Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

You Heard: Husein Machozi Adaiwa Talaka na Mke wake Aliyemuoa Mombasa Kwa Siri

$
0
0
Mwishoni mwa mwaka jana Husen Machozi alihojiwa na Gossip Cop Soudy Brown juu ya picha zilizo enea kwenye mitandao ya kijamii zikimwonyesha akiwa kwenye tukio linalofanana kwa asilimia mia moja na ndoa.

Husen Machozi alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa zile picha zilikua za movie aliyokodiwa kuigiza.

Sasa juzi kwenye kipindi cha XXL Segment ya You Heard mwanadada huyo alionekana kwenye picha anaolewa amejitokeza na kudai kuwa aliolewa kweli na anadai talaka yake kutoka kwa Mwanamuziki Hussein Machozi baada ya Hussein Machozi Kumkimbia na Kuanza kutanua na Wanawake wengine na kufikia hata kumtumia akiwa na hao wanawake zake .

Sikiliza You Heard hapo Bonyeza Hii link ..YOU HEARD



Baraza Kuu la Waislam Tanzania Latoa tamko la Kuikataa Katiba iliyopendekezwa

$
0
0
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KWA WATANZANIA WOTE, JUU YA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU SEHEMU YA MAREKEBISHO KWENYE SHERIA YA TAMKO LA SHERIA ZA KIISLAM

Awali ya yote tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi na vilivyomo, na Rehma na Amani zimfikie Kiongozi wa Ummah Mtume Muhammad (SAW).

Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah Wabarakatuh.

Tumekuiteni hapa kwa lengo la kueleza kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02, wa mwaka 2014 haswa kuhusu marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu. Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe 13 hadi 23 Mwezi huu wadau mbalimbali wataitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yao, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania tukiwa sehemu ya wadau muhimu tunapenda kuwaeleza kuwa mtiririko wa mchakato wa marekebisho ya sheria kwa mujibu wa muswada huu unaokusudia kutambua Mahakama za Kadhi Tanzania bara una kasoro kubwa na kwa dhati unaonesha wazi kuwa serikali haina nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi yenye hadhi kamili ya kimahakama na uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa muswada huu ni hadaa nyingine ya serikali hii ya CCM kwa Waislamu kwa sababu zifuatazo:-

1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya Mahakama ya Kadhi yana historia ya kupindishwapindishwa na serikali hii inayoundwa na CCM. Kwa mfano katika Ilani ya CCM mwaka 2005 iliahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi lakini kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni jambo la Kikatiba.

Hata hivyo mchakato wa Katiba mpya ulipokuja asilimia kubwa ya maoni ya Waislamu yalihitaji Mahakama ya Kadhi kuingizwa ndani ya Katiba, mapendekezo hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji Warioba kwa hoja kuwa katiba inayotengenezwa ni ya Muungano na suala la Mahakama ya Kadhi si la Muungano hivyo lisubiri wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika. Waislamu tukavumilia kuisubiri Katiba ya Tanganyika.

Lakini Bunge Maalum la Katiba likaikataa Katiba ya Warioba na kutunga Katiba Mpya Pendekezwa yenye mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano bila ya kuingiza Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa linaundwa na wajumbe wengi wa CCM hawakuona umuhimu wa kutimiza ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi katika katiba pendekezwa na kwa makusudi Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na wajumbe wengi wa CCM walishangilia jambo hili ili hali wanajua dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia kukiuka Ilani yao na ahadi kwa Waislamu.

Muswada huu ni sehemu nyingine ya hadaa kwa Waislamu kwani badala ya sheria kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kawaida ya uanzishwaji wa mahakama zote duniani muswada huu umeliacha jukumu hilo kwa taasisi binafsi ili hali Mahakama ya Kadhi kama zilivyo mahakama zingine ni sehemu ya chombo cha dola katika mfumo wa Mahakama yaani “the Judiciary”, hili limefanywa makusudi kutokana na kutokuwepo na nia ya dhati ya Serikali ya CCM kuanzisha na kuona Tanzania Bara kunakuwa na Mahakama ya Kadhi madhubuti na ya ukweli.

2. MUSWADA umempa mamlaka “Mufti” kuteua makadhi na kutengeneza kanuni za Uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi ili hali Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya Mufti isipokuwa uwepo wake unategemea katiba ya BAKWATA. Maana yake ni kwamba Mahakama ya Kadhi uwepo wake utategemea uwepo wa Katiba ya Bakwata inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa na mgogoro wa kikatiba Bakwata athari yake itaikumba na Mahakama ya Kadhi. Hakuna duniani mtu ambaye ofisi yake haiundwi na sheria kisha sheria ikampa mtu huyo madaraka ya kuunda chombo chenye mamlaka ya kisheria kama mahakama. Serikali ya CCM inalijua hili lakini imefanya makusudi kwa kusukumwa na nia yake ya kutopenda kuona Waislamu wanakuwa na Mahakama ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.

3. Kama tulivyoeleza hapo juu MUSWADA umempa Mufti mamlaka ya kutengeneza kanuni za uendeshaji wa Mahakama za Kadhi hili ni jambo la ajabu sana kwa ofisi ambayo haiundwi na sheria kuwa na mamlaka ya kutengeneza kanuni za kuendesha chombo cha kisheria ambacho ni Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani.

4. Kwa madaraka makubwa aliyopewa Mufti sheria haielezi ni nani mwenye mamlaka ya kumuondoa kadhi na wala haiweki sifa za kadhi na wala haiweki vigezo vinavyoweza kumuondoa kadhi yote hii inadhihirisha nia ya serikali ya CCM kuunda Mahakama ya Kadhi legelege na kiini macho.

5. MUSWADA unaeleza Waziri anayehusika na mambo ya sheria kupewa mamlaka ya kutunga taratibu za kutekeleza hukumu za Mahakama za Kadhi bila ya kushauriana na wanazuoni wa Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya muswada Mwanasheria wa Serikali ameeleza kuwa Waziri atashauriana na wanazuoni maelezo hayo ni hewa kwani si sehemu ya sheria.

6. MUSWADA umetoa hiyari kwa mtu kufungua shauri katika Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya Mahakama ya Kadhi iwe butu na kutoa mwanya wa kutokea mgongano baina ya Mahakama ya Kadhi na mahakama za kawaida ikiwa kila upande katika mgogoro utaamua kufungua shauri katika mahakama tofauti. Hili lisingewezekana kama serikali ingekuwa na nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi madhubuti.

7. MUSWADA kuitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:
MUSWAAD huu unaitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe badala ya kuendeshwa na serikali jambo ambalo halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani chombo kama mahakama kujiendesha chenyewe.

Mahakama ya Kadhi itafanya jukumu la serikali katika kutafsiri sheria za Kiislamu ambazo ni sheria halali kutumika Tanzania hakuna mantiki yoyote kwa chombo hicho kujiendesha chenyewe kama ambavyo serikali ya CCM inataka kufanya.

Isitoshe uwepo wa hii Mahakama ya Kadhi kutaipunguzia serikali mzigo na msongamano wa kesi katika mahakama za kawaida jambo ambalo serikali inapaswa kugharamia uwendeshwaji wake. Serikali kukataa kuigharamia hii Mahakama ya Kadhi ilihali katika nchi hii upande wa Zanzibar serikali inaiendesha Mahakama ya Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna nia ya kuidhoofisha mahakama hii ishindwe kujiendesha na kuwa na mahakama isiyokuwa na maana yoyote.

Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo zinaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote. Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara n.k. ni kwanini mahakama itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?

8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala la Mahakama ya Kadhi huletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila ya utekelezaji linazidi kutupa wasiwasi kwani inaonesha serikali ya CCM imeshazowea kuwacheza shere na kuwalaghai Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwa maslahi yao ya kisiasa. Tabia hii ni hatari sana kwa mustakabali na ustawi wa taifa letu.

Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo yaliyobainishwa katika taarifa hii, tunahitimisha kwa kusema:

a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) zimeukataa na kupinga mapendekezo ya marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria ya Kiislam kama lilivyo katika MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na. 02 wa mwaka 2014, mpaka utakapo andaliwa upya kwa kuhusishwa wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria wa Kiislamu waliobobea na kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na taifa kwa ujumla na pia Mahakama ya Kadhi ni lazima iingizwe katika Katiba ili kuipa uthabiti.

b) Kwa kuwa katiba inayopendekezwa haitambui Mahakama ya Kadhi na inapinga sheria yoyote inayokwenda kinyume na katiba hiyo ikiwemo Sheria za Kiislamu kwa kauli moja na kwa nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za Kiislamu (T) zitawahamasisha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA YA HAPANA katiba inayopendekezwa muda utakapofika wa kuipigia kura.

Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano mliotupa.

Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa taifa letu.

Kaimu Katibu
………………………….

Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T)

Askofu Gwajima mtetea Lowassa 'Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais'

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza amejitosa kwenye harakati za Urais kwa kutoa kauli za ukosoaji zinazowalenga baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoutaka Urais.

Katika mazungumzo yake na RAI, Gwajima alisema kauli zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba na Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya dhidi ya wanasiasa wenzao zina dhamira ovu ya kupakana matope.

Akizungumzia kauli hizo, Askofu Gwajima alisema wanasiasa wanaodai kuchukizwa na mafisadi na kusema kwamba Watanzania wasiwachague wagombea urais wanaotumia fedha, hawana hoja badala yake wanaendesha vita ya Urais.

"Kwani mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kwamba bila fedha huwezi kujenga mtandao wa Urais, ili ufanikiwe unahitaji kutumia fedha kujenga mtandao, kwa mfano unahitaji usaidizi wa watu wa Rukwa, Mwanza n.k; lazima uwe na watu huko Rukwa na Mwanza na lazima utoe fedha ili watu hao waweze kusafiri, kula na kulala."

"Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais, maneno yao yanalenga kupotosha watu kwamba wako watu fulani wasiotumia fedha, huku wakijua ukweli kwamba kila mtu anatumia fedha, kwa mfano fomu ya kuwania Urais ni shilingi milioni tano, sasa wao hizo fedha watakuwa wamezipata wapi? Kiujumla, hatua kubwa kama ya Urais inahitaji fedha," alisema.

Reginald Mengi kugombea Urais

$
0
0
Taarifa zisizo rasmi zinadai ya kuwa mwenyekiti wa IPP Dkt. Reginald Mengi ana mpango wa kugombea uraisi mwaka huu wa uchaguzi 2015.

Japo haijfahamika wazi kuwa atagombea kupitia chama gani au mgombea binafsi.

Katika kipindi cha hivi karibuni Mengi amekuwa akionekana kuwa mwiba kwa serikali kupitia maneno yake zikiwemo tweets na kupitia vyombo vyake vya habari huku akisisitiza uzalendo na uwajibikaji.

By Supu ya Mawe/Jamii Forums

Tamko Rasmi la Wanaume wa Dar Es Salaam Kuhusu Panya Road

$
0
0
Udaku Special
Baada ya kimya kidogo Ndugu zangu wote wanaume tunaoishi katika jiji hili la Dar es salaam, tumeshuhudia vibweka vya aina yake toka kwa baadhi ya vijana wanaojiita eti wanaume toka huko kanda ya ziwa kutulaani kwa kukimbia eti kuogopa panya road, niseme ukweli kwa niaba ya wanaume wote tuishio hapa hakuna aliyekimbia zaidi ilikua ni kuwatuliza kina mama watoto na wazee kutokana na woga walioingia na kuhofia kujeruhiwa na hao vijana panya road,

Sisi tulikua mstari wa mbele kuwangoja kwenye maeneo yetu ili pindi wakipita tuwashughulikie kisawasawa na si kukimbia kama baadhi ya vijana wa kanda ya ziwa walivyodai, na siku ile hatukulala hadi tulipohakikisha usalama umetulia na hali imekua shwari kabisa. Nawakaribisha wanaume wenzangu wa dar kutoa ya moyoni kwenu hapa dhidi ya udhalilishwaji huu.
Matusi na lugha chafu si msingi wa hoja hii karibuni

Zari: Sijawatelekeza watoto wangu, ninakaa nao siku 300, baba yao siku 65

$
0
0
Mrs Diamond Platnumz, Zari Ttale aka The Bosslady amesema hajawatelekeza watoto wake tofauti na watu wengi wanavyomshutumu kwakuwa siku za hivi karibuni amekuwa akiongozana na mpenzi wake huyo mpya.

Zari amesema katika mwaka hukaa na wanae kwa siku 300 na zingine zilizosalia hukaa kwa baba yao ambaye walishaachana.

That awkward moment when everyone thinks you abandoned your kids, so y’all kinda know when it’s my turn or his to have them. Smh,” alitweet.

I love my soldiers. Out of the 356 days in year am responsible for 300 days and the 65 are his….. take some chill pills. When you see me out and about its my days off…… he takes over as their dad too. How come nobody complains if not seen with the kids?,” amehoji mrembo huyo.

“Isn’t someone supposed to ask, how cme we never see him with the kids? But when it’s mummy. Hell breaks loose. Yep 300 days ain’t bad for me. We both have custody of our soldiers, we both play our roles, We have our arrangements as parents. We are ok so are our soldiers.”

So next time you see mummy out and about, Just know she has it under control her soldiers are safe and not ABANDONED. AITE?”

Aliye Mpa Diamond Offer ya Dola elfu 40 Amwache Zari ,Aja na Mpya , Adai Ameshawahi Kumlala Huddah wa Kenya

$
0
0
Hichi Ndicho kinaendelea huko Instagram , Baada ya Kumalizana kumchafua Zari sasa amehamia kwa Mrembo Huddah Monroe wa Kenya na Kudai alilala nae usiku mmoja na Kumlipa..

Hivi ndivyo alivyoandika:

"Can you be frank before God and declare how much I paid you for the Nite @huddahthebosschick. I called up and we negotiated the price. You came and we did our transaction. Im on my way to the hotel to try and get footage of us going into the room at nite and the time we left in the morning. By the way Huddah, what job to u do exactly? Men like me call you up, buy you a fast class ticket, book you into a good hotel and pay you. Thats what i did Bit..ch. Can u refund me? Bit..ches take cash so I don't have transfer proof bse i paid u cash." Says Kinglawrenc

Huddah Monroe Amjibu Kinglawrenc Baada ya Kusema Instagram kuwa Ametembea nae Kimapenzi

$
0
0

Huddah Monroe Naye Ameandika Hivi kuhusu huyu jamaa ambae alianza na Zari sasa amegeuka kwa Huddah...Jisomee Mwenyewe Hapo chini:

"After all is said and done, @Kinglawrenc needs to sit down and let us see the man behind his shady a..ss! I don't like to give my time to irrelevant people lakini Huyu pumbavu inabidi mtu amkomeshe! @kinglawrenc , your work is to disrespect women! Kazi yake huyu bwana, is to sleep with women and take videos then expose on the Internet! Before I go any further please can you POST the RECEIPT , or the BANK TRANSFER DOCUMENTS for the Range Rover you are telling Ugandans and EA you bought for me fool! What money do u have? Huyu pumbavu was brought to my hotel In SA by a friend coz he said he is a BIG FAN, only to realize he was looking for fame . I barely spent 2hrs with this faggot and his crew , I took pics with him like a Celeb and a fan then went back to my room , But he chose to use that ONE pic he has with me and say we are dating all over Ugandan news papers! Begging me to go to Uganda so that newspapers will believe we are dating! Can u afford me you bast,,rd? before you talk sh..t about a mother like Zari , please stop posting money , post a BANK STATEMENT that's what matters and that shows A REAL BOSS! And also Stop creating fake stories that u ELEVATE lives of East African female celebrities you dunno me , I don't know u! We met once, for hours at a hotel lobby and that's it! Stop looking for fame with other men's properties , cars and wives M..F grow up!" Huddah Monroe

Je kwa Maoni yako yupi Mkweli Hapo ?

CCM yalaani vurugu kuapishwa kwa viongozi Serikali za mitaa

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani vikali vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na CUF kwa viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa NEC; Itikadi na Uenezi CCM taifa, Nape Nnauye amesema vurugu hizo mbali na kuhatarisha na kuharibu mali pia zilizosababisha baadhi ya viongozi wa CCM kujeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali.

Amesema vurugu hizo zimetokea katika mkoa wa Mwanza ambapo Christopher Mgeta kutoka Mtaa wa Ibungilo na Pascal Charles wa Mtaa wa Kitangiri A katika wilaya ya Ilemela walivamiwa na kupigwa wakati wa kuapishwa.

Alieleza kuwa katika  Mkoa wa Dar es Salaam, Sultan Jeta wa mtaa wa Ukwamani katika jimbo la Kawe alifanyiwa fujo na wafuasi hao na Mtaa wa Msisiri A Kata ya Mwananyamala katika Jimbo la Kinondoni Juma Mbena alipigwa na kuvunjwa mkono.

“Katika Manispaa ya Ilala, wafuasi wa vyama vya upinzani walifanya vurugu wakati wa kuapishwa kwa viongozi wa serikali za Mitaa, jambo lililopelekea zoezi hilo kuahirishwa.

Nnauye amesema katika Mkoani Mbeya pia vurugu za aina hiyo zimetokea katika wilaya za Kyela na Rungwe ambapo wilayani Kyela zoezi la kuapisha viongozi wa serikali za mitaa lilishindika na kuahirishwa kutokana na vurugu za kurushiwa mawe zilizofanywa na wafuasi wa Chadema walioletwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Aliongeza kuwa katika Kijiji cha Ilundo wilayani Rungwe wafuasi hao wa Chadema waliwapiga mawe viongozi na wanachama wa CCM na baadae kufyeka mashamba yao ya migomba na kusababisha vijana sita kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe kwa sababu ya hasira za kushindwa uchaguzi.

“Vurugu hizi ni mwendelezo wa tabia na mazoea ya vyama vya upinzani nchini kutoheshimu na kufuata sheria na taratibu za nchi,   tabia hizi si za kiungwana na ni uthibitisho wa kuharibikiwa na kufa kwa vyama vya upinzani nchini. Mara zote wamekuwa wakikataliwa na wananchi kwa kura, wao hukataa uamuzi huo wa wananchi kwa kufanya fujo na vitimbi, ”amesema Nnauye.

Wakati haya ya kijiri kesho Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), itakutana Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kupanga ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho  itakayokutana Zanzibar Januari 13.

Aidha msemaji wa jeshi la Polisi  SSP Advera J. Bulimba  amesema jeshi hilo halitawaonea huruma wale wote watakaohusika katika vurugu, kwani litawachukulia hatua kali za kisheria, badala yake limewaasa wananchi ambao hawakuridhika na uchaguzi huo kufuata taratibu husika.
Chanzo:Mwananchi

Maelezo ya kushuka bei ya mafuta hayajitoshelezi

$
0
0
Pamoja na mamlaka husika kutoa maelezo kuhusu kushuka kwa bei ya mafuta, mjadala kuhusu bei hizo umezidi kupamba moto kila kona ya nchi kutokana na maelezo yaliyotolewa kutojitosheleza na badala yake kuacha maswali mengi yanayohitaji ufafanuzi wa kina.

Moja ya sababu zinazochochea mjadala huo ni kitendo cha Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuteremsha bei ya mafuta hayo hata baada kuwapo taarifa za muda mrefu kuhusu kuporomoka kwa bei ya mafuta hayo katika soko la dunia kutoka Dola 115 za Marekani kwa pipa hadi chini ya Dola 50 tangu Juni mwaka jana.

Ukimya wa Ewura ulikosolewa na watu wengi waliotaka kujua sababu za bei ya mafuta nchini kutoshuka kulingana na mwenendo wa soko la mafuta ghafi ulimwenguni.

Hoja ya wananchi wengi ilikuwa kwamba maelezo ya Ewura yalikuwa dhaifu, kutokana na ukweli kwamba kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana, bei ya mafuta ghafi ilishuka kutoka Dola 115 hadi Dola 56 kwa pipa, hivyo walihitaji maelezo kwa nini kushuka huko kwa bei hakukuleta unafuu wowote hapa nchini kwa kuwa bei ya zamani ndiyo iliyoendelea kutumika.

Tangu awali, Ewura ilionyesha bayana kwamba haikuwa na dhamira wala mpango wowote wa kuteremsha bei ya mafuta katika siku za karibuni.

Maelezo kwamba bei ingeshuka mwezi Februari kwa madai kwamba bei ya mafuta hushuka baada ya miezi miwili kwa sababu waagizaji huagiza mafuta mengi ambayo huchukua muda mrefu kumalizika, kwa maana kwamba wakati bei zinaanza kupungua katika soko la dunia, bado waagizaji wanakuwa na shehena kubwa ambayo haijanunuliwa.

Hoja hiyo imeonekana dhaifu kwa kuwa bei ya mafuta ilianza kushuka katika soko la dunia zaidi ya miezi sita iliyopita. Kenya, kwa mfano ilitangaza bei mpya Desemba 15.

Maelezo ya Ewura kuhusu ukokotoaji wa bei ya mafuta ghafi yanachanganya. Kama kweli mafuta safi ya petroli kwa tani katika soko la dunia imepungua kwa Dola 249 za Marekani, dizeli kwa Dola 189 na mafuta ya taa kwa Dola 180, inakuwaje bei mpya zilizotangazwa na Ewura bado ziwe juu kulinganisha na Kenya? Kwa mfano, wakati Ewura ikitangaza lita moja ya petroli itauzwa Sh1,955, nchini Kenya inauzwa Sh1,719.

Mbali ya kuwa Tanzania na Kenya ziko karibu na bandari zinazopunguza gharama za usafirishaji na zina mfumo wa asilimia 40 ya makato yasiyobadilika, bado bei za Kenya ni nafuu kuliko Tanzania.

Tunajiuliza Ewura inashindwa nini kuweka wazi mfumo wa kukokotoa bei za mafuta ili wananchi waelewe kinachoendelea kwa sababu wanayo haki hiyo. Kama bei ya mafuta ilishuka katika soko la dunia tangu Julai mwaka jana,

 fedha zilizookolewa ni kiasi gani na ziko wapi? Ipo hoja kwamba bei ya mafuta ingeshuka zaidi ya asilimia 15 kwa kutilia maanani kwamba fedha zilizookolewa ni nyingi na kwamba kiwango cha asilimia 40 ambacho Ewura inadai ni malipo ya usafirishaji na usambazaji wa mafuta kiko juu kupita kiasi.

Ndiyo maana tunasema Ewura ifanye kazi kwa uwazi na kutosubiri hadi wananchi walkalamike ndipo itoe ufafanuzi. Wananchi wanataka ufafanuzi kuhusu bei mpya za mafuta utolewe kwa wakati na uwe unajitosheleza.
Mwananchi

Mashindano ya Kukiss kwa Mara ya Kwanza Yafanyika Nchini Uganda

$
0
0
Hii inaweza kuwa ni Mara ya kwanza kuisikia ila huko Uganda kwa mara ya kwanza wakati wa siku kuu za mwaka mpya wakati wengine wakiwa kanisani huko sehemu inayoitwa Mukono limefanyika tamasha la kukisiana ambalo liliitwa The kissing festival , ambapo watu hushindana kukiss na mpenzi ama rafiki yako..Tamasha hilo limekuwa Gumzo sana nchini humo na lilivuta hisia za watu wengi sana wakiwemo pia waliolipinga na kusema halina maadili katika jamii..
Soon Tamasha Hili Litakuja Bongo , Trust Me....

Kama Unataka Kufurahia Mapenzi oa Mwanamke Asiye na Kazi

$
0
0
Wanawake wasio na Kazi wanakua hawana mambo mengi. Ukitoka kwenye mihangaiko yako anakupokea na kukukaribisha Nyumbani kwa furaha. Utakuta chakula kishaiva, utakuta Watoto wasafi kama mmebahatika kuwa nao, hata ukimuachia hela ya matumizi anatumia Vizuri tena unampa hela kwa furaha kabisa. Mkibahatika kupata Mtoto hutakuwa na mawazo ya Mtoto wako kupigwa na House girl. Ukitembelewa na Familia, hawataboreka kwani muda wote watakua na mwenyeji Mama mwenye Nyumba.

Jidanganye uoe Mwanamke mwenye Kazi. Asilimia kubwa wanarudi wamechoka kiasi kwamba hata mkilala hakugeukii wala hataki umguse. Atataka haki sawa eti akipika wewe ufue Nguo au umsaidie Kupika. Mara chache atakutengea Maji ya kuoga. Muda mwingi anatoka Kazini amenuna, hata akichelewa hataki umuulize alikua wapi.

Wana viburi sana, ukiwauliza kitu wanajibu kwa nyodo, hatakusikiliza. ukimsemesha kidogo tu ataenda kulala kwa marafiki zake au kwa ndugu zake. Haoni aibu kukukolomea Mwanaume hata mbele za watu. Anajifanya anawivu sana, atapiga Simu kila dakika kukuuliza ulipo as if wewe mtoto mdogo hujui pa kwenda.

Anapewa Mshahara lakini hautojua unaenda wapi kwani kila siku utaombwa hela ya Salon. Siku ukiishiwa ukamuomba hela ya Bia hatakupa bali atasema siwezi kukupa hela yangu ukahonge Malaya zako.

Siku akifurahi atakuletea zawadi ya Shati, mara moja kwa Miezi Mitano kana kwamba halipwi Mshahara. Dawasco wakimkuta hatawapa hela yake hata kama anayo, atawambia hayupo.

Ukioa Mwanamke mwenye kazi utamfaidi siku ukiumwa, ataomba ruhusa ili aje akuhudumie, atakununulia sana Socks na Matunda Matunda. akitaka kununua kitu atakua na kianzio sana sana ataomba umuongezee Hela.

Itakuwaje kama Ali Kiba na Diamond wataamua kuwa Juma Nature na Inspekta Harun wa zama

$
0
0
Juma Nature na Inspekta Harun ni wasanii wa muziki wa kizazzi kipya waliofanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye tasnia ya bongo fleva kipindi fulani kilichopita. Ni wasanii ambao kila mmoja kwa nafasi yake walifanikiwa kuandika rekodi mbalimbali zilizowafanya kuwa juu sana kimuziki.


Juma nature alifanikiwa kuweka rekodi ya maudhurio makubwa katika maonyesho ya uzinduzi wa album zake za ‘Nini Chanzo’ na ‘Ugali’. Pia alifanikiwa kwenye mauzo ya album zake na kuweza kufanya show nyingi sana ndani na nje ya Tanzania.

Inspekta Harun akiwa kama solo na memba wa kundi la ‘Gangwe Mob’ walifanikiwa kujaza watu wengi sana wakati wa uzinduzi wa album yao ya ‘Simulizi la Ufasaha’ na kuweka rekodi ya kipekee. Kupitia kundi lake waliweza kumiliki design za nguo zao zilizokwenda kwa jina la Gangwe Gear na website yao vitu ambavyo ni vikubwa sana kwa nyakati izo kufanywa na msanii wa kibongo na Afrika ya mashariki.

Inspekta Harun anakumbukwa kwa vibao vyake vilivyotamba kama ‘mtoto wa geti kali’, ‘Maisha ya uswazi’, ‘Asali wa moyo’, ‘Pamba nyepesi’ na vingine vingi alivyoimba mwenyewe au kwa kushirikishwa.
Juma Nature anakumbukwa kwa hits zake kama ‘Mgambo’, ‘Sitaki demu’ ‘Inaniuma sana’ ‘Hakuna kulala’, ‘Kighetogheto’ na nyinginezo.

Juma Nature na Inspekta Harun walikuwa ni wasanii wanaoshabiiana mambo mengi, kuanzia uhandishi wa nyimbo zao unaoelezea maisha halisi ya uswahilini na kiasi kikubwa namna ya kughani ambapo walitumia staili iliyojulikana zaidi kama ‘rap katuni’, pia maeneo wanayotokea ambayo ni ya uswahilini haswa, na ata pilika zao wakati wanaanza muziki inasemekana walishawahi kuangaika pamoja kwa namna moja au nyingine.

Kushabihiana uku kulipelekea washabiki wao kujaribu kuwalinganisha na kuwapima uwezo wao wa nani ni zaidi ya mwingine. Hii ilichochea kuibua mtafaruku baina ya wasanii wawili, wakatofautiana mpaka wakaunda makundi kwa washabiki wao ambao walikuwa wanajaribu kuwashindanisha . Mgogoro ukakuwa zaidi ukichochewa na vyombo vya habari pamoja na vijembe walivyorushiana kwenye nyimbo zao.

Baada ya ushindani na mgogogro uliofukuta baina yao kwa muda mrefu,wakaaamua kuweka chini tofauti zao na kufanya kazi ya pamoja chini ya mtayarishai nguli P Funk Majani.

‘Mzee wa busara’ ni kazi waliyofanya pamoja Inspekta Harun na Juma Nature, kazi iliyopokelewa vizuri sana na washabiki wa bongo fleva, na ikageuka kuwa gumzo kila kona ya Tanzania. Ni kazi iliyowaunganisha pamoja awa mahasimu wawili wakageuka kuwa marafiki,na pia ikawaunganisha pamoja na mashabiki wao kwa ujumla. Lengo ilikuwa kufanya albam ya pamoja kitu ambacho ata ivyo hakikufanikuwa. Nachoweza kusema ‘mzee wa busara’ ni moja ya nyimbo zilizosaidia kuisukuma tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwenda mbele zaidi.

Leo hii ukizungumzia muziki wa bongo fleva,watu wanausimamisha ni mastaa wawili Ali Kiba na Diamond Platnumz. Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao kila mmoja amefanya mambo makubwa na kujizolea mashabiki wengi. Ni wasanii wanaofanya kazi nzuri na zinazopendwa ndani na nje ya Tanzania.


Ali Kiba ana hit songs kama ‘Cinderela’, ‘Nakshi nakshi’, ‘Hadithi’, ‘Far way’, ‘Single boy’ ‘mwana’ na nyinginezo. Kiba amefanikiwa kufanya maonyesho kwenye nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani, amefanikiwa kufanya kazi moja na mwanamuziki nguli wa Marekani R Kelly.

Diamond Platnumz, amefanikiwa kutengeneza nyimbo zilizotamba sana kama ‘Kamwambie’, ‘Mbagala’, ‘Mawazo’,’Nitarejea’,’Kesho’ na ‘Number one’ ‘Mdogo mdogo’. Amefanikiwa kufanya maonyesho makubwa ndani na nje ya nchi pia amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika kama D Banj, Davido, Iyanya na wengineo.

Inspekta na Nature walifanya wimbo wa pamoja ukawa gumzo,ila hawakufanikiwa kutoa album. Itakuwaje kama Ali kiba na Diamond watafanya sio tu wimbo wa pamoja bali album nzima? Naamini itaweka rekodi ya aina yake ambayo haijawahi tokea kwenye muziki wa kizazi kipya. Kisha baada ya hapo tuwaone kwenye ziara ya pamoja sehemu mbalimbali. Tuwaone na mashabiki wao ambao ni wengi sana wakiunganika kuwaunga mkono kwenye kazi zao za pamoja. Na kuzidi kuusukuma mbele muziki wetu wa Tanzania kimataifa.

Muziki wa sasa ni biashara kubwa na kwenye biashara hakuna uadui wa kudumu. Penye fursa watu wanaojua biashara uweka tofauti zao kando na kutumia fursa kutengeneza faida. Nje ya kutengeneza faida Diamond na Kiba wana naafasi ya kutengeneza historia mpya na ya kipekee kwenye muziki wa nyumbani na kuzidi kuupa nguvu na ushawishi muziki wetu. Naamini hakuna kinachoshindikana.

By  GadoTz/Jamii Forums

Wolper Amshukia “Bidada” Anaetumia Jina Lake Picha na Sauti Yake Kutapeli Watu

$
0
0
Dunia ya Utandawazi, watu wanavipaji jamani!!!!. Wolper amempasha huyu kama ifuatavyo;

why why why unanichafulia jina we shuwainiiii mpumbavu mmoja maana kama unajua paka napokaa inamaana utakua ata insta uona kila kitu Mungu niokoe nilichokipanga kisifanikiwe nikakukamata mikononi mwangu nitafungwa kifungo cha maisha.. Alafu unaweka na picha yangu whatsup na sauti unageza yani sauti yangu kabisa muawaji mkubwa wewe fisi ,mende,peremende.Mungu akulaani wewe na kizazi chako tena kizazi chako mwanao mmoja aje kua star naafanyiwe kma unayonifanyia,Mungu akupofue macho na vidole vikatike ushindwe kudanganya watu nakula ela zao kwakuwatongoza nakujidai unashida.mfyuuuuuu” –Wolper aliyaandika hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kaa chonjo,tabia hii sio nzuri,tubadilikeni jamani.Pole sana Wolper

Mfumo wa Uzalishaji Muziki wa Tanzania na Jinsi Unavyozalisha Mateja Mitaani

$
0
0
Kuna namna nyingine inapaswa kufanyika....mlolongo wa recording studios na wasanii umekuwa mrefu lakini mfumo umebakia ule ule, ( kurekodi, kupeleka redioni, halafu kusubiri malipo ya show)..Avarage airplay kwa sasa ni angalau wiki tatu kwa hit wonder...wachache sana wanaofanikiwa kukaa zaidi ya mwezi na hii ni wote(wakongwe na chipukizi), utengenezaji wa matangazo unabakia kwenye rotation ya studio hazizidi Sita... Mwishowe madaraja ya stress yanajipanga..kuanzia kwa Msanii, Producer na sasa yanahamia hadi kwenye radio Stations..ila wahanga wakubwa ni recording Studio..mfumo wetu hauwapi fursa ya moja kwa moja ya kurudisha mitaji yao ya uwekezaji..mfumo wa royalty haupo na ni mgumu kuusumakisha katika mazingira yetu..lakini sidhani kama ni tija za ukuaji kwa mtazamo wa studio pale msanii anapolipa 400k kwa nyimbo..halafu mwimbo ukamuingizia zaidi ya 10m...kuna namna ambayo tu mfumo wa uzalishaji wa muziki Tanzania unapaswa kujikagua na kuangalia maslahi yao...otherwise..miaka mitano ijayo mateja wengi watakuwa ni producers kuliko wasanii

By Patrick Gondwe/Mlab Records

UKAWA Jiandaeni Kisaikolojia 2015, Huenda Yakatokea Kama ya Kenya

$
0
0
Mambo yanayotokea kwenye kutangaza na kuapisha washidi Wa uchaguzi Wa serikali za mitaa ni dalili mbaya ya kitakachotokea kwenye uchaguzi Wa urais Wa 2015 Kama UKAWA watashinda 2015.

Ukawa itashindwa tu 2015 Kama wasimamizi, wanaotangaza na kuapisha mshindi wataendelea kuteuliwa na kupokea na kutii maagizo na amri kutoka kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi Wa wilaya, wakuu wa mikoa na Rais Wa nchi.

Kama utaratibu utaendelea kuwa Kama ulivyo Sasa wapinzani ni bora kuanza kujiandaa kushindwa tu Tena 2015.

Vinginevyo hamna budi kuanza Leo kutafakari namna wasimami, watangazaji Wa matokeo na waapishaji Wa walioshinda watakavyokuwa huru uchaguzi Wa 2015.

Au muwe na cha kufanya Kama atatangazwa na kuapishwa yule ambae hakushinda Kama ilivyotokea kwa Mwai Kibaki kule Kenya.

Sanaa ya Tanzani Inauawa na Mfumo wa Kifisadi

$
0
0
Ni ukweli kwamba bila jitihada sanaa haitakulipa. Msanii mwenye kuipenda kazi yake na mwenye dhamira ya kweli ya kuona matunda ya kazi yake, sharti ajitume sana ili afanikiwe. Nasisitiza; jitihada huzaa bahati.

Msanii anahitaji vitu vitatu aweze kufanikiwa. Kipaji kama silaha yake namba moja, juhudi kisha nidhamu. Ukiwa navyo hivyo, jihesabu kwamba umekamilika na ni suala la muda tu kufikia mafanikio yako unayoyaota.

Kipaji unacho, unajituma sana pia ni mwenye nidhamu, hapo utaonekana na kuoneshwa njia ya kupita. Hata hivyo, kwa Tanzania ni zaidi ya vitu hivyo vitatu. Kuna ufisadi mkubwa sana ambao umejikita katika sekta ya sanaa.

Ni mfumo; Watanzania hawana uchaguzi kwa kile wanachopenda, isipokuwa wanajikuta wanavutiwa na kile wanachokisikiliza na kukiona mara kwa mara.

Huu ni mfumo wa kifisadi; Unaua vipaji, unadidimiza aina ya sanaa, unakuza rushwa, hatimaye na sanaa yenyewe inauawa.

Radio, TV, magazeti lawamani; Waajiriwa ni vijana wadogo ambao hawana weledi mpana katika sanaa. Wengi wao wanajua Bongo Flava tu tena juujuu! Matarajio yetu hapo ni nini?

Kwa kawaida mtu hufanya kile anachokijua. Ni kwa sababu hiyo basi, waajiriwa wengi katika vyombo vya habari hujikita zaidi katika nyimbo na habari za Bongo Flava tu. Maeneo mengine ni maji ya shingo na utosi, watafanya nini?

Mbaya zaidi hawataki kujifunza, angalau waweze kujua aina nyingine ya sanaa, hivyo kuwa na uhodari wa kucheza nyimbo na kutoa habari kuhusiana na sanaa tofautitofauti. Wanaamini Bongo Flava ndiyo mpango mzima (ndiyo kila kitu).

NI MFUMO WA KIFISADI;

Bongo Flava ndiyo iliyoleta rushwa ya muziki kwenye vyombo vya habari. Baada ya kufanikisha mpango wa kuiaminisha jamii kuwa Bongo Flava ndiyo nambari moja sokoni, watangazaji, ma-DJ na hata waandishi nao wakaona fursa!

Wewe mwanamuziki kama hutoi chochote, hupati promo! Ni ukweli kwamba lazima mwanamuziki ajitangaze, kwa hiyo inamlazimu yeye au menejimenti yake ihonge ma-DJ, watangazaji na waandishi ili kupata promosheni.

Mfumo huo ukasababisha kupotea kwa vipaji vingi, ama kwa kuwa na mikono ya birika, au hawakuwa na uwezo wa kuhonga. Kwa kawaida, rushwa husababisha kizazi cha watu katili, kwamba bora ufe kama hutoi kitu kidogo.

Ni wimbo mzuri lakini kwa sababu hauna maslahi, acha tu upite, unatupwa kapuni! Ni mwanamuziki mzuri lakini kwa sababu hatoi hongo, ataishia kutajwa juujuu tu. Au wimbo wake utachezwa bila mwenye wimbo kutajwa.

Biashara ya muziki katika ulimwengu wa kileo, inategemea sana vyombo vya habari. Inapotokea vyombo vya habari havitoi sapoti kwa aina fulani ya muziki, jamii lazima ijielekeze kwenye ile aina ambayo inapewa nafasi kubwa kwa maana ndiyo inayosikika.

Mfumo huu wa kifisadi, ulianzishwa kisera, kwamba Hip Hop haiuziki, kwa hiyo watu wakaaminishwa hivyo, mwisho wakaamini. Likatoka tamko, muziki wa Dansi hauna vigezo vya soko la kisasa, haukubaliki sokoni. Kweli jamii ikaamini.

Hapa naomba nifafanue; Kuna mgonjwa mahututi aliyepata nafuu na kusimama tena baada ya kunywa kikombe cha Babu wa Loliondo. Mtu huyo alirudi nyumbani akiwa mzima, mwenye matumaini makubwa.

Aliondoka akiwa hajiwezi, amebebwa lakini alirejea akitembea. Wiki tatu baada ya kurudi nyumbani, alipoteza maisha kwa sababu aliacha dawa alizokuwa anatumia kwa imani kwamba amepona. Unadhani kwa nini aliamka? Ni imani baada ya kunywa Kikombe cha Babu!

Imani ndiyo kila kitu! Leo hii vyombo vya habari vikiamua kumpa promo ya nguvu Timbulo, inawezekana kabisa baada ya miezi miwili, akageuka bidhaa adimu na yenye thamani kubwa kuliko Diamond na Ali Kiba. Huo ndiyo ukweli.

Promo hujenga imani kwa hadhira! Kitu kinachotangazwa mara kwa mara tena kwa kushupaliwa, huvuta hisia za msikilizaji na mtazamaji kisha kujenga imani kwamba kitu hicho ni bora sana na bila kupanga hujikuta anavutiwa nacho.

Ukiamka Diamond, mchana Diamond, ukifungua gazeti Diamond, usiku Diamond, facebook Diamond, twitter Diamond, instagram Diamond, utajikuta unamfuatilia na kuvutiwa naye. Hapa ndiyo kumaanisha promo hujenga imani.

Yupo atakayesema simpendi, huyo ameshavutiwa na ujumbe umeshamfikia. Ni imani ndiyo inayofanya akina TID, Q Chillah, Banana Zorro na wengine wengi kuaminika ni zilipendwa, wakati uwezo wao ni hai, tena wenye kiwango cha juu kabisa. Tatizo promo!

Akitokea mwekezaji mwenye malengo ya kuvuna fedha kupitia kwa Banana Zorro, hivyo kuamua kumwaga noti kila kona, ujio mpya wa Banana utaimbwa kila kona. Atapambwa mpaka kwa sifa za kutisha. Ni promo, ni fedha, ni mwendo wa kisasa.

Ni mfumo huu wa kifisadi ulioibua rushwa ya ngono, mtoto wa kike hapewi nafasi ya kung’aa kimuziki kama ataendelea kuubania mwili wake. Yupo mtangazaji wa kike ambaye naye anaamua kujiweka kwa mwanamuziki anayempenda. Akiingia studio, full mashauzi ya kumsifia bwana’ke.

Wengne (watangazaji na ma-DJ) hawaombi rushwa ya moja kwa moja, ila wanaandaa maonesho kisha wanawaita wasanii ‘kupafomu’ bure, anayekataa, nyimbo zake zitapigwa fitna mpaka ziondolewe kwenye mzunguko wa kuchezwa.

JE, NI KWELI MUZIKI WA DANSI HAULIPI?

Nyakati ambazo akina Banza Stone, Ally Choky, Muumin Mwinjuma walifanya atakavyo kwenye soko la muziki Tanzania zimepitwa? Zama za FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na kadhalika, zimekwenda wapi?

Si kweli kwamba muziki wa Dansi umeporomoka na kwama hauuziki. Ukweli ni kwamba vyombo vya habari viliamua kuugaya, au kwa lugha rahisi kuupotezea.

Mtanzania ambaye ni shabiki wa muziki, anataka asikie kwanza redioni kazi mpya za Twanga Pepeta, zimvutie ndipo akanunue CD na hata akisikia onesho Mango Garden, atapata mshawasha wa kwenda kuhudhuria.

Redioni Twanga hawasikiki, magazetin hawasomeki, runingani hawatazamwi, hiyo biashara watafanya na nani? Ukweli ni kwamba soko la muziki wa dansi linauawa na propaganda nyepesi ambayo ni kuacha tu kucheza nyimbo zao.

Ajabu ni kwamba mpaka makampuni ya kibiashara hasa yale yanayouza pombe, ambayo yalikuwa mstari wa mbele kudhamini bendi na maonesho ya muziki wa dansi, na yenyewe yameamini propaganda hiyo.
Kwa sasa, makampuni ya pombe yanajikita zaidi kwenye maonesho ya Bongo Flava kwa sababu ndiko wanakoaminishwa biashara ipo kubwa wakati si kweli.

Tafakari; Shabiki wa Bongo Flava yupoje? Ni kijana, ambaye akiwa kwenye onesho anaweza kusimama mwanzo mwisho. Kama siyo mwanafunzi ni kijana ambaye uwezo wake kununua pombe hauwezi kuwa wa kutisha. Akiwa na kampani, basi yupo na demu wake.

Shabiki wa dansi yupoje? Ni mtu mzima, akiwa kwenye ukumbi huwa na matumizi makubwa ya vilevi. Anaweza kuongozana na mkewe au wapambe ambao wote atawanywesha. Hii ndiyo sababu kwenye muziki wa dansi kukawepo mapedeshee! Wale watapanya pesa kama vile hazina kazi.

Kwa tathmini rahisi ni kwamba makampuni ya pombe pengine yangejikita kwenye muziki wa dansi, yanaweza kufanya biashara zaidi kuliko Bongo Flava kwa sababu ya kuangalia asili ya mashabiki na uwiano wa vipato pamoja na matumizi.

Hata hivyo, wameshaaminishwa kwamba Bongo Flava ndiyo mambo yote, unadhani watafanya nini? Hii ndiyo inaitwa promo katika mageuzi ya fikra.

Kampeni ilianza taratibu, kwamba nyimbo za Dansi ni ndefu, mwisho vile vipindi vyote vya Dansi viliondolewa. Vimebaki vituo vichache vinavyoendelea lakini kwa kusuasua.

UMEWASAHAU CHUCHU SOUND NA SAIDA KALORI?

Suala ni promo tu! Media ikiamua Mnanda ndiyo uwe muziki unaopendwa na kila Mtanzania itakuwa tu! Chuchu Sound wakati huo ikiundwa na Yusuf Chuchu (marehemu), Omary Mkali, Waziri Sonyo, Mao Santiago, Joniko Flower, Gabi Katanga (marehemu) na wengineo, ungeongea nini mbele yao.

Mduara uleule, wao waliuwekea vionjo na kuutangaza, baada ya hapo walitikisa kila kona ya Tanzania mpaka nchi jirani. Hapa ni kuthibitisha kuwa kila muziki unauzika na unalipa endapo utatangazwa kwa kiwango cha kutosha. Hakuna muziki usiolipa.

AT na miduara yake leo hii yupo wapi? Siyo kwamba harekodi kazi mpya, isipokuwa promo ni shida. Kijana huyu mwenye kipaji anakufa kimuziki hivihivi tunamuona.

Offside Trick walitajwa kama wapinzani wa AT, nao wamepotea. Mmoja wao akatangaza kuachana na muziki. Hayo ni matokeo ya kuzalisha wanamuziki wenye ‘stress’, wanafanya kazi nzuri lakini soko hakuna, jukwaa la kutangazia muziki wao limebanwa.

Je, Saida Kalori amesahaulika alivyojaza viwanja vya mipira kumuona akifanya vitu vyake? Kanda zake zikauzwa bei mbaya kuliko za mwanamuziki yeyote. Unadhani Saida hana uwezo tena? Ni promo tu! Jamii imeaminishwa amekwisha.

NANI KASEMA HIP HOP HAIUZI?

Baada ya kugusa maeneo tofautitofauti, sasa mjadala ukomee hapa. Nani mwanzilishi wa huu msemo kuwa Hip Hop haiuzi? Ni jamii hiihii ambayo inaaminishwa pia kuwa Reggae haina biashara.

Pengine hawajui au hawakuwepo kipindi marehemu Justin Kalikawe alipofanikiwa kuupenyeza muziki wake nchi nzima, japo hakukuwa na redio za kutosha. Alipofanya maonesho na watu walijaa, walimpenda na waliupenda muziki wa Reggae.

Unadhani kwa nguvu ya media iliyopo sasa, Kalikawe angekuwepo na kupata promo, Reggae ingekuwa wapi? Ukweli ni kwamba biashara bila matangazo ni ngumu. Akina Innocent Nganyagwa, Jhiko Man, wapo, hawana promo, kisha muziki wao unasemwa hauuzi.

Hip Hop ni muziki wenye nguvu, unauza na unalipa. Kitu cha muhimu ni kuangalia unaimba nini, yaani ule ujumbe wako unawezaje kuigusa jamii. Baada ya hapo, hakuna uchawi mwingine zaidi ya promosheni.

Hip Hop ni muziki wa harakati. Na kwa kawaida harakati ndizo huamsha na kukonga nyoyo za watu kisha kukusanya kundi kubwa. Unawezaje kusema Hip Hop haiuzi ikiwa ni muziki unaopendwa sana watu?

Hip Hop haiuzi kivipi ikiwa wasanii wa Hip Hop ndiyo huongoza kushangiliwa kwenye maonesho ya muziki? Ukitaka kuifanansha nguvu ya Ali Kiba na Diamond jukwaani, ukataka kuilinganisha na ya Weusi, MwanaFA, Roma, Prof. Jay jukwaani utakuwa unatania. Labda utakuwa hujui.

Kwa nini Weusi waonekane sokoni bei chee wakati jukwaani wanammeza Diamond? Hapa tatizo siyo nyota, ni promo tu! Weusi wakipewa promo ya kutosha, hawatakamatika.

JIBU UNALO;

Kama umesoma kwa makini, sasa unalo jibu ni kwa nini Niki Mbishi anatangaza kuacha muziki. Inahitaji mtu mwenye roho ngumu kuendelea kupambana na mfumo uliopo sasa. Wanamuziki wanafanya kazi, hazichezwi na bado wanaombwa pesa.

Inauma kuona mtu ambaye aliwekeza matarajio yake kwamba atafanikiwa kwenye muziki, anakumbana na kila aina ya changamoto, anamaliza miaka na bado changamoto haziishi.

Ukiwa unatabasamu, shangaa kwamba Miss Tanzania imefungiwa na Basata kwa miaka miwili, kwa kosa la udanganyifu wa Sitti Mtemvu, ila mpaka leo Prime Time Promotion wanadunda bila onyo wala adhabu wakati walimpandisha Davido kwenye jukwaa la Fiesta bila kibali.

By Luqman Maloto

Chuchu Hans Afunguka: Wanao Sema Ray Kaniacha na Kumrudia Johari Wamechemka

$
0
0
Stori: Musa Mateja na Gladness Mallya

STAA wa Filamu Bongo, Chuchu Hans juzikati alifungukia madai ya kwamba ameachana na mchumba wake Vicent Kigosi ‘Ray’, akaeleza kuwa, hakuna ukweli wowote juu ya hilo.Chuchu alifikia uamuzi wa kufafanua juu ya madai hayo juzi kufuatia tetesi zilizokuwa zimeenea kwamba yeye na kipenzi chake huyo wametibuana na sasa kila mtu kimpango wake.

Akifungukia juu ya uvumi huo Chuchu alisema: “Kutakuwa na watu wanaosambaza uongo huo, huwezi kuamini muda si mrefu nilikuwa na baby wangu Ray, tukawa tunashangaa tu juu ya umbeya huo.

Nahisi watu wamechukulia kwamba tumeachana baada ya mimi kuamua kubadilisha jina nililokuwa nikilitumia kwenye akaunti yangu ya kwanza ya Instagram, nimetoa neno The Greatest na kubakiza jina langu, ilikuwa ni uamuzi tu.

Siwezi kuachana na Ray na hata kama ikitokea tumeachana naamini kabisa Ray hawezi kurudiana na Johari wala Mainda, hao wanaosema eti kaniacha mimi karudiana na Johari wanachemka,” alisema Chuchu.

Ray C Awapa Diamond na Ali Kiba Somo la Madawa ya Kulevya

$
0
0
Stori: Laurent Samatta
SOMO! Mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ametoa tahadhari kwa wasanii kutotumia madawa ya kulevya (unga) ndani ya mwaka huu 2015 huku akiwatupia jicho zaidi nyota wanaofanya vizuri kwenye gemu kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba.

Ray C ambaye ni mmoja wa wasanii waliotumia madawa hayo na kumpa mateso makubwa kisha kuamua kuyaacha, amesema anahitaji kuona wasanii hao wakiwa mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya unga na si wao kuwa wa kwanza kutumia kwani vishawishi huwa  vinaibuka zaidi pale msanii anapokuwa juu kimuziki.

Madawa ya kulevya yanatakiwa kupigwa vita sana na kila msanii, wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba sitapenda kuwaona wakizama kwenye matumizi hayo mabaya, nahitaji kuwaona wakiwa katika nafasi za juu, wajihadhari maana umaarufu ndiyo unaoibua haya yote,” alisema Ray C.

Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba, Soma Kilichotokea

$
0
0
FUNGUA MWAKA: Mrembo na wigizaji wa Filamu hapa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Risasi,Mshenga amabe inadaiwa  kuwa ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam alifika nyumbani  kwa mama Lulu mida ya saa tano asubuhi ambapo alibisha hodi na kufunguliwa na mfanyakazi wa ndani (housegeli) ambapo mshenga alimpa barua hausigeli.

Mara baada ya muda kidogo hausigeli alimrudishia barua mshenga na haya ndio maelezo ya mshenga mara baada ya kukutana na mapaparazi alipouliza kama ni kweli alienda kupeleka barua ya uchumba.

“Kweli nimetoka nyumbani kwao na Lulu, nilipeleka barua ya uchumba ya bosi wangu.
“Nimefurahi nilipofika pale nikagonga geti, akatoka msichana mmoja, nilimuuliza kama mama Lulu yupo akasema yupo, nikampa barua akapeleka maana hakutaka mimi niingie,” alisema mshenga huyo.

“Baada ya muda yule msichana alirudi, akanipa barua akisema eti si ya Elizabeth wala Lulu. Sasa ni ya nani wakati jina la juu ya bahasha ni Elizabeth Michael.”“Naamini kabla mama Lulu hajaisoma aliangalia juu ya bahasha na kuliona jina la Elizabeth Michael ndiyo maana wakati ananirudisha tayari bahasha ilikuwa imefunguliwa.”

Mashenga aliendelea na kusema kuwa taratibu zote ya kuchumbia walizifauta ikiwepo kuweka pasa ya kishika uchumba “Tulifuata utaratibu wote, ndani ya bahasha tuliweka shilingi laki moja na zimerudi zote.”

Mama lulu alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu swala hili, mama lulu aliseama,
“Mimi mwenyewe nawashangaa ninyi waandishi. Mambo ya kuolewa anayetakiwa kuulizwa ni Lulu mwenyewe. Kama mtu alileta barua au nini, Lulu ndiyo atajibu.

“Halafu naomba kuwaambia kwamba nilishasema siku nyingi mimi sitaki mambo ya magazeti, hata hao mabosi wenu niliwahi kuwaambia,” alisema mama Lulu na kukata simu.

Lulu mwenyewe alipotafutwa kwa njia ya simu kuhusiana na ishu hii hakupatika.

Jionee picha za mshenga akipeleka baruda ya uchumba hapo juu.

Wajuzi mtuzuje hivi ndivyo watu hufanya wanapotaka kuchumbia?
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images