Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Ray C Hana Hamu na Panya Road , Wamfanyizia Kitu Mbaya Akimbia Polisi Bila Viatu

0
0
Juzi Mambo yalikuwa si Mambo katikati ya Jiji la Dar baada ya Vijana Wanaojiita Panya Road Kufanya Fujo Mitaa ya Sinza, Magomeni na Mwananyamala , Mmoja wa wahanga wa Fujo hizi ni Mwanamuziki Ray c..

Hichi Ndicho Kilichomtokea:

"Sina hamu na hawa panya road, jana nilikuwa sehemu flani sinza nakula kitimoto nilivyoona watu wanakimbia nikatoka nduki bila viatu nikaingia kwenye gari mbio mara mbele yangu nikakutana na lundo la watu wakinoa mapanga barabarani, niligeuza gari utafikiri niko kwenye movie nikajikuta nimefika osterbay polisi bila viatu mpaka askari wakanicheka! !!!!!!!!!!Serikali tunaomba mkamate hawa vijana kwakweli maana tumezoea amani sasa mambo kama haya yakitokea yanakosesha amani kabisa kwa wananchi!Na uhakika Jeshi la polisi litafanya kazi yake yani nilijihisi kama niko Rwanda maana nakumbuka mapanga yale niliwahi yaona kwenye muvi ya Somewhere in April na Hotel Rwanda!!!!Sasa wale waliosema bora damu imwagike nadhani kauli itabadilika maana kama Panya Road wanatupelekesha hivi je hiyo Vita!!!, Je hiyo vita, si tutapanda juu ya nyumba zetu!!!!! Jamani msicheze na haya mambo jamani, amani ndio sifa kuu ya nchi yetu........Eeh Mungu tuepushe na haya mambo....." Ray C


Breaking News:Mtoto wa Kiume wa Raila Odinga Akutwa Ameuawa Nairobi

0
0
Fidel Odinga Mtoto Mkubwa wa kiume wa Mwanasiasa maarufu nchini kenya Raila Odinga amekutwa amefariki ndani ya chumba chake alimokuwa amelala leo alfajiri, Police nchini kenya muda huu wanaendelea na uchunguzi mkali kubaini chanzo kama kinahusiana na mambo ya siasa, Hivi karibuni Raila Odinga amekuwa akiibana na kuishurtumu Serikali ya Kenyata kwa kushindwa kuwalinda wakenya hasa kutokana na mauaji ya Al shabab, Pia Wapinzani kupinga muswada ambao tayari ni sheria ya Ugaidi nchini kenya ambao Raila anaona hauwalindi wakenya. 

From Kenya-Today blog:

Fidel died at Nairobi Hospital where he was rushed by his wife last night. It is not yet known what killed hill.

Fidel had lunch with his dad on Sunday at Raila’s his Karen home. Raila told The Star this morning he was fine.

He then went out in the evening with some friends and came home at around 1am, he is said to have had breathing problems and was rushed in an ambulance to Nairobi Hospital where he died.

Raila confirmed the death of his son, he is at the scene

Msama Azungumza Kuhusu Kutokuwa na Rose Muhando, Akana Rose Muhando Kutumia Unga

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ametamka kuwa yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.


Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.

“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.

“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:

“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake.

Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.

Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,”alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.

Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.

Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.

Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.

Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” alisema Msama.

Ahadi za Jakaya Kikwete Zaitesa CCM Kuelekea Uchaguzi 2015

0
0
Ahadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi katika mikutano mbalimbali nchini  wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, huenda zikawa mwiba kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kutokana na nyingi kutokutekelezwa au kuwa katika hatua za mwanzo.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwa nyakati tofauti alitoa ahadi kusaidia kuwakwamua wananchi kutoka kwenye dimbwi la umaskini, maradhi na kuboresha upatikanaji wa elimu nchini. Ahadi hizo zilitarajiwa kukamilika kabla hajatoka madarakani.

Ikiwa imebaki takriban miezi 10 ya uongozi wa kipindi cha pili cha awamu ya nne kufikia ukomo, muda unakwenda haraka na utekelezaji wa ahadi hizo unasuasua jambo linalotia shaka iwapo kila ahadi itatekelezwa kwa wakati.

Kushindwa kutekeleza ahadi hizo ambazo zimo katika kitabu cha ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za urais 2010, kilichondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kunaiweka Serikali ya CCM katika wakati mgumu hasa pale itakaporudi kwa wananchi kutoa ahadi nyingine kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao.
~Mwananchi

Jestina George Kuwapandisha Ndege Yamoto Band Kwa Mara ya Kwanza Kwenda Kufanya Show UK

0
0
Mrembo, Blogger na Mfanyabishata Jestina George  ameingia deal na Yamoto band ya Kufanya show ya Music Jijini London Mwezi wa Pili Tarehe 21, 2015.
Jestina George Ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:

"Confirmed...21 Feb 2015..Yamoto! Yamoto! Yamoto Band Live in the UK For the first Time Ever...When we Say Live, we mean 
Live with Full Band & Dancers. This is one show that's not to be Missed... Sponsored by @officialjestinageorgeblog @bongodeejays@zuriihouseofbeauty

 It's gonna be bigger and better! UK & Europe people Save the Date. Their Live Performance is a must see..If you love live music
Make sure you get your tickets mapemaaaa...Hili ni Bonge la show kuwahi kutokea na watoto wameahidi kuweka historia" 

Soma Wazazi Walichofanya Kwa Mtoto wao Baada ya Kuibuka wa 48 Kati ya Wanafunzi 50 Katika Matokeo ya Mtihani

0
0
Wazazi wa mtoto mmoja walishindwa kuzuia furaha yao kwa mtoto wao ambaye kila mara alikuwa akishika nafasi ya mwisho darasani baada ya kuibuka nafasi ya 48 kati ya wanafunzi 50 katika matokeo ya Darasani hivyo kuwashinda wanafunzi wawili katika term hiyo .
Wazazi hao walimfanyia bonge la party kumpongeza kwa hatua hiyo pia walikwenda kutoa sadaka ya shukrani kanisani ...

Je wewe angekuwa ni mtoto wako ungemfanyia nini?

Africa Yazidi Kumtambua Diamond Platnumz, Huu ni Mchongo Mwingine Aliyopata

0
0
Diamond Platnumz ateuliwa kutumbuiza CAF
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014.
Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria.
Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo. ..... What more can i say kwa huyu kijana... Go go represent us....
#WhereistheKing????

JB Aweka Wazi Jinsi Anavyompenda Mke Wake na Kuithamini Ndoa Yake

0
0
Mwigizaji na mwogozaji wa filamu za hapa bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka ya moyoni  juu ya upendo wake kwa mke wake na kuendelea kudumisha ndoa yao.

JB tofauti na mastaa wengi wa hapa bongo, amemuweka na kumwambia waziwazi mke wake wa ndoa maneno  ya upendo ambayo huwafanya mashabiki wake wote kkujua na kumtambua shemeji yao au wifi yao.

JB leo hii ameweka picha hiyo mtandaoni akiwa na mke wake na kuandika maneno haya;

“Mke wangu,rafiki yangu, nampenda sanaa. Siku kama ya leo tuliingia kanisani tukatoa kiapo cha maisha,hakuna kilicho badilika wala kitakacho badilika mpaka kifo kitakapo tutenganisha. NAKUPENDA SANA MKEWANGU,Mungu azidi kuibariki ndoa yetu”. JB alimaliza.

Tunakupongeza JB kwakuendelea kuheshimu na kuitunza ndoa yako, tunawatakia baraka katika maisha yenu.
~Bongomovies

Ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian Hati Hati, Kanye Amnyima Kim Haki ya Tendo la Ndoa

0
0
NDOA ya Mastaa ya Wakubwa Duniani Kanye West na Kim Kardashian inaelekea pabaya kwa kile kinachoonekana ni kuchokana kimapenzi , Kim Kardashian amekaririwa na Mtandao mmoja mkubwa wa Marekani TMZ akisema kuwa West amekuwa hampi haki yake ya ndoa kama ipasavyo huku akijidai yupo busy na Kazi zake na anaporudi nyumbani huishia kucheza na mtoto kisha kulala fofo...Kim Amemtaka mumewe kuhuzuria Darasa la Ushauri nasaha wa mapenzi ili kunusuru ndoa yao....


Matokea ya Yanga na Polisi FC Kombe la Mapinduzi Haya Hapa

0
0
Team ya Yanga Imezidi Kusonga mbele na kujihakikishia Ubingwa Kwenye Kombe la Mapinduzi Baada ya Kuifunga Polisi FC mabao manne hivyo kuingia Robo fainal, Yanga kwa sasa ina mabao manane baaya ya mchezo wa Kwanza pia kupata mabao manne..

Mabao katika Mchezo wa Jana yalifungwa na Andriy Coutinho , Kper Sherman , Hamisi Tambwe na Simon Msuva.

Chadema Yawasaidia Kutoka Mahabusu Vijana Waliotembea kwa Miguu Toka Geita Mpaka Dar Kumuona Rais

0
0
Chama cha Upinzani cha Chadema Imewasaidia Vijana watatu kutoka mahabusu Baada ya Kukamatwa na Jeshi la Polis Ijumaa iliyopita, Vijana hao walitembea kwa Miguu kutoka Geita mpaka Dar es salaam huku wakiwa wamevaa magunia kwa muda wa mwezi mmoja ili kuja kumshinikiza Rais Jakaya kikwete kutatua matatizo yanayowakabili wananchi na kutumia vitega uchumi vizuri kwa faida ya kila mwananchi

Safari ya hao vijana kutoka Geita iliishia mikononi mwa polisi baada ya kufika Dar bila kutimiza lengo lao la kumuona Rais kwa kili kinachosemekana kuwa hawakufuata utaratiba unaopaswa ili kuweza kumuona Rais wa nchi hiii, chama cha Chadema baada ya kuwatoa kimesema kitahakikisha haki yao inapatikana na kama watashtakiwa basi itachukua jukumu la kuwasimamia mahakamani..

Je Mdau  wa Udaku Una Maoni Gani Kuhusu Hao Vijana Waliotembea Muda wa Mwezi mmoja na Mwisho hawakuweza kutimiza lengo lao?

Nani Zaidi Kwa Uzuri Kati ya Wema Sepetu na Zari The Lady Boss ?

0
0
Kwenye Mitandao ya Jamii Hasa Instagram kwa Sasa zimeibuka Team Mbili Kubwa zinazoshinda huko kwa Kupeana Vijembe vya Hapa na Pale Kuhusu Wema Sepetu na Mrembo Zari The Lady Boss wa Uganda, Ushandani huo wa Team Zari na Team Wema Umekuja Baada ya Mwanamuziki Diamond Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Wote hao wawili kwa Muda tofauti ambapo kwa sasa Diamond Ameweka Wazi Kuwa anatoka na Zari ...

Ubishi mmoja wapo ni kuwa nani ni mzuri wa Umbo na Sura kati ya wema Spetu na Zari , Nasisi hatuna hiyana tumeona tuwabambanishe Hapa tuone nani atapata kura nyingi ...

Haya Nani Mrembo zaidi kati ya Wema Sepetu na Zari The Lady Boss?

Mwigizaji Manaiki Sanga Akata Shauri, Aamua Kupeleka Posa Kumuoa Jack Wolper

0
0
Mwigizaji wa Bongo Movies Manaiki Sanga Amefunguka kuwa mwaka huu Ameamua kukata shauri na kuhakikisha anapeleka Posa kwa wazazi wa Jack Wolper ili kumuoa Jack , Manaiki Sanga amemwagia sifa kede kede Jack Wolper na kusema ni mwanamke mrembo sana na yupo tayari kufanya lolote ili ampate labda tu tatizo kubwa liwe kwake lakini hawezi kubadilisha nia yake.

Wanawake/Wasichana wa Aina Hii ni Hatari Sana Kuwa Nao Kimapenzi

0
0
Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..

1.Demu wako wa zamani
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi. 

5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.

Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu.

Ujumbe Toka Kanda ya Ziwa kwa Wanaume wa Dar es salaam Walioshindwa Kupigana na Panya Road

0
0
Wanaume wa dar kweli mmedhihirisha ni waoga wa kutupa. Ijumaa nyinyi wenyewe ndo mlikuwa vinara wa kutangaza hofu kuwa kuna panya-road, 
Alafu ndo wenyewe mlikuwa mstari wa mbele kufunga maduka na kukimbia hovyo hovyo hata hao panya hamjawaona. 

Ni aibu sana hii kwa mwanaume. Yaani badala ya kuhamasisha wanaume wenzenu mjitokeze kupambana na panyaroad, nyie ndio mnahamasisha watu wafunge biashara wakimbie! 

dah aibu kweli hii. Ulegevu huu huwezi kuukuta huku Kanda ya Ziwa maana kwenye dharula kama hiyo huwa kuna vitu vifuatavyo wanaume mlipashwa kufanya:

Kupiga yowe na kukusanyika kwenda kuwafyekelea mbali hao panya Road. 

Sasa basi ili muwe majasiri inabidi muache mambo ya kitoto kama:

Kunywa kahawa na kashata na joto lote lile.

Achaneni na kula pweza kuleni ugali wa mhogo na sangara.

Vitu kama ngisi, kachori na juice ya miwa vinawafanya muwe nare nare sana.

 Ni aibu kwa mwanaume kuweka chumvi pilipili na ndimu kwenye mahindi ya kuchoma au
kuweka chumvi kwenye embe.

 Acheni mara moja kula ubuyu mnajidharirisha mno.

 Komeni kuangalia tamthiliya kwenye Haya ndio baadhi ya mambo yanawafanya muwe mdebwedo wa kutupa. Mkiendelea hivi ipo Siku panya road watakuja kuomba wawekewe maji ya kuoga na wake zenu mchana kweupe na nyie mpo. Jiangalieni sana...

Zitto Aishukia EWURA Juu ya Kutoshuka kwa Bei ya Mafuta Tanzania

0
0

Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. 

Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta wakiwemo wenye daladala, mabasi wala taxi na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

EWURA, inasemekana wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi.

Kinachosikitisha ni kuwa, ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua 'bulky hazingetolewa kwetu na Mamlaka husika.

Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue.

Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu.

Hata hivyo, kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.

Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kuueleza umma ni kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia bila kutumia visingizio visivyo sahihi. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

Chanzo: Fikra Pevu

Rihanna Aanza Kazi Puma Kwa Kupost Picha Akiwa na Chupi za Puma Huku Akiwa Kifua Wazi

0
0

Mwanamuziki Rihanna Ameanza kazi yake Kwa kishindo aliyepewa na Kampuni ya Mavazi na Viatu vya Puma kama Mkuu wa ubunifu..
Amepost kwenye profile yake picha akiwa amevaa chupi za Puma , Haya wadada kazi Kwenu 

"Rihanna who is now the creative director of Puma is sure taking her job seriously. The seductive star showed off her figure in nothing but Puma briefs...
Now every lady would want to rock these"

Picha za Wolper Akifanya Mazoezi Zawa Gumzo Mtandaoni

0
0

Picha za mrembo na mwigizaji wa sinema za kibongo, Jackline Masawe ‘Wolper’ alizoziweka mtandaono akiwa nafanya mazoezi ya viungo zimezua mjadala na maswali mengi.

Wolper ambae kwasaa anaonekana  kuwa ‘Bonge’ , wiki iliyopita alitangaza kuanza kufanya mazoezi ili aurudie mwili wake wazamani,  toka juzi amekuwa akitupia mtandaoni picha hizo hapo juu  akiwa mazoezini.

Mbali na mashabiki wake wengi kumpamoyo kuwa aendelee kukomaa na mazoezi, wapo ambao waliona kama mwanadada japokuwani kweli anafanya mazoezi lakini lengo lake lingine ni kuonyesha watu tattoo zake alizojichora.

Jionee mwenyewe picha hizo, kisha toa mtazamo wako wewe umezionaje?
Chanzo:Bongomovies

After Rwanda and Burundi Zari and Diamond Platnumz to Rock Nigeria

0
0
Diamond Platnumz and Zari after the Rwanda show. Next Thursday, Diamond and his better half will be in Nigeria for the GLO-CAF awards Gala.

Zari the Boss Lady is Now Living the Life of a Super Star Than Never Before Meeting Diamond Platnumz

0
0
Zari has dated many ranging from basket ball star, LK4, muscle man Farouk Sempala and of course the father of her three children, Ivan Ssemwanga, but none of them has given her the life she has been yearning for. Ivan was close to getting her that life when she cruised the first Lamborghini in Kampala.

However, the Diamond Platnumz experience has been the epitome of Zari's relationships. She is now known in Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi and of course, she needs no introduction in Uganda.

On hooking up with the Bongo Flavour star, Zari told his followers to get ready for the "Uganda, Tanzania project" and so far, the project has been unveiled in bits and pieces..

The project kicked off with a music video that was recorded in Tanzania (we're still waiting for the video), then Zari was in South Africa with Platnumz for the Channel O Awards. One of Zari's ex-lovers tried to sabotage the relationship by leaking a s#x tape on the net, but this did not stop her.

Next, it was the All White Party which to the surprise of many was a sell out to the extent that the doors to Guvnor were closed to the public.

The couple was recently in Burundi with Zari right by Diamond's side at all times only to crown off their journey in Rwanda where they ushered in the new year with a performance at The Expo Ground on 31.Dec and another on 01.Jan at the Amahoro Grounds.

While in Rwanda, they visited the Kigali Genocide Memorial where they explained to them the history of Rwanda and the genocide of Tutsi's in 1994. Zari could not help crying after watching a short video of the Tutsi massacre.

Source:Ugandaonline
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images