Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Lemutuz Akata Watu Vidomo Waliosema Anagombania Chupa ya Coca Wakati Hana Jina Kwenye Hati ya Nyumba, Angalia Hapa

0
0

"Ok huwa sipendi maneno matupu napenda vitendo zaidi kuna mtu amenitumia ujumbe kwamba badala kugombea jina lako kuwa at Le Kopozzz pigania jina lako liwepo kwenye kumiliki HATI YA NYUMBA., namhakikishia aliyenitumia ule ujumbe kwamba HATI YANGU YA KUMILIKI SHAMBA LA EKA 5 NA NYUMBA hii hapa na huu ni mmoja wa urithi nitakaowaachia watoto wangu na bado naendelea kuchacharika na maisha kusudi ninunue hii apartment ninayoishi hapa downtwon na ile apartment yangu ya Changombe......sisi waKristo Bibilia inasema Baba mwenye busara huwachia watoto wake mali za urithi ndio maana nimekataa kuwa baba mwenye nguo ila baba mwenye majumba hahaha U know jamani USIKU MWEMA SANA LOVE U ALL! - le Mutuz

Inasikitisha:Aliyekuwa Mume wa Isha Mashauzi Akatwa Uume Kinyama Huko South Africa

0
0
Story Kubwa Leo Mitandaoni ni hii ya Jamaa Anajulikana kama Tevez Ambae alikuwa mume wa Isha Mashauzi , Kuna tetesi kuwa Amekatwa nyeti zake na washiriki wenzake wa madawa ya kulevya baada ya kuwadanganya wenzake kuwa Madawa yamepotea huko South Afrika..
Kuna picha zinasambaa akiwa amekatwa ili tumeshindwa kuziweka hapa live...Habari Hii Bado haijazibitishwa kama ni kweli ama laa..lakini ndo stori iliyosambaa leo
Ingia Hapa Ukitaka kuona.....<<PICHA>>


Kwa nini Leo Zitto Kabwe Alitia Mgomo wa kwenda kusoma taarifa ya PAC Bungeni?????.....Majibu yote Yako hapa.

0
0
Wakati  wa  Vurugu  za  Asubuhi  leo  Bungeni, Spika  wa  Bunge  alimtaka  Mwenyekiti wa  PAC, Mh Zitto  Kabwe  aende   kusoma  taarifa  ya  kamati yake....

Kilichotokea  ni  kwamba, Zitto  alitia  mgomo, nikiwa  na  maana  kwamba  alipuuza  agizo  hilo  na  hakunyanyuka  kabisa.
 
Unajua  ni  kwa  nini? Zitto  Kabwe  mwenyewe  amekwisha  lijibu  hilo  swali  kupitia  ukurasa  wake  wa   Facebook.

"Kwa  nini  sikwenda  kusoma taarifa  ya  PAC leo  nilipoitwa  na  Spika? Jibu rahisi  kabisa, siwezi  kuona madhila na uvunjifu  mkubwa  wa  HAKI  za  binadamu  nikaendelea  na  mambo  kama  hakuna  kilichotokea.Kitendo  cha  polisi  kutumia  nguvu, kupiga  raia  hovyo  na  kumdhalilisha  kiongozi  wa CUF, Profesa  Ibrahim Lipumba  ni  kitendo  cha  kulaaniwa  kwa  nguvu  zote"- Zitto Kabwe

Nuh Mziwanda: Shilole Nimekupa Ruksa, Nipige Mpaka Nikome!

0
0
Baada ya juzi kati, mwanamama Shilole kumpiga kofi mchumba wake Nuh Mziwanda mbele za watu, Jana usiku Nuh Mziwanda  ameibuka na kuandika bandiko hili mtandaoni.

Mwanaume lijali aliekamilika ampigi mpenzi wake wala kurudishia kibao au kofi alilopigwa na mpenzi wake.naamini kwenye mapenzi ya kweli wivu lazima na kugombana kwenye mapenzi ni kama kwenda chooni ni swala la kawaida sana.aaaaaaaya mke wangu nimekupa ruksa nipige mpaka nikome.ila all i know its love dats it.Nawapenda Mashabiki wangu pamoja sana ….zimaTaa sie tayari”Mziwanda aliandika baada ya kuweka picha hiyo hapo juu

Mh! Amakweli haya ndio mapenzi!! Kila la kheri……

Seth 'Unahitaji Kuoa Mke Malaya Kitandani, Mwanaume Amejaa Tamaa Masaa 24, Acheni Kuoa Vituko Alafu Full Michepuko'

0
0
Heri yako wewe unayesaka Mke mwenye TABIA NZURI,mi huo Msako nimeacha siku nyingiii,Kama ni Tabia nitamuazima Tabia zangu tukishaoana..Kisa cha Kujinyima vitu vizuri kisa nasaka MAMA PAROKO??

Wakati wa Kutafuta Mtoto TABIA HAITUMIKI,ni mwendo wa Ashki tu na jinsi ntakavyopagawishwa na kucha zake na amenigusa wapi..Unahitaji kupata Mke "Malaya wa Kitanda"
Nikirudi na Stress za kazini niikute hii figa iko ndani ya Bikini tu inanisubiri,anidake aanze "KUTUMA SALAMU KWA HISIA" huku analalamika kwa uongo na kweli...TABIA IKAE MBALI HUKOO

Nikialikwa mtoko na washkaji sina haja ya kujiuliza kama niende mwenyewe au lah,Ntamwambia "Mke wangu leo usiku tunatoka Outing,please DRESS TO KILL",na muda wote wa mtoko nitakuwa nimemshika kiuno ili kutuma Meseji kwa kila anayeniangalia kwamba "YES NAFAIDI HILI BUNO BURE DEILE" na hapa TABIA WALA HAIHUSIKI!Kuna watu kila ukiwaalika hawaji na wake zao japo walioa TABIA,kisa MKE HAANGALIKI MARA 2...Mi sitaki hayo mambo...Nataka nikishtuka Usiku wa Manane pamoja na lepe la usingizi kunizidia lakini macho yangu yapangue giza totoro la chumbani nione HILI BUNO pembeni yangu,nilishike kwa uchu halafu nimshtue taratibu,"BEBI NAOMBA KIMOKO"

Goodnite Wasaka Tabia Njema,Ndo maana mnaibuka na vitu kichefuchefu mpaka unajisemea LABDA ALIPEWA DISKAUNTI YA MAHARI!
Mke wangu wa Milele lazima awe ANANISHTUA NIKIMUONA,Tabia ntampunguzia za kwangu!
Usioe Mke ana Shepu kama TANGAWIZI eti kwa kisingizio cha TABIA,Mwanaume amejawa Tamaa Masaa 24,mnaoa vituko halafu full kuchepuka na MABUNO,Tabia nzuri waachie MAKATEKISTA!

By Seth

Njama za Kumrushia Wema Sepetu Mavi na Mkojo Kwenye Show Yake Yoyote Atakayo Fanya Zabainika

0
0
Ujumbe huu umetoka kwa mmoja wa shabiki wa karibu wa wema sepetu anyetumia acount hii
@mtaawapili ya instagram :

"Bad new nimezipata jana kuhusu wemasepetu dah mpka nimelia kwa uchungu kwanini teamdiamond na teamzari wamejipanga vizuri kumrushia wema mavi na mkojo kwenye show yake yyote atakayo fanya jamani mtto watu amefanya nini kwanini msimtafuteni wagomvi wa daimond sio wema. kisa ni kile kichotokea last week sasa hapa wema anaingiaje halafu sisi wabongo werevu sana hiyo nyaukomwe watu wako wanamtukana kila siku kwako hakuna mtu yyote anayempenda ndio maana nguvu yake kubwa bongo someni kwenye blog zako umeone mambo yake halafu hajuwi cchote nyie ........ kali kabisa kumbe bibie ana mpambe wake mkubwa ktk kundi la daimond wanataka kumpotea wema kabisa kwenye game coz bibie anajuwa wakati wwote diamond atarudi kwa wema kicho kitu hakuna kabisa njaa mbaya na yule linda anavyomtukana wema yaani lam speechless mtu wa karibu sana na wema ana comment kila na kulike soon nitamtaja nani...salamu hizi ni kwa teamwema wote na wale wanaopenda wema ninachakufanya kustop kuchukua mfano wema mdogo wako utajisikiaje ukisikia hili dah kwani wema amekula kitu cha mtu pls muacheni pls.. Haya wadau hayo ndio yalojiri huku insta team zikijibizana una ushauri nn kuhusiana na tukio hilo" By Mtaa wa Pili

Polisi Wamkamata Wema Sepetu Kwa Madai ya Kupiga Muziki Kwa Sauti Usiku

0
0
KATIKA hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo.

Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema.

Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.

“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu vibaya.


“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.


“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama  kwa ajili ya hatua za kisheria,” alisema.


Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa, alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye sherehe hiyo.

Imeandikwa na Gladness Mallya, Musa Mateja na Hamida Hassan.


Utata wa video ya Mchungaji iliyozagaa mitandaoni akiwa UCHI Afrika Kusini

0
0
Mchungaji maarufu Afrika Kusini Sthembiso Zondo ambae huwa anatoa mahubiri yake kwa njia ya Redio nchini humo, ratiba ya kurushwa kwa mahubiri yake imesimamishwa kurushwa hewani  baada ya kuvuja video inayomuonyesha akizungumza kwenye simu huku akiwa hajavaa nguo yoyote.

Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC) limetoa amri ya kusimamishwa kwa Kipindi cha mchungaji huyo hadi itakapotangazwa tena, maamuzi yaliyotolewa baada ya video inayomuonyesha Mchungaji Zondo akiwa hajavaa nguo iliyowekwa kwenye mitandao. Video hiyo inaonyesha kuwa ilirekodiwa na mwanamke aliyekuwa amevaa skirt ya pink lakini hakuweza kutambulika.

Taarifa zinasema kuwa Zondo aliomba radhi kutokana na kuvuja kwa video hiyo, japo kulikuwa na mvutano pia wengine wakilaumu aliyevujisha video hiyo huku wengine wakimfata mchungaji huyo ajieleze kuhusu video hiyo.

Video  iko  hapo  chini

Mwigizaji Bond na William Mtitu Katika Beef, Baada ya Mtitu Kusema Yeye Ndio Atakaye Mzika Sio Wahindi

0
0
Na Hamida Hassan/Amani
Mtangazaji na msanii wa filamu Bongo, Bond Bin Salim  ‘Bond’ hivi karibuni amemtupia kijembe msanii na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Five Efects,’ William Mtitu kwa kuhmwambia kuwa msemo wake wa kuwazika watu yeye ndiye anawaua?

“Namshangaa Mtitu, naomba ahojiwe, je, yeye ndiye anawaua wasanii? Kwa nini anapenda kusema mimi ndiyo nitakuzika siyo Mhindi?” alihoji Bond.

Baada ya kijembe hicho mwandishi wetu alimwendea hewani Mtitu ambaye alifafanua msemo wake na kusema: “Mimi ninavyojua huo ni msemo, hivi wasanii wakifariki si tunazikana wenyewe kwa wenyewe? Je, kuna ubaya gani wa kusema mimi ndiyo nitakuzika? Sipendi kumuongelea Bond kwa sababu ni mdogo san

Marando Amshukia Kikwete Asema Naye ni mtuhumiwa Escrow

0
0
RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.


“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Nimekuwekea Video ya dakika 10 ya Kipigo kizito Alichopewa Lipumba na Wanachama wa CUF

0
0
Hii  ni  Video  ya  kichapo  kizito  toka  kwa  polisi  walichopewa  wanachama  wa  CUF  wakati  wa maandamano  yalioyoongozwa  na  Mwenyekiti  wa  chama  hicho, Profesa  Ibrahim  Lipumba.


-----------------
 Peace cannot be kept by force; it can only be achieved by understanding.

Ndoa ya Wolper Yabuma......Wazazi wa Manaiki Sanga Wamkataa..Kisa Hichi Hapa

0
0

Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga,amesema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwa sababu wazazi wake wamemtolee nje ishu ya kwenda kumposa staa wa kike Bongo, Jacqueline Wolper.

Akizungumza kwa masikitiko, Manaiki alisema kuwa hivi karibuni alifunga safari na kwenda kijijini kwao Mbeya kwa ajili ya kuwaeleza wazazi wake nia yake ya kumuoa Wolper lakini imekuwa tofauti kwani wamemwambia kama anataka kuoa msichana atatoka nyumbani kwao.

Yaani nimeamini kabisa mbio za sakafuni huishia ukingoni, sikujua kama wazazi wangu watanikata maini kwa kuwa nilijua wazi hawatakuwa na kipingamizi lakini wameniambia kuwa lazima nioe nyumbani,” alisema.
-------------------------------
Learn from yesterday, live for today, hope for tomorrow. The important thing is not to stop questioning.

Sista wa Kanisa la Roman Katoliki Ajifungua Mtoto wa Kiume

0
0
Utata umeibuka  baada ya sister wa Kanisa Katoliki huko Italy aliyekuwa akilalamikia maumivu ya tumbo na kukimbizwa Hospitali na kujifungua mtoto wa kiume licha ya kuishi katika Jumuiya hiyo ya wanawake watupu.

Sister huyo  mwenye umri wa miaka 31 yupo kwenye kikundi cha masista cha Santa Chiara Italy, asili yake ni Amerika ya Kusini, alilalamikia maumivu makali  ya tumbo baadaye alianguka, madaktari walifika katika eneo hilo na baada ya kumfikisha Labour alijifungua.
Watu wengi wameshindwa kuelewa kwa jinsi gani ameweza kupata ujauzito licha ya kula kiapo cha usafi wa moyo na utii.

Dada wa Diamond Queen Darleen Achochea Bifu la Diamond na AliKiba 'Machupa kiboko yake Pesaa'

0
0
Mwanamuziki ambae ni dada na Diamond Platnum Queen Darleen amezidi kuchochea chuki na bifu kwa mashabiki wa Ali Kiba na Diamond Platnum baada ya kupost maneno ambayo mashabiki hao wanaona ni kama anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa wanamuziki hao ambao kwa sasa wamekuwa na ushindani mkubwa kimuziki.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na show kubwa ya muziki ambayo ilifanyika katika viwanja vya Ledears Club ambapo katika show hiyo iliwakutanisha Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba ambao kila mmoja alipata mapokezi tofauti kutoka kwa mashabiki wao.

Katika show hiyo kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa na furaha kushuhudia show ya wakali hao wawili wakati show inaendelea msanii Diamond Platnum aliweza kuwarushia noti za buku mbilimbli mashabiki wake.Kufuatia kitendo hicho ndipo msanaii Queen Darleen amefunguka na kusema kuwa dawa ya machupa stejini ni pesa. "Machupa kiboko yake pesaa,tunasaka hela na wewe saka"

Mashabiki wa Queen Darleen wameonyeshwa kutofurahishwa na kauli ambayo imetolewa na dada wa nyota wa muziki Diamond Platnum na wao wanaamini kuwa msanii huyo anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa Diamond pamoja na Ali Kiba

Sitta Awashukia Wadokozi Bandarini Wasipewe Dhamana, Awaita Wahujumu Uchumi

0
0
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema angependa kuona sheria inayataja makosa ya udokozi bandarini kama ya uhujumu wa uchumi ili watuhumiwa wanapokamatwa na kushtakiwa wasipewa dhamana.

Waziri Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), katika mfululizo wa ziara zake kwa mashirika, taasisi na mamlaka zilizo chini ya wizara yake kwa lengo la kufahamiana na kujua changamoto na kupanga mikakati yake katika utendaji.

Akizungumza katika mkutano na watendaji TPA, baada ya kusikiliza taarifa ya utendaji kazi iliyohusisha mikakati, mafanikio na changamoto za mamlaka hiyo, Sitta alisema duniani kote bandari ni kitovu cha uchumi wa nchi.

Alisema vitendo vyovyote vya udokozi na hujuma vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu ni kuhujumu uchumi wa Taifa, hivyo angependa kuona wahusika wanashtakiwa na kunyimwa dhamana.

Akizungumzia utendaji, Waziri Sitta aliwataka wote wenye mamlaka ya kufanya uamuzi kwa mambo mbalimbali wafanye hivyo bila woga wala kusubiri kushauriana na mamlaka nyingine.

“Nimekuja kuwaimarisha katika kufanya uamuzi, tuliowapa mamlaka lazima wawe na uamuzi wa haraka lakini uwe sahihi,” alisema Sitta.

Alisema katika kipindi cha miezi 10 kilichobaki cha uhai wa Serikali, ana kazi ya kufanya katika wizara hiyo ili wananchi waone mafanikio makubwa.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPA, Madeni Kipande alisema bandari imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, kwani inachangia kati ya asilimia 35 hadi 40 ya mapato ya Serikali. Alisema mapato yaliongezeka kutoka Sh389 bilioni mwaka 2011/2013 hadi kufikia Sh539.7 bilioni mwaka 2013/2014.

Mwanamuzi Bob Wine Yamkuta Makubwa, Amlea Mtoto kwa Miaka Saba Akizani Wake, Afanya DNA Test na Kugundua Makubwa

0
0
Staa wa muziki wa nchini Uganda, Bobi Wine ameibuka na kusafisha jina lake kwa kusema kuwa, tetesi za yeye kugundua kuwa alikua analea mtoto Simon ambaye si wake bila kujua kwa miaka kadhaa sasa ni za kweli.

Bobi wine ameelezea kuwa hili jambo halitamfanya yeye kumtenga mtoto huyo ambaye amekuwa akimtunza kama wake kwa muda wote.
Bobi Wine amesema kuwa, ataendelea kumtunza mtoto huyu kama sehemu ya familia yake kutokana na mahusiano makubwa ambayo tayari yalikwishajengeka kati yao ingawa atahitaji mama wa mtoto huyu kuomba msamaha kwa kila pande kwa kuficha ukweli juu ya ishu hii kwa miaka yote hiyo.
Taarifa za awali ziliweka wazi kuwa star huyo ameamua kukata mawasiliano pamoja na mahusiano kati yake na mtoto huyo pamoja na mama yake baada ya kugundua ukweli huu wa kushtusha, hatua ambayo ameikanusha kabisa.

Haya Hapa Ameandika Bob Wine:


"This is my whole story and I have evidence on everything. 7 years ago I met a one gal in London called Safina. By then I was not married and I made a mistake of my life. It was once and the next week this gal claimed that she was pregnant. Ng'omusajja omuganda I was happy to have a new member of the family. I have been taking responsibilities as a father and no one was complaining."

"This Christmas season, I invited Simon as my son to spend the festival with his fellow brothers and sisters. As soon as the boy landed in UG from UK, I said no, I have to do it this time,  so I secretly without any other persons knowledge took him for a DNA test coz for so long I have been suspecting this."

"Ashburg to my surprise or let me call it shock relief, the results are back and guess what? SIMON KYAGULANYI is not my son. Not even Barbie or Saphina knows this. I have decided to make u a star by giving u this info first and any question about this u will be the first to get the answer."

Proof of DNA test results and other concrete evidence will be out. I'm so sorry for my boy Simon but your mum is responsible. I'm sorry Barbie that you had to go through such pain, I'm sorry my family and fans. Shadrak, Shalom & Solomon are my only 3 biological kids as of 20th/01/2015."

Diamond Platnumz Tusamehe Watanzania Tumezoea kuitwa 'Kichwa cha Mwendawazimu'

0
0
Kwanza naomba ni declare interest kuwa mimi ni shabiki wa maendeleo katika nyanja zote. Lakini kwa leo nitazungumzia muziki wetu hapa nchini (Bongoflava). Lakini point yangu nitaielekeza haswa kwa mafahali wawili, yaani Diamond na Slikiba.
na nitachukua reference ya show ya Kiboko Yao iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo, iliyofanyika jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya leaders.

Ni ukweli usiofichika kwamba wasanii wote waliotumbuiza walijitaidi kwa kiwango kikubwa sana, hongera sana kwani kuna changes kubwa sana. Lakini kuna jambo halikuwa sawa katika show ile, alo ni kurushwa makopo stejini wakati Diamond akitumbuiza na hapo ndio hoja yangu inapojengeka.

Bila kuwachosha sana, Diamond ametuwakilisha Watanzania kwenye shoo nyingi za kimataifa, ni nyingi siwezi kuzitaja zote, mbona Wanigeria, Marekani, Canada, Germany, Rwanda, Burundi etc hawakumrushia makopo? Kwanini itokee nyumbani Tanzania? Ni wivu au chuki kiasi gani juu ya msanii huyu mwenye kuheshimika Afrika kwa sasa? Amewakosea Watanzania?

Natambua Watanzania wengi hatupendi kuona mtu anaendelea, tumezoea majungu, fitina, chuki, umbea, na wivu. Jamani tubadilikeni. Maskini ya mungu Diamond huna ugomvi nae unamchukia kwanini? Au alikikiba hata hujawai kumuona unamchukia kakukosea nini?

Nimetafakari nikagundua ndio mana tuko nyuma in everything. Nenda Kenya and see how Jaguar anathaminiwa nchini mwao, Go Uganda and see how Jose Chamilione is respected. Hivi vitu vya team ujinga in negative way ni ushamba uliopita kiwango, inatakiwa team in constructive way.

Tunaomba Alikiba na Daimond washirikiane kuendeleza muziki wetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Samahanini kwa kuwachosha. Asanteni kwa kunisoma.

By Fukara

Walisema Bangi zinanipoteza Hadi Mama Mzazi Alinifukuza Nyumbani Nikiwa Darasa la Saba:Ney wa Mitego

0
0
Mwanamuziki anaetamba na hits single ya Akadumba Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya utafutaji na kuhangaika na sanaa kuna watu wengi waliamini kuwa anapoteza muda.

Nay amesema watu hao pia wanadai kuwa bangi ndizo zinampotezana kufanya muziki ambao waliamini kuwa unaleta chuki au usingeweza kumtoa na kumtabulisha kama wasanii wengine ambao walitamba kipindi hicho yeye akitafuta kutoka.
Nay wa Mitego alisema kuwa katika kuhangaika na muziki ilifika mahali hata mzazi wake ambaye ni mama yake mzazi alimfukuza nyumbani kwake akiwa darasa la saba sababu ya muziki ambao leo umeweza kumfungulia njia na kumpa mafanikio ambayo hata mzazi huenda anayafurahia.
"Wakati Naanza kila mtu aliniona kama napoteza muda hivi, wengine walisema bangi ndo zinanipoteza. Ata mama mzazi alinifukuza nyumbani nikiwa darasa la Saba sababu ya huu Muziki ninao ufanya sasa."

Mbali na kukatishwa tamaa Ney anadai kuwa hakuweza kukata tamaa sababu alikuwa anatambua nini anakifanya hivyo alizidi kukomaa na kuona kuwa anafikia malengo yake ya kufanikiwa kupitia muziki wa Bongo Fleva na kupata heshima hata kwa watu ambao walikuwa wanaona anapoteza muda.

"Sijawahi kukata tamaa nikiamini siku moja nitakuja kufanikiwa na wataniheshimu wote wanaonidharau..Thnx God kwa kunipa moyo wa ujasiri mpaka nilipo Leo..!! Angalau naheshimika, nackilizwa..Wengi wao leo wanajivunia Ney-Wamitego"
Mkali huyo kupitia ukurasa wake wa Instragram amewataka vijana kutokata tamaa na wazidi kutafuta pesa kwani hata yeye moja ya ndoto yake ni kuona anaishi maisha ya kitajiri na anaamini yatatimia hivi karibuni.

"Washkaji zangu eeh!?? Tutafuteni #Hela tuacheni masihara kabisaa.Kiukweli mimi napenda kuishi maisha mazuri yakitajiri (like a boss) na nina imani nitaishi ivyo soon, coz nikikumbuka nilikotoka daah..!!! Huwa sometimes siamini kama ni Mimi (Ahsante Muziki_Media_Mashabiki).

Iyobo: Mimba ya Mpenzi Wangu Aunty ni Faraja Kwangu na Tulizo la Roho Yangu

0
0
Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul  ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa filamu, Aunty  Ezekiel.

Akizungumzia ujauzito wa mpenzi wake,  Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.

Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

GPL

Mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ashinda milioni 100 za promosheni ya Jaymillions ya Vodacom

0
0
Mkazi wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22), leo ameibuka mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 katika droo ya kumi na nne ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544

Magedenge binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Katika maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala wageni na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha,” alisema.

“Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu.”

Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.
~Bongo5
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images