sare za jeshi (JWTZ) na bastola.

Zitto: Tumependekeza Kumvua Ujaji Mh. Werema

0
0
Akihojiwa na mwandishi wa Tanzania Daima, mh. Zitto amesema PAC IMEPENDEKEZA

1. Kuanza mchakato wa kumvua UJAJI MH. WEREMA

2. Kumfikisha mahakamani

3. Wote waliohusika kuwajibishwa kulipa na kisha kupelekwa mahakamani.

Mh. Zitto amedai hii haiwezi kuisha kama EPA,lazima wahusika wafike mbele ya sheria.

Dully Sykes Ajitetea Kuhusu Wimbo wa 'Matusi' Aliyoutoa Hivi Karibuni

0
0
Siku chache baada ya wimbo wake wa Thats The Way uliojaa matusi yasiyoweza kuandikika gazetini kuanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao , msanii wa kitambo wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amefunguka kuwa halikuwa kusudio lake kuachia wimbo huo bali ulivuja kwa bahati mbaya mitandaoni.

Akipiga stori na Showbiz juzikati, Dully alisema kuwa wimbo huo aliomshirikisha mwanadada Maunda Zorro, aliurekodi miaka nane iliyopita kwenye studio yake ya Dhahabu Records na hakupanga kuutoa lakini kwa bahati mbaya ukavuja na kuingia mitandaoni.

“Siyo mpya, ni wa kitambo sana, nilirekodi miaka nane iliyopita nashangaa kwa nini watu wanafikiri ni mpya,” alisema Dully lakini alipoulizwa hata kama ni wa zamani kwa nini alirekodi wimbo wenye maneno ya kuhamasisha ngono, hakuwa na majibu.

Licha ya utetezi wake huo, wimbo huo unaonekana kuwa mpya kwani sauti ya Dully inafanana na ya kwenye nyimbo zake mpya za hivi karibuni.

Mabibi na Mabwana ile single mpya ya Waje na Diamond ndio hii imetoka

0
0
Ile single mpya ya msanii wa Nigeria Waje na Diamond Platnumz ‘Coco Baby’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sasa imetoka nakukaribisha uisikilize hapa

Wanaume wa Dar mnaongoza kuvunja mahusiano yetu sisi tulio mikoani

0
0
Jamani wanaume mliopo Dar es salaam tunaomba mtuhurumie sisi tulio mikoani, kwani ukiwa na mpenzi wako akikuaga anaenda Dar kusoma au kwa ndugu yake na akikaa angalau mwaka mmoja ujue akirudi sio wako tena mambo yanabadilika kabisa ..Maringo mengi na dharau juuu

Nashindwa kuelewa sijui mnawapa kitu gani wapenzi wetu wakija huko dar?

Naombeni Ushauri Wenu, Mpenzi Wangu Amekutwa na Maambukizi ya Ukimwi

0
0
Jamani nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mdada mmoja hivi takribani ni miaka 3 sasa.

Katika mahusiano yetu tumekuwa tukipendana sana na hatma ya yote lengo letu lilikuwa ni kuishi wawili kama mume na mke.

Huyu mpenzi wangu tumekuwa tukiishi mbali mbali kutokana na wote wawili kuwa na majukumu tofauti ya kiutumishi.
Hapo mwanzo nilipoanza nae tulipima afya zetu yaani hatukuwa na maambukizi ya vvu.

Kiukweli tokea hapo tulijihusisha na mapenzi kwa uaminifu kila upande. Nimekuwa nikimuamini sana na yeye pia kuniamini. Mimi mwaka huu nilikuwa nimepanga tufunge ndoa mwezi wa 12. Mimi naishi mwanza kikazi ila yeye anaishi dodoma.

Tokea mwanzo wa mahusiano yetu sijawahi kutumia kinga ninapokutana na yeye na nimekaa naye kwangu mara nyingi sana pindi anapokuwa na likizo.

Mwezi uliopita amekuja kwangu nikawa nimekaa nae kama wiki mbili hivi akawa amepata homa tu ya kawaida.

Ikabidi nimpeleke hospitali kupata matibabu,tulivyoenda hospitali nikamshauri ebu leo tucheki bas afya zetu? Kwani ni muda sasa hatujacheck vvu.

Alikubali tukawa tumeenda kupima,majibu yaliyotoka ni kwamba yeye ana maambukizi ya vvu na kwa upande wangu sijaonekana na maambukizi.

Kiukweli hiki kitu kimeniumiza sana na hapa nilipo sijajua hatma ya maisha yangu,na daktari alichoniambia ni kwamba mimi damu yangu sio rahisi kupokea maambukizi ya vvu kutokana na group langu la damu na lake.

Hivyo amenishauri niendelee kupima kila baada ya miezi mitatu ili kuwa na uhakika zaidi.

Kitu kinachoniumiza na kunisumbua kichwa zaidi ni kwamba huyu mchumba wangu analia sana na anasema kutengana na mimi ni bora yeye afe tu kuliko kukaa mbali na mimi.

Na kingine ni kwamba,anadai kutokana na upendo wangu juu yake anataka anizalie mtoto ili aniachie zawadi hata yeye akifa.

Kiukweli hapa nilipo sijitambui afya yangu na kushiriki tena tendo na yeye naogopa.

NIFANYAJE Ili kumfurahisha? nikubali kuzaa nae? Nifanyaje 

Haya Ndio Yanayoendelea Kuhusu Yule Binti Mfanyakazi wa Ndani Aliyeonekana Akimtesa Mtoto

0
0
Polisi wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.
Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wenegine.
Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.

Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.
Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka.
Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.
Afisaa mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama haya yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikologia.

Waziri wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na kitendo hicho kwa mtoto. Ingekuwa mtu mwingine angemuua mischana huyo wa kazi lakini alifuata sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika katiba kuhusu maslai ya watoto bungeni kuimarisha sheria zinazowajali watoto," alisema waziri huyo.
Polisi wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia msichana huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi wamesema kuwa mtoto huyo ametolewa hosipitalini na hali yake ya afya inaimarika.

Kulingana na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba ya mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi cha Kiwatule baada ya kuona video hio.
Kesi hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya uchunguzi, msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shataka la mateso katika mahakama ya Nakawa na kuzuuliwa katika gereza la Luzira.

Bwana Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu kwenye katika kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho kinajumuisha mashataka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa kumfunga mtu hadi miaka 15 gerezani.
Hata hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugegenzi wa pande za mashtaka kurebisha hukumu hilo kuwa kifungu cha maisha.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images