Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Ukweli Kuhusu wa Mwanamuziki Snura wa Majanga Kujifungua Mtoto wa Pili na Kumficha South Africa Huu Hapa

$
0
0
Alikuwa wapi? Baada ya kupotea kwa muda mrefu, staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi hatimaye ameibuka na kueleza sababu za ukimya wake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum, Snura amefunguka kwamba ukimya wake ulitokana na kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kushuti video ya wimbo wake wa Najidabua na siyo kweli kwamba alikuwa mkoani Mbeya kwa mwanaume.

Katika intavyu hiyo, Snura alikanusha tetesi za kuzaa mtoto wa pili na kusisitiza ana mtoto mmoja na wanaosema maneno hayo wamekosa la kusema.Ijumaa Wikienda: Huoni kukaa kwako kimya mashabiki wamekusahau?Snura: Hawajanisahau kabisa na hilo nililithibitisha hivi karibuni kwenye shoo niliyofanya Msasani Club (Dar), ambapo walijaa tofauti na mwanzo japokuwa mwanzoni kabla ya shoo nilikuwa nawaza wamenisahau.

Walifurahi sana kwani kwa sasa nimekuja na staili tofauti ya kukata mauno ambayo inatambulika kwa jina la Mauno ya Panya Road, yaani haya ni hatari.Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba wewe na mpenzi wako DJ Hunter wa Mbeya mmeachana, hili likoje?

Snura: Unajua katika maisha yangu Hunter ndiye mwanaume wa kwanza kumuanika na sikuwahi kuanika mapenzi yangu kabisa kabla ya hapo. Sasa baada ya kuwa tunatupia picha mbalimbali kwenye mitandao watu walinifuata na kunieleza kwamba ninavyofanya siyo vizuri.

Nilichukua ushauri wao na kuufanyia kazi na mpenzi wangu nikamwambia, tukaacha tabia hiyo.
Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.
Ijumaa Wikienda: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?
Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.

Diamond Atupiwa Jini, LAMPATA mama Yake

$
0
0
Diamond Akiwa na Mama yake Mzazi
Imevuja! Kuna madai kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametupiwa jini lakini likamkosa na kumpata mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kisha kumsababishia ‘gonjwa’ la ajabu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, watu wanaodaiwa kuwa ni wabaya wa Diamond (Anti-Diamond) walimtupia jini staa huyo lakini bahati nzuri likamkosa na kwa bahati mbaya likampata mama yake ambaye alipata ugonjwa wa kupooza ghafla.

“Ujue kumekuwa na sintofahamu kwa muda mrefu juu ya ugonjwa wa mama Diamond lakini habari za uhakika ni kwamba, mama Diamond yupo hoi baada ya kutupiwa jini ambalo mlengwa wake alikuwa Diamond.

“Mungu tu hakupenda limpate Diamond lakini inasemekana kwamba jini hilo ni hatari endapo lingempata Diamond kwa jinsi lilivyokuwa, basi pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND ALIJUA ‘MCHEZO’ HUO?
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, Diamond alijua kwamba mama yake ametupiwa jini ndiyo maana alikuwa akisuasua kutoa uamuzi wa kumuwahisha nchini India kwa matibabu ya hospitali.
“Diamond alijua kuhusu mpango huo wa wabaya wake kutaka kummaliza kishirikina ndiyo maana hakutaka kumkimbiza haraka hospitali na badala yake alijikita kwenye swala na dua kwani yeye anaamini katika dini zaidi,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, baada ya kutafakari kwa umakini wa hali ya juu, imeelezwa kwamba, Diamond alilazimika kumpeleka mama yake nchini India na kupatiwa matibabu kisha kurejea nchini.

ALIRUDI MZIMA
Kwa mujibu wa ndugu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, hivi karibuni (kabla ya Valentine’s Day), mama Diamond alirejea nchini akiwa na afya njema lakini siku chache baadaye alizidiwa tena na kurudishwa India huku ndugu wakijawa na hofu.

“Alirudi Bongo lakini hakukaa sana akazidiwa tena tukalazimika kumrudisha India kwani hali ilizidi kuwa mbaya. Tumekuwa hatutaki kueleza sana juu ya suala hili maana Diamond mwenyewe hapendi haya mambo yajulikane,” alisema ndugu huyo.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya chanzo hicho kuvujisha ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimvutia waya Diamond ambapo alikiri kwamba mama yake yupo India lakini hakutaka kulizungumzia zaidi eneo hilo badala yake akaanza kushusha lawama kwa wale aliodai wanamsema vibaya.

“Mama bado yuko kwenye matibabu nchini India na hali yake kusema kweli si nzuri, naomba hapo nisizungumzie sana. Kuhusu masuala ya kutupiwa jini, mimi namuamini Mungu, naamini mama atapona.
“Inaniuma kila siku ninaposikia watu wanaongea vitu ambavyo si kweli na kwa namna nyingine nashindwa kujibu vitu ambavyo mwenyewe sivijui hivyo yote namwachia Mungu, maana yeye ndiye jibu la yote.

“Halafu pia kuna muda ufike, watu wawe wanafahamu mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, wasiwe wananijazia vitu utafikiri mimi sina moyo, wawe waelewa, sipo katika kipindi kizuri kwa sasa na si kila kitu wanachosikia au kuona lazima mimi nikizungumzie, kuna mambo mengine ni ya ndani ya ukoo na yako juu yangu sana, hivyo ukiona kimya simaanishi kuna watu nimewadharau,” alisema Diamond.

TUMEFIKAJE HAPO?
Hivi karibuni kuliibuka madai kwamba kwa makusudi Diamond alishindwa kuhudhuria msiba wa baba Abdul Sykes ‘Dully’ na badala yake picha zikavuja zikimuonesha akiwa kisiwani Zanzibar na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ kitu ambacho mwenyewe alikikanusha.

“Si kila picha unayoiona katika mtandao wa kijamii basi itakuwa imepigwa muda huo, inaweza kuwekwa leo kumbe ni ya muda mrefu,” alisema Diamond.
GPL

Msanii Chege anaswa live na ndumba jukwaani..Hirizi Yaning'inia Live Mkononi

$
0
0
Katika bonanza lilopigwa mwishoni mwa wiki mjini Dodoma la Pspf..picha iliopigwa jukwaani wakati mshakaji akiwa busy kukata mapanga...pengine ile dhana ya wasanii na ndumba ni dam dam inaanza kujidhihirisha ..

No wonder Ally Kiba alipanda ukuta baada ya kuona hali ya sintofahamu ...na alikwepa kushiriki project ya Lekadutigite..mdogo wake akajifanya mbishi kwenda Kigoma Kuperform alichokipata ntawaleteeni uzi spesheli...

'HAKUNA MASKINI JEURI.. Na Ukiwa Maskini Jeuri Utakuwa Maskini Milele' Zamaradi Afunguka

$
0
0

HUTAKIWI KUWA NA HASIRA KATIKA PROCESS ZA KUTAFUTA MAISHA.... utakutana na changamoto nyingi sana na lazima ukubali.. kubali kudharauliwa, kubali kushushwa kubali kuonekana huna maana lakini lengo ni ufikie pale ambapo siku moja kila mtu atakuheshimu..

Lakini ukianza kuchukulia kila kitu personal, kuwa na vinyongo na watu na kukataa dharau za huku chini trust me HUTOFIKA POPOTE.. Ukitaka kuvimba kabla hujafika utachelewa.. wenye mivimbo wengi hawajafika mbali kwenye maisha.. kumbuka tu BOSS HANUNIWI!!! Huu msemo una maana kubwa sana pamoja na kwamba kila mtu anautafsiri kivyake.. lakini ni sawa na kusema tumikia kafiri upate mradi wako.. unachokihitaji wewe unakijua..

DHARAU zake ama chochote chake fanya kama hazikushughulishi.. maisha ni safari ndefu na hakuna aliewahi kuahidi kwamba itakuwa ni safari rahisi.. kubali vikwazo kama sehemu ya safari.. na wengi waliojishusha katika kutafuta tumeona matunda yao asikudanganye mtu HAKUNA MASKINI JEURI.. Na ukiwa maskini jeuri utakuwa maskini milele... ndivyo ilivyo na SI kwamba ni kitu kizuri ama kinasapotiwa.. la hasha!! Ila ndivyo maisha yalivyo.. wanasema LIFE IS NOT FAIR!!

 Haikugharimu kuwa mpumbavu pale ambapo unaona kuna faida na wewe.. unachotakiwa kujua 'KUJIFANYA MPUMBAVU mbele ya mtu ANAEJIONA MWEREVU ni kumfanya YEYE mpumbavu bila kujua...' kumbuka tu usije ukatumia hii vibaya ukajikuta umekuwa MPAMBE badala ya mtu anaetaka kutimiza ndoto zake - Zamaradi.

Picha za Show Nzima ya Yamoto Band Iliyofanyika Huko London Katika Ukumbi wa Royal Regency

$
0
0
Vijana wa Yamoto Band jumamosi iliyopita Walipiga Bonge moja la Show huko UK London katika Ukumbi wa Royal Regency na kuhudhuliwa na watu kibao wanaoishi huko, Hizi ni picha za matukio katika Show Hiyo.








Mbuta Nanga nae Alikuwepo.....


Lemutuz Atoa Somo 'Mwanamke wa Maana Tunamjua kwa Kuwangalia Marafiki Zake wa karibu Kwanza'

$
0
0
Lemutuz Ametiririka Haya Maneno Kwenye ukurasa wake wa Instagram , nimeona sio vibaya kushare na ninyi hapa.....Kwa sababu kuna ujumbe hapa...hasa kwa watu fulani hapa mjini:

'Mfano wa kuigwa kuwa mapenzi hayana macho! Mapenzi hayana Umri na Mapenzi ni Mapenzi tu hayalazimishwi na wala hayana vita wala ugomvi.....Mapenzi ni Natural thing ukilazimisha tu ukaingiza Unnatural basi unaharibu....Mapenzi yanatakiwa kuwa Mapenzi tu sio mara washabiki mara wapambe mara team pwanya road hayo sio mapenzi...na kukosea sio kosa ila kurudia kosa.....people kuna somo hapa la kujifunza kuhusu LOVE ukiwa kwenye mapenzi lazima uwe mtulivu uwe na subra na uwe mstaarabu na utulie....badala ya kupanda Mahindi na kutegemea kuvuna gademu Mihogo sheria ya maisha ni moja tu TUNAVUNA TULICHOPANDA.......I mean mwanamke wa maana tunamjua kwa kuwangalia marafiki zake wa karibu kwanza....I mean marafiki zako wote malaya hapa mjini na wengine malaya wanajiuza India hakuna hata mmoja mwenye serious relationship au ndoa si tunaruka ndege wa rangi moja! UKIPATA AJALI MAANA YAKE ULIKUWA UNAENDESHA KWA KASI SANA NA ULIKUWA HUJAWAHI KUPATA AJALI SASA UMEPATA AJALI JIFUNZE UBADILIKE WACHANA NA WAPAMBE MBURULAZZZZ'
 hahahaha U know This is Le Mutuz The King of All Bongo Social Media Network kuna mwenye gademu tatizo huko? HAHAHAHAHA U KNOW! - le Mutuz

Haya Je Hapo Jiwe la Gizani Limemlenga Nani?

Chege akanusha kuvaa hirizi kwenye picha iliyozagaa mtandaoni

$
0
0

Chege Chigunda amekanusha vikali tuhuma zilizotokana na kusambaa kwa picha akiwa jukwaani na huku mkononi mwake (karibuni na kwapa) akiwa na kitambaa cheusi ambacho baadhi ya watu wanahisi ni hirizi.

Mtu wa kwanza kuikuza picha hiyo na kuandika kuwa ana mashaka kuwa kitambaa hicho huenda kikawa hirizi, ni Maimartha Jesse.

“Angalia mkono wa kushoto wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ? any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata ukiniroga saw a Tu…japo cna imani hiyoo,” aliandika mtangazaji huyo wa zamani wa EATV.

Kauli hiyo ya Maimartha ilimfanya Chege kuamua kutoa ufafanuzi.

Ushamba+roho mbaya+uandishi bila kusomea ni hatari sana hahaaahahahahahhaa eti waandishi magumashi wanadai nimevaa hirizi hahahhaaaaa hii tulivaa juzi Dodoma siku ambayo alifariki msanii mwenzetu marehemu mez b,msiwe vimbele mbele @maimarthawajesse @waandishimagumashi,” aliandika Chege.

Picha: Vanessa Mdee na Jux wadhihirisha mahaba mazito Afrika Kusini

$
0
0

Vanessa Mdee na Jux wote wapo nchini Afrika Kusini walikoenda kufanya video ambayo hata hivyo hawajasema ni ya wimbo gani na kwa mujibu wa picha wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wanapeana kampani ya nguvu.

Hawajawahi kukubali hadharani kuwa ni wapenzi lakini picha zinaonesha wazi kuwa mastaa hao wapo kwenye dimbwi zito la mapenzi.

Kupromote wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’, Jux amepost picha akiwa na hitmaker huyo wa ‘Hawajui’ anayeonekana ‘akimchumu’ kwenye paji la uso.

Kabla ya picha hiyo, Jux alipost nyingine kadhaa akiwa na mrembo huyo katika pozi ambalo huwezi kuuliza kama ni marafiki tu.!

Hivi karibuni Vanessa Mdee aliiambia Bongo5 kuhusu uhusiano wake na Jux: I actually I like to keep my private life private. Nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji majibu.”

Jux na Vanessa wameongozana na Weusi na Navy Kenzo kwenye safari hiyo ya South.

JB, Mzee Majuto na Richie Wamtembelea Mama wa Mtoto Albino Aliyeuawa…Wamwaga Machozi

$
0
0

Wikiendi iliyopita staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na mastaa wenzake, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike ‘Richie’ walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.

Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo aliyetekwa mjini Geita hivi karibuni.

Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.

JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.

Mzee Majuto: Inasikitisha sana. Haivumiliki. Albino ni wenzetu na wana uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa letu. Wahusila lazima wakamatwe na tuone wakichukuliwa hatua kali.
Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.

Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio kwa uchungu.

Tayari mtoto Bahati amezikwa baada ya mwili wake kupatikana ukiwa hauna baadhi ya viungo huku mama yake akiendelea na matibabu baada ya kufanyiwa oparesheni sehemu ya kichwani aliyojeruhiwa vibaya wakati akinyang’anywa mwanaye.

Tunampa pole sana mama Yohana Bahati, watanzania tuungane kupinga ukatili huu.

GPL

Faiza: Kuwa Mama Poa Sana, Natamani Nizae Team ya Mpira!!

$
0
0

Mwigizaji wa filamu mwenye vituko vya aina yake, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto moja, aliezaa na Mbunge wasasa wa Mbeya mjini, ameyasema hayo  akiwa visiwani Zanzibar kwenye mapumziko mafupi.

Mwigizaji huyu ambae mara kabdhaa amekuwa akijisifia kwa kuwa na FIGA nzuri akidai hata baada ya kuzaa bado umbo na mvuto wake bado upo pale pale amesema angekuwa na uwezo wa kipesa  angezaa watoto wengi zaidi kiasi cha kufikisha idadi ya wachezaji wa timu ya mpira kwa sababu kuwa mama ni kitu kizuri sana kwake.

Kuwa mama ni kazi poa sana- naipenda sana yaani ningekua na uwezo wa kipesa ningezaa team ya mpira

Mbali na watu kuendelea kumshambulia kuhusu uvaaji wa nguo zake akiwa na mtoto wake mwananamama huyu ameonekana ni mtu mwenye kufanya kile anachokiamni  na sio watu wanataka nini.

Jionee baadhi ya picha hapo juu akiwa na mtoto wake ufukweni.

Picha: Studio binafsi ya Millard Ayo yashtua wengi

$
0
0

Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo na mshindi wa vipengele viwili kwenye Tuzo za Watu mwaka jana ni mtu wa mambo ya kimya kimya ndio maana picha ya studio aliyokuwa akiijenga nyumbaji kwake kwa mwaka mzima zimewashtua wengi.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha Amplifaya anakuwa mtangazaji wa kwanza Afrika Mashariki kama si Afrika nzima kuwa na studio ya kisasa ya redio ndani mwake.

Hajasema kwanini ameamua kufanya hivyo lakini amedai hiyo ilikuwa ni ndoto yake ya miaka mingi.

“Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja kumiliki studio yangu ya radio kutokana na jasho langu na leo namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini hii na baadaye watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA,” ameandika kwenye Instagram.

“Thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa.”

Hizi ni baadhi tu ya comments za followers wake kwenye Instagram:

1. Role model wa vijana weng TZ….plz usituangushe kwa hil for sure unastahik pongez sna kwa hil daaaah…safi sna @millardayo

2. Big up Millard upo clouds hata miaka miwili haijafika ushafanya mambo makubwa hivyo kuna wenzio wako karibia miaka kumi sasa hawana hata MIC

3. Kiukweli Millard huwa unanipa nguvu ya kusonga mbele na kuamini kuwa kila kitu kinawezekekana.am student nasomea masscommunication napata shida sana na kukata tama pale ambapo nanyimwa field nakudharaulika juu bt.name amini one day ntafika mbali zaidi na hawa wanaonidharau wataniheshimu nikutakie kila la kheri na hongera sana kaka angu kwa hatua hiyo.all the best@millardayo

4. U have totally inspired me to save more fo wat i want to accomplish before july

5. OMG I didn’t see this, @samchom thanks for the tag. Congrats Mill wange! I’m so proud of u! Hard work pays always! Hongeraa sana Mtu wangu wa nguvu @millardayo @mrs_mario30

Tunampongeza Millard kwa hatua hiyo.

Vurugu Ilula Mkoani Iringa, Mwananchi afariki, Kituo cha Polisi chachomwa moto!

$
0
0
Wananchi wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa,  wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo  kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake wakati anakimbia alichotwa mtama na Polisi na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo .
 
Mama huyo alikuwa anawakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita,  hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
 
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.


Picha CHAFU za Msanii Maarufu Uganda Zavuja Mtandaoni Akiwa kama Alivyozaliwa

$
0
0
Picha  chafu  za  Msanii  maarufu  wa  kike  nchini  Uganda  zimevuja  na  kusambaa  kwa  kasi  mtandaoni.....

Picha  hizo  Ambazo  zilianza  kusambaa  jana  zinamuonyesha  msanii  huyo  akiwa  kitandani  na  njemba  moja  huku  akiwa  mtupu  kama  alivyozaliwa.....

Picha  nyingine  zinamuanika  akiwa  mtu  na  wasichana  wenzie  kitandani.....

<< Kuona  Uchafu  wa  Msanii  huyo  BOFYA  HAPA>>

Iyobo Ashikwa na Kigugumizi Kuhusu Mume wa Aunt Ezekiel

$
0
0
Mcheza Dansi wa mwanamziki  Diamond, Mose Iyobo ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameshikwa na kigugumizi kuhusu tuhuma za kumpachika mimba Aunt ambaye ni mke wa mtu.

Mose alionesha kigugumizi hicho baada ya kutaitiwa na paparazi wa GPL akiulizwa anajisikiaje kumpachika mimba mke wa mtu na vipi kama mume wa Aunt anayedaiwa kufungwa huko Dubai ataachiwa huru na kurudi.“Aaahhaa.. Mhh..Hayoo ni ya Aunt mwenyewe mimi hayanihusu,” alisema Mose kisha kimya kirefu kikafuatia kabla ya kuikata simu yake.

MANAIKI: Bado Sijakata Tamaa Kumuoa Jack Wolper

$
0
0
Mwigizaji wa filamu mwenye mikasa ya aina yake, Manaiki Sanga  ‘The Don’ amesema kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Wolper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.

Akiongea na Gazeti la Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.

“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema Manaiki.

Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.

Joyce Kiria Adaiwa Milioni 500 kama Fidia ya Kumdhalilisha Mbunge Kupitia Kipindi cha Wanawake Live

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake.

Akiongea na Mwandishi wetu, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.

"Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .

Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alipelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.

Wana CCM Serengeti watua kwa Edward Lowassa.....Wamtaka Achukue Fomu ya Kugombea Urais

$
0
0
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamemwomba Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), kuchukua fomu ya kuwania urais muda utakapofika kwani wanaamini ni kiongozi anayefaa kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Vicent Nyamasagi, viongozi hao walitoa kauli hiyo jana Monduli baada ya kufika nyumbani kwa Lowassa kuwasilisha ombi hilo.

Lakini pamoja na viongozi hao kuwasilisha ombi hilo, Lowassa hakutoa jibu la kukubali wala kukataa na badala yake alirejea kauli yake kwa kusema kuwa suala hilo ni kubwa, linahitaji maombi na baraka za Mwenyezi Mungu.

“Historia yako inaonyesha ni mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, mapana na sahihi kwa masilahi ya nchi yetu.

“Kwa hakika una sifa zote za kuwa rais wa nchi yetu, tunakuomba muda ukifika chukua fomu, wananchi wana imani kubwa na wewe,” alisema Nyamasagi.

Aliongeza kuwa Watanzania wameshuhudia uwezo mkubwa wa Lowassa katika nafasi zote alizowahi kushika na ndiyo maana jina lake sasa ni tumaini pekee la wananchi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) wa Wilaya ya Serengeti, Patric Marwa, alisema hakuna kiongozi yeyote ndani ya CCM anayefanana na Lowassa kuweza kushika nafasi hiyo.

“Hakuna kiongozi mbadala wa Lowassa kwa sasa, anajua historia ya chama chetu na nchi, katika maisha yake yote ya utumishi amekitumikia chama kwa uadilifu mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, John Ng’oina, alisema wana imani na Lowassa na kuwa atasikia kilio cha Watanzania kumtaka achukue fomu kuwania urais.

Hatua hiyo ya viongozi hao imekuja kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Februari Mosi mwaka huu ya kutaka wana CCM wenye uwezo washawishiwe wachukue fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi ndani ya CCM.

Vifurushi vipya vya mitandao: TCRA yatoa tamko na maagizo kwa makampuni ya simu

$
0
0
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA imetoa tamko kuhusiana na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za simu nchini kufuatia kubadilika kwa vifurushi vya mawasiliano.

Malalamiko hayo yalikuja baada ya baadhi ya mitandao ya simu kupunguza ukubwa wa data anazopata mtumiaji wa simu anapojiunga na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na data kwa pamoja.

Baadhi ya mitandao imekuwa ikitoa Mega Bytes 8 peke yake ambazo kwa matumizi ya kawaida ni ndogo mno.

“TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamebadilisha bei, kwa ujumla bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana.

 "Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za data (MBs),” amesema Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne.

Kupitia kifungu cha 5 cha Kanuni za tozo (EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011, TCRA imeyataka makampuni ya simu kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza wateja wao kabla hazijaanza kutumika.

 Pia imeyataka kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo.

“TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sio ya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko,” imesema.

“TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja wao nafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji: Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au mwezi ambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho wako tayari kulipia kwa mazungumzo, meseji na intaneti.”

“TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi yao.

"Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma.

"Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe malalamiko yake TCRA,” imesisitiza.

“Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huria la mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi chochote au huduma yoyote.

"Watumiaji wa simu janja zinazowezesha matumizi ya huduma nyingi, maarufu kama “smart phone”, kuwa makini wakati wa kuzitumia. Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia data hata kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenye vifurushi.”

Katika hatua nyingine taarifa hiyo imetoa takwimu ya kuongezeka kwa matumizi ya simu na internet nchini katika kipindi cha miaka 10.

Imesema hadi sasa kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005.

“Idadi ya simu za mezani ni 151, ukilinganisha na 154, 420 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008.
 
"Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii,” imesema.

“Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza imeongezeka kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadi milioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014.

"Hii imewezesha huduma za simu kufikia asilimia 97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005.
 
"Kwa upande mwingine, muda wa kuzungumza kwa simu, ukiwa umepimwa kwa dakika zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji. Umefikia dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005,” imeongeza mamlaka hiyo.

“Matumizi kwa upande wa meseji, yaani SMS na data pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka 2014. Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10.”

PICHA: Joti Awakuna Wengi Kwa Mtoko Huu

$
0
0
Picha ya mwigizaji mkongwe wa vichekesho “KOMEDI” Lucas Mhuvile ‘Joti’  imewakuna watu wengi  na kufanya kuwa ni moja kati ya picha zinazo” TREND” mtandaoni toka jana.

Japo kuwa Joti akiwa kama ‘Bi kiboga’ ametokelezea kiofisi zaidi, watu wengi wamejituka wakiangusha komenti nyingi wakielezea kuvunjika kwa mbavu zao kwa kicheko huku wengine wakisema mnuno wake ndio balaa na wengine wakisema skuna ndio sheedah ilimradi kila mmoja kafurahi kwa mtindo wake.

Kiukweli kabisa kijana huyu ni moja kati ya wakali wa KOMEDI pengine sio hapa bongo tu  bali hata Afrika na Dunia .

 “Kwanini lakini!!!!!?????? @jotimdebwedo ..Angalau umefanya siku yangu iwe nzuri kidogo leo... ila sio kwa skuna hizo!!!! … kwa kumuangalia tu anapendezea kufanya kazi wapi!? amefanania na ofisi gani!!???? “- Zamaradi Mtetema aliandika haya mara baada ya kuiona hii.

Mzee wa Ubuyu

Shilole na Mchumba Wake Nuh Mziwanda Wachafua Hali ya Hewa Mtandaoni!

$
0
0
Mwigizaji na mwanamziki,  Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambae ni mama wa watoto wawili wa kike , akiwa na mchumba wake Nuh wamechafua hali ya hewa baada ya kutupia picha yao inayowaonyesha wakiwa watupu.

Nuh Mziwanda ndio alioibandika picha hiyo kwenye ukursa wake kwenye mtandao wa instagram na baada ya kuona wengi wanamshabulia aliamua kuibandua. Kwa kiufupi picha hii haina maadili na ukizingatia mwanadada Shilole ni mama na sijui watoto wake watajifunza nini hapa.

Wapo walioona kuwa kitendo hiki alichokifanya Mziwanda labda ni kutokana na umri wake hivyo hayo ni baadhi ya matokeo ya kuwa na mahusiano  na mtu mtoto mdogo  na kuona Mziwanda hana kosa hapa. Lakini pia wapo walioona kuwa wawili hawa wanatafuta KIKI tu ili media za hapa Bongo ziwazungumzie kama Zari na Diamond, ila pia wapo amabo wanaona hii ipo poa  na haina tatizo.

Nadhani kitendo cha Mziwanda kubandua picha hii ni kutokana na akili yake ku-CLICK kuwa amekosea, nampongeza kwa hilo na naamini atakuwa amejifunza kitu.

Nia na madhumuni ya kuileta hapa ni kutaka watu watambue kuwa mtandao ni zaidi ya tunavyofikilia kwani kosa la sekunde moja mtandaoni linaweza kukuhalibia maisha yako yote..Siku nyingine naamni watakuwa makini.

Mzee wa Ubuyu
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images