Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live

Kama Msichana Ushavuka Miaka 30 Bado Hujaolewa Jua Una Hali Mbaya

$
0
0
Kama wewe ni msichana na umeshavuka miaka 30 bado hujaolewa na wala huna mtu wa kueleweka ambaye amejitambulisha kwenu tambua kwamba una hali mbaya.

Wasichana wengi siku hizi wamekua na tabia ya kupenda vitu vya anasa hali inayopelekea sisi wanaume kuwaogopa kama ukoma.Mfano kutaka kufanyiwa shopping za bei mbaya,kumiliki simu za gharama zinazoanzia milioni moja na kuendelea,kupenda kuwa na mwanaume mwenye mshahara unaoanzia milioni tatu kwa mwezi na kuendelea n.k

Hali hii inasababisha hata sisi wenye kipata cha laki saba kushuka chini tuwaogope kwa kuamimini kwamba hatuna uwezo wa kukidhi mahitaji yenu hatimaye mnajikuta mnazeekea nyumbani kutaamakitaamaki miaka 45 hii hapa ambapo ndo kipindi cha menopause kwa mwanamke yeyote.

Msipende mteremko sababu hata huyo mwenye magari,majumba na kipato kikubwa hujui ametumia njia gani mpaka kupata hivyo vitu.Starehe hazina mwisho hivyo unapobweteka na starehe fahamu kwamba fainali uzeeni muda ndio refa.

Aliesikia na asikie na alieamua kupuuzia na apuuzie

Dillish: Hela Nilizoshinda Big Brother Afrika Zimekwisha Zote

$
0
0
Dillish Mathews, mshindi wa shindano la Big Brother Africa mwaka juzi, amedai kuwa amemaliza fedha zote alizoshinda.

Mrembo huyo wa Namibia aliyejishindia zaidi ya shilingi milioni 500 amepost video kwenye mtandao wa Instagram na kuongea maneno ambayo wengi wamechukulia kama utani kuwa hana tena fedha hizo.

“About what I did with my money that I got from Big Brother? It’s finished. A couple of Rolexes, kept going to Milan, London, Hong Kong, Shanghai…it’s finished. Kapu,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

Kwenye video hiyo aliandika: Read on social media im broke… So here it is just in case your life depended on it. I don chop finish”

Hata hivyo wengi wamekerwa na kauli yake.

Chris Brown Kuwahamishia Mwanae na Mama Yake Nyumbani Kwake, Anataka Kumuona Mwanae Kila Siku

$
0
0
Chris Brown amepanga kumchukua mwanae pamoja na mama yake na kuishi nao nyumbani kwake, mtandao wa Hollywood Life umesema.

Chris Brown, 25, anataka mwanae wa kike mwenye umri wa miezi tisa, Royalty na mama yake, Nia Amey, 31 kuhama kutoka Houston wanakoishi sasa, ili waishi naye nyumbani kwake jijini Los Angeles.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoongea na mtandao huo, Chris anataka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 26 akiwa na Royalty.

Chris anataka kuhakikisha kuwa anamuona mwanae kila siku.

Penny: Huu Usista Duu Utatumaliza Wasichana Bongo

$
0
0
ALIYEKUWA mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya wasichana mastaa kujiona masista duu itawamaliza kwa sababu watajikuta uzee unawakabili bila kuwa na ndoa.

Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mastaa wengi wanapenda kujiona ni matawi ya juu na kufikia hatua ya kudharau watu wengine kiasi kwamba hata wenye mapenzi ya dhati kwao hujikuta wakijiweka pembeni hivyo kuwafanya ‘kuchina’ wakati wakitafuta ndoa.

“Unajua kuna vitabia fulani hivi mastaa tunavyo, ya kisista duu ambayo inatufanya tuchine, maana wengi si wanatuogopa wakidhani sisi ni matawi ya juu wakati ni wa kawaida sana,” alisema Penny.

Lulu Afuata Nyayo za Wema, Ahamasisha Matumizi Bora ya Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwenye followers zaidi ya laki nne kwenye mtandao wa Instagram amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kujengana zaidi ikiwa ni siku chake baada ya staa mwenzake, Wema Sepetu kuwataka wanawake na jamii kwa ujumla kutumia mitando hiyo kuhamasishana kwenye vitu vya kimaendeleo zaidi.

“Nikiwa kama kijana mpenda maendeleo,mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu pekeyangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka....najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!
Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo ili wote tuweze kuwa sehemu flani siku moja.....” Lulu amendika

Nadhani Ujumbe umeeleweka.

Rose Ndauka na Producer Maneck Ndani ya Penzi zito, Wafuatana Kama Kumbi Kumbi

$
0
0
IMEVUJA! Baada ya uhusiano wake na Mbongo Fleva, Malick Bandawe kuvunjika, staa wa sinema Bongo, Rose Ndauka kwa sasa anadaiwa kuzama kwenye penzi zito la Prodyuza wa Bongo Fleva, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.

Kwa mujibu wa chanzo, kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa wakionekana sambamba kama kumbikumbi hasa nyakati za usiku katika maeneo tofauti ikiwemo studio ambayo Manecky anafanyia kazi zake na sehemu nyingine. “Rose na Manecky ni wapenzi kwani muda mwingi wako pamoja, wanaongozana kama kumbikumbi hasa usiku. Huwa tunawaona wanakuja maeneo ya hapa Afrika Sana wanakwenda kununua chakula cha jioni huku Manecky akijinadi kuwa ameamua kuwa na Rose kwa kuwa mke wake halali hivi sasa ni mjamzito,” kilisema chanzo hicho.


Mara baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao ili kuweza kujibu tuhuma hizo ambapo Manecky alipopatikana alikanusha na kudai ukaribu wao unaletwa na kazi. “Ukaribu wangu mimi na Rose ni kazi tu kwani kuna ‘project’ tunaifanya nadhani mwenyewe Rose ndiyo anaweza kuweka wazi hilo, kingine Rose anafanya kazi na mdogo wangu kwenye gazeti la Rozzie la mtandaoni,” alisema Manecky.

Alipoulizwa kama ameamua kutembea na Rose kwa sababu mkewe ni mjamzito, Manecky alizidi kusisitiza kuwa si kweli. “Hamna kitu kama hicho jamani.” Ili kupata upande wa pili, mwanahabari wetu alimvutia waya Rose ili kujua anazungumziaje tuhuma hizo likiwemo suala la kuonekana na Manecky mara kwa mara, naye aliruka viunzi:

“Hakuna kitu kama hicho jamani, kwani mimi nachaguliwa mtu wa kukaa naye? Acheni kusikiliza maneneo ya watu halafu Manecky ana mke ambaye ni mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote,” alisema Rose. Rose na Malick kabla ya kumwagana miezi michache iliyopita, walidumu kwenye uhusiano kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.

Mbasha: "Gwajima Mungu Amenilipa, Njoo Uniombe Msamaha Tumalize Ugomvi"

$
0
0
Licha ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya.


Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa hospitali ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu kwa dakika 15 juzi, Mbasha alisema: “Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine.

“Mimi ndoa yangu haipo,  mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?”

Mbasha alikwenda mbele zaidi kwa kutoa tamko na agizo kwa mchungaji huyo kwa kusema:

“Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha.

“Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye asiwe na kinyongo na mimi.”

Mbasha hakumalizia hapo, alipoulizwa kama kauli ya Gwajima iliyosababisha mtafaruku ilikuwa sawasawa au la! Mbasha alisema:

“Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe msamaha.”

Naye mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alipopatikana kwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya Mbasha, alisema: 
  
“Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.

“Gwajima na Flora hawana uhusiano wowote usiofaa. Sasa yeye anaposema kalipiwa, kalipiwa kitu gani? Mungu anaweza kulipa jambo la hisia?”

Wiki mbili zilizopita, kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkers ambako kuna kanisa,  Gwajima alitoa mahubiri yaliyolenga kumshutumu Kadinali Pengo kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Maaskofu Tanzania kuhusu msimamo wao wa Mahakama ya Kadhi nchini.

Hali hiyo ilimfanya Gwajima kuitwa Polisi Kituo cha Kati, Dar na kuhojiwa. Akiwa katika mahojiano, ghafla alisikia kizunguzungu, akaanguka na kupoteza fahamu. alikimbizwa katika Hospitali ya Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.

Juzi, Gwajima aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo lakini akachukuliwa hadi Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi na kuachiwa kwa dhamana.

Credit:  Amani/Gpl

Ukawa wavuruga Bunge Dodoma, Wadai Hawataki Kuburuzwa Buruzwa na Kupelekeshwa

$
0
0

Wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana walianzisha tafrani bungeni na kusababisha kikao cha Bunge kuvunjika saa 5.18 asubuhi baada ya kusimama na kupaza sauti wakishinikiza Serikali itoe kauli juu ya hatima ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura na upigaji wa Kura ya Maoni kupitisha Katiba Inayopendekezwa.

Huku wakiwa wamesimama walikuwa wanapiga kelele wakisema, ‘hatutaki kuburuzwa’, ‘tumechoka kupelekeshwa’, Watanzania wapo njia panda’ na ‘tunataka majibu,’ ‘Bunge lisitumiwe kuilinda Serikali’, ‘Waziri Mkuu yupo bungeni kwa nini asitoe kauli’ na maneno mengine mengi bila mpangilio.

Wabunge hao wa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF, kwa umoja wao walimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa majibu hayo muda huohuo, kabla ya jioni kutoa hutuba na kuahirisha mkutano huo wa 19 wa Bunge.

Baadaye jana usiku katika hotuba yake ya kuahirisha Bunge hadi Mei 12, utakapoanza Mkutano wa 20, Waziri Mkuu Pinda alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itatoa taarifa siku za hivi karibuni kuhusu upigaji wa kura ya maoni.

“Ni dhahiri muda uliobaki kuanzia sasa ni mfupi lakini Tume ndiyo itakayotujulisha ratiba kamili,” alisema.

Kenya Kimenuka Tena, Al Shabaab Wavamia Garissa University na Kuteka Wanafunzi Kadhaa

$
0
0
Masked gunmen attack Garissa University College, heavy gunfire reported in the institution as police and military engage attackers; scores injured.

Gunmen Thursday stormed Moi University campus in Garissa Town causing a major siege and casualties. Gunshots and explosions were heard from the compound for hours as police and military were mobilised to the institution.

It is not clear who is behind the incident but witnesses say there is heavy presence of police and military in the area. Witnesses say the gunmen went into the university as students went for morning prayers. Those calling from inside the university say there are many casualties.

Area residents say Kenya Defence Forces have surrounded the compound. The attack started from the Mosque inside the university where the attackers shot at worshippers indiscriminately. Students who escaped the attack said there were at least five gunmen. Many other students and teachers were by 8 am still being held hostage.

They said the attackers had posed as worshipers at a mosque in the college. Witnesses said ambulances were carrying casualties to Nairobi. Local security bosses say there had been threats on the institutions inthe area from terror a group

Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 imeanza safari kwenda Kigoma

$
0
0
Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.

Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku. 

Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.

Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.

Mch. Gwajima Amgomea Makonda, Asema Hatopoteza Muda Wake Kwenda Kumuona Mkuu Huyo wa Wilaya

$
0
0

Mchungaji wa makanisa ya kipentekoste mch. Josephat Gwajima amesema hatapoteza muda wake kwenda kumuona Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Amesema barua aliyoipata toka kwa Mkuu wa Wilaya imemfedhehesha na kasema hataijibu itajibiwa na maombi ya mnyororo yanayoendelea.

Chanzo: Kutoka magazetini.

Tundu Lissu: Filamu za Ponografia ama X Siyo Kosa Kwa Watu Wazima

$
0
0
Tundu Lissu amesema leo bungeni dodoma kuwa,Filamu za Ponografia siyo kosa la jinai dunia nzima isipokuwa ni mambo ya wakubwa,Na akaomba kifungu hicho kifutwe.

Kumbukeni lissu amesisitiza kwa watoto ndio kosa si kwa watu wazima.

Next time watakuja na muswada ku-control kila kinachofanyika bedrooms.

Nakupe 5 Lissu

CRDB Kujenga Ukuta wa Fensi ya Nyumba ya Daimond Platnumz Ulioanguka

$
0
0
Benki ya CRDB imepanga kumjengea ukuta wa fensi wa nyumba ya Daimond Platnumz ulioangushwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. CRDB wamesema hayo kuwa watamjengea ukuta huo kwa kuwa Dai aliikatia Bima nyumba hiyo.

Gharama itakayotumika kujenga ukuta huo ni milion 15.

Chanzo: E-Fm Radio

Viwanda vya Mikorogo Vikizimwa ulimwenguni tutawasahau wengi

$
0
0
Kufuatana na hali halis ya watu kujibadili sura mpaka kukalibia jini, siku ametokea muungwana mmoja Africa akasema viwanda vya vipodozi na mikorogo vizimwe na kutotumika tena. Ipo siku tutawasahau wengi, wengine tutawapa shikamoo bibi, wengine kuwakimbia kwa mabaka ya rangi nyingi tofauti.

Nawasilisha. Bajameni Mkorogo ni Hatari kwa afya yako, Ukatae usiruhusu kansa.

Davido Apost Picha Akiwa na Diamond Studio na Kuandika Ujumbe Uliotuacha njia Panda!

$
0
0
Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother Africa.


Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi

Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram.

Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”
~Bongo5


Breaking News: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Kura ya Maoni

$
0
0
Katika kikao cha waandishi walichoitisha leo mchana, Tume ya taifa ya uchaguzi wameahirisha kura ya maoni iliyokuwa ipigwe April 30 hadi watapotangaza vinginevyo kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR.

Magaidi Wavamia Chuo Kikuu Cha Garrisa Kenya......Waliofariki mpaka sasa ni 15

$
0
0
Takriban watu 15 wameuawa baada ya watu watano wanaodaiwa kufinika nyuso zao kushambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.

Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.

Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.

Taarifa  zaidi  zinaarifu  kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.

Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.Wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.

Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.

Wanafunzi 27 wamefanikiwa kutoroka na sasa wako katika kituo kimoja cha kijeshi.

Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulizi hilo ijapokuwa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab limeshukiwa kutekeleza shambulizi hilo.

Chuo hicho ndio taasisi ya kipekee ya masomo ya juu katika eneo hilo kilichofunguliwa mwaka 2011 na kiko takriban kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Nairobi.

WHO and HOW Garissa University Al-Shabaab Terror attack was PLANNED and EXECUTED

$
0
0

Al-Shabaab accessed Garissa University at 3.am and conducted a religious profiling exercise for nearly an hour before calling in the main attackers into the compound. The attackers had posed as worshipers at a mosque in the college

It is after separating Muslim students from Christians they began the killings.

Kenya Intelligence Service report that Senior Al Shabaab leader in Lower Juba, Abdurahman Mohamed alias Gamadere alias Dulyadeen planned and ordered the Garissa terror attack.

Kuno was aided by 2 local youths to conduct surveillance on the University.

The objective of religious profiling and killings is to inspire religious hatred.

They want the Christians to feel threatened and persecuted. Such feelings can elicit emotions that can prompt reprisals.

Religious reprisals can have serious ramifications including acts of violence besides increase Islamic radicalization and ethnic terrorism.

These strategies by the terrorists cannot work in Kenya. The country is relatively stable. There is religious tolerance in Kenya, and terrorists cannot manage to breach that, analysts point out.

Source:Kenyan Daily Post

KENYA:AL SHABAAB Claims Responsibility for Garisa Attack & Reveal what They Did to Students!

$
0
0
Somalia based terror group, Al Shabaab has claimed responsibility for the terror attack on Garisa University today.


The Al Shabaab attacked the university at 5.30 am on Thursday and started shooting indiscriminately killing at least 15 people as of 12 noon and wounding at least 65.


They also held hostage over 400 students and their fate still remains unclear.


However, speaking to BBC, the Al Shabaab indicated that they have killed many people, especially students, than it is being reported.


They told the BBC that they separated Muslims from non-Muslims and killed the kaffirs in large numbers and that Kenyans will be shocked when they go inside the university because bodies are scattered everywhere.


Here is what Al Shabaab told the BBC;-


Al-Shabaab to BBC: “We have killed many people. Kenyans will be shocked when they go inside.”


Al-Shabaab to BBC: “We separated Muslims from non-Muslims and released 15 Muslims and killed the rest.”



The Kenyan DAILY POST

Unaijua Mikoa 7 inayoongoza kwa Maisha Duni Tanzania?

$
0
0
Ripoti yataja mikoa 7 yenye maendeleo duni ya watu Tanzania.

DODOMA, KIGOMA, SINGIDA, KAGERA, TABORA, SHINYANGA na PWANI ndio mikoa inayoongoza kwa maisha duni ya watu Tanzania

Hayo yamo katika ripoti iliyozinduliwa Ijumaa na serikali, ripoti hiyo pia imeitaja mikoa inayoongoza kwa hali bora za maisha ya watu Tanzania kuwa ni:
 DAR ES SALAAM, ARUSHA, KILIMANJARO, IRINGA, RUVUMA, MBEYA and TANGA.

Vigezo vilivyotumika katika utafiti uliozaa ripoti hiyo ni, wastani wa muda wa kuishi (Life expectancy, max 83.6 - min 20), expected years of schooling, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme, lishe, vifo vya mama wajawazito na watoto, maendeleo ya jinsia.

Vigezo vingine ni, mazingira, kipato, umaskini, uhuru na upatikanaji wa mahitaji ya msingi kama chakula, maji na nyumba.

Utafiti huo ulifanywa na Economic & Social Research Foundation (ESRF) kwa kushirikiana na;
- National Bureau of Statistics (NBS).
- The Office of the Chief Government Statistician of Zanzibar.
- The Department of Economics of the University of Dar es Salaam.
Na kudhaminiwa na UN.

Source; The Citizen
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live




Latest Images