Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa

$
0
0
Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
 
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
 
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. 
 
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano  na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
 
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.

Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao. 
Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho

Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa

Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao

Athari 12 Za Sheria Mpya Ya Masuala ya Mitandao ( Tanzania Cybercrimes Act, 2015 ) Iliyopitishwa Jana Bungeni......Athari Hizi Zimechambuliwa Na Mbunge David Kafulila

$
0
0
Sheria hii ni muhimu duniani kote na ndio maana hata Tanzania ilikuwa inangojea kupata sheria ya kuongoza masuala ya mitandao yaani Cyber Law kutokana na uhalifu wa aina mbalimbali wa masuala ya mitandao.

Sifa kuu ya sheria ya kuongoza masuala ya mitandao ni kuweka bayana makosa ya mitandaoni na pia kuyatolea adhabu. Sheria hii inayopitishwa kwa dharura madhara yake ni:

Moja, Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

Pili, Kifungu 21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale zitakapohitajika (kwa lazima).

Tatu, Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).

Nne, Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

Tano, Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

Sita, Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa Kiingereza “not less than”

Saba, Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

Nane, Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

Tisa, Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

Kumi, Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

Kumi na moja, Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states. Askari Polisi wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua muda gani?

Kumi na mbili, Kifungu 31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au mtoa huduma ya mtandao, pale unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka husika (Kama sheria inavyosema), askari naye anaweza kwa wakati huohuo akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako, hivyo sheria inakinzana yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa kisheria.

Je, sheria hii ikisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tutapona?

DAVID Kafulila
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi)

I Made Davido Popular—Tanzanian Music Star, Diamond Boasts

$
0
0
Tanzanian artiste, Naseeb Abdul, aka Diamond Platnumz, is a household name in his home country. He holds eight Kilimanjaro awards. Veteran Tanzanian musician, Maalim Gurumo, once described as the best ‘Bongo Flavour’ artiste of the decade.
The singer recently did a duet with Nigerian music star, David ‘Davido’ Adeleke in the remix of his single ‘Number One’ and he disclosed his happiness for achieving such feat. 
Speaking about the collabo, Diamond revealed that the duet with Davido has now made the Nigerian star popular in Tanzania.

I met Davido when he came over to Tanzania for a show and when we were together, he heard my song. I told him I would love to feature him on the remix of my song, ‘Number One’, and he agreed. Currently the song is topping charts in various African countries.”
“Shortly after, he released Aye and that made him very popular in my country as well. They love the song in my country. I featured Davido on the track because I wanted to launch myself into the West African market and he was the best person for the job. I used Davido to break into the West African market,” 
The Tanzanian singer said further. Diamond was born on October 2, 1988.

Lulu: Ifike muda tutumie mitandao ya kijamii kusaidiana mawazo na sio kutukanana

$
0
0
Moja ya mambo sita tuliyoandika kuwa ni sababu ya watanzania kuupenda mtandao wa Instagram, ni kushuhudia matusi ambayo mastaa wanayavuna kutoka kwa followers wao.

Lakini unadhani Instagram inapaswa kuwa sehemu ya kihuni kiasi hicho? Hapana.

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka kwa vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika kufikia ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu nzuri ya vijana kupenda michongo na sio matusi.

Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.

Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”

Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.

Afya ya Gwajima Bado Migogoro, Polisi Wasindwa Kumuhoji kwa Mara ya Pili Jana, Sasa Kuhojiwa Alhamisi Ijayo

$
0
0
Mahojiano baina ya Jeshi la Polisi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima yaliyokuwa yanatarajiwa kuendelea jana, ikiwa ni siku mbili baada ya kuachiwa kwa dhamana na jeshi hilo, jana yalikwama kuendelea kutokana na kile kilichoelezwa kutoimarika kwa afya ya askofu huyo, na sasa yatafanyika Alhamisi ijayo.

Gwajima alidaiwa kuzimia wakati akihojiwa na makachero wa Polisi waliokuwa wanamhoji, alipojisalimisha alasiri ya Ijumaa iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo, kutokana na kufunguliwa jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.

Kutokana na hali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu usiku wakati akiendelea na mahojiano yaliyoanzia alasiri, alikimbizwa Hospitali ya TMJ, Mikocheni akiwa chini ya ulinzi wa Polisi hadi aliporuhusiwa kutoka Jumanne wiki hii na baadaye kuachiwa kwa dhamana.

Mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alithibitisha kuahirishwa kwa mahojiano kati ya mteja wake na Polisi, akisema mapema jana asubuhi aliripoti Kikuo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyotakiwa kuripoti kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo, alisema hakuweza kuhojiwa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa afya ya mteja wake haijaimarika vizuri na hivyo wamepangiwa kurudi tena kituoni hapo Aprili 9 mwaka huu, yaani Alhamisi ijayo kwa ajili ya mahojiano.

Mteja wangu alifika kituoni leo (jana) asubuhi kwa ajili ya mahojiano na pia kuripoti kama ilivyoagizwa siku alipopatiwa dhamana, hata hivyo afya yake bado haijaimarika na hivyo imewalazimu polisi wampatie muda zaidi hadi Aprili 9 atakaporudi tena kwa ajili ya mahojiano,” alisema Mallya.

Hata hivyo, Mallya alisema hali ya afya ya Gwajima imeanza kuimarika na kadri siku zinavyozidi kwenda, atakuwa na nguvu na ataendelea na kazi zake kama kawaida.

Mtumishi huyo alipatiwa dhamana katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kati kwa ajili ya mahojiano zaidi na kusubiri uchunguzi wa kesi yake ukamilike.

BREAKING: Garissa Campus SIEGE ends with 152 students KILLED and 81 injured

$
0
0

The campus siege at Garissa University has ended, Interior Cabinet Secretary Joseph Nkaissery announced that 147 people died however independent sources confirmed 152 were killed including the four alleged terrorists.

80 people were wounded in the Thursday attack and those in critical condition airlifted to Nairobi for further treatment. Others are receiving treatment at Garissa Level Five Hospital.

Addressing press after the siege ended, Nkaissery condoled with the families of those who perished in the attack. “I send my personal condolences to the families of those who have died in the attack”, the CS said. He added: “The National Youth Service will send buses to collect students tomorrow and take them to their homes”.

Nkaissery further said the Ministry of Education will communicate on the way forward. The siege lasted for 16 hours as security personnel battled the attackers who held students inside their hostels.

587 were students evacuated in the rescue operation. The institution is a constituent of Moi University and all the students were on session at the time of the attack.

Police have announced a curfew in four counties following the attacks that targeted Christian students.

Inspector General of Police Joseph Boinett announced that Garissa, Tana River, Mandera and Wajir counties will be under dusk to dawn curfew starting Friday to April 16.

He addressed the press in Garissa town flanked by Interior CS Joseph Nkaissey and other local leaders.

Wema Sepetu Ampongoza Diamond Platnumz Kwa Kumaliza Mjengo Ambao Katika Hatua za Mwanzo za Ujenzi Walikuwa Wote

$
0
0
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa hata yeye anampa pongezi mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa jitihada alizozifanya mpaka kufikia hatua ya kumaliza nyumba yake iliyopo Madale jijini Dar.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema kuwa hata kama hawako pamoja lakini kama kuna kitu cha kumsifia kwa jambo zuri alilofanya hana sababu ya kukaa kimya na akinyamaza atakuwa mnafiki.

“Nikikaa kimya bila ya kumpongeza Chibu nitakuwa mnafiki, amefanya jambo zuri la kuigwa hivyo binafsi nampongeza kwa hapo alipofikia,” alisema Wema ambaye katika hatua za mwanzo za ujenzi huo alishiriki.

Fikiria WEMA SEPETU Angefanya Haya Kwa Kutumia Jina lake na Umaarufu Alionao Hapa Bongo

$
0
0
Samahani kwa haya kama yatawauzi wengine hasa mashabiki wa Wema Sepetu .. Najaribu kufikiria kwa sauti tu kama Wema Sepetu kwa kutumia umaarufu wake na jina alilonalo angefanya biashara mbali mbali kama zifuatazo nadhani angekuwa ni mmoja wa wanawake wenye pesa za kufa mtu :
1.Spa and Beauty Parlour za kisasa-Duka la Urembo lenye jina lake ambapo wanawake wanaenda kutengeneza kucha (manicure and pedicure), nywele, massage, waxing, stem bath ama sauna na mengine mengi
2. Hotel ama Restaurant yenye jina lake ambapo siku moja moja yeye na marafiki zake wanakuwa wanahudumia na kutoa huduma special kwa wateja
3. Maduka ya nguo, viatu na handbags za kike ambapo kila mara anakwenda nje kuchukua vitu vipya na kuvitangaza kupitia page yake ya instagram yenye zaidi ya followers laki tano
Kwa ufupi ana potential kubwa kwa upande wa biashara kwa sasa as anapendwa na watu wengi ....
Thats it if only i was in her shoes...Nimemaliza.....

Makanisa Mengi ya 'KIROHO', ni Biashara Isiyo na Hasara

$
0
0
Ni uwekezaji kama ilivyo biashara nyingine yoyote yenye wamiliki kisheria na wanahisa pia
Kinachofanyika ni rahisi sana una karama ya kuhubiri na kukariri vifungu vya Biblia takatifu, muongeaji mzuri unakaa chini na wadau mnatengeneza plan ya gharama za uanzishwaji na uendeshaji! Mnagawana majukumu , washika dau wanatoa mtaji wa kianzio na kanisa linaaza

Sasa kwakuwa lengo kubwa ni kutengeneza pesa/faida basi mahubiri yote msisitizo unakuwa kwenye kutoa. Na mara nyingi watu maarufu wenye nyadhfa na madaraka kwenye kada mbalimbali wakiwemo matajiri na wasanii hutumika kama chambo cha hadaa na kuwavuta wengine 

Ni nadra saana kukuta mtu wa kawaida asiye na kitu amekaa mstari wa mbele, nafasi katika haya makanisa hutegemea wewe ni nani na una bei gani

Miaka ya nyuma wakati ule taasisi za kidini zikiwa na misamaha ya kodi, makanisa haya yalitumika sana kufanya biashara. Zinaingizwa mali bila kodi kisha zinauzwa kwa bei ambayo imelipiwa kodi! Ndio kipindi kile ambapo viongozi na matajiri wengi walikuwa wakionekana kwenye ibada za haya makanisa

Makusanyo ya sadaka kwa kanisa moja tu kwa ibada moja si chini ya milioni tano ukitaja kwa kiwango cha chini kabisa kwahiyo kwa mwezi mmoja tu ana uhakika wa kutengeneza milioni 20 kwa uchache kabisa

Sasa ili kuendelea kupata waumini wengi zaidi na kuwa na mvuto wengi wao huingia mpaka kufanya mambo ya ki shetani ulozi na uganga! Mambo yafanyikayo huko yanatisha lakini kwao si tatizo 

Kwenye haya makanisa hakuna huduma ya bure hata moja na wengine wamechapisha kabisa mchanganuo na gharama kwa kila huduma

Makanisa yetu haya mengine tunaona yanavyoisadia jamii kuanzia afya mpaka elimu na huduma nyinginezo lakini si makanisa haya ya mitume na manabii

Imani ni kitu kizuri sana lakini imani bila fikra ni mzigo na upofu mkuu, watu wanatajirika kwa kupitia vichwa vya wapumbavu ni wakati wa kubadili ka sasa na kuona mambo katika uhalisia wake

Dr Kessy Anakuletea Dawa za Kutengeneza Hips, Makalio, Nywele na Nguvu za Kiume Kwa Kutumia Dawa za Asili zisizo na Kemikali

$
0
0
Pendeza na Dr Kessy Products 
Ni dawa za Asili zisizo na Kemikali wala madhara yoyote kwa Binadamu, zimetengenezwa kwa kutumia mimea na matunda mbali mbali kukupa matokeo ya Haraka

1.Refusha Nywele na zisikatike  45,000/
2.Ondoa Mvi Sugu kichwani  45,000/
3.Toa Michirizi Mapajani, Chunusi na Madoa mwilini 40,000/
4.Punguza tumbo na Manyama uzembe 45,000/
5.Mkanda wa Kufunga Kupunguza tumbo 70,000/
6.Tengeneza Shepu Hips na Makalio  45,000/ ,Vidonge 80,000/
7.Ongeza Nguvu za Kiume  Jelly 45,000/ , Vidonge 60,000/
8.Ongeza Ukubwa wa Maumbile ya kiume Jelly 80,000/ , Mashine 160,000/
9.Kuongeza Mwili Mzima 40,000/
10.Kupunguza Mwili 45,000/
11.Kupunguza Maziwa na Kuyasimamisha 40,000/
12.Ongeza Mguu uwe wa Kupendeza 45,000/
13.Rudisha usichana ama Bikira 55,000/
14.Ongeza Hamu ya Kula 40,000/
15.Ongeza Hamu ya Kufanya Mapenzi 55,000/
16. Fanya mwili Kuwa Soft 60,000/

TUNAPATIKANA DAR NA MIKOA YOTE, HUDUMA ZINAFIKA POPOTE ULIPO , 
DAR TUPO KARIAKOO MSIMBAZI NA POSTA  MPYA

PIGA SIMU: 0719955528, 0756259180 au 0785371237

Nape Amtaka Zitto Kujenga Upinzani wa Kweli na Kuachana na Siasa Kama za Chadema

$
0
0
Salaam,nimesoma kwenye nipashe nape akimtaka kuanzisha upinzani wa ukweli sio kama wa chadema.kwa mujibu wa nape amesema chadema siasa zao zinaligawa taifa.mimi najiuliza ni upinzani gani anaoongelea nape kwa zitto? maana ili taifa lisigawanyike lazima wote tuwe ccm na ni upinzani gani anaomtaka zitto kuanzisha nakuifurahisha ccm?

Watoto 147 wakutwa misikitini Kilimanjaro Wakifundishwa Dini ya Kiislam Kinyume na Sheria

$
0
0
WATOTO 140 wenye umri kati ya miaka 10 na 21 wamekamatwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakilelewa katika misikiti mitatu tofauti. Taarifa zilizopatikana wilayani hapa zinasema watoto hao wamekuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watoto hao waligundulika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kupata taarifa na kuwafuatilia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kati ya Machi 25 na 27 mwaka huu.

Taarifa hizo zimeyataja maeneo waliyokutwa watoto hao kuwa ni Misikiti ya Masjid Bilal, Masjid Othiman na Msikiti wa Kwa Kiriwe.Taarifa hizo zimesema katika Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Mtaa wa Kibaoni wilayani hapa, walikutwa watoto wa kiume 70 wanaotoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Watoto wengine 50 wa kiume walikutwa katika Msikiti wa Masjid Othiman uliopo Mtaa wa Uzunguni ambao nao inasemekana wamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa hizo zinasema watoto wengine 27 walikutwa katika Msikiti wa Kwa Kiriwe ambako pia walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam na walimu Watanzania. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthoy Mtaka, alikiri kuwapo watoto hao wilayani kwake.

“Tukio hilo lipo na wanaohusika ni watu wanaotumia mwamvuli wa dini fulani kufanya mambo yasiyofaa katika jamii. “Kwa hiyo naziomba mamlaka husika likiwamo Baraza Kuu la Waisalam Tanzania (BAKWATA) kutambua miskiti na shughuli zinazoendelea katika nyumba hizo za ibada.

“Hili lazima walifanyie kazi kwa sababu hao vijana inasemekana wanafundishwa mazoezi makali ya kareti na judo katika nyumba hizo za ibada,” alisema Mtaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema atazungumzia tukio hilo leo. Kupatikana kwa watoto hao ni mwendelezo wa matukio ya watoto wanaolelewa kinyume cha sheria mkoani Kilimanjaro baada ya matukio mawili ya aina hiyo kuripotiwa hivi karibuni. La kwanza lilihusisha watoto 18 na la pili lilihusisha watoto 11 waliokutwa katika maeneo ya Lyamungo wilayani Hai.

Chanzo: Mtanzania

Rais Kikwete Aombwa Kutoupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandaoni, 2015 ....Ombi Hili Limetolewa Na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN)

$
0
0
Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni.  

Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

 Muswada  Wa  Sheria  Ya  Makosa  Ya  Mtandaoni,2015
Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika 

Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari.

Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu. 

Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho  sahihi?

Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari. 

Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia. 

Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013. 

Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’ 

Hii  inamaanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini. 

Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari. 

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

 IMETOLEWA NA;
Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN)
04/03/2015.
http://www.tbn.or.tz/

Mtangazaji Charles Hillary Anyakuliwa na Kituo cha AZAM TV Kutoka BBC..Sasa Kurudi Tanzania

$
0
0
Ngome ya kituo cha Azam TV inaendelea kuimarishwa, baada ya kuzinduliwa kwa studio kubwa na za kisasa za kituo hicho zilizogharimu zaidi shilingi bilioni 56, inadaiwa kuwa kampuni ya Azam Media itamrejesha nyumbani mtangazaji mkongwe wa BBC, Charles Hillary kwaajili ya kuja kujiunga na Azam TV.

Mchambuzi maarufu wa soka Edo Kumwembe ambaye pia hufanya uchambuzi kwenye kituo hicho, amepost taairfia hiyo kwenye akaunti yake ya Facebook kwa kuandika:

“….Mtangazaji maarufu wa BBC, Charles Hillary, anarudi nyumbani kujiunga na kituo cha Azam TV…..welcome home LEGEND….”

Hata hivyo chanzo kingine cha kuaminika cha ndani ya Azam TV kimethibitisha kuwa Hillary anarudi kujiunga na kituo hicho.

'Hatuko Tayari Kuzibwa Midomo Tunamtaka Lowassa Agombee Urais 2015' Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Jijini Mwanza

$
0
0
Shinikizo la kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuchukua fomu ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu, limeendelea na safari hii wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya jijini Mwanza, wametoa tamko la kumtaka kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, viongozi wa vyuo vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi  na Tiba za Afya (CUHAS), walimtaka Lowassa kuchukua fomu ya kuwania urais wakati ukifika.

Viongozi hao waliyazungumza hayo wakati wakikabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo Daima, jijini Mwanza.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa CUHAS, Godfrey Kisigo, alisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anapendwa na kila Mtanzania.

 Alisema wanamuomba muda ukifika awe mtu wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi ya urais.

Tamko hili ni la vyuo  vikuu vyote vya Mwanza, sauti zetu ni za busara kwa sababu zinataka kuikomboa nchi yetu kwa miaka 10 ijayo, tunayo imani kubwa na Lowassa katika hatma ya nchi hususan elimu kwa watu wote,” alisema na kuongeza:

Hatma ya nchi hii ipo mikononi mwako na sisi wanavyuo hatuwezi kusubiri kuona tunakosa kiongozi atakayelisaidia Taifa kwa kuzibwa midomo, tupo tayari kufa ili uwe rais uokoe watakaobaki na Tanzania.”

Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi SAUT, Christopher Mkodo, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisijaribu kukata jina la Lowassa kwani Tanzania bila kiongozi huyo Watanzania watakuwa wamenyimwa fursa ya kupata maendeleo ndani ya miaka 10.

Waliitaka CCM kusikiliza maoni ya wanachama wake  vinginevyo chama kitaharibika.

Mwakilishi wa CBE, Paul Dotto, alisema Lowassa ni chaguo la wanafunzi wa vyuo vikuu na wana imani ataifikisha Tanzania katika uchumi wa kati kabla ya malengo yaliyowekwa na Serikali.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na Zari The Lady Boss Wafunga Ndoa!

$
0
0
Jioni ya Jana Zimesambaa picha zikionesha Diamond na Zari wakiwa katika Mavazi kama ya Harusi ni kiwa na maana Shela na Suti ....Je watu hawa wameamua kuoana ama ni picha za kutubeep?
Picha hizo zimeacha maswali mengi juu ya wawili hawa....week iliyopota Diamond alimvisha Zari Pete ya Uchumba...

Diamond aliweka Picha hiyo na Kuandika Maneno haya Hapa chini:

'Wakati Mwingine Usiri Unabaraka zaidi.... Alhamdulillah
(Sometimes Privacy has more Blessings... Thank you so Much God'

Baadhi ya Comments za Mashabiki hizi Hapa kuusu picha hizo za Harusi:


miss_w91
Soo happy for u guys.msije baada ya muda mkatuambia oh ilikua project,mara sijui photo shoot tu,mara sijui tangazo au wimbo.mtanikera.love u two so much.be blessed

ma1boyt2c
Mmmh ni macho yangu au ni movie naona hapa

jwandzeun
Hahaha wonders shall never cease! Worst mistake. ......mnitusi sasa

divaryne
Bora u guys are done maana...u were on people's mouth sasa the talk will end i hooo

momomelisa
@milly_is_me 1st of may is when their real wedding ceremony will happen . it will be Friday meaning the form of marriage will be islamic in nature... these pictures are to let people get prepared to attend their wedding .. they couldn't say that they were going to get married..bt the pictures say everything... lets pray for dat day to come ed we officially celebrate their walking down of the aisle. wish whoever will attend da best . by the way......waiting for a baby shower hahhahahhhahha.. this year is full of their events..remember 1.


a.bakari
Uyo si kaolewa kama kaolewa bila ya kupewa talaka yake basi dhambi kubwa wanafanya ok

Diamond Aonyesha Hundi ya Pesa Aliyokabidhiwa na UAP kupitia CRDB Baada ya Ukuta wa Nyumba yake Kudondoka

$
0
0
Diamond Platnumz ameendelea kuwa na updates kila kukicha na hii ya leo ni baada ya ukuta wa nyumba yake kudondoka, Benki ya CRDB kupitia kitengo chake cha insurance imemkabidhi diamondi hundi ya hela kwa ajili ya kujengea ukuta wa nyumba yake.

Baada ya Amber Rose Kutoboa ya Moyoni, Kumbe Wolper Naye Yalishamkuta!!

$
0
0
Mara baada ya hapo jana mwanadada Amber Rose kutoboa ya moyoni na kueleza  kuwa  Wiz Khalifa ndio mwanaume pekee ambae anampa furaha na hatojali watu wanasema nini.

“My ManCrushEveryday you know what it is.... We went wrong somewhere and even if we never ever get back together ( Even tho I pray, dream and hope we do) he will forever be the love of my life. The media doesn't make it easy but fuck them we gotta live for reality and not society. We forever have a bond because we made a beautiful baby from our Love. Through all the ups and downs of our relationship my heart still beats for him every single day. I'm sick of putting on a front like I'm happy without him. I'm not. He makes me happy. He's the only one who can. Regardless of how our lives Turn out in the long run he will always be the skinny tatted up stoner that has my heart” Amber alimaliza na kubandika picha akidendeka na Wiz.

Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Jacqueline Wolper aliubandika tena ujumbe huo kwenye ukurasa wake mtandaoni na kundika maneno haya.

Asante dada Amber kitu hicho kimenitokea na niko happy Now na maisha yangu unajua beta kuwa Muwazi sema na moyo wako usiseme na mimoyo yao wanafkreee wanaojua kuongoza maisha ya watu kama wao ndo wamekuzaaa shenzeee .Sema na moyo wako rudi kwake ata kama wakikusema unajipendekeza poa tuu usisikize ushauri wamarafiki sometime wanakupoteza nahuwezi jua mapenzi yao kwako maana marafiki bwana ooh usijishushe we star we mzuri we unakosa nini.... Moyo aunaga uzuri wala ustar wala pesa.. Moyo ni moyo na mengne ni mengine maneno haya yametoka kwenye sakafu ya moyo wangu done ..happy 4 u Amber .

Picha: Ni Kweli Lulu Ana Mimba?! Jionee Mwenywe Hapa

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameweka tena picha yake mtandaoni (hiyo hapo juu)akionekana   mjamzito, hii ni mara ya pili baada ya hivi juzi kati kuweka picha  ya mwanamke mjamzito bila kuonyesha sura yake, kitendo ambacho kilionekana kuwa  sio yeye na niuongo kwani siku hiyo ilikuwa ni siki ya wajinga dunia.

Hata hivyo bado watu wengi hawajaamini kuwa mrembo huyo kwasasa ni mjamzito na hata lulu mwenyewe hajaweka wazi kuwa kwasasa ni mama kijacho japo wanasema “kusoma haujui hata kuona picha?”.

Wachache wanaohisi  kuwa  hizi ni picha akiwa anarekodi filamu  kwa hoja kuwa tumbo la mimba huwa halipo hivyo, hawa wanaweza kuwa wanakaribia kwenye ukweli.

Tuendelee kusubiri.

Gwajima Atoa Video Nyingine Yenye Maneno Yenye Utata, Angalia Hapa.

$
0
0
Gwajima Akiwa kwenye Kitu cha Wagonjwa Anaonekana Kwenye Video Akitoa Maneno yenye utata kumsema mtu kwa Mafumbo ..embu angalia hapa chini kwenye Video:
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images