Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live

Unalionaje Swala CHADEMA Kuwa na Jeshi Lake la Kujihami? Toa Maoni Yako

$
0
0
Hii Picha ni Jeshi la Chama cha Chadema Maarufu Kama RED BRIGADE huko Mwanza wakati wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa Chama Hicho Freeman Mbowe Siku ya Jumamosi ....

Nini Maoni yako juu ya Majeshi haya ya Vyama?

Ipi Adhabu Sahihi ya Mtu Anayetembea na Mke wa Mtu?

$
0
0
Kuna jamaa mmoja ni mwalimu wa Secondary huko masasi anajifanya mende wa kutembea na mke wangu nimemuonya zaidi ya mara mbili, naona anakaidi huwa anavizia mimi nikitoka huwa anawasiliana mke wangu kwahiyo anatoka masasi anakuja Tanga nilitaka kuweka picha yake hapa ila mtandao unasumbua.

Sasa nafikiria ni adhabu gani nimpatie maana ananisababishia mgogoro wa kifamilia, hivi sasa natumia muda mwingi kumfuatilia yeye nyendo zake badala ya shughuli zangu, nilitaka kumuacha wife lakini mtoto wangu bado mdogo naogopa kumtesa mwanangu pia kuna mtu amenishauri nimtege wife, ila inaniuma sana nahisi nikimkamata sijui nimfanyaje, najitahidi ili niweke picha yake hapa ili ajione na watu wengine wamuone na mkewe pia amuone.

Ushauri wenu tafadhali

Kodi Yamkimbiza Mama Kanumba Sinza

$
0
0
MAMA mzazi wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amefunguaka baada kuongea na FC kuwa moja ya sababu iliyofanya ofisi yake kuhama kutoka maeneo ya Sinza Meeda ilipokuwa wakati wa uhai wa mwanaye ni gharama za pango hilo kupanda kila mwaka.

“Kuna watu ambao wanadai na kuandika hata katika mitandao ya kijamii kuwa eti ofisi za Kanumba The Great Films zimefungwa na hazipo tena, si kweli kodi ni kubwa sana hivyo tumehamishia Kimara Temboni,”anasema Mama Kanumba.

Mama Kanumba amesema kuwa ofisi hiyo inafanya kazi wala haijafungwa na kwa uhakika ni kwamba kuna filamu ambayo imekamilika na itatoka hivi karibuni chini ya kampuni, filamu hiyo imewashirikisha wasanii Flora Mtegoa, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka na wasanii wengine.

Ngeleja: Zitto Aliomba na Kupewa Milioni 30 Kutoka kwa Rugemarila

$
0
0
Mh. Ngeleja akiwa anahojiwa na baraza la maadili amesema Mh. Zitto Kabwe alipokea shilingi milioni 30. Akaongeza kuwa kama wanahojiwa waliopokea fedha na Mh. Zitto aitwe kuhojiwa na baraza hilo.

Pamoja na kutaja wafanyabiashara na mashirika yaliyowahi kumsaidia, Ngeleja aliwasilisha vielelezo vya misaada hiyo.

Pia ,aliwasilisha kielelezo cha tuhuma zilizowasilishwa bungeni na Kambi ya Upinzani na mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde dhidi ya Zitto kuwa alipokea zaidi ya Sh milioni 30 kutoka Tanapa, NSSF na kampuni inayohusishwa na akaunti ya Escrow ya Power Solution Limited (PAP).

Kwa mujibu wa Ngeleja, pamoja na tuhuma hizo dhidi ya Zitto kuwasilishwa bungeni na vielelezo na kutaka Zitto afikishwe mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Ndio maana nasema hata kama ningepokea msaada huo kutoka VIP Engineering haukuwa kwa ajili ya maslahi yangu kwa sababu ni utamaduni uliojengeka kwa kampuni duniani kote kutumia sehemu ya faida zao kusaidia jamii, lakini pia nisingekuwa mbunge wa kwanza kupokea msaada wa aina hiyo,” alisema.

Pamoja na utetezi huo wa Ngeleja, Cyriacus, alisema utetezi uliowasilishwa na kiongozi huyo, hauna mashiko kisheria.

“Amejitetea kwamba fedha alizopokea zimetolewa kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake, lakini si kweli kwa sababu nyingine alichangia Kanisa Dar es Salaam, kutokana na hili naomba apewe adhabu kali iwe fundisho,” Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Hamisi Msumi, alisema baraza hilo limepokea na kusikiliza pande zote mbili na litawasilisha uamuzi wake kwa mamlaka husika ambapo itajulikana endapo mbunge huyo atahitaji kujibu mashtaka yanayomkabili au la.

Wanaume Watatu Wanyongwa Mkoani Kilimanjaro na Kisha Maiti Zao Kutelekezwa

$
0
0
Watu watatu wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo ya Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha majeraha maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela (pichani) alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema ametuma maofisa wake eneo la tukio na taarifa rasmi ataitoa itakapokamilika.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu hao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 28 na 32 wanadhaniwa ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mirerani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa maeneo ilipokutwa miili hiyo ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao miili hiyo ilikutwa eneo jirani na alipouawa bilionea wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya aliyeuawa kupigwa risasi kifuani.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema askari kutoka kituo cha Bomang'ombe walifika eneo la tukio majira ya saa 3:00 za asubuhi na kufanya uchunguzi katika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya vijana hao

Nguo Fupi Yamzalilisha, Wanaume Wakware Wamshambulia, Aokolewa na Bado Bado

$
0
0
Hiyo ni Picha ya Msichana ambayo siku ya jana imesambaa sana mitandaoni , inasemekana alipita maeneo ya Sinza akiwa amevaa kinguo kifupi ambacho kilivuta hisia za midume wakware na kuanza kumzonga zonga wakitaka kumvua kabisa kimini hicho ...huku wengine wakimchoma vidole sehemu zake za siri ..kwa bahati nzuri alitokea mtu wa boda boda na kuamua kumsaidia kwa kumpakia na kutimua mbio.......

Hii inatufundisha nini ?

Wema Sepetu Aamua 'Kuolewa'. Aenda Kumtambulisha Mume Nyumbani Kwao

$
0
0
Kwa mujibu wa tovuti ya Mange, inasemekana mwanadada Wema Sepetu ameamua kufanya kweli na kwenda kumtambulisha mume wako mtarajiwa nyumbani kwako Singida tayari kwa mipango ya ndoa.

Kupitia picha iliyowekwa kwenye tovuti hiyo, inayomuonesha mwanadada Wema akiwa na pete ya ndoa kidoleni anayodaiwa kuvalishwa na mchumba wake huyo ambaye wapasha habari wa hapa mjini wanadai ni yule tajiri wa Uganda - Ivan aliyekuwa mume wa mwanadada Zari ambaye kwa sasa ni mpenzi wa ex wa zamani wa Wema – Diamond Platnumz.

Wacha BongoMovie iendelee, Sisi yetu macho na masikio. Tunaisubiri ndoa hii kwa nguvu zote.

Unahisi Diamond na Zari watahudhuria kwenye harusi hii? Tupe maoni yako

Askari Polisi wa Kike Avuliwa Nguo na Kuachwa Mtupu, Watu Wanane Wafikishwa Kortini

$
0
0
Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde, kwamba kwa pamoja, washitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo kwa kumvua nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Waliopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Minde, ni Jasmin Iddi (40), Abdallah Hamduni (26), Ramadhani Bakari (32) wote wafanyabiashara wa mjini hapa pamoja na dereva, Saidi Saidi (50) .
Wengine ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace Daniel Paul (21), Happiness Kiluvya (23), Jackline John (20) na Constansia Masaki (21) wanaodaiwa ni wanachuo katika moja ya vyuo vya elimu ya juu mjini Singida.

Mwanasheria wa serikali, alidai wakati wote wa kitendo hicho cha udhalilishaji, polisi huyo, alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Tukio hilo inadaiwa lilifanyika Februari 14, mwaka huu saa 11.30 jioni ambako kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, inadaiwa polisi huyo wa kike alikutwa akiwa na mume wa mshitakiwa, Jasmin wakiwa kando ya Ziwa Singidani wakivinjari siku hiyo ya Wapendanao.
Hata hivyo, mume ambaye jina halikupatikana, inadaiwa alitoroka. Mutta alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu 138 A kifungu cha 16 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Wote walikana mashitaka

VIDEO – Sonko Rescue Team Documentary…Sonko Continues to Win the Hearts of Nairobi Residents

$
0
0
‘The essence of true leadership is to add value to the lives of those you lead during your period in leadership’. Those were the words of Nairobi senator Mike Sonko when he launched the Sonko Rescue Team.

The philanthropic senator kicked off this year with one goal in mind; to focus more on service delivery to his constituents. True to his word, the Sonko rescue team has had an undeniable and most welcome effect on the residents of Nairobi.
  
With the free service delivery team, Sonko has done something that has never been before. In a country where most of our leaders look out for themselves, Sonko’s altruism is winning the hearts of ‘Nairobians’ and credit should be given where it is due. He is doing a tremendous job and this is the kind of stuff that never goes unnoticed by the humanitarian community.

Here is the Sonko Rescue team documentary that puts everything he is doing in a perspective that my words cannot

Woman Kisses ERIC OMONDI Passionately in Front of Her Husband …. Some MEN Are Idiots

$
0
0
Eric Omondi recently recounted a moment when someone’s wife approached him and kissed him passionately in front of her husband. The husband shrugged it off and said that he understands that his wife was drunk and that is why she did that.

Here is what Eric said

"Her husband was standing just next to her when she ran and kissed me, passionately. I was glad the man was understanding enough because this was his wife...he said I should not worry because his wife was drunk"

Serengeti Boy 'Nimelifaidi Sana Penzi la Jack Wolper'

$
0
0
Siri imefichuka! Bwa’mdogo a.k.a Serengeti Boy kutoka Kundi la Makomando, Fredy Felix amesimulia namna alivyofaidi penzi la staa wa Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.

Akizungumza na GlobalTV Online kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke ambaye aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa Wolper.

“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia kila nilichohitaji.

Akizungumza na GlobalTV Online kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke ambaye aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa Wolper.

“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia kila nilichohitaji.
GPL

Ray C 'Mapaja Yangu Makubwa Yananitesa Sana'

$
0
0
Baada ya Kuachana na Madawa ya kulevya Mwanamuziki Ray C kwa sasa anahangaika na zoezi la kupunguza Mwili wake baada ya kuwa mkubwa sana kiasi cha kupoteza lile umbo lake la kiuno bila mfupa......

Soma Hapa Alichosema:

'No Filter,No Make Up!Mapaja bado yananitesa sana ila najua nitafika safari yangu ya kupunguza uzito hadi nifike mkoa wa kilo 65........Bado Njia ni ndefu na safari ndo kwanza imeanza ila ninachojua ni kwamba ukitaka chochote kizuri maishano ni lazma ukitolee jasho!ma ndio ninachofanya!Hakika nitafika!

20kg to go!Safari ya kupunguza mwili bado inaendelea!nashukuru nimeanza kuona mwanga mbele yangu!Si rahisi ila nimezoea kupambana na lolote mbele yangu na na uhakika ntashinda na hili pia!Am doing ths for all my fans around the world!' Ray C

Unamshauri Nini Ray C Kuhusu Huo Upaja?


Mvua ya Mawe Yaleta Maafa Makubwa Mkoani Shinyanga Watu 35 Wafariki Dunia

$
0
0
Watu 35 wamefariki dunia na wengine 55 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba zao kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Nuh Mziwanda Anusurika Kupigwa Chupa na Shilole ambaye ni Mpenzi Wake.....Hili ni tukio la Pili

$
0
0


Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.

 

Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini haikumjeruhi.

 

Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.

 

 ‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe hiyo.

 

Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka chini.

 

Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa amelala.

 

Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na kuahidi kutompiga tena.

Nay Wa Mitego Baada ya Kupima UKIMWI......Akiri Kumsaliti Mpenzi wake

$
0
0

Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego hivi karibuni aliweka wazi majibu yake baada ya kupima UKIMWI kupitia account yake ya Instagram na kwamba alikuwa yupo safi yaani(Negative).

 

Alipoulizwa sababu ya kupima ngoma alisema kuwa alikuwa akiumwa ugonjwa wa Malaria na alikuwa hajaugua kwa muda mrefu na alipokwenda hospitali ilibidi apime na ngoma ingawa ni kawaida yake kupima mara kwa mara.

‘’Nilipima baada ya kuumwa Malaria lakini huwa ni kawaida ya kupima ngoma hata mke wangu(Siwema) alipokuwa mjamzito tulikwenda pamoja kupima hospitali,"alisema Nay. 
Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.

 

"Unajua ni mambo ya ujana, ni kweli nilishawahi kuchepuka lakini siwezi kusema ni mara ngapi si unajua mama watoto anaweza kukasirika? Lakini nilikuwa makini sana na namwomba sana msamaha mke wangu na sitegemei kuchepuka tena,’’alisema Nay. 


Q-Chillah,TID wataka kutwangana kisa,ngoma mpya ya Ali Kiba

$
0
0

Mastaa wa Bongo Fleva,Q-Chillah na TID mwishoni mwa wiki hii walitaka kutwangana walipokutana katika Klabu moja usiku.
  
Kwa mujibu wa Q-Chillah akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alikwenda kwenye klabu hiyo kuangalia shoo iliyokuwa ikifanyika lakini baadaye aliamua kutoka nje kucheza ‘pool table’ ndipo alipomuona TID.

 

‘’Nilimuona jamaa(TID) akiniangalia na baadaye alinifuata akaniambia kuwa anataka kuongea na mimi nikamwambia ile siye sehemu yake atafute muda mwingine ndiyo tuongee,’’alisema Q-Chillah. 

 

Aidha Chillah aliongeza kuwa TID aliendea kumuongelesha ndipo alimwambia kuwa anachofanya kumuongelea yeye vibaya siyo vizuri na kile alichokipost hivi karibuni kuhusu kuuponda wimbo mpya wa msanii Ali Kiba uitwao ‘Cheketua’ aliouachia hivi karibuni kupitia account yake ya Instagram hakikuwa kitu cha busara ilitakiwa amsapoti kama msanii mkongwe kuliko kumponda hadharani kupitia mitandao.
‘’Kiukweli kitendo cha TID kuandika Instagram kuwa ngoma mpya ya Alikiba ni mbaya na baada ya miezi mitatu haitokuwepo siyo kizuri nilimwambia yeye ni msanii mkubwa inabidi kumsapoti Ali Kiba na kwamba nilitaka kumpiga kwa fimbo ya pool table siyo kweli nilikuwa nikimueleza tu,’’aliongeza Q-Chillah.

Kwa muda mrefu wasanii hao wawili ambao waliwahi kuwa pamoja kwenye bendi ya (Top Band) wamekuwa kwenye bifu zito wakitupiana maneno kwenye vyombo vya habari.

Mchungaji wa Kanisa Awapachika Mimba Wanawake zaidi ya 20 wa Kanisa Lake

$
0
0
Huko nchini Nigeria wanawake zaidi ya 20 wakiwemo wake za watu na mabinti wamepachikwa mimba na "nabii" wao ambaye amedai aliambiwa na Roho mtakatifu kufanya nao mapenzi wanawake hao. Nabii huyo alifahamika kwa jina la Timothy Ngwu ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity huko Enugu tayari anashikiliwa na jeshi la polisi la jimbo hilo kwa kosa la kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na wanawake hao.

Mchungaji huyo amedai anatii wito wake wa kinabii na kiroho alioitiwa na kufanya sawa na mapenzi ya Mungu kwa kuwapa mimba yeyote yule aliyechaguliwa na kuwekwa wazi na Roho mtakatifu bila kujali kama mwanamke huyo ameolewa ama la

Taarifa kutoka kwa familia za mchungaji huyo zinasema mkewe aitwaye Veronica Ngwu ambaye alichoshwa na tabia ya mumewe hasa alipompa ujauzito mdogo wake na kuamua kumripoti Polisi...
alimfukuza mkewe wa ndoa waliyezaa naye watoto watatu na kuanza kuwajaza mimba wake za watu na mabinti wadogo, we angalia boma lote limejaa watoto wa jinsia zote alilalamika kaka wa nabii...
Kuna mmama amepewa mimba yeye na binti yake.

Shape ya Shilole Yazua Vimaneno Msiba wa Kapteni Komba..Mwenyewe Adai ndivyo Alivyo

$
0
0
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni alichovaa bi’dada huyo.

“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri  maumbo yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.

Paparazi wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake ndio lilivyo.....

Wema Sepetu Amkana Kajala Masanja live.."“Sikuwahi Kuwa na urafiki na Kajala"

$
0
0
“Hali ni tete, Madam ameibua bifu upya alipofunguka kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na Runinga ya EATV, hapo ndipo ilipodhihirika kwamba wawili hao hawawezi kuzikana wala kusameheana.

“Wafuasi wa Kajala hawakufurahishwa na maneno ya Wema ambayo walidai yalikuwa na lengo la kumvua nguo mwenzake, yale matumaini ya kusameheana hayapo tena, ni bifu hadi wanakwenda kaburini,” kilisema chanzo hicho.

Kwenye kipindi hicho, mbali na mambo mengine, Wema alieleza kuwa Kajala hakuwahi kuwa rafiki yake lakini alijitolea kumlipia faini kumuepusha na kifungo kutokana na kuguswa na kuingiwa na moyo wa huruma kama msanii mwenzake.

Sikuwahi kuwa na urafiki na Kajala, kilichonifanya niwe karibu naye ni mwanaye ambaye alikuwa akinipenda na kutaka kukutana na mimi...,” alisema Madam.

Kupitia kipindi hicho, Wema pia alizungumzia kiini cha ugomvi wao ambapo alianika kinagaubaga kwamba alichukizwa na suala la Kajala kumsaliti kwa kutembea na mchumba wake aitwaye CK (yule kigogo aliyesumbua mjini kwa kutapanya fedha).“Kajala hana fadhila, huwezi amini mtu ambaye niliamua kujitolea kwa moyo wangu kumlipia Sh. milioni 13 huyohuyo aje kutembea na mchumba wangu, huku ni kukosa ubinadamu kulikopitiliza,” alisema Wema.


Je ni Kweli Wema Hakuwahi Kuwa na Urafiki na Kajala?

Picha: Wema Sepetu Atoa Baraka kwa tumbo la Aunty!

$
0
0
Mrembo na mwigizaji wa filamu mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii hapa Bongo, Wema Sepetu  ame-share nasi picha kadhaa akiwa na rafiki yake kipenzi, mwigizaji  Aunty  Ezekiel ambae kwa sasa ni mjamzito na karibu kujifungua.

Kwenye picha hizi Wema anaonekana akiwa amelishuka tumbo la Aunty kitendo ambacho kinaashilia kuwa mwanadada huyo alikuwa akitoa baraka zake kwa kiumbe kilichomo ndani mbali na ujumba ambao Wema aliutupia kuonyesha kuwa yeye na aunty ni marafiki  wa kweli na wanafurahia pamoja.

Kitendo hiki cha wema kiliwafurahisha wengi na kumsifu Wema kuwa na moyo wa upendo kwa jamaa zake.

Nami naungana nao kumsifu Wema kwa moyo huu aliouonesha, kwani rafiki wa kweli ni yule ambae mnakuwanae wakati wote…

Mzee wa Ubuyu
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live




Latest Images