Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Mtangazaji Edzen Apata Aibu ya Mwaka..Mpenzi Wake Amrekodi Akiwa Uchi na Kupost Mitandaoni

0
0
Habari ya Mjini leo ni Hawa watu wawili Mtangazaji Edzen na Moza..Ambao inasemekana walikuja kuwa wapenzi baada ya Edzen kuachana na Dida..leo imesambaa video kwenye Insta na whats app ikionyesha Edzen akitoka kuoga na kuingia chumbani akiwa na taulo na kisha kulivua na kuweka mambo hadharani ..huku akivaa boxer.....Video inasemekana imechukuliwa na Moza , Mazingira yanaonyesha ni chumba cha msichana hivyo alikuwa kwa moza .....

Aibu sana hii kitu mpaka nimeshindwa kuweka video kwa ajili ya Maadili ..Embu Edzen badilika sasa we kila siku majanga tu na hawa wadada.....

Flora Mbasha Atoa Ushahidi wake Kwa Siri Kuhusu Kesi ya Ubakaji Inayomkabili Mumewe, Emmanuel Mbasha

0
0
Kesi ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.

Kesi hiyo ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5 hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.

Siku hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana.
 
Mbasha anashtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara nyingine eneo hilohilo.

East Africa’s Finest Socialites Huddah and Zari to Host Nairobi Party Together

0
0

Two of East Africa’s finest socialites, Kenya’s Huddah Monroe and Uganda’s Zari are all set to host an epic party together.

Zari will be jetting into the country this month for the one of a kind gig at Skyluxx lounge. Dubbed ‘Art of Luxury’, the party will go down on the 21st of March.

Entertainment will be catered for by Creme de la creme, DJ Pierra and DJ Incredible.

Zari had this to say,

“Nairobi are you ready? will be blazing ur town on the 21st March with the sexy huddahthebosschick”

Lady Jay Dee Akerwa Kuzushiwa Kutundikwa Mimba

0
0
Mwanamuziki nguli wa kike hapa Tanzania Lady JayDee ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao walimuelewa vibaya baada ya kupost picha jana na kusema kuwa tumbo lake limevimba na kusema ana mimba

"Imebidi nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini ??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakayewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba..Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa." aliandika Jide

Unalipi la kumwambia Jide hapo?

Albino Kukatwa Mkono: Waganga 10 Pamoja na Baba Mzazi Watiwa Mbaroni

0
0
Polisi mkoani Rukwa inawashikilia watu 17 wakiwemo waganga wa jadi 10 wakihusishwa na tukio la kikatili katika kijijini cha Kipeta , Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga ambako mtoto mlemavu wa ngozi (albino), Baraka Cosmas (6) mwishoni mwa wiki alishambuliwa na kukatwa kiganja cha mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana.
 
Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa ni watu saba ambao wanatuhumiwa kushiriki katika kumkata kiganja mtoto huyo mlemavu wa ngozi akiwemo baba yake mzazi, Cosmas Yoram (32).
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao kufuatia msako mkali uliofanyika katika vijiji vinne vya wilaya za Sumbawanga na Nkasi.
 
Aliwataja waliokamatwa pamoja na baba mzazi wa mtoto huyo kuwa ni pamoja na Mwendesha William (30), Masunga Bakari (50), na Ngolo Masingija (47) wote kutoka kijiji cha Kaoze .
 
Wengine ni Paschal Jason (40), David Kiyenze (45) na Mageta Shimba (46), wote wakazi wa kikiji cha Kipeta , Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.
 
Kwa mujibu wa Rwegasira, katika msako huo pia walikamatwa waganga wapiga ramli chonganishi 10 akiwemo Sererino Kachingwe “Nakalango”(70), mkazi wa kijiji cha Miangalua wilayani humo ambaye pia alipatikana na bunduki aina ya Shot gun greener yenye namba G 73354 TZD,CAR 47478 ambayo anaimiliki isivyo halali .
 
“Mtuhumiwa huyu pia ni mganga wa kienyeji ambapo alikutwa na wanyama wawili aina ya Kalunguyeye wakiwa hai pamoja na dawa mbalimbali za miti shamba.
 
"Pia katika msako huo amekamatwa mganga mwingine wa kienyeji , Eliza Malongo mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kijiji cha Kamnyalila akiwa na nyara za Serikali, “ alieleza.
 
Aliongeza Eliza alikutwa na ngozi ya chui, wanyama wanne waliokaushwa aina ya Kalunguyeye na nywele zinazodhaniwa kuwa za binadamu pamoja na mfupa wa swala.
 
Waganga wengine waliokamatwa katika msako huo ni pamoja na Sodeli Malimbo ‘Chuchi” (69) mkazi wa kijiji cha Miangalua, Akobo Chinzwe (50), Leonard Samson (59) na Engelbert Kasinde (45) , wote wakazi wa kijiji cha Kamyalila.
 
Katika orodha hiyo wapo Boniface halya (49) na Julius Simbamwene (40) wote wakiwa wakazi wa kijiji cha Mpui .
 
“Watuhumiwa hawa walikutwa na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli vikiwemo vioo viwili, pembe moja, ndege na wanyama ambao hawakuweza kutambulika mara moja, mizizi ya aina mbalimbali na dawa mbalimbali za kienyeji,“ alieleza Rwegasira.
 
Akifafanua zaidi, Rwegasira alidai kuwa msako huo pia ulifanyika wilayani Nkasi ambako alitiwa nguvuni mganga wa kienyeji aitwae Charles Misalaba (47) , mkazi wa kijiji cha Kacheche ambapo alikutwa na yai la mbuni , kucha za chui , pembe ya korongo , ngozi ya paka pori na kobe aliyekaushwa.
 
Amesisitiza kuwa msako huo bado unaendelea na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali wa shauri lao kukamilika.
 
Kwa mujibu wake msako huo unafuatia watu wasiojulikana kumshambulia na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha kutokomea nacho kusikojulikana usiku wa kuamkia Machi 08, mwaka huu.
 
Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32) na Prisca Shaaban pamoja na watoto wengine wawili ambao nao ni albino wakiwa na umri wa miaka nane na minne.
 
Alisema tukio hilo ni la saa nane usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo akiwa amelala na mama yake. Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo.
 
Akielezea zaidi, Kaimu Kamanda Rwegasira alisema usiku huo kikundi cha watu wasiojulikana walivamia nyumba alimolala Baraka na mama yake mzazi, Prisca wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo mapanga na fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumcharaza viboko Prisca baada ya kukataa kuwapatia mtoto huyo, mwenye ulemavu wa ngozi.
 
“Baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo walimwamuru mama mzazi wa mtoto Baraka kuwakabidhi mtoto huyo, lakini alikaidi ndipo walipoanza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumjeruhi vibaya …
 
“Waliingia ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia na kuondoka nacho kusikojulikana,” alibainisha.

Bifu la Lady Jaydee na Madam Ritha wa BSS

0
0
Katika kusheherekea sikuuu ya mwanamke Duniani, Mwanamuziki mwenye hadhi ya kipekee bongo, Judith wambura mbibo maarufu kama Lady jaydee ame share story yake fupi kuhusu bifu lililowahi kutokea miaka ya nyuma kati yake na Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha.

Akitiririka kwenye ukurusa wake wa Instagram, staa huyo ambaye hana mpinzani ndani ya Bongo Fleva, alikiri kutofautiana na mwanamama huyo, baada ya madam ritha kumpaka make up lady Jaydee ambapo Jide alikuwa akiifuta hali iliyompelekea Madam kumgombeza hali iliyozua tafrani kwa mwanamuziki huyo, na kusababisha ugomvi ambapo bifu hilo lilidumu kwa mda Wa miaka mitano bila mastaa hao kuongeleshana wala kusalimiana.

Hata hivyo staa huyo amekiri kumaliza tofauti yake na mwanamama huyo kwa kudai ulikuwa ni utoto na sasa hivi bifu kati yao limeisha.

Source: Lady Jaydee

Wadada wa Mjini Akiwemo Jack Wolper Wajitosa Kumtafutia Nuhu Mziwanda Mchumba, Wamchoka Shilole

0
0
Shilole na Nuhu Mziwanda
Story ya kwenye U Heard ya leo March 10, inahusu tetesi zilizoenea kuwa wa dada wa mjini akiwemo muigizaji, Jacqueline Wolper wamemchoka msanii Shilole kwa madai kuwa amekuwa akimpiga mpenzi wake Nuh Mziwanda mara kwa mara na wanataka kumtafutia  mpenzi mwingine ambae hatampiga, mpango uliopangwa siku ambayo Shilole alimpiga Nuh na wasanii waliokuwepo kuingilia.
Soudy Brown amemtafuta Shilole na kumpa taarifa hizo na kusema sio kweli ila watu wanazusha ili kuwagombanisha jambo ambalo hawatafanikiwa kwa kuwa anajiamini sana, kwa upande wa  Nuh amesema kuwa ndio kwanza anasikia taarifa hizi ila mwanaume huwa hatafutiwi mwanamke na Shilole hampigi kama wanavyodai zaidi ya kuishi kwa raha.

Diamond Apata Mshituko Mkubwa Baada ya Kuambiwa Anadaiwa Shi Mil 800 na Serekali

0
0
Diamond Platnumz na Avril
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwepo madai ya kudaiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 na serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

ILIKUWAJE?
Mwishoni mwa wiki iliyopita, barua inayodaiwa kuandikwa na mamlaka hiyo halali ya serikali, ilisambazwa mitandaoni, ikielezwa kuwa ilikuwa imetumwa kwa meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ndiye yupo juu, ikimtaka kupeleka nakala za mikataba yote ya muziki aliyoingia kwa ajili ya kufanya shoo, kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.

GUMZO MITANDAONI
Baada ya kuwekwa kwa barua hiyo mitandaoni, watu mbalimbali walitoa maoni yao walionyesha hisia tofauti, baadhi wakipinga kwa madai kuwa wanamuonea huku wengine wakisema siyo Diamond tu, bali wasanii wote wanastahili kulipa kodi kutokana na mapato wanayopata kupitia kazi zao.

KODI ZIPOJE KIBONGOBONGO?
Mtaalam mmoja wa mambo ya kodi aliyezungumza na Risasi Mchanganyiko, alisema kwa mujibu wa taratibu zao, msanii huyo anastahili kulipa kodi kiasi cha asilimia kumi ya fedha anazopata katika kila mkataba anaoingia.

“Kuna walipa kodi wengine kama wafanyabiashara, hawa wanalipa kile ambacho kitaalamu kinajulikana kama Capital Gain, yaani kulipa kadiri unavyopata. Mtu anakwenda TRA mwenyewe na kueleza mapato yake na mamlaka itampangia kiasi cha kulipa. Ila watu kama wasanii na wengine wanaolipwa, wanatakiwa kutoa asilimia kumi ya malipo,” alisema mtaalam huyo aliyekataa kutajwa jina gazetini.

DIAMOND ANADAIWA SH. NGAPI?
Kama suala hilo litafanyika kwa mujibu wa mtaalam huyo, Diamond ambaye malipo yake kwa shoo moja yanatajwa kuwa ni shilingi milioni 20 kwa sasa, atatakiwa kulipa kiasi kinachozidi milioni 800 kutokana na hesabu zilizofanywa na watu wanaofuatilia muziki wake.

“Jamaa anafanya wastani wa shoo kama tatu kwa mwezi hapa nyumbani (Tanzania) na tatu zingine nje. Zile za nje analipwa siyo chini ya dola 25,000 kwa shoo moja. Nadhani unajua kwa sasa huyu dogo ndiye anakimbiza sana katika soko, yupo juu na kila promota anahitaji huduma yake,” alisema mdau huyo wa Bongo Fleva.

MCHANGANUO ULIVYO
Kama hesabu za mdau huyo zitakuwa sawa, inamaanisha kuwa Diamond anaingiza wastani wa shilingi milioni sitini kwa mwezi hapa nyumbani, na milioni 127  kwa mikataba ya nje ya nchi (Dola moja ya Marekani ni sawa na shilingi 1700), ikimaanisha kuwa kwa mwezi mmoja, kijana huyo aliyekulia Tandale, anaingiza kiasi cha shilingi milioni 187.5.

JUMLA  YA MAPATO MIAKA MINNE
Kwa mahesabu hayo, Diamond Platnumz anaingiza wastani wa shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka, fedha ambayo ukijumlisha kwa miaka minne, ameweka kibindoni shilingi za kitanzania bilioni 8.8, ambazo asilimia kumi yake ni shilingi milioni 880, ambazo ndizo zinazotakiwa kulipwa.

MENEJA AFUNGUKA
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Babu Tale alipotafutwa na gazeti hili na kuulizwa kama ni kweli alipewa barua au kujua kuwa barua hiyo ipo, alikataa kulizungumzia suala hilo, akisema siyo jambo la kulielezea kwenye vyombo vya habari.“Hata mimi nimeiona hiyo barua (anautaja mtandao wa kijamii maarufu sana nchini), sina cha kuelezea kwenye media,” alisema meneja huyo huku akikataa katakata kusema kama ameipata au la.

DIAMOND MWENYEWE SASA
Baadaye Risasi Mchanganyiko liliwasiliana moja kwa moja na Diamond mwenyewe, ambaye alikuwa nchini Nigeria, alikoenda kwa ajili ya shoo iliyoandaliwa na Africa Magic Viewers Choice Awards jijini Lagos, alishtuka sana na kuomba asizungumzie suala hilo.“Daah! Milioni 800? Anyway naomba nisizungumzie suala hilo kwa sasa.”

TRA WAIKANA BARUA
Gazeti hili lilipomtafuta ofisa wa TRA, ambaye jina lake limeandikwa katika barua hiyo, aitwaye Tillya V.M. T, alikanusha kuandika barua hiyo na kusema ni mambo ya kugushi yanayofanywa mitandaoni.
“Hakuna kitu kama hicho, its something created,” alisema bosi huyo akimaanisha kuwa jambo hilo ni la kutengenezwa.

NYOTA YA WEMA YAHUSISHWA
Wakati hayo yakijiri, baadhi ya wadau wamesema suala hilo linahusishwa na mojawapo ya kauli iliyowahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu kuwa mwanaume yeyote anayekuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi, nyota yake hung’aa, lakini anapoachana naye, hufifia.

WENGINE WAMHUSISHA ZARI
Aidha, wadau wengine walisema ishu hiyo huenda imeibuka kama mkosi uliochangiwa na kujiingiza katika mapenzi na mwanadada raia wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye mashabiki wanadai ni mtu mwenye mikosi, kwani Diamond ni mwanaume wake wa nne rasmi, wa tatu wa kwanza kila mmoja akiwa amezaa naye.

Edzen Jumanne Tukio la Pili Sasa Unazalilika Mwanaume Mzima, Badilika Sasa

0
0
Edzen Jumanne
Barua ya Wazi Toka kwa Mdau Kwenda kwa Edzen
Mimi ni shabiki wako mzuri sana Kutoka Mwanza ila nimesikitishwa na Video yako ukiwa uchi na unachukuliwa Video na Mdada..Tumezoea kuona wadada ndo wanachukuliwa Video ..naomba Nikuabie haya Machache labda yatasaidia ...
Juzi Juzi tulikisia Umeachwa na Aliyekuwa Mke wako Dida wa Times FM na Kufungasha virago kutoka Kwake ulipokuwa ukiishi..Mara Tukasikia Unatoka na huyu Moza ila wewe ulikataa kabisa , sasa  Video ya jana imekuumbua tena kibaya zaidi imechukuliwa upo kwake kitu ambacho kinapigilia tetesi kwamba wewe ni Marioo unaependa kulelewa na wadada wa mjini ..Kwanini usiwe na Kwako ukajilia vitu vitamu  kwako ..hawa viumbe wanaakili sana ukiwaendelekeza watakupiga Danadana mpaka utalijua jiji vizuri ...Embu Badilika Mwanaume Mzima...

By Crispa, Mwanaza

Wema Sepetu Katika Picha Ambazo Hujawahi Kuziona za Wakati Anaanza Kupata Umaarufu

0
0
Wema Sepetu
 Picha za Wema Sepetu Miaka Kadhaa nyuma kabla ya Kuwa na Umaarufu aliyonao kwa sasa , Picha hizi zinaonyesha mtoto alikuwa hana makuu Kabisa..Sura ya Upole na Ngozi Natural Kabisaaa..Hapo Alikuwa Toto Bikra...Bado Kina nani hawajaamza Kumrukia na Kumuumiza Mtoto wa Watu .....




7 Signs She Will Be Great In Bed, No. 6 Is A Must Read

0
0
Signs She Will Be Great In Bed

One of the biggest turn off for a guy is to find out that the girl you have been chasing for the longest time is very poor in bed. When a man makes a move to a girl its because he sees you attractive enough, but many a times men fail to be keen enough of the most crucial early signs of perfection in bed. Men here are seven key factors to consider before you make that last move; 

1. She's a great kisser - The way a woman kisses is basically a preview to the way she will behave in bed. So, if the woman you're dating begins running her hands over your body as she kisses you while gently biting your lip, pressing herself into you and creating s3xu@l anticipation, chances are she's going to be a great lover.

2. She is confident and comfortable within herself - If the woman you're dating offers flirtatious or coy looks and has chosen to reveal some of her body by wearing a low cut dress, a tight skirt or is showing off her legs around you, she is happy about her appearance and has a healthy amount of self-worth. If a woman is confident about her body, chances are she'll be great in bed and will actually let you see her n@ked with the lights on.

3. She enjoys the taste of food - Another trait that can translate exceptionally well to the bedroom is how a woman eats. If she puts food in her mouth sensually, delights in her meals and takes the time to savor the flavors, she may have a deep appreciation for c@rn@l pleasures. If she lingers over a meal, she may just take her time in bed as well.

4. She openly talks about s*x - A woman who openly discusses what she likes/does in bed is probably good at s*x and has the confidence to do what she wants in the bedroom. If she makes too many s3xu@l references, however, she may be overcompensating, and could just be a tease. 

5. She initiates touching on a regular basis - A great lover is one who values sensuality both in and out of the bedroom. So if you're seeing a woman who is willing touch your hand, your face or your body without you making a similar movement first or initiates a game of footsie with you under the table on dates, she probably enjoys initiating physical contact. That's a great sign that she both enjoys s*x and is good at it because it shows that she will follow her instincts instead of repressing them. 

6. She's flexible and works out  - Physical conditioning is fundamental to good s*x and there are some aspects of s*x that are like athletic contests; therefore, a flexible woman who is in good shape and involves herself in things like yoga or ballet will likely be able to exhibit more endurance in lovemaking. Furthermore, the ability to move her body in a flexible fashion allows for more possibilities in bed and can provide great thrills for both of you. 

7. She's a great dancer - A woman's dancing prowess along with her rhythm can not only suggest her energy and creativity – it can give a hint to what she moves like in the bedroom. So, watch her moves on the dance floor and you'll get a good idea of her skills between the sheets. 

Amber Rose shows us how she sleeps at night..

0
0
Lol this woman doesn't give a damn anymore...Call Her Whatever you Want...Last Night She shared the above picture showing how she sleeps at Night...Thats Amber Rose For You....

Breaking News: Ajali Mbaya Iringa Kontena Laangukia Basi la Abiria

0
0
Hizi safar hizi...jaman ukipanda gar unashukuru na ukishuka salama pia husisahau kushukuru....  Amjali imetokea changalawe mafinga basi la Majinja limeangukiwa na kontena muda huu hali si nzuri.... Inasemekana watu Karibia wote Wamapoteza maisha.....MUNGU AZILAZE MAHAL PEMA PEPON ROHO ZA MAREHEM JAMAN.....DUH...

Updates 

Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lililolaliwa na lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.



Wema Sepetu Amsifia Chaz Baba kuwa Ndiye Aliyekuwa Mwanaume Halisi

0
0
Wema Sepetu
Wema Sepetu amekanusha kurudiana na mpenzi wake wa zamani Chaz Baba japo amedai kuwa muimbaji huyo wa muziki wa dansi ndiye mwanaume wa pekee ambaye hakuwa na masuala ya kiswazi baada ya kuachana.


Wema ameiambia U Heard ya Clouds FM Jumatano hii kuwa Chaz Baba kwa sasa ni mshkaji wake na hata alipooa alimchangia pesa.

Chaz Baba alikuwa ni msikaji wangu naweza kusema ndio boyfriend pekee asiye na mambo ya Kiswahili,” amesema. “Tulizinguana tukafika pointi tukasaidiana, ameoa nikamtolea mchango, nimeenda kwenye harusi yake sioni tatizo.”

“Mimi na Chaz Baba tulikuwa tunapendana na baada ya kufikia point ya kuachana tukaachana, tukawa hatuongei for sometime mwisho wa siku baada ya kila mmoja kukaa kwake tukawa tunazungumza. Sio kama watu wengine tukigombanaga tunatafuta mabifu, hatusemeshani,” ameongeza mrembo huyo aliyesisitiza kuwa ‘sina bwana’.

Mwanasheria Albert Msando Afunguka kuhusu Kufukuzwa Zitto Kabwe Chadema

0
0

Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV

Kuhusu Zitto Kabwe: CCM wamecheza game of mind kuelekea uchaguzi mkuu

0
0
Zitto Kabwe
Maoni Huru kutoka kwa Mdau:
'Hatujui kweli kinachofurukuta mdani ya CHADEMA na hatujui kama kosa lilikuwa linavumilika ama haivumiliki.

Ila kitendo cha mahakama kufuta kesi ya Zitto haraka haraka inaweza ikawa ni game mind ya kisiasa ya CCM kwa sababu wanajua kuwa wazee wa kukurupuka watamfukuza haraka haraka na lazima kuna damage itatokea.

Au mnadhani kwa nini kesi imefutwa kuelekea uchaguzi? 

Mimi sio mamluki hata huyo ZZK, sijawahi kumuona zaidi ya kwenye magazeti, ila kilichopo kwa sasa ni kuwa CCM imechokwa na CHADEMA haijajiandaa'

By Saint Ivuga

Bob Junior: Sikupenda Ndoa Yangu Ivunjike

0
0
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records, Bob Junior amesema hayakuwa mapenzi yake kuacha ndoa yake ivunjike.

Bob Junior ameiambia Bongo5 kuwa kilichotokea ni majaliwa ya mwenyezi Mungu.

Nitaoa lakini sio miaka ya karibuni ni miaka ya mbele sana kwa sababu niliingia kwenye ndoa halafu mwisho wa siku ndo haikukaa muda mwingi ikanishinda,” amesema.

Yaani siwezi tena kusema niache halafu nione tena, simaanishi kwamba ndoa ya kwanza nilikurupuka, ilitokea kwa neema za Mungu na bahati mbaya kwa majaliwa ya Mungu ikavunjika. Watu wanauliza sana hili suala lakini mimi nipo single kabisa. Mimi nashangaa watu wanaendelea kuniuliza,” ameongeza.



Mashabiki watakiwa kutowapa lawama magoli kipa

0
0
Viongozi wa Vilabu na mashabiki nchini wametakiwa kuachana na tabia za kutoa lawama kwa magoli kipa wanaofungwa magoli mbalimbali ikiwemo kuhama goli na hatimaye kuweza kufungwa.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Kituo cha Magoli Kipa nchini TGC, Peter Manyika amesema, katika mazoezi kipa anafundishwa na kutahadharishwa mambo mbalimbali hususani kulinda goli inapotekea hatari ya kufungwa.
Manyika amesema, mashabiki na viongozi wanapoendelea na lawama watakuwa wanabadilisha magolikipa kila kukicha kwani kila Golikipa anakuja na tatizo lake na suala linalotakiwa ni kufundishwa zaidi ili kuweza kufanya vizuri na wapo magoli kipa wanaofundishwa lakini wanafungwa aina ya magoli ambayo huzuilika.
Manyika amesema, Golikipa anakuwa amebeba jukumu la watu wote hivyo suala la kufanya makusudi ili aweze kufungwa katika mechi mbalimbali linakuwa ni gumu kwania anaamini kila mtu anamtegemea yeye awapo langoni.
--------------
Note: 

Mlinzi Dr. Slaa, Akanusha Kutaka Kumuua, Adai CHADEMA Wana Chumba Cha Mateso, Aonyesha Alivyopigwa na Kuumizwa

0
0
Mlinzi wa DK Slaa
Aliyekuwa mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya chama hicho.

Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari leo, amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.

Amesema kutokuelewana kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho kulianza pale alipoanza kupishana kwa maneno kati yake na mke wa Dk. Slaa ambapo Slaa alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa Dk. Slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya Jumamosi aliitwa Makao Makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuta vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke, kumtesa, kumvua nguo, kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha CCM ili amuue katibu mkuu dk. Slaa.

“Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii, tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”

“Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa Slaa kwa muda wa miaka mingi sana, tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki” amesema Kagenzi

Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefichua mipango ya kitesaji na kigaidi inayofanya na CHADEMA huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.

“Jamani hiki chama ambacho kina ndoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia? Maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu na kuweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote, eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma, jamani nawaambia mimi hanitumi mtu” ameedelea kusema Kagenzi.

Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .

Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.

Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa

Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawahi kupokea pesa hizo.

Hatua atakazochukua

Kagenzi amesema hatua iliyobaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubiri kesi mahakamani ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya kiuaji.

Maneno Haya ya Lulu ,Yachukulie Kama Changamoto

0
0
Mrembo na staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe  mzuri ambao  kiukweli unaweza kukupa nguvu zaidi kufikia malengo yako kama mtu unaejitambua.

 “The more they try to slow you down on the road of purpose, the faster you have to go..!
You only meet opposition when you're going the right way”

Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema “kwa jinsi wanavyozidi kujaribu kukurudisha nyuma katika njia ya mafanikio ndio inakubidi uongeze mwendo…..na utapingigwa tu pale unapokwenda njia sahii”.

Kwa upande wangu, huu ni ujumbe mzuri sana ambao ningependa niulete hapa  kwenu wadau ili nanyinyi muuchukue kama changamoto ya kufanyikisha mambo yako.

Asante sana Lulu kwa maneno haya mazuri.

Mzee wa Ubuyu
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images