Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Mashabiki Wamshabulia Aunty Ezekiel kwa Nguo Anazovaa!

$
0
0
Baadhi ya mashabiki  wa staa wa Bongo Movies, Aunty Ezekiel wameonyesha kuchukizwa na nguo anzaovaa staa huyo ukizingatia kwasasa ni mjamzito.

Kwa mara kadhaa Aunty amekuwa akibandika picha mtandaoni akiwa amevaa nguo ambazo "followers" na mashabiki wamekuwa wakisema hazifai kuvaliwa na mwanamke mjamzito, kitu ambacho aunty mwenyewe na baadhi ya mashabiki wamekuwa mara zote wakisema ni sawa kitu ambacho mara zote husababisha mabshano na hadi kutoleana lugha chafu.

Mbali na wengi kusema nguo anazovaa zinambana sana tumbo kitu ambacho sio kizuri wa ustawi wa kiumbe kilichopo tumboni,wapo wailosema mavazi hayo hayana heshma kwani kwa hali yake ya sasa inabidi ajistili  nasio kujiweka wazi wazi kama anavyofanya sasa.

Mimi sio mjuzi sana wa maswala ya nguzo za wamama wajawazito ndiomana nimezileata hapa baadhi ya picha hizo ili wenye uelewa wa maswala haya watujuze kam ni sawa au sio sawa...kwani kuna baadhi ya dada zetu wanapenda sana kuigaaaaaaa.

Mtoto wa ajabu azaliwa Hospitali ya Mkoa Shinyanga

$
0
0
Maskini Huyu mtoto amezaliwa usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya serikali ya Shinyanga akiwa na Vingo sehemu zisizo sahihi na baada ya muda alifariki Dunia

Najiuliza kwa Sauti Je nini Sababu za Watoto Kama Hawa ? Kwani matukio ya wazazi kujifungua watoto wa ajabu yamekuwa mengi nyakati hizi....

Masogange Shows off her goodies while doing physical exercises

$
0
0

Masogange Socialite From Tanzania Showing off her goodies while doing physical exercises in South Africa....

Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

$
0
0
“Watanzania wenzangu, naombeni leo tujiulize: mitandao ya kijamii ina kazi gani kama sio kuelimisha, kuendeleza na kunufaisha jamii?

Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu, tushashabikia vya kutosha.

Imefika hatua ya kunyanyuana, sio kushushana. Kuelimishana, sio kusemana. Kupeana moyo, sio kukatishana tamaa.

Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.

Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.

Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!

Wewe je? “.-Wema  mwenye followers zaidi ya laki nne mtandaoni ameandika haya na kuungwa mkono na mashabiki wengi na hata wale wanomdisi.

Asante sana Wema, ujumbe umefika.

Kwa jina naitwa Mzee wa Ubuyu  na leo hii nimeamua kesho yangu haitakauwa kama jana yangu.

11.03.2015 -  Tags:  WEMA

Meseji za Mapenzi za Kajala na Bwana Aliyekuwa na Wema Sepetu Zanaswa

$
0
0
BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala Masanja kudaiwa kumuibia bwana aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu na kukosa ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi wa SMS za mapenzi za Kajala na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo zimenaswa, Amani linakumegea mchongo kamili

Chanzo makini kilichokuwa karibu na Kajala na kigogo huyo, kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa meseji za Kajala kupitia kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu katika penzi na Wema kisha kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.

“Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi nikafanikiwa kupata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema, kama vipi niwatumie,” kilisema chanzo chetu.Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa akiitana baby na kigogo huyo, huku wakiwa ‘dip kimalovee’ kiasi cha kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala mahitaji mbalimbali.

“Jamaa walikuwa wanapika na kupakua, kigogo alikuwa akigharamia kila kitu, kuanzia misosi ya nyumbani, usafiri wa location na hata kwa wazazi wa Kajala, alikuwa anatuma fedha,” kilisema chanzo hicho.

Mwanahabari wetu alifanikiwa kuzinasa SMS hizo na kujionea zikiwa na majibizano ya muda mrefu huku zikitaja pia marafiki wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.

Baada ya paparazi wetu kumwagiwa SMS hizo, alimvutia waya Kajala ambaye alizikana SMS hizo na kuomba atumiwe ndipo atoe jibu ambapo mwandishi wetu alifanya hivyo lakini hakujibu chochote na hata alipopigiwa tena, hakupokea.
GPL

Majina ya Abiria Wote Waliokuwa Katika Ajali iliyouwa Watu Iiringa Jana

$
0
0

"Ni ajali ambayo haijawahi kutokea katika maeneo haya," ni baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wakazi wengi wa mjini Mafinga na vitongoji vyake, ambao jana walishuhudia ajali  katika historia ya mji huo.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26)  na basi aina ya Scania namba T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).

 

Wakati lori lilikuwa likielekea Barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.

 

Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 42 wakiwemo 40 waliokuwemo katika basi na wawili katika lori hilo, ilitokea katika eneo la Changarawe takribani kilometa 5 kutoka mjini Mafinga, mkoani Iringa, katika barabara kuu ya Mafinga-Mbeya.

 

Kati ya waliokufa yupo dereva wa basi hilo, huku dereva wa lori akijeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa na kitu kama nondo shingoni mwake.

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi saa tatu na nusu.

 

Kamanda Mungi alisema jeshi lake kwa kushirikiana na hospitali za Mafinga na Mkoa wa Iringa wanaendelea kutambua majina ya watu waliokufa na  majeruhi.

 

Kamanda Mungi alisema taarifa zao za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara. Mungi alisema lori na basi hilo yaligongana uso kwa uso wakati madereva wake wakishindana kuwahi kuchepuka moja kati ya mashimo makubwa yaliyopo pembezoni na katikati mwa barabara hiyo katika eneo hilo.

 

Baadhi ya watu waliotajwa kuwepo katika basi na lori hilo ambao hata hivyo hawakuweza kufahamika mara moja, nani kafa na nani kajeruhiwa ni pamoja na Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni na Frank Chiwango.

 

Wengine ni Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine, Mwajengo, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri.

 

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge na Juma Sindu.

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

 

Habari kutoka Mbeya zinaeleza kuwa wakati basi hilo linaondoka kituoni abiria waliokuwepo kwenye basi hilo walikuwa ni 37 ambao ni: 

 

Baraka Ndone  ambaye ni dereva, Yahya  Hassan ambaye ni kondakta, Esther    Emmanuel, Henry Lugano, Lusekelo Enock, Jeremia  Watson, Hamad, Olga Solomon, Neto, Theresia Kaminyoge, Frank Chiwanga, Luteni Sanga, Alfred Sanga, Doto Katunga,  Juliana Bukuku, Esther Fidel,  Paulina Josia.

 

Wengine ni Iman Mahenge,  Catherine Mwate, Mathias Justine,  Rebeka Kasambala,  Upendo William, Mbamba Ipyana,  Ndulile Kasambala, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule, Mustafa Ramadhani,  Musa, Omega Mwakasege, Shadra Msigwa, Lucy Mtanga, Charles Mweisonga, Martin Haule, Dominick Mashauri, Kelvin Ebadi, Juma Saidi,  na Nicko.

 

Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA

$
0
0

Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Kauli ya hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kumvua uanachama Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema kutokana na hali hiyo, Zitto bado ni mbunge halali wa Kigoma Kaskazini na kwamba anapaswa kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

Dk Thomas Kashililah, amebainisha kuwa endapo Bunge litapata taarifa rasmi ya Chadema kumvua uanachama Zitto, lazima Bunge hilo lifanye kwanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndipo litoe uamuzi.

Pia amesema sakata la mbunge wa Bunge hilo kuvuliwa uanachama na chama chake si la kwanza, kwani tayari kuna mbunge aliyevuliwa uanachama na chama chake lakini Bunge hilo halikumvua uanachama wake baada ya kumaliza uchunguzi wake. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo.

“Utaratibu ulivyo, chama huliandikia Bunge kuhusu kumvua uanachama mbunge na Bunge kabla ya uamuzi wowote hufuatilia kwanza sababu za kuvuliwa uanachama huo, ili kujiridhisha kama zilikuwa halali au la,” alisema Kashililah.

Alisema baada ya hapo Bunge hilo huwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili ofisi hiyo ya msajili iweze kupitia Katiba ya chama husika na kupitia sababu za chama husika zinazoweza kumvua uanachama mwanachama wake na kama kweli zimekiukwa.

“Baada ya suala hilo kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, Spika wa Bunge, hutoa uamuzi baada ya kuchunguza na uamuzi huo, hupelekwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi,”alisisitiza.

Aidha alisisitiza: “Si lazima Spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa mbunge husika kwani kama haikuwa halali kwa mbunge huyo kuvuliwa uanachama, Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika,” alisema.

Alisema Spika Anne Makinda katika kipindi chake alishawahi kutoa uamuzi wa kubatilisha mbunge fulani kuvuliwa ubunge hata baada ya chama chake kumvua uanachama.

Akizungumzia suala hilo, Zitto, alisema kwa upande wake bado ni mbunge na anaendelea na kazi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) hadi pale atakapopatiwa taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na ubunge wake.

“Naendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea, sina taarifa yoyote ya kuvuliwa uanachama wangu wala ubunge, habari hizi nimezisikia kwenye vyombo vya habari, sijaitwa na Mahakama kuambiwa kinachoendelea,”alisema Zitto.

Alisema kwa sasa anaendelea kuongoza kamati hiyo na jana alikutana na menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo kamati yake inatarajia kukutana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watakutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwanasheria Mkuu kuhusu mapato ya akaunti za madini.

Aidha alisema pamoja na kuendelea kama kawaida na shughuli zake za kibunge bungeni, pia anatarajia kesho kwenda Kigoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo jimboni kwake, kabla ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza rasmi Machi 17, mwaka huu.

Alisema kwa upande wake, anachukulia suala hilo kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika medani za siasa nchini na duniani kote.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama hicho kinajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, ikiwemo kuandaa na kuiwasilisha wakati wowote barua inayomvua uanachama Zitto, ili suala hilo lifanyiwe uamuzi mapema.

“Kwa sasa suala hili la Zitto limewaingia Watanzania wengi, sasa sisi tunataka tulifanyie kazi mapema, ili uamuzi ufanywe mapema na suala hili liishe. Kuna mambo mengi ya maana yanahitaji kujadiliwa kitaifa kama vile masuala ya uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa BVR,” alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye juzi alitangaza kuwa chama hicho kimemvua uanachama mbunge huyo, jana alimwambia mwandishi kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho litaifikisha taarifa ya Zitto kuvuliwa uanachama kwa Kamati Kuu ya chama ifikapo Mei, mwaka huu.

Alisema, "Kutokana na utaratibu uliopangwa wa Kamati Kuu kukutana kila baada ya miezi mitatu, suala la Zitto litasubiri kikao kingine cha kawaida cha kamati hiyo kitakachokaa mwezi Mei. Kikao kilichopita kilikaa Februari mwaka huu".

Kwa maelezo ya Lissu, baada ya hapo ndipo wataiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuijulisha kuwa Zitto si mwanachama wa chama hicho tena au la.

Aunty Ezekiel Amejifungua?!!

$
0
0

Muigizaji Aunty Ezekiel kwenye ukurasa wake wa Istagram jana usiku aliweka video ikimuonesha akiwa Hospitali na akiwa amembeba mtoto mkononi ilivuma na katika picha zake zote hiyo ndo ilipata comments nyingi zaidi watanzania wakimpongeza kwa kujifungua,  Mose Iyobo ambaye mara nyingi ametajwa kuwa ndiye baba wa mtoto huyo, amesema  Aunty yuko location wanashoot movie mpya aliyocheza na msanii Dude.

Ni movie kweli au kajifungua?

Yanga yagomea ushindi wa Simba FIFA

$
0
0
Yanga jana wameliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga ushindi wa Simba walioupata dhidi yao Jumapili iliyopita wakitaka wanyang’anywe pointi tatu na kama TFF itashindwa kufanya hivyo basi wameweka wazi dhamira yao ya kulipeleka suala hilo mpaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutafuta haki yao.

Kikubwa kilichoifanya Yanga kufikia uamuzi huo na kuitaka Simba ipokonywe pointi hizo ni baada ya Simba kumchezesha mchezaji wao, Ibrahim Ajibu mwenye kadi tatu za njano.

Awali kabla ya mchezo huo, Yanga ilituma barua TFF kutaka kujua ni kanuni ipi inamruhusu mchezaji mwenye kadi tatu kuchagua mechi za kucheza wakati ipo wazi kwamba anapaswa kukosa mechi zinazofuata kisha akaendelea na nyingine, lakini ilikosa majibu na ndipo ikaamua kuandika nyingine iliyotumwa jana iliyojumuisha na azimio jingine la Simba kunyang’anywa pointi tatu.


Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alifafanua kuwa endapo kama wao wangeshinda mchezo huo basi ingebidi Simba wapigwe faini lakini kwa kuwa wameshindwa, basi inapaswa Simba wanyang’anywe pointi tatu ambapo alisisitiza kuwa katika hilo hawatarudi nyuma mpaka wapate haki yao stahiki.

“Tumeandika barua leo (jana) mapema na tayari tumeshaipeleka TFF kuhusu kutaka Simba kupokwa pointi walizozipata kwenye mchezo wetu wa Jumapili kwa kuwa walimchezesha Ibrahim Ajibu, mwenye kadi tatu za njano, kitu ambacho ni kinyume na kanuni za soka zinavyotaka.

“Na kama itatokea TFF watakosa jibu stahiki la kutupa au kushindwa ‘ku-solve’ kesi hii, basi sisi tutasonga mbele na tutakwenda Caf (Shirikisho la Soka Afrika) na kama hapo pia itakosa ufumbuzi basi tutafika mpaka Fifa, ilimradi tuhakikishe haki yetu inapatikana.

“Kama ingekuwa tumeshinda sisi siku ile, basi Simba lazima ingepigwa faini lakini kwa kuwa wao wameshinda basi adhabu yao ni kupokonywa pointi tatu, hata mechi zao walizocheza na Stand United na Prisons pia zinapaswa kupokonywa pointi kwa kuwa walikiuka kanuni kama hii.

“Kitu cha kujiuliza ni kwamba kanuni zinawezaje kubadilishwa bila ya wahusika ambao ni timu za ligi, kuwa na taarifa isipokuwa Simba pekee.

Sikiliza na Download Linex Ft. Diamond Platnumz - Salima

$
0
0

Sikiliza ama Download Wimbo mpya wa Linex Akishirikiana na Diamond Platnumz..Wimbo unaitwa Salima Huu Hapa Chini ..Ukishasikiliza Toa Maoni yako:

Nimemharibu Mpenzi Wangu ila yote Kasababisha Mwenyewe

$
0
0
Kwa muda wa miezi 3 sasa nipo kwenye mahusiano na dada mmoja toka kule visiwa vya karafuu,ni mzuri ana sifa zote ila tatizo lake huja wakati wa faragha,toka nimekuwa nae kwenye game yeye ananipa kinyume na maumbile tu haijalishi nitapiga mara ngapi.

Kiukweli na mimi nimezoea ingawa namwonea sana huruma ila yeye anadai nisijali niendelee kufanya hivyo, sasa tatizo limekuja anadai nipeleke barua kwao, lakini kwa jinsi nilivyomfanya kinyume na maumbile napata mashaka kuwa nikishamuoa haitakuja kuwa aibu kwangu.Je kuna uwezekano wa kule back kwake kukarudi hali ya kawaida.

Ushauri wenu wakuu

Aunt Ezekiel Akanusha Taarifa za Kujifungua

$
0
0
Aunty Ezekiel
Baada ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel kujifungua, mwanahabari wa GPL ametia timu nyumbani kwa Aunt na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na taarifa za kujifungua si za kweli.

Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande cha video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote ambapo mashabiki wake walimiminika na kuanza kumpongeza wakijua tayari kajifungua.

Akiongea na mwanahabari wa GPL Aunt amesema kuwa , hicho ni kipande cha mojawapo ya filamu yake aliyocheza siku nyingi. Na taarifa zilizoenea mitandaoni kuwa kajifungua si za kweli.

Kwa upande wa pili kijana anaesemekana ndio alimpa ujauzito huo, Mosesi Iyobo ambae ni mcheza dansi wa mwanamziki Diamond alibandika mtandaoni picha ya mama akiwa amebeba katoto (itazame hapo juu) na kupeleka watu kumpa pongezi pia.

Juma Jux Showing His House, The Whole House This Time...Tuone Kama na Hii Mtaponda!

$
0
0
Some Weeks Ago Juma Jux aliweka Picha ikionyesha kipande cha nyumba yake , picha hiyo ilitafsiriwa vibaya na  baadhi ya mashabiki wake na wengine kusema anajenga gala...Sasa leo amepost ikiwa inaonekana vizuri na kusema haya

Major plans for my humble abode - home recording studio, gym and pool and maybe a puppy for bae. God is good! Planning ahead #RealEstate #Lifestyle #Property #Blessings #AfricanBoy


Picha: Ni Wema Sepetu na Ommy Dimpoz wakipeana 'Kiss' mdomoni huku wakiwa kwenye hali ya mahaba mazito!

$
0
0
Hatimaye ile project iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu sasa kesho ndio siku rasmini itakayo toka. Ambapo Ommy Dimpoz ame share picha ikimuonyesha akiwa na Wema Sepetu kitandani kama wana peana kiss mdomoni nakuandika "Tomorrow...Saa 4 Asubuhi kwenye TV na Radio zote Ndani na Nje ya Nchi....#WANJERA"
Lakini pia hata Wema Sepetu ame share picha ikionyesha wamesimama na Ommy Dimpoz wakiwa kwenye hali ya kimahaba na kuandika "Stay tuned... tomorrow @10 am... Kweny radio na Tv zote....(Local & International) I cant wait... Finally...!!Wanjera..!!!".

Sipendi Watu Wanavyoniambia Nina Kalio Fake, Wakati Nimebarikiwa na Mungu

$
0
0
Admin , Sipendi Jinsi watu wanavyonisema kila nipitapo eti makalio yangu ya Mchina wakati mimi nimezaliwa hivyo hivyo toka nikiwa mdogo makalio yangu yalikuwa makubwa , kama unabisha uliza hata nilio soma nao shule ya msingi , Ki kweli sipendi hiyo tabia ya watu kila wakiona mtu amejaliwa basi eti ni fake wengine tumezaliwa hivyo jamani ..Khhaaaa Wabongo Acheni Ushamba

By Camila, Sinza

Polisi Wamkamata Moza Kwa Kudaiwa Kumdhalilisha Mtangazaji wa TV1 Edzen kwa Video ya Uchi

$
0
0
Polisi wamemkamata moza kwa kudaiwa kumdhalilisha mtangazaji wa kituo TV1 ezden jumanne...uchunguzi ukikamilika ataburuzwa mahakamani muda wowote...moza aliyekuwa mpenzi wa ezden na kuachwa alimrecord video hiyo kipindi cha mahusiano yao...moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu oysterbay polisi....ezdee alisema mimi ni mtu ninayejiheshimu so kitendo alichokifanya hakunitendea haki na amenidhalilisha...moza amedaiwa kufanya hivyo baada ya kuachwa ili kumkomoa dida...mwisho wa kunukuu.....INASEMEKANA MOZA KAMUANGUKIA EZDEE KUMUOMBA SAMAHANI NA YAMEISHA SIJUI........MIMI BINAFSI NASEMA HIVI HAKUNA ASIYEJUA MITANDAONI WASICHANA NDIO WANAONGOZA KWA KUDHALILISHWA KWA KURECORDIWA AU KUPIGWA PICHA CHAFU...SIWEZI KULAUMU MOJA KWA MOJA ZINAPOTOKEA PICHA CHAFU ZA MTU SABABU WENGINE WANARECORDIWA AU KUPIGWA PICHA WAKIWA HAWANA TAARIFA KAMA HIVYO EZDEE HAKUWA NA HABARI SO MTU AKIPANIA ANAKUFANYIA TU UBAYA....SASA IFIKE WAKATI WASICHANA MJITAMBUE USIKUBALI KUPIGWA PICHA YA UTUPU HATA UKIGUNDUA UMEPIGWA BILA KUJIJUA KAMSHITAKI FASTA MUHUSIKA AWE BADO MPENZIO AU MMEACHANA PELEKA POLISI FASTA MTU ANAYEKUPENDA HAWEZI KUKUFANYIA HIVI....HATA KAMA MMEACHANA HANA HAKI YA KUKUDHALILISHA HIVYO...MMEONA WANAUME WALIVYO NA MSIMAMO??....MKIWA WAOGA MTAENDELEA KUSHIKA RECORD YA KUDHALILISHWA....

Usipojipanga Nitakupanga

Makalio Makubwa Yampaisha Chat Agness Masogange Marekani na Nigeria..

$
0
0
Staa  aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na makalio yake, Agnes Gerald ‘Masogange’ sasa amepaa kimataifa zaidi na kuwa  gumzo hadi Marekani baada ya hivi karibuni mtandao mmoja wa watu maarufu nchini humo kumpa shavu.

Masogange aliripotiwa na mtandao wa Media Take Out na kumuelezea kuwa ni staa mwenye makalio makubwa barani Afrika akitokea Tanzania.Mbali na maelezo kibao ya kusifia wowowo lake, mtandao huo uliposti picha kibao za mwanadada huyo ambaye sasa anaishi Afrika Kusini akiweka mapozi tofauti ya kimitego.. Baada ya Mtandao huo Mkubwa kumuandika Mitandao mingine mikubwa ya Nigeria Kama Aquavibes nao walimuandika

Hata hivyo, baadhi waliponda maelezo hayo kwa kusema kuwa, Afrika ina mabinti wenye maumbo tata kuliko Masogange hivyo mtandao huo ungefanya uchunguzi kabla ya kuripoti habari hiyo.

Video ya Ommy Dimpoz na Wema Sepetu Iliyoleta Ngumzo Hii Hapa..Wanjera

$
0
0
Ommy Dimpoz na Wema Sepetu walichukua headlines kwa zaidi ya mwezi mmoja kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha zenye utata zikiwaonyesha wakiwa mapenzini na ikapelekea watu kujua labda Ommy ameamua kurithi kiti cha Diamond Platnumz.
Kumbe bwana ilikua ni video mpya ya Ommy aliyokwenda kuifanya South Africa na imemuhusisha Idriss wa BBA pia, itazame hapa chini alafu uniachie comment yako umeionaje mtu wangu, uigizaji wa Wema, Idriss na idea nzima ya video.

Wakamatwa na Viungo vya Albino Mwanza

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewakamata waganga wa kienyeji 55 wakiwa na viungo vya binadamu vikiwamo meno na nywele vinavyodaiwa kuwa ni vya watu wenye albino. Vitu vingine walivyokutwa navyo ni ngozi ya simba, nyumbu, mamba, vibuyu, njuga, vioo, shanga na debe tatu za bangi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema waganga hao walikamatwa katika wilaya za Mkoa wa Mwanza kwenye msako ulioanza juzi. Alisema katika msako huo wamefanikiwa kuwakamata waganga hao wanaodaiwa kupiga ramli chonganishi zinazosababisha kuchochea matukio ya mauaji kwa albino na vikongwe.

“Katika msako wa Jeshi la Polisi ulioanza juzi tumefanikiwa kuwatia mbaroni waganga wa jadi 55 ambapo kati yao tumewakuta na nywele, meno za watu wenye albino waliouawa katika matukio tofauti mkoani hapa,” Mlowala.

Kamanda huyo wa Polisi alisema waganga hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwamo kumiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria pamoja na viungo vya binadamu.

Mbali na tukio hilo, taarifa kutoka wilayani Misungwi zinaeleza kuwa watu wanne wamefikishwa kortini mjini hapa kwa tuhuma za kuuza mafuta maalumu ya ngozi yanayotumiwa na watu wenye albino. Mafuta hayo yenye thamani ya Sh milioni tano, ambayo yalitolewa na Hospitali ya Bugando kwa watoto wenye albino wilayani humo.

Chanzo. Gazeti la Mtanzania

Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kimapoteza Wanafunzi Watano Katika Ajali ya Basi Iringa..Majina Haya Hapa

$
0
0


Takribani wanafunzi watano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wamepoteza maisha katika ajali iliyotekea juzi
Wanafunzi hao walikuwa wakirejea chuo baada ya likizo kuisha.
WALIOFARIKI WATANO NI
1. CHIWANGU DIDIMO (mwaka wa 3)
2. KILLEO ERICK ( mwaka wa 3)
3. SOSTEN DAUD (Mwaka wa 3)
4. WATSON JEREMIA (Mwaka wa 2)
5. MBAULE FRANK (Mwaka haujajulikana)
MAJERUHI WAWILI
1. TUPATE MOSIGWA (Mwaka wa 1)
2. RAPHAEL NELBERT (Mwaka wa 1)
Tunawapa pole wafiwa na Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi ..
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images