Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Al Shabaab Waichimba Mkwala Kenya Baada ya Shambulio la Garissa, Wasema Wataendelea Kumwaga Damu Kenya Asipotimiza Masharti Haya

$
0
0
Kundi la Kigaidi la Al shaabab Kutoka Somalia wametoa official Statement (Tamko) Kuwa Wenyewe ndio walio husika na Tukio la Kuvamia Chuo kikuu cha Garissa na kuuwa wanafunzi Takribani 147 wiki iliyopita..

Katika tamko hilo Al shabaab wamesema tukio hilo ilikuwa ni majaribio tu kwani wanapanga mauji makubwa zaidi ya hayo nchini humu kama Kenya Haita ondoa majeshi yake nchini Somalia ..

Taarifa hiyo imesema kuwa Wanajeshi wa Kenya wamekuwa Mstari wa Mbele kuuwa Wasomalia wa Kiislam huku Somalia na Kuwabaka Wanawake ovyo hivyo matukio haya wanayofanya sasa ni kulipiza Kisasi...

Nukuu:
"There will be no safer place for Kenyans as long as their troops are in Somalia," Rage said.

Over 5,000 KDF forces are currently in Somalia fighting the Al Shabaab militia.

“You will see more deadly attacks in your country, Kenya," said Rage as he praised the martyrs who butchered 147 kafirs (non-believers) and blew themselves up

Udaku Specially

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Lulu: Nilimtolea Uvivu na Kumpa vidonge vyake Shabiki Huku Instagram ili iwe Fundisho kwa wengine

$
0
0
ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa juzikati aliamua kumjibu shabiki mmoja mtandaoni kutokana na kuwepo kwa watu wengi wanaomsema vibaya mitandaoni

Akizungumza na mwanahabari wetu mara baada ya kumjibu shabiki Gladmarry Edwine aliyemkejeli kupitia mtandao wa Instagram kuwa ikifika siku ya Kanumba Day (Aprili 7, mwaka huu), Lulu atajiliza ndipo staa huyo alipomtolea uvivu iwe fundisho.

“Yule alinikuta siku hiyo siko vizuri halafu niko Instagram nikaamua kumtolea uvivu kwa kumpaka maneno ya shombo iwe fundisho,” alisema Lulu.

“Yule alinikuta siku hiyo siko vizuri halafu niko Instagram nikaamua kumtolea uvivu kwa kumpaka maneno ya shombo iwe fundisho,” alisema Lulu.

Lulu alimwambia mtu huyo kuwa asijifanye anamjua sana Kanumba kuliko yeye ambaye alikuwa akilala naye kama mchumba wake.

Mke Wa Mtu Afumaniwa Akingonoka Na Mume Wa Mtu

$
0
0
Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mtu yeye alijikuta akiiserebukia kwa fumanizi gesti, tena akiwa na mume wa mtu!

Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka

Katika fumanizi hilo, timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa mtupu bila kujali hali hiyo.

Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba Somoe, mkazi wa Kongowe (nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam) alimchepuka mke wake (mama Somoe) na kuanzisha uhusiano na mwanamke huyo.

Chanzo kikazidi kudai kwamba mkewe huyo alianza kutilia shaka mwenendo wa mumewe kutokana na kubadili tabia, hasa za kuwa beneti na simu hivyo alianza kumfuatilia kwa karibu.

“Katika kumfuatilia, siku moja akabaini meseji. Akamuuliza mumewe kuhusu meseji hiyo naye akawayawaya bila kuwa na majibu sahihi,” kilisema chanzo hicho.

Habari zaidi zilisema kuwa kutokana na ukweli kwamba, ndani ya nyumba yao, mama Somoe ndiyo kajaliwa uwezo wa kumiliki fedha, alimpa masharti mumewe kwamba achague mawili, watengane na aondoke na begi lake la nguo au atoe ushirikiano, ‘mwizi’ huyo anaswe.

“Mume akasema cha kufia! Akakubali kutoa ushirikiano ili mchepuko wake afumaniwe,” kilidai chanzo chetu.

Ali Kiba ‘habari nyingine’ afunika Shoo ya Mwana Dar Live

$
0
0
Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live.
Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Ali Kiba akizidi kuitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
 
Kwa picha na habari zaidi ya shoo hiyo ingia  << HAPA >>

Gwajima Avunja Ukimya.....Asema Atakufa na Lowassa na Dr. Slaa, Asisitiza huu sio Muda wa Kuchaguliana Marafiki

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alihubiri akiwa katika kiti cha magurudumu na kusema hawezi kuwatupa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi.

Pia askofu huyo, amewataka waumini wote wa kanisa hilo kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi, Alhamisi ijayo siku ambayo atakwenda kukamilisha mahojiano dhidi ya tuhuma za kumtukana Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.

Akihubiri mamia ya waumini waliofika kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Pasaka jana, Gwajima alisema kumekuwa na uvumi kwamba kuhojiwa kwake na polisi kulitokana na kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa nyakati tofauti na kuzungumza na waumini wake.

Alisema alifahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 wakati huo mbunge huyo akiwa Waziri wa Ardhi na tangu kipindi hicho amekuwa mtu wake wa karibu.

Alisema alifahamiana na Dk Slaa tangu mwaka 1994 kabla hajagombea nafasi ya urais kupitia Chadema na kwamba tangu wakati huo amekuwa rafiki wa familia.

“Hawawezi kunichagulia marafiki, hawa ni watu wangu wa karibu hata kabla hawajawa na ndoto za kugombea urais, nitaendelea kuwa nao karibu,” alisema.

Asimulia mahojiano
Akizungumzia mahojiano yake na polisi, Gwajima aliwaeleza waumini wake kwamba mambo mengi aliyohojiwa hayakuhusiana na suala la kumkashifu Kardinali Pengo.

“Polisi walinihoji mambo mengi binafsi yanayonihusu mimi na hayakuhusiana kabisa na Pengo, maswali ya Pengo yalikuwa machache sana,” alisema.

Hata hivyo, Gwajima alisema hana ugomvi na polisi wala Serikali kwa kuwa amekuwa akitoa ushirikiano kwa vyombo hivyo. Akitoa mfano, alisema Februari mwaka huu alipeleka barua polisi kueleza anataka kudhamini kampeni kwa ajili ya kupinga mauaji ya albino kwa kushirikiana na jeshi hilo.

“Niliwaeleza kwamba tungezunguka na polisi mikoa yote Tanzania na wamenijibu kwamba nipeleke ratiba ya shughuli hiyo ili tuanze,” alisema.

Alisema pia alidhamini mafunzo ya ulinzi shirikishi kwa vijana 400 kwa kushirikiana na polisi... “Shughuli hizi zinaonyesha kwamba sina ugomvi na polisi, bali nimekuwa rafiki kwa kushiriki katika shughuli zenye masilahi kwa Taifa.”


Viongozi wamiminika
Alisema pia hana ugomvi na Serikali na kwamba viongozi wake wamekuwa wakimiminika katika kanisa lake.

Aliwataja viongozi hao kuwa ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe.

Viongozi wengine, alisema ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee na wabunge wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa na Vicky Kamata wote wa CCM
 
 “Kama ningekuwa na ugomvi na Serikali viongozi hawa wasingekuja katika kanisa langu kwa nyakati tofauti. Hii inaonyesha nilivyo na uhusiano mzuri na Serikali,” alisema.

Alhamisi ijayo
Askofu Gwajima amewataka waumini wake kumsindikiza katika Kituo cha Polisi siku ambayo atahojiwa kwa mara nyingine. “Nitakwenda Central Police Alhamisi saa moja asubuhi, nawaomba waumini wote mfike katika eneo hilo lakini msilete fujo wala kumtukana mtu, kuweni watulivu wakati wote nitakapokuwa nahojiwa,” alisema.

Askofu huyo alitakiwa kuhojiwa Alhamisi iliyopita lakini polisi waliahirisha kutokana na hali yake kutokuwa ya kuridhisha.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Jeshi la Polisi halitaruhusu mkusanyiko wa watu katika eneo hilo wakati Askofu Gwajima atakapohojiwa.

“Atatakiwa kufika na wakili wake na mtu mmoja ambaye ataona anafaa kuingia naye kwenye mahojiano. Kama kuna waumini wanajiandaa kukusanyika katika ofisi zetu hapa Central Polisi, wafahamu kwamba haturuhusu na wakikaidi tutachukua hatua.”

Ilivyokuwa kanisani
Gwajima alifika katika kanisa hilo lililopo kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe saa 5.00 asubuhi na kupokewa kwa shangwe na waumini walioanza kufika tangu saa 2.00 asubuhi.

Msafara wa magari matatu; Toyota Land Cruiser mbili na Hammer, yaliwasili kwenye viwanja vya kanisa hilo na kulakiwa na waumini walioyazingira kwa shangwe na vigelegele wakitaka kumwona Askofu Gwajima.


Waumini hao walikuwa na shauku ya kumwona Gwajima na walionekana wakisukumana ovyo kila mmoja akitaka kumwona.

Akiwa amevaa suti ya rangi ya kijivu na shati jekundu, Gwajima aliteremka katika Hammer akishikiliwa na wasaidizi wake na kukalishwa katika kiti cha magurudumu mawili kilichokuwa kikisukumwa na wasaidizi hao kuelekea kwenye jukwaa la kanisa hilo.

Baada ya kufika, vikundi vya kwaya viliendelea kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali za kumtukuza Mungu.

Gwajima alizungumza na waumini wake kuanzia saa 5.30 hadi saa 6.45, akiwaeleza kilichotokea kuanzia siku alipofika polisi kwa mara kwanza, mahojiano hadi alipotoka hospitali.

Katika mahubiri yake, Gwajima alisema ataendelea kuwaonya viongozi wa Serikali na wa dini watakaokosea masuala mbalimbali.
 

 “Sitajali ni kiongozi wa aina gani amekosea nitawakemea. Rais akikosea nitamkemea. Waziri akikosea nitamkemea na viongozi wa dini wakikosea nitaendelea kuwakemea,” alisema.

Kauli ya Shibuda kuhusu kuhamia chama Kipya Cha ACT-Tanzania

$
0
0
Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amekataa kuhusishwa na Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), akisema hana mpango wa kujiunga nacho.

Shibuda ambaye ameshatangaza kutogombea ubunge kupitia CHAsdemA katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, amesema “Pamoja na kusema sitagombea kupitia CHADEMA lakini nisilishwe maneno…siendi kwenye chama hicho cha ACT.”

Kauli ya Shibuda imeondoa uvumi ulioenea kwamba angejiunga na ACT baada ya kuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu na CHADEMA.

Akichangia hoja ya muswada wa sheria ya makosa ya mtandao bungeni wiki iliyopita, Shibuda alitumia dakika mbili kuweka sawa uvumi huo akisema, “sitaki kusemewa…nitasema mwenyewe kuhusu mstakabali wangu kisiasa. Huu ni uzandiki.”

Hii si mara ya kwanza kwa Shibuda kuhusishwa na mpango wa kuhamia katika vyama vingine vya upinzani. Mwishoni mwa mwaka jana pia kulikuwa na uvumi kwamba yuko kwenye mazungumzo ya kukinunua Chama cha TADEA kinachoongozwa na Lifa Chipaka.

Hata hivyo, Shibuda alikanusha uvumi huo akisema analishwa maneno.

Itanichekesha sana kama Boko haram watapoa katika utawala wa Bukhari

$
0
0
Dunia ina mambo sana. Uchaguzi umepita Nigeria na kigezo kilikuwa ni Boko Haramu. Kabla palikuwa na tetesi kuwa askari fulani walikuwa wakisusa kuwapiga Boko Haram. Jonathan akapewa shinikizo lingine kuwamaliza boko haramu pamoja na suala la rushwa mbalo kila mtu anajua Nigeria haiwezi tibika kwa hilo zaidi ya propaganda kupikwa ili kubadilisha wapiga kura wasiulize rushwa. Rais Bukhari Dictator wa zamani aliengia kiraia ana kila connection katika majeshi na haswa watu wanye imani moja na yeye. Rais aliyekuwa na mikono na support kutoka kaskazini na nchi za jirani kaskazini, leo kaahidi kuwa Boko haramu watapotezwa haraka, sijui itakuwa haraka kama kuzima mshumaa. Cha kujiuliza ni kwamba hakuwa na mkono katika kuhujumu majeshi waislam wasiwapige boko haramu? Je hana link na boko haramu? Je anawezejae kuiambia dunia si boko haramu wameacha kwa kuona kaingia rais wao na pengine kuna hatua za hila zinatengenezwa ili baadhi ya malengo ya boko haramu yaanze jadiliwa na kupitishwa, kisha akiingia tena Mkristu Boko haramu waibuke na kuleta fujo ili lingine lipite? Itashangaza sana wakifanikiwa kuzima boko haramu.

Nay wa Mitego Ana Laana ya Picha Zangu za UCHI"....Fatuma Ayubu

$
0
0
Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.

Akiongea  na  mwandishi wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano

“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye mitandao ya kijamii,  jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.

Tattoo ya Wema Sepetu Mgongoni Mwa Kajala..Is it Still There??

$
0
0
Wema Sepetu na Kajala Masanja Walikuwa Marafiki wa kufa mtu , baada ya Wema Kumlipia Kajala Mil 13 ili aachiwe kutoka Gerezani Kajala alijichora Tattoo mgongoni mwake yenye jina la Wema , Sasa am just wondering kama hiyo tattoo bado anayo baada ya urafiki wao kuvunjika kwa muda mrefu?

Hii hapa ndio ilikuwa habari ya Kajala kujiweka Tattoo ..bonyeza Hapa:

Kajala Aamua Kujichora Tattoo ya Wema Sepetu Kumuenzi

Naombeni Msinilaumu kwa Uamuzi Huu Niliouchukua kwa Mume Wangu

$
0
0
Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe

Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe

wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu

kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..

nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.

Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile

Is Wema Sepetu A Follower And Not A Leader?

$
0
0
Today I followed up on Wema's past friendships and to think of it most of the things she does depends on the friends she keeps. She always looks up to the characters of the current "best" friend


At this time, her hairstyles and her look was clearly based on Kajala's.
Then Wema became friends with Snura and all hell broke lose. She suddenly started to bleach her skin with cheap products. The picture speaks for itself!!!!
Clearly all the above was just the tip of the ice berg. Wema finally kissed the ultimate frog. This friendship has lasted longer than the others. Show me your friends and i'll tell you your character!!!

What do you think about this one?

K-LYN amfunga ndomo ZARI kwa "PESA" Sasa K-Lyn Ndio Bosslady wa Ukweli

$
0
0
Miss Tanzania wa mwaka 2000 na mwanamuziki wa bongo fleva, jackline ntuyabaliwe aka k- lyn hatimaye amekuwa mke mke rasmi wa mfanyabiashara maarufu na TAJIRI nambar moja nchini, Reginald mengi baada ya kufunga ndoa iliyohudhiriwa na mastaa mbali mbali wa nchini ufaransa na Tanzania.

Kama ilivyo ada kwa mke wa raisi kuitwa "FIRST LADY vivyo hivyo kwa mke wa tajiri jina hubadilika na kuwa "BOSSLADY ". Kutokana na hali hiyo kuanzia sasa k-lyn anakuwa ndiye raisi wa ma bosslady wote afrika mashariki kutokana na pesa aliyonayo mumewe mzee reginald mengi.

Awali kabla ya k-lyn kutwaa wadhifa huo, mwanamuziki na mfanyabiashara toka uganda ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki nguli wa bongo fleva diamond platnumz, zarinah hussein aka zari aliaminika ndiye anayeongoza kwa pesa kwa mastaa Africa mashariki. Kwa sasa hali imebadilika na taji hilo kuelekea kwa mwana mama mrembo K -lyn.

Akon Awajibu Wanamuziki wa Kenya ni Baada ya Kulalamika kuwa akon Hataki Kufanya Nao Colabo

$
0
0
Mwanamuziki mwenye tuzo la kimataifa Akon amesema kuwa hakuna hata mwanamuziki mmoja wa Kenya ambaye amemuomba kufanya naye 'kolabo'mara zote tano ambazo ameweza kuzuru Kenya.
Akon Hatahivyo ameliambia jarida la Mondayblues nchini Kenya kwamba wasanii wa muziki barani Afrika pia wanafaa kuimarisha viwango vyao ili kutoa changomoto kwa wasanii kama yeye ili kuweza kushirikiana nao.
Tamko la msanii huyo linajiri kufuatia madai kutoka kwa wanamuziki wa Kenya kwamba hayuko tayari kufanya nao Kazi.

Chakujifunza Kutoka kwa Wolper, Kajala na Irene Uwoya

$
0
0
Kama ulikuwa hujui basi nakuhabarisha, mastaa ambao wameshibana kwa sasa, namzunguzia wema sepetu pamoja na aunty Ezekiel. Hapo awali waliwahi kuingia kwenye bifu zito kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la aliyekuwa mcheza filamu maarufu nchini, marehemu kanumba. Bifu hilo lilifikia pabaya ambapo mastaa hao walirushiana maneno makali kwenye mitandao kila mmoja akimshtumu mwenzie kumuibia bwana ake, bifu hilo lilidumu kwa mda mrefu, lakini sasa ivi mastaa hao wameshibana na kuishi kama ndugu, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.

Unakumbuka kipindi kile kwenye Interview ya zamaradi mketema alipowahoji irene uwoya na wema sepetu kuhusu bifu lao na jackline wolper? Bifu lilikuwa zito, ambapo chanzo kinadaiwa kuwa ni mwanaume, warembo hao walinuniana na kutupiana maneno machafu mitandaoni. Hivi sasa mastaa hao wanaishi kwa amani na maisha yanaendelea.

By Warumi-on JF

Zari wa Diamond Awakata Haters Kidomo domo..Awaonyesha Tumbo lake Live Live

$
0
0
After all is said and done about Zari faking pregnancy, she decided to come out and show off her baby bump , Haters !! Its for real ....Congrats to you Zari and Diamond


Hemedy 'Nimeamua kubadilisha maisha yangu, Mwaka Huu Lazima Nioe'

$
0
0
Mwanamuziki na Mwana Bongo Flava Hemedy PHD amekuja na Mpya na Kusema kwa sasa ameamua kubadilisha maisha yake na kuacha maisha ya Usela....Msikilize hapa Kwenye Video akitoa ahadi za kuvuta jiko mwaka huu:
Video

Jeshi la Kenya Lafanya Shambulio Somalia Kulipiza Kisasi Baada ya Al Shabaab Kuuwa Wanafuzi 148 Kenya

$
0
0
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.

Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.

Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.

Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita

.Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

Udaku Specially Blog

Askofu Pengo akaza uzi, Asema Hawezi Badili Msimamo wake "Waacheni Waumini Wafanye Maamuzi yao Wenyewe Juu ya Kupiga Kura ya Ndio Ama Hapana"

$
0
0
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema msimamo wake kuhusu Katiba Inayopendekezwa uko pale pale na ametaka wanaoamini alichosema, wasambaze ujumbe wake kwa wengine.

Akizungumza na Chama cha Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) hivi karibuni, Askofu Pengo alitoa wito kwa waumini kuachwa huru wafanye maamuzi yao wenyewe juu ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana Katiba Inayopendekezwa badala la kushinikizwa na viongozi wa dini kuipigia kura ya ‘hapana’ katiba hiyo.

Aidha, amesema kamwe hawezi kubadili kile alichosema kwani ni ukweli anaouamini na alishaweka hilo wazi.

Jakaya Kikwete Ajipalilia na Kujivunia Miaka Kumi ya Kuiongoza Tanzania kwa Mafanikio Makubwa

$
0
0
SERIKALI ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Aidha, Rais Jakaya Kikwete anayeiongoza awamu hiyo, amesema anatumaini uchaguzi mkuu ujao utakaotoa wabunge, madiwani na rais ya awamu ya tano unaotarajiwa kufanyika Oktoba , utakuwa huru na wa amani.

Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi urais mrithi wangu katika hali ya utulivu,” Rais alisema.

Rais aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson.

Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia,” Rais Kikwete alisema na kuongeza anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo mwaka 2020.

Je kwa Upande wako unaona JK ameleta Mafanikio Tanzania ?

Udaku Specially Blog

Ndoa ya Mwigizaji Shamsa Ford Yavunjika 'Dick Ameninyanyasa na Kunipiga kwa Muda Mrefu ila nilificha Kuepuka aibu''

$
0
0
Staa  mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford amefunguka rasmi kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake ya kimila aliyofunga na mwanaume wake wa siku nyingi, Dickson ‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda mwingi kwa mtu ambaye hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Akizungumza  na gazeti la Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.

Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu  lakini kuepuka aibu ya kuwa mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema Shamsa.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images