Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Prof. Muhongo Kung'oka kabla ya Bunge kuanza la Sivyo Bungeni Hakuto Kalika

$
0
0
Habari nilizofikishiwa ni kuwa Prof.Muhongo atang'oka kabla ya Bunge linalotarajiwa kuanza week ijayo , hii ni kutokana na shinikizo kutoka nje na hofu ya Bunge linalotarajiwa kuanza hivi karibuni kutokukalika na uwezekano wa kutokea vurugu na mangumi ni mkubwa sana , kwani kuna wabunge hawajaridhika kabisa na jinsi Rais alivyoshuguliakia mapendekezo ya bunge kuhusu sakala la Escrow

Idris Sultan Atoa Jibu Kuhusu Mjengo wake Mpya Kama Amenunua au Amepewa

$
0
0
Swali lililokuwepo kuhusu mjengo wa kifahari ambao mshindi wa BBA Hotshots, Idris Sultan ni kama amenunua au amepewa, na tayari mshindi huyo wa $300,000 za Biggy ametoa jibu.

Idris amesema mjengo huo ni wa kwake, na ni zawadi kutoka kwa aliyekuwa boss wake:

Sasa hivi nina status flani kwahiyo natakiwa kujiweka vizuri kwasababu ni kioo cha jamii honestly I need to have a good house, Alikuwa boss wangu ni mwenye kampuni ya Alosco, niko nae karibu, amenipa, amenipa ina kama muda, nahamia huko Jumapili.” Amesema Idris kupitia 255 ya XXL ya Cl;ouds Fm.

Idris alipost Instagram picha ya nyumba hiyo iliyoko Mbezi na kumshukuru mtu aliyempa aitwaye Ghalib Said Mohammed ambaye alikuwa ni boss wake.
Idriss Sultam BBA Winner 2014

I have seen thousands of people through my life time, got helped and expected to do alot in return, broken and crushed with no one to pick me up. I have struggled from ground level with all sorts of sayings like “you will never make it” to where i am now. I have shaken millions of hands not knowing who has good intentions with me. The world is for everyone who has a dream and a good will to it. The world is for all who want to change lives and make people smile. The world full of good hearted people is a dream. I stand today and say “my name is Idris Sultan and am not that special, that unique, that strong than most of you. I just dared to go for what i want, put my heart to it and here i am today. This is just the beginning. You’re welcome to join.” Ghalib Said Mohammed you’re a man with a golden heart i will love to be like you in a blink of an eye. Thank you for my new house. #Godbless #Alhamdulillah #GSM #dream #achieve #dare #youCan #success

Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Ajifungua Ndani ya Daladala Baada ya Kumeza Dawa za Kutoa Mimba

$
0
0
Huyu ndio yule mtoto wa kidato cha pili kajifungua ndani ya daladala kwa Aziz Ally Dar.......anasoma Kesho sec
alijaribu kunywa dawa ya kutoa mimba mambo ndo yakawa hivo....yaani alivyovaa shungi sidhani kama mzazi wake ataamini....hivi nini kifanyike ili utapaji mimba kwa wanafunzi upungue/uishe....elimu ya mapenzi salama ifundishwe shule au wazazi wawe wawazi kwa watoto zao kuwaeleza njia salama za kufanya mapenzi maana KUMKATAZA haiwezekani maana inaonekana imeshindikana!

~Chanzo:Usipojipangantakupanga

Rais Kikwete afanya Mabadiliko katika Baraza la Mawaziri... Sitta, Mwakyembe wabadilishiwa Wizara!

$
0
0
Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo mchana, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Ombeni Sefue alitaja mawaziri hao wapya ambao wameapishwa leo jioni na wizara zao kwenye mabano kuwa ni: George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).

Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).

Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

Mwenzenu Nimetoa Penzi kwa Shemeji yangu Bila Kutongozwa, Imeniuma Sana

$
0
0
Ni rafiki yake na aliyekuwa mtu wangu kwani baada ya mtu wangu kufariki kwa ajali mwishoni mwa mwaka jana amekuwa karibu sana nami, ukaribu huu haukunitia mashaka kwani kipindi bado mtu wangu yupo tulikuwa tukiambatana naye sehemu mbalimbali zikiwemo za starehe na hata kwenye shida pia.

Sasa baada ya kumaliza msiba amekuwa akinitumia pesa kidogo kidogo kwani nasoma nje ya mkoa tunaoishi hasa siku za weekend na kuniambia "mwanafunzi nenda kapate mbili tatu maana najua ulikuwa umeshazoea", na kwa sababu tumekuwa kama family friend kwa muda mrefu sikutilia shaka hata kidogo. Toka mwezi wa kumi hadi juzi ndo alikuja kikaz huku ninakosoma na ndo haya yakanikuta.

Jana akataka kinitoa out kwa kwa kuwa kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya mitihani inayoanza jumatatu nikamtaka iwe jioni kwani muda wa mchana na asubuhi nitakuwa najiandaa kwa kujisomea, akasema na ndio utakuwa muda mzuri kwani hata yeye atakuwa ameshatoka kwenye semina pia.

Ilipofika jioni tukakubaliana tukutane kwenye resort moja hivi ambayo pia huwa kunakuwa na performance ya live band, na kweli ikawa hivyo kwa hiyo tulikula na kunywa pia. Muda wa kuondoka ulipofika dala dala zikawa zimeisha barabarani na kwa boda boda ni mbali kiasi kwamba ingeweza leta shida kwani nilikuwa nimelewa pia, tax kwa umbali ule ingekuwa ni gharama sana hivyo akanitaka niambatane naye hadi hotelin alikofikia kwan haina tatizo.

Kwa kuwa hata siku za nyuma nilishawahi kumsikia akisema kuwa yeye kama hajaamua kufanya mapenzi hawez kufanya hata kama atalala na mwanamke kwa mwezi mzima nikaamua kumwamini na isitoshe yeye ni shemeji kwa upande mwingne sikuhofia lolote.


Tukaingia kulala japo sikuvua nguo nililala na nguo zangu, sijui ilikuwaje mpaka ikawa hivyo sielewi nieleze ilikuwaje na hivi nilikuwa na pombe kidogo kichwani sielewi jamani,

Inaniuma sana kwani angenitongoza nisingemkubalia hata kidogo lakini ndo imekuwa hivyo,
nimechanganyikiwa, mke wake ni rafiki yangu sana hata sijui nifanyeje maana nikisema nimwambie nahatarisha ndoa yao, nikipiga kimya akijaga kujua itanielewaje, mwanangu na wanaye ni marafiki kiasi kwamba hata shule wanaenda kwa gari moja, nishaurini mwenzenu hata sijui nifanyeje.

Na kuhusu huyu shemeji yangu nifanyeje kwani siku zote walishasema muonja asali haonji mara moja hapa nimechanganyikiwa kiasi kwamba hata kujiandaa na mitihani tena siwezi na ndo inaanza jumatatu.Naumia sana hapa nilipo nimekosa uelekeo kuninusuru na hili janga.

Naombeni ushauri.

Mtangazaji Jerry Murro Kuzua Balaa Jipya Mjini

$
0
0
Baada ya kutoa documentary ya mgogoro wa ardhi Loliondo ikaleta utata, sasa kutoa ya pili. Na baada ya hapo atakuja na documentary ya kuonyesha jinsi biashara ya madawa inavyofanyika nchini, atakuja na yale majina aliyo nayo rais kikwete. Ameyasema hayo asubuhi alipokuwa katika kipindi cha asubuhi kinachorushwa live Clouds 360 clouds tv. Akiongea kwa jazba amesema haogopi yeyote na amejitoa mhanga.
------------------------

Try to make at least one person happy every day. If you cannot do a kind deed, speak a kind word. If you cannot speak a kind word, think a kind thought. Count up, if you can, the treasure of happiness that you would dispense in a week, in a year, in a lifetime!

Luiza Mbutu Amtaja Aliyemfundisha Aisha Madinda Kuvuta Unga na Kusababisha Kifo Chake

$
0
0
Msanii wa bendi ya Twanga Pepeta,Luiza Mbutu amesema kilichomfanya Aisha kutumia madawa ya kulevya ni uvutaji sigara uliompelekea kuvuta bangialiyofundishwa na Banza. Banza alikuwa anamchanganyia bangi na unga hadi ikafikia hatua ya kuwa addicted na na unga. Kabla ya Aisha kuaga dunia alikuwa ameachana na madawa ya kulevya,na kwenda Dubai kwa kudanganywa ni maswala ya bendi. Kumbe ni kwenda kuwa mfanyakazi wa ndani. Ndipo baada ya kukataa wakamnyang'anya pasport yake,ndipo akaenda kushtaki ktk ubalozi wa huko na kurudi Tanzania,akakutana na mashoga zake ambao alikuwa anatumia nao akawa anaendelea kutumia huku akiwa anatumia dawa za kuacha kutumia unga hadi kufikwa na mauti.
 Source: Radio Tumaini

-------------------
Every day I get up and look through the Forbes list of the richest people in America. If I'm not there, I go to work.


Wastara Amchunguza na Kumpiga Msasa Bond Kabla ya Kumuweka Wazi Kama Mpenzi Wake

$
0
0
Baada ya tetesi kuzagaa mitaani kwamba wasanii wa filamu Bongo, Wastara Juma na Bondi Bin Salim wanatoka kimapenzi, bidada huyo ameibuka na kufunguka kuwa bado hajamkubalia jumla Bondi kwani bado anamchunguza.

Akipiga stori na paparazi wa GPL, Wastara alisema anamrekebisha baadhi ya vitu ili aweze kuwa wake na kama hatabadilika, atampiga chini.

“Bondi ninamchunguza kwanza na kumpiga msasa awe wa tofauti na alivyokuwa zamani sijamtangaza rasmi kwa sababu kuna vitu bado sijajiridhisha kwake na naendelea kuvifanyia kazi nikijiridhisha basi ndani ya mwaka huu nitamtangaza rasmi,” alisema Wastara.
------------------------
Every day is a gift from God. There's no guarantee of tomorrow, so that tells me to see the good in this day to make the most of it.


Mwenyekiti Auawa Kinyama, Viungo Vyapikwa Kama Mboga Kwenye Sufuria

$
0
0
Mwenyekiti  wa Kitongoji    cha  Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa  shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa  viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri  na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  mauaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.

Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe  Meklina  Mussa na  ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na  kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.

Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga  waliingia chumbani kwa marehemu  na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.

 Alisema  baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu  kwa  kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu  akilia kwa uchungu.

Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.

Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu  na  kuziweka kwenye  safuria  jingine  kwenye moto   na kutokomea kusikojulikana huku  viungo hivyo vikiendelea kuchemka  ndani ya safuria hizo.

 Kidavashari alisema  mke  wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kukuta viongo hivyo vikiwa  ninaendelea kuchemke  kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake


 Amesema uchunguzi wa  awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji  kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora  ambae  alikuwa akimtuhumu marehemu  kuwa amemnyanya  mwanamke ambae walikuwa  na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua   kuhama nae kijijini  hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele  Wilaya Mlele

  Kamanda Kidavashari  alieleza   jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili

Angalia Video Mpya Kutoka kwa Yamoto Band ya Wimbo wao Mpya Nitakupwelepweta

$
0
0
Style ya muziki wanaoufanya imewafanya kupanda mashabiki wa umri tofauti,Yamoto Band wametuletea video yao mpya hii inaitwa Nitakupwelepweta, imeongozwa na Adam Juma.

Bonyeza play kutazama:


Mwanamuziki Diamond Amwaga Pesa Kwa Mashabiki wake Jukwaani Tamasha la Tigo Kiboko yao

$
0
0


Show ya kiboko yao jana ilikuwa ni vita nyingine kati ya Kiba vs Diamond vituko kadhaa vilijitokeza ikiwemo Diamond Kugawa kwa Kurusha Pesa kwa Mashabiki kitendo ambacho wengine wamekichukilia kama matumizi mabaya ya pesa kwa kuwaig a wanamuziki wa Marekani, Pia wengine wamechukulia kitendo hicho kuwa alikifanya ili kuzima watu midomo asizomewe.

Je wewe unachukuliaje kitendo hicho cha kumwaga pesa kwa mashabiki?

Okwi Anusurika Kifo Pambano la Simba Dhidi ya Azam

$
0
0
Mshambuliaji machachari wa timu ya soka ya Simba, Emmanuel Okwi, jana jioni amenusurika kifo baada ya kupigwa kiwiko nyuma ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu na kuzimia kwa dakika kadhaa uwanjani.

Mkasa huo ambao umethibitishwa na daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, ulitokea wakati wa pambano la ligi kuu ya Vodacom baina ya timu hiyo na Azam FC lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuisha kwa sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifunwa na Okwi wakati lile la Azam likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.

Kwa mujibu wa Gembe, Okwi alipatiwa huduma ya kwanza uwanjani hapo kabla ya kupelekwa kwenye zahanati iliyoko pia uwanjani hapo na kisha baadaye kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

“Ilikuwa mbaya sana na angeweza hata kupoteza maisha,” alisema Gembe na kuongeza;

“Tuliendelea kumpatia matibabu kwenye zahati ndogo uwanjani hapo mpaka aliporejesha fahamu ndipo tukaanza kuelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi yaliyochukua takribani masaa mawili. Ila kwa sasa yuko vizuri.”

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za daktari, Okwi atakuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa wakati akiwa chini ya uchunguzi kuangalia maendeleo ya afya yake. Hiyo ni pamoja na kuwa nje katika ratiba ya mazoezi ya timu hiyo.

Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu zilizopigwa wikiendi hii:
Kagera Sugar 1 –  2 Ndanda FC
Stand United 0 – 1 Coastal Union
JKT Ruvu 1 – 1 Mgambo JKT
Ruvu Shooting 2 – 1 Mtibwa Sugar
Mbeya City 2 – 2 Prisons
Polisi Moro 0 – 1 Yanga

Madai ya Kubeba Unga: Ray C Ajisalimisha Polisi

$
0
0
Baada ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ na baadaye ‘kustaafu’, madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ‘msala’ ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa hiyari yake ajisalimishe polisi.

Hivi karibuni, Ray C alijikuta akiangua kilio ndani ya Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar baada ya kuhusishwa na ishu ya uuzaji wa unga.

Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na ‘kumbloku’.

Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI.

Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi.

“Ray C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi,” alisema.

Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo, alisimama na jamaa huyo aliyekuwa akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na kumtaka Ray C ashuke ndani ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia kuwa alikuwa amebeba unga.

Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alisema kuwa yeye ni askari.

Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.

Baada ya kuona hivyo, Ray C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay lakini jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo Ray C alishindwa kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia waambatane hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge.

Jamaa huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa kasi na kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na alipoona wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo.

Ilisemekana kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku akiangua kilio.

Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima.

Alifunguka: “Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge baada ya kufika kwenye makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na trafiki akiwa pembeni, nikawasimamisha na kuwaeleza.

“Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.

“Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi.

“Bada ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume nikaongozana nao hadi katika gari langu na kupekua kila sehemu lakini wakasema hapakuwa na chochote kibovu, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa kituo akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda Hospitali ya Mwananyamala kumeza dawa."

Credit: Gpl

Wanawake Wengi Wanadanganya Wamefika Kileleni, Kuwa Makini

$
0
0
Haya mambo ya mapenzi yana uwanja mkubwa sana. Na kila mtu ana mapito yake kwenye hili swala. Kufika kileleni kwa mwanamke imegundulika sio wote wanafika kileleni, niwachache sana wanaofika japo ni wengi wanaosema nimefika kileleni kwa kudanganya, waongo.

Unajua kufika kileleni ni sifa katika maswala ya mapenzi na mwanaume anajisikia special kama amemfikisha kileleni mwenza wake na mwanamke anafurahi sana afikapo kileleni na kuona mwanaume amefurahia penzi lake so atafanya kila jitihada kuhakikisha anamfurahisha Mwanaume ikiwemo kujifanya analia eti anaumia japo wapo wanao umia kweli. Wanawake wanajua wakifika kileleni mwanaume anafurahi sana. So ili kumfurahisha mwanaume ataact kufika. Wajanja sana na wanatupenda jamani dah!!.

Hata hivo kuna baadhi ya sabau zinazosababisha adanganye awe ajifanye kufika kileleni. yaani unakuta mwanamke anajinyonganyonga, anapiga kelele, anakukumbatia kwa nguvu kama mtu anayetaka kufikia mshindo kumbe ni mbwembwe tu. Baadhi tu ya sababu chache ni:-

1. Wanafanya hivo ili kumlidhisha mpenzi wake wa kiume ili ajisifie kafanya kazi. anamtia moyo ili asijioni hawezi kitu. Kwana mwanamme inatakiwa umfikishe mpenzio.

2.Mwanamke anakua hayupo kwenye mood ya kufanya mapenzi so anaamua kujifanya anamaliza ili usiendelee kumsumbua. So atajifanya kafika kileleni na kukushukuru asante mpenzi wangu. yaani nmechoka hata siwezi kurudia tena. so anajifanya kafika ili kumfanya mpenzi wake amalize haraka/anamuongezea presha ya kumaliza.

3. Kama anaumia. Mwanamke kama anaumie atajifanya anafika kileleni ili kumuwahisha mpenzi wake kumaliza.

4.Akiwa amekasirika. Mwanamke akiwa amekasirika hawezi kufanya mapenzi kabisa, ndo maana wanashauri mfanye mapenzi miwa katika hali nzuri ya furaha. Hata hivo mwanamke anaweza kufanya mapenzi ili asimuudhi mpenzi wake. hata akifanya atajitahidi anahakikisha mwanamme unamaliza haraka kwa kukupa presha kana kwamba anafiaka kileleni.

5.Kukosa mbinu za mapenzi. Unapokua kwenye uwanja wa mapenzi au sita kwa sita wenyewe wanavoita, mwanamke ndie kocha. mwanamme cha kufanya ni kumsikiliza na kuchokua hints. Akikuambia nenda haraka haraka basi fanya, akikuambia punguza supidi fanya hivo, akikuambia tufanye hivi msikilize kwa makini vinginevo utamuudhi. Na ukishamuudhi ili akuage kwa uzuri atakuambia namaliza. akishamaliza mchezo umeisha.

6.Kuchoka. Mwanamke akiona mwanamme kachoka na bado anaforce basi atajifanya anamaliza ili kukufanya upumzike coz anajua akikuambia pumzika utajisikia vibaya ataonesha dalili za kufika kileleni. na wewe utaamini kweli kumbe wapi. hawa viumbe wajanja sana.

7.Sio wote wanaofikishwa kieleleni na uume hata ukeshe. So ni vizuri kumjua mpenzi wako. Kuna wanaofika kileleni just kwa kuchezewa sehemu zao, kunyonywa, kupapaswa n.k.

Zipo sababu kibao zinazo sababisha japo kwa leo nimewaelezea hizi chache. Japo nyingine ni za kiwizi wizi.

Ushauri wangu. Mwanmke na mwanaume ni vizuri kuwa muwazi kwa mpenzi wako. Sema kile unachotaka kufanyiwa. huna haja ya kufake. Wiki ijayo nikipata nafasi ntawaelezea mikao mizuri ya kufanya mapenzi ambayo itawanya kila mmoja afurahie na kufika Kileleni bila tabu.

Asante sana.

Kumbuka, Women can fake an orgasm, Men can fake a whole relationship .

------------------------------
A birthday is just another day where you go to work and people give you love. Age is just a state of mind, and you are as old as you think you are. You have to count your blessings and be happy.

Adris wa Big Brother Abakisha Mil 200 , Atahadharishwa Asipokuwa Makini zitaisha Bila Kujua

$
0
0
Stori: Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
Mambo ya fedha! Takribani wiki saba tangu anyakue zaidi ya Sh. Milioni 500 baada ya kuibuka mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan anadaiwa kubakiza takribani kiasi cha Sh. milioni 200 baada ya kudaiwa kununua mjengo wa ghorofa wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 300.
Kwa mujibu wa Idris, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar hivyo kwa sasa naye ni baba mwenye nyumba.

Jamaa huyo alitarajia kuhamia kwenye mjengo huo jana Jumapili.
Mjengo huo una vyumba kadhaa, sebule mbili, bustani na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Habari zinadai kwamba kama kweli ametumia kiasi hicho cha fedha huku akimshukuru mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed kwa kufanikisha jambo hilo, basi atakuwa amebakizi milioni 200 ambazo wataalam wa mambo ya uchumi wanamshauri kufungulia kampuni au biashara.

Wataalam hao walifafanua kwamba, Idris anatakiwa kuzitumia fedha hizo kujiongezea kipato la sivyo atazitumia kuhudumia nyumba hiyo kwa vitu kama kulipia bili mbalimbali, kodi na kuajiri wahudumu.
“Anaweza akaona kwamba kununua nyumba ni matumizi mazuri ya fedha alizoshinda lakini anatakiwa awe makini, aidha kwa kufanyia biashara au kutoa huduma itakayokuwa ikimwingiza kipato.

“Pia asisikilize watu wanasema nini juu ya fedha zake. Anatakiwa kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo kabla hajazipata,” alisema mmoja wa wataalam hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe.
GPL
------------------------------
Some days are just bad days, that's all. You have to experience sadness to know happiness, and I remind myself that not every day is going to be a good day, that's just the way it is!


Waziri Mpya wa Nishati na Madini, Simbachawene Ashikilia Msimamo wa Prof. Muhongo, Wazawa Hawawezi Kuwekeza kwenye Gesi

$
0
0
WAZIRI mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema ni vigumu kupata mwekezaji mzawa katika kazi za uchimbaji wa gesi, kwa kuwa kazi hiyo ni gharama kubwa duniani na kampuni za uchimbaji gesi hazizidi kumi.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, Simbachawene alisema kauli kwamba wazawa hawawezi kuwekeza katika gesi, iliyotolewa na aliyemtangulia, Profesa Sospeter Muhongo, haikueleweka vizuri.

Alifafanua kuwa Watanzania wanaweza kuwekeza katika nyanja ya utoaji huduma kwa wachimbaji wa gesi na kuongeza kuwa mpaka sasa kuna maeneo ya huduma ambayo Watanzania wangeweza kuwekeza, lakini hawajafanya hivyo.

“Kuhusu kutoa vitalu kwa Watanzania kila mtu angependa kupewa kitalu cha gesi. Ukipata kitalu ndio umeshatoka, hata mimi ningependa kupata kimoja halafu nikitoka nakwenda Huston (Marekani) na kukiuza na kutoka,” alisema.

Alisema la msingi ni kuhakikisha mikataba ya uchimbaji gesi, inanufaisha Watanzania wote na katika kutoa huduma kwa wachimbaji, atapigania Watanzania wapate fursa ya kuwekeza huko. Alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi na kuongeza kuwa lakini katika ushirikiano huo, lazima kuwepo na uwiano kati ya ushirikiano na maendeleo ya wananchi.

Kuhusu jukumu la kusambaa umeme, Simbachawene alisema atachukua Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuanza nayo, ili kuhakikisha mafanikio ya usambazaji umeme yaliyopatikana chini ya uongozi wa Profesa Muhongo, yanaendelezwa na hatimaye Watanzania wote wapate umeme.

Naye Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema anajua Watanzania wengi wanateseka kwa kunyang’anywa ardhi katika maeneo mbalimbali na hasa Dar es Salaam.

Amesema kwa kuwa amewahi kufanya kazi katika jiji la Dar es Salaam, ambako alikuwa Mkuu wa Mkoa, anajua hali ya unyanyasaji katika ardhi ilivyo na kuwataka Watanzania wenye matatizo na ardhi, kutoa taarifa ili wasaidiwe.

Lukuvi alikiri kukabiliwa na changamoto ya baadhi ya watendaji wasio waaminifu katika sekta hiyo na kuongeza atajitahidi kukabiliana na changamoto hiyo kwa uaminifu.
Chanzo:Habarileo.

Dr. Mwakyembe Aibua Mshituko.....Wasomi Wahoji Sababu za Kumwondoa Wizara ya Uchukuzi na Kumuweka Sitta

$
0
0
Wasomi na wananchi kadhaa jana walizungumzia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wengi wakihoji sababu za kumhamisha Dk Harrison Mwakyembe kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Rais alifanya mabadiliko kwenye baraza hilo baada ya mawaziri wawili kuanguka kutokana na kashfa ya uchotwaji takriban Sh306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Ikiwa imesalia miezi isiyozidi sita kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa na akitakiwa kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa Wizara ya Nishati na Madini na Profesa Anna Tibaijuka aliyekuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rais Kikwete alifanya mabadiliko 13, yakihusisha mawaziri wanane na manaibu watano.

Miongoni mwa mabadiliko hayo manane ya mawaziri, ni uhamisho wa Dk Mwakyembe kutoka Uchukuzi kwenda Afrika Mashariki huku Samuel Sitta, ambaye aliwahi kumwelezea mbunge huyo wa Kyela kuwa ni mmoja wa “marafiki wa kweli”, akihama kutoka Wizara ya Afrika Mashariki kwenda Uchukuzi.

Watu wengi walioongea na mtandao huu, walisema hakukuwa na haja ya kumhamisha Dk Mwakyembe kutokana na kazi nzuri ambayo ameshaifanya kwenye wizara hiyo, ambayo ina tatizo kubwa la usafiri wa reli, kuyumba kwa Shirika la Ndege (ATCL) na utendaji mbovu kwenye bandari, mambo ambayo Dk Mwakyembe alionekana kuyashughulikia kwa nguvu zote.

Sitta, mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, pia aliwahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

“Tulikuwa tunaziona jitihada za Dk Mwakyembe,” alisema mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Frank Tily. “Na kuhamishwa kwake kunamaanisha kuwa mambo yote yaliyokuwa yanaendelea yatatakiwa kuanza upya. Nashindwa kuelewa ni kwa nini waziri huyu amebadilishwa… ingekuwa bora zaidi kama angeachwa.”

Dk Frank Tily alisema kuwa kutokana na haja ya kuongeza mawaziri ili kuziba nafasi mbili zilizoachwa wazi, hakukuwa na haja ya kuwabadilisha wale waliofanya vizuri katika wizara zao.

Aliongeza kuwa nafasi ya uwaziri isiwe inajazwa bila ya sababu za msingi, bali ifanywe tu endapo kuna haja kweli ya kufanya mabadiliko na akasisitiza kuwa “wizara ya uchukuzi haikuwa na sababu za kubadilishiwa waziri.”


Naye mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, Samwel Chacha alisema kuwa, mabadiliko hayo yatakuwa na athari japo zinaweza zisionekane kwa muda mfupi.

“Mwakyembe alikuwa na mipango ambayo ilianza kuonekana na kudhihirisha uzalendo katika Wizara ya Uchukuzi. Kama angeachwa aendelee nayo, kungekuwa na mabadiliko ambayo yangetutambulisha Watanzania kwa kuwa na vitu vyetu kwa manufaa ya nchi nzima,” alisema Chacha.

Ofisa Mikopo wa Benki ya NMB, Tito Mwanjala alisema mabadiliko yaliyofanywa, yamekosa mwonekano mpya kutokana na wabunge wengi kukosa sifa zinazotumika kuwapata mawaziri hao.

“Baada ya Bunge kupitisha maazimio, Rais hakuwa na jinsi zaidi ya kutekeleza. Sura zimeendelea kuwa zile zile kutokana na kukosekana kwa watu wenye sifa kwa sababu waziri lazima awe mbunge ambaye anatoka chama tawala. Nadhani Rais atakuwa ametumia muda mwingi kuwapata mawaziri wapya aliowaingiza katika baraza lake,” alisema Mwanjala.

Aliongeza kuwa, mabadiliko yaliyofanyika katika Wizara za Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Uchukuzi, yanaweza yakawa na athari za kiutendaji kwani “viatu vya Mwakyembe vinaweza visimwenee Sitta” kutokana na muda mfupi uliobaki kwa waziri huyo kuonyesha tofauti iliyofanywa kwa muda mrefu na mtangulizi wake.

Hata hivyo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Musa Salum alikuwa na maoni tofauti kwa kueleza kuwa, mabadiliko hayo ni sahihi na kwamba anaamini kutakuwa na ufanisi katika wizara zote kutokana na wateule wake kuwa watendaji wazuri.

“Mabadiliko ya Waziri Mwakyembe na Sitta yatakuwa na faida kwa wizara zote mbili kwa kuwa hawa wote wanafanya kazi kwa kujituma. Kila mmoja ataanzia pale alipoishia mwenzake na kufikia malengo yanayotarajiwa,” alisema Alhaji Salum.

Alifafanua kuwa hata mawaziri wengine nao watakuwa na mchango mkubwa kutokana na jitihada walizozionyesha walikotoka na kumtolea mfano George Simbachawene kuwa alijituma vya kutosha alipokuwa naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi.

ACT Walia Kiongozi wao Kuuawa......Ni yule Aliyechinjwa Kinyama na Kupikwa kwenye Sufuria kama Nyama ya Kuku

$
0
0
CHAMA cha ACT-Tanzania kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika na tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masigo wilayani Mlele mkoani Katavi, Christian Kahongo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba, ilieleza kuwa chama hicho kinalaani mauaji hayo ya kinyama ambayo hayaendani na haki za binadamu.

Alisema walimkata kichwa na kukitenganisha kabisa na kiwiliwili kisha wakakata sehemu za siri na baadhi ya viungo vingine vya kichwa wakaanza kuvikaanga kwenye sufuria.

Alisema huo ulikuwa ni unyama wa ajabu ambao hatujawahi kuushuhudia.

ACT-Tanzania tumepoteza shujaa namba moja kati ya mashujaa wanaokiwakilisha chama chetu kwenye vyombo vya Serikali. Ndiye mshindi wa kwanza kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia ACT-Tanzania na alipita bila kupingwa na kuwa wa kwanza kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masigo kupitia ACT-Tanzania.

Tumepoteza shujaa kama chama taifa, Mkoa wa Katavi umepoteza shujaa, Jimbo la Mlele wamepoteza shujaa, vivyo hivyo kwa wanachama wa Kata ya Inyonga na tawi la Inyonga,” alisema Mwigamba.

Alisema chama kitashiriki msiba huo kwa kuwakilishwa na Mwenyekiti Taifa wa muda pamoja na Katibu wa Ngome ya Vijana Taifa.

Ikumbukwe kuwa wauaji hawana rangi, kabila wala vyama, pia hawachagui nani wa kumuua kama ilivyotokea hivi karibuni kwa askari wetu katika Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

“Sisi ACT-Tanzania tunalaani kwa nguvu zote mauaji haya ya kiongozi wetu si tu kwa sababu aliyeuawa ni kiongozi wa ACT-Tanzania, bali tutalaani na kupinga mauaji ya Mtanzania yeyote,” alisema Mwigamba.

Tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea Januari 24, mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa Christian Kahongo na kumuua kwa kumkatakata mapanga.

Ushuhuda Huu wa Mzungu Kuhusu Wauza Madawa ya Kulevya 'Unga’ Ufanyiwe Kazi

$
0
0
Kwa zaidi ya wiki tatu sasa, Watanzania wamekuwa wenyeji wa mgeni ambaye ujio wake nchini umekuwa wa aina yake. Tunaweza kusema ugeni huo siyo wa kawaida, kwani tumezoea kuona ziara za wanasiasa, wafanyabiashara na wageni wengine wengi kutoka katika mataifa mbalimbali wanaokuja kwa ziara za kiserikali na nyinginezo, mbali na watalii wanaotembelea nchi yetu kujionea vivutio lukuki vilivyosambaa kila sehemu.

Hata hivyo, ziara ya Padri John Wootherspoon, raia wa Australia aliyekuja nchini Januari Mosi, mwaka huu ni tofauti kabisa na ziara nyingine tulizozizoea. Yeye anaishi China na amepata kibali cha Serikali ya China kutembelea magereza mbalimbali nchini humo na kuwafariji wafungwa. Katika kufanya kazi yake hiyo katika magereza nchini China na majimbo yake ya Hong Kong na Macau, amekutana na wafungwa wengi kutoka nchi mbalimbali duniani na kugundua kwamba kilichowaingiza magerezani ni biashara ya dawa za kulevya.

Kabla ya kuja hapa nchini, Padri Wootherspoon aliliambia gazeti hili, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likifuatilia huduma zake katika magereza nchini China kuwa, alikuwa na mpango wa kuitembelea Tanzania baada ya kugundua kwamba idadi ya Watanzania wanaotumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini China ni kubwa mno ikilinganishwa na wafungwa wengine kutoka nchi nyingine. Anasema wafungwa zaidi ya 130 kutoka Tanzania wako katika magereza ya Shek Pik, Stanley, Loo Woo na Macau na kwamba kila mwezi Watanzania wanne hadi sita wanafungwa magerezani kwa makosa hayo.

Kutokana na hali hiyo, Padri Wootherspoon aliamua kuja Tanzania kwa gharama zake mwenyewe ili kuwasaidia wafungwa hao kuwasiliana na familia zao hapa nchini, baada ya kupata mawasiliano ya familia hizo kutoka kwa wafungwa hao. Anasema wafungwa hao walitumiwa tu na wafanyabiashara wakubwa (ambao majina yao tunayahifadhi kwa sasa) kupeleka dawa hizo nchini China na kwamba tangu awasili nchini amewasiliana na familia nyingi za wafungwa hao, ambazo amesema zimo katika umaskini mkubwa. Padri huyo tayari amekutana na Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, ACP Godfrey Nzowa na kumtaka aende nchini China kupata taarifa za kina kutoka kwa wafungwa hao.

Sisi tunadhani ziara ya Padri huyo hapa nchini ni fursa ya pekee kwa Serikali kupata taarifa muhimu za kusaidia kutokomeza biashara hiyo. Juni, mwaka jana Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi alisema wakati wa kuadhimisha Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kwamba kazi ya kuwanasa vinara wa biashara hiyo imekuwa ngumu na akisema vijana wa Kitanzania 65 kati ya 403 waliokamatwa nchi za nje kwa kuhusika na usafirishaji wa dawa za kulevya wamehukumiwa kunyongwa nchini China.

Waziri Lukuvi pia alisema vitendo vya rushwa vimekwamisha jitihada na mikakati ya kuwatia mbaroni vigogo wa biashara hiyo. Bahati nzuri ni kwamba Padri Wootherspoon yuko nchini kama sehemu ya suluhisho la tatizo hilo.

Ni matarajio yetu kwamba Serikali itafanya kila linalowezekana kushirikiana naye ili kupata taarifa muhimu zitakazosaidia kuwakamata wamiliki wa biashara hiyo. Hatua hiyo pia itaondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi kwamba kikwazo kikuu katika vita ya kukomesha uhalifu huo kimo ndani ya Serikali yenyewe.

Diamond Platnumz Agundua Dawa ya Wazomeaji Katika Show zake, Wazomeaji Wageuka Ghafla na Kuanza Kumshangilia

$
0
0
Msanii  anayetesa  katika  mziki  wa  kizazi  kipya  hapa  nchini, Nassib  Abdul  'Diamond  Platnumz' usiku  wa  jumamosi  iliyopita  alijikuta  katika  wakati  mgumu  baada  ya  kuzomewa  na  mashabiki  kwenye  viwanja  vya  Leaders  Jijini  Dar  es  Salaam.

Mbali  ya  kuzomewa, Diamond  pia  alirushiwa  chupa  za  maji  ambazo  zilileta  kadhia, lakini  Diamond  alionekana  akiwahimiza  madancer  wake  wafanye  kazi  iliyowapeleka  pale  licha  ya  zomeazomea  kuzidi  uwanjani.....

Msanii  huyo  alipoona  vitendo  vya  kutaka  kumkwamisha  asiimbe  vikiendelea, aliamua  kuwamwagia  fedha  mashabiki hao, ndipo  wakaacha  kuzomea  na  kuanza  kugombea  fedha  hizo  kisha  kuanza  kumshangilia....

Baadhi  ya  wadau  walisikika  wakidai, kundi  hilo  lililokuwa  likimzomea  liko  upande  wa  mmoja  wa  wasanii  mahiri  hapa  nchini.Wasanii  wengine  walioonja  joto  ya  jiwe  ni  pamoja  na  Khamis  Mwinjuma  'Mwana FA' na  Ambwene  Yesaya  'AY'.

Aidha, baadhi  ya  mashabiki  walilaani  vikali  tukio  hilo  la  kumzomea  Diamond  na  kumrushia  chupa  za  maji  ambazo  inadaiwa  zilikuwa  na  haja  ndogo  ndani  yake.

Mashabiki  hao  walisema  tukio  hilo  halipendezi  na  linapaswa  kukemewa  na  kuwataka  waratibu  pamoja  na  jeshi  la  polisi  kuzidisha  ulinzi  katika  matamasha  makubwa  kama  hayo.

Hii  ni  mara  ya  pili  kwa  Diamond  kuzomewa,tukio  la  kwanza  likiwa  kilele  cha  tamasha  la  Fiesta  mwaka  jana  kwenye  viwanja  hivyo.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images