Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Baada ya Kuzimia na Kuzinduka Gwajima sasa Atakiwa Kwenda Kujieleza Kwa Mkuu wa Wiliya ya Kinondoni Paul Makonda

$
0
0
Baada ya Jana Askofu Gwajima kuzimia wakati akijojiwa na Polisi kuhusu kumtukana Hadharani Askofu Pengo , Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda naye amemtaka Askofu Gwajima kufika ofisini kwake Jumatatu Kujieleza kwanini alitoa Maneno hayo machafu kwa Askofu mwenzake ....

"Hatuamini kama kweli imefikia wakati sasa nyumba za ibada zinatumika kama sehemu za kupashana badala ya kuhuburi injili ili watu waokoke"..alisema Paul Makonda

Kimenuka! Stella Tillya Aka Chagga Barbie Adai Mimba ya Zari si ya Diamond Bali ni ya Mr Katunzi..Diamond Analea Tu

$
0
0
In the on going battle between Zari and Chagga Barbie it has been revealed that Zari’s pregnancy is not Diamond’s! Chagga Barbie wrote to remind Zari that she is carrying a baby for a man she named by one name ‘Katunzi’

This message comes from a lady known as Stella Tillya or Chagga Barbie but due to some circumstances she calls herself Muke ya Muganda. Stella is a Tanzanian Socialite in USA.

Dr. Slaa amtembelea Gwajima TMJ hospital

$
0
0
Asalaam aleykum !
Dr slaa ameonesha upendo wa hali ya juu sana alipomtembelea mtumishi wa bwana askofu Gwajima, hali ilikuwa shwari utulivu wa hali ya juu na ulinzi ukiwa umeimarishwa mara dufu.

Nimejaribu kudadisi afya ya Gwajima inaonekana inaendelea vema na baadae tutajulishwa zaidi akipata nafuu na kuruhusiwa. Makachero wanamlinda Gwajima ila kivutio ulikuwa ujio wa Dr Slaa shughuli zilisimama na wagonjwa wakapata nafuu nakusema yuko wapi Rais wa mioyo ya watu tumshike mkono!

Tanzia: Mwanzilishi na Bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge afariki dunia..Chanzo cha Kifo Chake Hichi

$
0
0
Tasnia ya muziki wa kizazi kipya jana imepata pigo baada ya muasisi wa kundi la muziki la tiptop Abdul TaleTale (Abdul Bonge) kufariki jioni ya jana jumamosi

Abdul amefikwa na mauti alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni Kagera.

Marehemu atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya kuwaibua wasanii kama Madee, MBDog, PNC, PINGU NA DESO, KEYSHA, Z ANTON na Nk

Marehemu alipumzika kujishughulisha na Muziki na kumpisha Mdogo wake BABU TALLE Kuendelea na kazi hiyo.

Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera

Habari na Picha: Mkutano Mkuu wa ACT-Tanzania ulivyofana.

$
0
0

Zitto Kabwe akihutubia na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Tanzania.

NA KWA KUWA tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi.


KWA KUWA tumeamua kuhakikisha kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini

kwa nia moja tumeamua kujenga Chama chenye kufuata misingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa ACT wazalendo wakisikiliza wagombea nafasi mbalimbali
Wajumbe wakishangilia kwa pamoja hotuba ya hotuba ya Prof. Kitila ndani mkutano Mkuu
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Act wakifuatilia taarifa ya Chama Kwa umakini

Rais Kikwete: Serikali haitaanzisha Mahakama ya Kadhi

$
0
0

Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano.

Pia,Rais Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu suala la katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana.

Rais Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam.

Chanzo: ITV

Siri Imefichuka:Rais Kikwete “Abariki” Mbio za Urais wa Lowassa

$
0
0
SIRI imefichuka. Mbio za Edward Lowassa, kusaka urais kwa udi na uvumba, zimebarikiwa kwa asilimia 100 na Rais Jakaya Kikwete.
Lowassa amekutana na Kikwete mara kadhaa na kufunga makubaliano ya siri yanayolenga kumsaidia yeye kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Yote yanayofanywa na Edward (Lowassa), yamebarikiwa na Kikwete. Bila hivyo, Lowassa asingekuwa na ubavu wa kufanya anachokitenda,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.
Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Jamhuri.
Kuibuka kwa taarifa kuwa Lowassa amefunga makubaliano na Kikwete, kumekuja katika kipindi ambacho mwanasiasa huyo aliyeapa kufia katika vita ya kuwania madaraka, ameanza kupokea makundi ya wananchi akidai wanamuomba kugombea urais.

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, “Kikwete na Lowassa wanakutana sana, tena kwa siri. Wamejadili mengi, ikiwamo kinyang’anyiro cha urais. Itakuwa ajabu, bwana huyu kutokuwa mgombea kupitia CCM.”

Waziri mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa kufua umeme, kati ya serikali na kampuni ya Richmond, tayari amefungulia anaowaita “wafuasi wake,” kushawishi baadhi ya watu kwa lengo la kutafuta kila upenyo kuhakikisha anapata nafasi ya kushika utawala Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu walio karibu na mwanasiasa huyo, makubaliano yake na Kikwete ndiyo yanayomfanya kuwa “mbogo” hadi kuikuka taratibu za chama chake.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu – kuchagua rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online anasema, pamoja na kuwapo makubaliano hayo, bado Lowassa hawezi kujihakikishia nafasi ya kuwa mgombea.
Anasema, Lowassa anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa makundi ya yaliyopachikwa jina la “wahafidhina” ndani ya chama chake.

Tumia Bidhaa za AFRICAN BEAUTY PRODUCTS Kupata Muonekano wa Kupendeza kwa Kuongeza Hips, Makalio, Mapaja, Kurefusha Nywele na Mengine

$
0
0

Je unataka Kuwa Mrembo na Muonekano wa Kupendeza kwa Kuongeza Hips, Makalio, Mapaja, Kurefusha Nywele, Kupunguza Unene na Kuondoa Tumbo? Basi African Beauty Products Wanakuletea Hii:
Kabla ya Kutumia Dawa na Baada ya Kutumia Dawa zetu

1.Kuongeza Hips Makalio na Mapaja 100,000/
2.Kunenepesha Miguu iwe chupa ya Bia 70,000/
3.Kuwa Mnene Mwili Mzima 80,000/
4.Kupunguza Tumbo na Nyama Uzembe 80,000/
5.Kupunguza ama Kuongeza Maziwa 60,000/
6.Kuwa Mweupe na Soft Mwili Mzima 100,000/
7.Kuondoa Chunusi na Madoa 60,000/
8.Kuondoa Michirizi na Mabaka 70,000/
9.Kupunguza Unene Mwili Mzima  80,000/
10.Kuongeza urefu na unene wa Uume 90,000/

Bidhaa Zetu ni Uhakika Matokeo  Ndani ya Week Moja..

Tuwasiliane kwa Simu Namba:
0756697906 ,0716805391 au 0783300397
Kwa watu wa Dar es Salaam Utaletewa Popote Ulipo ..Kwa Watu wa Mikoani tunatuma kwa Basi

Zitto Kabwe Ameshinda Nafasi ya Kiongozi Mkuu wa- ACT Wazalendo

$
0
0
Hongera sana ndugu zitto zuberi kabwe kwa kujinyakulia nafasi ya kiongozi mkuu, kazi iliyoko mbele yako ni kukitangaza chama kitaifa ili uweze kuwa na wabunge na mdaiwani-octoba 2015,Hakuna kazi kubwa kama kuwa kiongozi inahitaji busara na hekima ya hali juu

Diamond new song already trending in Nigeria and a hit in Youtube less than 24 hr

$
0
0
From Nigeria Blogs:

Diamond Platnumz Released yet another outstanding video to his recent single entitled Nasema Nawe featuring Khadija Kopa. Directed by Hanscana, peep it below.


Read more at DOWNLOAD VIDEO: Diamond Platnumz – Nasema Nawe ft. Khadija Kopa | 360Nobs.com

http://www.360nobs.com/2015/03/video-diamond-platnumz-nasema-nawe-ft-khadija-kopa


MY TAKE

In less than 24 hours has already had over 120,000 youtube hits! This guy is in his own level! Surprising none of entertainment media in Kenya has covered his new song release be it ghafla or Mpasho! Is this sabotage the entertainment industry in Kenya was trying to do on Diamond since he refused to involve himself in a beef between Jaguar and Nigerian artists?

Hemed PHD Afunguka Kuhusu Kutumia Poda za Kike, Ndoa yake Kubuma na Kwanini Anapendwa Sana na Wadada

$
0
0
Udaku Special TV inakuletea Mahojiano tuliyoyafanya na Mwanamuziki na Mwigizaji Mwenye Skendo Nyingi Bongo..Tulimweka Mguu Kati na Kumbana Vilivyo na Kuweza Kufunguka Kwanini Anatumia Poda na Lipshine za Kike pia Kuhusu Ndoa aliyohaidi 2014 kubuma na mwisho alisema kwanini anapendwa na Wadada mpaka muda mwingine kumgombania

 ANGALIA VIDEO FUPI HAPA CHINI AKIFUNGUKA UKWELI WAKE:

Polisi Yawashikilia Watu 15 Kwa Kosa la Kula Njama ya Kumtorosha Gwajima, Majina yao Haya Hapa

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
29/03/2015
WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao hivyo waliwakatalia kuingia.
Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa kundi hilo.
Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa na Begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya PUMAChaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi, Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24, Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62, Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30, Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva, Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60, Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39, Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Kauli ya Askofu Pengo Baada ya Sakala la Gwajima Kumtukana Kupitia Mitandao ya Kijamii

$
0
0
'Kuna mtu mmoja,ambaye hata jina lake silikumbuki,ameinuka na kunena maneno juu yangu,ambayo yamewaudhi baadhi hata yenu.Langu mimi kwake ni msamaha tu,nasema nimemsamehe kutoka ndani ya chembe ya moyo wangu kabisa.
Endapo liko jambo linafanywa na wakuu wa serikali,nadhani hao wanatekeleza tu wajibu wao.
Mimi narudia tena, nimemsamehe tena kabisa na ninawaomba tumuombee ili Mungu adumishe amani ya Taifa hili.' Pengo amesema

Afrika Magharibi yakoshwa na utamaduni wa mswahili uliooneshwa na Diamond kwenye video ya ‘Nasema Nawe’

$
0
0
Video hiyo inaonesha utamaduni wa mswahili wa pwani ambaye amerithi mambo mengi kutoka kwa waarabu.

Hivi ni vitu ambavyo Afrika na dunia nzima imevisoma kwenye historia ya ukoloni. Kupitia video na wimbo wake, Diamond amewapa mashabiki wa muziki wa Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nchini zingine nje ya Afrika Mashariki, picha halisi ya maisha ya mswahili.

Taarab na mduara ni nyimbo zenye asili ya Tanzania na hivyo wimbo kama ‘Nasema Nawe’ inawakilisha kile tunachoweza kusema kwa kujigamba kuwa ni muziki wa Tanzania. Kitendo cha kumuongeza Khadija Kopa, malkia wa mipasho nchini, kimeuongezea thamani kubwa sana wimbo huo.

Nisisahau kusema kuwa Khadija Kopa na Hanscana wamewekwa kwenye sehemu ambayo sasa jicho la Afrika linawaona.

Hivi ni vitu vigeni kwa nchini kama Nigeria na Ghana. Hivi ni vitu ambavyo wasanii wao hawawapi kwasababu sio utamaduni wao. Ndio maana pamoja na kutoelewa Kiswahili, bado wamevutiwa na video na wimbo huo kwasababu wanasikia ladha mpya na kuona picha za tofauti.

“I dont understand a single word,but Diamond is honestly as his name says. Loyal fan from Namibia. #teamdiamond,” ameandika Rauha Vroutjie.

Jana jina la Diamond lilifanikiwa kushika namba moja kwenye trend topics za kwenye mtandao wa Twitter masaa machache tu baada ya kuachia video hiyo. Kwa msanii wa Tanzania kutrend Lagos, Nigeria si kitu cha kawaida, ni kikubwa.

Diamond amevuka hatua ya kuwa msanii maarufu Tanzania peke yake na kuwa msanii maarufu Afrika. Akishuka Luanda, Angola ama Gaborone, Botswana, hakuna shaka wengi watakuwa wanaifahamu sura yake.

Sehemu alipofikia ana uwezo wa kufanya wimbo wowote na Afrika ikamuelewa. Kutengeneza wimbo wenye vionjo vya Tanzania ni uamuzi mzuri zaidi alioufanya.

Kwahiyo msisitizo ninaopenda kuutoa hapa ni kwamba hatuwezi kuwashtua wanaijeria ambao kwa sasa ndio wameushikilia muziki wa Afrika, kama tukiiga muziki wao na kuwapa ladha ile ile wanayopewa na wasanii wao. Hawawezi kushtuka!

Hebu fikiria mfano huu. Kama wewe ni mkazi wa Bukoba na ukaja kumsalimia ndugu yako wa Dar es Salaam halafu chakula pekee atakachokupa kikawa ni ndizi, utajisikiaje? Umeziacha ndizi pomoni Bukoba halafu unakuja Dar unapikiwa ndizi tena? Tafakari.

Kwahiyo wasanii wanaopata bahati ya kuwashirikisha wasanii wakubwa wa Nigeria au Afrika Kusini, ili collabo zao zionekane za maana wanatakiwa kutengeneza nyimbo zenye ladha ya Tanzania ili kuwapa wapenzi wa muziki huo muziki tofauti.

Kwa wasanii ambao wamepata bahati ya kuwa na majina makubwa, kama wanataka kuchukuliwa serious, wahakikishe kama hawatengenezi nyimbo zenye mahadhi ya dunia (universal genres) ambazo ni pamoja na Hip Hop, R&B ama Pop, basi watengeneze nyimbo zenye ladha halisi ya Tanzania, yaani Bongo Flava.

Mtanzania akifanya Kwaito au muziki wa Naija nahisi kama hatofika popote.

Hiki Ndo Chanzo cha Kifo cha Abdul Bonge, Mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection

$
0
0
Kifo cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul  Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, juzi jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini.

Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.

Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
"Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo"– Babu Tale.

Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo

Jela ilivyovunja Uhusiano wa Mastaa Bongo Hawa wa Bongo Movies

$
0
0
Katika ulimwengu wa wapendanao kuna changamoto nyingi ambazo wapenzi hukutana nazo huku wengine wakizishinda na baadhi kushindwa.

Wapo wapenzi walioshindwa kuendelea na uhusiano wao mara baada ya mmoja kuugua, kupata ulemavu na sababu nyingine nyingi, lakini wapo walioendelea kuvumiliana pamoja na sababu zote hizo na hatimaye penzi lao likazidi kuimarika na kuwa mfano katika jamii.

Hali hiyo haipo kwa watu wa kawaida peke yao bali hata kwa mastaa wetu wamejikuta wakiangukia katika mtihani huo na kushindwa kuhimili kusimamia mapenzi yao. Kifungo au jela ni moja ya sababu zinazosababisha ndoa au uhusiano wa mastaa wengi na wenza wao kuharibika.
Katika makala haya tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao wamekumbwa na sakata hilo:-

Jack Patrick,
Mumewe na Jux
Jack Patrick ambaye aliwahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania 2011, alijikuta akitiwa jela mwishoni mwa mwaka 2013 huko Macao, Hong Kong, China baada ya kudaiwa kukutwa na kete 66 za heroin. Wakati Jack anatumikia kifungo chake mumewe wa ndoa, Abdulatif Fundikira alidaiwa kushindwa kuvumilia na kumuoa kisiri Miss Tanzania 2011, Salha Israel hivyo kuhitimisha rasmi uhusiano wao.

Hata hivyo, wadadavuzi wa mambo walidai kuwa hiyo ilitokana na malipizi kwa kuwa hata wakati Abdulatif aliposwekwa lupango akihusishwa na ishu hiyohiyo ya madawa ya kulevya, Jack Patrick naye aliwahi kumsaliti kwa kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’.

Kajala na Mumewe
Kajala ni staa wa muvi ambaye sakata lake lilianza baada ya yeye na mumewe kuswekwa ndani kwa kosa la kutakatisha fedha na mashtaka mengine. Kajala alitakiwa kutoa faini ya shilingi milioni kumi na tatu (13) au kwenda jela miaka saba (7) huku mumewe, Faraja Chambo akienda jela kutumikia kifungo cha miaka 12 baada ya kushindwa kutoa faini ya shilingi milioni 213.  Ashukuruwe Wema Sepetu ambaye alimtoa Kajala kwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akiwa uraiani, Kajala alidaiwa kushindwa kuvumilia kukaa na upweke na kukwaa skendo za mapenzi ikidaiwa kutoka na wanaume tofauti lakini kubwa ni ya kutoka na Kigogo mmoja (jina tunalihifadhi) anayetanua naye sehemu mbalimbali wakati mumewe akiozea jela bila msaada wowote kutoka kwake, japokuwa mara kadhaa amekuwa akimuomba Kajala amtoe.

Binti Kiziwi na Z. Anto
Baada ya kutoka na video ya Wimbo wa Binti Kiziwi, Mbongo Fleva, Z. Anto aliamua kumuoa binti aliyetumika katika video hiyo ‘video queen’ (Sandra Khan).

Hata hivyo, misukosuko ya ndoa yao ilianza baada ya kutimiza miaka mitatu ambapo Z. Anto na Sandra walitengana kwa kudai kuwa mkewe alikuwa akishirikiana na makundi mabaya. Uhusiano wao uliisha rasmi baada ya Sandra kunaswa mwanzoni mwa mwaka 2013 huko Hong Kong, China akiwa na ‘mzigo’. Katika moja ya mahojiano, Z. Anto alidai kuwa kwa sasa anaendelea na maisha yake na anatafuta msichana mwingine wa kuoa.

Aunt Ezekiel na Sunday Demonte
Staa wa muvi, Aunt Ezekiel aliwashtusha watu baada ya kuolewa na Sunday Demonte, Mtanzania aishiye ughaibuni.

Habari zilidai kuwa mumewe huyo ameswekwa rumande jijini Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) kwa kesi ya madawa ya kulevya. Kama mastaa wengine, Aunt Ezekiel naye alishindwa kujizuia na kuchepuka na dansa wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, Mose Iyobo na hatimaye kubeba mimba ambayo siyo ya mumewe Sunday.

Chanzo: GPL

Prof. Lipumba Akwepa Uzinduzi Wa ACT- Wazalendo

$
0
0
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa chama cha ACT-Wazalendo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Prof.Lipumba anadaiwa kukwepa uzinduzi wa chama kipya cha siasa cha ACT-wazalendo. Uzinduzi wa chama hicho umefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo 29 Machi 2015.

Aidha,Prof. Lipumba ni miongoni mwa wageni walioalikwa kutoa mada katika uzinduzi wa chama cha ACT-Wazalendo kufuatia habari zilizotolewa na chama hicho.

Hata hivyo wageni waalikwa kutoka nje ya nchi ambao ni Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa Ghana, Osagyefo Kwame Nkrumah.
Wengine ni Ababu Namwamba-Katibu Mkuu wa Chama cha ODM cha Kenya; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya, mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini, kiongozi wa vyama rafiki vya Ujerumani, Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto Progressive Alliance nao hawaja hudhuria uzinduzi wa chama hicho.

Katika hatua nyingine wanachi mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuhudhuria uzinduzi huo.

Vurugu na Matusi Zatawala Kwenye Semina ya Wabunge Kuhusu Sakata la Mahakama ya Kadhi......Wabunge Wegi Wapinga Kuanzishwa Kwa Mahakama hiyo

$
0
0


Mambo magumu yameibuka katika suala la kujadili uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, baada ya kutokea  malumbano makali na vurugu huku idadi kubwa ya wabunge wakiitaka serikali kuuondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe bungeni. 

Wabunge wengi walisema kufanya hivyo kunaweza kusababisha mpasuko na kuvunjika kwa amani nchini.

Aidha, wamesema suala la Mahakama ya Kadhi linataka kufanywa kama mtaji wa kisiasa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ili kutafuta kura za Waislamu.

Mvutano huo uliibuka jana wakati wa semina ya wabunge kujadili Muswada wa Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 ambao ndani yake kuna  Muswada wa Mahakama ya Kadhi ambao umepangwa kuwasilishwa Aprili Mosi mwaka huu siku ya kuahirisha mkutano wa 19 wa Bunge.

Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratias Ntukamazina, alisema Kamati ya Katiba Sheria na Utawala ilipowaita viongozi mbalimbali wa dini kuzungumzia suala hilo Waislamu walitofautiana katika suala la uteuzi wa Kadhi kufanywa na Mufti Mkuu wa Tanzania na wakataka waelewane kwanza kabla ya suala hilo kupelekwa bungeni.


Alisema katika mkutano huo makundi 11 ambayo hayakubaliana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), walisema Muswada wa Mahakama ya Kadhi uletwe bungeni baada ya kuridhiana kwa sababu hawakubaliani na Bakwata ambalo kiongozi wake ni Mufti Mkuu wa Tanzania.

Walisema maaskofu walisema hawana tatizo na suala la Mahakama ya Kadhi, lakini isiwe na muundo kama wa mahakama nyingine na kwamba mawazo ya waasisi wa Taifa, hawakutaka serikali iwe na dini na ndiyo maana hawakuruhusu mahakama hiyo.

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Rukia Kassimu, alihoji ni kwanini Mahakama ya Kadhi inataka kuundwa na kupewa jukumu Mufti ambaye anatoka Bakwata ambayo ni taasisi binafsi na imesajiliwa na Mamlaka ya Rita.


“Bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine, haikubaliki, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi suala la Mahakama ya Kadhi ili Waislamu wampigie kura kwa sababu anataka kugombea urais mwaka huu, alisema.

Rukia alisema ni marufuku serikali kuwalazimisha Waislamu kuwa chini ya Bakwata na kwamba Waziri Mkuu, Pinda anafahamu kwa kina suluhisho na mvutano huo wa Mahakama ya Kadhi.

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), Moses Machali,  alisema suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kuingizwa katika mfumo wa mahakama za kawaida inajichanganya na ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema mwaka 2011 Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua msikiti wa Gadaf alisema suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi lisihusishwe na serikali kwa sababu wapo watu wengine ambao kila mmoja ana imani yake.

Alisema hatua ya serikali kutaka kuuleta muswada huo wakati bado Waislamu wenyewe hawaelewani ni kuwakosea Waislamu na kwamba inawezekana Waziri alilizungumzia suala hili sababu ya malengo yake ya urais.


Machali alisema kama muswada huu utapelekwa Bungeni itatoa fursa kwa madhehebu mbalimbali kila moja kuanzisha mahakama yake hali itakayoleta machafuko nchini kwa kuwa nchi itakuwa katika mfumo wa mahakama za dini.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema muswada unapendekeza kutambua kitu ambacho mfumo wa sheria za nchi hauna na kwamba uongo unaotumiwa na serikali ndiyo unafanya watu wawe na hofu.

Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM), Ally Kessy, alisema: “Katika nguzo tano za Kiislamu Mahakama ya Kadhi haipo, nguzo sita za imani pia haipo, sasa inakuwaje wanadai kitu ambacho hakitambuliki katika nguzo za kiislamu.”

Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi urudishwe ukaboreshwe badala ya kuharakisha kuupeleka bungeni wakati bado una utata hata kwa waislamu wenyewe.

Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambali Nyangwine, alisema Muswada  wa  Mahakama  ya  Kadhi usimamishwe ukafanyiwe utafiti kwanza kwa sababu ndani ya Waislamu wenyewe hawaelewani.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alisema Wabunge wasipokuwa makini na suala la Mahakama ya Kadhi, Bunge litaingia katika historia kuvunjika kwa amani.


Selasini alisema serikali iachane na kutoa ‘jini’ lililofungiwa na waasisi Mwalimu Nyerere na Karume na kwamba tukifanya mchezo nchi itabaki katika vipande vipande.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa,  alisema jambo hili litaligawa Taifa na kwamba waasisi hawakuwa wajinga walipokataa serikali isiwe na dini.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa, alisema nchi inaelekea kubaya kwani msingi wa kuleta Mahakama ya Kadhi ni kutaka kuwachota Waislamu kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

“Serikali kama imedhamiria kuleta Mahakama ya Kadhi ilete katika utaratibu mzuri, lakini kwa huu utaratibu ni unafiki na mwenyezi Mungu hapendi unafiki, tusiwahadae Waislamu,” alisema.

 Khalifa alisema kwa hali ilivyo muswada huo haujaiva na kwamba usiletwe  bungeni hadi hapo serikali itakapojipanga vizuri.

 Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema),David Silinde, alisema suala la imani siyo la chama cha kisiasa kwani suala la Mahakama ya Kadhi litaipeleka nchi kubaya na inawezekana ikawa ndio mwisho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Mnataka kutuvurugia nchi sababu ya kutafuta kura za Waislamu, kwa hili Waziri Mkuu umechemka sana, nalisema hili kwa sababu wewe Waziri Mkuu ndiye uliyeahidi kuleta bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi,” alisema.

Mbunge wa Kisarawe (CCM), Suleiman Jafo, alisema yasifanyike masikhala mswaada huyo uwasilishwe bungeni.

Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM),Mchungaji Lackison Mwanjale, alisema serikali ikajipange upya katika suala la Mahakama ya Kadhi kabla ya kuuleta bungeni muswada kwani bado suala hilo halieleweki kwa jamii.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM),Martaza Mangungu, alisema hakubaliani na suala la Mufti kupewa jukumu la kuchagua Kadhi Mkuu wakati Waislamu wengi hawakubaliani na Bakwata ambayo inaongozwa na Mufti.

Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi wapelekewe wahusika kabla ya kuletwa bungeni ili wajadiliane na kukubaliana mambo ya msingi wanayoona yatawafaa katika uanzishwaji wa mahakama hayo.

 Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Peter Kafumu, alisema serikali imeshindwa kusimamia vizuri suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi jambo hilo.

Mbunge wa Chwaka (CCM), Yahaya Kassim Issa, alisema  Waislamu wanataka Mahakama hiyo kwa kuwa wanakosa haki hivyo serikali iruhusu kuanzishwa kwake.

Pinda: Tutatafakari  Upya

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akihitimisha mjadala huo alisema kulingana na maoni yaliyotolewa na Wabunge ameelewa kwamba bado hakuna maelewano miongoni mwa Waislamu wenyewe na pia hakuna uelewa wa jamii kuhusu suala hilo.

Alisema mambo yaliyowasilishwa kuhusiana na muswada huo ni maamuzi ya Bunge Maalum la Katiba na siyo yake, bali anabebeshwa msalaba tu kwa sababu alikuwa anaiwakilisha serikali.

Pinda alisema kutokana na hali hiyo, serikali itakaa kushauriana tena na Spika pamoja na Rais waone wafanye nini katika jambo hilo.

Vijembe  na  Matusi

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, wakati akichangia hoja hiyo alishindwa kuvumulia baada ya baadhi ya wabunge kuingilia mchango wake kwa kumzomea na kusema maneno yaliyomuudhi na kuamua kuwatolewa maneno ya kuudhi (matusi).

Mbunge wa Fuoni (CCM), Said Mussa Zubeir, aliwaita baadhi ya wabunge walikuwa wakimzomea wakati akizungumza kuwa ni ‘wapumbavu’.

Wakati wa majadiliano hayo ilipofika saa 8:17 wakati Mbunge wa Kisarawe, Jafo akiendelea kuchangia kulitokea vurugu ambazo nusura wabunge wapigane huku baadhi yao wakiamua kutoka ukumbini.

Kutokana na kutokuwapo hali ya utulivu ukumbini, baadhi ya askari pamoja na maofisa usalama waliokuwapo nje, walilazimika kuingia ndani kuhakikisha amani haivunjiki.

Spika wa Bunge, Anna Makinda, alituliza  vurugu  ukumbini kwa kuwataka wabunge wawe wavumilivu wakati wenzao wakichangia.

Katika majadiliano wabunge zaidi 30 walichangia na zaidi ya 20 walikataa muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe Bungeni  siku ya Jumatano wiki hii.

Kabla ya kuanza majadiliano, Mbunge wa  Kuteuliwa, James Mbatia, alitoa hoja kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, kwamba wakati wa majadiliano waandishi wa habari wasiwepo ukumbini kwa kile alichoeleza ni unyeti wa jambo hilo.

Hata hivyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini,Kessy, alisema kama waandishi wataondolewa ukumbini naye atalazimika kuondoka huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, akisema hakuna sababu ya kuwaondoa waandishi kwa sababu jambo linalojadiliwa wananchi wanataka kulifahamu kupitia vyombo vya habari.

Ndugu wa Marehemu Abdu Bonge Wataka Uchunguzi zaidi Ufanyeke Kuhusu Kifo Chake, Mwili Wahamishiwa Hospital ya Muhimbili

$
0
0

MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge, mapema leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Mtandao huu ulishuhudia jamaa wa marehemu huyo wakiuhamisha mwili huo wakisema ni lazima mwili huo ukafanyiwe uchunguzi wa kina kutokana na utata wa kifo chake.

Mdogo wa marehemu aitwae Idd Taletale alisema endapo uchunguzi huo utamalizika leo utasafirishwa leo kuelekea Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.

Ngasa Aendelea Kuipasua Kichwa Yanga..Sasa Anataka Mshahara wa Mil 6 kwa Mwezi la Sivyo...

$
0
0

YANGA imetamka kuwa haina lengo la moja kwa moja kuachana na mshambuliaji wao Mrisho Ngassa na katika kuthibitisha hilo kwa vitendo, tayari uongozi wa klabu hiyo umeweka mezani Sh. 80 Milioni wakimtaka asaini dili jipya la kumbakisha timu hiyo.

Mmoja wa mabosi wa klabu hiyo aliyeko katika kamati ya usajili amesema kuwa uongozi wao chini ya mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji hauna nia ya kutaka kumtosa Ngassa ambapo tayari wameshampatia ofa hiyo kuhakikisha anasaini mkataba mpya.

Bosi huyo alisema katika ofa hiyo, Ngassa amepewa masharti mawili muhimu ambapo ametakiwa kutumia sehemu ya fedha hizo kumaliza deni lake la benki analodaiwa huku mshahara wake wa Sh. Mil. 4 ukibaki kama ulivyo.

Hata hivyo sharti hilo la mshahara linaenda tofauti na ofa ambayo Ngassa alitaka kupatiwa na klabu hiyo akitakia alipwe dola 3,500 (Sh. Mil 6.5) kwa mwezi ombi ambalo uongozi wa Yanga umeligomea.

“Hatuna nia ya kumuondoa Ngassa kuna vitu ambavyo anakosea, anaongea sana, haangalii kwamba juhudi zetu tunazozifanya tumeshampatia ofa hiyo afikirie sasa kama kweli anataka kubaki hapa,” alisema bosi huyo.

“Tumempa hiyo ofa lakini tatizo lake ni moja anataka mshahara mkubwa sana, kiasi ambacho ametaka tumpatie ni kikubwa sana kama atakuwa muelewa katika hili atakubali kusaini.”

Ngassa amekuwa akionekana kujuta kwa maamuzi yake ya kukataa ofa ye kwenda El Merreikh ya Sudan iliyomtaka wakati akiwa Simba kwa mkopo akitokea Azam ili tu akipige Yanga na kukumbana na adhabu ya kuwalipa Wekundu wa Msimbazi fedha alizosaini awali kabla ya kukimbilia Jangwani..

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images