Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Mwigizaji Jack Wolper Ashutumiwa Kumpiga Mizinga Mume Mtarajiwa na Wastara Juma

$
0
0
Mwigizaji Wastara Juma, akiwa na mume wake mtarajiwa Mark Edi.
Gazeti la Risasi Limetoa Shutuma Kubwa kwa Mrembo na Muingizaji Jack Wolper ya kuwa huwa anampiga mizinga Mume mtarajiwa wa Wastara...

Chanzo hicho cha hii Habari Kimehabarisha kama ifuatavyo:


AIBU! Staa wa sinema  za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji Wastara Juma, Mark Edi.

Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.

“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.

“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada zinaendelea.

Je una Maoni Gani Kuhusu Hii Habari?

Siwema Amjibu Nay Wa Mitego..Asimulia Yote ..Asema Hata Mtoto sio wa Nay ni wa Obasanjo

$
0
0
Siwema na Mpenzi wake Nay wa Mitego
Sakata la Nay wa Mitego na Aliyekuwa Mpenzi wake Siwema limeingia ukurasa mpya baada ya Siwema Kumjibu Nay wa Mitego na Kusema mambo makubwa yakushtusha.....

Haya ni Maneno aliyosema Siwema baada ya Nay Kumwacha na kumyang'anya Mtoto kwa Shutuma za kumfumania na Mwanaume Kitandani:

"Daah,siwezi endelea kukaa kimya aisee!! Ts hurt,iko hivi:@nay,naomba usisahau kama niwewe uliniambia nitafute boyfrnd..tena ulintukania hd mamang marehem,nilikushukuru tu..nilikaa kimya kwa siku kadhaa but nilirudi tena kukuomba msamaha..mamaako.mzazi anajua,dadaako tina anajua...unasema umenifumania,jaribu kumuogopa mungu,we unakuja kwangu umekuta nmembeba curtis metoka kumpa maziwa..leo unasema umekuta mi nasex kitandani..dahh ,ongea ukweli..nay mimi ndio nilikua nakupenda,hukuwah onyesha mapenzi hata siku1 kwangu,nilikua natetea penzi letu sanaaa..mimi ndo napost insta watsap lakin hukuwah kuonyesha hlo japo unaeza sema ulinisamehe ile ishu ya obasanjo ,wallah nilikupenda mungu anaona mpaka nikamkana yule baba alikua ananipa kila kitu nikaamua kua nawewe,sikuwah kuijua shida..naezasema ulinisamehe kinafiki caus tangia hapo hadi najifungua sikua na raha..huu sio mwili wangu mimi,kila siku mamaako alikua analia na mimi ,okey haijalishi umenifumania au nini caus tayari ulishanitamkia umenchoka nay..namimi sio mjinga kusex sasahiv mwanangu akiwa mdogo..nmebeba mimba miez9,nmezaa kwa uchungu..niwewe ndo ulisababisha mimi nisimnyonyeshe mwanangu cz sikuaeza kupata maziwa kwasababu ya stress..leo unatangaza umeninunulia gari,unanipa kila kitu..nay nini umenipa?gari nimali yangu,where's ma lexus,verrosa?kweli hujawah kunipiga lakin ulikua unaninyanyasa .mwanamke yyte ambae angekua mimi lazima angecheat tu,wewe huyohyo unafanya enterview unaulizwa kuoa unasema huwez utashuka kimziki akati mimi niko kwako na mtoto mdogo...na moyo gani?vingap umenfanyia?siwez ongea kila kitu ila jua umenrudisha nyuma saaana tu.mamaako shahidi wangu!!...unakumbuka ulikua unaniambia kila siku wewe unawatoto,nikwel unao,wengi tu nawajua sio hawa watatu unaowasema..waseme wooote..

Sasa nataka nikwambie tu hivi hata curtis sio wako ,babake ni obasanjo.yule alienivalisha pete!!..am done kwa hapa ila nnamengi tu,naumia sana sanaa!! ,pls nisiulizwe kitu tena wapenzi,nawapenda n thanx"

Zitto Noma, Aamua Kujiuzulu Ubunge Kabla Chadema Hawajamfukuza Rasmi Kwa Barua..Aandika Barua Hii Hapa ya Kujiuzulu

$
0
0

Wakati bado Chadema Hawajatoa Barua Rasmi ya Kumfukuza Zitto Chadema , Zitto Ameamua Kujiuzulu yeye mwenyewe na Kuandika Barua hiyo Hapo Juu ....

Je unaonaje Kuhusu Hilo ?

CHADEMA: Kung'atuka Kwa Zitto, Chadema, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!".

$
0
0
ZITTO KABWE
Sakata la Mbunge Machachari wa Chadema, Zitto Zuberi Kabwe na chama chake cha Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limefikia mwisho, limekwisha rasmi, it's over!, the rest is now a history!.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe, licha ya yeye kuwa ndio 'the most active MP of all time!', kwenye bunge la sasa, leo ameweka historia nyingine kwa kuwa ndie mbunge wa kwanza kung'atuka rasmi ubunge kwa kuaga rasmi kwa barua na kisha kulihutubia Bunge kuliaga!.

Hatua hii, sio tuu inamfanya Zitto kuendelea kuwa shujaa, bali pia kwa hatua hiyo, ameipiga Chadema bao la kisigino, kwa sababu sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema na sio Chadema imemfukuza!.

Uanachama wa chama cha siasa, hauombwi kwa kauli tuu bali kwa maandishi ya kujiandikisha uanachama, na kufukuzwa rasmi kwa uanachama, haufukuzwi kwa kuitishwa press conferences, kusema fulani sii mwanachama wetu, bali hufukuzwa kwa barua, hivyo mpaka hapa ninapoandika, Chadema ilimfukuza Zitto kwa kauli tuu ambayo sio kufukuza rasmi, lakini kwa barua ya Zitto, hii sasa ndio barua rasmi ya uthibitisho kuwa sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema!.

Ama kweli Zitto ni shujaa sijaona mfanowe!.

Hii ni threadi ya angalizo kwa Chadema na wapenzi wake, msishangilie sana hadi mkajisahau, wekeni na akiba japo kidogo ya aftermath ya kung'atuka kwa Ziito kwa sababu, kujiuzulu huku kwa Zitto, mnaweza kukuhesabu kuwa sasa ndio mwisho kabisa wa kirusi chenye jina la ZZK, and you have closed the chapter and move forward!, bora jiandaeni kabisa!, kunaweza kusiwe ndio mwisho bali sasa ndio mwanzo wa series za 'karma' effects ambazo ama zitamtandika Zitto mwenyewe kama kweli ni msaliti, ama zitaindandika Chadema, bila huruma, kama ni kweli Chadema haikumtendea haki!.

Kwa mnaoijua 'karma', shangilieni kwa kiasi tuu!, msimbeze, msimdhihaki wala msimtukane kwa sababu hakuna mkamilifu. Zitto alikuwa mwanachama wenu, hakuwabeza, hakuwatukana amewaaga rasmi kwa heshma, nanyi mnategemewa mtairudisha heshma vile vile!.

Nashauri wale msio jua "karma" ni nini, jipeni homework kidogo tuu, kisha ndio mje kuchangia!.
Nitazijibu hoja zote za msingi, ila kwa wale vichwa maji na madebe matupu, mtanisamehe, nitawashukuru tuu kwa kuchangia uzi wangu.

Pasco.

Note to mode: This is opinion article na sio reportage!

Ni mtamu, Shape Nzuri, Lakini Namuacha kwa Hili

$
0
0
Aisee asikwambie mtu, mi ni mroho wa shape za kibantu zilizojaaliwa kalio la kutosha kumtoa nyoka pangoni. Sikosi kugeuka nikiona sampuli ya hivyo ikipita nasindikiza kwa macho hadi anakoishia ama kumfuata na kufanya application kabisa.

Juzi kati nimefanikiwa kunasa mdada mmoja mwenye vigezo kama hivyo ni nikafanikiwa kupiga naye show ya kikubwa kunako 6x6. Aisee ni mtamu ile mbayaaaa.

Baada ya kukolea nami akataka kujenga uhusiano wa kudumu japo hata kwa mchepuko ama nyumba ndogo! Kwa jinsi hata mi nilivyokolea kwake nikamkubalia.

Kitakachofanya nimuache pamoja na vigezo vyake vizuri, ni kwamba ana majini na kaniambia yeye mwenyewe , kanitajia idadi na majina ya hayo majini hadi nikaogopa.

Yaani hapo nawaza hivi siku yakicharuka hayo madude yake japo sijui huwa yanafanyaje, si itakuwa balaa.

Aisee kwa kweli naachia ngazi huku bado nalitamani hilo dada la kibantu lilioumbika vizuri, limeenea kila idara.

Kigogo Polisi Afisa wa Barabarani Ubungo Akumbwa na Tuhuma Nzito

$
0
0
Sheria
AFISA Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kituo cha Ubungo-jijini Dar es Salaam, Inspekta Kamote, anadaiwa kusababisha kupotea katika mazingira ya kutatanisha mkazi wa Makuburi mtaa Mwongozo, Haeshi Mohamed (59).

Kwa mujibu wa familia ya Mohamed, mzazi wao ambaye pia ni dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (Bajaj) eneo la Ubungo, amekuwa akiandamwa na Insp. Kamote tangu Machi 7 mwaka huu, alipokamatwa kwa kosa la kuegesha pikipiki yake eneo lisiloruhusiwa.
Familia inasema “tanashangazwa na hatua ya Insp. Kamote kufika nyumbani kwetu mara mbili saa saba usiku akiwa na askari wenzake bila kuongozana na mwenyekiti wa mtaa na kudai kwamba wanamsaka baba”.

“Tuhuma ambazo tunaelezwa ni kwamba Bajaj ya baba ilioneshwa kwenye kituo cha runinga cha TBC1, ambapo mmiliki wake anadaiwa kutafuwa kwa wizi…mara wanasema baba ametishia kumroga na kumuua Insp. Kamote,” wanasema.
Mmoja wa wanafamilia, Ali Salum Kautipe, ameiambia Online kwamba mpaka sasa wanamtafuta baba yao mzazi, hawajui alipo na hawana uhakika kama amekamatwa na polisi au amekufa.

“Inashangaza Insp. Kamote kudai kwamba bajaj ya baba ni mali ya wizi. Hii ni mali halali aliyoinunua mama yetu mzazi, Zaina Ali Kapenda baada ya kuuza shamba lake la urithi wa baba yake.
“Hii Bajaj nilianza kuiendesha mimi na katika kumuenzi babu yetu ndipo nikaamua kuiandika kwa mbele “babu Kapenda”, halafu nikamwachia baba awe anaifanyia biashara…sasa leo inakuwaje mali ya wizi,” amehoji Ali.

Akisimulia chimbuko la mzozo huo, Ali amesema kuwa baada ya baba yake kukamatwa Machi 7 kwa kosa la maegesho, aliwekwa mahabusu kituo cha Ubungo kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 7 usiku alipodhaminiwa.

Amesema kuwa licha ya baba yake kuwa maarufu kwa askari polisi akiwemo Insp. Kamote kutokana na kuwa kiongozi wa waendesha Bajaj eneo la Ubungo, bado dhamana yake ilikuwa ya kutatanisha kutokana na mizengwe aliyowekewa.

“Baada ya kumdhamini usiku ule alikuwa akilalamika sana maumivu kwenye mbavu zake, akidai alipigwa sana. Kesho yake Machi 8, aliripoti polisi Ubungo na kuomba fomu ya matibabu (PF.3) lakini akanyimwa.

“Kwa kuwa hali yake haikuwa nzuri, tuliamua kwenda kituo kingine cha polisi Mwongozo ambapo alipatiwa PF.3 kisha tukampeleka Hospitali ya Sinza ambapo aipewa dawa na kutakiwa kurudi kwaajili ya vipimo vya X-ray,”amesema.

Ali anaongeza kuwa Machi 9, baba yao, aliripoti kituoni Ubungo na kisha kupelekwa makamani Kinondoni ambapo alisomewa kosa la kuegesha Bajaj eneo lisiloruhusiwa . Alikiri kosa na kutakiwa kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya sh. 20,000.

Online imeona stakabadhi ya malipo namba 3416838 iliyotolewa na Mahakama ya Kinondoni kuthibitisha kwamba Mohamed alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na baadaye alikabidhiwa Bajaj yake iliyokuwa ikishikilia kituoni Ubungo.

Ali anasema, “tukiwa kituoni kabla ya kwenda mahakamani, Insp. Kamote alimnyang’anya baba vielelezo vyake vya matibabu ili asiweze kurejea tena hospitali kwa ajili ya vipimo”.

Familia hiyo inadai kuwa baada ya siku mbili kupita tangu kumalizika kwa kesi hiyo, ndipo usiku wa saa saba walivamiwa na askari polisi wakiongozwa na Insp. Kamote wakidai kumsaka baba yao kwa tuhuma za kutishia kumroga na kumuua afisa huyo.
“Kwanza tulishtuka sana kuona askari wanakuja kupekua nyumba yetu kumtafuta baba bila ya kuongozana na mwenyekiti wa mtaa kama ilivyotaratibu za utawala bora… walipekua kila mahala na kuwabughudhi wapangaji wetu.

Insp. Kamote aliingia hadi chumbani kwangu nikiwa nimelala na mke wangu, akawasha taa na kuizima,” amesema.
Familia inaongeza kuwa tukio hilo la kuvamia mara mbili na askari usiku kisha kupekuliwa, limewafanya wapangaji wao kutaka kuhama kwani wanahofia wanaweza kukamatwa.

“Tangu askari walipofika hapa siku ya kwanza, baba yetu hakuonekana tena hadi leo, hatujui kama walimkamata au kapotea na kufa…maana bado tunaambiwa anatafutwa,”wamesema.
Alipoulizwa Insp. Kamote kuhusu tuhuma hizo, alikiri kutafutwa kwa Mohamed akisema, “ameunda genge na wenzake na kunitisha kwamba wataniroga na kuniua, kwa hiyo bado tunawatafuta”.

Online liliotaka kujua taratibu za kisheria kama zinaruhusu kwa yeye mlalamikaji kufanya tena kazi ya ukamataji wa mtuhumiwa, Insp. Kamote aling’aka na kusema, “sina muda wa kuongea na wewe…wewe nani unaifundisha polisi kazi”, kisha akakata simu.

Baada ya dakia mbili alipiga tena na kumtaka mwandishi amfuate ofisini kwake ili ampatie majibu, lakini alipotakiwa kuyatoa kwa njia hiyo ya simu, akasema, “una ajenda yako, andika munavyoona…wewe raia unaweza kumhoji polisi, unataka kutufundisha kazi”.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wabura, alipoulizwa kuhusu sakata hilo amesema, “mwambie huyo anayelalamika afike kwangu ndipo naweza kufanya uchunguzi”.

Ameongeza kuwa kwa sasa itakuwa vigumu kwake kulitolea taarifa halisi na za uhakika ikiwa hajapata malalamiko ya wanafamilia hao.

House Girl ( Binti wa Kazi ) Asababisha Kifo Baada ya Kufumaniwa na Bosi Wake Huko Arusha......Morani Wachoma Nyumba Kulipiza Kisasi

$
0
0
Makundi ya vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa jamii ya kimaasai maarufu kama “Morani” katika eneo la Olasiti Jijini Arusha, wameteketeza kwa moto mali mbalimbali zikiwemo nyumba pamoja na magari ya wakazi wawili wa eneo hilo, wanaotuhumiwa kumpiga na kumsababishia kifo kijana mmoja wa jamii hiyo.

Kijana Melita John anadaiwa kuuawa na Bernard Kavishe mkazi wa Olasiti akishirikiana na majirani zake wawili akimtuhumu kijana huyo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wake wa kazi za ndani ambaye ni binti wa miaka 17 anayefahamika kwa jina la Monica Emanuel.

Taarifa zaidi zinadai kuwa hatua ya morani wa kimaasai kujichukulia sheria mkononi na kuteketeza nyumba na magari pamoja na mali nyingine za watuhumiwa hao ni katika kulipiza kisasi kutokana na kifo cha mwenzao wanayedai hakuwa na hatia.

Inadaiwa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji hayo Benard Kavishe baada ya kuwasili nyumbani kwake majira ya saa saba mchana na kugonga gate la nyumbani kwake ilimchukua muda wa dakika kumi msichana wake wa kazi kufungua ndipo alipoingia ndani na kumkuta kijana Melita akiwa bila nguo ndipo alipowaita majirani wenzake na kumshambulia kwa kipigo hadi kumsababishia mauti

Jeshi la Polisi kupitia wa Kaimu kamanda wa Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Edward Balele akithibitisha tukio hilo amesema baada ya watuhumiwa wanaosadikiwa kushiriki katika mauaji ya kijana Melita wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi..

Masheikh 50 Waandamana Kwenda Kwa LOWASSA Kumtaka Agombee URAIS 2015.......Wamkabidhi 700,000 Imsaidie Kuchukua Fomu

$
0
0
MASHEKHE wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania Urais 2015.
  Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia kwenye picha juu) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.

Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
  Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu," alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Lowassa amesema "nikifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu."

Mrembo Vera Sidika Apata Aibu Kubwa..Meseji zake Akichat na Mwanaume Wakikubaliana Kuhusu Kufanya Mapenzi zawekwa Mtandaoni

$
0
0

Have you ever wondered where these Socialite Girls Get all the Money that they flaunt in Social Media
-----
This is How Socialite Girls like Kina Agness Masogange , Huddah Monroe and Corazon Makes Money..
VERA SIDIKA's messages asking for 1.5m from a man who wanted to have S£X with her Exposed Below:







Agness Masogange Akijirusha na Mwanamuziki Shetta Huko South Africa

$
0
0
Masogange and Sheta Spending the night together in the club.....in South Africa

Diamond Platnumz Aamua Kuonyesha Mjengo Wake Ulipofikia Baada ya Watu Kumsimanga Sana

$
0
0
 Baada ya Watu Kuchonga Kuhusu Nyumba ya Diamond kuwa amesimama kujenga huku wengine wakisema amezidiwa na Jux , Diamond Ameamua Kuonyesha Mjengo wake ......


Afande Sele (Seleman Msindi) ajiengua CHADEMA na kujiunga na ACT Kumfuata Zitto Kabwe

$
0
0
Mwanamiziki Suleiman Msindi (Afande Sele) Asubuhi hii naye amejiengua CHADEMA na amejiunga pamoja na Zitto katika Chama cha ACT.

Una Maoni Gani?

Edward Lowassa: Lowassa: Nimeshawishika, Nitagombea Urais 2015

$
0
0
Edward Lowassa
Katika Kurasa za magazeti ya Leo zimepambwa na tarifa mbambali za kurasa za mbele za magazeti zinaonyesha dhahiri Edward Lowassa kukubali kugombea Urais, Okello nimelifuatia suala hili kwa karibu mengi nimeyapata kutoka kwa Mashekh wa Bagamoyo. Ni ukweli dhahiri upande wa Jakaya katika dhamira yake ya dhati ni kumkabidhi Edward Lowassa ikulu ya magogoni.

Mengi katika vipaumbele vya ujumbe wa Jakaya katika ni kuhakikisha Edward Lowassa anaendeleza Yale ambayo ameyaacha ikiwemo elimu, Afya bora, miundombinu na kufuta umaskini kwa Watanzania wote.

Kumejitokeza makundi mbali mbali yakimtaka kugombea Urais, yeye binafsi amesema anafarijika kuona Watanzania wanasimama nae katika hili, mbali historia ya uongozi wake uliotukuka basi hii nafasi ya Watanzania kumuomba atangaze nia inampa nguvu hasa Dk. Jakaya kumtumia ujumbe mzito.

MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.

~John Okello

Dr Kessy Anakuletea Dawa za Kutengeneza Hips, Makalio, Nywele na Nguvu za Kiume Kwa Kutumia Dawa za Asili zisizo na Kemikali

$
0
0
Kifaa cha Kurefusha uume Kinachouzwa 160,000


Pendeza na Dr Kessy Products 
Ni dawa za Asili zisizo na Kemikali wala madhara yoyote kwa Binadamu, zimetengenezwa kwa kutumia mimea na matunda mbali mbali kukupa matokeo ya Haraka

1.Refusha Nywele na zisikatike  45,000/
2.Ondoa Mvi Sugu kichwani  45,000/
3.Toa Michirizi Mapajani, Chunusi na Madoa mwilini 40,000/
4.Punguza tumbo na Manyama uzembe 45,000/
5.Mkanda wa Kufunga Kupunguza tumbo 70,000/
6.Tengeneza Shepu Hips na Makalio  45,000/ ,Vidonge 80,000/
7.Ongeza Nguvu za Kiume  Jelly 45,000/ , Vidonge 60,000/
8.Ongeza Ukubwa wa Maumbile ya kiume Jelly 80,000/ , Mashine 160,000/
9.Kuongeza Mwili Mzima 40,000/
10.Kupunguza Mwili 45,000/
11.Kupunguza Maziwa na Kuyasimamisha 40,000/
12.Ongeza Mguu uwe wa Kupendeza 45,000/
13.Rudisha usichana ama Bikira 55,000/
14.Ongeza Hamu ya Kula 40,000/
15.Ongeza Hamu ya Kufanya Mapenzi 55,000/
16. Fanya mwili Kuwa Soft 60,000/

TUNAPATIKANA DAR NA MIKOA YOTE, HUDUMA ZINAFIKA POPOTE ULIPO , 
DAR TUPO KARIAKOO MSIMBAZI NA POSTA  MPYA

PIGA SIMU: 0719955528, 0756259180 au 0785371237

Huwezi Amini Diamond Asema Choo cha Nyumba Yake Kimetengenezwa Kwa Mil 70 , Mwenyewe Akiita STATE HOUSE

$
0
0
Diamond Platnumz
In my 70Million Pure Gold plated toilet...pupping and Movies Lol!....i can't wait to play dirty game with her tonight ...IN THE MAKING OF STATE HOUSE!!!..thanks alot @Red_interiors i cant wait for the State house to Be Done! Done!"-Diamond captioned this photo

Lil Wayne: Drake Aliwahi Kulala na Demu Wangu

$
0
0
Drake and Lil Wayne
Drake hakuishia kumfanyia usnitch Tyga peke yake, bali pia bosi wake wa YMCMB, Lil Wayne.

Kwa mujibu wa kitabu ambacho Lil Wayne ameandika, Drake aliwahi kulala na demu wake.

Wakati akiwa gerezani Rikers Island kwa kosa lake la kumiliki silaha mwaka 2010, Weezy anadai kuwa Drake alimtembelea na kumwambia ukweli kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake.

Kwenye proposal ya kitabu hicho ambayo mtandao wa TMZ umeipata, Wayne anaandika: This is the type of s**t that a man never wants to find out when he’s locked up. Or, maybe so, cause only God knows what I would have done if I wasn’t locked up right now.

Anaongeza: I woke up feeling fu**ed up about the fu**ed up day that I had. Finding out that she fu**ed Drake was the absolute worst thing I could’ve ever found out. As a man, honestly, that s*** hurt … and not because it was Drake, it could have been any man. It would’ve hurt the same.

Kwa Maneno Haya, Wolper Anajivunia Mpenzi Wake Aliempa ‘Ndinga’ Hili

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Jacqueline Wolper ametupia picha hizi kwenye ukurasa wake  mtandaoni na kuziandikia maneno kwa lugha ya “Malkia” ..

Being with someone who won't give up on you”.  Akaandika tena  “Be with someone who is proud to have you. Thug life mentality”.

Kauli hizi zinaonyesha mrembo huyu kwasasa yupo kwenye mahusiano na mtu ambaye  anampenda na anaonyesha kumajali sana mrembo huyu na pengine kwa swaga za mitandaoni , naungana na wengi waliompongeza kwa kupewa ndinga hilo na huyo anaesifa hapo.

Mzee wa Ubuyu.

Wema Aendelea Kuwapa Hamasa Wanawake,Chukua Hii Kutoka Kwake

$
0
0
Wema Sepetu
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu  mwenye followers zaidi ya laki nne kwenye mtandao wa Instagram kwa siku za hivi karibuni ameonyesha njia kwa mastaa na watu wengine baada ya kuamua kuanza kuposti  jumbe mabalimbali zenye manufaa kwa jamii na sio majungu ambayo hayana faida yoyote, Wema amekua akiachia jumbe hizo na  huku akitumia tag mbili za BeWemaFanyaWema na 2015WalkToRemember.

Amekuwa akiandika vingi kuhamasisha wanawake kwenye kujitafutia maendeleo huu ni muendelezo tu. Baada ya hivi juzi kuwa balozi na kuzindua gari mpya ya kampuni ya Mitsubishi ASX alibandika hii.

Mwanamke simama imara. Usipojiamini mwenyewe atakuamini nani? Hamna kisichowezekana!

Huu ni mfano mzuri sana Madam tupo nyuma yako.

Waigizaji Bondi, Aunty Lulu Wapashana na Kupeana Vidogo Wazi Wazi..Hawa Walikuwa Wapenzi Wakatemana

$
0
0
Anti Lulu na Mr Bond Enzi za Mapenzi yao
Mastaa wa Bongo Movies  na watangazaji waliowahi kuwa wapenzi, Bondi Bin Suleiman na Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni walipashana baada ya kila mmoja kumdhihaki mwenzake kuwa hana kazi anayofanya mjini.

Bondi alisema kitu kikubwa anachokifanya Aunty Lulu ni kubadilisha wanaume ndiyo sababu ya kushindwa kuendelea na kazi yake ya utangazaji na filamu, akiishia kudanganya kuwa yeye ni mjasiriamali.

Lakini Aunty Lulu naye alijibu tuhuma hizo akisema mwandani wake huyo wa zamani atakuwa anatafuta kitu kutoka kwake, kwani kama ni kazi, hata yeye mwenyewe hana anachokifanya mjini zaidi ya kuuza sura kwani kama anaringia utangazaji, yeye ndiye alimtafutia kazi hiyo.

Mama Nay wa Mitego Apata Mshituko Issue ya Nay Kumfumania Siwema na Siwema Kudai Mtoto si wa Nay

$
0
0
Nay wa Mitego na Siwema
JAMBO limezua jambo! Siku chache baada staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kudaiwa kumfumania mpenzi wake Siwema Edson kisha kuondoka na mtoto wa miezi mitatu (Curtis), mrembo huyo ameibuka na kudai mtoto huyo si mali ya Mbongo Fleva huyo hali ambayo imesababisha mama yake mzazi Nay apate mshtuko, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo hatua kwa hatua.

Ijumaa iliyopita, gazeti tumbo moja na hili la Ijumaa liliripoti tukio la Nay kutonywa kuwa mchumba’ke anachepuka jijini Mwanza anakoishi ambapo Nay aliamua kufunga safari kutoka Dar hadi Mwanza na kumfumania Siwema akiwa na ‘serengeti boy’ wake.

HABARI YAMTIBUA SIWEMA

Mara baada ya habari hiyo kupeperuka hewani, rafiki wa karibu na Siwema alimvutia waya mwanahabari wetu ambapo alieleza jinsi gani Siwema amechukizwa na habari hiyo.

TUJIUNGE NA SHOSTI

“Nilikuwa na Siwema, kusema kweli amemlalamikia sana Nay, anasema tangu alipokuwa mjamzito alikuwa na mgogoro mkubwa sana na Nay, hata alipojifungua amekuwa akivumilia vitu kibao kutoka kwa jamaa (Nay)

ETI HALIKUWA FUMANIZI

“Zaidi alichokuwa akilalamikia Siwema ni juu ya Nay kusema alimfumania wakati siku hiyo yeye alimkuta anamnyonyesha mwanaye, hata anaposema kamkuta na mwanaume, haoni hoja ya Nay kusema hilo wakati mwenyewe alimwambia hamtaki na kumruhusu kutafuta bwana sasa amemkuta analalamika nini tena?

KIGOGO AMPA JEURI SIWEMA

“Kwanza Siwema ana kigogo wake serikalini ndiye anayempa jeuri, sasa sijui hata anamfuatafuata wa nini,” alisema rafiki huyo.

SIWEMA ANASEMAJE?

Baada ya kunasa mazungumzo hayo ya shosti huyo, mwanahabari wetu alimsaka Siwema mwenyewe ili kujua anazungumziaje sakata hilo, alipopatikana, alifunguka:

“Yaani we acha tu katika maisha huwa kuna siri sana, najua watu wengi wanaongea mambo ambayo hawayajui vizuri, nimeanza uhusiano na Nay siku nyingi sana na kote huko mimi mambo yangu yalikuwa safi kuliko yeye ambaye hata jina alikuwa hana, namshangaa sana leo maneno anayoropoka kwa watu eti alinifumania wakati siku anakuja kwangu alinikuta nimembeba mwanangu Curtis na nilikuwa namnyonyesha, nafikiri ajaribu kumuogopa Mungu kidogo.

AZIDI KUFICHUA MAOVU

“Kuna uchafu mwingi sana alikuwa akinifanyia na hata hivyo kusema kanihonga gari, ni muongo kwani hili gari (Toyota Mark X) ni langu, hakumbuki zile Toyota Lexus na Toyota Verossa zangu nilizompa? Amenirudisha nyuma sana kimaisha hata mama na dada yake anajua haya, tangu nimekuwa naye mimi ndiyo mkosaji tu? Mimi huyuhuyu ndiye nilikuwa nikimuomba msamaha kila kukicha hadi mwisho akanitamkia nitafute boyfriend, hata hilo bado hakumbuki na kuendelea kuongea vya uongo?”

APIGILIA MSUMARI WA MTOTO

“Najua kweli ana watoto zaidi ya watatu nafikiri hata hao wengi bado ana muda wa kuwataja tu na wajulikane kwenye jamii asijifanye anampenda sana Curtis,  amuache tu maana si wake mimi ndiye ninayeweza kujua zaidi baba wa mtoto na asijifanye kimbelembele na kutaka kunichafulia kwenye jamii wakati ukweli naujua mimi,” alisema Siwema.

MAMA APATA MSHTUKO

Kufuatia habari hiyo ya Nay kumfumania Siwema na mchumba huyo wa mwanaye kufunguka kuwa mtoto si wa Nay, chanzo kilicho karibu na familia ya msaanii huyo kimepenyeza habari kuwa mama mzazi wa Nay, Matlida Mwaipopo alipata mshtuko na kushindwa kuzungumzia suala hilo.

“Mama Nay amepata mshtuko mkubwa, presha imepanda na hapa tunavyoongea na wewe, tumejaribu kumtuliza ili aweze kusaidia tatizo hili kifamilia, ameshindwa kuzungumzia lolote,” kilisema chanzo hicho.

NAY ALIA USIKU KUCHA

Alipotafutwa Nay kuhusina na tukio hilo, alishindwa kuzungumzia lolote zaidi ya kulia kutwa na hata alipotafutwa baadaye bado alizungumza huku akilia.

“Suala la kuambiwa mtoto si wangu linaliza na hadi muda huu naumia sana, inafikia wakati nashindwa hata niseme nini ila anachokitaka kwangu atakipata, wewe mwacheni aendelee kuropoka na kunidhalilisha huko Instagram, ukweli mimi sina neno naye na zaidi nimechukua mtoto wangu na nawapenda sana wanagu wote,” alisema Nay na hata alipotafutwa usiku sana siku hiyo (Ijumaa iliyopita), bado alisikika akilia kwa uchungu.

KIKAO CHA FAMILIA CHAANDALIWA

Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo makini kilivujisha habari kuwa kuna baadhi ya ndugu wa karibu wa Nay wanaandaa kikao cha familia ili kutafuta suluhu ya jambo hilo.

“Kuna kikao kizito kinaandaliwa cha familia kutafuta suluhu lakini tutakujuza zaidi kitakapofanyika,” kilisema chanzo hicho.
GPL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images