Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Ajifungua Watoto Mapacha Walioungana Katika Eneo la Kifua

$
0
0
Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara, Helena Paulo (20), amejifungua watoto wawili mapacha ambao wameungana katika eneo la kifua hadi tumboni tukio ambalo limevuta hisia za mamia ya wananchi ambao wamefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kwa lengo la kutaka kushuhudia tukio hilo.

Akizungumza katika wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo Muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma, amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua Januari 5, 2015 usiku wa saa saba kwa njia ya operesheni ambapo watoto hao wenye jinsi ya kike wamezaliwa wakiwa na uzito wa kilo 4.6.


Amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Hospitali hiyo na kwamba hali ya mwanamke huyo na watoto zinaendelea vema na taratibu za kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Bugando zimekamika.

Taarifa kutoka jijini Mwanza na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasmali Watu wa hospitali hiyo, Leah Kagine, zinasema tayari mwanamke huyo na watoto wamefikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.

Picha: Ni Hatari Kuendesha Gari Wakati Umetumia Kilevi, Wawili Wafa Kwa Ajali Arusha

$
0
0


Inatisha sana jamani usiendeshe wakati umetumia kilevi.

Mke wa mmiliki wa Hotel ya Aquiline Hotel iliyopo Arusha maeneo ya Stend, amefariki hapo hapo yeye na wifi yake baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya kikatiti.

Watu waliofika eneo la tukio wanasema walikuta chupa za pombe aina ya konyagi ndani ya gari wakati wanawanasua.

Inasemekana ajali hiyo imesababishwa na wao wenyewe baada ya gari yao kuhama njia na kugongana uso kwa uso na bus la abiria.

Kibonde Amchukiza Kamanda Kova, Ni Kuhusu Panya Road - Amvaa na Amwambia Haya

$
0
0
KILE kinachoonekana watu wameanza kuchoka na Vituko vyake pamoja na Visa anavyofanya Mtangazaji Maarufu wa redio ya Clauds Fm Eprahim Kibonde, baada ya leo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaa Kamishna Suleiman Kova kumjia Juu mtangazaji huyo na kumwambia aache utoto na kama anataka umaarufu atafute njia nyengine.

Kauli hiyo Kamishna Kova imekuja siku chache baada ya Mtangazaji huyo wa Kipindi cha Jahazi kujitokeza na kusema katika Vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita zilizofanywa na Vijana wa Panya Road katika maeneo mbalimbali ya jiji hili,katika watu walikumbana adhia hiyo mtangazaji huyo alipata matatizo,baada ya kudai kupigwa na vijana hao.

Kalipio hilo la Kamishna kova ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi Habari alipokuwa akilizungumzia sakata la Panya Road,ambapo pamoja na mambo mengine huku akizungumza pasipo kumtaja jina lakini tayari waandishi wa habari walikuwa wamegundua anamlenga mtangazaji huyo,alisema inasikitisha watu wanakuwa wanapotosha umma kiasi ambacho wangetakiwa kuwa wakweli kutokana na kazi wanazofanya za kutoa habari kwa jamii.

“Hivi mtu mwenye kama Yule tena maarufu sana na jamii inapenda kumsikiliza kwenye kipindi chake kupotosha watu kwamba panya road wamemvamia inashangaza sana,maana jeshi la polisi tumechunguza tumebaini akufanyiwa kitendo chochote kabisa, bali yeye anafanya hivyo huku akitaka umaarufu wakijinga”alisema Kamishna Kova.

Kamishna kova aliongeza kuwa jamii inahitaji watu kama hao kutoa taarifa za ukweli ila inasikitisha kuona wanataka umaarufu wa kijinga ambao hauna tija katika jamii kwani umaarufu aliokuwa nao unatosha kama mtangazaji huyo anataka kujilikana zaidi atafute njia nyengine.

Katika Hatua Nyingine Kamishna Kova aliwataja Viongozi wa watatu aliowakamata ambao walihusika katika kusimamia vitendo hivyo vya kiovu ambao ni Halfani Nurdini miaka 24,mkazu wa tandale Sokoni Jijini Dar es Salaam,Said Mohamed miaka 22 naye pia ni makazi wa Tandale,

Jack Wolper Aonyesha Nguo yake ya Ndani Sidiria na Kuandika 'He Love'z My Style'

$
0
0
Kweli Mrembo na Mwigizaji Jack Wolper ni Stylish Kama Anavojiita kwenye ukurasa wake wa Instagram, Hivi Karibuni amepost picha akionyesha nguo ya ndani aina ya sidiria na Kuandika Maneno haya Hapa chini:

"People will stare .Make it Worth Their While baby. he love'z My style"

Baadhi ya Comments Katika Picha Hiyo hizi Hapa:

amani_john
kunakipindi ulikuaga unavaa vzuri cjui,sijui kwa nn umeacha kuvaa vle..

abeljy
Sweatyyy;!!!!!ee bwana we ni mzuri tuache tu unfiki

love_lucie_crazzy_baby911
Hapo sasa ..!! Me love thiss style ..! Big up kwako @wolperstylish

Sheikh Ponda Anyimwa Dhamana, Polisi Watumia Nguvu Kutuliza Wafuasi Wake

$
0
0
Sheikh Ponda Issa Ponda
Jeshi la Polisi limefanikiwa kudhibiti vurugu zilizotaka kutokea baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda kunyimwa dhamana katika kesi inayomkabili.

Tukio hilo limetokea baada ya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro kupinga maombi ya dhamana kutokana na kuwepo kwa hati iliyotolewa na mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP iliyotaka mshtakiwa huyo kutopewa dhamana.
Jeshi la polisi kwa kutumia askari kanzu na FFU waliokuwa na mbwa, silaha za moto pamoja na marungu walilazimika kuimarisha ulinzi mkali katika eneo la mahakama hiyo kwa kile kilichohofiwa kuzuka kwa vurugu baada ya Sheikh Ponda kunyimwa dhamana.
Hali ya vurugu ilionekana kujitokeza baada ya Sheikh Ponda kufikishwa mahakamani hapo majira ya saa 3: 20 asubuhi kwa kutumia gari dogo aina ya Toyota Carina na hivyo wafuasi hao wa Sheikh Ponda kutaka kuingia ndani ya mahakama hiyo kushuhudia kesi hiyo inavyoendeshwa ambapo askari mmoja alijeruhiwa mkononi kwa kuchanwa na kiwembe.

Askari walilazimika kutumia nguvu kuwazuia na kuwatuliza nje ya uzio wa mahakama huku wafuasi hao wakiendelea kusoma dua na kumuomba Mungu ili kiongozi wao aweze kuachiwa kwa dhamana.
Dhamana moja ya maombi matatu yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi Desemba 22 kupitia wakili Juma Nasoro akishirikiana na wakili Bathoromeo Tarimo na Abubakar Salimu ambao wanamtetea Sheikh Ponda katika kesi inayomkabili mahakamani hapo.
Maombi mengine yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi yalikuwa ni kubadilishwa kwa hati ya mashtaka baada ya Sheikh Ponda kushinda rufaa yake katika mahakama kuu na kupanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa zaidi saa mbili, mawakili wa pande zote mbili walionekana kutokubaliana hasa katika suala la kubadilisha hati ya mashtaka, hali iliyosababisha hakimu wa mahakama hiyo Mary Moyo kusitisha mahakama mara mbili kwa dakika 15 ili kutoa nafasi kwa mawakili hao kujadiliana na kutoa maamuzi.

Wakili Kongora alidai kuwa shitaka la kwanza linalomkabili Sheikh Ponda ni la kupinga amri halali iliyotolewa na mahakama ya kisutu Mei 9, 2013 ambayo ilitokana na hukumu iliyomtaka Sheikh Ponda kutohusika na uchochezi na badala yake kuhubiri amani.
Imedai kuwa amri hiyo ilivunjwa na Sheikh Ponda baada ya kuhusika na kutoa maneno ya uvunjifu wa amani na uchochezi kosa ambalo alilifanya katika eneo la kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro ambapo pamoja na shitaka hilo pia alishitakiwa kwa kosa la madai ya kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini nyingine na kushawishi na kutenda kosa.
Wakili Kongora alidai kuwa upande wa mashitaka utaendelea na mashtaka yote matatu na kwamba yote yataweza kuthibitishwa mahakamani hapo kupitia kwa ushahidi na hivyo aliiomba mahakama kuridhia maombi ya kusikilizwa kwa ushahidi huo Januari 26 na 27 mwaka huu.

Kuhusu dhamana hakimu Moyo amesema kuwa mshtakiwa ataendelea kukaa rumande hadi mkurugenzi wa mashtaka DPP atakapotengua maamuzi yake kupitia hati aliyoiwasilisha mahakamani hapo ya zuio la dhamana na kwamba hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kutengua hati hiyo ya DPP mpaka kesi itakapomalizika.

Breaking News:Polisi Yafyatua Mabumu Ubungo Kuzuia Vurugu

$
0
0
Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa serikali Mitaa zinafanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa na kambi ya upinzani ambayo imelalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana.

Nchemba: Wahisani Wamerejesha Misaada iliyokuwa Imesitishwa

$
0
0
Wizara ya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One. 

Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. “Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,” alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati.

Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230. 

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. 

Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

CHANZO: NIPASHE

Wakati Wengine Wakitambulisha Wapenzi Wao Ali Kiba kaanza Mwaka kwa Kuwatambulisha Watoto wake kwa Mashabiki

$
0
0
"Nawapenda sana watoto wangu! Kingine ambacho kinabeba na kita endelea kubeba uzito kwenye maisha yangu ni familia yangu na hasa watoto wangu. Wananipa FURAHA sana. Inshaallah Mwenyezi Mungu awalinde siku zote, Amin
Una lipi la kumwambia Kiba hapo?

Barabara mpya ya Msata-Bagamoyo inasambaratika hata kabla ya ufunguzi

$
0
0
Kwa mtu yeyote aliyepita barabara hii hivi karibuni, hawezi kuacha kushangaa kwa kusambaratika au kuchanika kwa hii barabara ambayo wala haijamalizika kujengwa.
nimeona kukatika huku kwa lami takriban karibu kilometa 20 au 25 hivi.

Aunty Ezekiel na Wema Sepetu Waangua Vicheko Kaburini kwa Ngwea, Wapita Njia Wawashangaa

$
0
0
Stori: Musa Mateja
INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!

Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.

ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.

ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.

CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!

Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-

WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.

Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.

WEMA AJIELEZA KWA RISASI
Baada ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”
GPL

Ewura Yasalimu Amri , Yashusha Bei ya Mafuta Kuanzia Kesho

$
0
0
The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Ewura) yesterday announced a significant reduction in fuel prices.

Prices are lowest in Dar es Salaam and its environs, where a litre of petrol will for the next month be selling for Sh1,955, down from Sh2,029, according to Ewura Director General Felix Ngalamgosi.    This translates into a price reduction of Sh74.

The price of a litre of diesel is down by Sh63 and the fuel now sells for Sh1,846 instead of Sh1,909

Kerosene, which previously retailed for Sh1,888 a litre, is now down to Sh1,833, with consumers saving Sh55 on every litre they buy.

Fuel prices are still highest in Uvinza District, Kigoma Region, where  a litre of petrol  now retails for Sh2,198, down from Sh2,272.  Diesel is down from Sh2,152 to  Sh2,089, while kerosene now retails at Sh2,076 from Sh2,131.

The price of a litre of petrol has fallen by Sh312 in Dar es Salaam between last September and this month, a reflection of the plummeting oil prices in the world market, Mr Ngalamgosi told a news conference yesterday.

Mbinu Mpya za Kusafirisha Dawa za Kulevya Zagunduliwa

$
0
0
Baadhi ya wanawake wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya China na Hong Kong, walishika ujauzito kama moja ya mbinu ya kupitisha dawa za kulevya bila kugundulika kwenye viwanja vya ndege na mipaka mingine ya kimataifa. Mwananchi limebaini.

Watanzania wanne walio katika magereza ya China na Hong Kong walijifungua watoto kwa nyakati tofauti wakiwa wanatumikia vifungo na wamekiri kuwa walibeba ujauzito kama mbinu ya kupitisha dawa hizo bila kukaguliwa.

Watoto wanaozaliwa magereza baada ya kufikisha mwaka mmoja hupelekwa katika vituo vya watoto yatima na kusomeshwa na Serikali ya China hadi pale wazazi wao watakapomaliza adhabu.

Imebainika kuwa watoto wawili wapo katika vituo hivyo, mmoja tayari yupo Tanzania baada ya bibi yake kumrejesha na mwingine bado yupo gerezani na mama yake.

Wanawake hao ambao wote wana umri wa kati ya miaka 20 na 30 walieleza masikitiko yao jinsi ambavyo wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wanavyowarubuni ili kubeba dawa hizo kwa ahadi za kuwapa fedha nyingi.

“Tunapata mimba makusudi kwa sababu tulijua kuwa katika viwanja vya ndege vingi wajawazito hawakaguliwi hasa wakiwa na mimba kwa hiyo tungebeba unga na kuupeleka China, halafu baadaye tungerudi nchini na kutoa mimba au tukiamua tunajifungua,” alisema mmoja wa wafungwa hao.

Hata hivyo, mbinu hiyo ilifanikiwa katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), lakini haikufua dafu katika viwanja vya ndege vya China, Hong Kong, Macau na Guang Zhou.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Diwani Athuman alisema hana taarifa za Watanzania hao lakini ofisi yake inafanya taratibu za kuwasiliana na China ili kujua hali za wanawake hao.

Mkurugenzi wa JNIA, Moses Malaki alisema kwa kawaida kila mtu hukaguliwa kwa uangalifu bila kujali mjamzito au la. Akielezea namna wanavyopimwa, Malaki alisema kwanza kila msafiri hupimwa kwa mashine ya kawaida ambayo hubaini uwepo wa kifaa chochote kisichotakiwa mwilini kwa mfano chuma kama hereni, bangili, mikanda lakini si ndani ya tumbo.

“Iwapo mashine ya awali itatoa mlio hata baada ya msafiri kutoa vitu vya chuma, basi atatakiwa kwenda katika chumba maalumu cha ukaguzi wa mikono,” alisema.

Kamanda wa kitengo cha Polisi cha Dawa za Kulevya, (SACP), Godfrey Nzowa alisema wapo wanawake kadhaa raia wa Zambia, Zimbabwe, Nigeria, Afrika Kusini na Malawi ambao wamefungwa katika magereza ya Tanzania kwa kusafirisha dawa za kulevya wakitumia mbinu hiyo ya ubebaji wa mimba.

Alisema mbinu hizo zinatumiwa na wanawake kwa sababu wajawazito hawakaguliwi kwa mashine za x-ray na kwamba wengi walikamatwa kutokana na taarifa za kikachero.

Kipa Juma Kaseja Ndani ya Giza Nene Yanga

$
0
0

IPO misemo mingi ambayo huashiria kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao dalili ya mvua ni mawingu.

Msemo huu unaweza ukawa na na maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar  es salaam.

Mchezaji huyo mwenye heshima kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi, lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili ya ushiriki wa kombe la shirikisho.

Matukio hayo yote yameibua maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..

Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.

“Ni vizuri tukianza kuwakumbusha wapenzi wetu tulipotoka tulipo na tunapoelekea na mimi nilipoingia nililikuta hili tatizo lipo na tulipoamua kulifuatilia na kulipatia ufumbuzi, lazima tuseme ukweli na kweli itatuweka huru, matatizo ya Juma Kaseja na Yanga yalisababishwa na yeye mwenyewe  alipoona hana kipaumbele na Yanga”.

Na hii ilitokana na kutokupangwa mara kwa mara katika michezo mingi ya Yanga tofauti na zamani watu walivyokua wakimuelewa kama kipa bora Tanzania, lakini kwa mabadiliko ambayo klabu imekua ikipitia kwa namna moja na kwa mahitaji ya timu labda yalikua hayamfurahishi Juma kama binadamu’’ alisema.

Muro ameendelea kusema kwamba “ndani ya uongozi wa yanga benchi la ufundi liliamua kumtumia Dida kutokana na uwezo wake jambo ambalo Juma hakupata nafasi kutokana na mahitaji ya timu hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki kulalamika kwa nini hapangwi”

“Lakini tuweke kumbukumbu zetu vizuri Kaseja kapangwa mechi ya Mtibwa kafungwa magoli mawili, kachezeshwa mechi dhidi ya CDA ya kirafiki na nyingine kule Shinyanga,  pia ikumbukwe wakati Juma yupo Simba na hata na Yanga alikuwa anapangwa michezo yote hadi ya kirafiki, mbona wenzake hawakulalamika hadi kuamua kuondoka?

“ Lakini kwanini watu wanahoji kipindi hiki ambacho klabu imeamua kuinua vipaji na kutafuta watu wengine wa kuchukua nafasi ya Juma …? Aliuliza Muro, na kuongeza huo ndio mgogoro na Juma na sio wa maslahi…

Kuhusiana na kutoonekana mazoezini  Muro amesema juma alipoona hapewi nafasi akaamua mwenyewe kuacha kuhudhuria mazoezi na tatizo hili lilianza taratibu.

“Ghafla Juma akasema haji mazoezini kwa sababu anaidai Yanga mara akageuka akaandika barua akasema hana matatizo na Yanga, mara mwanasheria wake akatuandikia barua ya masuala ya kisheria”

Hata hivyo, Muro amesema kuhusu ni lini Juma hajafika mazoezini aulizwe mwenyewe lakini kama hafanyi kazi hakuna atakacholipwa na wanataratibu zao.

“Hata kama una mkataba haufanyi mazoezi haulipwi na hili hatupepesi macho kama hatuna taarifa zako kutoka kwa mwalimu au daktari wa timu hatujui kuhusu mambo yako ya familia huji mazoezi hulipwi chochote na hatulipi chochote”.

Huo ni upande wa Yanga ambayo bado ina mkataba na Kaseja, mchezaji mwenyewe anasemaje! Juhudi za kumtafuta Juma Kaseja zinaendelea.
Chanzo:shaffihdauda

Mboni Masimba haogopi macho ya watu, Ujauzito Wake Waleta Gumzo

$
0
0
MTANGAZAJI wa kipindi maarufu cha The Mboni Show, Mboni Masimba amesema watu wengi wanamshangaa kwa uamuzi wake wa kubeba ujauzito, lakini anaamini yuko kwenye njia sahihi kwa sasa kwani kitendo hicho kinaweza kumtokea mwanamke yeyote.

“Mimi ni mwanamke kama wanawake wengine, kwa hiyo sidhani kama ni kitu cha ajabu sana na kama kazi nafanya kama kawaida, kuna watu ambao wapo kama mimi na wanafanya kazi mpaka miezi tisa,” alisema Mboni na kuongeza:

“Kwa nini nishindwe kufanya kazi? Kama mnavyoniona nina nguvu tu na ni mrembo pia, naamini msimu wa pili wa kipindi changu kinachoanza kuonekana leo Ijumaa TBC, hautamchosha mtazamaji kwa sababu ya hali yangu,” alisema kwa utani.

Mboni alisema kipindi chake ambacho kimelenga katika kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya Watanzania, kina mtazamo chanya ambao umeweza kuwasaidia wengi tangu alipoanza kukiandaa miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, alisema kuhama kwake katika televisheni ya awali iliyokuwa ikionyesha kipindi chake EATV, hakutazuia wala kupunguza chochote kwani ana hakimiliki ya The Mboni Show.

Zari na Diamond Mguu kwa Mguu, Mbona Haikuwa Hivyo Kwa Wema Sepetu?

$
0
0
KATIKA mambo yanawaacha hoi wapenzi wa pea ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu ‘Madam’ ni ukaribu uliopo hivi sasa kati ya Zarina Hassan maarufu kama Zari ‘ The Boss Lady’ na nyota huyo wa muziki Afrika kwa sasa.

Zari ambaye alianza kuonekana na mkali huyo katika utolewaji wa tuzo za Channel O mwezi Novemba, amekuwa akimsindikiza Diamond katika kila shoo anayokwenda hivi sasa, ukilinganisha na ilivyokuwa kwa mpenzi wake wa siku nyingi Wema Sepetu kitu ambacho kimeleta maswali mengi kichwani kwa watu kama kweli alikuwa akimpenda kwa Dhati .

Je wewe una maoni gani juu ya Hilo Swala?

Faiza:Hata Baada ya Kuzaa Naona Bado Nina Mvuto! Kudadadeki

$
0
0
Mwigizaji wa filamu alietoa kali ya  mwaka jana kwa kuvaa  Diaper  wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’ kwenye kusherekea siku yake ya kuzaliwa, Faiza Ally leo ameibuka  na picha akiwa ufukweni amevalia vinguo vya kuogelea huku pembeni akiwa na mtoto wake nakudai kuwa bado ana mvuto hata baada ya kuzaa mtoto.

“Hata baada ya kuzaa naona niko sexy ile mbaya kudadadeki!!!!” Faiza aliandika


Haya hebu jionee na umwambie kitu mama huyu mwenye mvuto.

Chanzo:Bongomovies

Diamond Apewe Ofa ya Dola 40,000 ili Amuache Zari The Lady Boss Akatunze Watoto Wake

$
0
0
Katika Hali ya Kushangaza Jana kwenye Mitandao hasa Instagram aliibuka mtu anayejiita Kinglaurenc ambae inasemekana ni rafiki wa Baba watoto wa Zari Akimtaka Mwanamuziki Diamond Kupokea Dola za Kimarekani elfu 40,000 ili amwache Zari Akalee Watoto Wake..Hii imekuja baada ya Zari muda wote kuonekana kuzunguka na Diamond katika Show zake huku akiwaacha watoto wake na baba yao South Africa.


Je wewe Mdau Unamshaurije? Achukue na kuachana na Zari ama Apotezee?

Viongozi wa Siasa Wamcharukia Rais Kikwete…..Wamtaka Afanye Maamuzi juu ya Waziri wa Nishati na Madini.

$
0
0
Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es Salaam ya kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini ambaye alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili lakini hadi leo amekaa kimya.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema suala la viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia serikali hasara au kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji ukawa ni kwa kila mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa taifa

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba suala hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya baadhi ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.

Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na kuenguliwa uteuzi wao maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi kufikia hatua ya kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio watuhumiwa wote hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.

Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa Diamond Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna Tibaijuka na kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof Muhongo

Coutinho: Maximo angenipoteza, sasa ninafuraha Yanga

$
0
0
MSIKIE kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, anachosema kwamba anafurahishwa na mfumo wa sasa wa timu yao chini ya kocha Hans Van Der Pluijm kwani unamfanya aonekane bora uwanjani tofauti na alipokuwa chini ya Mbrazili mwenzake, Marcio Maximo.

Coutinho aliliambia Mwanaspoti kuwa soka la kuzuia wakati wa Maximo lilikuwa linampa tabu na hakuufurahia mfumo huo tofauti na sasa ambapo amepewa uhuru wa kucheza kwa kushambulia.

Alisema hakuwa na amani wakati Yanga ilipokuwa chini ya Maximo kwani alikuwa anajua safari ya kurudi kwao Brazil inaweza kumkuta muda wowote kwa kuwa angeonekana wa kawaida uwanjani kama ilivyokuwa kwa Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye pia aliponzwa na mfumo wa kuzuia.

“Sikuwahi kufurahia soka wakati nipo na Maximo hapa Yanga, kwani tulikuwa tunacheza kwa kuzuia na sikupata muda mwingi wa kushambulia kwa uhuru na kazi ilikuwa kubwa ya kushuka kuzuia na wakati huohuo mpandishe mashambulizi,” alisema.
Chanzo:Mwanaspoti

Matokea ya Simba na Taifa Jang'ombe Kombe la Mapinduzi 2015 Zanzibar

$
0
0
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wametinga kwa kishindo hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi 2015 kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe uwanja wa Amaan Zanzibar usiku huu.

Ibrahim Hajib amefunga mabao  matatu ‘hat-trick’ katika dakika ya 46, 62 na 75, wakati bao la nne limefungwa na Shaban Kisiga katika dakika ya 80.
Mapema kipindi cha kwanza Simba walianza kucheza mpira wa polepole wakigongeana pasi za uhakika na kufika eneo la hatari la wapinzani wao, lakini Maguli na Sserunukama walishindwa kujipanga vizuri na kupoteza nafasi nzuri za kufunga magoli.

Kiungo wa ulinzi, Jonas Mkude alipiga pasi rahisi na fupi fupi kwa viungo washambuliaji wa Simba  na mawinga wa pembeni na kuwafanya Simba wasogee zaidi eneo la hatari wapinzani.

Mabeki wa pembeni, Mohammed Hussein (kushoto) na Hassan Ramadhan Kessy (kulia) walipandisha timu na kupiga krosi, lakini bado washambuliaji wa kati hawakuwa na mipango mizuri.

Simba walitengeneza nafasi nyingi, lakini walikuwa na tatizo la umaliziaji.

Maguli alionekana kucheza chini ya kiwango, akishindwa kumiliki mpira vizuri na kupiga mashuti, lakini kocha Kopunovic aliendelea kumwacha mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Hata hivyo, Simba walijitahidi kupiga mashuti yaliyolenga lango na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa wamepiga mashuti matano dhidi ya mawili ya wapinzani wao.

Katika kipindi hicho cha kwanza, Simba walimiliki mpira kwa asilimia 57 dhidi ya 43 za Taifa ya Jang’ombe.

Katika kipindi cha pili, Simba walianza kwa kushambulia lango la Taifa wakitafuta  bao la kuongoza.

Mapema dakika ya 46, Simba waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Ibrahim Ajibu kufuatia kuukuta mpira eneo la hatari baada ya purukushani ya mabeki wa Taifa ya Jang’ombe na Danny Sserunkuma ambapo alipiga shuti lililozama nyavuni.

Purukushani hiyo ilitokana na pasi iliyopigwa na Kessy kwa Saimon Sserunkuma aliyempatia pasi ndugu yake Danny ambaye alipambana na mabeki wa Taifa na mpira kumkuta Ajibu akiwa eneo zuri.

Dakika ya 62 almanusura aandike bao la pili akijaribu kumalizia krosi ya Simon, lakini mlinda lango wa Taifa, Karim Musa aliokoa na kuwa kona.

Katika dakika hiyo hiyo, Ajibu aliandika bao la pili kwa shuti akimalizia mpira wa kona uliochongwa na Simon.

Dakika ya 73 Ajibu alimpiga chenga Hassan Soud eneo la hatari akielekea kufunga, lakini Abdallah Haji akamuangusha na mwamuzi akaamuru mkwaju wa penalty.

Akiwa tayari ana mabao mawili, Ajibu alikwenda kupiga mkwaju huo wa penalti katika Dakika ya 75 na kufanikiwa kufunga bao safi na kuandika ‘hat-trick’ ya pili katika mashindano hayo baada ya ile ya Saimon Msuva.

Msuva alifunga mabao matatu peke yake katika mechi ya ufunguzi ya kundi A Yanga ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe.

Dakika ya 80, Shaban Kisiga aliifungia  Simba bao la nne kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya Mohammed Hussein kufanyiwa madhambi.

Mechi nyingine tatu za robo fainali zitapigwa kesho uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mechi ya mapema itaanza saa 9:00 alasiri ambapo KCC watachuana na Polisi Zanzibar.

Azam fc watashuka dimbani majira ya saa 11:00 jioni kucheza robo fainali ya tatu katika uwanja wa Amaan dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi ya mwisho itapigwa majira ya 2:15 usiku ambapo Yanga wataoneshana kazi na JKU ya Zanzibar.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images