Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Jux na Vanessa Mdee Hawalifichi Tena Penzi Lao, Jack Patrick Hana Chake

$
0
0
Jux na Vanessa Mdee hawataki tena kuficha uhusiano wao. Tangu mwaka mpya uanze, waimbaji hao wameuachia ulimwengu ufahamu kuwa ni wapenzi na wanapenda baada ya kipindi kirefu cha tetesi za uhusiano wao ambazo walikuwa wakizikanusha.

Uhusiano huo umepelekea hadi Jux amtumie Vee Money kama mpenzi wake kwenye video ya ‘Sisikii’ na kama umeitazama utakuwa umegundua chemistry ya kuvutia kati yao.

Weekend hii wawili hao wakiwa pamoja na Navy Kenzo, walikuwa na show visiwani Zanzibar ambapo Jux pamoja na kutumbuiza nyimbo zake, alipanda jukwaani kumpa kampani mpenzi wake huyo kwa kuchukua nafasi ya Barnaba wakati alipokuwa akitumbuiza wimbo ‘Siri’.

Baada ya show hiyo wapenzi hao walijumuika pamoja kula upepo kwenye beach za Zanzibar na mashabiki wao wanafurahia tu kuwaona pamoja.

Jack Patrick Kabla hajakamatwa na Madawa ya Kulevya Maccau Ndio alikuwa Mpenzi wa Jux , Akitoka Jala Atakuta Jux si wake Tena.....

Masogange :Sina Mpango Wa Kurudi Bongo Karibuni, Subirini Kwanza Huku Ndo Kuna Maisha

$
0
0
Mrembo aliyejizolea umaarufu katika video mbalimbali za wasanii Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa hatarajii kurejea nyumbani hivyo mashabiki wake watamsubiri sana.

Akizungumza na mwandishi wa Udaku Specially kwa njia ya simu, Masogange alisema kuwa alivyoondoka nchini na kuelekea Afrika Kusini ameona baadhi ya vitu vyake vinamuendea sawa na maisha yake yanasonga mbele siku hadi siku na kwa kuwa ana uraia wa Afrika Kusini, hategemei kurudi hivi karibuni.
“Bongo kwa sasa wasubiri kwanza kwani kuna vitu muhimu sana nafanya huku na nikishakamilisha nitakuja Bongo kidogo kusalimia maana siku hizi si unajua ni wa hukuhuku,” alisema Masogange.

Here is One thing ZARI and BEYONCE Have In Common

$
0
0
Ugandan socialite and Diamond Platnumz girlfriend, Zari Hassan and an American singer, songwriter and actress, Beyonce have one thing in common ... but it is weird and very annoying one to their beloved ones — find out what it is!

Zari was photoed peeping at Diamond platnumz phone while he was busy texting — as they say watch your man. Is she worrying about diamonds ex-girlfriend Wema sepetu..?

Same thing happened to Jay-Z, her photo went viral showing her peeping at Jay's phone while he was texting..

She posted the above photo on Instagram and made a caption—  "Thought I was the only one who does this... where ma ladies at?" Refering to beyonces same thing as she did..

Well, she must be worries as now she is Exclusive to Diamond and they are expecting a baby together that means their Project is really serious now.

Nyumba ya Capt.John Komba iliyopo Dar es Salaam yapigwa Mnada Baada ya Kushindwa Kulipa Deni

$
0
0
Nyumba ya Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni Mstaafu, John Komba (CCM), yapigwa mnada. Nyumba hiyo ipo Kinondoni Maeneo ya Mbezi katika Jimbo la Kawe. Nyumba hiyo ipo katika kitalu namba 1030. Habari hii imechapishwa kwenye Gazeti la The Guardian la leo ukurasa wa 11.

 Siku za nyuma Komba alikua anadaiwa na bank ya CRDB millioni 900 aloshindwa kulipa. Hapo nyuma alijenga Shule inayooitwa Bakil Muluzi kule maeneo ya Mbweni, lakini biashara haikwenda vizuri. Ile Shule haifanyi vyema sana kibiashara. Nahisi hii ndo itakua sababu ya Kupigwa mnada kwa hii nyumba.

Wanafunzi wapigwa Mabomu ya Machozi Wakitadai Kiwanja chao cha Kuchezea

$
0
0
Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.

Polisi hao wakiwana Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi

Sakata la Kushushwa Kwa Bei za Filamu.Watayarishaji Filamu Nao Waibuka

$
0
0
Lile sakata la kushushwa kwa bei za filamu, limeingia katika sura mpya baada ya watayarishaji wa filamu nchini kujitokeza na kutoa malalamiko yao kwa Bodi ya Filamu, kuhusu kutoshirikishwa katika vikao vinavyoendelea.

Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara, TRA, TBS, imekuwa ikifanya vikao vya ndani zaidi ya viwili sasa na wasambazaji wa filamu ili kuzungumzia suala ya bei ya filamu.

Mtayarishaji wa filamu Mike Sangu aliliambia Gazeti la Mwananchi kuwa kitendo cha bodi hiyo kuendesha kikao pasipo wao kushirikishwa, kimewaumiza na kwamba wanahitaji haki itendeke ili biashara ya filamu isonge mbele kwa manufaa.

“Tunaiomba serikali kupitia vyombo vyake vyote vinavyoshiriki haya masuala ya filamu, kusifanyike mkutano wa aina yoyote ile kuzungumzia bei ya filamu bila kushirikisha maprodyuza, sisi ndiyo wenye filamu na ndiyo tunaotengeneza sasa iweje tusishirikishwe,” alisema Sangu na kuongeza:

“Inashangaza ikiwa msambazaji atapanga yeye bei, badala ya sisi ambao ndiyo wazalishaji, kwa sababu tungeweza kusambaza wenyewe, lakini tunawauzia wao ili wafanye biashara, hivyo lazima na sisi tujue nini kinaendelea, kikao cha pili tulipata taarifa juu juu kupitia watu tuliamua kuhudhuria ili kujua bei wanazopanga na sisi tuwauzie kwa bei gani, badala yake tulifukuzwa na kikao kikavunjika.”

Mwongozaji na mtayarishaji filamu Chiki Mchoma naye alisema kumekuwa na upotoshaji kwamba msambazaji mkubwa ndiye aliyeamua kushusha bei ya filamu, lakini wao ndiyo waliomtaka afanye hivyo.

“Kuna mkanganyiko wa bei kutoka kwa msambazaji mpaka kwa mlaji ndiyo umesababisha migogoro hii, ilianzia kwetu baada ya kuona hali halisi ya mfumo wa bei ya filamu bado haukui, soko linazidi kuyumba tuligundua kwamba wizi wa filamu umekuwa ndiyo mtihani wetu, tukaona kuna kila sababu ya kuhakikisha tunaudhibiti, tulimuomba msambazaji mkuu ambaye ni Steps Entertainment kuhakikisha kwamba anatafuta mbinu mbadala,” alisema Mchoma.

Alipoulizwa kuhusu sakata hilo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Ukaguzi wa Michezo ya Kuigiza Tanzania, Joyce Fisoo alisema hawajawatenga watayarishaji, bali walizingatia upande mmoja kwanza kwa kukaa na wasambazaji ili maamuzi yatakayofikiwa wayatangaze kwa wasanii wote kwa ujumla.

“Tunapoendesha vikao vinavyohusu masuala ya filamu, huwa tunafanya kwa makundi, sasa suala linalowahusu wasambazaji, hatuwezi kukaa na watayarishaji lazima tutashindwa kufikia muafaka, sisi hatubagui mtu bali kila mwana tasnia huwa tunakutana naye na kuzungumza naye,” alisema Joyce.

Alisema suala la kibiashara limewafanya wazungumze na wafanya biashara ambao ni wasambazaji, bali watayarishaji nao wangeshirikishwa baadaye.

“Kikao cha wiki jana tulikaa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, TBS, TRA, Cosota na wengineo ili kufikia muafaka. Kikao cha juzi hakikuwa cha kupanga bei bali kilihusu maadhimio ya kikao kilichofanyika Desemba 30 mwaka jana,” alisema Joyce.

Alisisitiza kuwa watayarishaji bado wana nafasi yao na wataitwa ili kutoa ushauri wa nini kifanyike kuhusu sakata hilo, kwani serikali ilihitaji kupata taarifa kutoka upande wa wasambazaji kwanza.

Mwananchi

CRAZY: What's Wrong With This Secretary....One word to her

$
0
0
CRAZY: What's  Wrong With This Secretary....Bosi Hana Hamu anakaliwa Mikao Mbali Mbali ya Kumtega ila bosi kakaza hategeki
One word to her!!!

Nani Mkali Kati ya Jokate na Lulu Michael Katika Hizi Picha zao Mpya za Mwaka 2015

$
0
0
Jokate Mwegelo na Elizabeth ‘Lulu’ Michael wameshare zao za walizopiga kwaajili ya miradi yao mipya. Kupitia Instagram, warembo hao wamewaonesha mashabiki wao muonekano wao wa 2015 na jinsi walivyo warembo. Lakini yupi ni zaidi? Tazama picha hizi na kisha weka maoni yako chini.

Lulu Michael

Lulu Michael Katika Pozi

Jokate Katika Mapozi Tofauti


Aunt Ezekiel Achukizwa na Mabishano ya Kidini Yaliyozuka Baada ya Posti Yake!

$
0
0
Aunty Ezekiel 
Mwigizaji wa filamu Aunt Ezekiel ambae kwasasa ni mjamzito, amechukizwa na kitendo cha baadhi ya watu ambao ni followers wake kwenye mtandao wa Instagram kumshambulia na kuzua malumbano ya maswala ya Dini, hii ilitokea hapo jana (Jumapili) mara baada ya mwigizaji  huyo kubandika picha (hiyo hapo juu) mtandaoni na kuandika maneno haya “When Jesus say YES no body can say No …..Happy me”

Kitendo hiki kiliwafanya baadhi ya watu wenye imani tofauti na ukristu kuibuka na kuanza kumshambulia kwa maneno ambayo yalikuwa ya kiponda imani yake na huku baadhi ya watu nao wakijibu mapigo kwa kujibishana, kitu ambacho kilisababisha malumbano ambayo Aunt Ezekiel hakufurahishwa nayo na hivyo akaweka bandiko jipya ambalo lilisomeka kama ifuatavyo;

"Dini ni Imani ya Mtu toka Moyoni mwake plz Ukijua dini yako inatosha usilazimishe kujua na yawenzako Naheshimu na Kuamini Dini zote mbili usitake kujua zaidi Alhamdulilaah kwa yote Muwe na jumapili Njema dah!"

Jamani tukubali kila mtu na imani yake, hata kama hauipendi ya mwenzako, mheshumu basi.

Dunia Kwisha! Wakamatwa na Polisi Kwa Kushiriki Mapenzi ya Jinsia Moja' Usagaji' Kisa Hichi Hapa

$
0
0
Lucy na Maua Ambao wote ni Wasichana Wanao sagana
DUNIA imekwisha! Wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24), mkazi wa Stakishari, Ukonga wilayani Ilala na Lucy Fred (23), mkazi wa Karakata jijini Dar es Salaam, wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga, Dar kwa kesi yenye jalada STK/RB/463/2015  wakidaiwa kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Warembo hao walikamatwa Januari 12, mwaka huu saa sita mchana, nyumbani kwa Maua wakidaiwa kufanya ngono kinyume cha sheria ya kujamiiana ambapo watu wa jinsia moja ni makosa kukutana kimwili.

NDUGU, MAJIRANI WAKERWA 
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, kukamatwa kwa Maua kulitokana na taarifa za baadhi ya ndugu na majirani zilizopelekwa polisi kwamba, wasichana hao wanapokuwa kwenye tendo la ndoa wamekuwa wakipiga kelele za udhalilishaji kwa familia zao.

WALISHAONYWA, HAWAKUSIKIA
Vyanzo makini kutoka jirani na makazi ya Maua vinadai kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu walijitolea kuwaonya wasichana hao kuwa na staha wawapo kwenye faragha yao lakini pia wao ni wanawake haiwezekani wacheze mchezo huo wenyewe kwa wenyewe lakini hawakutaka kusikia.

MAJIRANI WAFUNGULIA REDIO SAUTI YA JUU
“Ilifika mahali wakiingia chumbani kuanza mambo yao sisi majirani tunazidisha sauti za redio ili watoto wasisikie lakini na wao sauti zao zinakuwa juu kushinda za redio,” alisema jirani mmoja akiomba jina lake lifichwe ili kukwepa uhasama.

Alisema kutokana na hali hiyo waliamua kufikisha habari hizo polisi kwani ni kinyume cha sheria watu wa jinsia mmoja kukutana kimapenzi.

HISTORIA YA LUCY
Wakizidi kuzungumza na Uwazi, majirani hao walisema, Lucy ambaye ndiye anaitwa mke na Maua amekuwa akitoka nyumbani kwa wazazi wake Karakata kwa lengo la kumfuata Maua.

SIKU YA TUKIO
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, majirani walipoanza kusikia ‘zile sauti zao’, waliwapa polisi namba ya simu ya mtu wa jirani na Maua kwa lengo la kusaidia kufika nyumbani hapo.

“Polisi walipofika waligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa na kelele za mahaba zilizidi kusikika.  Baadaye, nadhani wakati wanapumzika sasa, Maua alifungua mlango mkubwa na kukutana na macho ya polisi, wakambana na kumtaka waende wote alipo Lucy, wakaenda chumbani na kumkuta.
“Pia polisi walikuta kidude ambacho huwashwa kwa betri kilichodaiwa pia hutumika wakati wa tendo,” kilisema chanzo.

HISTORIA YA MAUA
Maua ni binti ambaye ni yatima, amekuwa akiishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo kubwa ya familia  hivyo kumwita Lucy mara kwa mara kwa madai ya kufanya ufuska huo kwa vile wana uhuru.
Inasemekana kuwa, Maua siku zote amekuwa akivaa mavazi ya kiume licha ya kwamba, ni mwanamke kamili.

POLISI WASHANGAA
Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya jeshi la polisi zinadai kwamba, hata wakiwa mahabusu ya kituo hicho, wawili  hao wamekuwa wakioneshana mapenzi baina yao kitendo kilichowashangaza mahabusu wengine na polisi pia.

Uwazi lilifika nyumbani kwa Maua na kukutana na mdogo wake aitwaye Aziz ambaye alikiri kukamatwa kwa Maua na kwamba tangu akamatwe hajarudi na wala hajui kinachoendelea huku akisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa sababu ya kutupiwa lawama na wanandugu kwamba yeye ndiye aliyepeleka taarifa polisi.
Chanzo: GPL

Imebainika Kumbe Mtu Aliyefichua Maficho ya Osama Bin Laden Mpaka Akapatikana ni Kutoka Tanzania, Sasa Anawadai Marekani

$
0
0
Osama bin Laden in Pakistan
Did information that led to the killing of Osama bin Laden in Pakistan in May 2011, originate from an informer in Dar es Salaam? This is the question begging an answer following new claims that a man who tipped off the US security agencies about the whereabouts of bin Laden in Dar es Salaam is now demanding his reward of $27 million.

Fresh details suggest that the informant revealed where bin Laden could be found via the US embassy in Dar in 2005. According to the International Reward Centre (IRC) website, originally the US claimed that bin Laden was located in 2011 using electronic intelligence. However, the website, www.internationalrewardcentre.com, disputes that, asserting that the work was accomplished thanks to an unnamed informant who walked into US embassy in Dar in 2005 to reveal that the then world’s most wanted terrorist was holed up somewhere in Abbottabad, in Pakistan.

But, The Citizen couldn’t independently verify these claims because efforts to get the US embassy officials yesterday proved futile. It is noted that until yesterday, the embassy had remained closed as all top officials had been on their year-end leave since December, last year.

 The IRC doesn’t clearly state how the alleged informant came to know about bin Laden’s whereabouts, but it insists that basing on evidence produced, the source was very valuable for indeed, he had connections with insiders within the al-Qaeda operations.

Fresh claims from IRC

 The IRC, a New Zealand-based company, which is acting on behalf of the informant, has electronic documents which show that an informant supplied the US embassy in Dar with information to the effect that bin Laden was in Pakistan in October 2005.

According to IRC, the informant also supplied the US State Department with the names of terrorist cell leaders in Tanzania, including their modus operandi, plus a brief on al Qaeda’s mission in Tanzania.

For the record, the US embassy in Dar was attacked by suicide bombers on August 7, in 1998, resulting in the killings of 11 people and injuries to 85 others.

“Given the magnitude of the information supplied to the US special agent, whose identity and those of his associates in Dar the website declined to disclose, one would expect the informant’s revelation to set off alarm bells from Tanzania all the way to the US…,” reads part of the report posted on the IRC website.

The website says the special agent never made any further contact with the informant and that’s also what IRC wants to know, and what the US State Department should want to know.

It further says it believes further information could have been readily provided if the US special agent in Dar had been more diligent in his communication with the informant.

 “Can anyone imagine the thoughts that would be going through an informant’s mind after passing on such highly sensitive information, in a land peppered with terrorists, then to receive no follow up communication? He was acting against his own physical safety; he put his life on the line for America, yet he has not received one cent of the $27 million reward offer, no acknowledgement, no call from the State Department, no thank you note, nothing,” the IRC says on its website

Picha:Amzika Mtoto Mwenzake Kutokana na Tatizo la Njaa

$
0
0
Hii picha imenitoa machozi, Mtoto huyu hakujulikana jina mara moja ameonekana akimzika mtoto mwenzie aliyekufa kwa ajili ya njaa huko Sudan ya Kusini.

Wakati wewe unakula, unashiba na kutupa chakula kingi, kuna wengine sehemu fulani wanakufa kwa ajili ya njaa, inatia simanzi sana.

Hata hapa nchini kwetu, zipo familia zinalala njaa, hazina mavazi na mambo mengi tu, tuzidi kuombeana ili Mungu awapatie ulinzi katika maisha yao.
Amen

Kinana Ampiga Stop Mwigulu Nchemba, Amtaka Asitishe Ziara Zake Zote za Mikoani

$
0
0
Mwigulu Nchemba Ziarani
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anadaiwa kuwa amepiga marufuku ziara zinazofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida amekuwa akifanya ziara za kuzunguka wilaya na mikoa mbalimbali kwa kutumia usafiri wa helikopta.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, maswahiba wake walidai kuwa wameona barua ambayo Mwigulu ameandikiwa na Kinana ya kumtaka kuacha kufanya ziara hizo mara moja.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa Mwigulu ni kwamba barua hiyo ya Kinana kwa sehemu kubwa inaeleza namna ambavyo amekuwa akifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya bila ushirikishwaji kamili wa makao makuu, mikoa na wilaya hasa kamati za siasa.

“Nimeona ile barua ambayo Mwigulu amenitumiwa, kuna sehemu inaeleza wazi kuwa kwa kauli na matendo yake ameonesha kujiandaa kugombea nafasi ya wewe, pia umeshaonesha kwa kauli na matendo yake kujiandaa kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.

“Na kwamba ziara anazofanya mikoani na wilayani zinamuelekeo wa kampeni, jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya chama,” alisema mmoja wa rafiki wa karibu wa Mwigulu wakati akizungumzia barua hiyo.

Alidai pamoja na maelezo mengine yaliyomo kwenye barua hiyo ya Kinana kwa Mwigulu kuna eneo ambalo anaagizwa kusitisha ziara zote na iwapo atataka kufanya ziara yoyote ya kichama itabidi apate kibali chake na kutakiwa kutekeleza maagizo hayo mara moja.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa Mwigulu ni kwamba sababu za kufahamu kama kuna barua ya onyo amepewa ni kutokana na kulalamikia kupewa barua hiyo. Hata hivyo, hawakuwa tayari kueleza kama amekubali kusitisha ziara zake au la.

Wakati kukiwa na taarifa hizo za Kinana kumpiga ‘stop’ Mwigulu kufanya ziara hizo baadhi ya wadau wa siasa wamekuwa wakihoji wapi anakopata fedha kwa ajili ya kukodi helikopta anayotumia kwenye ziara zake kwa kuzunguka mikoa mbalimbali.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali ambapo juzi alikuwa mkoani Tanga kabla ya kwenda Morogoro.

Hata hivyo, Mwigulu hakuweza kuelezea kama amepewa barua na Kinana inayomtaka asitishe ziara zake.

Tetesi:Ndoa ya Mh. Lazaro Nyalandu inapumilia Mashine

$
0
0
Ndoa ya Lazaro Nyarandu ambaye ni waziri wa Maliasili na Utalii na mrembo Faraja Kota iko 'ICU'

Kwa mujibu wa Mwanafamilia wa Waziri huyo hapa Arusha amehabarisha kuwa wawili hao kwa sasa wametengani sababu ikiwa ni kukosa uaaminifu kwa bwana Lazaro.

Kwa sasa Nyalandu yupo kwenye Hekalu lake Njiro Jijini Arusha na Faraja yupo kwa wazazi wake Dar es salaam.

Nyalandu anatuhumiwa kujirusha na vimada kwenye mahoteli makubwa hasa ya New Africa akiwa Dar es salaam ana hata nje ya Nchi.

Kilichomtia nyongo zaidi ni tuhuma za hivi karibuni kuwa mimba ya Aunty Ezekiel ni yake naame wanaendeleza uhusiano huku wakitaraji mtoto wakati wowote.

Nyalandu kwa sasa anahaha kumtuliza mkewe kwa kila jinsi na leo amemtumia ujumbe kupitiakipindi cha Clouds FM cha Leo tena kuwa anampenda sana na ni tulizo la roho yake.

Pia anahaha kunusuru ndoa yake ili ajiweke vizuri katika nia yake ya kugombea Urais October 2015.

~Jamii Forums

Lady Jaydee Atua kwa Mpiga Ramli wa Kihindi, ni Baada ya Kuachana na Gadner

$
0
0
Katika Kipindi chake cha Diary of Lady Jay Dee Mwanamuziki Huyo Maarufu ameonekana akiwa kwa Mpiga Ramli wa Kihindi Ambae alikuwa anamtabiria Mambo mbali mbali ya maisha yake katika mwaka huu mpya 2015
Baadhi ya vitu alivyotabiriwa ni hivi :

Anatarajiwa kufunga NDOA 2017 , Atapata Pesa Nyingi sana Mwaka huu ila zikisimamiwa na Mwanaume , Pia Kuna Dalili ya kupata Mtoto Kubwa tu ! so ni swala la Muda tu Mpo ??

Wasanii Ambao Hata Watoe Nyimbo Unajua tu Hamna Kipya, Sauti na Melody zile zile

$
0
0
1.Roma Mkatoliki,..beats zake karibia zote sawa,nyimbo zake zote ujumbe sawa(harakati)

2.Izzo Bizness yaanii huyu beats zinafanana kila wimbo,mfano chorus ya wimbo mmoja unaweza kuimbia nyimbo zake
zote bila tabu.

3.AY,huyu ndo hana kipya style ile ile,mfano video ya leo na nyimbo baada ya hapo kitu kile kile hamna kipya.

4.Tuda man,huyu hata huwezi kujua analia au anaimba,iwe wimbo wa starehe kama analia tu.

5.Stamina (huyu atachokwa mda si mrefu anadhani misamiati ndo kuwashika watu

6.Young Killer asipoimba bongo fleva hatadumu.

7.Linex nyimbo zake hamna tofauti,kinachomfanya asikike ujumbe wa nyimbo zake.

8.Ben Pol huyu naye hana kipya

9. Jaquar wa Kenya Naye Balaa Nyimbo zake zote zinafanana

10. Bob Junior Mzee wa Kulia kulia kila nyimbo

Toa mawazo yako na ikiwezekana ongeza list 

Mwigulu: Namzimia Sana Zitto -Kuliko Wanasiasa Wote vijana, ila Kwenye urais Anisubiri kwanza.

$
0
0
Mwigulu Nchemba na Zitto Kabwe Wakiteta Jambo
Mheshimiwa Rais mtarajiwa Mwigulu Nchemba aka KIKWETE WA PILI, jana alipoulizwa na Salama kwenye kipindi cha Mkasi kuhusu mwanasiasa gani kijana anayempenda Tanzania, alimtaja mshirika wake, yule kijana aliyetuhumiwa kushiriki kwenye njama za kukipakazia CHADEMA ugaidi ili kife kabla ya 2014, Mh ZITTO KABWE. Ila akaonya urais asubiri kwanza.

Toa Maoni Yako Kuhusu Wanasiasa Hawa Wawili

Warioba Azungumzia Tetesi za yeye Kuhamia Ukawa na Kuwania Uraisi 2015

$
0
0
Jaji Joseph Warioba
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema kamwe hawazi kugombea urais wala kurudi kwenye harakati za siasa na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema kuna ‘wakubwa’ fulani wanaoendesha kampeni ya kumkejeli na kumkashifu; huku wakizusha kwamba ana mpango wa kuhamia Upinzani; tuhuma ambazo alisema siyo za kweli.

“Miezi michache iliyopita, kulikuwa na habari zinazunguka kwa wakubwa fulani zikisema nimejiandaa kuhama CCM kwenda Ukawa. Nikaona ni katika mtindo ule ule wa kutaka kuchafua jina langu,” alisema.

Alisema: “Mwanzo, wakubwa hao walimchafua kwa kudai kuwa amemsaliti Mwalimu Julius Nyerere na sasa wamekuja na hoja kwamba anataka kwenda Ukawa na kufikia hatua ya kutaja hadi siku atakayotangaza kuhamia Ukawa jambo ambalo halikutokea.”

Alisema watu wanaoibua tuhuma hizo ndio wamekuwa wakimtukana, wakimkebehi na kumkejeli.

Alisema mwaka 1995 aling’atuka kwenye utumishi wa umma na mwaka 2002 aling’atuka kwenye uongozi wa chama ambako alikuwa kwenye vikao vya chama kwa takribani miaka 26.

“Na baada ya hapo sina hata wazo la kusema tena nirudi ama kwenye utumishi wa umma ama kwenye siasa, wanaosema hivyo wanaejenda yao. Yote haya yanayosemwa hanaya msingi, hakuna njia ambayo mimi ninaweza kurudi tena,” alisema.

Alisema hata kama angetaka kurudi kwenye siasa asingekwenda Ukawa bali angefuata taratibu za chama chake.

Lema: Nikimkuta Bungeni Muhongo na Chenge Siku Hiyo Ndio Nitafukuzwa Ubunge, Ntawashika Mikono na Kuwatoa Bungeni kwa Nguvu

$
0
0
Tarehe 27 January nakwenda bungeni kufanya kazi moja tu, nikimkuta Waziri wa nishati na madini Sospeter Muhongo bungeni ndipo nitafukuzwa ubunge moja kwa moja. Nikimkuta Muhongo bungeni na Chenge ambao ni wahusika wa Escrow bado ni viongozi mimi nitakwenda kumshika Muhongo nimtoe bungeni kwa sababu Katiba inaruhusu kila raia kukemea uovu.” Alisema GodBless Lema Mbunge wa Arusha mjini
Unakubaliana naye kwenye hilo au unampinga?

Rushwa Katika Vituo vya Radio..Kama wasanii wakubwa wanalalamika kushamiri kwa hongo redioni ili nyimbo zichezwe, kuna tatizo

$
0
0
Wasanii waliofanikiwa kufanya vizuri miaka ya nyuma na hadi leo majina yao ni makubwa walikuwa na bahati sana. Pamoja na kwamba muziki wa zamani haukuwa wa kibiashara kivile, ulikuwa walau na usawa kwakuwa kama msanii alikuwa na ngoma nzuri basi wimbo wake ulikuwa ukichezwa bila hiyana.

Kukua kwa muziki na mabadiliko ya hapa na pale kumeufanya muziki uwe mgumu sana. Matatizo ni mengi na asilimia kubwa ya wasanii wanalalamika.

Tatizo kubwa ambalo makala hii itajaribu kulimulika ni kushamiri kwa rushwa na hongo au maarufu kama ‘hela ya promo’ ambayo watangazaji na madj wengi huhitaji ili kucheza ngoma za wasanii.

Kama imefika wakati hata msanii mkubwa kama Ben Pol analalamikia jambo hili, basi ujue kuwa limefika pabaya na wamiliki wa vyombo hivyo wanatakiwa kuwa wakali.

Hongo inaua muziki, wanaposema huu muziki ni biashara wanatufumba, wanamaanisha kumwaga hela ndo kubaki kwenye kick zao,” alitweet Ben Pol. “Sasa hatushindani tena kutoa nyimbo kali bali tunashindana kumwaga hela…okay.. je, chipukizi masikini vipi, watatoka?” alihoji Ben Pol.

Ben Pol ni msanii mmoja tu kati ya wengi wanaokutana na vikwazo hivyo lakini kama kila msanii akiamua kuongea ya kwake, mambo mengi mazito yangeibuka. Na hebu fikiria tu kuwa kama Ben Pol ambaye kipaji chake kinajulikana na sikumbuki ni lini alitoa ngoma mbovu anaathirika na trend hiyo, vipi kwa wasanii wachanga?

Nafahamu kuwa wakati mwingine inakuwa sio rahisi kila wimbo kupata muda wa kutosha hewani, lakini kwa kupunguza playlist ya nyimbo za nje, kila ngoma kali ya msanii ina uhakika wa kuchezwa walau mara tatu kwa wiki.

Uongozi wa vituo hivi vya redio unatakiwa kuja na sheria zitakazowaongoza wafanyakazi wake kuhakikisha kuwa nyimbo zote zenye ubora na kali zinapata nafasi ya kuchezwa na kutoentertain kabisa ngoma mbovu.

Kama kila msanii mwenye kipaji na anayetoa ngoma kali atapata nafasi, hapo ndipo kiwanda chetu cha muziki kitakua.
~Bongo5
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images