Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Jackline Wolper Akubali Kuposwa, ila Masharti na Vigezo Kuzingatiwa

$
0
0
BAADA ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya kutaka kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na kumjibu kuwa na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema katika mila za Kiafrika, posa haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.

“Nimesikia habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu yeye kama yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na masharti huzingatiwa, afuate utaratibu tu,” alisema Wolper.

Jokate Akanusha Kutoka na Millard Ayo!

$
0
0
Mwanamitindo na mwigizaji, Jokate Mwegelo ameucho molea vilivyo uvumi uliozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.

Uvumi huo ulianzia mitandaoni ambapo mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate juzikati, aliweka plain ukaribu wake na Millard ambaye ni mtangazaji mwenye mvuto mkubwa kwa jamii.

“Millard ni mshkaji, namkubali kutokana na uchapakazi wake, anajua kujituma na ni mpambanaji lakini nje ya hapo hakuna cha zaidi,” alisema Jokate.

Picha: Jokate akiwa katika pozi na Millard Ayo

GPL

Mtu ahack namba ya simu ya AY, awaomba mamilioni watu wake wa karibu

$
0
0
Mtu asiyejulikana amehack namba ya Tigo ya AY na kuanza kuwaomba mamilioni watu wake wa karibu.

AY ambaye kwa sasa yupo jijini Nairobi, Kenya, ameiambia Bongo5 kuwa anashangaa kugundua kuwa namba yake ya simu inapatikana wakati chip anayo yeye na haipo kwenye simu.

Fundi Frank ni miongoni mwa marafiki wa AY walioombwa fedha na mtu huyo

    Kuna mtu amehack namba yangu ya Tigo anaomba watu pesa

    — Ambwene AY (@AyTanzania) January 12, 2015

    Niko Kenya line yangu iko off but nashangaa huko Tanzania iko ON na inatumika

    — Ambwene AY (@AyTanzania) January 12, 2015

Kufuatia tukio hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameziagiza mamlaka husika kufuatilia haraka jambo hilo.

    “@Tigo_TZ: @JMakamba @AyTanzania tunalipeleka swala hili kwenye idara husika lifanyiwe uchunguzi.”>>>lipatiwe ufumbuzi.

    — January Makamba (@JMakamba) January 12, 2015

Msichana ni Mzurii Lakini Haeleweki..Naombeni Ushauri

$
0
0
Kuna msichana ambaye ni Jirani yangu sana na kusema kweli ni mzuri sana. Nilipataga hofu ya kumtongoza kwa sababu ya uzuri wake na ni gate kali. Ila kila alipokuwa anapata upenyo anakuja getto kwangu tunacheki movies na kula kwangu.

Siku moja nikajisemea moyoni kuwa Jamii na masela wangu wataniona kama sitampa mtoto haki yake mbali na kumuoa. Basi kidume nikajipanga na alivyo kuja kwa mara ingine gheto nikampa makavu live bila kupepesa macho. msichana aliniangalia na hakuweza kusema kitu akang'oa nanga na kuondoka.

Sikuwa na haja ya kumsihi arudi kwani alikasirika,ila moyoni nilijua massege sent. Ikapita kama wiki mbili bila kumwona tena ila kwa bahati nilikuwa nakatiza mtaani nikakutana nae akitokea sokoni nikampa hi na akaipokea bila kusita.

Nilivyompita na kumwacha nyuma aliniita "Ras" Lete habari,naomba unisaidie haka kamfuko huku akinitazama kwa jicho la madaha akiashiria kukubalian na ile sms nliyomtumia.

Basi tukiwatunasonga na safari huku story za hapa na pale nikaona ni vyema kumuuliza vp juu ya ile sms. Cha ajabu alikasirika zaidi ya mwanzon na kuninyang'anya kale ka mfuko na kuniambia nimemboa na hataki kampan yangu wala swaga zangu.

Naommbeni ushauri wenu nimfanyie Suprise gani huyu msichana ili anielewe kuwa nampenda.

Dida na Edzen Mambo Safi Tena..Wapenzi Wakigombana Shika Jembe Ukalime

$
0
0
Unaambiwa Ndugu Ama wapenzi wawili wagombanapo Shika Jembe Ukalime...Usiingilie na kujifanya wajua sana itakutokea puani na kuonekana mchonganishi.

Hahaha Wambea Sisi tulivyoshupalia ugomvi wa Wapenzi wawili Dida na Edzen Mpaka wakaachana Utafikiri tunahusika kwa Vijembe na Meneno mengi mtandaoni..Unaambiwa Kwa sasa wawili Hao Mambo safi wameshapata ugomvi umeisha na mamba ni kama dhamani ng'are ng'are , Wenyewe wanawasiliana kama kawa na kusaidiana katika vitu vidogo vidogo japo kila mmoja alichukua hamsini zake..Tujifunze kwa hawa watu si lazima mnuniane na kuchuniana mkiachana kimapenzi , mnaweza kuwa marafiki kama kawaida..

Urafiki wao kwa sasa umejidhihirisha baada ya Dida kuingia mtandaoni na kuandika haya hapa chini


Shamsa Ford: Nalala na Mume Wangu Nikiwa Kambini

$
0
0
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ambae ameolewa na ana mtoto mmoja, amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa kambini akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.
Akizungumza na Uwazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo analifanya kwa kuwa yeye ni mke wa mtu na huwa anapewa chumba chake maalum.

“Mara nyingi ninapokuwa lokesheni kama si mbali na nyumbani basi naenda kumuona mume wangu na mtoto lakini kama ni mbali kidogo mume wangu huwa anakuja na kulala na mimi chumbani kwangu, asubuhi anaondoka naendelea na kazi yangu,” alisema Shamsa.
~Bongo Movies

Lulu: Mapedeshee ndiyo wanawalipa wasanii wa kike siyo filamu

$
0
0
ELIZABERTH Michael‘ Lulu’ amefunguka kuwa wasanii wa kike wa filamu wana biashara nyingine iliyojificha ndani ya ile ya filamu ambayo inawalipa zaidi.
Lulu amepasua kuwa wasanii hao wanawategemea mapedejee kuendesha maisha yao huku wengi wakiamini kwamba mabinti hao wa Bongo Movie wanalipwa vizuri kutokana na filamu wanazoigiza.

“Ukweli hauko hivyo, hali hii inatokana na wengi wetu kudumaa na hatuwazi kufanya mambo makubwa kwa kuigiza na wasanii wakubwa lakini hakuna anayeliona hili,” alifafanua.

“Hakuna anayefirikiria kuigiza na wasanii wa kimataifa kama Ritha Dominic ili sanaa imlipe na wengi wanawategemee mapedejee au biashara zisizo rasmi, kwani filamu inaonekana ipo juu lakini wahusika wake wanalipwa kwa staili nyingine kabisa,” alisema.

Mwanaspoti

Diamond Atoa Wimbo Mpya wa Mduara-Nasema na Wewe..Download Hapa

$
0
0
Sasa ni zamu ya Mduara ,Mwanamuzi Diamond Platnumz ameamua kuwakata kiu wapenzi wa Mduara kwa kuachia wimbo mkali unaoitwa Nasema Nawee ambao upo katika mirindimo ya kimwambao zaidi..
Sina mengi ya kuongea kama ila embu bonyeza hapo chini uweze kupata uhundo huo mtamu kutoka kwa mkali Dangote...

Bonyeza <HAPA> Ukitaka Kuusikiliza ama Kudownload---

5 Things East African artistes can learn from Diamond Platnumz

$
0
0
Tanzanian sensation Diamond Platnumz has taken the airwaves hostage. Even if you don’t like the guy, you’ll still find yourself grasping the lyrics to his songs by default. His music has enslaved us and as we all nod our heads in appreciation, Meanwhile, Kenyan artistes are wondering what they aren’t doing right. Well, sometimes it’s wise to borrow from the template of a genius so here are a few things our stars can learn from the Bongo king.

Gigs

You can tweet, hashtag, come up with all the fan pages that you like but you can’t beat good old fashioned gigging. Playing your music in front of real people is still by far the best way to grow your fan base. People don’t forget a great gig in a hurry, and if it is great they won’t shut up about it any time soon either.

It’s a competitive world out there hence there’s no time to relax. A successful artiste like Diamond can be excused for chilling for a week or two but he never does that. He’s always traversing regions and doing shows. Even on Christmas day, he had a show. Well, I know that getting shows in Kenya can be hard sometimes due to ‘difficult promoters’ but that’s where connections come in. A well connected artiste never misses shows

Kenyans don’t buy music. You just have to perform to get the money. Even in the international arena, the number of fans that buy music is decreasing with every passing day. All of the world’s music can be gotten for free. As a result, the only greater joy fans can derive from an artiste is seeing them perfrom live

Ignore the hate unless it’s constructive criticism

If your music is receiving airplay and you are getting money, never listen to the haters. Like Diamond, don’t listen to those who say they are better than you or those who say you are too soft or too boring. If someone says they are better than you yet you are getting more recognition than them, there’s no need to fret. Diamond never tried to prove he was better than Ali Kiba even after the ‘Run Dunia’ crooner claimed that Mr. Platnumz had nothing on him. All artistes are in it for the fame and money. Let’s not kid ourselves here. If those elements are coming through, don’t listen to the jealous nincompoops who only wish they were you because they’ll only shift your focus from where it’s supposed to be.

Fashion

Some artistes dress like campus freshmen, leaving fans wondering whether they are indeed serious with their careers. And these same artistes wonder why there are no screaming ladies at the front rows of their shows. Whether you are underground, bubbling under or a mega star, a good artiste has to be a fashion killer. The purists will tell you it doesn’t matter and ‘It’s all about the music, man’. Of course the music comes first, but the fashion follows in a close second. If you go through Diamond’s Instagram page, you will easily notice that he doesn’t have even a single fashion fail. From hair to attire, he pays attention to detail. I know some of y’all Kenyan artistes are hardcore and stuff but at least do it for the ladies out there.

Keep yourself in the news

This doesn’t mean that you should roam around engaging in desperate activities in order to get to Ghafla and other blogs. Diamond has mastered the art of staying in the headlines He makes sure everything he does is photographed. He wants us all to keep talking. He went ahead and acquired a socialite girlfriend, boosting his public image further and creating more conversation angles. The truth is, even if you are releasing good music but your life is boring A.F, no one will hold you in high regard

Make music for the masses not for the intellectuals

By listening to all of Diamond’s track we easily learn one thing. Hhe didn’t try to be too clever while coming up with them. ‘Nataka Kulewa’, ‘Kesho’ , ‘Ukimwona’ and ‘Number One’ are all tracks that the masses can relate to. The ordinary raiyaas are the one’s who’ll give you the relevance you badly want. And with the relevance, the opportunities will come. Intellectuals will only serve as critics for your work. They won’t say ‘huyo mchamaa ni mnoma pwana’. Hahaa. If your aim is to pass a message, then well and good,. You can focus on whomever you want but if you want to sell out, simplify your music.

Written by: Philip Etemesi of Ghafla (Kenya)

Diamond Azihirisha Kwamba yeye ni Rijali , Ampa Zari Ujauzito ,Wema, Jokate na Penny Mpo?

$
0
0
Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib Abdul – Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa, HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza kudokezwa juu ya ujauzito alionao mwanadada ZARI ambao ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata wapi” ambao wachunguziwa mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake maarufu wa zamani.



USHAHIDI WA UJAUZITO HUO

Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema “I can not wait to have you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku akiambatanisha na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye akapost picha yake akichukuliwa vipimo hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha wananchi wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu

Je unafikiri hii inaweza kuwa “Project nyingine” au ni kweli wawili hawa wanatarajiwa kuwa wazazi?? Tupe maoni yako

'Mimi Bado ni Chuma Cha Reli Nina Lipa , Nikiamua Kuolewa Naweza Tena Bila Shida' Monalisa

$
0
0
Mwigizaji mkongwe wa filamu hapa  Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (33) amesema kuwa yeye siyo gubegube kwani alishawahi kukaa ndani ya ndoa lakini sasa ameamua kutulia.
Yvonne Cherly ‘Monalisa’
Akipiga stori mbili-tatu na  Gazeti la Uwazi, Monalisa alisema kuwa hata kama akiamua kurudi upya kwenye ndoa anaweza na kutilia msisitizo kuwa mwanaume atayemuoa lazima atambue kuwa anayemuoa ni Yvonne Cherly na si Monalisa kwani jina hilo litakalokuwepo kwenye cheti cha ndoa.

“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza kuonekana zaidi,” alisema Monalisa.

Aibu Kubwa: Mtumishi wa Mungu Afumaniwa live na Mke wa Mtu Wakibanjuka Nyumbani Kwa Mwanamke

$
0
0
Stori: Risasi Mchanganyiko
Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani, Risasi lina mkanda nzima.

Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ Akijitete 

Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.

Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa Operesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.

Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.

OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu na kunyetishiwa juu ya uwepo wa Muinjilisti huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia pikipiki zao ziendazo kasi walianza safari na baada ya dakika chache walikuwa wamefika kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.

Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.

Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.


Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.

Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.

Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii gazetini kesho n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni pale Bamaga ee, napajua sana pale”.


OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama atafika ofisini kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri kumi za Mungu.

Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.

Chanzo:Global Publishers

Amanda Apata Kashfa ya Kujiuza Mtandaoni..Mwenyewe Ashtukia Anayemchafua

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amechafuka baada ya mtu anayejitambulisha kwa jina lake, kujinadi kwa kujitongozesha katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
 Amanda huyo feki amekuwa akijiuza bila aibu katika mtandao huo kwa kujitongozesha kwa wanaume, kitu kinachomuumiza muigizaji huyo ambaye pia anawashangaza wasanii wenzake juu ya tabia hiyo ya kuchefua.

“Yaani nimekuwa nikiulizwa sana, lakini juzi ndipo nilishtuliwa na msanii mwenzangu, nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba kuna mtu ananichafua kupitia mtandao, mashabiki wangu watambue kuwa mimi sijawahi kujiuza na ninajiheshimu,” alisema Amanda.

Lemutuz 'Kwenye Shida Ndio Utajua Marafiki wa kweli na Mburulazzz, Lulu Michael Ndio Rafiki wa Kweli'

$
0
0
The King Of All Bongo Social Media Network, Le Mutuz ukipenda muite Mzee wa mabebezz amemshukuru mrembo na mwigizaji lulu kwa kuonyesha kumjali wakati wa matizao na kuwashukia baadhi ya marafiki zake ambao huwa wao pamoja nae wakati wa raha tu, ila wakataki washida wote hupoatea. Le mutuz alifunguka

Kwenye shida ndio utajua marafiki wa kweli na le super gademu mburulazzz mazafantazzzz.....nilipotangaza my House warming Party yanapiga simu kila dakika kuomba mualiko lakini nimesema Mama yangu anaumwa hamna hayapigi simu le mazafantazzz.....thank U Super Star Lulu you are a true friend sio le mburulazzzz yanajua kuulizia Party tu the brainlessss mazafantazzz hahahahahahah U know! - le Mutuz”

Kwa mujibu wa Le Mutuz, kwasasa mama yake yupo poa
Sasa wale mabebez wengine anaopigaganao mapicha watakuwa kwenye hali gani baada ya Le Mutuz kuwapa makavu.

Wanawake Mnaojichubua Ngozi Mnaniudhi na Mnakera Mno

$
0
0
Mimi sijawahi kuona wanawake warembo kama weusi, ni warembo mno, infact wanavutia sana.

Cha kushangaza sasa, kuna mijitu yenye upungufu wa akili kichwani inajichubua bila huruma, kibaya sasa, kwenye zile joint za mikono na miguuni unakuta rangi yake ya asili inabaki, na hata sehemu zingine za mwili unakuta mabaka mabaka, yaani huwa nasikia hasira sana.

Ki ukweli Hata uwe Mzuri wa Aina Gani yaani Ukiwa  umejichubua ngozi mimi nakushusa samani 100% siwezi hata kukupa mistari , Na ukiangalia wanawake wengi waliojichubua ni watata hata kwenye ndoa zao huwa hazidumu kiivyo....

Maoni yako Tafadhali kuhusu Wanawake wanaojichubua



Dawa ya Mapenzi, Mvuto, Kumvuta Aliyembali, Kumshika Mpenzi Yapigwa Marufuku

$
0
0
Kumekuwa na tabia hasa kwa wanawake kwenda kwa waganga na kutaka dawa na kumvuta mpenzi ama kumdhibiti mwaname
Sasa kwa taarifa yako kwa wale wanaopenda kutumia Ushirikina kwenye suala la Mapenzi sasa mwisho wao umewadia, Serikali imeshapiga marufuku Waganga wa kienyeji wenye shughuli zinazohusiana na kupiga ramli.

Jipangeni upya mapenzi si ramli wala Mitishamba..
Huko kwa waganga mnaenda kudanganywa tu na mwisho kujikuta kutumia hela nyingi sana bila sababu , na kuna habari kuwa waganga wengine wanakulala kwanza wewe wakidai wanakuwekea dawa kwa njia ya kufanya mapenzi ili uwe na mvuta kama inavyoonekana hapo kwenye picha..

Akila Kimkichwa mapenzi si Ndumba Jamani

Ali Kiba Atangaza Kuanza Mwaka na 'Surprise'

$
0
0
Star wa muziki Ali Kiba, amesema kuwa mapokezi ya video yake ya Mwana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania yamekuwa ni ishara kwake kuwa kuna mtu alikuwa amemiss katika game na katika mchango wa kuitangaza nchi kimataifa kupitia sanaa.

Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015
Kiba a.k.a Fundi ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari.

Kutana na Mwanaume Mwenye Hips Kubwa Kuliko Wanaume Wote Dunia

$
0
0
20-year-old Micah is a man but his body features will amaze you! He has hips that are larger than life, the type of hips that most women will go under the knife to get.

The guy who has the eyes of many through his Instagram account says he is an upcoming singer and songwriter from Chicago. From the photos he posts on Instagram, it is obvious he enjoys and loves who he is and all the attention that comes with it.

Qoute of the Day
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'

Mfahamu kwa undani Zarinah, mwanamke anayezima Nyota ya Wema Sepetu

$
0
0
JINA la Zari hivi sasa limekuwa jina maarufu katika masikio ya Watanzania, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya mwanadada huyo mfanyabiashara na mwanamuziki wa Uganda kuwa na urafiki na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kwa jina la usanii Diamond Platnum.
Zari The Lady Boss
Kwenye mitandao ya kijamii kama Tweeter, Facebook,Instagram na hata Whatsapp lazima utakutana na jina Zari akiunganishwa na Diamond na wengine wataunganisha na Wema Sepetu aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Uhusiano kati ya Zari na Diamond umezua gumzo kila eneo Tanzania na Afrika Mashariki huku wakifananishwa na mastaa wa nje kama vile Kanye West na Kim Kardashian kwa namna wanavyofuatana wakati wote huku Diamond akionesha kila aina ya mbwembwe za kumjali mrembo huyo kutoka Kampala, Uganda.

Uhusiano wa Zari na Diamond umewafanya kuandamana kila sehemu hivi sasa. Wawili hao walianza kuonekana kuwa na ukaribu wa mahusiano tangu Diamond alipokwenda Afrika Kusini kwenye Tuzo za Channel O ambapo Diamond aliibuka na ushindi wa Tuzo tatu.

Baada ya Tuzo hizo, Zari alimualika Diamond kushiriki katika ‘pati’ maarufu ambayo mwanadada huyo huandaa kila mwaka nchini Uganda ambapo mwaka huu ilijulikana kama All White Ciroc Party.

Wawili hao baada ya sherehe hiyo, walifuatana ambapo Zari alimsindikiza Diamond nchini Rwanda na Burundi alipokwenda kutoa burudani nchini humo, na picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kuwafanya wawili hao kuwa gumzo hivi sasa katika mitandao Tanzania na Afrika Mashariki.

Je, Zari ni nani hasa? Zarina Hassan Tlale.Maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini.

Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006,Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports .

Mwanadada huyo ni binti wa Halima Sultan Hassan na Nasur Hassan akiwa na asili ya damu mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ya Kihindi , Toro, Somalia na Burundi kutoka mji wa Jinja, Uganda. Babu mzaa mama yake anatoka India na bibi yake ni kutoka Uganda. Babu yake mzaa baba ni kutoka Somalia na bibi yake mzaa baba anatoka Burundi.

Zari maarufu kama The Bosslady aliwahi kuolewa na mwanamume anayejulikana kwa jina la Ivan na kubarikiwa watoto watatu wa kiume Pinto, Didy na Quincy na anamiliki kampuni tatu.

Mwanadada huyu alizaliwa Septemba 23,1980. Zari amekulia katika mji wa Jinja katika nchi ya Afrika Mashariki inayojulikana kama Uganda.

Zari alisoma shule ya msingi, kisha kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja ambapo alisoma kwa bidii kutimiza ndoto zake. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, mwanadada huyo alihamia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala ambapo alikuwa akitoa burudani ya muziki katika maeneo ya starehe kabla ya kuhamia mjini London, Uingereza na kusomea Stashahada ya masuala ya urembo (cosmetology).

Historia yake kimuziki inaonesha Zari alianza kuimba akiwa na umri mdogo wakati akisoma shule ya msingi ambapo alikuwa akitoa burudani katika matamasha ya muziki yaliyokuwa yanaandaliwa na wafanyakazi wa shule,wakati wa hafla za mwishoni mwa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya akiwakilisha shule yake.

Ingawa amekulia katika familia ya Kiislamu yenye wasichana sita na wavulana wawili, Zari hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Alianza muziki akiwa na umri mdogo na albamu yake ina nyimbo kali kama ‘Toloba’ na ‘Hotter Than Them’. Watu waliomvutia katika muziki ni Wasanii wa Marekani Arethal Franklin na Whitney Houston wakati akiwa sekondari.

Afrika waliomvutia akapenda muziki ni wanamuziki wa Afrika Kusini Brenda Fassie, Miriam Makeba, Lucky Dube na Malkia wa Muziki Afrika Kusini, Yvone Chaka Chaka. Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi,drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.

Baada ya miaka miwili ya kufanya vizuri katika majukwaa na matamasha ya shule, alipumzika na kuhama kutoka Uganda kwenda London, Uingereza na kuendelea na masomo yake lakini bado mapenzi yake kwa muziki yakiwa mawazoni mwake. Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .

Mwaka 2008 Zari alishinda Tuzo ya Channel O ya Video Bora ya Muziki ya Msanii Bora Afrika Mshariki. Hafla ya tuzo hizo ilifanyika Johannesburg, Afrika Kusini. Tangu hapo Zari ameendelea kutoa nyimbo zaidi za kuvutia, huku akitiwa moyo na mashabiki wake wakati huo.

Mwaka 2009 alipata Tuzo inayojulikana kama Diva ya mwaka katika kipengele cha Diaspora tangu hapo aliendelea kutengeneza muziki. Zari hivi sasa anaishi Afrika Kusini ambapo anamiliki maduka makubwa ya vipodozi na shule ya elimu ya juu mjini Pretoria wakati akiendelea kujijenga kimuziki.

Inaelezwa kuwa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan wanamiliki Shule ya Brooklyn City ambayo ina kampasi sita Afrika Kusini, huku kila moja ikiwa na wanafunzi kati ya 800 hadi 2,100. Wanafunzi hao hupewa vyeti vya taifa wanapomaliza mwaka. Vile vile Zari amejenga hosteli iliyopo barabara ya Sir Apollo Kaggwa, Kampala na anamiliki nyumba kadhaa katika mji huo hasa eneo la Munyonyo, pamoja na duka kubwa la nguo Afrika Kusini.

Ingawa muziki wake haujafanya vizuri kama wanamuziki wengine wa Uganda akiwemo Jose Chameleone, Bebe Cool, Bobi Wine na Ragga Dee, Zari amekuwa akifurahia kwa mafanikio zaidi kwenye biashara na kutokana na hilo anasema lazima arudishe kwa jamii na hivyo kuamua kusaidia vituo na taasisi kadhaa zinazohitaji misaada kama Katalemwa Cheshire Home, Sanyu Babies’ Home pamoja na Gereza la Luzira.

Mfano mwaka 2013 kutokana na moyo wake wa kusaidia,kwa kutimiza hilo baada ya sherehe zake anazozifanya kila mwisho wa mwaka aliamua kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha M-Lisada kilichopo Nsambya siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi, akifuatana na watoto wake Pinto, Didy na Quincy.

Alitoa zawadi maalum kwa watoto hao, ambapo Zari alishiriki kuandaa chakula cha Krismasi na kisha baadaye wanawake, sukari, biskuti, mchele na matoke. Mbali na masuala mengine yote, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,watu wengi nchini Uganda wanakubaliana kuwa Zari ndio Mwanamke Mrembo zaidi nchini humo.

“Sitafuti umaarufu, wenyewe umaarufu ndio hunifuata,”aliwahi Zari kusema kupitia mtandao wa Red Pepper akikanusha habari za baadhi ya watu wanaodai kuwa anatafuta umaarufu kwa nguvu.

Habari zake kuandikwa katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zake za uhisani zimesababisha wengi kudai kuwa anataka tu umaarufu, kujulikana na kuzungumziwa kila wakati.Hata hivyo akijibu madai hayo, Zari alisema umaarufu unamtafuta yeye na sio kwamba yeye anautafuta.

Quote of The Day:
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'

Msafara wa Waziri Muhongo wazomewa Kahama kisa fedha za Escrow

$
0
0
Muhongo
WAZIRI wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Baada ya kufika katika eneo hilo wananchi hao walianza kumzomea wakidai ni “mwizi wa fedha zilikuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kelele ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni waziri yupi.
Hata hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo ambaye yuko ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali katika eneo hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima wa mgogolo wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya Escrow.
Pamoja na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake wilayani Kahama ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kuwaahidi umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.

Qoute of the Day
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live


Latest Images