Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Godbless Lema asema atangaza kuwania ubunge Kinondoni uchaguzi wa Octoba 2015

$
0
0
Katika kikao chake na waandishi wa habari mchana huu katika hotel ya Snowcrest jijini Arusha, Lema amesema anaenda kupambana na Iddi Azan kwenye jimbo la Kinondoni ktk uchaguzi mkuu ujao mwezi October mwaka huu. Akielezea nia yake hiyo mbele ya mamia ya waandishi wa habari, Lema amesema anataka kuleta mapinduzi ya fikra kwa wana kinondoni na kuijenga ngome imara ya chadema jimboni hapo. Alisema mpango wake huo alikuwa nao toka mwaka 2013 pale alipovuliwa ubunge na alitafakari kujiingiza kwenye changamoto mpya kisiasa ifikapo mwaka 2015.

"Wana wa Arusha wasiwe wanyonge, kamanda wao naenda kupambana kwenye uwanja mwingine wa vita lakin wajue tupo pamoja" Alinukuliwa akisema bw. Lema. Hata hivyo alikwepa kujibu swali la mwandishi wa Radio 5 aliyetaka kujua kama pengine ni mbinu ya Lema kukwepa aibu ya kushindwa kwenye uchaguzi huu ikizingatiwa historia yake tata ya utekelezaji wa ahadi zake alizotoa mwaka 2010 na pia ushindani mkali unaomkabili ndani ya chama chake. Imefahamika kuwa wanachama zaidi ya 30 wameshatangaza waziwazi kuchuana na Lema kwenye uchaguzi wa Octoba.
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya Lema kukimbia changamoto na kujaribu karata yake mahali pengine

Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Abakwa Mpaka Kufariki na Kutupwa Kwenye Sinki la Kuogea

$
0
0
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Rwanda Nzovwe jijini Mbeya , Elika Mkubwa (8), amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulukana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.

Akizungumza eneo la tukio na paparazi huru, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.

"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya"

Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwake January 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani kwake.

Siwema Mchumba wa Nay wa Mitego Atupia Picha ya Faragha Akiwa na Mpenzi Kitandani

$
0
0
Mchumba wa siku nyingi wa staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' , Siwema Edson'Mama Curtis' amepost  picha za mahaba akiwa kitandani na mzazi mwenzie huyo kupitia Account yake ya Instagram, Siwezi ambae siku za nyuma alikuwa Gumzo mitandaoni baada ya Video yake akivishwa pete na Pedeshee kuvuja , Nay na Siwezi Hivi Karibuni Wamejipatia Mtoto wa kiume ..


Mbunge Joseph Mbilinyi apata ajali milima ya Kitonga

$
0
0

Mh.Sungu Mbunge wa Mbeya Mjini  amenusurika ajali leo akiwa katika harakati za kudelete magamba maeneo ya mlima kitonga.
Tuchukue frusa hii kumtakia pole kamanda wetu mungu amwepushe na mabalaa haya,Ni ulozi tu wa migamba Pole saaana Mh Sugu, tunamshukuru Mungu kukuepusha kwa ajali hio mbaya.

Habari zinadai kuwa ajali hiyo imesababishwa na Break za Gari Kushindwa kufanya kazi wakati wanateremka katika mlima huo mkali ikabibidi waigongeshe ukutani maana bila hivyo wangetumbukia korongoni.
Wote waliokuwa katika gari hilo wapo Salama Kabisa..

Mchungaji Afa Maji Baada ya Kuwaambia Waumini Wake Anaweza tembea Juu ya Maji Kama Yesu

$
0
0
Kutembea juu ya Maji si Kitu cha Mchezo Jamani , Sio kila mtu anaweza kufanya hivyo kama alivyofanya Yesu .

Mchungaji Franck Kabele wa huko Nigeria Aliwaambia waumini wake kwamba anauwezo wa kutembea juu ya maji na asizame kama Yesu.

Siku moja aliwachukua waumini wake hadi Beach ambapo alitaka washuhudie muujiza weka wa Imani , ila baada tu ya kuingiza mguu mmoja kwenye maji akazama na kisha kupotelea kabisa katika maji na kufariki .

Hili si tukio la kwanza chini humo kwa wachungaji kujifanya wanaweza kutembea juu ya maji na kisha kupoteza maisha.


Shocking! Students Caught Doing it While Pretending to Swim in Sea Water

$
0
0
Matukio mengine hata kuyaelezea ni ngumu , ngoja nitumie kizungu kidogo hapa...

I wonder what this country is turning into..According to report, This students where caught doing the unthinkable as you see in the Photo Above ..This incident  Happened in Dar es salaam Last Month Along side Coco Beach,

Tukio Hilo Limetokea Mchana mchana na wote hao walikuwa ni wanafunzi wa shule moja maarufu katikati ya Jiji  Dar es salaam,

inasemekana siku hiyo hawakwenda shule kabisa , kwani mashuhuda wanadai walikuwepo maeneo hayo toka mida ya asubuhi wakitembea pembezoni mwa bahari huku wakichezeana na kucheka cheka , baadae walianza kuogelea na kufanya huo uchafu ambapo report aliweza kuwapiga picha bila wenyewe kujua .

These Is The Biggest MPODODO Ever Seen In The Streets; Why Lie..!

$
0
0
I wonder what women today have as diet... Every morning when i wake up am shocked with the viral photos of the biggest a$ spotted around town and am like is evolution taking place in women?!

These trending viral photo happens to be the biggest b00ty as seen in the streets and this looks like a fries shop... i usually see all the big a$ in studio photos and just none like this... if Vera Sidika and Agness Masogange has bigger than this, why lie that's a disease or some sort of malignant growth that needs doctors attention with immediate effect... damn!

Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye..Nifanyeje?

$
0
0
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?

Jack Wolper Nusura Atibue Uchumba wa Nay wa Mitego Kwa Siwema

$
0
0
Stori: Musa mateja
KIMENUKA! Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.

Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe jijini Dar  ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia bebi wake huyo.

Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”

Baby Madaha 'Namsaka Mwanaume Mwenye Sifa za Kunizalisha'

$
0
0
Stori: Mayasa Mariwata
MAHABAT! MKALI wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amesema anatamani kuwa na mtoto lakini bado hajamuona mwanaume wa kuzaa naye na kuanika vigezo vya mwanaume anayestahili kuwa baba bora kwake.

Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Baby alisema suala hilo linahitaji umakini mkubwa katika uchaguzi na sifa anazozihitaji yeye ni upendo wa kweli na uhodari wa chumbani katika uwanja wa mahaba.

“Namsaka mwanaume mwenye sifa za kunizalisha, awe  baba bora maana ishu ya kumpata mwanaume huyo si suala la mchezo lazima uwe makini ili mtoto wako ajivunie kwa mzazi aliyenaye, sichagui rangi ila awe mrefu na mwili uliojijenga, akiwa amenizidi umri au mdogo
freshi tu ilimradi aweze kazi,” alisema Baby.

SAKATA LA IPTL: Mabalozi waitaka Serikali kuchukua hatua kali

$
0
0
Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la Serikali.

Nchi hizo, ambazo zilizuia takriban Sh1 trilioni za ufadhili na kuchangia nakisi ya bajeti ya Serikali, juzi zilikiri kuanza kuruhusu sehemu ya fedha hizo baada ya baadhi ya maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kumvua uwaziri Anna Tibaijuka, kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na kumuweka kiporo waziri wake, Sospeter Muhongo na kusababisha Jaji Fredrick Werema kujivua wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu.

Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshaeleza kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili juzi, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Timothy Clarke alisema kwamba Serikali imeonyesha jitihada za mwanzo, lakini wanasubiri kuona hatua kali zaidi zikichukuliwa pamoja na kuja na kauli moja kuhusu fedha hizo.

Alisema alichobaini ni kwamba wananchi wengi wanataka kujua hatima ya sakata hilo ndiyo maana walitumia vyombo vya habari kufanya mijadala mbalimbali kuzungumzia wizi wa fedha za escrow ambazo haijawekwa wazi kuwa ni za umma ama ni za Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL

Mauaji Mengine Kenya Mombasa, Sasa yamehamia Kanisani

$
0
0
Polisi nchini Kenya wanasema afisa mmoja wa kanisa amepigwa risasi na kuuawa alipokuwa akielekea katika maombi.

Madhumuni ya mauaji hayo hayajatambulika, lakini Muungano wa Makanisa mjini Mombasa tayari umesema ni mauji ya kidini.

Mauaji ya afisa wa kanisa jijini Mombasa yanatishia kuhangaisha wakaazi walioanza mwaka kwa amani baada ya machafuko mengi ya mwaka 2014.
Polisi wanasema afisa wa kanisa moja jijini Mombasa alipigwa risasi na kufariki alipokuwa akiingia ndani ya shule moja ambayo wameikodisha kufanya maombi yao.

Mkuu wa Upelelezi wa Uhalifu Mombasa Ondiek amesema mtu mmoja aliyekuwa na bunduki alimfuata jamaa huyo hadi akaingia ndani ya uwanja wa shule kabla ya kumpiga risasi. Alikufa papo hapo.
Aidha Ondiek amesema Polisi waliokuwa wameshika doria shuleni walisikia sauti za risasi na hivyobasi kumkabili muuaji huyo, lakini akahepa ndani ya vitongoji vilivyo karibu na shule.

Shilole Awashukia Wanaomtukana, Awataka Wampe Pesa!

$
0
0
“Hivi mashabiki zangu niwaulize swali!??? Hivi unapom-follow mtu ili uwe unamtukana Tuuùu kila akipost picha yake?? Au unam-follow ili upate kuona anafanya nini?? Katika kazi , kiukweli mimi nakelekwa sana na baadhi ya mashabiki zangu naona kama wakuwa sio wazalendo kabisaaà kila ufanyalo yeye kwake anaona baya tu acheni roho za kwanini! Ukiona mtu kafanya vizuri msifie tu na kama unaona hajakufurahisha mwambie tu kwa uzuri kwani matusi hayajengi! “

Shilole aliendelea;

Mimi kama msanii nategemea maoni yenu mazuri na sio matusi yenu tujaribu kuiga mifano kwa nchi za wenzetu wanapenda wasanii wao na kuwajali lakin huku sisi kutwa mnatuchamba loh! Na sisi pia wakati mwingine tunaumia na matusi yenu yasio na maana! But ukitaka kunitukna uwe na tusi jipya la 2015 yani unitukane huku unanipa PESA.  Nawapenda sana team saport wasanii wa home kuweni na J2 njema”-Shilole alimaliza.

Ujumbe umefika, tubadilike jamani

Download Wimbo Mpya Kutoka Kwa Mike Tee-I Missed You

$
0
0
Mwanamuziki Mike Tee Ameachia Wimbo Mpya Unaitwa I Missed You , Wimbo umetengenezwa na Producer Pancho Latino kwenye Studio inayomilikiwa na Mike Tee Mwenyewe inayoitwa Mykey Records.
Unaweza Kuudownload Kwa Kupitia link ifuatayo hapa chini :

Click>>https://www.hulkshare.com/mnyalu1/i-missed-you-mike-tee-produced-by-pancho

Artist ; Mike Tee
Song ; I Missed You
Studio ; MyKey Records
Producer ; Pancho Latino
Link for Downloads /Uploads/ Listening
Distributed Under Kitaa Promotion Co. Ltd

Vijimambo tu: Aunt Ezekiel Ajiwezi Hata Kuvaa Viatu! Moses Iyobo Achukua Jukumu

$
0
0
Mimba ya muigizaji Aunt Ezekiel imeanza kumtibua baada ya nyota huyo kushindwa kufanya baadhi ya kazi ambazo alikuwa akizifanya mwenyewe.

Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, kutokana na tumbo kuwa kubwa, Aunt kwa sasa hawezi kufunga viatu vyake, kufua, kuosha vyombo na hata akitaka kwenda toileti inabidi apewe kampani na mtu.

“Mh! Jamani Aunt hata kuinama ni mtihani sasa sijui kama ni kujidekeza au nini maana anapokuwa karibu na bebi wake ndiyo usiseme ni full kudeka anasema akiinama anaumia jamani?“Eti sasa hivi shosti wake Wema Sepetu na bebi wake Mose Iyobo ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kumsaidia kila kazi nyingi anazoshindwa,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya chanzo hicho kupenyeza habari,  paparazi wa GPL alimsaka Aunt na kufanikiwa kumnasa kwa nyakati tofauti akiwa anasaidiwa kufungwa viatu na Wema pamoja na Iyobo.Alipoulizwa Aunt kama anashindwa kweli kufanya kazi mwenyewe au anadeka, alifunguka:

“Jamani hivi niiname nimkunje mtoto wangu bila sababu za msingi na watu wapo ambao wanaweza kunisaidia kwa nini nijiumize, acheni nisaidiwe,” alisema Aunt.Kwa upande wake, Mose ambaye inaaminika kuwa ndiye mhusika wa mimba hiyo ya Aunt alipozungumza na mwanahabari wetu, alijisifu na kusema anafurahi kuwa baba bora wa Aunt.

“Sioni tatizo kutamka, mimi ndiye mhusika mwenyewe, baba bora mimi, watakaochukia wachukie,” alisema Iyobo.Kabla ya kuanzisha uhusiano na Iyobo, Aunt aliolewa na mfanyabiashara, Sunday Demonte anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya.

Picha:Uzinduzi Wa Kitabu Cha Kanumba Hapo Jana

$
0
0
NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga,  jana amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven Charles Kanumba, Kinachoitwa ''Steven Charles Kanumba: The Great Fallen Tree'' kilichoandikwa na Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.

Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.

Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.

Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.

Wasanii mbalimbali wa filamu wali hudhulia uzinduzi huo huku bendi ya malaika chini ya Christian Bella ilitumbuiza kusindikiza uzinduzi huo.

Tazama baadhi ya picha za tukio hili hapo juu.

(Na Gabriel Ng'osha/GPL).

Faiza Awacharukia Wanao Mponda Kwa Kuvaa Pampers Siku ya Kuzaliwa Kwake

$
0
0
Stori: Hamida Hassan
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ‘Mama Sasha’ amewafungukia watu ambao wanamponda yeye kutinga na ‘pampers’ ukumbini na kusema kuwa hiyo ni moja ya maamuzi yake binafsi.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Faiza aliyetinga vazi hilo katika siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni, alisema kuvaa vile hafikiri kama kuna ubaya kwa mtu yeyote kwa kuwa kila mmoja ana maamuzi yake na  hakumdhuru mtu.

“Mimi na maamuzi ya kuvaa chochote ambacho najisikia na kama hakina shida na mtu nakivaa na kuvaa vile ni moja tu ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa na nilitaka kuwa tofauti,” alisema Faiza kuwajibu wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakimponda mtandaoni juu ya tukio hilo.
GPL

Le Mutuz Awashukia Wanaomlaumu Kuhusu Nyumba ya Mama yake Huko Mbeya

$
0
0
U Super Star Kazi Kweli kweli Kila Utakacho fanya ama Kuonyesha Lazima Kiibue mjadala ..William Malecela Aka Lemutuz Alipiga Picha akiwa nyumbani kwa Mama yake Mbeya na Kuweka Instagram Kisha Baadhi ya Mashabiki wake waliibuka na Kuanza kuponda , Sasa nae Lemutuz ameibuka na Kuwashukia wanaoikaindia nyumba ya mama yake , huku akiwataka waonyeshe za mama zao!
Kama zina hadhi ya kama ya mama Le Super Star Lemutuz



Ndoa ya Petit man na Mdogo wa Diamond Yajibu..Esma Aomba Kupumzika Instagram

$
0
0
Mwaka Jana Tulishuhudia Mdogo wake Mwanamuziki Diamond Platnumz anajulikana kwa jina la Esma Platnum Akiolewa na mmoja wa Wafanyakazi Wa Wema Sepetu Upande wa Kampuni ya Endless Fame Anajulikana kama Petit Man.
Leo Asubihi January 12 Petit Man Amepost Picha ya Mke wake Esma Akiwa Mjamzito Kama inavyoonekana Kwenye Picha....

Wakati huo huo Nae Esma Platnum Ameandika Haya Kwenye Ukurasa wake wa Insta:

"Morning IG daah kuna watu humu km unamoyo mdogo unaweza kufa kwa presha haki ya mungu naona kwanza nijipumzishe na insta kwanza hali yangu muhimu sana kuliko hata kitu chochote na mi binadamu ninamoyo...nisubilini nikifa muanze kunipa sifa hata zingine nisiokuwa nazo... now siitaji tress I LOVE U ALL"

Hongereni Petit Man na Esma Platnum

Sinta Acharuka Akana Kujipendekeza kwa Wanawake wa Mwanamuzi Diamond

$
0
0
Mrembo wa Ukweli na Blogger Maarufu Sintah Amecharuka na kutoa makavu kwa shabiki mmoja aliendika kwenye instagram kuwa Sintah anajipendekeza kwa Wanawake wa Diamond...

Shabiki anayeitwa Rahma_Rahyuuh Alifunguka Hivi:

"Ila we Sinta una Dhambi sana--yan Hakuna Mwanamke wa Diamond Baada ya Wema Ambae hukuwa ukijipendekeza nae ' we mwanamke unajua na haya hayana mmoja! Mungu tunaemuabudu ni mmoja na @wemasepetu nae mtu ! Ohhoo--Muumuze tu lakini aibu itakurudia mwenyewe"

Sintah Naye Akafunguka Hivi:
"Huyo Mungu unaemjua mshitakie mabaya yangu uone kama atajibu coz anajua whats going on, siwezi nikaelezea vitu vingine but my close pipo know so go ahead n curse....kwahio urafiki wangu na Zari unaingilianaje na huyo Wema??please ongea vitu vya maana na mwisho leo kuweka huu upupu hapa, maisha ya zari ni ya kwake naomba nieleweke mimi ni rafiki tu i can advise ila siwezi ku control maisha yake


Kuna watu hawawezi kumaliza siku bila kunitaja jina langu tena kwa herufi kubwa bila hata aibu , sasa mimi ninajipendekeza kwa wanawake wa Diamond wanisaidie nini kwa mfano? wao wana nini na mimi nina nini?

Narudia tena mie ni blogger n aweka kila jambo linalo husu mastaa, na huyo Zari mie nimemjua leo?? angalia calender yako vizuri labda unatumia za Ethiopia kuwa updated isitoshe labda wewe ndio unamuona zari ni malkia wako to me ni kawaida sana coz she is bin a friend ever since sio yeye tu familia yake nzima

halafu siwezi kumchagulia mtu maisha yeye kama anaamua kuwa Dimondo awe shemeji yangu kila la kheri kama ni Ivan sawaa yeye ndio anajua yupi mzuri kwake mimi sivai viatu vyake kujua maumivu gani anayapata" Sinta

Je wewe Msomaji Una Maoni Gani Kuhusu Hilo?
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images