Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Uchaguzi wa serikali za mtaa: Wakurugenzi Watano Wafukuzwa Kazi

$
0
0
Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana
na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.

Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu,
Serengeti, Sengerema na Bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na wa Manispaa ya Sumbawanga.

Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine
watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.

MY TAKE 
mwaka huu kila mtu atakuwa mamluki nabadooooo

Jaji Frederick Werema awakatia simu Sauti ya Amerika

$
0
0
Mwanasheria Mkuu aliyejiuzulu Jaji Fredrick Werema Amekata simu aliyopigiwa na Sauti ya Amerika walikuwa wanataka kujua kama kweli kweli Kajiuzulu. Walipiga simu wakamsalimia, badala ya kujibu salamu yeye kama Asante. Wakamuuliza tena, Tunasikia umejiuzulu kiti chako chako, Yeye akajibu sikua na kiti kisha akakata simu.

 Bonyeza Hapa Kusikiliza:

Rais Kikwete alaumiwa CCM kupoteza viti Uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete, ametupiwa lawama na makada wa CCM kwa kusababisha kushindwa CCM viti vingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, kutokana kuchelewa kutoa maamuzi juu ya sakata la wizi wa Tsh 306 bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Liyewahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini, Lapilali Ole Molloiment alisema kitendo cha Rais Kikwete kuchelewa kutoa maamuzi, katika sakata la Escrow kumechangia sana kuondoa imani ya wananchi kwa CCM.

"Kama Bunge letu, tayari lilitoa mapendekezo, kwanini Rais amechelewa kutoa maamuzi, hili ni tatizo ambalo limechangia CCM kushindwa,"alisema.

Alisema Watanzania wa sasa ni tofauti na zamani, wanajua vitu vingi hivyo, ni vigumu kuwaficha mambo ambayo yapo wazi na ambayo yanagusa maisha yao.

"Mimi ninachoona washauri wa Rais ndio wanampotosha hili suala la Escrow, jambo hili lilitawala kampeni za Ukawa, hivyo ilipaswa kulifanyia maamuzi mapema na kuzima maneno kuwa CCM inawatetea waliohusika,"alisema.

"Mimi ni Kada wa CCM, nasema tusipobadilika na kuwaondoa wachache wanaotuvuruga, tujiandae kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2015,"alisema.

Kada Mwingine wa CCM, Joram Kaaya alisema, matokeo wa Uchaguzi wa Serikali za mtaa yana maana kubwa kwa uchaguzi ujao hivyo, ni muhimu kwa CCM kujipanga.

"Lazima CCM tujipange haiwezekani watu wachache wavuruge chama alafu tubaki, mimi naungana na Katibu Mkuu wetu, Kinana wote waliohusika na haya mambo ya Escrow waondoke,” alisema Kaaya.

Chanzo:Mwananchi

Miss World na uhalisia Wake, Kamati ya Miss Tanzania Wanacho cha Kujifunza?

$
0
0
Kwa mara ya kwanza nimeamua kuangalia mashindano ya Miss World lengo likiwa kujua ni wasichana wa aina gani wanaenda huko na vitu gani hasa wanavipa kipaumbele. Ukweli usiopingika ni kwamba shindano hili limejikita sana kwenye personal abilities mfano talents, uwezo wa kufanya kwa vitendo matendo ya kuhudumia watu/jamii wanaokuzunguka/inayokuzunguka au unaowawakilisha (huduma kwa nchi yako), practical problem solving skills, namna mrembo ameinspire vijana wenzake (kwa vitendo) na kwenye uwezo wa kujieleza.

Ni beauty with purpose na talents. Physical appearance imechukua nafasi ndogo sana. (mfano Miss sudan kusini wa mwaka huu alikuwa wakawaida kabisa ila alifika top 10, kenya alikuwa wa kawaida pia ila top 10 alifika kwa kujihusisha na kuihudumia jamii) Hii imenifanya kuyathamini mashindano haya kutokana na kwamba kumbe nchi ikiwa na muwakilishi mwenye upeo na sifa husika anaweza kuibadilisha jamii kwa kiwango kikubwa sana kwani kuna kampuni kubwa nyuma yake inayomuwezesha kufanikisha haya. 

Mfano mzuri ni Miss India wa mwaka 1994 ambaye ameweza kushinda tunzo mbalimbali za kimataifa na kuwezeshwa kutekeleza shuhuli za maendeleo ya jamii kimataifa na kitaifa. 

Kulingana na ambavyo haya mashindano yanaendeshwa kitaifa hapa Tanzania kamwe hatutaweza kushinda. hii ni kutokana na ukweli kwamba vigezo vya kimataifa havizingatiwi rushwa imewekwa mbele, wanaangalia zaidi muonekano na si pamoja na upeo wa hali ya juu, hawaangalii mshiriki ameigusa vipi jamii kwa vitendo na talents zake (huenda talents wanaangalia ila si serious sana), shindano linaonekana la kihuni sana kulingana na waandaji kutokuwa serious na kuzingatia maadili ya kazi, na pia kubebana. 

Ninakiri kwamba Miss world ni nafasi nyingine ambayo kama Tanzania itaamua kuitumia vizuri uwezekano wa kuchangia kwenye juhudi za kuuondoa umasikini kwa kugusa jamii kubwa ya watanzania unawezekana. Fursa hii itatumika tu pale ambapo kamati ya miss tanzania kuanzia vitongoji itakuwa makini kwenye kuwapata washiriki na kuepukana na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa ujumla. 

kama ambavyo diamond anaitangaza tanzania kimuziki, Miss world ni sehemu nyingine ya kuitumia ipasavyo kwani ni njia nyingine tunayoweza kuitumia kugusa jamii na kupunguza umasikini uliokithiri. 

Mwisho Mashindano haya sio uhuni (kama ambavyo wengi wanayachukulia) bali waandaaji ndio wanafanya tuyaone ni ya kihuni kwa kutozingatia vigezo.

Picha: Waziri Mwanamke wa Jamaica azua Mjadala Mtandaoni kwa Kupost Picha Akiwa Nusu Utupu

$
0
0
Waziri wa Vijana na Utamaduni wa Jamaica , Lisa Hannah amezua mjadala kwa kupost picha akiwa amevaa bikini na top yenye picha ya Bob Marley.

Lisa ambaye amewahi kuwa Miss World mwaka 1993, alipost picha hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook na kusababisha mjadala juu ya picha hiyo, wengine wakisema sio sahihi kwa kiongozi ambaye ni mbunge na waziri kufanya hivyo, huku wengine wakisema ni sawa.


Baadhi ya maoni:

Andrea Barrett
Whats wrong with it..is she wearing swim suit to parliament???? Isn’t the attire appropriate for the place she is at????? oh please!!!!!!!!

Edwin Walton
A little too revealing for a lady in her position, extremely beautiful no doubt but remember, she is the minister… and should be setting an example for the young ladies to look up to her.

Annette Apple Green
“The minister does not seem too acutely aware of her public persona… very nice but i think she should resist the urge to display these photos.”

Corinne Matheson
Sorry at my age I never have that physique. I wouldn’t have on anything. Leave her alone let she show it off, cho, every damn thing bother oonu

Don Crichton
Minister… I hardly noticed the bikini … what I am seeing is a woman who is in a very powerful place mentally… and more importantly .. Spiritually.

Keddy-ann Batson
Mi say I don’t know what do some people. You can’t please them….she’s at the beach for god sakes.

Source: Jamaica-gleaner

Idris Awapiga Chini Goitse na Ellah na Kumtambulisha Rasmi Samantha Ukweni!

$
0
0
Mr Lover Man kwa sauti ya IK, Idris Sultan ameamua kuchagua moja (kwa sauti ya Fid Q). 

Baada ya kubadilisha title na kuwa milionea, Idris ameamua kumleta nyumbani mrembo wa Afrika Kusini, Samantha au kwa lugha ya vijana wa kisasa ameamua kumfanya ‘main chick’ na kutuachia kitendawili kama Goitse Kgaswane wa Botswana na Ellah wa Uganda watakuwa ‘side chicks’ ama wamepokea kibuti rasmi.

    Shocked by the size of this pineapple though. I feel like my whole life has been a lie. #tanzanianthings pic.twitter.com/MT9eAOP6PA

    — Samantha BBA HotShot (@SamanthaJay17) December 16, 2014


Samantha alitua Dar Jumatatu hii na mwenyeji wake amekuwa akimzungusha kwenye kwenye maeneo muhimu ya mji huu wenye joto kama jangwa la Kalahari. Na Samantha ameweka wazi rasmi kuwa anaipenda Tanzania.


    Tanzania nakupenda Sana 

Diamond: Sina Beef na Davido, Watu Walinielewa Vibaya Tu!

$
0
0
Akiongea na waandishi wa habari jana baada ya kuwasili jijini Kampala, Uganda kwaajili ya kutumbuiza kwenye party ya mpenzi wake mpya, Zari The Bosslady, Diamond alisema watu walichukulia tofauti kauli yake.

“Professionally hakuna kitu kama hicho, hatuna beef yoyote,” alisema. “Ni kwamba tu nadhani watu walichukulia visivyo. Hiyo ilikuwa ni lugha ya kisanii na watu waliitafsiri tofauti lakini hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.

Diamond anazungumzia kauli yake aliyosema usiku wa fainali za Big Brother baada ya yeye pia kutwaa tuzo ya TFA ya huko Nigeria.

“Thanks God, we have Cheated another one on The Future Awards Africa in Lagos Nigeria… #SameDay #SameNight Thank you Allah,” aliandika kujibu tweet ya Davido ilisomeka: And They cheat Again.. Lol.”

Katika hatua nyingine, akiongea na Ugandan Allstar, Diamond Platnumz alidai kuwa baba yake Mzee Abdul ana asili ya Uganda. “Ni kama nipo nyumbani sasa hivi,”alisema.

“Sikujua kuhusu hilo, baba yangu anatokea hapa (Uganda).”

Prof. Tibaijuka Akataa Kujiuzulu, Asema Kujiuzulu Sio Fasheni

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, akiongea na wanahabari hivi punde ndani ya Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam amesema haoni sababu ya kujiuzulu kutokana na sakata la akaunti ya Escrow.

Aongeza kuwa watu wanaona suala la kujiuzulu kama fasheni ila yeye hayupo katika fasheni hiyo.

Mimba ya Aunty Ezekiel Yazua Mambo, Mke wa Mwanaume Anayesadikika Kampa Mimba Aunty Aropokwa Haya

$
0
0
SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa mjamzito, mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezua balaa baada ya mwanamke anayedaiwa kuibiwa bwana na mwigizaji huyo anayefahamika kwa jina la Mwengi kuibuka na kufunguka mazito.

Mwengi ambaye yupo ndani ya bifu zito na mwigizaji huyo, alizaa na dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo ‘Moze’ ambaye sasa inasemekana amekolezwa vilivyo na penzi la Aunt.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, siku chache zilizopita Mwengi alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo alitupia picha kibao zikimuonesha akilishana keki na Moze kuashiria kwamba wana mahaba niue huku akisindikiza na ujumbe huo wa kumtisha Aunt.

Kazi kwako shangazi hii ndiyo bethidei halali familia imetimia, toto langu la maana siyo wewe uliyetoa mimba kibao tutaona na hiyo mimba kama mtoto atazaliwa, haya mume wangu miye kazana kumchuna pesa huyo shangazi uniletee tutumie atakalia kuchunwa tu yeye shangazi kazi yake si kutoa,” aliandika Mwengi.

Mapaparazi wetu walipomtafuta Aunt ili kusikia anamzungumziaje Mwengi ambaye amemtupia madongo ya kutosha, simu yake iliita bila kupokelewa.

Johari: Kizazi Changu Kinafanya Kazi Namsubiri Mwanaume wa Kunifungua tu Akishanioa

$
0
0
Na Laurent Samatta
PAMOJA na tetesi kuwa nguli wa filamu za Kibongo Blandina Chagula ‘Johari’, ameshindwa kushika mimba, mwenyewe ameamua kufunguka na kudai kuwa kizazi chake kinafanya kazi na anachosubiri ni kumpata mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa ndipo atakaporuhusu kuzalishwa.

Akizungumza na Amani, Johari alisema kuwa endapo akitokea tayari yupo ndani ya ndoa anaweza kufanya hivyo lakini kwa maneno ya watu kamwe watasubiri kwani anaamini kizazi chake kipo imara na wakati wowote akiamua kushika mimba kitafanya kazi.

“Kizazi changu kinafanya kazi na mipango hiyo ya kushika mimba mimi siwezi kukubali nipate mtoto kabla ya kuolewa, suala la kufanya jambo kwa lengo la kuwafurahisha watu mimi siwezi kufanya hivyo,” alisema Johari.
GPL

Lemutuz Amnasa Lulu Michael, Wala Bata la Kufa Mtu kwenye Hotel ya Kifahari

$
0
0
Mrembo na mwigizaji wa filamu hapa Bongo, Elizabeth Michael aka Lulu jana alionekana viwanja vya Hilton Double Tree Hotel  akiwa anavinjali na mzee mzima Le Mutuz anaejiita “The King Of All Bongo Social Media Network”.

Wakiwa kwenye viwanja vya hotelini hapo wakiwa wenye nyuso za furaha na mbele yao kuna meza yenye glass mbili za vinywaji, Le Mutuz ambae jina lake halisi ni Wiliam Malecela alizitupia picha hizi mtandaoni na wakiwa katika mpozi mbalimbali na kuandika;

Leo ni all my Super Friend Actress Super Star Lulu U know nampendazzzz mpaka naumwa U know she is just sweet chick U know and smart no nonsense baby! - le Mutuz”
Tofauti na zile za Wema na Van Vicker, Hizi watu wengi hawajazitilia shaka juu ya nini kinaendelea kati yao kwani wengi wanamjiua Le Mutuz nimpenda kupiga  na watu mastaa,maarufu na hadi wakwaida lakini hasa mabebezz …..U Know.

Van Vicker Ashangazwa na Habari za Yeye Kutoka na Wema Sepetu

$
0
0
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker ameshangazwa na vyombo vya habari za udaku za hapa Bongo, kwa kile ambacho kimelipotiwa kuhusu yeye na muigizaji Wema Sepetu.

Kwenye blogs na magazeti mbalimbali ya udaku hapa Bongo zilijaa habari za kuwa Wema na Van Vicker mbali kucheza movie kuna mambo mambo walifanya eti kwa sababu tu Wema ameachana na aliekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz na hivyo alitaka kumrusha roho, kitu ambacho hakina ukweli wowote.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM, Van Vicker aliweka picha hiyo hapo juu na kui-caption

We are in the news in Tanzania...but the headline tho. Lol@wemasepetu

Akionyesha kuchekeshwa na vichwa vya habari zilizoenea hapa bongo kuhusu yeye na Wema.

Sasa sijui kuna watu wamemsomea mastori ya kutoka kwenye lile jumba kongwe la udaku hapa nchini.

Kajala Akunwa na Waimbaji wa Skylight Band Amwaga Mipesa Jukwaani Mpaka Back Stage

$
0
0
Msanii wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.
 Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.
Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.

Diamond Amwaga Ukweli 'Wema, Jokate, Penny Hawakutaka Kuzaa Na Mimi'

$
0
0
Akizungumza kwenye kipindi cha Live Chumba cha Habari kinachorushwa na Global TV online, Msanii wa muziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alieleza jinsi wapenzi wake wazamani ambao ni Mwigizaji Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na matangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Diamond alifunguka baada ya kuulizwa kwamba amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana hata wa dawa licha ya kuwa na uhusiano  na wanawake tofoutitofauti.

Diamond: “Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana.“Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa real (hawakumaanisha) hivyo wakawa wanachengachenga.”

Diamond aliendelea kueleza kuwa mwanadada Penny aliwahi kupata ujauzito wake mara mbili.

 “Ukweli Penny ningezaa naye, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake niikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia. Siku mbili tatu akasema mimba imetoka.

“Nikaja nikamjaza kingine cha pili (mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana.“Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu. Mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye.

“Lakini kusema ukweli kabisa natamani sana kuwa na mtoto.
“Hapo juzikati nilitaka kuoa, kila kitu kilikuwa sawa, nikaja kubadili mawazo.”
Swali: ”Ulitaka kumuoa nani?”Diamond: “Ah! Siwezi kumsema hapa. Diamond alimaliza.

Kifo cha Aisha Madinda Chazua Utata, Mengi Yaibuka..Ndugu Wataka Ufanyike Uchunguzi wa Kina

$
0
0
MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.

YALIYOSEMWA
Akizungumza kwenye msiba wa mnenguaji huyo nyota nyumbani kulikokuwa na kilio, Kigamboni jijini Dar, mwombolezaji mmoja ambaye ni mtu wa karibu na marehemu alisema:

“Unajua siku za karibuni, Aisha alirudia kubwia unga kama zamani, sasa majuzi mimi nilikutana naye akasema yuko kwa rafiki yake, Mwananyamala (Dar), lakini huyo rafiki aliyenitajia ni mmbwia unga mkubwa na amekuwa akiwadunga sindano wenzake.

“Sasa si unajua kwamba, sindano zile ukidungwa bila kipimo ni sumu mwilini. Uwezekano ni mkubwa kwamba, sindano alizodungwa na mwenzake ndizo zimechukua uhai wake,” kilidai chanzo hicho.

CHANZO KINGINE
Kwa mujibu wa chanzo kingine msibani hapo, upo wasiwasi kwamba tangu Aisha arejee Bongo akitokea Dubai kuna mtu amekuwa akimtishia maisha kwamba atamtoa roho.
Chanzo hicho kilidai kwamba, staa huyo ambaye alirudi akiwa vizuri amekuwa akipewa vitisho na mtu huyo bila kutaja sababu.

SIKU YA KIFO
Siku ya tukio, juzi Jumatano, habari zinadai kwamba, Mkurugenzi wa Vipindi wa Radio Clouds FM, Ruge Mutahaba alipigiwa simu na daktari mmoja wa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala na kuambiwa kuwa, kuna mwili wa mtu anayefanana na Aisha Madinda umetelekezwa hospitalini hapo na watu wasiojulikana na wameondoka.

Baada ya taarifa hizo, Ruge alimwendea hewani Bosi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka na kumjulisha madai ya daktari.
“Asha Baraka alikuwa Kigoma. Kwa hiyo alipopewa taarifa hizo alimpigia simu kiongozi wa wanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Nyoni Mbutu na kumpa maelekezo kwamba afuatilie habari alizoambiwa na Ruge kama ni kweli.”
AISHA MADINDA NDANI YA MOCHWARI
Ikazidi kudaiwa kuwa, Luiza na wanamuziki wenzake, Lilian Tungaraza ‘Lilian Intaneti’ na Maria Soloma walifunga safari hadi Mwananyamala na kuukuta mwili wa Aisha ukiwa tayari mochwari, wakamjulisha Asha ambaye  alifunga safari na machozi juu kurejea Dar.

MTOTO WA MAREHEMU, ANAITWA NAOMI
Akizungumza na gazeti hili ndani ya Hospitali ya Mwananyamala muda mfupi baada ya mwili wa mama yake kuingizwa mochwari, binti wa Aisha, Naomi  huku akimwaga machozi, alisema:
“Mama alikuwa akiishi Kigamboni siku za karibuni. Mimi pia nikaamua kwenda kuishi naye.”
Akaendelea: “Kuna kama siku tatu nyuma mama hakuwa akilala nyumbani, jana (Jumanne sasa), asubuhi mama alinitumia meseji akisema anaomba nimtumie pesa, nikamtumia.

“Lakini leo (juzi, Jumatano) mchanamchana nilisema nimpigie simu mama nimuulize huko aliko anaendeleaje? Kabla sijafanya hivyo, mama mkubwa alinitumia meseji na kuniambia mama amefariki dunia, ndiyo nikaja huku.”

KIKAO CHA FAMILIA AELEZEA KIFO CHAKE!
Binti huyo aliendelea kusema kuwa, siku za karibu, marehemu aliwahi kuwaita ndugu zake na kuwapa ujumbe wa ajabu.
“Kuna siku aliwaita ndugu zake nyumbani akasema katika familia yetu wote, mimi ndiyo nitakayeanza kufa. Sijui mama alijua atakufa ndiyo maana akasema vile,” alisema binti huyo.

MASWALI YA MSINGI
Mpaka sasa maswali ambayo yalitawala msibani ni haya! Je, ni nani aliyeufikisha mwili wa marehemu Hospitali ya Mwananyamala na kuutelekeza? Je, dokta alijuaje kuwa alikuwa Aisha Madinda?
Je, mwili wake ulipelekwa hospitalini hapo na mtu mmoja au wengi? Walitumia usafiri gani? Bajaj au teksi? Ni vyema pia polisi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar wakafuatilia kifo hiki kwa undani.

Inna lillah, wainna ilaih rajiuun!
GPL


Video ya Zari The Boss Lady Akijishebedua Baada ya Kumwona Diamond Platnumz Iko Hapa.

$
0
0


Wakati siku ya Jana msanii Diamond Platnumz yuko ndani ya Uganda kwa ajili ya show ya Zari the bos lady kutoka Uganda, mapokezi yake yalikuwa ya laana, licha ya magari lakin hiyo furaha aliyokuwepo nayo zari ilikuwa imepitiliza yani mpka mwenyewe alikiri lakini story zikawa zinavuma kwenye blogs facebook na twitter lakin hukufanikiwa kuona video nimekuwekea hapa video


Baadhi ya Picha zilizochukuliwa usiku wa Show yZari_AllWhite_CirocParty Hizi Hapa

$
0
0
 Baadhi ya Picha zilizochukuliwa usiku wa Show yZari_AllWhite_CirocParty Hizi Hapa





Shocking:Aliyekuwa Mke wa Mbunge Mh. Sugu Faiza Ally Atoa Mpya..Avaa Pampers Siku ya Sikukuu ya Kuzaliwa Kwake na Kutinga Ukumbini

$
0
0


Wanasema ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni. Katika hali isiyo ya kawaida, mchumba wa zamani wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza Ally, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuvaa diapers!!

Sherehe hiyo ilifanyika juzi kwenye hoteli ya Seacliff na kuhudhuriwa na wageni kibao. Je ni sawa?

Dully Sykes Awachana Watangazaji wa Kenya Kwa Kutopiga Nyimbo za Wasanii Wao Redioni, Awaita Wanaigeria Wezi

$
0
0
Popular Tanzanian musician Dully Sykes bashed Nigerian artists and Kenyan radio presenters recently during an interview on PiliPili FM.

Dully was speaking with presenters Chris and Chigulu on the 'Mwake Mwake Number One Drive Show' when he addressed the matter of local stations not playing local music and instead promoting foreign and Nigerian music.

"You presenters should change and lookout for your local artists. When you start playing music from out there, your local acts lose market because you wait for people to get the music elsewhere so that you can play the music.... Nigerian music, did they search for it from Google? They heard it on air, where do they request the songs? isn't it on radio?

Nigerians are everywhere.. they can even use witchcraft to advance their careers. Let us take it back to the way it used to  be..." he said at the interview.

 He claims that Nigerians are evil, selfish and thieves because they do not make their investments in Kenya. They make money in Kenya and go spend it in their own country which is not good for the country's economy.

Listen to the full interview below:

Charles Mihayo,Mtanzania aliyewauwa watoto wake wawili Australia ahukumiwa kifungo cha maisha

$
0
0


Charles Mihayo, (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi April, 20, 2014 aliwauwa watoto wake wawili wadogo wa kike nyumbani kwake huko Melbourne, Australia (Ingia hapa) amehukumiwa kifungo cha maisha.

Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.

Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia, na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema “tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.

Baada ya kufanya mauaji Mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi ambao baada ya kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia , “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama yao] sababu.”

Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.

Licha ya kuhukumiwa kifungu cha maisha, Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images