Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Aunt Lulu Ashushiwa Kipigo cha Nguvu na Mpenzi Wake Tena

0
0
Stori: Gladness Mallya
MWANADADA mwenye umbo tata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amedaiwa kubondwa tena na mpenzi wake aitwaye Amani, kisa kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.Mwanadada mwenye umbo tata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.

Chanzo cha habari ambacho ni jirani na msanii huyo kimeeleza kuwa, Aunt Lulu alichezea kipigo hicho hivi karibuni akiwa nyumbani kwao Mbezi Salasala jijini Dar baada ya bwana wake kukuta sms tata kwenye simu yake.

Mimi nilisikia mtu akipigwa huku simu ikitajwa, Aunt Lulu kapigwa sana kwa kweli,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuinasa ishu hiyo, mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo na alipoulizwa juu ya kipigo hicho, alikiri kugombana na mpenzi wake huyo lakini akasema, hawezi kuzungumzia kwa undani kwani ni tukio lililopita.

Picha, Mtoto wa Rugemarila Akila Ujana na Msanii Rihana Ulaya

0
0
Ni baada ya kupata mgao wa mabillion ya pesa za Escrow alizopewa na babake ...Picha hii Imeenea Mitandaoni Kila Kona 

Teamwema Wampiga Debe Boss Wao Kwa Ex Husband wa Zari the Bosslady

0
0
Hii ni zaidi ya mwaga mboga nimwage ugali....Team Wema imeamua sio tu kumwaga ugali ila kutoboa sufuria na kuzima mato ili pasipikwe kabisa, 

Mashabiki wa Wema Sepetu wameamua kuvaa miwani za mbao na kumfanyia udalali wa mapenzi boss wao kwa aliekuwa mme wa le project Zari the bosslady bwana Ivan, amsha amsha hizo zimeanza punde tu baada ya wema mwenyewe kuanza kumfollow Ivan.

maskini baba wa watu hadi kishapachikwa jina eti aitwa Ivanwema (ila madam mbona siku zote hukumfollow jamaa why sahivi?...mi nawaza tu)Wema ndo amekuwa wa kufanyiwa udalali hivi kama kiwanja cha bondeni duh! ndo njia ya kumfariji hiyo? huku ni kuaibishana tu na hizi teamushuzzz!!!Haya tunangoja project ya Ivan na Madam....!!!!

Soma Hapa:




'Najisikia Raha Kukaa Uchi Niwapo na Mpenzi Wangu'….Jokate

0
0
Modo ambaye pia anafanya muziki na ujasiriamali, Jokate Mwegelo amefunguka  kuwa, awapo chumbani na mpenzi wake huwa anasikia raha kutovaa chochote.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema haoni aibu kusema akiwa faragha na mpenzi wake hapendelei kuvaa kitu kwani ni eneo la kujiachia.

“Kwa kweli nikiwa chumbani na mpenzi wangu sipendi kuvaa kitu kabisa,” alisema Jokate kwa kifupi

Huyu Ndio Yule Mwanamke Anaye Fanana na Wema Sepetu Unywele Mpaka Ukucha

0
0


Ule usemi wa duniani  watu wawili wawili umedhiiika kwa muigizaji wa bongo movies,Wema Sepetu.Je hii ni kweli?.Hebu kutana na huyu mwanadada anaetumiajina la TUERNY kwenye mtandao wa INSTAGRAM.Kizuri zaidi wema mwenye anamfahamu hii nikutokana na moja kati ya marafiki wa Wema Ku-comment kwenye picha ya dada huyu akidai kuwa dada huyu anafanana na Wema na dadae Wema Ku-reply kwa kuonyesha kuwa anamfahamu na anamuita mke mweza.....Hebuzicheki picha zake hizi na kisha useme kama kunaumuhimu wa wawili hawa kupimwa DNA

WASTARA: Imenisikitisha Kuzushiwa Kifo

0
0
Muigizaji wakike  wa Filamu hapa nchini, Wastara Sajuki amesikitishwa na taarifa za uongo zilizo enea nchini Burundi kuwa alishafariki kwa ajali ya gari. Kupitia ukurasa wake wa matandao wa INSTAGRAM muigizaji huyo  ambaye aliondoka hapa nchini juzi kuelekea nchini humo kizazi, mbali na kuonekana mwenye furaha kwa picha alizoziweka kwenye ukurasa huo akiwa sehemu za ufukweni (Baadhi ya picha kama unavyoziona hapo chini), Wastara alikutana na mashabiki wake na taarifa za kuwa walidhani amekisha fariki ndipo alipozipata.

Hii.imeniskitisha saana baada ya kukutana na mshabiki.wangu.na kusema taharifa walizonazo burundi nilishafariki kitambo kwa ajali.shughuli ilikuwepo nilionekana kma nimefufukia.burundi daah aliyezusha hivyo.naimani nitamzika yeye kabla yangu kigupi sijafa.maahabiki wangu.wa burundi.niko.hai.naendelea.kutumikia taifa.langu.nanyi.pia.Mungu ni.mwema.bado.ananipa.pumzi –Wastara

Quick Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na Kajala

0
0
Quick Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu, Kajala Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Quick amesema ana girlfriend hivyo uvumi huo unaweza ukamharibia uhusiano wake.“Nasema hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa na Lamata. Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga chemistry. Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi moja inabidi mchongo tuufanikishe,” alisema rapper huyo. “I have a girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli.”

Mahakama ya ICC imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili Rais Kenyatta

0
0
Mahakama ya Kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai iliyokua inamkabili Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta kutokana na kutokamilika kwa ushahidi.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Katika Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo iliyopo nchini Uholanzi imesema kesi yake haikua na ushahidi wa kutosha wa Kenyatta kuhusika moja kwa moja na mauaji ya maelfu ya Wakenya wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 akituhumiwa pamoja na William Ruto ambaye ni Makamu wa Rais ambapo maelfu ya wananchi walipoteza maisha.

Kafulila Aibuka Tena Upya,Sasa Amvaa Kikwete Kwa Kuwalinda Wezi Wa Escrow

0
0
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisuasua kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa na Bunge kuhusika Katika Wizi wa zaidi ya Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta Esrcow ,naye Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila Ameibuka upya na Ameivaa Ikulu
       Na kusema Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi waliohusika katika kuiba pesa hizo,baada ya kumzuia Mkurugenzi wa ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa PCCB Dk Edward Hosea kutoiwasilisha Taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la Esrcow  kwa Umma kutokana na Ripoti ya PCCB kuwataja vigogo wa Ikulu kuhusika katika kuchota pesa kwenye Benk ya Stabink. Hayo yamebuliwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kafulila  huku akizungumza kwa uchungu alisema Inasikitisha kuona jinsi Ikulu inavyotumia ubabe wake kumzuia Dk Hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya uchunguzi.

   “Tunafahamu wazi serikali inataka kuwalinda watu waliochota pesa,kutokana na kitendo chake kumzuia PCCB asiweka hadharani ripoti kwa kisingizia uchunguzi ujakamilika,ujakamilika kivipi wakati tunakumbuka wazi Mkurugenzi wa PCCB Dk Hosea wakati kongamano la SADC  kuhusu Rushwa  uliofanyika mkoani mwanza mwezi Novemba”
“Alisema ripoti yake ya uchunguzi kuhusu Akaunti ya Escrow umekamilika na tayari wameshamkabidhi Waziri Mkuu ingawa waziri huyo mkuu alikana,na hii yote inafanyika hivi ni kutokana na Ripoti ya PCCB kuwepo  na majina ya Vigogo wa Ikulu ambao walichota pesa kwenye Benki ya Stabink”alisema Kafulila
      Kafulila aliongeza kuwa leo majina ya watu waliochota pesa kwenye Benki ya Mkombozi tu wanatajwa ,huku wengine kwenye Benki ya Stabink Benki wakiachwa kwa kuwa ni vigogo wa Ikulu.
      “Leo majina ambao kamati ya PAC waliyopewa na PCCB ni ya Benki ya mkombozi huku majina ya Benki ya Stabink ambao watu walichota pesa kwa maboksi,Sandalusi,magunia ambao wengi wao ni vigogo wakubwa wa ikulu wakiachwa,na ndio maana Ikulu hii inakataza Ripoti ya PCCB iwekwe wazi kwakuwa itaweza kuvuruga nchi kwasababu wahusika waliochota pesa wengi ni watu wa Ikulu”aliongeza Kafulila.
   
 Kuhusu Jeuri ya Mmiliki wa IPTL Bwana Seith
       Kafulila ambaye  pia ni katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR Mageuzi alisema Jeuri aliyekuwa nayo bwana Seith kwa kuzivimbia Mamlaka zote ikiwemo Mamlaka ya ukusanyaji Kodi TRA inatokana na kigogo huyo kufahamu wizi huo ameufanya na vigogo wa kubwa wanchi.

   “Huyu bwana seith anakuwa jeuri sana kwakuwa anauhakika pesa za Escrow amekula na wengi hata akifanya jambo anajua wazi hakuna wakumchukulia hatua kwakuwa wako wengi, na  hii inatokana kutokuwa na serikali makini ndio maana inamuacha huyo taperi kufanya anavyotaka ila serikali ijue huyo mtu avyojisifu hivi atakujakuleta machafuko nchini”alitabainisha Kafulila.

AUNT EZEKIEL: Chagueni wenyewe ni Kitambi au Mimba

0
0
Japokuwa hadi sasa Muigizaji  Aunt Ezekiel Grayson anakanusha kuwa hana ujauzito, stori zake za kuwa na ujauzito zimezidi kuenea kwa kasi zaidi kwenye mitando ya kijamii na blogs mbalimbali za hapa BONGO.

Hii nikutokana na kuonekaana kwenye Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.

KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU                                      
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.

AUNT ANASEMA AKANUSHA

Kwamujibu wa Global Publishers.info, Aunt  Ezekiel alikanusha na kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
“Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa,” alisema Aunt kwa kifupi.

ALICHO-POST INSTAGRAM

Jana kupitia ukurasa wake wa instagram,Aunt Ezekiel aliweka picha yake akiwa tumbo wazi na kuandika ujume kuwa lazima tujue kutofautisha kati ya mimba na kitambi

Lazima ujue Kutofautisha kati ya Kitambi na Mimba Sasa hiki Chagueni wenyewe ni KITAMBI AU MIMBA!!!!!legoooooooooo.....

Binti wa Msanii Kajala, Paula Azidi Kuwa Mrembo Kama Mama Yake

0
0

Mtoto wa  msanii wa filamu na Mkurugenzi wa K. Entertainment, Kajala Masanja, Paula Paul ukipenda muite Paulitte. Sasa hivi anaoneka amekuwa binti mkubwa  na mrembo zaidi….Mbali na kuwa mama yake ni staa mkubwa kwa upande wa Bongo Movie, baba yake , P. Funk  aka Majani pia ni mtayarishaji wa music mkongwe na mwenye mafanikia makubwa kwenye upande wa Bongo Flava. Paula japokuwa bado yupo shule lakini maisha yake ya kuwa karibu sana na mama yake kwa ujumla yanamfanya ajuane na ajulikane sio tu mastaa wengi bali hadi kwa jamii kwa ujumla…..Tunaamini huyu nae atakuwa staa wa kesho ….

Zari Amwambia Wema Sepetu Atulie Diamond Sio Mume wala Mchumba wa Mtu

0
0

Zari Ameibuka na kumwambia Wema Sepetu kuwa Diamond Sio Mume wa mtu na wala sio mchumba wa mtu kwa sasa hivyo kitendo cha yeye kutoka out naye ni sawa kwani ni maamuzi ya Diamond Mwenyewe kwa vile kwa sasa yupo huru kabisa..Hivyo Wema Sepetu na Team yake wakae Kimya Waangalie tu jinsi Project inavyokwenda kwani muda wake wa kujivinjari na Diamond ulishapita....
Mweee.. Ndimu zikuwapi 

Huyu Zari Vipi? Mbona Kamganda Diamond Hivyo..'Magazeti ya Uganda'

0
0
MITANDOA ya kijamii na vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.

Gazeti la udaku la Red Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo jijini Dar es Salaam.

Mitandao hiyo ilimshambulia Zari kwa kumwambia kuwa kavuruga uhusiano baina ya Wema na mkali huyo wa video ya ‘Ntampata Wapi’, huku ikiponda picha ambayo Zari aliiweka mitandaoni ikimwonyesha akiwa na Diamond.

Mitandao hiyo imeponda kuwa Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.

Wiki tatu zilizopita Zari amekuwa bega kwa bega na mwanamuziki Diamond, baada ya kutengeneza wimbo wa pamoja katika studio za Tuddy Thomas. Zari alionekana akipiga picha kadhaa na nyota huyo kabla ya kumsindikiza katika tuzo za CHOAMVA, Afrika Kusini na baadaye kurudi naye nchini.

Diamond ambaye alinyakua tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’, itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.

Rais JK Hashinikizwi, Anaamua kwa Maslahi Mapana ya Nchi

0
0
Nimegundua Jk ni rais ambaye hakika Watz hatutomsahau na hatupaswi kumsahau, ametoa uhuru hata wa kumtukana akakaa kimya,wa kumshinikiza na bado akawa calm,wa kujaribu kuichezea na kuijaribu serikali yake na bado akakuvumilia. Neno moja kwenu nyie vibaraka wa wasaka U-rais, wafanyabiashara madalali na wengine wenye kariba ya kutotaka kuona mwenzio anaweka historia ya kuitumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa,wakati Rais Kikwete anaingia madarakan ni asilimia 6 wa wananchi wote walokuwa wanapata umeme,leo hii Watz asilimia 35 wanaaccess na umeme hasa vijijini, barabara za rami ameongeza kwa asilimia 25 network ya barabara za rami, huduma za afya karibu kila kijiji kina zahanati na kila kata kuna kituo cha afya na mengine mengi, juzi nimepata kusikia tunafanya vizuri katika kupambana na rushwa. Ila siwalaumu sana ila ndo tulivyo na itabaki kama challenge kwa rais ajaye, ila kwa ufupi serikali hii imejitahidi sana tena sana but one word kwenu vibaraka, mipango yenu na mabeberu wa magharibi inajulikana na mtashindwa

Zitto: Nina Sharti Moja tu Kurudi CHADEMA

0
0
Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.

Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa “akimiss” harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.

Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini hakudokeza lolote kuhusu Chadema.

Hata hivyo, mapema wiki hii, Zitto, ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa nyadhifa zote kwenye chama hicho kwa tuhuma za kukihujumu, lakini akafanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe.

Baada ya kuongoza PAC kuchunguza wa tuhuma za Escrow na kufanikiwa kulishawishi Bunge kufikia maazimio manane ya kuwashughulikia kisheria wahusika kwenye uchotwaji huo wa fedha, kumekuwapo na wito kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema kutaka pande hizo mbili zimalizane.

“Kabla ya jambo lolote kufanyika, ili kukata kiu ya Watanzania wanaotaka kuona tunaondoa tofauti zetu, ni lazima kusema ukweli na kila upande kuwa tayari kuomba radhi hadharani pindi ikibainika ulifanya makosa,” alisema Zitto alipotakiwa kuzungumzia harakati hizo za kumrejesha Chadema.

“Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini? Lakini mimi ninaona sina kosa ndani ya Chadema. Ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka makosa yangu mimi ni nini,” alisema na kuongeza:

“Nitakuwa tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa na kama ikibainika chama kilifanya makosa, nacho kiwe tayari kuomba radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano.

“Kama hakutakuwa na ukweli itakuwa vigumu kupata mwafaka. Mimi sina tatizo. Nirudie nilivyosema bungeni kuwa nina-miss sana (ninapenda sana kuwamo kwenye) harakati za mageuzi kipindi hiki za kuiondoa CCM madarakani.”

Batuli: Mtunisi Hana Mvuto Kwangu, Nimepata Mzungu

0
0
Msanii ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mwigizaji Nice Mohammed ‘ Mtunis ’ aitwaye batuli, amemchana zilipendwa wake huyo kwa kumwambia hana
mvuto!

Kuonesha msisitizo, Batuli alisema kwa Mtunis ilikuwa ni kama daraja tu , alishapita hivyo hana mpango naye tena kwani tayari amepata mchumba wa Kizungu , raia wa nchi moja barani Afrika, ambaye muda wowote atamtangaza kuwa mume wake .

Alisema anaamini kwamba si kila jambo lililowahi kumtokea lina maana kwake kwani hata kutoka na Mtunis ilikuwa ni kipindi cha muda mfupi na mchumba wake wa sasa ana mvuto zaidi kuliko zilipendwa wake huyo .

Akizidi kumwagia sifa mpenzi wake wa sasa ,Batuli alisema anajivunia kuwa ni mtu sahihi kwake, ni mfanyabiashara mkubwa kutoka nje na Bongo ana kampuni nyingine kubwa hivyo si mtu wa maisha duni kama wengine .

“Mtunis wapi bwana sasa hivi kwangu ? Hana mvuto na kama niliwahi kutoka naye basi kipindi kile , sasa hivi kiukweli nipo na wanaume ambaye nampenda na muda ukifika , ataniweka ndani, kila mmoja atamjua, ” alisema Batuli.

Video ya Ngono ya Zari the Boss Lady imevuja Rasmi kwenye Mitandao

0
0
Yule Mdada tajiri, Mjasiriamali na anayeaminika kuwa ni mrembo mwenye mkwanja mrefu zaidi Afrika Mashariki, Zari Hassan almaarufu kama ZARI The BossLady, amekwaa skandali mpya kufuatia video zake za utupu akiwa kwenye tendo la kitandani na mwanaume ambaye bado hajafahamika ni nani (sura yake haitokezi).

Zari amefanikiwa kupata 'recognition' katika vyombo vya habari vya Bongo kufuatia madai yanayoendelea kuzagaa kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongofleva nambari moja kwa sasa , Diamond Platnumz.

Habari ikufikie kwamba hii ndio skendo nambari moja kwa celebrity huyu wa Uganda kwa sasa.

Mafundi Wapigwa na Kudhalilishwa Kwa Kuachwa Uchi Wakidaiwa Kuhusika na Wizi Nyumbani Kwa Wema

0
0
Nyumbani kwa  muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.

Wema akiwa ndani

Kwamujibu wa  Bongo5.com ambao walizungumza jana na jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.

“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”

“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa! Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo. Wema na ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana,” ameongeza mama huyo.

“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,” alisema Mama Steve.

Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. “Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,” alisema.

Kwamujibu wa Bongo5.com,mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini hakupatikana ilikuthibitisha na kutujuza kile kinachoendelea katika sakata hili.

Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, aliiambia Bongo5.com kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo. “Yeah kuna tukio limetokwa,lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo,” alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.

Wanaume Tunachangia Sana Wanawake Kuwa Malaya

0
0
Nyumbani kwa  muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.

Wema akiwa ndani

Kwamujibu wa  Bongo5.com ambao walizungumza jana na jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.

“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”

“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa! Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo. Wema na ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana,” ameongeza mama huyo.

“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,” alisema Mama Steve.

Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. “Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,” alisema.

Kwamujibu wa Bongo5.com,mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini hakupatikana ilikuthibitisha na kutujuza kile kinachoendelea katika sakata hili.

Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, aliiambia Bongo5.com kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo. “Yeah kuna tukio limetokwa,lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo,” alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.

Ukistaajabu ya Wema na Diamond, Utayaona ya Chriss Brown na Karrueche

0
0
Aiseee nimepitia mitandao kadhaa pamoja na page ya bwana mkubwa Chriss Brown aisee ni sheeda, kamchana huyu bi dada karrueche, naskia kagonoka na Drake. Pitia clip hii Youtube juzi ijumaa kwenye show yake akatangaza yu Single na kumporomoshea mitusi bi shost loh!

Kweli ukistaajabu ya project utayaona ya Zari Ze Boss Lady!
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images