Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live

Meneja wa zamani wa Diamond aeleza kwanini msanii huyo anazidi kufanikiwa

$
0
0
Papa Misifa ( wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Cassim Mganga
Meneja wa zamani wa Diamond Platnumz, Msafiri Misifa maarufu kama Papa Misifa, amesema wasanii wengi wanashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kuhifadhi wanachokipata.

Kassim Mganga na mdau wa muziki
Papa Misifa ( wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Cassim Mganga

Papa Misifa aliyewahi pia kuwa meneja wa Dully Sykes na Cassim Mganga, ameiambia Bongo5 kuwa Diamond ni msanii pekee aliyeweza kufuata mafunzo yake na ndio maana anaendelea kufanikiwa mpaka sasa.

“Tatizo kubwa wasanii sana wanapopata riziki wanashindwa kujipangilia. Na mafunzo mengi niliyompa Diamond ndo maana mpaka leo anajua kujipangilia mpaka pale alipofika. Wasanii wanashindwa kupangilia pesa zao. Tatizo wanapopata pesa wanabadilika. Ukitaka kujua tabia ya mwanadamu ngoja apate pesa ndo utajua tabia yake,” amesisitiza.

“Wasanii wengi hawalengi kufanya vitu vya maendeleo, wanalenga kufanya starehe kwenye baa. Ndio maana watu wanasema wanamuziki wa zamani wamefulia ni kweli kwa sababu hawakujipanga. Hawakutambua kesho yao, wewe unafikiri kwanini Diamond anaiogopa kesho yake? Ni kutokana na maisha yalivyo ukipata nafasi itumie ipasavyo.”

Picha: Crazy GK aingia studio na Vanessa Mdee kuandaa ngoma mpya

$
0
0
Msanii wa East Coast Team, King Crazy GK ameingia studio kurekodi ngoma mpya na Vanessa Mdee.

Kazi hiyo mpya inayoandaliwa na mtayarishaji mkongwe, John Mahundi akishirikana Marco Chali, inasimamiwa na AY.

“Yeah mzigo upo jikoni na soon utausikia maskioni,” GK ameiambia Bongo5. “Sidhani kama itaathiri kutoka kwa kazi za East Coast ila inawezekana kwasababu huwezi kuachia kazi mbili kwa pamoja, lazima moja ianze kwanza na nyingine ifuate,” ameongeza.

“Beat kila kitu kimeandaliwa na John Mahundi na Vanessa ndo anaingiza vocals kwa Marco Chali. Kiukweli hii kazi imesimamiwa kila kitu na AY na baada ya hapo hii project itatoka.”

GK amesema anamshirikisha Vanessa kwakuwa ni muimbaji wa kike anayemkubali zaidi.

“Unajua Vanessa ni hatari sana kwenye muziki, ana uwezo mzuri sana ndio maana ukamuona kwenye hii project yetu.”

Diamond Apondwa Kusafiri na Kundi Kubwa la Watu Kwenye Show ama Safari zake za Kustarehe

$
0
0
Blogger Mmoja Maarufu Amemshukia na Kumshauri Diamond Kuhusu Kusafiri na Kundi kubwa la watu wasiokuwa na Ulazima Pale anapoenda kufanya show ama kustarehe ..

Ameandika hivi :

"Anyways,wewe kama mtanzania unaonaje hizi swagga mpya za Diamona kusafiri au kufatwa nyuma na kundi la watu wakiwemo mameneja wake, ndugu,mpiga picha, etc….
Kwa maoni yangu naona kama mameneja wake wanampoteza tu. Itakuwa kaambiwa akitaka kuonekana ni big star basi lazma awe anafatwa nyuma na kundi la watu everywhere he goes.,,,,,
Nimemuelewa kidogo sababu labda kaona mastaa wakubwa wakubwa duniani huwa wanakuwaga na entourage kubwa ya watu ila jamani they can afford kuwa na watu wote wale… Some of them make over 10million dollars a year sasa kulipa watu wote hao kumfata fata ni pocket change kwake. Tayari wana utajiri ambao hata wajukuu zao watakuja kuukuta ,wana majumba in every city wengine mpaka Palm Jumeirah Dubai wana mavacation home sasa huyu kijana wetu ambae mpaka leo bado anaishi kwenye nyumba ya kupanga kwanini analipa watu kumfata fata nyuma hivi? wakati it’s very unnecessary"

Je wewe unaonaje kuhusu Hili Swala?

Wastara Azimia Kisa Penzi la Bond

$
0
0
Diva wa filamu nchini, Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.

“Tunakushangaa unavyojinadi kuwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya bethidei wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni. Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza, ni wa nne,” kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.

Chanzo hicho kifunguka kuwa, baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu, alizimia ghafla na kulazwa hospitali.“Wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo, nasikia walimkimbiza hospitali, akapewa huduma nasikia kidogo sasa hajambo. Ishu ilikuwa mbaya, Aunty Lulu alimmchana laivu.”

Risasi  lilimtafuta Aunty Lulu ambaye hapo awali alikuwa akilalamikia penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikia mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.

“Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa Bond.
 
“Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito, kwani nilichoka, kama amepata presha na kulazwa hilo mimi silijui,” alisema Aunty Lulu.

Kwa upande wake, Wastara naye alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hospitalini, lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya kusikia taarifa hizo, bali kutokana na kuzidiwa na malaria.

“Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali, nilikuwa nimepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10, kwa muda wa wiki mbili nilikuwa naumwa, lakini nikazidiwa kidogo, hivi sasa niko sawa na hapa ndiyo nashuka uwanja wa ndege natokea Mwanza,” alisema.

Mwanahabari wetu alipombana zaidi Wastara kutaka kujua kuzimia kwake kama kulitokana na kupata habari za Bond kuwa na watoto wanne, alisema siyo kweli kwani asingeweza kushangazwa na jambo hilo hasa kwa vile Bond ni mwanaume lijali na pia ana maisha yake ambayo hayamhusu.

“Mimi nina maisha yangu, yeye ana maisha yake, sasa jamani mimi nitapatwaje na presha kwa mambo hayo? Labda nikuambie tu kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yangu na yeye zaidi ya masuala ya kikazi tu. Ninaomba uelewe hivyo kwa sababu huo ndiyo ukweli,” alisema.

Msanii wa Bongo Movies Aibuka na Kudai Ana Mimba ya Marehemu MEZ B

$
0
0
MSANII wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali’ amefunguka kuwa kifo cha staa wa Bongo Fleva, Moses Mshagama ‘Mez B’ ni pigo kubwa sana kwake kwani marehemu alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa na mimba yake.

Akizungumza na gazeti hili huku akionesha sura ya masikitiko, Queen Magali alisema kinachomuuma zaidi ni kwamba, ujauzito wa marehemu aliokuwa nao, ulichoropoka saa chache baada ya kupokea taarifa za msiba huo.

“Nilipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, sikuamini, hata ndugu zake marehemu walinipigia simu, sikuamini hadi nilipompigia shangazi yake ambaye alinithibitishia msiba huo, hapohapo nikapata mshutuko, hali yangu ikawa mbaya hadi nikalazwa.

“Nashukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri.
“Kiukweli msiba huu kwangu umekuwa ni pigo kubwa, tulikuwa na mipango mingi na marehemu katika maisha yetu, alishanitambulisha kwa ndugu na jamaa zake wote wa karibu lakini nasikitika zaidi kwa kuwa nimechelewa kuhudhuria mazishi ya mpenzi wangu kutokana na kuzidiwa ghafla lakini nitafanya kila liwezekanalo ili nikaweke japo mchanga kwenye kaburi la mtu niliyempenda katika maisha yangu,” alisema Queen Magali.

Baadhi ya wapenda ‘ubuyu’ waliokuwa wakisikiliza mahojiano ya Queen Magali na mwanahabari wetu, walisikika wakihoji kwa nini mrembo huyo asianike uhusiano wake na Mez B kabla hajafariki lakini mwenyewe alidai walikubaliana uchumba wao uwe wa siri.
Mez B alifariki dunia nyumbani kwao Dodoma Ijumaa iliyopita ambapo alizikwa katika makaburi ya Wahanga wa Reli, Dodoma.

Demu Kutoka Kenya TIARA Anayemtaka Kimapenzi Diamond Aingizwa Mkenge na Diamond Platnumz

$
0
0
Socialite and Singer Tiara 
Demu wa Kenya Anayejulikana kama TIARA ambae alishindwa kuficha hisia zake na kumtumia Video na Picha za mitego Diamond kwa Kupitia Udaku Special Blog Ametuhabarisha kuwa baada ya Video na picha zake kusambaa alitafutwa na  Diamond Platnumz na kuanza kuchat nae na kutumiana picha mbali mbali  na alifikia mahala akasema anamtumia Ticket za kuja Dar wafanye yao pamoja na Collabo ya Mziki ..Lakini mpaka leo Tickets hazijatumwa....Sasa baada ya tickets kutokutumwa na Diamond kukaa kimya ilibidi aanza kufanya uchunguzi kuhusu huyo Diamond na Mwisho kugundua anachat na Diamond Fake...anatumia jina la Diamond..kwenye facebook anajiita : Diamond Wasafi Platnumzz

Hizo Hapo Juu ni Baadhi ya Messeji walizokuwa wanachat kabla ya kugundua sio Diamond wa Ukweli .....

TIARA amesema Bado Hajakata Tamaa na Anasema Diamond Kama Anasoma habari hii Soon atakuja Tanzania yeye mwenyewe kukutafuta Face to Face mpaka kieleweke....

Katika Hatua nyingine TIARA amesema Mwezi ujao ataachia Single yake mpya itakayoitwa Kuparty........

Unamshauri nini TIARA?

Pole Chris Brown mwenzako nilichekwa-Ommy Dimpoz

$
0
0
Msanii Omary Nyembo alimaarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa watu wa uhamiaji duniani kote huwa hawatambui umaarufu wa mtu pindi wanapogundua kuna kitu hakijaenda sawa,Ommy Dimpoz amefunguka hayo leo kapitia ukurasa wake wa

Intrgram baada ya mwimbaji kutoka Marekani Chris Brown kuzuiliwa kuingia Canada na kusababisha kusitishwa kwa show zake mbili ambazo alitakiwa kuzifanya Canada ndani ya wiki hii.
Ommy Dimpoz ameonyesha njisi gani watanzania na mashabiki wake walilipokelea suala lake tofauti na kuonyesha kuwa watu wengi walimcheka na kumchamba wakiamini kuwa yeye ni mtu maarufu hivyo asingeweza kupatwa na suala hilo.
"Pole braza Kristofa, haya ni Mambo ya kawaida ila Mwenzio nilivyozuiwa kuingia Nchini kwenu Basi nilivyorudi kwetu nimechekwaaa,Nimechambwaa khaa,hawajuagi mambo ya Uhamiaji hawajali we nani."
Wiki ya wapendanao msanii Ommy Dimpoz alirudishwa Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa kukosa vibali vinavyomruhusu kuingia nchi hiyo kufanya show

Shilole Ataja Chanzo cha Migogoro na Nuh Mziwanda

$
0
0
Mwanamziki na mwigizaji wa filamu za Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, ameamua kuweka wazi chanzo cha migogoro yake na mumewe mtarajiwa, Nuh Mziwanda kuwa ni marafiki.

Shilole alidai kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana, lakini chanzo kikiwa ni maneno ya uchonganishi kutoka kwa marafiki zao wa karibu ambao wana lengo la kuwatenganisha.
Mwanadada huyo alidai kutokana na hali hiyo, hivi sasa ameamua kutowahusisha suala lolote linalohusu maisha yake ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara baina yao.

Alisema wale walio karibu yao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yao, ukizingatia hivi sasa wapo kwenye harakati za kufunga ndoa baada ya wazazi wa pande zote kukubali uhusiano wao.

“Tumegundua kuwa mashoga ndio wanaotugombanisha, kwani kila mara mchumba wangu anapewa taarifa zinazonihusu mimi huku hao hao wakiniletea habari zake, jambo hili limesabababisha nisihitaji tena marafiki wengi wao ni wanafiki,”alisema

NDOA ya staa wa filamu nchini, Salim Omary ‘Slim’ na mkewe Asia Morgan imevunjwa rasmi

$
0
0
NDOA ya staa wa filamu nchini, Salim Omary ‘Slim’ na mkewe Asia Morgan imevunjwa rasmi na Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni jijini Dar kufuatia mgogoro wa muda mrefu. Hakimu aliamuru watalaka hao kugawana mali zote walizochuma pamoja likiwemo gari walilozawadiwa wakati wa harusi yao, ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha mgogoro huo.

Unahisi kwanini ndoa za vijana wengi wa sasa hazidumu. hakuna upendo wa kweli, tamaa zinasumbua au unahisi nini?

JB na Scandal Mpya Ndani ya Bongo Movies.....

$
0
0
Msanii anayefanya vizuri kunako bongo movie, Jacob Steven maarufu kama JB, hivi karibuni amekwaa scandal mpya ambayo imemshushia HESHIMA kama sio kumpunguzia credit ndani ya tasnia hiyo.

Msanii huyo maarufu amekumbwa na scandal hiyo baada ya muvi yake mpya kutoka inayofahamika kwa jina la MZEE WA SWAGA.

Muvi hiyo inayofanya vizuri sokoni inasadikiwa kukopiwa na ku paste kama ilivyo na moja ya movie maarufu kutoka bollywood inayofahamika kwa jina la "Ladies VS Ricky Bahl".

Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na JB, Kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya "mzee wa swaga" imeiga kama ilivyo kuanzia story hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.

Mtangazaji huyo amelaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya JB huku akijifanya yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa story hiyo wakati ukweli anaujua mwenyewe.

Kama uko above 30 huna mke/mume wala mtoto we ni masikini tu

$
0
0
Niliwahi kuwa na mwanazuoni mmoja wa dini fulani akasema kwenye dini yao utajiri hauishii kwenye mali bali familia kwa maana ya mke na mume na watoto. Mtu anapomisi kitu kimoja wapo hapo uhesabika kuwa ni masikini tu hata kama ameacha mali kiasi gani.

Miaka hiii ya karibuni kuna watu maarufu hususani wasanii wanakufa wakiwa above 30 hawana mchumba ,mke,mtoto,hata nyumba hawana hao ni zaidi ya masikini tunatakiwa kuwaweka kundi la kapuku,usikubali kufa kapuku wanaume tuoe na wanawake muolewe acheni kuchaguachagua kama mnachagua nazi gengeni.

Filamu za Kibongo za Zidi Kupasua Anga za Kimataifa! Soma Hii

$
0
0

Filamu za kitanzania maarufu kama Bongo Movies zimezidi kuvuka mipaka na kupata fursa ya kuonekana zaidi duniani.Hii ni kutokan na hiki ambacho blogger maarufu  Jestina George  mtanzania aneishi ughaibuni kushea nasi kile alichokutana nacho akiwa ndani ya ndege.

"I was very happy hivi karibuni wakati nasafiri ndani ya Emirates kukutana na hii .BongoMovie ..MkeMchafu humo ndani ninaemjua ni Johari Chagula pekee yake . but lengo lakuleta hapa ni kuwapongeza sana maana ni hatua nzuri and I hope tutaendelea kukutana na movie zingine pamoja na miziki yetu pia kwenye mashirika mengine ya ndege.. Kwani waowaweze sie tushindwe tuna nini"-  Jestina wa Jestina-george.com aliandika  mtandaoni  na kuwa tag baadhi ya wasanii wa bongo movies.

Hizi ni dalili nzuri, wasanii endeleni kukaza buti,wadau tuendelee kuwasapoti kwa kupenda vya kwetu.

Maimartha Amweka Kiti Moto Aunty Lulu kuhusu Kulala Gesti na Kutoka na Wanaume Wasio na Maana Mjini

$
0
0

MTANGAZAJI maarufu wa Runinga, Maimartha Jesse hivi karibuni aliamua kumtolea uvivu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kwa kumpa kitchen party ya nguvu.

Akichonga na Centre Spread, Mai alisema kuwa anachoumia ni kwamba kila mtu mjini hapa anamsema Lulu vibaya wakati yeye alikuwa ni rafiki yake wa karibu.

“Kama atalia na alie, kama atacheka na acheke lakini nimeshachoka na mambo yake kwa sababu yeye ni umiza kichwa, anasumbua vichwa vya watu kwa matendo yake,” alisema Mai.

Aidha, Mai alisema anamsema Lulu kama mdogo wake na mtu aliyemfanya akapata jina mjini hapa kuwa aache tabia ya kulalala gesti na  kuwa karibu na wanaume wasio riziki.

Baada ya Kutemwa na Ray, Johari Atoa Sifa za Mwanaume Amtakae Kwa Sasa...

$
0
0
Blandina Chagula ‘Johari’
STAA wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ ameamua kuvunja ukimya wa muda mrefu baada ya kuweka wazi mwanaume ambaye anahitaji amuoe na sababu inayomfanya asijichanganye na mastaa wenzake.

Katika makala haya Johari amefunguka mengi, msome;

 Mwandishi: Kwa nini mara nyingi hupendi kujichanganya na mastaa wenzako?

Johari: Ujue nina kampuni ambayo wakati wote nahitajika kuwepo hapo, na kama kujumuika, najumuika na wenzangu pale pa muhimu kama kwenye misiba.

 Mwandishi: Tangu umeingia katika tasnia ya filamu kuna mastaa ambao mara nyingi wanawaweka wazi wapenzi wao lakini wewe haijatokea ni kwa nini?

Johari: Unajua kwa sasa ni kama dada wa mastaa, kitendo cha kuwaweka wazi wapenzi, wengi wanakuwa akili zao hazijakomaa, lakini najitambua na ninaelewa akili za wanaume, unamtambulisha leo kesho kakukimbia utakuwa unatambulisha wangapi?

Mwandishi: Mbona kuna tetesi kuwa Ray alikuwa anakukataza kumtaja hovyo wakati wengi wanajua ndiye mpenzi wako?
Ray na Johari Enzi za Mapenzi yao 

Johari: Sipendi kuzungumzia chochote kuhusu Ray kwa sababu kila mtu ana maisha yake na kwa nini anikataze?

Mwandishi: Kuna wanaume wengi huko nje wanapenda kukuposa lakini wanaogopa wakijua kuwa mastaa hawawezi kuposwa na watu wa kawaida, unalizungumziaje hilo?

Johari: Hapana! Kwanza kwa upande wangu nahitaji kuolewa na mwanaume wa kawaida ambaye anaweza kunijali na kujua thamani yangu na siyo wa kujibweteka, ajue kuchakarika na wala sichagui, maelewano tu.

Mwandishi: Mastaa wengi hawafanyi kazi mara nyingi wanategemea filamu pekee ambazo haziwasaidii, unalizungumziaje hilo?

Johari: Hilo hata mimi linaniumiza sana kwa kuwa mastaa wengi wa kike hawajitumi, asilimia kubwa ni tegemezi kwa wanaume ila ninachoona ni bora kuridhika na moja ya kwako kuliko elfu moja ya wenzako.
Mwandishi:
Mwandishi: Mara nyingi huonekani katika kumbi za starehe, kwa nini?

Johari: Kikubwa ni kazi na kukosa muda, pia sipendi kujichanganya sehemu kama hizo.

Mwandishi: Mna bifu lolote na Chuchu Hans?

Johari: Mmmh! Sina, sipendi zaidi kuzungumzia hilo, samahani.

 Muda unazidi kusonga mbele na karibia mastaa wengi wana watoto, vipi wewe unangoja nini?

Johari: Sidhani kama kuna mtu ambaye hatamani kuwa na mtoto, kwa upande wangu lazima nitafute baba mwema nitakayemzalia.

Mwandishi: Haya asante Johari.

Johari: Karibu tena.

Ile picha ya askari wa Tanzania kupigana mabusu iliteka Dunia.....Hapa iko Picha mpya toka Uingereza

$
0
0
Unakumbuka ile Stori ya askari Asuma Mpaji na Veronica Nazaremo kufukuzwa kazi Mkoani Kagera baada ya picha zao kusambaa mitandaoni wakionekana kupigana mabusu? safari hii nakuletea tena stori inayofanana na hiyo ambayo imetokea Nchini Uingereza.
 
Polisi wa nchi hiyo ya Uingereza waliamua kumshtaki mwenzao baada ya kufanya kitendo cha kudhalilisha jeshi la nchi la nchi hiyo kwa kufanya tendo la ndoa tena mbele za watu akiwa na sare za kazi.

Kitendo hicho kimemfanya kufukuzwa kazi bila kupewa taarifa za awali haraka baada ya kwenda kwenye shughuli zake za kila siku za usalama na kufanya kitendo hicho huku akijua ni kinyume na sheria tena akiwa amezungukwa na watu.

Msaidizi mkuu wa kituo hicho Russ Middleton alisema wanaamini hatua hiyo itakua fundisho kwa wengine kutokana na kitendo hicho cha udhalilisha.

Kwa upande mwingine polisi mwingine nchini Uruguay naye alikumbwa na mkasa unaofanana na huo baada ya kucheza na mwanamke akiwa uchi katika kituo chake cha kazi.

Picha ya askari huyo zilinaswa na mitandano mbalimbali na kujikuta zikisambaa kwa kasi hali iliyosababisha ashtakiwe kwa kosa hilo.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Aua Mwanafunzi Mwenzake Darasani Wakati Wakigombania Daftari la Notes

$
0
0
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu, saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano katika Shule ya Msingi Ilola iliyopo katika Kata ya Ilola, Tarafa ya Itwangi, Wilaya ya Shinyanga.

Wamesema mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew (12).

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Andrew Chenge Agoma Kuhojiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma.....Adai kuna zuio la mahakama kuu, hatima yake kujulikana leo

$
0
0
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Mtemi Andrew Chenge, jana ameonyesha utemi wake mbele ya Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, baada ya kusema haiwezi kumjadili kwa sababu kuna kesi mahakamani.

Alisema kuna zuio la Mahakama Kuu ambalo limevitaka vyombo vyote vya Serikali kutojadili suala la miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa.

Tume hiyo inamtuhumu mbunge huyo kuwa alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alitumia madaraka yake vibaya katika uuzaji wa hisa za Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwenda Kampuni ya VIP Engineering Tanzania Limited.

Itakumbukwa wakati suala la Tegeta Escrow likijadiliwa bungeni, Chenge alidaiwa kupewa sh bilioni 16 na mmiliki wa VIP Engineering Tanzania Limited, James Rugemalira.

Jana, kabla ya Chenge kuieleza Tume ya Maadili kuwa haiwezi kumuhoji, Mwanasheria wa tume hiyo, Hassan Mayunga, alisoma mashtaka yanayomkabili.

“Mlalamikiwa akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mwaka 1995 aliishauri Serikali kuingia mkataba wa miaka 20 wa kuongeza uzalishaji wa umeme na Kampuni ya IPTL.

“Mlalamikiwa baada ya kustaafu wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Desemba 24, mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya VIP Engineering Tanzania Limited iliyokuwa na hisa asilimia 30 kwenye Kampuni ya IPTL.

“Kitendo cha kuingia mkataba na Kampuni ya VIP ni ukiukwaji wa kifungu cha 6(i) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma ambayo inamzuia kiongozi wa umma kujinufaisha katika utumishi wake uliopita kwa kutumia taarifa alizozipata wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake kwa masilahi binafsi,” alisema Mayunga.

Alisema kitendo cha mlalamikiwa kuendelea kuwa mshauri wa Kampuni ya VIP huku akiwa na wadhifa wa ubunge, ni ukiukwaji wa kifungu cha 6(e) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma ambayo inamzuia kiongozi wa umma kujiingiza katika mgogoro wa kimasilahi.

Mayunga alisema mkataba ambao mlalamikiwa aliingia na VIP, ulimpatia masilahi ya kifedha ya Sh bilioni 1.6 kinyume na kifungu cha 12(1)(e) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

“Mwaka 2014 mlalamikiwa aliingiziwa fedha kiasi cha Sh bilioni 1.6 na kampuni hiyo katika Benki ya Mkombozi wakati hakutamka mapema kama aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa Serikali na kwamba ana masilahi binafsi na kampuni hiyo wakati alikuwa akijua kuwa Shirika la Umeme (Tanesco) lina mgogoro na IPTL,” alisema. Chenge

Baada ya kusomewa mashtaka, Chenge aliyakana na kuomba mwongozo kwa madai kuwa suala hilo lina zuio la Mahakama Kuu, hivyo basi tume hiyo haiwezi kujadili suala hilo hadi kesi ya msingi itakapokwisha.

“Napata shida kujadili suala hili, mimi nikiwa kama mwanasheria linanisumbua kidogo, kutokana na umahiri wako jaji, ninaomba upitie zuio lililotolewa na Mahakama Kuu kwa kina ili uweze kuangalia kisheria, je inaruhusiwa kujadili au la,” alisema Chenge.

Baada ya majadiliano hayo, Mwanasheria Mayunga alisema amri ya mahakama haihusiani na kazi za baraza kwani katika oda ya mahakama, hakuna kipengele cha kuzuia kujadili suala hilo.

“Ibara ya 132 ya sheria ya mwaka 1987, ibara ndogo ya kwanza ambayo inaeleza kuwa kutakuwa na sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma ya kuchunguza mienendo ya viongozi na watumishi wa umma.

“Taasisi hii ni huru na kwamba inafanya kazi endapo kuna taarifa ya ukiukwaji wa maadili kwa viongozi katika suala la rushwa au kutumia madaraka yao vibaya,” alisema Mayunga.

Baada ya kusema hayo, Mwenyekiti wa barza hilo, Jaji Mstaafu Hamis Msumi, alihairisha shauri hilo na kusema watapitia zuio la mahakama hiyo ili waweze kuangalia kama ni kweli linaweza kuwazuia kufanya kazi zao au la na leo waweze kutoa uamuzi.

“Tumeomba muda kidogo ili tuweze kuipitia hii oda ya mahakama na kuiangalia kwa umakini kama ni kweli inatuzuia tusijadili suala hili au la, leo tutatoa uamuzi kamili,” alisema Jaji Msumi.

Aliongeza kutokana na hali hiyo, baraza hilo linapitia hoja ya mlalamikiwa na mlalamikaji ili kuangalia mambo ya kisheria yanayohusu kujadili au kutokujadili suala hilo.

Chenge akiwa nje ya Ukumbi wa Karimjee ambako mashauri hayo yanasikilizwa, waandishi walitaka kusikia maoni yake juu ya suala hilo na yeye akawajibu: “Andikeni kama mlivyoona na kusikia.”

Mbunge huyo alifika katika viwanja vya Karimjee saa 3:00 asubuhi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri lake saa 3:15 baada ya jopo la majaji na mwenyekiti wa baraza hilo kuwasili.

Baraza hilo pamoja na kutolea uamuzi wa shauri la Chenge wa kusikilizwa au kutosikilizwa leo, pia linatarajia kumuhoji Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kwa siku mbili – leo na kesho.

KASHFA ZA CHENGE
Chenge ametajwa kuhusika katika kashfa mbalimbali, zikiwamo za rada, ajali iliyoua watu wawili na uchotwaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Rada
Chenge alitajwa katika kashfa ya ununuzi wa rada, ambayo ilimlazimu kuachia uwaziri.

Rada hiyo ilinunuliwa kutoka Kampuni ya BAE System ya Uingereza kwa dola milioni 40 mwaka 2001, kiwango kilicholistua Bunge la Uingereza.

Katika uchunguzi wa suala hilo, ilibainika kuwa Chenge alikuwa na akaunti kwenye Kisiwa cha Jersey iliyokuwa na zaidi ya dola milioni 1 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.8) hali iliyofanya ashinikizwe kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri wa miundombinu.

Ajali iliyoua wawili
Wakati kashfa ya rada ikiendelea, Chenge alihusika katika ajali iliyoua wanawake wawili mmoja akitajwa kuwa mtu wake wa karibu.

Baada ya ajali hiyo, alishtakiwa kwa makosa ya kuendesha gari kizembe na bila kuwa na bima.

Alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh 700,000 ambazo alilipa.

Tegeta Escrow
Mwaka jana alijikuta kwenye kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambapo alidaiwa kuchotewa Sh bilioni 1.6.

KAULI TATA
1. Alipopata kashfa ya kuchota Sh bilioni 1.8 za rada, alisema ‘Ni vijisenti’.

2. Alipopata kashfa ya kuchota Sh bilioni 1.6 za Escrow, alikuja na kauli mbili: “Mimi ni tumbili, hata kwenye hii (kashfa ya Escrow)” na “Mimi ni nyoka wa makengeza, nawatafutia wananchi fedha.”

3. Wakati wa kelele za kumtaka Chenge na wenzake kujivua gamba, mbunge huyo alisema: “Gamba limevuka limeishia kiunoni”.

4.Ashauri waliohusika na kashfa ya Escrow, mamlaka ya uteuzi (Rais) iwashughulikie na wapinzani wakaungana naye, lakini CCM wakagoma.

NYADHIFA ALIZOWAHI KUSHIKA
2014: Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba Mpya.
2006/15: Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
2006/08: Waziri wa Miundombinu.
2006: Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
1993-05: Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
1991-93: Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
1972-73: Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM.

Mwanamuziki Stara Thomas Akana Kufumaniwa na Mpenzi Wake

$
0
0
Aliyekuwa mwimbaji muziki wa gospel na baadaye kurudi kwenye Bongo Fleva,Stara Thomas amekana habari zilizoenea hivi karibuni kuwa amefumaniwa na mpenzi wake nyumbani kwake.

 Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa mwanamke kama yeye hawezi kufumaniwa na kwamba mpenzi wake wa sasa kinachomsumbua ni wivu wa kimapenzi bila kumtaja jina mpenzi wake huyo wa sasa.

Aidha ameongeza kuwa hayuko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sasa ndiyo maana amekaa kimya tangu habari hizo zitoke kwenye magazeti.

‘’Nimeamua kunyamaza kimya lakini ipo siku ntazungumza kila kitu kuhusiana na habari hizi," alisema Stara.

Licha ya Kumchapa Makofi Mpenzi Wake Shilole Atoa Ahadi ya Kumzalia Nuhu Mziwanda Watoto Wawili

$
0
0
Shilole amedai kuwa mpango wake ni kumzalia mchumba wake Nuh Mziwanda watoto wawili.

Muimbaji huyo mwenye watoto wawili wa kike amesema hayo wakati akiongea kwenye kipindi cha The Mboni Show.

“Nitamzalia watoto wawili, nina wawili,” alisema Shilole aliyeongeza na mchumba wake huyo kwenye kipindi hicho kinachorushwa TBC1. Shilole amesema kuwa kadri siku zivyonaenda anazidi kumpenda zaidi Nuh kutokana na mapenzi anayomwonyesha.

Mwaka jana Nuh alimvisha pete mchumba wake huyo.

Mabinti Acheni Kuwakalia uchi waume za watu..Hawa Viumbe ni Wadhaifu Sana

$
0
0
Jamani inasikitisha sana, pale binti anapoamua kutafuta mazingira tu na kuamua kumkalia uchi kwa makusudi kabisa mume wa mtu kwa lengo la kumpata, mkasa huu umetokea nyumba ninayoishi, kuna wapangaji vyumba vyao vipo karibu karibu, huyu mmoja ana msichana wa kazi, mwingine hana.

Huyu binti katafuta mazingira na kumkalia yule jamaa uchi kilichotokea ni yule jamaa kujikuta anaanza kumfuatilia msichana, na hali ukizingatia hakua hata na wazo na huyo dada na ni muda mrefu wanaishi hapo, kumbe dada na namba ya simu alishatafuta si ndo kuanza kuchati nae oh mpenzi sijui nini na nini.

Kindumbwe ndumbwe juzi wife wa jamaa kaona message, hapajakalika ugomvi na nyumba nzima wamejua. Jamaa akajitetea, ''Yaani mke wangu wala siko hivyo, na wala sina wazo na huyu mjinga, ila juzi tu nipo hapo uwani nafua nguo zangu si ndo akanikalia uchi, then badae ananitumia message tukachati, na wala sijui namba zangu kapata wapi''.

Aibu ndo hivyo tena!

Jamani mabinti acheni sio vizuri kumbuka hata na wewe utakuja olewa, kama unaona mwanaume haonyeshi muda na wewe muache na sio kumfanyia visa. Hawa viumbe 98% ni wadhaifu sana, Paja tu hoi, na nyie wanaume ukiona binti anakukalia uchi kama umetazama kwa bahati mbaya basi usigeuke tena potezea, hata binti atakuona una msimamo.

Asante kwa kuelewa.
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live




Latest Images