Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104780 articles
Browse latest View live

Rose Ndauka Ajuta Kuzaa Nje ya Ndoa, Asema Sasa Atakuwa Makini Kutumia Mipira

$
0
0

Udaku Special Blog: DIVA wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa alikosea kuzaa nje ya ndoa, na sasa hana mpango huo tena....
Rose alisema suala la ujauzito wakati mwingine linaweza kumjia mtu bila kupenda lakini kwa sasa atajitahidi kuona anazaa akiwa ndani ya ndoa.

“Lolote linaweza kutokea lakini kiukweli kwa sasa nitakuwa makini kidogo na ninamuomba Mungu anisaidie mtoto wa pili nimzalie ndani ya ndoa,” alisema Rose ambaye alizaa na Mbongo Fleva, Malick Bandawe kisha kumwagana.

Mwigizaji huyo kwa sasa ameandaa jarida lake ambalo litakuwa linatoka mtaani kila Jumatatu.

Aunty Lulu Awaendea Kwa Mganga wa Kienyeji Wabaya Wake Wanaomfanyia Mambo Mabwana zake Wayeyuke

$
0
0

MWIGIZAJI asiyekaukiwa matukio Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa amekwenda kwa mganga (babu) Mtwara kwa ajili ya kuweka zindiko wabaya wake wasimsumbue.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Aunty Lulu alisema kuna wabaya wake wamekuwa..
wakimfanyia ‘mambo’ mabwana zake wayeyuke hivyo hayupo tayari kuona nyota yake inafifia.
“Nimeona bora nikarekebishe kidogo maana mjini kila kukicha watu wanakutafuta na kukuharibia mambo yako, niko fiti sasa,” alisema Aunty Lulu.

Kama Ulikuwa Huamini Ushahidi Mwingine wa Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Kitandani Huu Hapa

$
0
0
Udaku Special Blog: Wenzangu na mie ambao mlikuwa hamuamini kuna ka Project kanaendelea kati ya Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Basi Hii ni picha nyingine wakiwa Kitandani huku Ommy Dimpoz akiwa kwenye usingizi na Wema Akaibia Selfie huku akitabasamu.......
Je Bado Hujaamini?

Lulu Atoboa Siri ya Kufanya Vizuri Chuoni na Kuwazidi Wanafunzi Wengine Kwenye Matokeo

$
0
0
Udaku Special Blog
Mwigizaji Lulu Michael Ambae sasa Ameamua kwa moyo mmoja kurudi Shule pale chuo cha Serekali cha Magogoni Amehabarisha na Kutuambia ni kweli Darasani anafanya vizuri na kuwapita wenzake kwenye mitihani kama tulivyosikia na Siri yake moja kubwa ni
kujisomea hasa usiku wakati wengine wamelala , lulu Michael amesema kwa sasa starehe ameweka pembeni kabisa na kawaida analala saa saba usiku ....

Hongera lulu Kazi Buti

Picha za Ngono za Nay wa Mitego zilizosambaa Mitandaoni Zamtoa Machozi Mchumba Wake

$
0
0
Udaku Special Blog
Siku tatu zilizopita picha ambazo anaonekana mwimbaji Nay wa Mitego akiwa na msichana kitandani huku wakiwa nusu utupa wakifanya yao zilisambaa mitandaoni na kuzua sintofahamu kwa mashabiki wake ..
Habari zilizotufikia zinasema mchumba wa Nay anayejulikana kama Siwema nae aliziona picha hizo na kuzua timbwili kubwa mpaka akaondoka nyumbani kwa Nay Usiku wa manane huku akimwachia Nay Mtoto Mchanga...Nay kesho yake ilibidi atumie juhudi kubwa kumweleza mchumba wake mpaka akaelewa kuhusu hizo picha, inasemekana kwa sasa wako vizuri na wanaendelea na maisha baada ya Siwema kuingizwa KING...

Wema Sepetu Khaaa! Aenda South Africa kula Bata na Aliyekuwa Mume wa Zari ‘What Goes Around Comes Around'

$
0
0
Kuanzia Kulia: King Lawrence, Ivan Ssemwinga na Wema Sepetu
Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zari The Bosslady na aliyezaa naye watoto watatu ameanza kurusha mashambulizi kwa adui yake namba moja, Diamond Platnumz....



Mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini huenda akalipiza kisasi kwa Diamond anayetarajia kupata mtoto wake wa kwanza kutoka kwa Zari kwa mbinu ya ‘jino kwa jino’ ama zile za ‘kama noma basi iwe noma’.

Picha liko hivi, Wema Sepetu kumbe yupo nchini Afrika Kusini ambako hata hivyo hatufahamu ameenda kufanya nini. Mshkaji wa karibu wa Ivan, King Lawrence (Yule mchizi aliyempa ofa Diamond ya $40,000 ili aachane na Zari), ameshare picha kwenye mtandao wa Instagram akila bata na Wema huku Ivan akiwpo pia.
Wema, Ivan na Lawrence akiwa na demu wake

Kwenye picha hizo, Lawrence anaonekana akiwa amekaa juu ya mapaja ya msichana asiyejulikana na pembeni yake yupo Ivan huku Wema aliyevaa kigauni kifupi cheusi akiwa kulia kwake.

Lawrence pia amepost video kadhaa akiwa kwenye club hiyo na kuziandika ujumbe wa mfumbo ambao unaeleweka wazi kuwa unawaendea Zari na Diamond. “Rich Gangstas – What goes around comes around,” ameandika. “Oh Z*** get out of the way,” ameandika kwenye video nyingine ambayo unasikika wimbo wa Ludacris, Move Bitc*.

Awali Lawrence alipost picha nyingine hiyo chini akiwa kwenye eneo lile lile ambalo Wema alipiga picha.

Ni mapema sana kuhitimisha kuwa Ivan anataka kulipiza kisasi kwa Diamond kwa kumchukua Wema, lakini ni wazi kuwa kambi yake inataka kupeleka ujumbe ulio wazi kwa Chibu kuwa ‘vita imeanza’.

Acha project iendelee…

Wema Sepetu Awapa Vidonge Vyao Wale Wanao Sema Hawampendi na Huku Wanaendelea Kufuatilia Mambo yake na Kila Anachopost Mtandaoni

$
0
0
Udaku Special Blog: Mrembo na mwigizaji wa filamu ambae kwasasa amekuja kivingine na mwingine, Wema Sepetu amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaosema hawa mpendi na kumchukia lakini bado wanapeleleza na kumfualitia kila anachokiweka mtandao, na kutumia akaunti feki kumchafua kwa maneno machafu....
amewaita jina baya na kuwambia wanatamani kuwa kwenye matawi yake....

“If u say u Hate me and still come spying on what i post plus create fake accounts to insult me, BI..CH you actually Envy me... Gnyt now....” Wema aliandika maneno haya mtandao jana usiku.

Nadhani ujumbe umefika!!!

Lady Jaydee ajibu Kwanini hafanyi collabo na wasanii wa kike, na kama ana mpango wa kupatana na Radio/wasanii aliogombana nao

$
0
0
Udaku Special Blog: Lady Jaydee ametoa nafasi kwa mashabiki na followers wake wa Instagram kumuuliza maswali na kuahidi kuyajibu. Miongoni mwa maswali mengi aliyoulizwa ni pamaoja na kwanini hafanyi collabo na wasanii wa kike, na kuhusu Ugomvi / Tofauti na watu (wasanii) /Radio na mpango wa kupatana nao.


“Duuuh maswali yako mengi sana karibia 300 Ila ki ukweli yote yanafanana So, what i will do I will pick top 10 ya maswali yaliojirudia, halafu nitalijibu moja baada ya jingine. Watu wooote nikiwakusanya, maswali yenu hayazidi 10, Leo mtaelewa kwanini sijibu comments. Sababu nikifanya hivyo itabidi niache kazi zote, Kaeni tayari kwa majibu, moja baada ya jingine” aliandika Jaydee kabla hajaanza kuyajibu.

Haya ni baadhi ya maswali na majibu.
Swali: Kwanini sifanyi collabo na wasanii wa kike?
Jibu :
“Nimewahi kufanya na wasanii mbali mbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1.Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Kaysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba nae Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu.

Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio.
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo”

Swali: Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio Na mpango wa kupatana nao
JIBU :
“Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha,Otherwise hakuna miujiza.Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .

Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asie kosea Ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.

Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua. Je! Hili jibu limejitosheleza?.Naamini hata nyinyi mmewahi kutofautiana na watu wenu wa karibu.
Kukubali kosa ndio mpango”

Swali: Siasa
Mchango katika jamii
JIBU:
“Sio mpenzi na sitegemei kujihusisha na siasa, wala chama chochote. Kila binadamu ana mchango katika jamii kwa njia moja au nyingine, Direct au indirect.

Ukitambua moja lolote nililowahi kulifanya likakupa furaha ndio mchango wangu, samahani kwa yaliokuudhi.

Swali la 4 mpk la 10 ntamalizia kesho, yasipoisha hata kesho kutwa.Najua kuna maswali mazito mnayosubiria majibu, yale ya kidaku zaidi. …Na mimi kwa kuwarusha roho nayaweka mwiiiishooo.Yatajibiwa tu, msitie shaka. …”

Wastara Awacharukia Wanao Mtukana Mumewe Mitandaoni...

$
0
0
Udaku Special Blog: Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayemkamata kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.



Akizungumza na gazeti  la  Ijumaa, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha Sajuki.

“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
GPL

Zitto Kabwe Aongoza Kwa Wafuasi Wengi Mtandaoni Awazidi Wasanii

$
0
0
Utafiti huo uliotolewa hivi karibuni, unaonyeshsa kuwa mwanasiasa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anaongoza miongoni mwa Watanzania wanaotumia mitandao hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambayo mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii.

Inaelezwa kuwa hiyo imetokana na ujasiri wake wa kutoa hoja za kashfa za ufisadi pamoja na ubadhirifu katika vikao mbalimbali vya Bunge katika Serikali ya Awamu ya Nne jambo linalomfanya awe mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa zaidi.

Mpaka wakati ripoti hiyo inatolewa, Zitto(38), alikuwa na wafuasi 219,000. Idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi baada ya habari hizo kuandikwa na kusambazwa mtandaoni pia.

Kwa rekodi hiyo, Zitto anakuwa ndiye Mtanzania mwenye wafuasi wengi akiwazidi wasanii, wanamichezo na viongozi na wanasiasa wenzake akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye akaunti yake imefungwa.

Mbunge huyo, mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kwa wananchi na wafuasi wake popote nchini na duniani kwa ujumla.

"Mimba My Foot"... Mashabiki wa Zari (Mpenzi wa Diamond ) Wamvaa Wema Sepetu baada ya kukejeli Mimba Yake

$
0
0
Wema Sepetu anahisi ujauzito wa Zari The Boss Lady ni geresha tu, hakuna lolote!

Hii ni kwa mujibu wa picha inayoonekana kuwa iliwekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 na ex wa Diamond Platnumz.


Picha hiyo haipo tena lakini Zari alifanikiwa kuipata na kuiweka kwenye ukurasa wake  wa  pili (zarithebosslady_) kuelezea alivyosikitishwa na kauli ya Wema kwenye picha yake (Zari) isemayo ‘mimba my foot’.

Kwa mujibu wa urbandictionary.com msemo ‘my foot’ humaanisha: An exclamation that means that one believes the previous speaker’s statement to be untrue

Mrembo huyo wa Uganda anayetarajia kumzalia Diamond mtoto wake wa kwanza, aliipost picha hiyo na kuifuta tena baadaye na kuandika:

"Astagafululah! May God Protect Zarimond and chibu junior #zaritlale #chibujunior #zarihassan #chibudangote"

Wasaka Urais Vijana: Utafiti Wamng'arisha Mwigulu Nchemba akifuatiwa na Zitto Kabwe

$
0
0
Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Elimu (TEDRO), limesema katika utafiti walioufanya kuhusu ushiriki wa vijana katika siasa na matarajio kuelekea uchaguzi mkuu 2015, umeonesha kwamba endapo mgombea urais kijana atapendekezwa atakubalika kwa asilimia 82.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jacob Kateri alisema katika wananchi hao waliohojiwa pia asilimia 11 walisema vijana hawatakubalika na asilimia saba walisema hawajui.

Alisema utafiti huo umeandaliwa na kufanyika Tanzania Bara na maeneo yaliyohusishwa ni kanda za kijiografia ili kuwezesha uhusishwaji mpana wa Watanzania na katika kila wilaya wamehojiwa wananchi wa vijiji vitatu kwa kuzingatia siasa za eneo husika.

Aidha alisema utafiti huo umeonesha sababu mbalimbali zinazoweza kuwa kichocheo cha vijana kuingia katika siasa ambapo zilizochukua uzito ni uzalendo kwa asilimia 67 ambapo wananchi walisema vijana wengi wameingia katika siasa kwa sababu ya uzalendo.

“Sababu nyingine ni kimbilio baada ya kukosa ajira kwa asilimia 57, uwezo mdogo wa watangulizi wao katika nafasi husika kwa asilimia 60, mafanikio ya wanasiasa vijana walio mahiri asilimia 72, vyama vya siasa kuwapa nafasi vijana katika vyama vyao kwa asilimia 59 na kukubalika kwa vijana kwa asilimia 63,” alisema.

Aidha alisema wanasiasa vijana waliopendekezwa kupitia chama tawala aliyeoonekana kuongoza kwa kukubalika ni Mwigulu Nchemba kwa asilimia 38, Dk Emmanuel Nchimbi kwa asilimia 26, January Makamba kwa asilimia 24, William Ngeleja kwa asilimia 11 na Lazaro Nyalandu kwa asilimia 10

Wengine ni Hamisi Kigwangala kwa asilimia saba, Deo Filikunjombe kwa asilimia tano, Esther Bulaya kwa asilimia 2 na waliosema hakuna anayefaa walikuwa asilimia 9 na asilimia 13 walipendekeza wengine wasio vijana.

Utafiti huo pia unaonesha kwamba kijana anayepewa nafasi kubwa endapo atasimamishwa kupitia upinzani anayeongoza  ni Zitto Kabwe kwa asilimia 18, James Mbatia kwa asilimia 16, Tundu Lissu kwa asilimia 14, Halima Mdee kwa asilimia nne na David Kafulila kwa asilimia sita.

Wengine ni Julius Mtatiro kwa asilimia nne, John Mnyika kwa asilimia saba, Joshua Nassari kwa asilimia mbili, Moses Machali kwa asilimia nne na asilimia 11 ya wananchi walisema hawajui na asilimia 16 walisema hawaoni anayefaa.

Hata hivyo, utafiti huo ulionesha kwamba endapo wakishindanishwa vijana wote bila kujali itikadi zao anayeongoza  kwa kukubalika ni Mwigulu Nchemba kwa asilimia 27, Zitto Kabwe kwa asilimia 19, January Makamba kwa asilimia 14, James Mbatia kwa asilimia 11 na Emmanuel Nchimbi kwa asilimia nane.

Wengine ni Lazaro Nyalandu kwa asilimia saba, Tundu Lissu kwa asilimia tano, Hamis Kigwangala kwa asilimia nne, wengine waliotajwa wasio vijana ni asilimia nne na wasiofaa walikuwa ni asilimia mbili.

Mapema Mkurugenzi wa Mafunzo wa Utafiti wa TEDRO, Jackson Coy alisema utafiti huo wameufanya bila shinikizo kutoka kwa mtu yeyote na waliufanya kuhusu siasa kutokana na kwamba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.

Alisema lengo la utafiti huo limechambua ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea, mchango wa wanasiasa vijana katika kufuatia misingi ya utawala bora na uwajibikaji, utekelezaji wa ahadi za wagombea kwa wapiga kura na matarajio ya wananchi kwa vijana katika kuelekea uchaguzi mkuu.

“Utafiti tunaoendesha ni mwendelezo wa uchambuzi wa changamoto za elimu, ndani ya dira ya TEDRO na programu ya mchango wa elimu katika kufungua fursa za ajira, siasa ikiwa ni mojawapo ya fursa zenye kimbilio la vijana,” alisema.

Hadi sasa TEDRO inaendesha utafiti wa Mitandao ya Kijamii inavyoathiri wanafunzi wa sekondari na kutazama njia rafiki katika kutumia mitandao hiyo kama njia ya kujifunzia na kuendeleza sekta nzima ya elimu.

Utafiti huu uliotarajiwa kuhusisha wilaya 24 Tanzania Bara, umeendeshwa katika wilaya 18, kila wilaya ikiwa imewakilishwa na wahojiwa 45 waliochaguliwa 15 kutoka kila kijiji; hivyo utafiti huu kuhusisha vijiji 54 kwa ujumla.

Wilaya ambapo utafiti umefanyika ni Njombe Mjini, Ludewa, Mbeya Mjini, Kilwa, Lindi Mjini, Mtwara Mjini, Morogoro Mjini, Kisarawe, Kinondoni, Tanga Mjini, Vunjo, Arumeru, Singida, Kasulu, Kigoma Mjini, Bukoba Vijijini, Biharamulo na Mwanza Mjini (Nyamagana).

Katika utafiti huu uliohusisha watu 910, taarifa binafsi za wahojiwa zilizokusanywa ni pamoja na zile zinazohusu umri wa wahojiwa, jinsia, hali ya ndoa, kazi, kiwango cha elimu na vyama vya siasa vinavyoongoza majimbo sehemu uchaguzi ulipofanyika.

Lakini wakati matokeo hayo ya utafiti yakianikwa, kwa upande wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akiwa mjini Songea, Ruvuma alikokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho, alisema chama chake bado hakina mgombea mpaka sasa.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kuwashawishi wanaoonekana kuwa na uwezo wa kuongoza huku wakiwa hawana 'madoa’ waweze kujitosa katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.

Mike Mushi wa Mmoja wa Waasisi wa JamiiForums kwenye kipindi cha MKASI

$
0
0
Katika ulimwengu huu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, fursa nyingi zimejitokeza katika jamii yetu! Moja ni uharaka wa kusambaa kwa habari, njema au mbaya; upatikanaji wa jukwaa la watu kutoa maoni yao....lakini la zaidi....imefungua nafasi lukuki za vijana kujiajiri na kuajiri mamia kama sio maelfu ya wengine..

Mfano hai hapa Tanzania ni Jamii Forum! Wengi tunaufahamu kwa umahiri wake wa mijadala mbali mbali na zaidi ya kisiasa, ukiwa kama mtandao wa kwanza wa jamii wenye mizizi yake Tanzania kupata kukubalika na watu wenye hulka tofauti. Kitu ambacho wengi wetu hatujui ni.....Ni Nani Alie Nyuma ya Injini za JamiiForums?

Leo tunawaletea mmoja wa vinara wanaoiweka JF hewani na kutupa sisi uwezo kujinafasi, Mjasiriamali Kijana, Mtanashati na Mwenye akili za Kipekee.....Bw. Mike Mushi!

‪#‎MikeMushi‬ ni nani? Katokes wapi? Nini ndoto zake? Tutegemee nini kutoka kwake na timu yake siku za karibuni? Na nini nafasi ya JF katika harakati za uchaguzi na maamuzi ya katiba mwaka 2015?

Jiunge nasi saa 3:30 usiku, EATV, kwani Salama, Mubah na John....hawataacha kigae bila kukipindua!

Source: MkasiTV

Uongozi wa Msanii Chris Brown Upo Tayari Kufanya Kazi na Ally Kiba

$
0
0
Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni za SAMSUNG....


Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY,

MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya ONE 8. Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa.

Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha

Japokua anahitaji marekebisho madogo sana. BBC SWAHILI Tunampongeza msanii Ali kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii, kuipata habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au unaweza kuipata katika American Spring news.

Aunty Ezekiel:Naamini Kabisa Huyu Mwanangu Atakuja Kunifuta Machozi na Kunifariji Kwa Kuondokewa na Wazazi Wangu Wote

$
0
0
MKALI wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amefunguka kuwa pamoja na kupoteza wazazi wake miaka kadhaa nyuma pindi akiwa mdogo, anaamini mtoto atakayejifungua atamfuta machozi ya muda mrefu ya kuwapoteza wazazi wake..
Aunty alifunguka ishu hiyo kwa upole, ambapo alisema kifo cha wazazi wake kilimfanya kulelewa na bibi yake pamoja na shangazi.

“Kutokuwa na wazazi ni pigo kubwa kwangu, lakini hata hivyo naamini kwamba mwanangu atakuwa na furaha ambayo nilikuwa naipata kutoka kwa wazazi wangu, atakuwa ni zaidi ya rafiki au ndugu, ndiye atakayenifuta machozi ya kufiwa,” alisema Aunty.

Utata Mtoto wa Flora, Mbasha Amtaka Flora Amuogope Mungu na Kueleza Watu Ukweli Ulio Moyoni Mwake

$
0
0
SIKU chache baada ya kuibuka utata mkubwa juu ya kichanga cha kike cha mwimba Injili maarufu Bongo, Flora Mbasha huku mitandao ya kijamii ikieleza kwamba baba wa mtoto huyo si aliyekuwa mume wa mwanamuziki huyo, Emmanuel Mbasha ‘Ima’, familia ya mwanaume huyo inadaiwa kufanya kikao kizito jijini Dar ili kupata ufumbuzi, Ijumaa Wikienda linakujuza.


Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Mbasha, familia hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita nyumbani kwa Ima, Tabata-Kimanga, Dar ili kulizungumza suala hilo na kuona kama wanaweza kukubaliana kukilea kichanga hicho endapo ni damu yao.
“Ndugu walitofautiana, kila mtu alikuwa na mtazamo wake hivyo wakaona bora wakutane na kutafuta jibu la pamoja kama wanalea au hawalei,” kilisema chanzo hicho.

KIKAO CHAVUNJIKA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana ndugu hao kutofautiana kimisimamo kwani kila mmoja alitoa mawazo yake.

MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha ambaye sasa anatamba na Wimbo wa Haribu Mipango ya Shetani ambao inadaiwa amekuwa akiutumia kama kijembe kwa Flora, alisema aachwe kwanza kwani suala hilo linamuumiza kichwa na ni la  kifamilia zaidi.
“Naomba mniache kwanza, sipo vizuri kwa sasa,” alisema

CLIP YAONESHA MSIMAMO
Kwa mujibu wa ‘clip’ ya sauti yake (Mbasha) aliyoituma kwa Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye ana mtoto mmoja tu, Elizabeth Emanuel Mbasha ’Liz’ ambaye ana miaka kama kumi na moja.
Mbasha alisema hajui nini kinaendelea na kwamba ameambiwa habari za Flora kujifungua mtoto wa kike lakini yeye haoni kama habari hizo zinamhusu sana!

MSIKIE
“Mimi sijui niseme nini? Nimeambiwa kwamba Flora amejifungua. Kwa hiyo? Mbona yeye Flora hajaniambia, si anajua taarifa hizo hazinihusu? Amuogope Mungu, yeye angewaambia watu ukweli.”
Ijumaa Wikienda: “Kwa hiyo unataka kusema mtoto si wako?”
Mbasha: “Yeye anajua.”

NDUGU WA MBASHA
Ijumaa Wikienda lilizungumza na ndugu mmoja wa Mbasha (jina lipo) ambaye alizungumzia sakata la shemejiye kujifungua mtoto akiwa mbali na nyumbani:
“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.

KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mara baada ya ugomvi wao na kuondoka nyumbani miezi saba iliyopita, Flora aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akikiri kuwa na ujauzito na kusema: “Ndiyo nina mimba lakini siyo ya Gwajima.”

AZUNGUMZIA UNDUGU WAKE NA GWAJIMA
Hata hivyo, hivi karibuni, Flora alikazia tena maneno yake kwa kusema kuwa Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ni anko (mjomba) wake kwa hiyo watu wajaribu kuliangalia hilo, hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi  na mjomba‘ake.

KUHUSU MADAI KUWA MTOTO NI WA GWAJIMA
Mwanasheria: “Kwanza nataka kusema kwamba, chombo chochote cha habari ambacho kiliandika habari ya kumchafua Flora tutakishitaki. Iwe ni magazeti iwe ni mitandao ya kijamii. Wanaosema ni mtoto wa Gwajima ndiyo wanaomchafua Flora kwa sababu si kweli.”
GPL

Mwigizaji JB Akubali Kushindwa , Asema Umri Wake Umeenda Kupenya Kimataifa katika Filamu

$
0
0
Udaku Special Blog
Mwigizaji Nguli wa Bongo Movies Amejibu Swali Aliloulizwa Kuhusu Kufanya Movies na Waigizaji wa Nje ili apenye Kimataifa...Jibu lake hili Hapa:
“Jana nilikuwa najibu maswali ya wadau wa jerusalem.wengi wanapenda kuniona kimataifa.niliahidi kulijibu leo...ndugu zangu kwanza nashukuru kwa kuniona nafaa kuwawakilisha kimataifa.lakini mwenzenu umri umekwenda.kitaalamu umri mzuri wa kuanza utafutaji ni20-35.nina zaidi ya 40.nguvu zimepungua.ndio maana akili yangu naiweka zaidi kuwa producer kupitia Jerusalem zaidi kuliko kuigiza.ndoto zangu ni kuifanya kampuni hii iwe kubwa africa.na hao waigizaji wa nje watamani kufanya kazi nasi.lengo ni filam yetu moja kuuzwa zaidi ya bilion1.inawezekana kwa sababu soko lipo.mchakato umeshaanza subirini.soko halitafutwi linajengwa.tuamke,tusifikiri kikawaida tufikiri tofauti.In Jesus Name. ..” JB alimaliza.

Picha: Batuli na Joel wa Fresh120media Katika Mapozi Tata!!

$
0
0
Kila mtu anajua uzuri na raha ya picha, hizi ni za mwigizaji Batuli akiwa na Joel Joseph wa fresh120media  siku ya sherehe yake  ya kuzaliwa.


Watu wanasema picha huzungumza, lakini Batuli mwenyewe asema wao ni marifiki tuu, na sisi tunakubali, lakini wapo ambao wanaona kunachazaidi hapa....

Katika kuona picha hizi zina utataaa, kwenye moja ya picha hizi Batuli aliandika kwa kumuliza joel kiutani.

Can I ask u something!? Joel do u have a girlfriend!? Maana nahisi kama utapigwa hivi...... Halafu unajua nina bae au hujui!? Unajua kazi ya silaha hizi!? (akaweka picha yavisu na bastola)

Wewe je utakubali wako atokelezee namna hii na Me/Ke wako?

Mrembo Zari wa Diamond Aonyesha Mwili Wake Akiwa Ndani ya Bikini Wakati huu wa Ujauzito

$
0
0
Udaku Special Blog
Mrembo Zari wa Uganda Ambae sasa ni le Mbebiz wa Mwanamuziki Diamond Ameweka Picha Akiwa ndani ya Bikini na kuonyesha mwili wake wakati huu akiwa mjamzito wa Miezi Kadhaa..

Hit or Miss?

Mtoto Afungwa kwa Kutumia Mnyororo Kwenye Kitanda cha Chuma kwa Muda wa Miaka Miwili

$
0
0

Tukio hilo limetokea jana Iringa Mjini maeneo ya Kihesa,baada ya majirani kutoa taarifa kwenye serikali ya mtaa kuwa kuna babu anamfungia ndani na kumnyima chakula mtoto wake mwenye miaka kumi ambaye ni mlemavu wa akili.

Picha kama mnavyoiona hapo, dada wa kazi wa binti babu huyo sasa bado yupo kituo cha polisi hapa mjini kwa mahijiano zaidi.
Viewing all 104780 articles
Browse latest View live




Latest Images