Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live

Lady Jaydee Azitaja Sifa za Mwanaume Amtakaye kwa Sasa..Soma Hapa Huenda Ukawa Nazo

$
0
0
Baada ya kutangaza kuwa kwa sasa yuko single, miongoni mwa maswali ambayo Lady Jaydee amekutana nayo ni kuhusu sifa za mwanaume ambaye anamtaka awe mpenzi wake kwa sasa.
Kupitia Instagram Jide aliorodhesha sifa za mwanaume amtakaye kwa sasa, soma huenda ukawa nazo (kama wewe ni mwanaume mwenye ndoto za kuwa na staa huyo).



Yapo maswali mengine pia ambayo yanahusiana na mahusiano ambayo ameyajibu.

“SWALI: Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa?
JIBU : Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.
Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona )
Asiwe tegemezi
Hata km sio tajiri lakini asinitegemee
Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar ,
Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale
Nikikohoa tu awepo hapo

SWALI: Una boyfriend sasa hivi? 
JIBU : Nashindwa kutofautisha boyfriend na lover, wanaojua kizungu wanaweza kunisaidia.
Ila kama ni kwa maana ya rafiki wa kawaida wa kiume,
Nina boyfriends not boyfriend By the way, marafiki zangu wengi ni wanaume zaidi kuliko wanawake. Kama nimeielewa kwa maana hiyo ninayodhania mimi.
Ila kama sio maana hiyo, sina boyfriend then.

SWALI: Eti una boyfriend mzungu?
JIBU : Nina marafiki wa kiume kadhaa ambao sio raia wa hapa, wenye ngozi tofauti na yangu, urafiki wetu ni wa kubadilishana mawazo, kwenda dinner, ku party kiaina na kualikana ma nyumbani kufungua Champagne na kuchoma nyama.
Kama mmeniona nao huko, we were just having fun, nothing serious.
Na sehemu nnazo kuwa nao ni kwenye mkusanyiko wa watu wenye jinsia tofauti.
Not in a bedroom.

SWALI: Una mpenzi kwa sasa? 
JIBU : Ndio, ninae mpenzi kwa miaka mingi sana.
Ananipa karibia kila nnachotaka,
Amenijengea nyumba
Ameninunulia viwanja
Ameninunulia magari
Ananilisha na kunivisha
Anasomesha ndugu zangu
Amenifungulia restaurant Na ameahidi kuninunulia Beach House, na Land Rover model ya 2015.
Ila hizo ni ahadi, bado hajazitimiza.
Kila nikitaka kwenda holiday anagharamia kila kitu
Nikikohoa nataka kwenda kwa fasi ya Paris ana lipa
Tena ananilipiaga ndege business class
Sasa hivi ameniahidi kunilipia trip ya Italy nikawaone kina Kayumba….Ma shopping n.k Hajawahi kunisaliti
Jina lake anaitwa MUZIKI

Maswali yote yanahusu mapenzi / mahusiano lakini nafikiri hayahusiani na ndoa,
Hivyo swala la ndoa naomba nilitenge nitalijibu Ijumaa / Friday ndio litakuwa no. 10 na la mwisho Vipi kwani, mbona wengine mnasonya?”

Lady Jay dee' Aeleza juu ya Umiliki wa EFM Radio 93.7

$
0
0
Maswali yamekuwa mengi kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchin Judith Wambura 'Lady Jaydee' juu ya maisha yake ambapo aliulizwa juu ya kuachana na mumewake lakini pia kuhusiana na kufungua kituo cha matangazo kwa njia ya sauti (Radio) na au umiliki wa EFM Radio inayo patikana kwenye masafa ya 93.7 Fm jijini Dar es Salaam.
Haya ndiyo aliyo sema kupitia account yake ya Instagram.

Ulituahidi utafungua Radio mbona kimya mpaka leo?
JIBU :"Niliandika hiyo kitu siku ya wajinga duniani, April 1, sikuwahi kuahidi.
Lakini matamanio yangu ni siku moja kumiliki kituo cha radio na ikibidi hata television.
Hakuna linalo shindikana, palipo na nia.EFM radio ni yako?
JIBU : Hapana sio yangu
Nafikiri inadhaniwa hivyo kutokana na kila mtu ku tamani, mimi niwe na radio.
Je!mtaniruhusu na mimi niwaulize swali?
Kwanini mnatamani sana niwe na radio? ?
Mungu akijaalia ntakuwa nayo " Ameandika Lady JayDee.

Faiza Kessy Awachokoza tena Wabongo Atupia Picha Akiwa na Kichupi Ufukweni

$
0
0
Mrembo na muigizaji wa filamu, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto mmoja amezibandika picha hizi kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa maeneo ya ufukweni mjini Bagamoyo.
Mbali na ukweli kuwa hapa amevalia nguo za ufukweni, mahabiki wengi wamemshabulia kuwa..
mavazi haya hayafai kwani yeye sasa hivi ni mama tena amezaa na Muheshimiwa, huku wengine wakisema hapo ndio mahali pake na wa muacha afurahie maisha yake.

Japokuwa ni kweli kuwa Faiza aliwashangaza wengi mwaka jana kwa kuvalia “pampers” kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, lakini kwa hizi  nadhani  tumwache, amependeza sana.

Sijui wewe umezionaje!!.

Gari Aina ya Land Rover ya Mwaka 1976 Aliyokuwa Akitumia Bob Marley Yafufuliwa

$
0
0
Hivi ndio mwonekano wa Land Rover aliyokua akiitumia Bob Marley ilivyokua ikionekana kwenye makumbusho ya masanii huyo nchini Jamaica.


Mwonekano wa ndani\Land Rover hiyo inavyoonekana kwa sasa baada ya kufamyiwa matengenezo upya na kampuni ya Land Rover ya Jamaica kwa ushirikiano na familia ya Bob Marley ambaye kama angekua hai angekua amefikisha miaka 70 Februari 7 mwaka huu.
Mwanekano mpya wa gari hiyo
Pamoja na mwonekano mpya pia gari hiyo linaendesha kama jipya.

Mwonekano wa Ndani

Mwigizaji Vicent Kigosi ‘Ray’ Amtapeli Upya Johari

$
0
0
Gazeti la udaku la KIU, limeripoti kuwa hali ndani ya kampuni ya RJ inaendelea kutokuwa shwari kwa kile kinachodaiwa kuwa kuwa wakurugenzi waanzilishi wa kampuni hiyo Vicent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’ kutokuwa na maelewano mazuri na sasa ikidawa kuwa chanzo ni pesa kutoka kwa wadhamni waliokuwa  wakihitaji  kudhamini filamu inayotengenezwa na makampuni hayo.

Chazo hicho ambacho kipo ndani ya kampuni hiyo kilisema kuwa pesa hizo zilitolewa na mfanyabiashara maarufu ambaye aliombwa kutoa msaada  katika kufanikisha filamu hiyo ambayo ilikuwa iwashirikishe wasanii kutoka Nigeria lakini imeshindikana kutokana na mgogoro wa kiuongozi uliopo kati ya wakurugenzi hao wawili.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa mtu wa kwanza amabaye anaonekana  sio muaminifu katika pesa hizo ni Ray kwani mara baada ya  mfanyabiashara huyo kukubalia pesa hizo alikuwa akienda kufuatilia msaada kinyemela akiwa na Chuchu huku Johari akibaki ofisini.

Aliendelea kusema kuwa Ray alikuwa akitumia mwanya wa kuwa na mahusiano na Chuchu kwa hiyo hata walipokuwa wakitoka ofisini Johari alikuwa akijua kuwa ni mtoko wa kimapenzi ya kawaida lakini  kumbe wao walikuwa wanakwenda kwa mdhamini kuchota pesa za filamu hiyo.

“Baada ya Johari kugundua kuwa kuna mchezo unaochezeka nyuma ya pazia ndipoalipoamua kwenda moja kwa moja  kwa mfanya biashara huyo kwasababu yeye ndiye aliekuwa connection ya  mchongo huo”.

Gazeti la hilo liliwasiliana na Johari kwa njia ya simu kuhusiana na jambo hilo lakina mara baada ya kupokea simu  alisema kuwa yupo kikaoni atafutwe badae.

Kwasasa nipo kwenye kikao siwezi kuzungumzia swa hilo nitafute badae” alisema Johari na kukata simu.Licha ya kutafutwa badae simu yake haikuwa hewani mpaka gazeti hilo linakwenda mitamboni. Ray hakupatikana kabisa kwenye simu.

Ommy Dimpoz: Diamond Amepotea Maboya Kwa Kushindwa Kumpetipeti Wema Sepetu na Kumtumia Ipasavyo

$
0
0
Katika kile kinachoashiriankuwa ni kunogewa na joto la mahaba, mwanamziki wa Bongo Fleva Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ nadaiwa kuanza kumcheka  swahiba wake Diamond Platnumz kwa kushindwa "kumpetipeti" na kumtumia ipasavyo aliekuwa mpezi wake Wema Sepetu.



Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu  na Ommy zinasema kuwa  mwanamuziki huyu amekuwa akitoa maneno matamu matamu akimsifia Wema na wakati mwingine akimnanga Diamond.

“Inawezekana kwamba wapo katika project lakini ukweli ni kwamba Wema amtawala Dimpoz akilini,mazungumzo yake yote ni kuhusu Wema na anadai kuwa Diamond amepeotea maboya kuachana Wema kwani nyota ya Wema haizuiliki hata kwa radi”, alisema  rafiki huyo. Hii ni kwa mijibu wa gazeti la KIU.

Lakini kwa ujumla mahusiano baina ya wawili hawa bado yanawaweka watui njia panda kwani sio Ommy wala Wema aliejitokeza hadharani na kuthibitisha mahusiano yao, lakini mbwembewe za wapambe wao kwenye mitandao ya kijamii zionyesha kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi huku wengine wakiamini kuwa Ommy anataka kung’aa kupitia nyota ya Wema na hakuna swala la mahusiano ya kimapenzi.

'Magaidi wa Tanga' Watiwa Mbaroni.....Mwili wa Mwanajeshi wa JWTZ Aliyeuawa katika Mapigano hayo Waagwa

$
0
0
Serikali imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga, ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu.
Aidha, imesema  watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo.
 “Tunawashikilia ila mpaka sasa siwezi kukueleza idadi yao na kwamba ni wa kikundi cha ugaidi au ..
la. Hao watu tunafanya nao mahojiano ili kuweza kuelewa kama wanahusika kwenye tukio hilo,”  alisema Kaimu Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Ndaki alisema hali katika kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari. “Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha zilizoibwa,” alisema.

“Tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa wanapoona watu wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili nasi tuweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hili”, alisema.

Ingawa Kamanda hakuelezea mazingira ya kukamatwa kwa watuhumiwa, waandishi wa habari waliozuru eneo la Amboni  yalikotokea mapigano, waliarifiwa kwamba baadhi ya wavuvi kwenye Mto Zigi, walimkamata mtu wakimtuhumu kukutwa akifua nguo zenye damu.

Katika mapigano hayo baina ya askari na wahalifu, yalisababisha kifo cha askari wa JWTZ,  Sajenti Said Kajembe na wengine kujeruhiwa.

“Asubuhi wavuvi kadhaa walikuwa hapo mtoni ghafla walikutana na mtu pembeni ya mto akiwa anafua kanzu pamoja na vifaa fulani kama nguo za kufunika uso ..’maski’ ikabidi wawapigie haraka polisi simu lakini hawakuweza kupatikana na ndipo wakawapigia askari wa JWTZ ambao walifika haraka eneo la tukio na kumkamata mhusika”, alisema mkazi mmojawapo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Magalula Said Magalula aliwataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na hali ya usalama ni  shwari.

Pia, aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea eneo la kihistoria la Mapango ya Amboni, kuendelea na ratiba zao kwa sababu eneo hilo liko salama na tangu awali halikuhusika kwenye vurugu hizo.

Magalula ambaye pia alikutana na waandishi wa habari, alisema “Hali ni nzuri ulinzi na usalama uko imara… naomba wananchi waondoe hofu, wawe na amani na waendelee na shughuli zao za uzalishaji… hakuna tatizo kabisa usalama umedhibitiwa vizuri.”

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alisisitiza  “Naomba Watanzania wenzangu muelewe kwamba eneo lilipofanyika tukio la mapigano na wahalifu si pale yalipo mapango ya Amboni ... maeneo hayo yapo mbali na nitoe mwito kwa wageni wenye mpango wa kutembelea hapo wawe huru kufanya hivyo mahali hapo ni salama.”

“Naomba Watanzania nchini kote kwa ujumla wawe na amani kwa sababu Tanga iko shwari hakuna tena hizo vurugu za wahalifu… naomba wasiamini sana taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii… sisi tuko shwari na shughuli za kijamii zinaendelea kama kawaida ikiwemo Amboni,” alisema.

Akizungumzia mapigano hayo yaliyotokea  Februari 14,  alisema licha ya majibizano ya kurushiana risasi yaliyofanywa na askari wa Polisi kwa kushirikiana na wa JWTZ , uchunguzi unaendelea  kuwapata wahusika.

“Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kuwasaka pamoja na kutafuta silaha zetu lakini hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa … zipo simulizi mbalimbali zinazoendelezwa kwenye mitandao ya kijamii ila sisi serikali ya mkoa bado hatujathibitisha kwamba watu hao ni wa kikundi gani ila ninachokifahamu hao watu ni wahalifu”, alisisitiza.

Kuhusu kuongezeka kwa matukio  katika maeneo mbalimbali mkoani humo,  alisema kila tukio linachukuliwa kwa uzito mkubwa na linashughulikiwa kwa namna linavyotokea.

Aidha, amewataka wakazi wa Tanga hususan wanaoishi eneo la Amboni na vitongoji vyake kuhakikisha wanaendelea kutoa habari sahihi kuhusu watu mbalimbali wanaowatilia shaka . Alisema taarifa hizo zina umuhimu wa kipekee kwa askari katika kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.

Kutokana na maswali mengi ya wanahabari na wananchi, kudai kutoridhishwa na mwenendo  wa utoaji taarifa kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa aliruhusu watembelee eneo la tukio  kuthibitisha kama hali ni shwari katika eneo husika.

Timu ya wanahabri takribani 10 kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa chini ya ulinzi wa askari walipelekwa eneo la tukio, ambalo liko umbali wa takribani kilometa tano kutoka yaliko Mapango ya kihistoria ya Amboni.

Eneo hilo limetawaliwa na miamba ya mawe makubwa yenye mapango, ambayo hayatumiki kwa shughuli za kihistoria, kama ilivyo katika kitongoji cha Kiomoni yalipo mapango ya kihistoria ya Amboni.

Shughuli zinazoonekana kufanyika jirani na eneo hilo, ni ulipuaji wa miamba kwa kutumia baruti ambao hufanywa na wachimbaji wadogo kisha kuvunja kokoto  kwa ajili ya viwanda vya kutengeneza chokaa pamoja na mawe kwa shughuli za ujenzi mjini hapa.

Eneo wanakodaiwa kuishi wahalifu hao,  liko umbali wa meta 300 kutoka upande wa pili zinapofanyika shughuli za upasuaji  kokoto zinazoendeshwa na wakazi wa kitongoji cha Majimoto na Mafuriko huko Amboni.

Katika eneo hilo,  kulikuwa na ukimya kutokana na kutokuwapo shughuli yoyote hususani uvunjaji kokoto iliyozoeleka kutokana na wananchi kusimamishwa kutokana na tukio hilo.

Waandishi wa habari walilazimika kufuata maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na wanausalama waliokuwa wakiwaongoza  kufika ndani ya pango husika.

Mwonekano wa eneo hilo, ulidhihirisha ni la hatari kutokana na mapango kufunikwa na vichaka. Ndani ya pango hilo, upo uwazi mkubwa unaoashiria uwepo wa shughuli za kibinadamu zilizokuwa zikiendelea.

Ndani ya pango hilo, zilikutwa nguo; hususan suruali, madumu ya kuhifadhia maji, vikombe kadhaa vya plastiki, chupa za maji ya kunywa zilizotumika hatua ambayo imedhihirisha kuwapo binadamu waliokuwa wakikaa humo licha ya kwamba, kufika kwake ni kwa shida.

Wakazi wazungumza
Wakizungumza na waandishi, baadhi ya wakazi wa maeneo jirani na eneo hilo, walisema hawajaruhusiwa kufika eneo hilo kwa kuwa linaendelea kulindwa  na askari wa Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)  kwa kushirikiana na JWTZ.

“Muda mfupi tu kabla ya ninyi kwenda huko, askari wa FFU walitoka huko , ninyi mnaelezwa kwamba pako shwari lakini sisi bado hatujaruhusiwa kufika kule kwa sababu panalindwa muda wote na askari… ,” alisema mkazi  aliyejitambulisha kwa jina moja la Mrisho.

Katika hatua nyingine, askari wa JWTZ aliyefariki wakati akitibiwa kwenye Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa kwenye mapigano hayo ya mwishoni mwa wiki,  mwili wake uliagwa jana mjini hapa kabla ya kusafirishwa kuelekea wilayani Korogwe kwa maziko yaliyofanyika katika kijiji cha Bungu

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta Amsimamisha Kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Madeni Kipande

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande kutokana na kile kilichoelezwa kuwa uendeshaji mbovu wa utoaji wa zabuni.


Aidha, amemteua Awadhi Massawe kushika wadhifa huo. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa Meneja wa Bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sitta alisema uamuzi huo umetokana na kuwapo malalamiko ya kutofuatwa kwa taratibu za zabuni na ucheleweshaji wa barua kwa wanaoshinda.

“Ni muhimu sana taratibu zetu za ununuzi katika bandari ziwe wazi na ziheshimike duniani kote, maana miradi hii ni mikubwa sana inayopitishwa na bodi ya zabuni ya TPA,” alisema.

Sitta alisema,  aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Dk Harrison Mwakyembe alianza kushughulikia masuala hayo, lakini hayajakaa vizuri. Alisema hakuna uwazi na kumekuwa na ubabaishaji mkubwa, ikiwemo kubadilika majina ya kamati za kutathmini zabuni.

Wakati huo huo  Sitta ameunda timu ya watu sita itakayochunguza tuhuma za Kipande. Imepewa wiki mbili iwe imefanya kazi hiyo.

Timu hiyo itaongozwa na Jaji mstaafu, Augusta Bubeshi na Katibu wake, Deogratius Kasinda ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Uchukuzi.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Manunuzi ( PPRA) Dk Ramadhani Mlinga, Samson Lugigo , Happiness Senkoro na Flavian Kinunda ambao walishawahi kushika nyadhifa za juu ndani ya TPA.

“Nimejitahidi kuchukua hawa wastaafu kwa sasa hivi hawatafuti cheo chochote, naamini watatenda haki, watachunguza tu bila kufanya uonevu,” alisema Sitta.

Waziri Sitta alisema bandari ni eneo muhimu, kwani takwimu zinaonesha kwamba asilimia 43 ya makusanyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yanatokana na kodi ya ushuru wa forodha. Kati ya makusanyo hayo, asilimia 87 yanakusanywa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa Kipande,  alisema hawezi kupinga hatua iliyochukuliwa na waziri .

Hata hivyo, alisema anaamini kipindi chote cha uongozi wake, alifanya ambayo yalikuwa sahihi na hana wasiwasi na uamuzi huo.

"Mimi sina wasiwasi na hilo sababu huo ni uamuzi wake; lakini nina imani kuwa katika bandari hii, nimefanya kile ambacho nilikuwa natakiwa kufanya,  hivyo sina shaka na hilo," alisema Kipande.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto ametaka serikali kujenga matangi ya kuhifadhia mafuta na kujenga bomba la mafuta kwenda mikoani.

Aidha, kamati hiyo imetaka TPA kuangalia uwezekano wa kununua hisa 50 za Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (Tiper) imilikiwe kwa asilimia 100 na Serikali.

Kuhusu ujenzi wa matangi, Zitto alisema hatua ya Serikali kujenga matangi yake ya kuhifadhi mafuta, itasaidia kujua kiasi cha mafuta yanayoingia na kuweza kukadiria kodi kwa uhakika.

Akitoa mfano wa Kenya, alisema Serikali inamiliki matangi ya kuhifadhia mafuta,  wanayapima kujua kiasi cha mafuta kilichoingia na kukitoza kodi  kabla ya kupelekwa kwenye matangi ya waagizaji.

“ Walichofanya, wamemtaka kila muagizaji kuwa na flow meter  yake na yakitoka kwenye meli yanaingia kwenye matangi ya Serikali na baada ya kujua kiasi na kutozwa kodi hupelekwa kwa walionunua,” alisema.

Zitto  alisema wakati umefika sasa kwa serikali kujenga mabomba ya kusafirishia mafuta na kwa kuanzia yakawa matatu, ambayo yatasaidia kuondoa mfumo wa sasa wa kusafirisha kwa magari.

“Linaweza kujengwa bomba moja kwenda Mbeya, likawa na matoleo kwa ajili ya mikoa ya Morogoro, Iringa na mikoa iliyo jirani, kwa kufanya hivyo tutaondoka na hali ya sasa ya kusafirisha mafuta kwa magari,” alisema.

Alisema katika kuimarisha reli, ni vyema ukaanzishwa mfumo wa kutoza kodi asilimia 1.5 kwa kila bidhaa inayoingia nchini na fedha hizo ziimarishe usafiri wa reli.

“Kwa sasa asilimia 99 ya mizigo inasafirishwa kwa barabara, hili si jambo jema kwa uchumi, najua nikisema hivyo wenye malori watalalamika, lakini wanaweza kufanya biashara nyingine,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Awadhi Massawe alisema asilimia 60 ya mafuta yanayoingia nchini hupitia kwenye boya la Single Buoy Mooring (SBM).

Alisema wamejipanga kujenga mita ya kisasa ya kupimia mafuta maeneo ya Kigamboni huku ile ambayo haitumiki, wamepanga kuiboresha na kuwa ya kisasa.

Kuhusu maendeleo ya ujenzi wa gati namba 13 na 14 ambazo zabuni  yake iliingia utata, Massawe alisema ripoti ya maandishi wataipeleka kwa Kamati hiyo ya Bunge ifikapo Machi Mosi mwaka huu.

Pia, Massawe alisema hatua ya kitengo cha kupakua kontena kupewa mtu binafsi, inawapunguzia mapato na kuwa hiyo ndio sekta ambayo inaingiza fedha nyingi.

Alisema ili kupambana na hali hiyo, wamejipanga kuimarisha gati namba 1 hadi 7 na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kupakua makasha na kuwa kwa mwaka jana waliweza kupakua makasha laki Mbili.

Wema Sepetu na Ivan it's ON, Wana-date, Ommy Dimpoz na Wema Sepetu ni Zuga Tu

$
0
0
In other news, Tanzania’s sweetheart ,Wema Sepetu is officially dating mheshimiwa Ivan kutoka Uganda ambae kwa sasa anaishi South Africa. Kwa msiomfahamu IVAN ni ex-husband wa GF wa Tanzania’s superstar Diamond PLATNUMZ anaejulikana kama Zari the boss lady.



Yes, this is 120% confirmed,no, its 200% CONFIRMED. Kwasasa hawataki kuweka relationship yao out there kama kina fulani sababu wao wako pamoja sababu wanapendana na sio sababu wanataka kushindana na their exes au sababu they are looking for attention.

I think Wema kajifunza kuwa hizi relationship za mapicha kila baada ya dakika 5 huwa hazi last so kaamua yeye na Ivan mapenzi yao yawe ya kwao wao mpaka hapo watakapo ona wamejuana vizuri ndo watayaweka wazi. Yes, wengi wataona kuwa sio sawa hawa kuwa pamoja kwa sababu zilizo wazi ila pia mkumbuke kuwa sometimes watu hukutana kwenye circumstances za ajabu ajabu.

Yes, labda wasingejuana kama sio exes wao kutoka pamoja ila again labda ndo ilikuwa njia ya Mungu kuwakutanisha wawili hawa.

Hata Rihanna aliimba ” We found love in a hopeless place” naongea hivi sababu, it is real between these 2 na wanapendana haswaaaa. Na nimeamua kuwa support mapenzi yao sababu wanayaficha which means ni mapenzi ya kweli, sio mapenzi ya magazeti au kuonyesha watu au kutafuta attention like kina fundenge

Yaani ni mapenzi ya kiutu uzima sio ya nursery school. Nimeyapenda mnoooo… Na mdogo wangu mnamjua kwa kufall in love! Hahahaha!


Also Im sure utakuwa umenotice hiyo DP kwenye insta ya wema hiyo ya Lipstick ni kwamba Wema analeta lipstic za maana zenye jina lake, in each and every color. Na project nzima iko funded na mzee mzima Ivan….

STAY TUNED!

Haya ndo mapenzi mazuri sasa…..Ukimpenda mwanamke unamnyanyua ili na yeye aweze kujitegemea na awe your equal.. Na mwanamke pia akiwa na mwanaume anaemnyanyua hivi atampendaje sasa? Yani mwanaume utafurahi maisha mbona….

Anyways, siku hii news ya Wema and IVAN iki break out officially, just remember where you heard it first… hahahahhahaa! So, Yes, Wema na Dimpoz hakuna kitu chochote kinachoendelea, Walikuwa wanafanya music video, basi!

Ila wana enjoy jinsi wanavyowazingua na mapicha na ku divert attention from the real couple….hahahaha…Alafu naskia King Lawrence kapigwa mkwala wa hatari na Ivan, not to say or publish any pics ya relationship yake na Wema..

Jamani ndo maana siku zile wakati King anamdhalilisha Zari nilikuwa nawaambia kuwa dont blame King, King anafanya vile anavyotumwa na IVan, nothing more, nothing less. Mbona issue ya Wema kaambiwa aache na kaacha? hahahahahha!

Mmmh, ona Ivan na Wema wanavyozuga watu huko instagram. Wema anacomment kwenye picha za Ivan na Ivan ane anamjibu kama vile hawajuani…hahaha!

Chanzo: U-turn

Valentine Yamkalia Ommy Dimpoz Vibaya Azuiliwa Kuingia Marekani Kufanya Show..Arudia Uwanjani

$
0
0
Nasikia viza aliyokuwa amekata haikuwa ina mruhusu kufanya show nchini marekani! Inasemekana alitakiwa kukata viza ambayo inaonesha ana kwenda kufanya show nchini marekani na bila shaka gharama zake ni tofauti na ile ya kwenda kutembea!Viza aliyo kuwa amekata ilikuwa ya kwenda kutembea tuu na kusalimu ndugu na jamaa si kufanya show....


Sasa kilicho tokea alipo fika uwanja wa ndege akazuiwa kuingia nchini marekani kwani viza aliyo kuwa amekata ilikuwa haimruhusu kufanya show ni baada ya kuhojiwa!

Ninacho jiuliza kwanini watanzania tunafikiri kila sehemu tunaweza kufanya ujanja ujanja? Kwanini hatupendi kufata utaratibu?Bahati mbaya zaidi show ilikuwa imesha andaliwa na jana kama si juzi ilibidi afanye!

Yani mtu anataka pesa halafu anaogopa kuingia gharama kukata viza itakayo mruhusu kufanya show nchi ya watu!

Mapigano ya Magaidi na Polisi Mapango ya Amboni Tanga Hii ndio Full Story

$
0
0
NI kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video wakizungumzia uhalifu....


Cha ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya  Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.

MASHUHUDA WA MAPIGANO 
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili hivi.

“Mke wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi. Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia tena.”

WAZIKIMBIA NYUMBA 
Mwanahawa Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.”

SIKU MBILI HAKUNA KULALA 
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.

“Mimi na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.

INAVYODAIWA 
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu nchi jirani ya Kenya.

Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.

“Lengo lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.

“Yule jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.

WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.

“Kutuambia wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?” alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.

Kusema ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally, mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.

KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.



Watu hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.

KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
“Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,  askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.    

Johari Aibuka na Kusema Hawezi Kuwa na Ray Tena , Na Wala Hapendi Wanaume Mastaa

$
0
0
STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’ bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke......


Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtafutaji,” alisema Johari.

Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi mapenzi yao yalikuwa ni ya ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ na wala si ndoa.
GPL

Masikini..Kijana Aingizwa Mochwari Akinizaniwa Amekufa

$
0
0
Kijana mmoja, Omary Ramadhani, 28,  (pichani) mkazi wa Sinza Madukani, Dar  amenusurika kifo baada ya  kupata  ajali ya kugongwa na ‘Break Down’ alipokuwa akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi, Mwenge,  jijini Dar es Salaam.


Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari hilo hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua  na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka apimwe.

Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo, Omary alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa shida.

Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.

Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia tena.

Alisema alipata matibabu kwa muda wa miezi sita ndipo aliruhusiwa kuondoka lakini alitakiwa atoe shilingi 1,000,000  kwa ajili ya tiba maalum kwenye mashine ambayo siijui jina, lakini nimeshindwa kuzipata na ndugu zangu ni walalahoi.
Omary alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki sawasawa na akienda maliwatoni  huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo hutoka kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa anapata mara moja kwa wiki.

Omary  amewaomba Watanzania wenye moyo wa huruma kumchangia ili atibiwe, aepukane na mateso makali anayopata. Namba yake ni 0656  168 034.

This is what Happens Tp a Girl's Mouth on February 15 After Valentine's Day

$
0
0
This is what Happens Tp a Girl's Mouth on February 15 After Valentine's Day

Chris Brown and Karrueche Tran reunited in New York back in love

$
0
0
They have had more ups and downs than a roller coaster but looks like Chris Brown does not plan to let Karrueche Tran go any time soon.
After breaking up over the Christmas holidays then spending Valentine's day apart on Monday, the
on and off again couple finally were back together on Monday.
With a night off from his tour, the 25-year-old rapper flew into to New York to be with his girlfriend, who is there for Fashion Week and the NBA All Star Weekend.


Hatujakama Jambazi yoyote Mapango ya Amboni Tumewazidi Nguvu Wakatutoroka-Polisi

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini, limesema majambazi waliokuwa wamejificha katika mapango ya Amboni nje kidogo ya jiji la Tanga wamekimbia.
Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja, akizungumza..
jana alisema majambazi hao wamekimbia baada ya kuzidiwa nguvu na askari wa jeshi lake wanaoshirikiana na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Nini unataka kuliambia jeshi la polisi?

Matano ya Jerry Muro kuhusu Panya Road, Ubunge, Rushwa, Familia, Yanga… Yote kutoka MkasiTV

$
0
0
Leo February 16 kwenye show ya Mkasi kulikuwa na Interview na Mwandishi wa Habari Jerry Muro, mengi kayazungumzia ikiwemo kuhusu familia, kazi yake na kesi za rushwa, pamoja na mapenzi yake na timu ya Yanga yalikoanzia....

Alichokijibu kwanza kuhusu familia;“Nna mke.. watoto hapana, ni suala la muda na wakati kujipanga. Hawa ambao wana watoto sasa hivi hawakukosea lakini hata ukiangalia mfumuko wa watoto wengi Panya Road wametoka wapi. Mtoto akipatikana kwa wakati sahihi na ukimleta duniani kwa malengo sahihi hawezi kwenda kuwa Panya Road“

Kuhusu ishu ya watu kukimbia taaluma ya ualimu;“zamani wakati tunakua tukienda Kijijini tunaambiwa ‘ile ni nyumba ya mwalimu’, zamani mtu kuwa mwalimu alikuwa na nafasi kubwa kwenye jamii kuliko hata Waziri.. Ualimu wa Nyerere ndio ulimpa nafasi kubwa sana tangu ameanza harakati zake mpaka kushika madaraka.. Hakuna jambo tulilikosea na hatutasamehewa kwa Mungu tulipoamua kubinafsisha sekta nyeti sana, elimu na afya“
Suala la kugombea Ubunge; ” Naamini kiongozi bora ni yule ambaye amesha demonstrate tangu mwanzo kabisa na ameshaonyesha vitu ambavyo vinaashiria huyu ni kiongozi. Mimi sijisemi kuw ni kiongozi mzuri kwa wale wanaojua kazi nilizozifanya kipindi kile niko kwenye uandishi wa habari nili demonstrate“

Kuhusu ishu ya kesi ya Rushwa;” Mimi sikuomba rushwa nikakamatwa.. askari mmoja akahoji hapa tunaandikaje, tunakupa dhamana kwa kosa gani?
Baadaye nikaenda Mahakamani ikasomewa niliomba Rushwa.. Kwenye kesi yangu wakati Hakimu anatoa ruling alisema hapakuwa na ushahidi wa mimi kuomba rushwa..“
Sijawahi kuomba Rushwa lakini nimekutana na mazingira mengi ya kupewa Rushwa. Mimi ni mwandishi wa kwanza wa pekee wa television kuonesha mtu mwenye dhamana ya Serikali.. mwenye crown akila rushwa hadharani.. Nilifanya hiyo nikiwa ITV, baadhi ya watu wakasema huyu si ameotea tu.. Nilipoenda TBC nikafanya tena story ileile nikarusha.. Tangu nilipomaliza kesi yangu mpaka leo sijaajiliwa na mtu yoyote“


Hapa alizungumzia mapenzi yake na Klabu ya Yanga yalikoanzia;“Mapenzi na Yanga yalianzia kwa baba yangu.. Baba yangu alikuwa anapenda Yanga.. Ukifanya utafiti wa juu juu tu katika nchi zilizo kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki Tanzania inaongoza kuwa na mazingira mazuri sana ya mchezo wa mpira wa miguu. “
Nimekurahisishia kwa kukuwekea hii sauti hapa, bonyeza play kuisikiliza sehemu ya Interview hiyo..

Usithubutu Kupendwa na Nuhu Mziwanda...Mana Napenda Mpaka naboa...No cheating

$
0
0

"Ofcoz najua kupenda sijui kutenda na nikikupenda nimekupenda ndo mana mtoto kasalenda.usithubutu kupendwa na mziwanda.mana napenda mpaka naboa.No cheating inakua safari njema sana na yenye amani ya moyo na maisha yangu pia' Mziwanda

Unazungumziaje Nuhu Mziwanda?

Kiongozi wa Team Wema Afunguka ' Wema Anaye Mpenzi Wake Handsome Boy Fulani na Miakili Tele ila wapo Kiprivate Zaidi'

$
0
0
Kubwa la Maadui Dougiemasta wa Instagram Ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Team Wema Sepetu amefunguka Kuhusu wale wanaotaka kujua kama wema ana mpenzi ama la kwa sasa baada ya kuachana na Mwanamuziki Diamond Platnumz...Haya ndio aliyoyasema:

'Kabari habari zenyu wananchi.kwa watu jana wameni uliza kwanini wema ajamuonesha mpenzi wake na wala ajaonesha wapi walikwenda kwenye valentine day banange kwani ukipiga picha halafu umepozi kama uko kwenye mahaba kwaiyo hapo inamaanisha kuwa mnapenda sana ? just picha aina maana yoyote. Valentine day sio lazima utoke out na mpenzi na vitu fulani una weza kukaa home na unayempenda basi maisha yanakwenda. Haya mapenzi ya mitandao yasiwasumbue akili zenu watu wanatumia pesa nyingi kuonesha wapizani wao kuwa wao wanapenda

Nakumbukeni kuwa wema alisema mwaka huu anataka kujifunza yale makosa yako yote ,wema yupo bussy sana na mambo ya kikazi na biashara kuweni wavumilivu mtaona vitu vyake mwaka huu.Wema Sepetu anaye mupenzi wake handsome bay fulani hivi good looking kichwani miakili tele mpenda maendeleo yaani ni mchapa kazi  tulizo la moyo wake wanapenda sana ssa wapo private zaidi sio kujionesha mwisho wa siku mnapata aibu.valentine day just one day tu tena tayari imepita ssa kama ulikuwa unalazima ili uonekane kama unapenda siku kama ya leo unajita kimoyo moyo acheni kuzuzuka siku hiyo say big No to matusi'

Picha: Range Rover ya AY yamdatisha Daz Baba, asema AY ni mfano wa kuigwa

$
0
0
Msanii wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amemmwagia sifa kibao rapper Ambwene Yessayah aka AY kuwa ni msanii wa kuigwa.
AY alitinga kwenye mazishi ya Mzee Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover ya rangi ya kijivu kitu ambacho kilimvutia Daz Baba...


Daz ameiambia Bongo5 kuwa AY ni mshikaji wake toka kipindi cha nyuma na anavutiwa na hustle zake.


AY akiondoka katika makaburi ya Kisutu baada ya mazishi ya Ebby Sykes akiwa kwenye Range Rover

“AY yuko vizuri sana, ni mfano wa kuigwa, mzee wa commercial toka kitambo anafanya muziki mzuri ndo maana unamuona hivyo, ” alisema Daz. “Jamaa anajituma, anafanya kazi kwa bidii ndio maana unaona hayo mafanikio yote,” aliongeza.

Pia Daz amesema kuna mpango wa kufanya ngoma na muimbaji huyo wa ‘Zigo’.

“Nina mpango wa kufanya naye kazi. AY ni mshkaji wangu toka kitambo kwahiyo kila kitu kitaenda sawa.”


Viewing all 104705 articles
Browse latest View live




Latest Images