Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Ommy Dimpoz:Diamond si yupo na Zari au? Sidhani kama amemind mimi kufanya kazi na Wema

0
0
Mwanamziki Ommy Dimpoz ameyasema hay oleo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga picha za kuutangaza wimbo huo.

Ommy alisema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.

 “Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”

Watu Waanza Kuhoji Mimba ya Zari..Wadai Siku Zinaenda na Hawaoni Chochote

0
0
Nimekutana na Huu Mjadala Jamii Forums Mdau mmoja Ameuliza kuhusu Mimba ya Zari aliyepewa na Diamond.......

Mdau Alifunguka Hivi:

'waungwana ile mimba ya mwana bongo fleva platinum kwa mke wake zari imefikia wapi?
Nauliza hvyo kwakua siku zinavyo zidi kwenda mzigo hauonekani au ni macho yangu mimi
Samahanini kwa usumbufu'

Baada ya Mtoa Mada kuandika hayo hizi ni Baadhi ya Comments walizotoa:

-Hahaha hapo sasa inatia mashaka sna

-afu zari mbona ana block watu saana mimi mmoja wapo kani block

-Hahaaa...hapo ndo kwenye mashaka

-mh mawifi na mashemeji wa Tanzania mna gubu sana....

-Si vibaya kutaka kujua, ukishakua celeb. ni kawaida raia kufuatilia each of ur biz., hata unavyotiana.

-Wengi wenu ni timu mama Ubaya.!

-jana tuu katoka kuwaambia amebebewa na mama zao, sasa sijui hawakielewa??

-mtoa mada jaribu kufikiri hata kwa kutumia akili za kukopa,, mimba ya Zari ww inakuhusu nn??

Wema Sepetu Afunguka Haya 'Mume wa Zari Anataka Kunioa'

0
0
Wema Sepetu na Mume wa Zari South Africa
MAMBO hadharani! Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa, Risasi Jumamosi lina full stori.

WALIANZIA KUKUTANA SAUZ
Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.

“Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.”

ALIBANA, AKALEGEZA
“Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia lolote.

“Tulikubali, wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.

IVAN AANZA ‘KUIMBISHA’
Akizidi kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya muhimu.

Msikie Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”

AHADI  NI  MAGARI, NYUMBA
Wema alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali.
Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).

Wema anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya hivyo.”

ATAKIWA KUTOICHEZEA BAHATI
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa.
“Wema kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu. Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi chenga,” kilisema chanzo hicho.

WEMA KUWA KAMA MCHARO?
Akizungumzia suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko alivyo sasa.

“Jamaa yupo serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu kama mcharo,” alisema rafiki huyo.

KINACHOMPA WASIWASI WEMA
Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).

“Kwa hiyo Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara, biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo.

Chanzo:Globalpublishers/Mateja

Penny Adaiwa Kunywa Sumu Kisa Kunyang'anywa Bwana na Shosti Yake

0
0
MTANGAZAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana.

Kwa mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa.

“Diana kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha madai hayo.
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny.

Chanzo:Globalpublishers

Tanzania Yapaa Wiwango vya Mpira FIFA

0
0
Tanzania imepaa kwenye viwango vya kila mwezi vya FIFA kwa kupanda kwa nafasi saba (7)  katika viwango vya shirikisho hilo la kimataifa vilivyotolewa leo.
Rwanda ndiyo imetia fora kwa kupanda kwa nafasi nane (8) na kuongoza Afrika Mashariki ikiwa nafasi ya 64 duniani ikifuatwa na Uganda (74), Tanzania, Kenya (118) na Burundi (126).

Algeria wanaendelea kushikilia usukani Afrika wakifuatwa na Ivory Coast, Ghana, Tunisia, Senegal, Cape Verde, Nigeria, Guinea, Congo DR na Cameroon wanaokamilisha 10 bora barani.

10 bora duniani inaendelea kuongozwa na Ujerumani wanaofuatwa na Argentina, Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ureno, Ufaransa, Uruguay na Italia waliopanda kwa nafasi mbili na kuitoa Hispania.

God Will Forever Bless SONKO - He Did This for OJWANG After Everyone Abandoned Him-KENYA

0
0

Philanthropic Nairobi Senator, Mike Mbuvi Sonko’s Rescue Team has once again lived up to its expectation of saving the lives, not only for Nairobians, but all Kenyans.

This is after it rescued Mr. Benson Wanjau Karira, popularly known as Mjee Ojwang, one of the pioneers of Kenya’s TV comedy who has graced our screens for over three decades.

The Sonko Team rescued Mzee Ojwang, who was suffering from depression and visual impairment, and rushed him to hospital when his condition got worse.

Ojwang got into depression when he was fired from KBC together with the comedy crew where they spent almost all their lives building a career that hardly bore fruits.

 Sonko sent a team of doctors and ambulances to take Mzee Ojwang to Losesho Hospital where he underwent specialized check up and treatment, including surgery, and is expected to regain his sight and health.

The Nairobi Senator also agreed to settle his hospital bill and promised to present the matter to President Uhuru Kenyatta so that the Government can take care of the veteran comedian and other Kenyan heroes who have done this country proud in various fields.

He expressed disappointment that the Government had left its heroes like Ojwang to languish in poverty.


The Kenyan DAILY POST

Is Wema Sepetu going back to school?...see this photo

0
0

Is Wema Sepetu going back to school?...Watch this Space ......

Wema Sepetu Posted the Above Photo and wrote:

"Kupendeza ni muhimu ila kuelimika ni muhimu zaidi. Je, unajaribu kujifunza kitu kipya kila siku?"

Unahisi Adhabu Gani Inawafaa Waganga ama Watu Wanaohusika na Mauaji ya Albino?

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewakamata waganga wa kienyeji 55 wakiwa na viungo vya binadamu vikiwemo meno na nywele vinavyodaiwa kuwa ni vya watu wenye albino. Inasemekana waganga ngio huagiza watu viungo vya albino ili wawafanyie dawa.

Kwa maoni yako, watu hawa wanaosababisha ndugu zetu albino wanauwawa, unahisi adhabu gani inawafaa?

Ma Group ya Whats app ya Mahusiano (Makungwi) Yanavyoharibu Ndoa na Kudhalilisha Utu

0
0
Hey guys...naomba nimalizie kutoa dukuduku langu kuhusu Makundi ya Mahusiano sijui makungwi kwenye whatsapp groups....asilimia 80 yanatumika kuharibu ndoa za watu au kuvunja kabisa mahusiano ya mapenzi au hata urafiki! humo watu wanafundishana kila kitu... upuuzi na kuna wasichana/wanawake wajinga wanapenda kuhurumiwa wanaanza kuongea siri zao za ndani....then watu wana copy maongezi na kusambaziana...matokeo yake unalia umedhalilishwa mara huamini tena mtu au yanamfikia mhusika lkn chanzo ni wewe.

Yapo makundi ambayo ni mazuri ila huwezi kujiingiza kichwa kichwa eti umeumizwa na boyfriend unalia lia kwenye whatsap groups kwani huyo mumeo? Yaan unajifunuaaa maisha yako yote kwa watu ambao si mamako au ndugu yako. Jaman!!! Wengine mnafundishwa jinsi ya kufanya mapenzi na kuweka madude kibao sehemu za siri...seriously? ?? Hapo hujaolewa..baadae ukikutwa na kansa ya kizazi? Jitihada zoote halafu asikuoe?? Utasingizia kungwi wa whatsapp ukute hata hujawahi kuonana naye?

Kama unataka kufundwa muulize mzazi wako au mtu mzima au jichagulie mtu mmoja utakayemwamini sana hakuna siri zaidi ya watu wawili, soma vitabu mbali mbali khs mahusiano au hapana soma vitabu vya dini vimeeleza kila hatua ya kuishi na mwenzi wako. Mnatozwa pesa huko whatsap halafu mambo bado hayaendi unavyotaka unabaki kulalamika...tatizo ni UFAHAMU wako. Samahan simharibii mtu biashara yake ila acheni kutumia madhaifu ya wengine kama dampo la kuwapoteza zaidi, kwanini usiwasiliane na mtu binafsi mpaka kumuunganisha kwenye magroup?

Jifunzeni kutunza siri zenu. Usimuamini kila mtu.

Mrekebisha Tabia

Mwanamuziki Matonya Ataja Sababu za Kwanini Ngoma zake Hazihit Kama Zamani

0
0
Mwanamuziki Matonya
Matonya amesema sababu kubwa iliyomfanya apotee kwenye muziki na nyimbo zake za sasa kutofanya vyema kama mwanzo ni kukosa uongozi mzuri wa kumsimamia.

Matonya ameambia Bongo5 kuwa muziki wa sasa hivi upo tafauti na ule wa zamani uliokuwa hauhitaji mambo mengi kama muziki wa sasa.

“Tatizo kubwa kadri siku zinapozidi kwenda wasanii tunazidi kuwa wengi, zamani wasanii walikuwa wanafanya kazi ndogo kwenye muziki wao tofauti na muziki wa sasa ambao kila msanii anataka kuwa juu ya mwenzake,” amesema msanii huyo. “Pia kazi zangu nilikuwa nazisimamia mwenyewe kitu ambacho ilifika wakati hali ikawa ngumu baada ya kushindwa kufanya kila tu. Ila sasa hivi nimejipanga kikamilifu kuna kampuni inaitwa 360 ni ya kwangu lakini nimewapa watu kazi mbalimbali za kusimamia muziki wangu kwahiyo sasa hivi tayari nimeanza kuona utofauti kwenye mapokezi ya ngoma zangu, hii ni dalili kila kitu kitakaa sawa siku za usoni,” ameongeza.

Kwa upande mwingine, Matonya amesema sasa hivi amerudisha mahusiano yake na Tunda Man ambaye walikuwa hawaelewani.

“Tunda hana tatizo na mimi, yule ni mdogo wangu na soon kuna kazi inakuja nikiwa naye, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula.”

Zitto Achukua Maamuzi Magumu..Akutana na Wazee wa Jimbo lake na Kusema Haya

0
0

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Zubery kabwe Leo Alikutana na Wazee wa Jimbo Lake na Kutoa Maamuzi magumu mbele ya wazee hao kama hatogombea tena Ubunge kwenye jimbo hilo alilolitumikia kwa muongo moja (miaka 10) huku wazee wakimbariki achukue maamuzi  yanayofaa kulingana na hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa.
Katika page yake ya facebook amepost ujumbe huu kama unavyosomeka hapa chini:


Kinana Afunguka Urais ..Lowassa safi, Nyalandu Anazurura Tu

0
0
Kinana
Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.

Akiwa Kondoa, Kinana alitumia muda mwingi kujibu kilio cha wananchi wanaosumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kumponda Waziri Nyalandu kuwa anazurura bila kushughulikia matatizo ya wananchi, lakini saa chache baada ya kuwasili Monduli alimsifu Lowassa kuwa ni kiongozi shupavu.

Tayari Nyalandu ameshatangaza nia ya kugombea urais, wakati Lowassa, mmoja wa wanachama wa CCM wanaotajwa sana kwenye kinyang’anyiro hicho, hajatangaza uamuzi wake lakini anatumikia adhabu ya chama chake kilichomfungia kujihusisha na harakati za uongozi pamoja na makada wengine watano.

Baada ya msafara wa Kinana kuwasili Monduli na kupokewa na viongozi wa chama hicho wa eneo, katibu huyo wa CCM, Kinana alipata nafasi ya kuzungumza machache kabla ya kuanza safari ya kukagua shughuli mbalimbali.

“Hatuna shaka na Monduli kwa kuwa yupo kiongozi shupavu, ndugu yetu Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa (Halmashauri Kuu ya CCM) Nec,” alisema Kinana akiwaelezea wananchi waliokuwapo eneo hilo.

“Wa Monduli mna kiongozi shupavu na mchapakazi. Hongera Bwana Lowassa.”

Baadaye, Lowassa aliwakaribisha akisema: “Mmefanya kazi kubwa sana ya kukijenga chama chetu. Nawashukuru sana, karibuni.”

Naye katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: “Nafurahi kuwa katika jimbo la mzee wangu, rafiki yangu Edward Lowassa. Mapokezi mazuri, bila shaka Arusha mmeamka.”

Kinana amekuwa akitumia sehemu kubwa ya ziara yake kushuhutumu viongozi wa Serikali na hasa mawaziri kwa kushindwa kuwatatulia wananchi matatizo yao na ilifikia wakati aliwataja mawaziri wanne aliowaita kuwa ni mizigo, tofauti na alivyofanya kwa waziri mkuu huyo wa zamani.


Sakatala kuuawa Dk. Slaa lageuka..Wanachama Watatu Wafikishwa Kizimbani

0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kumchunguza Josephine Mushumbusi, ambaye ni mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, anayetuhumiwa kula njama za kumuangamiza.


Uchunguzi dhidi ya Mushumbusi ulitangazwa jana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyia ofisini kwake, Dar es Salaam.


Kamishna Kova alisema kuanzishwa kwa uchunguzi huo ni matokeo ya maelezo ya Khalidi Kangezi, ambaye alikuwa mlinzi wa Dk. Slaa aliyefikishwa polisi baada ya kuteswa na kutekwa kwa tuhuma za kushiriki mipango ya kumuua bosi wake huyo.


Alisema, Kangezi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, katika maelezo yake aliwataja Mushumbuzi na mchungaji mmoja ambaye jina lake halijawekwa hadharani kuwa ndio waliokuwa na mpango huo, lakini yeye aliuzuia


Mbali na wawili hao, Kamanda Kova alisema uchunguzi huo pia utawagusa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, ambaye ametajwa na baadhi ya makada wa chama hicho kuwa mmoja wa wahusika wa mpango wa mauaji ya Dk. Slaa.


Wakati Jeshi la Polisi likitangaza kuanzishwa uchunguzi huo, wanachama
watatu wa Chadema wanaotuhumiwa kumteka na kumtesa Kangezi, jana walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutenda makosa mawili.


Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Janeth Kitali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, majira ya saa nane mchana.
Wakili Kitali alidai mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza la washtakiwa, Diwani Boniface Jacob (32), Mlinzi Hemedi Sabula (48) na Ofisa Utawala wa chama hicho, Benson Mramba, ni kumjeruhi Kangezi, kosa ambalo walilitenda Machi 7, mwaka huu.


Katika shtaka hilo washtakiwa wanadaiwa kwamba tarehe hiyo wakiwa Makao Makuu ya Ofisi za Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, walimjeruhi Kangezi kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.


Aliendelea kudai kuwa tarehe na eneo walipofanya kosa la kwanza, walitenda kosa jingine la kumteka Kagenzi na kumpeleka katika Hotel ya River View Hotel iliyopo Sinza, Kinondoni, Dar es Salaam, kwa nia ya kumnyima uhuru wake


Washtakiwa hao wanaotetewa na Wakili Peter Kibatala na John Malya, walikana mashtaka yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo kesi iliahirishwa hadi Machi 26 mwaka huu, itakapotajwa tena.


Hakimu Lema aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao wanatoka katika taasisi inayotambulika au serikalini isipokuwa walimu. Wadhamini hao walipaswa kusaini hati ya dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10.


Washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa gereza la Keko hadi hapo upande wa mashtaka utakapomaliza kufanya ukaguzi wa barua za wadhamini wao kuona kama wamekidhi vigezo.


Kabla ya kupandishwa kizimbani kwa washtakiwa hao, Kamishna Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa kitendo cha makada watano wa Chadema cha kumuweka chini ya ulinzi na kumtesa kwa muda wa saa 15 Kangezi ni kosa kisheria, hivyo Jeshi la Polisi limewafunguliwa shauri la kushambulia hadi kumjeruhi mlinzi huyo.


Kova alisema Jeshi la Polisi limechukua uamuzi huo kutokana na maelezo pamoja na majeraha aliyoyapata Kangezi mara baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Alisema, ingawa Wakili wa Chadema, John Malya alimfikisha Kangezi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia shitaka la kupanga njama za kumuangamiza Dk. Slaa kwa kumuwekea sumu kwenye maji au chakula, Kangezi kwa upande wake alitoa maelezo ya kutekwa nyara na makada watano wa Chadema ambao walimuweka chini ya ulinzi na kumtesa hadi kumuumiza.


“Tumefungua mashauri mawili, la kwanza ni uchunguzi dhidi ya tuhuma na mpango wa kutaka kumdhuru Dk. Slaa na pili ni uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kumtesa kwa kumshambulia Kangezi na kumsababishia majeraha mwilini mwake,” alisema Kamishna Kova.


Kamishna Kova alisema kutokana na maelezo ya Kangezi, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa waliotajwa na Kangezi kuhusika kumtesa na kumteka.
Alisema baada ya uchunguzi wa awali wa mashauri yote mawili kukamilika, yatapelekwa kwa Wakili wa Serikali ili wote wanaohusika katika suala hilo wafikishwe mbele ya sheria.


Chanzo:Mtanzania

Nini kilivunja Pah One, je watarudiana tena? Navy Kenzo ilianzaje? Hapa yako majibu

0
0
 Pah One 
Ola amesema walikuwa Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kimuziki pia huku wenzao wakijitoa na kuunda Navy Kenzo.

Pah One wamerudi Tz, Ola amesema hawezi kujiunga na Navy Kenzo, kingine alichokisema ni ishu ya beat za album ya kundi hilo kuuzwa kwa wasanii wengine.

Soudy Brown alimtafuta Nahreel ambaye amesema toka kundi hilo livunjike hawajawasiliana ila chanzo cha kuvunjika ilikuwa nidhamu akaamua kujitoa, kuhusu beat kutumiwa na wasanii wengine amesema ni kweli imetokea hivyo ila yeye ndio alizitengeneza na hazikuwa mali ya kundi hilo.
Bonyeza play hapa mtu wangu kusikiliza U Heard la leo March 13…

Binamu Yangu Anapenda Kukaa Utupu Kila Akiniona Sijui Kwanini?

0
0
Mimi ni kijana ninaeishi na kufanya kazi Dodoma, mwezi desemba nilienda kumtembelea binamu yangu alieolewa Dar es salaam, anaishi maeneo ya ukonga.

Kuna matukio yanayotokea na kunishangaza,sasa chumba anacholala binamu yangu na mme wake vinapakana na choo na bafu kama mara tatu hivi wakat naenda bafuni kuoga nilimkuta binamu yangu kaacha mlango wazi huku yuko uchi nikageuka haraka nikarudi nilikotoka.

Mara ya pili binamu yangu alikua ametoka chooni, sasa mimi nilikua naenda kuoga nikamwona bwana akiwa uchi, mara ya tatu tena alikua uchi chumbani huku ameacha mlango wazi cha kushangaza alipogundua hakuhangaika kujisitiri aliendelea na mambo yake,nilipogeuka kumkwepa ndio nikasikia samahani huku yupo very relaxed.

Sijui nifanye nini wadau,msaada tafadhali

Mtoto Albino Anusurika Kuuawa na 'Wawindaji' wa Albino Alipokuwa Mpirani Akicheza..Wenzake Wamuokoa

0
0

Mtoto wa umri wa miaka sita, mwenye ulemavu wa ngozi (albino), anayeishi Kijiji cha Ndoleleji, amekoswakoswa na watu waliokuwa wakimvizia akiwa katika michezo, baada ya watoto wenzake kuchukua uamuzi wa kumlinda.

Taarifa zilizomfikia mwandishi, zilieleza kuwa ‘wawindaji’ hao waliokuwa na gari lililokuwa na vioo vya giza, walionekana wakimfuatilia mtoto huyo Jumamosi ya wiki iliyopita alipokuwa akiogelea mtoni na baada ya kumkosa, wakamfuatilia katika uwanja wa mpira Jumatatu, ambako nako walimkosa.

 

Akizungumza na mwandishi, diwani wa Kata ya Shagihilu wilayani Kishapu mkoani hapa, Mohamed Amani alisema  kumefanyika majaribio mawili ya kutaka kumteka mtoto huyo (jina limehifadhiwa), lakini kwa msaada wa watoto wenzake hayakufanikiwa.

 

Kwa mujibu wa Diwani Amani, Jumamosi iliyopita watu watatu wakiwa kwenye gari hilo, walifika kijijini hapo na kwenda mpaka mtoni, ambako mto huyo mwenye ulemavu wa ngozi alikuwa akicheza na wenzake.

 

Baada ya kufika mtoni, watu hao wote watatu waliteremka kwenye gari na kusogea katika eneo la mto, hatua iliyowashitua watoto wenzake waliokuwa wakicheza wote mtoni.

 

Kwa mujibu wa Amani, watoto hao wenye umri mkubwa zaidi ya mtoto huyo, walitambua hatari iliyokuwa ikimkabili mwenzao mwenye ulemavu wa ngozi na dalili za watu hao waliokuwa hawawafahamu, waliokuwa wakizidi kuwasogelea.

 

Baada ya kuona watu hao wakizidi kusogelea eneo lao la michezo, watoto hao walimshauri mwenzao mwenye ulemavu wa ngozi, akimbilie nyumbani kwao na mtoto huyo akasikia ushauri huo na kurudi nyumbani.

 

“Baada ya mtoto (albino) kukimbilia nyumbani kwao, wale watu waliingia kwenye lile gari na kuondoka,” alisema Amani na kuongeza kuwa hatua ya watu hao kutosema lolote kwa watoto hao lilizidi kuwapa mashaka.

 

Jumatatu ya wiki hii jioni wakati mtoto huyo alipokuwa na wenzake, wakiwemo wale aliokuwa nao mtoni, wakicheza mpira wa miguu katika kiwanja cha kijijini hapo, gari hilo lililoonekana mtoni, lilifika uwanjani hapo na kusimama.

 

Inaelezwa kuwa baada ya kusimama, watu wale watatu walioonekana mtoni walishuka katika gari hilo, wakaegemea gari na kuangalia watoto hao wakicheza mpira, akiwemo mwenzao mwenye ulemavu wa ngozi.

 

“Safari hii haikuwa mtoni, bali katika eneo jingine tena la wazi ambalo mtoto huyo alikuwa akicheza mpira na wenzake… walipofika walisimama nje ya gari lao,”alisema Diwani Amani.

 

Kutokana na hali hiyo, watoto hao walihisi kuna hali ya hatari kwa mwenzao, baada ya watoto hao kuona gari hilo kwa mara nyingine, na watu hao wakiwa wamewasimamia na hawakuwa wakizungumza chochote.

 

Diwani huyo alisema watoto hao walisitisha mchezo wao, na kumtaka mwenzao kwa mara nyingine akimbilie nyumbani kwao, ili kusalimisha maisha yake kutokana na utata wa usalama ulioanza kujitokeza hapo.

 

Akizungumza na mwandishi, mama mzazi wa mtoto huyo, Regina Malando, alithibitisha kurejea nyumbani mara mbili kwa mtoto wake huku akikimbia.

 

Wanafunzi Wakutwa Wakilawitiana Katika Shamba la Migomba huko Moshi

0
0
Wanafunzi  wawili wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ongoma iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamekutwa wakilawitiana katika shamba la migomba jirani na shule hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Jerad Kesi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 5 mwaka huu.

Kutokana na tukio hilo, Mwalimu Kesi alisema mmoja wa wazazi wa watoto hao alivamia shuleni hapo na kuwapiga walimu kwa kile alichosema kuwa walimu hao walikuwa wamemdhalilisha mtoto wake.

“Siku ya tukio, wanafunzi wawili wa darasa la pili na mmoja wa darasa la kwanza walikutwa na mwalimu wangu wakilawitiana kwenye migomba.

“Walipojua mwalimu amewaona, walikimbia na kuacha nguo zao pamoja na yule wa darasa la kwanza. Tulipomhoji yule mtoto aliyebaki alikubali kwamba amekuwa akilawitiwa na kwamba ameshafanyiwa kitendo hicho kama mara saba hivi,” alisema Mwalimu Kesi.

Baada ya wanafunzi hao kutimua mbio, Mwalimu Kesi alisema walirudi nyumbani na baadaye mmoja wa wazazi wao alifika shuleni hapo na kuwashutumu walimu hao kwamba wamemdhalilisha mtoto wake kwa kumvua nguo.

“Baada ya majibizano kati ya walimu na mzazi huyo, mzazi huyo aliwapiga walimu kwa fimbo na kuwajeruhi.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda kutoa taarifa polisi na kupewa RB namba MJ/RB/988/15 kwa ajili ya kumkamata mzazi huyo,” alisema mwalimu huyo.

Naye Mwalimu Idda Kilawe ambaye ndiye aliyewakuta wanafunzi hao wakilawitiana, amesema kuwa siku ya tukio aliwakuta wanafunzi hao wakiwa ndani ya kibanda walichokuwa wamekijenga kwenye migomba.

“Niliwakuta wakiwa wamejenga kibanda cha miti na kukiezeka kwa matawi ya miti na ndani yake walikuwa wanafunzi watatu na wawili kati yao ndiyo walikuwa wakilawitiana.

“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa natoka kuchukua matokeo ya mitihani na nilipokaribia eneo la tukio, nikasikia sauti za watoto. Niliposogelea eneo hilo niliwaona wanafunzi wawili wakiwa uchi na yule mdogo ndiye alikuwa amevaa sare. waliponisikia, wakakimbia,” alisema mwalimu Kilawe.

Watu Wamvaa Aunty Ezekiel, Wamlaumu kwa Kudanganya Amejifungua

0
0
Kutokana na uzushi  ulioenea  kuwa staa wa  Bongo Movies, Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu, jamaa na marafiki kibao walijazana nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi, lakini walipokuta habari tofauti walimvaa na kumlaumu kwa kuwadanganya.
Jumatano usiku katika mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela, alitupia picha ikimuonyesha akiwa na kitoto kichanga, ambacho watu wengi waliamini ni wa kwake, hasa kwa vile katika siku za hivi karibuni ameonekana kupunguza mitoko.
Watu wa karibu wa muigizaji huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza shoo wa Diamond Platnumz aitwaye Iyobo, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kumpongeza, lakini walipatwa na mshangao baada ya kumkuta akiwa na tumbo lake kama kawaida.
“Sisi tulijua mwenzetu amejaaliwa kujifungua salama, sasa jambo la kushangaza wenzake tumekuja kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa, hivi aliwaza nini kuweka picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa kinachoendelea,” shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili nje ya nyumba yake, lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.
Mmoja wa marafiki waliodaiwa kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt, alikuwa ni shosti yake Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa mapema kuhusu ukweli wa ishu hiyo.
“Nilishtuka kweli, nikasema inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye mitandao ya kijamii? Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya fair bwana,” alisema Aunt.Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia mwezi wa saba, hivyo wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata kiumbe njiti.
GPL

Wimbo Mpya wa Ommy Dimpoz Wapondwa ila Video Yasifiwa

0
0
Baada ya Video mpya ya Ommy Dimpoz Kutoka Jana Baadhi ya Watu wakiwemo bloggers Maarufu kama U-turn Wameendeleza kuponda tunzi na melody za nyimbo zinazotolewa hivi sasa hasa kutoka kwa wanamuziki wakubwa ..Tukija kwenye hii nyimbo mpya ya Ommy Dimpoz ya Wanjera Wengi wamesema hakuna jipya kwenye wimbo na mashairi ila Video imetokea bomba hasa ukichukulia na uwepo wa Wema Sepetu ndani yake ... ...Bado msisitizo wa wasanii wakubwa kukubali kutungiwa nyimbo unawekwa ili kupata ladha tofauti ...Je wewe una maoni gani??

Moza Akana Kumrekodi Edzen Akiwa Uchi, Polisi Wambana, TCRA Wajitosa Kushugulikia

0
0
Uwiiiii tatenaneeeee, mambo yamefika mahala pake, Moza alikamatwa monday na kuwekewa dhamana jumatano na kesi bado inanguruma, haaa picha linaanza pale ambapo yeye mwenyewe anakataa oooh sio mie niliochukua ile video ze police wakamuuliza pale ni kwako YES so nani alichukua video sio miee, nasubiria movie iendeleee haki vile palipofika nimefurahi hatimaye TCRA watalifanyia kazi si kwa wanaume /wanawake hii ni kwa wote wanaowadhalilisha watu umelala na mtu halafu unamrekodi ili iweje?? kama sio kudhalilishana ni nini kwa kweli im so hapyyyyyyy na TCRA big up kwa ku follow up this case, its high time vimbelembele wavitulize 
NB
mwanamke/mwanaume  mwenye akili zake hawezi kufanya hivi ukiona mtu anafanya hivi ujue maisha yake hajielewi of-course she/he got nothing to lose, jamani hata Ezden mwenyewe nilivyoongea naye katika simu nimemwambia na nyie muangalie na wanawake wa kutoka nao jamani khaaaaa.
~Sintah
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live


Latest Images