Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

TAZAMA PICHA ZA MWANAJESHI FEKI ALIYEKAMATWA LEO TANGA AKIMTAPELI DC

$
0
0
'Koplo' feki akiwa na pamoja na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko

Na Mashaka Mhando,TANGA
VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa,vinamshikilia Edwin
John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na
kujitambulisha kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka
kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa. "Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego
Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani
hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa
kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT).

Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye
ni afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani
ambapo aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate nafasi. 
Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya
Tanga,Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa
Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi. 
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema
baada ya mahojiano ilibainika kuwa Mponji sio askari wa JWTZ ndipo
akalazimika kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa
alipopekuliwa alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo. 
Alisema wakati akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la
Polisi lakini alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni
alifanya njama za kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka
ambaye alitoweka nayo. 
Mponji alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya
jeshi la Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya
kueleweka juu ya wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri
kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841
KJ Mafinga. 
Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili
kubaini mtandao wake.

MWIGIZAJI WA ISIDINGO LESEGO MOTSEPE AMEFARIKI DUNIA

$
0
0

JOHANNESBURG – South African actress Lesego Motsepe, best known for her role as Lettie Matabane in the SABC 3 soapie Isidingo, has died.

Motsepe was found dead at her Randburg home at around 11 am on Monday.

On World Aids Day in 2011, the actress disclosed that she had been living with HIV since 1998.

Family spokesperson Gabi Tabane says the family are saddened by the loss.

“Today, we are really heartbroken to share that Lesego Motsepe passed away. She was found dead this morning at 11 o’clock by her brother Moemise Motsepe,” he says.

“She was confirmed dead at one o’clock by paramedics who indicated that she died of natural causes.”

Motsepe was 39 years old.

In 2012, Motsepe revealed she had decided to end her use of antiretroviral medication and rely instead on a special diet.

The announcement was met with condemnation by HIV and Aids activists.

ONYO KWA WANAOPENDA KUCHAFUA WATU WENGINE MAKUSUDI KWA KUPITIA COMMENTS

$
0
0
Kumekuwa na Tabia ambayo imeanza kujitokeza siku za karibuni kwa watu kuchafua wengine kwa makusudi kwa kupitia comments as Anonymous wakizani kuwa hatuwezi kuwajua...Hiyo ni tabia isiyo vumilika kabisa katika jamiii ..kuanzia sasa ikiwa utamchafua mtu na muhusika akilalamika tutachukua jukumu la kufuatilia wewe ni nani na kukuchukulia hatua zinazohusika....
Asante...Enjoy Posts zetu

DIVA LOVENESS AMCHANA STARLISHA KIANA KWA KUANIKA MESSAGE PRIVATE ZA PREZZO MTANDAONI

$
0
0
Mtangazaji matata wa Clouds Fm Anayejulikana kwa jina la Loveness Diva jana usiku katika kipindi chake Alifunguka kiana kuhusu wapenzi wanapogombana na kuanza kuweka mitandaoni Private Message walizokuwa wanatumiana wakiwa ndani ya Mapenzi...Aliwaasa wakina dada waache huo mchezo kwani ni kujiabisha mbele ya jamiiii ..kwani inafika mahali mpaka unasema jinsi maumbile ya mpenzi wako yalivyo...Hili linaonekana ni ndogo kiana kwa Mwanadada Starlisha a.ka Chagabibie Ambae Jana Ilikuwa Gumzo mitandaoni Baada ya Kuweka Conversation zake na Prezzo Aliyekuwa Mpenzi wake na kufikia kumwita Kibamia ...

Je wewe unasemaje ...ni sahihi kuweka private msg za mpenzi wako online baada ya kuachana?

MADAWA YA KULEVYA KWA WANAWAKE NI JANGA-WAPEKULIWA MPAKA SEHEMU ZA SIRI

$
0
0
Na Makongoro Oging'
JANGA la kusafirisha madawa ya kulevya Bongo limezidi kuwa zito kufuatia takwimu za hivi karibuni kuonesha kwamba, idadi ya wanawake kujihusisha na shughuli hiyo inazidi kupanda.

Akizungumza na Uwazi juzi, Kamanda wa Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alisema wanawake wamekuwa ni janga kwa kuwa  wanaongoza kwa kukamatwa kutokana na kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ‘unga’.

NZOWA AANIKA MAMBO
Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Kamanda Nzowa alisema inasikitisha, inashangaza kwani kwa kipindi kifupi cha kuanzia Desemba 11, 2013 mpaka Januari 6, 2014  watuhumiwa watano walikamatwa na unga, kati yao wanawake walikuwa wanne.

“Hata mwaka jana mpaka Juni, wengi wa watuhumiwa tuliowakamata ni wanawake ukilinganisha na wanaume, hii ni mbinu inayotumiwa na wasafirishaji wa mihadarati kwa kuwatumia wanawake,” alisema Nzowa.

ANAJUA KITAKACHOENDELEA
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Tunajua, wahusika wakiona wanawake wanadhibitiwa sana watabadilisha na kutumia wanaume kusafirisha madawa hayo, hii hali inatisha lakini tumeigundua.”

UWANJA WA NDEGE DAR UPENYO?
Nzowa alisema kuwa, watuhumiwa wote hao walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar wakiwa wamepakia kete za madawa hayo tumboni wakiyasafirisha kwenda nje ya nchi.

KUPANDA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE
Kamanda huyo aliongeza kwamba wanawake watatu walikamatwa Desemba 11, mwaka jana uwanjani hapo wakiwa na madawa tumboni wakielekea nchini China.

Aliwataja wanawake hao kwa ni, Mariam Hamad (29), mkazi wa Tabata- Kimanga, Dar. Alikutwa na pipi zenye uzito wa gramu 670. Hadija )Abdu (30, mkazi wa Magomeni, Dar alikutwa na kete zenye uzito wa gramu 1,227.

Wengine ni Sabrina Salum (34), mkazi wa Kiwalani, Dar. Alikutwa na unga wenye uzito wa gramu 310 na Salama Omar (miaka haikutajwa), mkazi wa Tabata, Dar alikutwa na madawa yenye uzito wa gramu 1,975. Alikamatwa Januari 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kukamilika.

Imeelezwa kuwa, wanawake wengi wamekuwa wakitumika kusafirisha unga kutokana na tabia iliyokuwepo huko nyuma kwamba, walikuwa wakiaminika na hawakuwa wakikaguliwa kwa undani walipokuwa wakipita viwanjani.

NZOWA ATAHADHARISHA 
“Nawatahadharisha wale wote, wakiwemo wanawake wenye nia au wanaofanya biashara hii haramu kuacha kwa sababu vyombo vya dola vitawakamata,” alisema Nzowa.

WANAOGOPWA VIWANJA VYA NDEGE
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipohojiwa na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema wanawaogopa sana wanawake wanaosafiri siku hizi.

“Hivi sasa tunawaogopa sana wanawake wanaosafiri kwa ndege kuliko wanaume kwa sababu wanaweza kukuingiza katika matatizo ikiwa watapenya na madawa ya kulevya na kukamatwa hapa Dar au huko nje ya nchi,” alisema mfanyakazi mmoja.

Alifafanua kwamba, kutokana na hilo wamekuwa wakiwapekua wanawake kila sehemu za miili yao hata sehemu nyeti ikibidi ili kuhakikisha hawapiti na madawa hayo uwanjani hapo.

WANAWAKE HAO WAPO MASTAA
Hivi karibuni baadhi ya mastaa Bongo wamenaswa kwa kujihusisha na biashara hiyo. Baadhi yao walikutwa na hatia na kuhukumiwa, wengine kesi zao zinaendelea.

Wasanii hao ni Jacqueline Patrick (alikamatwa Macau-China), Saada Kilongo (JNIA-Dar), Agnes Gerald  ‘Masogange (Afrika Kusini) na Melisa Edward (Afrika Kusini). Pia yumo Mbongo aliyenaswa Misri aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma huku Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ akitumikia kifungo cha miaka mitano China.

JK AKASIRIKA, AWAONYA WASANII
Akizungumza katika mkutano mmoja na wasaniiwa Rais  Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ alionesha hasira zake za wazi kwa wasanii wanaotumika kubeba unga kwenda nje ya nchi.

JK aliwaonya wasanii wenye tabia hiyo na wale ambao wapo katika ushawishi wa kujiingiza kwenye biashara hiyo inayopigwa vita kwa sasa duniani kote kuacha kufanya hivyo. 

PARTY 2:PRIVATE MESSAGE NYINGINE ZAIDI ZA PREZZO NA CHAGGA BARBIE

$
0
0
 
Lile penzi la mkali kutoka Kenya Prezzo na mdada kutoka uchagani Chagga Barbie limeota mbawa na hatimaye kilichofata ni matusi kuwekeana mambo hadharani bila hata aibu, Mdada ameamua kumwaga kila kitu hadharani na hapo chini ni kila kitu alichoongea mwanadada kutoka TZ aishie USA.
 Swahilitz imefatilia mkasa huu na tumeona sio mbaya tukakuwekea picha hapa uone jinsi mdada alivyofunguka vya kutosha. 












- See more at: http://cutelady05.blogspot.com/2014/01/exclusiveeee-matusi-na-siri-zote-za.html#sthash.Yv9Y8r9G.dpuf

MAMA WEMA AFUNGUKA KUHUSU DIAMOND.

$
0
0
Huu ndio ujumbe wake:

“Mimi nimekerwa sana na huyo Diamond wenu. Najua hajamrudia Wema kwa mapenzi, amemrudia ili apate nafasi ya kumharibia maisha. Ni kijana hatari sana.
“Nina taarifa kutoka kwa watu wa karibu naye kwamba alikwenda kwa mganga akazika kondoo watatu ili mwanangu aharibikiwe.

“Simpendi na sitaki hata kumwona. Hana nia nzuri na mwanangu, najua. Kwanza mama Diamond (Sanura Kasim) hampendi Wema, anampenda Penny, nampongeza sana kwa uamuzi huo,” alisema mwanamke huyo.

“Kama angekuwa mwanaume kweli ana pesa zake angekubali vipi kulala kwenye kitanda alichonunua mwanaume mwenzake (Clement)?

Source: Edwin Tanzania 255

BOND"NILIMPA JACK CLIFF MIL 2 AIGIZE KWENYE MOVIE YANGU AKANISONYA NA KUSEMA HANA SHIDA"

$
0
0
MTANGAZAJI wa kituo cha chanel ten Bond Bin Slim ambaeye inadaiwa hivi sasa ni yuko katika mahusiano na mjane wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo marehemu Said Juma Kilowoko “Sajuki”, Wastara Juma amesema siku chache kabla ya mnyange Jack Cliff hajaelekea China ambako alidakwa na dawa za kulevya, alimtolea maneno machafu na dharau na kukataa kupokea kitita cha milioni 2 za kitanzania kama malipo ya kufanya filamu pamoja na Wastara.

Bond alisema kwamba alimpigia simu Jack na kumueleza Ishu hiyo kwani alikuwa miongoni mwa wasanii walioonekana kufaa kucheza filamu lakini mwanadada huyo alimsonya kwa dharau na kumtakia manno machafu na mazito huku akisema hana shida na visenti kama milioni mbili.
“Siongei kwasababu Jack amekamatwa huo ndiyo ukweli.alikataa katakata kupokea pesa hizo na kudai kwamba ni vijihela kwake ambavyo haviangaikii kwa kucheza filamu. Alisema eti mi nimeona hela milioni mbili??” Alifunguka Bond

“Milioni mbili ni pesa nyingi sana kumlipa msanii wa kike hapa Tanzania ili acheze filamu tena vipande vichache. Wasanii wanalilia nafasi hiyo. Nilisikitika sana kwa mtu kama Jack ambaye hana jina kubwa kwenye filamu kukataa tena kwa maneno ya dharau.
“Kukamatwa kwake huko kumenipa picha fulani. Dada zetu wengi wana matatizo sana unapowahitaji kwenye filamu kwasababu wanadai wana pesa nyingi. Hivi kupokea milioni mbili yangu na kubebeshwa mzigo kisha kukamatwa kipi bora??. Alimaliza kwa kusema hayo Bond

NIMEKUFA NIMEOZA KWA BABA MWENYE NYUMBA WANGU..NIMEJIPITISHA NA KUJIBALAGUZA LAKINI WAPI..

$
0
0
Ndugu  zangu, naombeni  nisieleke  vibaya.. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26. Nina mwaka wa kwanza tangu nianze kujitegemea mara baada ya kumaliza shule. Nimepanga kwenye nyumba moja iliyoko  maeneo ya  Mbezi.
Tatizo langu ni kwamba nimetokea kumpenda  sana  baba mwenye nyumba wangu ambaye ana watoto na familia. Kila nikijibaraguza siwezi. 
Nimefanya  kila  mbinu  kuzificha  hisia  zangu  lakini  nimeshindwa.Kimsingi simpendi mwanamume mwingine zaidi yake.

Nisaidie kuniepusha na mtihani huu  mgumu.Asanteni
Anna

HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui. 
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.

Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.


SAMAHANI KWA PICHA HIZI AJALI MKOANI LINDI BASI LAGONGANA NA ROLI KUMI WAFARIKI 28 MAHUTUTI

$
0
0



Jana majira ya saa nane alasiri Basi lenye lenye jiona maarufu kama ALLHAMDULILAH lilipata ajali mbaya huko makoani Lindi watu kumi walipoteza maisha papohapo na 28 mahututi wapo Hosptali ya mkoa wa lindi  sokoine,

Chanzo cha habari kiliieleza paparazi kwamba chanzo cha ajali hio ni baada ya Basi hilo kugongana na Roli la mizigo wakati basi hilo likitokea Dar kuelekea mtwara, 

Likapoteza muelekeo na kupinduka mita kadhaa kutoka barabarani istoshe kulikuwa na utelezi mkali kutokana na mvua kubwa iliyonjesha mda mchache kabla ya ajali.


NINA MIAKA MINNE KWENYE NDOA ILA MUME WANGU HAJAWAHI KUNIFIKISHA KILELENI..NIFANYAJE?

$
0
0
Mimi ni msichana wa miaka 27 nimeolewa miaka minne iliyopita na nina watoto wawili wote wa kike. Mwanzoni mwa mahusiano yetu na mume wangu (wakati tukiwa wachumba) na hata kama mwaka mmoja na nusu hivi kwenye ndoa yetu, baba watoto alikuwa ananiweza kweli….yaani nikikutana nae…aaah, allahmdullillah, nilikuwa naiona anga kwa uhalisia kabisa….na akiwa amechoka sana, basi hata mbili nitapata na kweli nilikuwa najisikia nime…..! Na kwa wiki nilikuwa napata kama siku nne hivi, yale mapigo ya sawa sawa.

Sasa kwa kipindi kama cha mwaka mmoja hivi…da, baba watoto kwa kweli ana underperform kabisa….wakati mwingine inapita wiki nzima, sionji na mimi mwanamke huwa nahitaji…nikimwambia anasema nimechoka sana kazini. Kwa heshima niliyo nayo kwa mume wangu, huwa namwambia sawa, lakini moyoni huwa nabaki na maswali mengi kuliko majibu. Huwa nahisi moja kati ya mambno haya:

1) Huenda mume wangu ameanza mambo ya nyumba ndogo, so akitoka kazini huenda anamalizia huko huko then akirudi nyumbani anakuwa hoi

2) Labda umbile langu limemchosha, coz kabla hatujaoana nilikuwa na bambataa ya wastani na kiuno chembamba, lakini now sio utani, nyonga imebaki vile vile lakini makalio yameongezeka mara-dufu, so huwa hafikii pale “Dar es Salaam“ kisawasawa kama tunado ile style ya chuma mboga.

Haya yoye ni mawazo yangu ambayo ninayo moyoni. Sasa sijajua kama nimuulize au na mimi nianze kupiga show za nje kwani wanaonitongoza nikiwapanga kuanzia Dar, basi watafika hadi morogoro……tatizo nampenda baba watoto na nimempa muda wa kama miezi 6 hivi, kama hatobadilika, basi nita-confirm namba (1) ya hapo juu….so na mimi nitaanzia  kutafuta wa kurusha nae roho.

Naomba mnisadies what to do at the moment!

KAGAME ANUSURIKA KIFO

$
0
0
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amenusurika kifo baada ya msafara wake nchini Kenya kupata ajali na kusababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), imeelezwa kuwa ajali hiyo ilihusisha mojawapo ya magari ya msafara wake nchini Kenya, alipokuwa kwenye ziara za kikazi.

Hata hivyo, Rais Kagame hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi jana eneo la Limuru nchini Kenya. Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru, hata hivyo gari hilo lilikuwa mbali na msafara wa rais huyo. Aidha majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa haraka hospitalini.


Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la Magavana wa Kenya mjini Naivasha katika Bonde la Ufa.

Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya, kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.

PICHA YA MSANII DAVIDO AKIWA NA MDADA ACTRESS WA KIBONGO KITANDANI YAVUJA MTANDAONI

$
0
0
Msanii maarufu wa muziki wakizazi kipya ajulikane kwajina la davido tika nchini Nigeria anaetamba na kibao chake cha SKELEWU,hivi ndivyo alivyo pigwa picha na mwana dada huyu anaedaiwa kuwa mwigizajiwa bongo wakiwa katika pozi la mahaba alivyokuja Bongo.

AIBU:DIVA NAYE AJIBU BAADA YA KUTUKANWA MATUSI YA NGUONI NA TEAMCHAGGABARBIE

$
0
0
Drama zinazidi kuendelea, leo imeibuka akaunt ya instagram inayojiita teamchaggabarbie na imemtolea maneno machafu na ya nguoni mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm Loveness Malinzi almaarufu ka a Diva. Hebu soma hayo maneno hapo chini Na alichokijibu yeye
Haya Ndio Majibu ya Diva Lovess


SNURA TUHUMA NZITO...ADAIWA KULIKIMBIA DENI LA PRODUCER WAKE ALIYE MTOA

$
0
0
Stori:  Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata 
STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi ameingia kwenye majanga baada ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza Mohammed Kandoro wa Studio za Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo kadhaa wakati akisaka kutoka.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Snura ameingia mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za prodyuza huyo na kwamba sasa amehamia studio nyingine.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Kandoro na kumwuliza kuhusu ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na kusema: “Ni kweli namdai laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu lakini sasa naona ameamua kuondoka na deni langu.”

Snura alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu madai hayo, alifunguka: “Kama kuna deni basi meneja wangu HK (Hyper Man) ndiye anayehusika, maana kila kitu nilimkabidhi yeye na naamini alilipa, sasa kama hakulipa hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si mimi tena.”

Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti hili liliwasiliana na meneja wa Snura, HK ambaye alisema hana deni lolote analodaiwa na Kandoro, ingawa alikiri kumhamisha Snura studio.

“Kilichopo ni kwamba tumehama kwenye hiyo studio, sina ugomvi nao wala Snura hajawahi kutofautiana naye. Tumefanya hivi kwa lengo la kutafuta ladha tofauti... hayo mambo ya madeni, si kweli.

Hivi kama leo hii tunaweza kulipa zaidi ya shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) tunashindwaje kulipa laki nne tu? Hayo ni maajabu,” alisema HK.

Source:GPL

MAJANGA YAZIDI KUMKUMBA BABY MADAHA AKIRI NAKUSEMA "NIMEUMBUKA"

$
0
0
Jambo limezua jambo! Ile skandali ya kunaswa baada ya kuingia mkenge kwenye mtego wa kujiuza imemtokea puani staa wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ambaye amekiri kuumbuka.

Habari hiyo iliruka hewani kwenye gazeti dada la hili, Ijumaa wiki iliyopita toleo namba 862 la Januari 17 hadi 23 likiwa na kichwa cha habari ‘BABY MADAHA ANASA MTEGO WA KUJIUZA.

SAFARINI 
Ilielezwa kuwa wakati skendo hiyo ikiingia mitaani, mwanadada huyo alikuwa safarini kuelekea Nairobi, Kenya ambako ndiko yaliko Makao Makuu ya Kampuni ya Candy n Candy iliyompa mkataba mnono wa takribani Sh. milioni 200 ili wasambaze na kuuza kazi za Baby Madaha.

MAPOKEZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini nchini humo, imezoeleka kuwa kila Baby Madaha anapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi kwa ajili ya kazi za kampuni hupokelewa na timu maalum kisha kuchukuliwa na lile gari la bei mbaya aina ya Audi TT.

Ilielezwa kuwa baada ya habari ya kunaswa kwake kusambaa, alipotua uwanjani hapo hakukuwa na mtu aliyekwenda kumpokea kwa kile kilichoelezwa kuwa viongozi wa kampuni hiyo walichukizwa na jambo hilo.

“Unajua tatizo ni simu ambazo viongozi wa Candy n Candy wanapigiwa na vyombo vya habari kutaka kujua undani wa skendo hiyo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

MITANDAO
“Pia mitandao nayo imechangia kuwashtua viongozi hao maana kila ‘blogi’ imekopi kutoka kwenye mtandao baba lao wa www.globalpublishers.info na kupesti kwao.”

NYUMBANI
Baada ya kugundua kuwa alitelekezwa uwanjani, Baby Madaha alifanya mpango wa kwenda kwenye nyumba ya kampuni hiyo ambayo huwa anaishi lakini huko nako alikutana na ‘mbwa mkali’. Aliambiwa uongozi umekataza yeye kutia maguu ndani ya nyumba hiyo.

Kiliendelea kutiririka kuwa wakati huo, tayari Mkurugenzi wa Candy n Candy, Joe Kairuki alishawasiliana na Baby Madaha ambaye alimwambia kuwa skendo hiyo haikuwa ya kweli bali ‘promo’ ya filamu yake mpya ya The Gal Bladder.

OFISINI
“Hata angejitetea vipi, wale jamaa walikuwa hawamwelewi kwani alikwenda hadi ofisini kwao lakini hawakutaka kumsikiliza hadi hapo baadaye.
“Wanacholalamikia ni kwamba Baby Madaha amechafua sura ya kampuni na wanaonekana wanafanya kazi na msanii anayejihusisha na ufuska,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

GARI
“Hata hilo gari la Audi TT atakuwa analisikia kwenye bomba. Alizoea kukatiza nalo mitaa hapa Nairobi lakini sasa matatuu (daladala) zinamhusu.”

MSIKIE
Baada ya kujazwa data hizo, gazeti hili lilimtafuta Baby Madaha ambaye mwanzoni alikataa kutoa ushirikiano kwa kigezo kwamba ameharibiwa maisha.
Risasi: Baby lakini ni vizuri ukawa muwazi kuliko kuwa mkali. Je, ni kweli Candy n Candy wamevunja mkataba na wewe?
Baby: (kilio) Nasema niacheni kwanza mimi siyo msemaji wa Candy n Candy, mtafuteni mkurugenzi.
Alipomaliza kusema kwa hasira, Baby alikata simu. 

MKURUGENZI
Hata hivyo, alipotafutwa mkurugenzi huyo, Joe alikuwa na haya ya kusema:
“Yaa tumeingia kwenye matatizo kwa sababu ya hiyo habari.”
Risasi: Matatizo gani?

Joe: Tumepigiwa sana simu na vyombo vya habari kuthibitisha hiyo skendo. Tunaonekana tunafanya kazi na mtu ambaye siyo. Anatuharibia image (sura) ya kampuni.
Risasi: Kwa yeye (Baby Madaha) amewaambiaje?
Joe: Anasema ni mambo yake ya filamu, kimsingi hatujamuelewa ndiyo maana hatujampa muda wa kumsikiliza kiundani.


Risasi: Kwa hiyo mtavunja mkataba wake na ninyi?
Joe: Ndiyo lengo letu lakini siyo jambo la haraka kwani kuna masuala ya kisheria.
Risasi: Vipi kuhusu gari na nyumba mlivyomkabidhi?

Joe: Kwa sasa kila kitu kipo chini ya kampuni.
Risasi: Nini hatima yake (Baby Madaha) sasa?
Joe: Yeye ndiye mumuulize nini hatima yake.

BABY MADAHA TENA
Baada ya mazungumzo hayo, gazeti hili lilimrudia Baby Madaha ambapo safari hii alikuwa mpole: “(kilio cha kwikwi) jamani nimeumbuka. Yaani huku wameichukulia kuwa ishu kubwa sana.”
Risasi: Sasa nini hatima yako?
Baby Madaha: Mi nipo Nairobi najaribu kuweka mambo sawa. Namwamini Mungu, najua atanijalia haja ya moyo wangu.

AMEFIKAJE HAPA?
Baby Madaha aliingia mkataba na kampuni hiyo mwaka jana ambapo mpaka sasa amesharekodi nyimbo mbili za Squeeze na Summer Holiday huku akirekodi filamu moja ya The Gal Bladder iliyozinduliwa hivi karibuni, jijini Dar.
GPL

BREAKING NEWS! USAJILI WA OKWI YANGA WAADUNDA

$
0
0
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata hivi punde jina la Emmanuel Okwi halijaidhinishwa kwenye usajili wa klabu ya Yanga.Kwa maana hiyo Okwi hataruhusiwa kucheza raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom mpaka sakata lake la usajili kutoka klabu ya Etoile du Sahel litakapotafutiwa ufumbuzi. Endelea kufuatilia mtandao huu kwa taarifa zaidi

MWANAMUZIKI LINAH SANGA APANGUA SKENDO INAYOMKABILI YA KUTOKA NA KIGOGO

$
0
0
Mwanamuziki Linah Sanga Amekana katu katu Skendo kuwa anatoka na kigogo mmoja wa serekali na kuwa amempachika ujauzito ..

Linah Amesema yeye sio mjamzito na wala hatoki na Kigogo yoyote, hizo ni shutuma tu za uongo mimi nina mchumba wangu kabisa na anatambulika kwetu  yote mnayoyasikia ni mambo ya kuzusha tu mitaani....Mnikomeee

JUMA NKAMIA AWAANGUKIA WADAU WA HABARI...AOMBA USHIRIKIANO KAULI ZAKE ZAMPONZA

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (pichani), amewaomba wadau wa habari kushirikiana naye katika kujenga na kuiboresha tasnia ya habari.  Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa ofisi rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.  “Kwa sasa nimekabidhiwa ofisi ili nipiganie haki na maslahi ya wanahabari na siyo kama watu wanavyofikiria kwamba nimekuja kudidimiza sekta ya habari,” alisema Nkamia. 

Aliongeza: “Mimi nimekuwa mwandishi wa muda mrefu na mwanamichezo. Najua changamoto zilizopo katika tasnia ya habari. Kwa hiyo, ndugu zangu waandishi tushirikiane pamoja ili tuweze kutatua matatizo yanayoikabili tasnia hii ya habari kwa jumla.”
Nkamia amekuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiwabeza wanahabari katika vikao vya Bunge mjini Dodoma. 

Miongoni mwa kauli alizowahi kuzitoa zilizoonekana kuwa ni za kukebehi tasnia ya habari, ni ile aliyohoji kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF) ni NGO’s (mashirika yasiyokuwa ya kiserikali) au taasisi ya serikali kiasi cha kutoa tamko na nyingine kuwaita waandishi wengi Watanzania kuwa ni makanjanja.  

CHANZO: NIPASHE
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images