Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete Afuta ADA ya shule za Sekondari Nchi Nzima

$
0
0
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ametimiza ahadi yake aliyoitoa Agosti mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, kwamba amekusudia kufuta ada ya shule za sekondari nchi nzima.


Akizindua Sera mpya ya Elimu na Mafunzo 2014 katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitangaza kufutwa kwa ada ya sekondari, kuanzia mwakani.

Kwa tangazo hilo, Bajeti ya mwisho ya uongozi wa Rais Kikwete itakayoanza kujadiliwa Mei mwaka huu, itatakiwa kuwa na fungu la kulipa gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitoa kwa watoto wao wanaosoma elimu ya sekondari katika shule za Serikali nchi nzima.

Kwa sasa wazazi wamekuwa wakilipa Sh 20,000 kwa shule za kutwa na Sh 70,000 kwa shule za bweni, ili watoto wao wapate elimu ya sekondari.

Ubora
Alisema sera hiyo imezingatia stadi za msingi ambazo ni kuandika, kusoma na kuhesabu, ili kuwezesha watoto kujengwa kwenye msingi mzuri na hata kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hilo limezingatiwa.

“Hata kwenye mpango wa BRN tumelizungumza ili kuhakikisha inatolewa elimu bora. Tusifanye mambo ya kuchekesha mtoto anafika madarasa ya juu hajui kuandika, kusoma na kuhesabu.

 “Kuanzia sasa kama mtoto anafika darasa la pili, hajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), ni bora asiende darasa la tatu…naamini watoto wakiimarishwa katika stadi za KKK itaondoa matatizo haya,” alisema.

Tathimini ya Msingi ya Taifa kwa ajili ya uwezo wa wanafunzi katika KKK, kwa wanafunzi wa Darasa la Pili iliyofanyika mwaka jana, ilibaini kuwa asilimia 98 ya wanafunzi wa Darasa la Pili nchini, walikuwa hawaelewi wanachokisoma.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema, tathimini hiyo imefanywa kwa baraka za Wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), ili kupata taarifa kuhusu hali halisi ilivyo ya wanafunzi wa Tanzania kumudu stadi za KKK wanapofika Darasa la Pili.

Mafanikio
Mbali na mafanikio ya kufikia uwezo wa kuanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bure, huku msisitizo ukiwekwa katika utoaji wa elimu bora, Rais Kikwete pia ilitangaza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambayo yamefikiwa katika uongozi wake wa miaka kumi.

Rais Kikwete alisema sasa elimu imepewa kipaumbele katika sera na shughuli za serikali, ndio maana Bajeti ya Elimu, ndio kubwa kuliko bajeti zote.

Alifafanua kuwa mwaka 2005/06 bajeti hiyo ilikuwa Sh bilioni 6.7, wakati mwaka huu wa fedha imepanda na kufikia Sh trilioni 3.1.

Hatua hiyo ya kibajeti kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni ongezeko la mara tano ya Bajeti ya mwaka 2005 sawa na asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ambayo inatengwa kwa ajili ya elimu.

Katika suala la mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema imetoka Sh bilioni 56 kwa mwaka wa fedha 2005/06, hadi kufikia Sh bilioni 345 kwa mwaka huu wa fedha.

Aidha, kwa mwaka jana, wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliongezeka kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000.

Kwa upande wa shule za msingi, alisema zimeongezeka kutoka 14,000 kwa mwaka 2005 hadi kufikia shule 16,343 kwa mwaka 2014, huku shule za sekondari zikiongezeka kutoka 531 kwa mwaka 2005, hadi kufikia 4,576, mwaka 2014.

Idadi wanafunzi wanaojiunga na sekondari, Rais Kikwete alisema imeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi milioni 1.8.

Rais Kikwete alisema pia vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka vyuo 184 mwaka 2005 na kufikia vyuo 744 kwa mwaka 2014, huku vyuo vikuu vikiongezeka kutoka vyuo vikuu 26 mwaka 2005 na kufikia vyuo vikuu 50 kwa mwaka 2014.

Alikumbusha kuwa kama sio kuanzishwa kwa shule za kata, idadi ya wanafunzi pia isingeongezeka.

“Hali imebadilika, sasa wanafunzi wengi wanakwenda shule na vyuoni na suala la watoto na vijana kupata fursa ya kusoma, sio tatizo katika sekta ya elimu, sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha inapatikana elimu bora kwa kuboresha mazingira ya elimu,” alisema Rais Kikwete.

Mpekuzi Huru

Le Mutuz Anatafuta Mke 'Kwa Kweli Nahitaji WIFE Baby U Know Nahitaji Bonge la Mke, Niombeeni '

$
0
0
William Malecela Aka Lemutuz Ametangaza kuhitaji Mke katika Page yake ya Instagram huku akiomba watu wamuombee apate Bonge la Wife. lemutuz alipost picha akionyesha kitanda kikiwa hakija tandikwa na kuandika maneno haya hapa chini kama caption ya picha hiyo:

"kwa kweli nahitaji WIFE baby U know nahitaji bonge la mke hahahah people niombeeni basi nipate Le Wife U know this is not good yaani mpaka aje mfanyakazi je ukitokea moto hapa watu wakaingia wanakuta bed iko kwenye this mess U know jamani niombeeni nipate Le Wife hahahahahahah U know......Off to the Airport!, A-Town here I come leo DOWNTOWN KARATU LIVE! - le Mutuz

Ommy Dimpoz Anogewa na Penzi la Wema Sepetu, Soma Maneno yake Akikiri

$
0
0
Mahaba: Mwanamuziki  Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’  ameamua kukiri wazi kuwa ananogewa na penzi la Wema Sepetu ‘Madame’.

Akizungumza na wa GPL Februari 11, mwaka huu maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Dimpoz alisema anawashangaa sana watu kuendelea kumsakama juu ya uhusiano wake na Madame wakati yeye anafahamu shemeji yake kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni Zarina Hassan ‘Zari’ kwa sasa.



Nashindwa kuelewa kuna watu wamekuwa wakinitumia ujumbe eti Diamond atanimaindi kwa ukaribu wangu na Wema, Diamond atanichukia wakati ninavyojua demu wake kwa sasa ni Zari? Niwaambie tu ukaribu wa mimi na Wema ulianza tangu zamani alipokuwa na Diamond,” alisema Dimpoz.

Mahabati ya Dimpoz na Wema yalianza kuonekana laivu juzikati wakati wawili hao walipokuwa nchini Afrika Kusini wakidai kuna ‘project’ ya ngoma mpya ya mwanamuziki huyo waliyokuwa wakiifanya kisha picha zilizowaonesha wakiwa kimahaba zikavuja na kuzua gumzo mitandaoni.

Wakati Nyalandu Anakanusha Kuhusika na Mimba ya Aunty Ezekiel, Iyobo Nae Ana Haya..…

$
0
0
Baada ya hapo jana Waziri Lazaro Nyalandu kupitia Clouds FM kukanusha tuhuma  zilizokuwa zimezagaa kwenye magazeti  na mitandaoni za kuwa anachepuka na mwigizaji wa filamu hapa bongo, Aunty Ezekiel na kusisitiza kuwa yeye sio  muhusika wa ujauzito wa mwigizaji huyo, nikaamua kupitapita  kwenye kurasa za  mcheza shoo wa Diamond, Moses Iyobo ambae ndio
anasemekana kuwa  yeye ndio amempa ujauziko mwigizaji  huyo.

Kwanza nilikutana na andiko la malalamiko kutoka kwa Iyobo, ambae alikuwa ameweka picha ya Aunty na kuandika haya;

Kama kumpenda nampenda sana lakini kinacho nipasua kichwa mie kuni save dalali kwenye cm yake yani sielewi ata kidogo

Lakini kilichonipa faraja ni picha hiyo hapo juu akiwa na Aunty kitandani na kuandika ule msemo kutoka Yamoto Band ambao unamaanisha mtu akipenda amependaaa.

‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila..........’

Kwa picha na ujumbe huu ni wazi Iyobo ndio baba kijacho kutoka kwa Aunty Ezekiel.

Mzee wa Ubuyu/Bongo Movies

Matokea ya Kidato Cha Nne kwa Wanafunzi Waliomaliza Mwaka 2014 Haya Hapa

$
0
0
Matokea ya Kidato cha nne kwa wanafunzi waliomaliza mwaka 2014 sasa yametolewa rasmi na baraza la mitihani Tanzania. Bofya hapo chini kuyaangalia.
>>MATOKEO

Updates:Askari Polisi Wanne Wamejeruhiwa katika Mapambano na Magaidi Tanga.

$
0
0
Hadi sasa taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa askari wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania wamejeruhiwa katika mapambano dhidi ya vikundi vya kihalifu (kigaidi) katika eneo machimbo ya Amboni mkoani humo.
Taarifa zaidi zinasema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga kwa matibabu zaidi na kuna watu wawili ambao wamekamatwa kuanzia jana hadi sasa wakihusishwa na tukio hilo.

Aidha, mmoja wa Askari waliopo katika eneo la tukio amesema mapema leo asubuhi Helkopta ya Polisi ilinusurika kudunguliwa na vikundi hivyo vinavyosadikiwa kuwa viko zaidi ya vinne.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa kila kona ya eneo hilo imeelezwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani Tanga atatoa taarifa ya tukio hilo saa 15:00pm.

UPDATES II:
Pango walimojificha magaidi limevunjwa kwa kutumia mizinga, na hatimae jamaa wametoroka hakuna aliekamatwa, Sergeant Kajembe wa JWTZ aliepigwa risasi ya Tumbo ameshafariki Dunia, majeruhi waliopo hospital ni PC mmoja wa FFU, Sergeant wa JWTZ aliejeruhiwa sikio, Corporal alijeruhiwa mguu.

Askari wote wameshatawanyika eneo la Tukio na walichokuta ni Pikipiki, baiskeli, vyakula na nguo.

Tanzania ya Kipa Kingereza Kwaheri Shuleni na Mtihani wa Darasa la Saba Wafutwa

$
0
0
Jana mheshimiwa Rais wa Tanzania alizindua Sera mpya ya Elimu ambapo kati ya mengi yaliyomo ndani ya sera hiyo ni kufutwa kwa mtihani wa Darasa la Saba na Elimu ya Msingi kuongezwa hadi Kidato cha Nne..pia lugha ya kiswahili ndio itakuwa ikutumika katika masomo na kukitupilia mbali kingereza..
Soma zaidi hapa chini:
The newly-launched education system has abolished national examinations for primary school leavers and extended basic education to four years at secondary level—meaning students will sit their final examination after 11 years in primary and secondary school.

The policy makes Kiswahili the medium of instruction from primary school to university level, thereby ditching English —which has dominated Tanzania’s education system from secondary to tertiary level.

But it will take decades for the new system to take root because extensive preparations will have to be carried out before English is phased out. The policy, which President Jakaya Kikwete launched yesterday, also gets rid of school fees at both public primary and secondary levels and guarantees free education.

President Kikwete said the new policy was in line with Vision 2025 and takes into account global economic, social and technological changes. “In the next seven years, we will have built capacity whereby every child who starts Standard One will reach Form Four,” he said during the launch of the policy in Dar es Salaam.

But, given the timeframe, there are doubts that the new policy will yield significant results in the next decade. Critics say school fees in public schools are just a small portion of the cost of education, given that parents are required to make numerous contributions.

According to the Permanent Secretary in the Ministry of Education and Vocational Training, Prof Sifuni Mchome, the new education system will incorporate vocational education in the basic education syllabus so that students who do not make it to Form Five have skills to contribute to the development of the country.

“It’s our hope that when students complete this basic education, which is compulsory up to Form 4,” Prof Mchome said, “they will be at an age ready to contribute to the country’s development.”

Unlike the current policy, which focuses on filtering and rejecting students without skills through final exams, according to Prof Mchome, the new one raises the number of educated Tanzanians with skills.

“We need a critical mass of skilled labour for the country’s development,” he explained, “but you can’t get it through the current traditional system, which only filters and children go back home after failing Standard Seven final exams.”

Mr Kikwete declared it a significant day in the history of the education sector and said the new policy was a must so the country could proceed in line with global economic and technological changes.

The President assured the public that the new direction would take Tanzania to the next level, where the nation will have skilled people with both practical and theoretical knowledge.

Is Kiswahili a solution to education woes?

Speaking yesterday during the launch, the assistant director for policy at the ministry of education and vocational training, Mr Atetaulwa Ngatara, said it was proper that Kiswahili be the channel by which the skills are transferred to students. Language studies will then be available to enable students to communicate in English. “To think that learning in English will lead to students communicating in English is wrong,” he said. “Communicating in English is something else, which has to do with language studies.”

The document says the government will continue strengthening English in teaching along with Kiswahili during the transition period because using only Kiswahili will require a lot of resources.

Kiswahili is currently the language of instruction at primary level and English remains a subject. Thereafter, English becomes the language of instruction from secondary level to higher learning.

According to the policy, making Kiswahili the language of instruction at all levels of education is aimed at bringing sustainable efficiency in providing the skillful workforce that is needed for national development.

But in a globalised economy where English dominates almost everything—from trade to politics—it is not clear which way Tanzania wants to go in the next five decades.

After years of being driven by market forces, private schools in Tanzania will have a regulator to ensure that the cost of education is realistic and provides value for money. The idea is to make sure that school owners do not overcharge parents who shun public schools in search of quality education in the mushrooming private schools.

President Kikwete said the policy would set indicative fees for private schools and put an end to the exploitative fees some unscrupulous school owners charge. Consistency in text books

The policy also provides consistency in both text and reference books used to teach in both public and private schools, contrary to the current situation where every school chooses what it considers suitable. This will eliminate the trend where schools use different books for the same subjects, which has been blamed for the poor performance of students.

“It’s impossible that every school uses its own reference book when the final examinations are the same,” the President said. “How do we expect children to pass in these conditions?”

No national examination for Standard Seven

According to the assistant director for policy in the ministry of education and vocational training, Mr Atetaulwa Ngatara, students will be tested to check their level of understanding at each level before they get to Form 4. “Let’s say there will be a test at standard three,” he explained. “Teachers will arrange special programmes to help those who fail to get over their weaknesses and they can then proceed to another class.”

But judging by the fact that the reading culture has almost died off, dropping national examinations for primary school leavers will likely have negative consequences in terms of the quality of graduates.

The new policy further declares that the government will make nursery education compulsory for not less than a year for children aged between three and five.

Basic education—from Standard One to Form Four—will take 10 years. Standard One pupils should be aged four to six, depending on ability of the child, and the government will ensure that education at this level is free.

According to Mr Kalistus Chonya, an economist in the policy department of the ministry, implementing the new policy will not happen immediately as the policy must go through several more stages.

The document President Kikwete launched was a national policy that will produce an executive policy. It will then lead to a Bill that will be tabled in the National Assembly.

Mr Chonya, who was not in position to say when the new policy will take off, said there were still other stages to be worked on, including preparing strategies and an action plan.
Source: The Citizen

Miaka 9 Katika Ndoa - Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri

$
0
0
Udaku Special Blog
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33 mume wangu ana umri wa miaka 41. Sote ni wasomi na wafanyakazi. Tumefunga ndoa miaka tisa iliyopita tuna mtoto mmoja ana umri wa miaka 7.Wakati tunafunga ndoa wote tulikua mabikra. Mimi nilikua sijawahi kuwa na mpenzi na mume wangu akuwahi kua na mpenzi..

Tulianza kushiriki tendo la ndoa siku ile tulipofunga ndoa. Kwa kweli kwa ujumla maisha yetu ya ndoa ni ya furaha kwa mambo yote lakini sio ya kiunyumba.

Mimi na mume wangu atujawahi kuwa mbali kikazi. Maisha yote hadi leo tuko Dar es salaam pamoja. Tulipofunga ndoa miaka ya mwanzoni tulikua tunaweza kukutana kimwili hata mara tatu kwa mwezi, miaka ilivyokua inazidi kwenda ikawa kukutana kimwili inakua mara moja kila baada ya miezi miwili na tukikutana ni bao moja tu.

Sasa hali imezidi kua mbaya kwani sasa imepita miezi sita tunalala kitanda kimoja mume wangu ajanigusa, hali hii inanisononesha kwani natamani mtoto wa pili. Kwakweli atuna ugomvi wowote. Mimi na mume wangu wote ni wacha Mungu.

Mume wangu ni mchapakazi sana tukitoka kazini tuko wote na sio mtu anaependa kwenda kutembea bila familia. Jumamosi na Jumapili mara nyingi tunatoka out tukirudi home akuna kinachoendelea, anageuka ukutani analala kama mtoto hadi asubuhi, wala hata anigusi nikimsogelea hata ashtuki.

Na asubuhi tukiamka tunaenda ofisini na akifika ofisini lazima anitumie message, mke wangu nakupenda sana. Simuelewi na nashindwa kumuuliza maana mimi kama mwanamke naona aibu.

Kwakweli mawazo ya kutoka nje ayapo kabisa kichwani mwangu maana simjui mwanaume mwingine zaidi yake pia namuogopa Mungu siwezi kucheat.Ila kwa hali ilipofikia naona bora nitengane nae niishi maisha yangu maana bila unyumba amna maana ya ndoa na nataka sana mtoto.

Wadau naomba ushauri je hii ni kawaida, nifanyeje.

Wastara: Bond we ni Zaidi ya Maneger, My Director, My Friend, My Boy and My Lov....

$
0
0
Udaku Special Blog
Hatimaye Wastara Amwita Mr Bond Mpenzi wake hadharani , leo ni siku ya kuzaliwa kwa MR Bond na wastara ambae kwa muda mrefu amekuwa akihisiwa kuwa na mapenzi ya Siri na  Bond Ameandika maneno haya:

"Happy birthday Bond Bin Sinnan Mungu akupe umri mrefu, sina jipya la kukwambia maneno yoote umeshayasikia midomoni kwa watu ila touti ni vitendo tu ambavyo si vyote uliwahi kuviona na kufanyia hicho.ndicho minachokuahidi kitakuwa kipya katika maisha yako mapya unayoyaanza ya kutimiza miaka kadhaa leo hii mungu.ni mwema na mwingi wa huruma na kutoa pale anapoombwa tumwamini yeye anaweza kutuoa kilakitu mungu akutangulie katika siku yako hii ya kuzaliwa".

Muda kidogo akaibuka na huu mara baada ya kuweka picha hiyo juu;

We ni zaidi ya manager katika kazi, ni zaidi ya rafiki katika upendo kwa kweli mungu ni mwema kwa kukuleta duniani na ninaimani anakila sababu za kukufanya uishi miaka mingi ukiwa na afya njema, furaha na mafanikio zaidi
Nafurahia kuwa nawe karibu maishani mwangu. Happy birthday my Manager, my Director, my Friend, my boy and my Lov..Happy birthday".

Udaku Special Inamtakia Mr Bond Happy Birthday,  Mtunze Wastara Akutunze

VIDEO: Majigambo ya Vijana wa Tanga (Magaidi) Baada ya kuwapora Silaha Polisi

$
0
0
Nimeiona hii video, hivi Tanzania tumefikia huku? Tuna watu wanajitangaza waziwazi hivi na Serikali imenyamaza tu? Itazame video hii na utoe mtizamo wako:

Aunty Lulu Azua Tafrani Baada ya Kuzuka Bar Akiwa Nusu Utupu, Wengi Wachukizwa

$
0
0
MTANGAZAJI na muigizaji wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amezua tafrani la aina yake baada ya kutinga kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar akiwa nusu utupu.



Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo Lulu alipoingia alipita katikati na kwenda katika kaunta ya baa hiyo huku akijitingisha makusudi na kusababisha wanaume waliokuwa wamekaa kwenye baa hiyo wapige kelele wakimtaka aondoke.

Hii sasa ni sifa haiwezekani atuvalie kigauni kifupi namna hii, akibakwa atasemaje? Hatukubali, bora ingekuwa usiku, tumwambie mwenye baa kama anataka amtoe huyu au sisi tuondoke, hata kama tuko baa lakini tunajieheshimu,” alisikika mmoja wa wanaume hao.

Huu ujinga bwana sisi tunajiheshimu, hawezi kuvaa hivi tena inaonesha hana hata kufuri, bora niondoke eneo hili,” alisikika mwanaumwe mwingine na kuondoka zake.Hata hivyo, meneja wa baa hiyo aliwasihi watu kubaki na kumvumilia lakini wengi wao waliamua kuondoka kwa hasira.

Waandishi wetu walipomuuliza sababu ya kufika pale na kiguo hicho alisema kuwa alifika kwa mambo yake muhimu na kukutana na rafiki zake Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha hivyo kama wateja wengine wamemsusuia, watajijua.

Mwigizaji Amanda Mwenye Shape Matata Aanika siri Nzito ya Kutowapenda Wanaume

$
0
0
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi amefunguka na kueleza siri nzito kuwa hawapendi wanaume kutokana na kufiwa na
mchumba wake muda mfupi baada ya kuzungumza naye miaka…iliyopita.

Akipiga stori na gazeti hili, Amanda alisema stori ya mwanaume ambaye alikuwa ni mchanganyiko wa Mgiriki na Mbongo aliyejulikana kwa jina la Alan kila akiikumbuka huwa inamuumiza  moyoni kwani ni mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati.

“Huwa naumia sana nikimkumbuka Alan mchumba ambaye alikuwa ameshajitambulisha kwetu lakini akafariki kwa ajali nusu saa baada ya kuzungumza naye kwenye simu akiwa Ugiriki huku akiniachia ujauzito wa miezi mitano lakini ilipofika miezi saba mtoto alifia tumboni. “Tangu hapo sipendi wanaume na sijawahi kumpata mwanaume mwenye upendo wa dhati kama huyo,” alisema Amanda.
GPL

Japo Huwa Anamtandika Makofi Lakini Kifua cha Nuhu Mziwanda Ndio Mto wa Kupatia Usingizi Shilole..

$
0
0

Udaku wa Instagram
Siku ya Jana ilikuwa ni siku ya Wapendanao ambapo watu mbali mbali walishow love kwa Watu wanao wapenda , mwimbaji Shilole ambae hivi karibuni ameingia katika skendo ya kumchapa vibao mchumba wake Nuhu Mziwanda Jana alipost haya maneno kuhusu Nuhu:

'My lv wangu mm wa uban! Nikiwaga nimekwazika na ya walimwengu basi akilinilaza kwenye kifua chake mawazo yote yanaisha na ninaweza sinzia kabisa! Nakupenda sana jackson wangu! Mm huwa napenda kumuita hivyo japo nyinyi mnajua kwa jina la NUH happy valentine my hubby." Aliandika Shilole

Haya Muache Kupigana Vibao sasa!

Diamond: Ningekuwa na Sauti Kama ya Ally Kiba, Ningefanya Makubwa Zaidi

$
0
0
Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita baridi.


Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya habari.

Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti anaouona kati ya wasanii hao.

Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana hazina kubwa ya sauti na anakumbuka kuwa Diamond aliwahi kuisifia.

“Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi.” Amesema G-Lover.

Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho Diamond anakifanya sasa hivi.

Jerry Muro: Nipo Tayari kurudi ITV Hata Usiku wa Manane

$
0
0
Jamaa anasema alienda kusoma na alipirudi akakuta kibarua chake kimeota ngaro
Ila anakiri ITV ndio kituo bora cha TV Tanzania,Amesema wakimwita hata usiku wa manane yupo tayari kwenda kufanya kazi ni sehemu bora na kituo bora kabisa.
Majuto mjukuu!

Kikundi cha Magaidi kilichoko Tanga Chajeruhi Polisi Wanne na Kuua Mwanajeshi mmoja wa JWTZ wakati wa Mapigano yaliyoanza Juzi Usiku

$
0
0
Askari sita wakiwemo wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamejeruhiwa vibaya kwa risasi wakati wa mapigano baina yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati wa Msako Maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya
Amboni.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, amebainisha hayo alasiri ya  jana, wakati akitoa taarifa kwa wanahabari jijini Tanga kuhusu hali ya matukio ya uhalifu  yanayoendelea jijini humo.

Alisema mapambano hayo yalitokea muda mfupi tu wakati wa msako maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni, yaliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga.

“Baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wasiri wetu ndipo alfajiri ya leo (jana) askari wetu walienda eneo la tukio kwa lengo la kutafuta hizo silaha na ghafla wakavamiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa wamejificha”, alisema.

Alisema kujeruhiwa kwao kumetokana na mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu kwa dakika 15 alfajiri ya kuamkia jana katika mashimo ya mawe ambayo yako jirani na mapango ya Amboni.

Kamishna Chagonja alisema chanzo cha mapambao hayo, ni tukio la Januari 26 mwaka huu, wakati askari wawili walipovamiwa na watu wasiojulikana na kunyang’anywa bunduki mbili aiana ya SMG, zilizokuwa na risasi 60.

“Upelelezi wetu uliendelea baada ya tukio hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwasaka na tukafanikiwa kupata wahalifu…jana asubuhi tuliarifiwa kwamba silaha hizo zimefichwa kwenye moja ya mapango ya Amboni  na ndiko wakapeleka askari huko ili kuzitafuta,” alisema.

“Wakati askari hao wakiendelea kutafuta, ghafla walivamiwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa wamejificha kwenye eneo lingine la pango hilo …ikalazimika wajibu mapigo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kuzima mapigano, waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko, pikipiki moja, baiskeli tatu, silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mishale, pinde ,
visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.

Akizungumzia kuhusu watu hao kwamba ni kikundi cha wahalifu wa Alshabab au la, alisema mpaka sasa Polisi haijabaini kutokana na ukweli kwamba katika opereshi hiyo hawajafanikiwa kukamata mtu ambaye wanaweza kumfananisha na magaidi hao.

“Msako wetu unaendelea tunaomba wananchi watoe ushirikiano… kwa ukweli ni mapema sana kuthibitisha kwamba hao wahalifu ni wa kikundi cha Al-Shabab kama inavyodaiwa mitaani, kwa sababu  mpaka sasa hatujatambua  sura zao na kubaini ni watu wa aina gani,” alisema.

Alisema askari waliojeruhiwa, wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na hali ya afya zao inaendelea vizuri.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya  Hospitali ya Bombo, imeeleza kwamba askari mmoja wa JWTZ amefariki dunia jana saa 8.30 mchana ingawa Chagonja amekataa kuthibitisha kifo hicho.

Licha ya kudai kwamba hali imerejea kuwa shwari, lakini mpaka sasa wako kazini na ulinzi umeimarishwa kuanzia katika eneo la Utofu lililoko umbali wa kilometa 5 kutoka mjini, ambapo askari wanaonekana kutaka kupata taarifa za kila mtu na magari yanayoendelea kutumia njia hiyo.

Mitaani hali ya ulinzi na usalama miongoni mwa wananchi katika halmashauri ya Jiji la Tanga, iliendelea kugubikwa na hofu kubwa na mashaka kutokana na mapigano yaliyokuwa yakisikika baina ya askari na kikundi cha wahalifu hao.

Mapigano hayo yalikuwa katika kitongoji cha Mikocheni kilichopo kata ya Kiomoni kwenye machimbo ya mawe ambayo yameambatana na eneo la Mapango ya Amboni.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo iliyoko umbali wa kilometa  10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga, walianza kuona vurugu za magari ya askari wa kutuliza ghasia pamoja na JWTZ wakikatiza katika maeneo hayo huku ikisikika milio ya risasi na vishindo vikubwa.

Agata Juma, mkazi wa Kiomoni Majimoto, alisema vurugu hizo zilisababisha wapate hofu na kukumbuka tukio la hivi karibuni la mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono, uliotokea wiki tatu zilizopita kwenye eneo hilo.

“Yani hatuelewi kinachoendelea, maana askari hawazungumzi kitu na wananchi bali tunasikia sauti za ving’ora pamoja na mishindo ya vitu kama mizinga mikubwa ikilia … mambo hayo yanafanyika huko jirani na mampango ya Amboni,” alidai.

Naye Jumaane Amboni, alidai usiku kucha hawakupata usingizi kutokana na hofu, hasa baada ya kupata taarifa ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Polisi, kwamba eneo hilo limevamiwa na kikundi cha Waislamu wenye itikadi kali wa Al-shabab.

“Usiku wa kuamkia leo mambo yalikuwa magumu sana mana tumesikia risasi zikirindima na vishindo kama vya mizinga vikilia mara kadhaa pasipo kuelewa cha kufanya…. tumeamua kukaa ndani na kujifungua.

“Tunachofanya hapa ni kujaribu kukusanya mahitaji ya muhimu kama chakula na vitu vingine, kwa sababu hatuelewi hayo mapigano yataisha lini hasa ikizingatiwa kwamba eneo walilojificha ni ndani ya sehemu ya mapango ya mawe ambayo hayatumiki kabisa,” alisema.

Hata hivyo baadhi ya wakazi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Tanga, ingawa shughuli zinaendelea kama kawaida lakini wamekuwa katika hali ya wasiwasi.

Matokeo Form Four: Shule 10 Bora kwa Ufaulu na Shule 10 za Mwisho ziko hapa

$
0
0
Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.



Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni:

  • Kaizirege mkoa wa Kagera
  • Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
  • Marian Boys mkoa wa Pwani
  • St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
  • Abbey mkoa wa Mtwara
  • Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
  • Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
  • Marian Girls mkoa wa Pwani
  • Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

  • Shule 10 za mwisho ni:
  • Manolo mkoa wa Tanga
  • Chokocho mkoa wa Pemba
  • Kwalugulu mkoa wa Tanga
  • Relini mkoa wa Dar es salaam
  • Mashindei mkoa wa Tanga
  • Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
  • Vudee mkoa wa Kilimanjaro
  • Mnazi mkoa wa Tanga
  • Ruhembe mkoa wa Morogoro
  • Magoma mkoa wa Tanga.

Diamond na Zari The Lady Boss Wakielekea Kumpumzika Kisiwa cha Mahaba Zanzibar..Team Nanii Mpo?

$
0
0
Udaku Special
Unaambiwa Mtoto Zari Hakubaki nyuma siku ya Wapendanao , Kampandia ndege Diamond na Kutua Bongo , Hapo kwenye picha Wakienda zao Zanzibar kula Raha
DIAMOND amepost picha hiyo na kuandika #ValentineWeekEndInZanzibar

Una lipi la Kusema?

PICHA: Timbwili Mitandaoni, Diamond Akiwa na Zari Huku Wema Akiwa na Ommy

$
0
0
Kweli mafahari wikigombana nyasi ndio uumia! Picha za mwanamziki Diamond akiwa na mpenzi wake Zari  wakiwa ndani ya gari alizoziweka mtandao usiku wa kuamkia jana siku ya wapendanao na kuandika kwa maneno ya lugha ya kingreza kuwa wanaelekea siku ya Valentine “Road to Valentine...”
Zilizua timbwili la maneno miongoni mwa mashabiki wa Diamond ambao walikuwa wakisifia
“Project hii” na wale wa Wema  aka TeamWema walikuwa wakiponda na kumshabulia sana mwanadada Zari ikiwemo kumuiga mtindo wa nywele Wema. Hii ilipelekea watu kutupiana maneno makali na mazito yanayoweza kukufanya msomaji upofuke macho.

Baada ya mvutano mrefu kuhusu picha hizo za Diamondi na Zari, Ikatupiwa picha hiyo ya Wema akiwa na Ommy, hapo tena moto ukawaka wale wa mashabiki wa Diamond wakaanza kuponda huku TeamWema wakisifia. Mwisho wa siku watu wakaamua kuzileta pamoja ili watu waseme bila ushabiki kuwa ipi ni project ya ukweli na ipi feki….

Nami nikaona nizilete hapa kwenu,ila sio kushindanisha bali upate kuziona na kukupa ubuyu wa kile kinachoendelea kuhusina na picha za mafahari hawa wawili wenye mashabiki wengi zaidi hapa Bongo.

Jamani mashabiki acheni kutukanana huko mitandaoni, mbona wenyewe hatukanani?

Mzee wa Ubuyu

Tanzia: Baba Mzazi wa Mwanamuziki Dully Sykes Mzee Sykes Afariki Dunia

$
0
0
Baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Dully Sykes, Mzee Sykes amefariki dunia leo akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam. Udaku Special Blog inatoa pole kwa Dully Sykes na familia nzima ya Mzee Sykes kwa msiba huu mzito. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live




Latest Images