Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo, Anaponzwa na Kibuli cha Kujiona Hakuna zaidi ya Yeye.

$
0
0
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”
Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”

Udaku Specially

Sababu 10 za Kuifanya CCM iendelee Kutawala milele na ACT Kuwa chama kikuu cha Upinzani Tanzania

$
0
0
Bila shaka mnajua fika kwenye uchaguzi ujao october CCM itaendelea kutawala kama kawaida na hii ni kutokana na sababu nyingi tuu ..leo nitaeleza tano tuu na pia nitaeleza sababu tano zitakacho kifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu cha Upinzani Tanzani...

Moja ya sababu inayoifanya CCM kuendelea kutawala ni kuwa na hazina ya wapiga kura..huu ni ukweli ulio wazi maana wapiga kura walio wengi ni wakina mama na wakina baba na hawa wengi ni CCM na hata ukichukulia mfano kwenye zoezi ili linalo endelea la uandikishaji wa wapiga kura utagundua kuwa walio hotokeza wengi ni wakina mama na wakina baba ambao wengi ni wapiga kura wa kudumu wa CCM..wapiga kura wa chadema wao wamejaa kwenye mitandao lakini huwa hawaendi kujiandikisha na hawana sifa ya kupiga kura hii huwapa ushindi wa mezani CCM kila leo.

Pili CCM wanajua kutatua migogoro inayo jitokeza bila kuleta madhara ukilinganisha na vyama vya upinzani hasa Chadema na UKAWA..mtu anaweza kujidanganya muda huu kuwa CCM imevurugika oooh CCM kuna makundi na yatakimaliza lakini mkitaka kuhakikisha kuwa CCM itatawala milele na inajua kumaliza makundi subiri muone wakati wakuelekea uchaguzi mkuu ndio hapo kila mtu ataamini kuwa hiki chama kita tawala milele na kama mtakumbuka kipindi kilicho pita kabla ya Jk kulijitokeza makundi mengi lakini yalikwisha na CCM ikasonga mbele wakiwa wamoja...tofauti na UKAWA hasa Chadema hawana uwezo wa kuhimili vishindo vya makundi bila kuleta madhara na mkitaka kuamini subirini wakati wa kumpata wagombea mbalimbali kuputia UKAWA hasa mgombea Urais hapo ndio mtaamini UKAWA hawana uwezo wa kuhimili makundi na watasambaratika au watakwenda wakiwa wamegawanyika kabisa na ndio maana hadi sasa hakuna anaye onesha nia ya kugombea hasa Urais maana wanajuana walivyo(patachimbika)

Tatu CCM wana hazina ya viongozi ambayo ni ndefu kwa hiyo wana uwezo wa kuuwa makundi kwa kuwaacha wote walio kwenye makundi na kuchagua mtu ambaye hatoki kwenye makundi na wakaendelea kutawala milele...maana njia pekee ya kuuwa makundi ni kujichinjilia mbali wote walio kwenye makundi na kuchukua mtu tofauti na wote wata tulia maana kila mmoja kakosa..lakini huko UKAWA safu ni nyembamba saba kiasi kwamba ni vigumu kuchagua nje ya makundi hasimu..mfano UKAWA kuna kundi la Slaa , na Lipumba..ukiwatoa hawa hakuna mwingine mwenye sifa au anaye weza kugombea kiti cha Urais sasa kazi inakuja jinsi ya kuunganisha haya makundi bila kuleta mpasuko ni ngumu maana nje ya hao hakuna na ukipendekweza mmoja kati ya hao bado kutakuwa na mpasuko na hapo ndio mtakubaliana nami kuwa CCM itatawala milele..

Nne CCM ina umoja wa vijana ambao ni hazina,hai na wenye nguvu...hapa pia ndipo CCM inapo tofautiana sana na UKAWA ambao wamejaza vijana wengi lakini ni wapiga kelele tuu na wengi wao kujiandikisha hawaendi na hawana sifa za kupiga kura halafu wengi wao wana nunulika kirahisi..kwa mfano ukiangalia Bavicha ni kama imekufa kabisa tota aondoke Heche imekufa kabisa kazi zote zina fanywa na wazee ..Bavicha wameponzwa na makundi ya kugombea uenyekiti na ndio yanao utafuna umoja huo kiasi kambwa mwenye kiti wao ana kosa ushirikiano na anashindwa kuwaunganisha vijana.. Bavicha wengi wanacho fahamu ni kuongea kama Mbowe tuu ...pia huu ni ushahidi CCM kutawala milele..

Tano CCM wanajua jinsi ya kujipanga na kukabili yanayo wakumba hasa maswala ya ufisadi wa baadhi ya wanachama na huja na suluhu ndio maana hata wakienda kwa wananchi huwa sikiliza lakini tofauti na UKAWA hasa chadema huwa hawana majibu zaidi ya kuadithia story za ufisadi na hawana lingine la kuwambia wananchi zaidi ya story za ufisadi na ni waongeaji sana kuliko vitendo hivyo hilo linawafanya wananchi wawachoke na waonekanae hata wakipewa nchi nao watakula tuu!

Pia kuna sababu tano zitakacho kifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu upinzani kuanzia October...

Kwanza ACT kinatangazwa sana na kupewa airtime na vijana wa chadema kiasi kwamba kila mtu anataka kukifahamu na watu wametamani sana kujiunga na hiki chama kipya ambacho kina isumbua chadeema kiasi hiki hadi wana sahau mambo yao..

ACT kitapata majimbo mengi hasa ya upinzani hasa ya chadema kutokana na nguvu aliyo nayo bwana Zitto kabwe na hivyo atawashawishi sana wananchi na watakichagua maana kila mtu anajua nguvu ya Zitto kwa wananchi hata UKAWA wana fahamu hilo.

ACT itakuwa kimbilio la vijana wengi kutokana na nguvu ya Zitto na bila shaka hili halina ubishi kwa kuwa ni wazi kuwa Vijana wengi walio chadema wamepwnda siasa na wameipenda Chadema kupitia Zitto na walivutiwa na Zitto kutokana na uwezo wake mkubwa katika siasa hivyo wengi watajiunga nae na hapo Chadema hawato amini bali wajiandae sana kwa upinzani mkubwa...wabunge wengi vijana wa chadema wamepata ubunge kwa kupitia nguvu ya Zitto na hilo hawawezi kubisha.

Tatu ACT imepata mtu mwenye ushawishi mkubwa na mwenye uwezo wa kujenga hoja kuliko kiongozi yeyote yule wa upinzani..Zitto ni mtu aliye barikiwa nguvu ya ushawishi kabisa kila mtu anajua anapo simama kuongelea jambo kila humvuta kila mtu bila kujali itikadi yake ...tofauti na kule chadema ambapo wote wameigana jaziba hakuna anaye weza kuongea jambo bila jaziba au munkari hili litakifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu cha upinzani..

Nne ACT imepata pakujifunza maana wameona wenzao hasa chadema walipo kwama hasa uwezo mdogo wa kushawishi watu kuwapigia kura....maana chadema hawana njia nyingine ya kushawishi watu zaidi ya kusema ufisadi na hii imewachosha watu maana watu wanajua hata wao si wasafi lakini kwa timu ya ACT hakika kutakuwa na suluhu hivyo chadema wata sahaulika.

Mwisho ACT kitajengwa sana na walio kosa haki zao chadema hivyo wataona ni sehemu ya kukimbilia ..pia wabunge wengi au vijana watakao kosa nafasi kutokana na mfumo wa chadema wa kuwapata viongozi au wabunge ambao hautoi haki ACT itakuwa kimbilio lao!

Karibuni wana jamvi..
#zamuyakokijanakajiandikishe
By Ruttashobolwa

'Jokate Anatutia Aibu Sana' Wanakwaya Wenzake Waja Juu, Picha za Nusu Utupu Zatajwa

$
0
0
Jokate 
Ile skendo ya kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho, ukijumlisha aibu mpya ya kukata mauno mbele ya wanaume, staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewakera wanakwaya wenzake ambao wamedai kuwa anawatia aibu...

Ishu ya Jokate kutupia picha za nusu utupu mitandaoni si mpya, mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kwa tabia yake hiyo kiasi cha kuwakera wanakwaya hao wa kanisa analosali la Saint Peter lililopo Oysterbay jijini Dar.

Mbali na picha hizo, safari hii anaandamwa na skendo mpya ya kudaiwa kukata mauno mbele ya midume anapokuwa kwenye shoo zake baada ya kutumbukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Nchini Afutiwa Dhamana

$
0
0
Mahakama mkoani Dodoma imefuta dhamana ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya kutowazuia wafanyabiashara kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea mahakamani

Akitoa taarifa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu, Mwendesha mashtaka wa serikali Rose Shio amesema kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba mahakama kutengua dhamana ya mshtakiwa kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
  Amesema kuwa pamoja na hilo Mwenyekiti huyo amekuwa akiendelea kufanya mikutano na wafanyabiashara kwa ajili ya kuwahamasisha wasiendelee kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za efds kitenda alichosema kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
  Hata hivyo wakili wa mshtakiwa, Godfrey Wasonga ameiambia mahakama kuwa tangu mteja wake apewe dhamana ahajawahi kuitisha mikutano na wafanyabiashara kwani hata juzi hakuwa na mkutano bali wafanyabiashara waliokuja mjini Dodoma kusikiliza kesi ya mwenyekiti huyo, waliposikia kuwa yupo Dodoma walikwenda kumsalimia baada ya kupata taarifa kuwa yuko katika hoteli ya Image Hill.
  Na kuhusu suala la kufunga maduka mwenyekiti huyo hakuwashawishi wafanyabiashara nchini kufunga maduka yao bali ni wafanyabishara wenyewe ndo walioamua kufunga maduka yao kwa ajili ya kwenda kusikiliza kesi ya mwenyekiti wao.
  Hata hivyo hakimu Mbilu amesema kuwa ameridhika na hoja za upande wa mashtaka na hivyo akatengua dhamana ya Minja na kumtaka kubaki rumande hadi April Mosi mwaka huu ambapo kesi yake itatajwa tena.
  Amesema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali April 9 mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.

Aibu Kubwa:Afumaniwa Gesti na Mume wa Dada Yake...

$
0
0
Binti aliyetajwa kwa jina la Biena mkazi wa Kawe jijini Dar, hivi karibuni alipata aibu baada ya kufumaniwa ndani ya gesti (ipo maeneo hayohayo) akiwa na mume wa dada yake.

Chanzo makini kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, Biena na mume wa dada yake aitwaye Abasi wamekuwa na uhusiano kwa muda mrefu kabla ya juzikati kunaswa laivu wakiwa gesti.
  “Beina anaishi na dada yake aitwaye mama Saida, amekuwa akimzunguka kwa kutembea na shemeji yake hadi sisi majirani tukakereka.

“Sasa siku ya tukio mama Saida ambaye ni mjamzito alikuwa kalala, tukamuona  Abasi na Biena wakielekea gesti. Uzalendo ukatushinda, tukaona tumsaidie dada wa watu kuwafumania.

“Tukaenda hadi kwenye ile gesti, tukawafumania wakiwa ndani, Abasi akaingia mitini mpaka leo hajulikani aliko, Beina akatoka na kukimbilia nyumbani kwa dada yake,” alisema mtoa habari huyo.

Mama mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la mama Farida alisema ni kweli binti huyo alikuwa akitembea na shemeji yake na majirani walichoshwa na hilo ndiyo wakaamua kumtolea uvivu.

Biena alipobanwa alikiri kufumaniwa lakini akadai aliponzwa na tamaa ya chipsi kuku, akaomba msamaha kabla ya kurejeshwa kwao Tunduma. Mama Saida alipofuatwa na waandishi ili aongelee tukio hilo alishindwa kutokana na hali yake.
Credit: Gpl

USHIRIKIANO: Kagame ammwagia sifa Kikwete

$
0
0
Kagame na Jakaya Kikwete
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemwagia sifa Rais Jakaya Kikwete kwa kuboresha huduma za Bandari ya Dar es Salaam na kuwezesha mizigo inayosafirishwa kwenda Rwanda kufika mapema zaidi kuliko ilivyokuwa miaka michache iliyopita.

Akizungumza kwa furaha wakati marais hao walipotembelea kitengo cha kushusha na kupakia mizigo cha TICTS bandarini hapo jana, Rais Kagame alisema hatua iliyopigwa ni mafanikio kwa Rwanda.

“Napenda nimpongeze Rais Kikwete kwa mafanikio yaliyopatikana bandarini, kazi ikiwa nzuri (bandarini Dar), huko kwetu Rwanda tunafaidika,” alisema Rais Kagame. Alisema Rwanda itaendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika kibiashara.

Rais Kikwete alisema tangu ameingia madarakani, ameitembelea Bandari ya Dar es Salaam mara nne, lakini ziara tatu za mwanzo hazikuwa za furaha kutokana na wizi, ucheleweshaji wa mizigo na malalamiko yaliyokuwa yamekithiri bandarini hapo.

Huku akionekana mwenye furaha, Rais Kikwete alisema Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inatakiwa ipongezwe kwa kufanikiwa kuwaondoa wezi waliokuwa wakiirudisha nyuma.

“Kwa hiyo kusikia habari nzuri zinazofanywa hapa mnanifurahisha sana. Kulikuwa na genge la wezi, sifa mbaya, meli zinakaa siku 23, mambo ya ajabu sana, leo meli zinakaa kwa muda mfupi na hakuna udokozi, kumbe mnaweza kuwa waaminifu,” alisema Rais Kikwete.

'My Husband Is Too Big Down There, Takes Too Long To Finish' - Wife Complains On Facebook

$
0
0
According to a popular adage; One man's meat is another man's poison. What some ladies are crazy about, others are complaining. A woman posted this on Facebook complaining about how big her husband's d'1ck is, yet on top of that it takes 'forever' for him to finish, and so she is just not enjoying her s*x life anymore. She wants to see a divorce lawyer or report him to the police.

See the Facebook post below:


I am Looking For a Good Tanzanian Man To Love Me - Please

$
0
0

My name is Sarah living in Nairobi.

I am 26 years and as a person I like to think of myself as confident but not overly. I'm a very good girl. I understand that there's a time to love and I also believe in standing up for what I believe and not being walked on.

I'm always there for my friends and loved ones. I don't run from adversity. I care what people think of me because I believe in being the best woman I can be. I want people who come across me to think "hey what a cool lady". It's not about attention for me. It's about the importance of one’s own honour and respect for those around me.

I am a person who has a great ambition in life, a person who tries the best that I can and not afraid to fail because I believe that failure is just only a challenge on us to believe ourselves more similarly I am a person who has a good attitude or characteristic. Am trustworthy, honest, religious and most of all respectful, caring, loving, and simple,

I can’t deny the fact that I really want to meet a Tanzanian man that has a good heart, wherein he will accept me for who I am.......a person who is understanding in all aspects of life.

Because I came from a poor and simple family, my father is only a farmer, and my loving mother is a house wife and being the 4th sibling in my family, I really do the best of everything. I have a Bachelor of Education and currently working in Nairobi.

I am financially stable so I will not ask for specific characteristics, I just want a good and clean hearted man who can love me.

If you know for sure you are a good man, leave your email as a comment.

Sarah Mosha



Maneno Haya ya Faiza ni Darasa Tosha wa Wanawake Wengine

$
0
0
Staa wa Bongo Movies Faiza Ally ambae ni mzazi mwenza wa Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amebandika hili andiko hili mtandaoni, hebu chukua muda wako kulisoma andiko hili, kuna punje utazipata.

Nimepata marafiki wengi wapya - na wengine ni baada ya kuona kipindi kinacho endelea Jana (juzi) na leo (jana) Claud's TV - nataka tu niwaambie kwamba wakati huo wa uzuni na uchungu mwingi ulisha pita sasa hivi niko sawa kabisa na nimekubali matokeo ya maisha yaliopo sasa- na zile tofauti haziko tena na baba mtoto japo hatuko pamoja .    

Niwaambie tu kitu kimoja ni kwamba wakati unapo kuwa ktk wakati mgumu wa maisha unakua unaona kama haupiti na kipindi cha siku unaweza ukaona ni Kama mwaka kwa ule uchungu ulio nao- na pia unaweza unafanya Mengi kupitia wakati huo .

Faiza Ally
 Lakini cha msingi na muhimu usijasahau wewe ni nani na una thamani gani ktk maisha yako, ni kwamba lia futa machozi na uendelee na maisha yako - hakuna atakae badili maisha yako zaidi ya wewe - usikubali uchungu uka haribu maisha yako yote.

Jikaze simama na usonge - muweke Mungu karibu fanya vitu unavyo penda basi taratibu utarudi ktk hali yako ya kawaida na usimn'gan'ganie mtu asie kutaka atakuumiza zaidi hata kuhurumia kabisa  mwanaume ni mzuri pale anapo kuhitaji wewe Lakini akikuchoka hawezi kukumbuka hata jambo lako 1 zuri yote yatakua mabaya .. Lakini usiumie sana japo yanaumiza usijione hufai kwa ajili ya mtu mmoja mwingine akikuona wa nini wengine wanasema tutampata lini.

 Sasa nina furaha uchungu wa mapenzi uliisha na hauna nafasi tena kwenye maisha yangu nawaza mambo muhimu tu juu ya mwanangu maisha yangu na watu wangu wanao nikubali .... Basi msinipe pole tena maana nimechoshwa na pole kwa kweli - Asenteni- Faiza alimaliza.

 Asante Faiza kwa kushare nasi experience yako kuna watu wamejifunza kitu hapa, kila la kheri kwenye maisha yako.

Mzee wa Ubuyu

Diamond Platnumz Afurahi Ujauzito wa Zari Mpaka Ameanza Kupata Mashavu Dodo

$
0
0
Diamond na Zari
Unaambiwa kwa sasa katika Wanaume wenye Furaha Bongo Basi huwezi kumwacha nyuma Mwanamuziki Diamond, Furaha hiyo inatokana na Ujauzito aliompa Mrembo Zari , Diamond ameweka picha hiyo hapo kwenye ukurasa wake wa facebook akionyesha furaha yake huku akionekana kunawiri na kutoka shavu dodo........


Askofu Gwajima Atakiwa Kujisalimisha Kituo cha Polisi Haraka Kujibu Tuhuma za Kumtukana Askofu Pengo

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na:
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

Zitto atajwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti ACT Tanzania

$
0
0
Zitto ni mmoja kati ya wanaotajwa kugombea nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi wa chama cha ACT unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni....

Treni Yagongwa na Gari Maeneo ya Karume Jijini Dar es Salaam

$
0
0
TRENI ambayo ilikuwa na kichwa kimoja ikielekea kuchukua mabehewa asubuhi ya leo imegongwa na gari kubwa la mizigo eneo la Karume jijini Dar na kusababisha foleni ndefu eneo hilo.

Tukio hilo limejiri asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi bila kufuata alama za barabarani zinazoonesha sehemu ya reli.

Akizungumza na mwandishi wetu, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed  Kanka,  alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.

Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa  Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.

Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana  na madereva wasiokuwa waangalifu.

Hali ya Mama Yake Diamond si shwari, Diamond Agoma Kusema lolote

$
0
0
TUMUOMBEE! Afya ya mama mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz, Sanura Kassim ‘Sandra’ bado si shwari juzikati hali yake ilibadilika ghafla na kuilazimu familia yake kumkimbiza katika Hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar ambako amepewa kitanda, Ijumaa limetonywa.

Diamond alipotafutwa kuzungumzia afya ya mama yake aligoma kusema lolote zaidi ya kuomba aachwe kwani wanao uwezo wa kuzungumzia mambo mengine bila kugusia kuhusu mzazi wake.“Naomba unipe muda maana nina matatizo sana, hata kuzungumzia ishu hiyo nadhani hakuna haja,” alisema Diamond.

Nikifa mazishi yangu nataka yawe ya mwaliko maalum – Lady Jaydee

$
0
0
Lady Jaydee haogopi kufa na infact anataka mazishi yake yawe na mwaliko kama vile harusi zilivyo.

Katika muendelezo wa post zake ‘controversial’ Lady Jaydee ameweka picha za majeneza mawili ya kifahari ambayo anapenda akifa azikwe.

Hata hivyo ana masharti – mazishi yatakuwa ya mialiko maalum na hatopenda mwili wake ufunuliwe.

“I’ve changed my mind Sitaki tena lile la purple Moja kati ya hayo hapo juu #MsiMind #KilaMtuAtakufa #Msiogope Nilikuwa nafikiria pia iwe invitees only #SitakiKufunuliwa,” ameandika Jide.

Zari is far away from Wema...Look what she is doing and read what she wrote....

$
0
0
zari
Zari owns Several Ladies Clothing shops in Uganda and they are doing fine in terms of Business, she passed on one of her shop and wrote this on her Instagram page:

"The grass is not greener on the other side. The grass is greener where you water it..... Passed by the Store Today!"Zari

Barnaba: Diamond sio Mwanamuziki wa Kweli Anaimba Kiunjanja Tu

$
0
0
Jana, Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT, Barnaba Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa maelezo kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo alimtaja Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki' mwenye kujua kuimba muziki kiufundi.

Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati wakiimba.

Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.

Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye mwenyewe.

Watch "Diamond Platnumz ft Khadija Kopa - Nasema Nawe ( Official Music Video )

$
0
0
Watch "Diamond Platnumz ft Khadija Kopa - Nasema Nawe ( Official Music Video )" on YouTube - Diamond Platnumz ft Khadija Kopa - Nasema Nawe ( Official Music Video )

PHOTOS- Meet Soni The Most Beautiful Policewoman in Kenya

$
0
0
Gone are the days when Kenyan female cops were stone-faced ladies with pathetic body-shapes.

Nowadays, the police force is full of sexy cops with a body to die for. A case in example is this hot cop known  as Soni,  shes a real beauty. Check her gorgoeus photos below




Askofu Gwajima ajisalimisha kituo cha Polisi Kuhojiwa juu ya Kutoa Lugha Chafu Dhidi ya Askofu Pengo

$
0
0
Gwajima na Team yake
Pamoja na leo kipande cha sauti kusambaa kuwa Gwajima angejisalimisha Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu. Kwa sababu ambazo hazijatolewa bado, askofu Gwajima amejisalimisha kituo cha Polisi tayari leo Ijumaa ili kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live




Latest Images