Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Baada ya Kutemwa na Kunyang'anywa Mtoto Siwema Aendelea Kupeta, Anunua Gari Mpya Kwa hela zake Mwenyewe

0
0
 Wakati Mpenzi wake wa zamani Nay wa Mitego akiwa Bize na Baby yake Mpya Shamsa Ford , Siwema Ameamua kujipoza machungu ya kuachwa na kunyang'anywa mtoto kwa kununua gari mpya.....
Ameweka Picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na Kuandika yafuatayo:

wemalicious:
 Thank u ZAMZAM MOTORS LTD.....kwakufanikisha hili...u always good to me#magari yenu yako bomba ile mbayaaa # namba ikitoka ntawambia ili msinipite barabarani!!!!
wemalicious :
She cheat again......# whaaaat?

Toa Maoni yako Hapa chini

Mkeo/Girlfriend Katuma Picha zake za Uchi kwa Mwanaume

0
0
Wakuu naombeni ushauri... nimeishi na mke wangu wa ndoa kwa miaka kama 10 hivi sasa. Ila ndani ya muda huo ndani kumekuwa na migogoro ya hapa na pale ya kutoaminiana. Ila katika hali hiyo yeye ndiyo alikuwa ananishutumu mimi kuwa nina michepuko na yeye kujiona yupo innocent kama malaika. Lakini juzi kati hivi, katika pita pita yangu nikgundakuna mwanaume yupo nae busy ofisi kwake.

Nilipomuuliza akaribu kutoa utetezi ambao sikuridhika nao, nikaanza kumfutilia kimyakimya kenye simu zake n email zake. Siku ya siku nikkutana na chats kwenye whatsap baina yake na uyo mwanaume.. na mke wangu kimtumia huyo mwanume picha zake akiwa mtupu kigia kwenye kitanda chetu...

Hebu nipeni ushauri, maana hatua ya kwanza niliyoichukua ni kumrudisha kwa wakati natafakari maamuzi ya kudumu. Mpaka sasa yupo kwa mjomba wake..

Advice please guys!!!

Waziri Steven Wasira Awafukuza Kazi Wakurugenzi Watendaji Watatu Kwa Kuisababishia Serekali Hasara ya Sh Billioni 2.5

0
0
WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia  hasara ya Bilioni 2.5 Serikali .

Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Wassira amesema  baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa  vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo, aliunda  timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo.

“Baada ya kuunda tume  kutoka hapa Wizarani ikishirkiana   na Hazina, walienda  kwenye shirika hilo  kufanya  ukaguzi.Tume ilibaini kwamba mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi  hawa  walijifanya  wahasibu, wakawa  wanakuanya  pesa  wenyewe  na  kutembea  nazo.Walifanya  maksudi tu ili kujiwekea mianya ya kuiba  Fedha” Amesema  Wassira

Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.

Waziri Wassira amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini kwamba watendaji hao wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi yaliyo  kinyume  cha  utaratibu
ikiwemo pesa zilizotengwa kwa ajili  maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo  zimetumika  ndivyo  sivyo.

Vilevile Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa ajili ya kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa na watendaji , tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.

Aidha,Waziri Wasira amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya shirika la Ludaba kuwafukuza kazi mara moja watendaji hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja huku  taratibu na sheria za kuwafikisha mahakamani zikifanyika.

Toa Maoni yako Hapa Chini

Wanabongo Fleva wa 5 Anaowakubali Wema Sepetu, Diamond Namba Moja

0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu pamoja na kutengena na mpenzi wake Nassib Abdul ‘Diamond’ lakini alipoamua kutaja wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva mtaliki wake huyo kampa namba moja katika wasanii watano ambao yeye anaona wanafanya vizuri katika muziki.

“Muziki umeshika kasi na kuna wasanii ambao wanafanya vinzuri kuliko wengine, kwangu Top 5 yangu 1 Nassib, wa pili ni Ashley, Ali kiba, Barnaba na wa tano ni mirrow hawa ni wasanii wanzuri wapo level za kimataifa,”anasema Wema.

Aidha Wema amesema kwa upande wa wasanii wa kike anampenda sana mwimbaji Vanessa Mdee kwani anaimba na kucheza katika kiwango cha juu na kumfanya awe ni mpenzi wa kazi za msanii huyo, pia anataka watu wasimuelewe vibaya ni kwa mujibu wa mapenzi yake na maono yake.

Toa Maoni Yake Hapa Chini

Shilole Awataka Watu Wamuache Afanye Yake

0
0
Staa mrembo wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Shilole ‘Shishi Bybee’ amewataka watu wamuache afanye kile anachokitaka kwenye maisha yake na sio kumpagia aishi vipi.

Shishi Bybee aliyasema hayo mara baada ya baadhi ya watu kumshambulia kwa maneno baada ya kuweka picha picha akiwa yupo kwenye bwawa la kuogelea.

Yaani watu mnapenda kunipa raha sana mimi mwenywe nimejikubali na mimi nipo swimming mlitaka nivae dela??? Nioge nalo kwa hiyo tunapangiana na maisha ya nyumban pia lol! Kila mtu na life yake naombeni mniache nifanye yangu” Shishi alisema.

Baadhi ya watu walionyeshwa kukelwa na picha hizo (hapo juu) za Shilole wakidai kuwa zinamdhalilisha kama mwanamke kwani sehemu kubwa ya mapaja yake yapo wazi.

Toa Maoni Yako Hapa Chini:

Polisi Yazuia Wafuasi Wa Askofu Gwajima.....Vikosi vya Mbwa, Farasi,Magari sasa kila Kona.

0
0
Jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  limesema  wafuasi  wa  Askofu  mkuu  wa  kanisa  la  ufufuo  na  uzima,Josephat  Gwajima  wasithubutu  kutia  mguu  eneo  atakalohojiwa  askofu  huyo.

Kauli  ya  jeshi  hilo  imekuja  siku  chache  baada  ya  Askofu  Gwajima  kuwataka  wafuasi  wake  kumsindikiza  leo  kituo  cha  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  ambako  anahitajika  ili  kuhojiwa.

 Msimamo huo  ulitolewa  jana  na  kamishna  wa  polisi  katika  kanda  hiyo, Suleiman  Kova  wakati  akizungumza  na  mtandao  huu  ambapo  alisisitiza  kuwa  anayehitajika  kufika  katika  kituo  hicho  ni  Gwajima  na  mwanasheria  wake.

Kamishna  Kova  alisema  ni  vema  wafuasi  hao  wakaendelea  na  kazi  zao  za  uzalishaji,kwani  kwenda  kituoni  hapo  bila  mwito  au  kukamatwa  ni  kosa.

Kova  alisema  eneo  hilo  haliruhusiwi  watu  kukusanyika, hivyo  kwa  usalama  wao ni  vyema  wakaendelea  na  shughuli  zao  na  kuliacha  jeshi  hilo  lifanye  mahojiano  na  Askofu huyo  wakiwa  huru.

"Napenda  kutumia  nafuasi  hii  kumuomba  Gwajima  awaambie  wafuasi  wake  hawahitajiki  kufika  eneo  hilo  kwani  anayehitajika  ni  yeye  na  mwanasheria  wake," alisema  Kova.

Kova  alisema  iwapo  kila  mtu  atafuata  taratibu  hakuna  nguvu  itakayotumika  kutoka  jeshi  la  polisi, lakini  endapo  watakiuka  hakuna  njia  mbadala  ambayo  inaweza  kutumika  zaidi  ya  kutumia  nguvu.

Kauli  ya  Kova  inakuja   kutokana  na  kauli  ya  Gwajima  aliyoitoa  wakati  wa  sikukuu  ya  pasaka  kuwataka  wafuasi  wake  kujitokeza  katika  kituo  hicho  wakati  atakapokwenda  kuhojiwa.

Gwajima  alisema  lengo  la  kuwataka  wafuasi  hao  kujitokeza  ni  ili  waweze  kujua  kila  kitu  kinachoendelea  katika  sakata  hilo  kwani  kuna  taarifa  ambazo  zimekuwa  zikizushwa  na  watu  kupitia  mitandao  mbalimbali.

Akizungumzia  hali  ya  usalama  katika  jiji  la  Dar, Kova  alisema  ni  shwari  na  kuahidi  kuwa  wanaendelea  na  oparesheni  ya  kukamata  wauza  dawa  za  kulevya, wahalifu  na  kulinda  maeneo  ya  fukwe.

Pia, alisema  wamejipanga  kukabiliana  na  vitendo  vya  kigaidi  ambapo  wanafanya  uchunguzi  kila  mahali  kwa  kutumia  vikosi  vya  mbwa, farasi,helkopta, magari, pikipiki  na  kutembea  kwa  miguu  katika  maeneo  yote  ya  jiji.

Toa Maoni yako Hapa Chini:

Baada ya Kunusurika Kifo Sauz TEVEZ wa Isha Mashauzi Afanya Dua la Kumshukuru Mungu

0
0
Tevez aliwakusanya ndugu, jamaa na marafiki na kufanya dua hiyo, Ijumaa iliyopita nyumbani kwao Msamvu, Madawa jirani na Shule ya Msingi Msamvu ‘A’ ambapo alifanya kisomo hicho kilichoambatana na dua na chakula.

“Mungu amemnusuru na balaa lile, amemkingia hivyo ameona ni vyema aandae dua ya kumshukuru,” alisikika mmoja wa waalikwa.Baadhi ya mashehe na waumini wengine wa Kiislamu waliohudhuria dua hiyo walimpongeza Tevez kwa kitendo hicho cha kumkumbuka Mungu na kumshukuru kwa kumlinda na majanga yaliyomkuta.

“Hili ni jambo jema sana alilofanya Tevez ambapo tunaelekezwa na mitume wetu kwamba tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema mmoja wa waumini wa dini ya Kiislamu.Kwa upande wake Tevez alisema amamshukuru Mungu kwani amempigania sana uhai wake.

“Lilikuwa  ni tukio kubwa kwangu, sikutegemea kama ningenusurika, Mungu amenipigania sana nimeona bora nijumuike na ndugu, jamaa na marafiki kumshukuru Mungu,” alisikika Tevez.Januari mwaka huu, Tevez alitekwa na watu wasiojulikana katika mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambapo mwenyewe alibainisha kuwa mwenyeji wake mjini humo alivujisha habari kuwa ana fedha ndipo akavamiwa, akateswa na kuporwa fedha na simu zake mbili

Tevez aliwafungulia mashtaka vijana waliohusika na tukio hilo ambapo kesi inaendelea kuunguruma nchini humo.
GPL

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Rose Ndauka na Shetta Wadaiwa Kulala Chumba Kimoja Hotelini Morogoro

0
0
KIMESANUKA! Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nurdin Bilal maarufu kama Shetta anadaiwa kulala chumba kimoja na staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka katika hoteli iitwayo Kingway iliyoko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Chanzo makini kinachofahamu kwa undani kinachoendelea baina ya mastaa hao wawili, kimelidokeza gazeti hili kuwa tukio hilo lilijiri wakati wakielekea katika shughuli za mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge aliyezikwa kijijini kwao Mkuyuni mkoani humo, ambako watu wengi maarufu walihudhuria.

“Si unajua mastaa kibao walikuwepo kwenye ule msiba, basi Rose na Shetta nao walikuwepo na wakati wa kwenda Mkuyuni, walipanda gari la Shetta hadi Morogoro mjini ambako walichukua chumba na kulala wote hadi kesho yake walipohudhuria mazishi na kurejea Dar es Salaam,” kilisema chanzo hicho.

Ili kushibisha maelezo yake, mtoa habari huyo alilitumia gazeti hili video ya wawili hao wakiwa ndani ya gari la Shetta inayomuonyesha Rose akiimba nyimbo mbalimbali za mkali huyo anayetamba na kibao chake kipya cha Shikorobo ambacho video yake imefanywa na mtayarishaji anayetamba nchini kwa sasa, Godfather wa Afrika Kusini.

Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama uhusiano wa wawili hao ni wa siku nyingi au umeanza hivi karibuni, ingawa gazeti hili linafahamu kuwa Shetta ni mume wa mtu akiwa amezaa naye mtoto mmoja.
Amani lilimtafuta Shetta na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu yake ya mkononi na aliposomewa mashtaka, kwanza alicheka na kusema kuwa ni kweli alikuwa msibani na alirejea Dar akiwa na Rose katika gari lake.

“Ninachoweza kusema ni kuwa ni kweli nilimpa lifti Rose wakati tunaenda kwenye mazishi ya Bonge. Kulikuwa na magari mengi ambayo mtu yeyote angeweza kupata lifti na ni kweli pia tulilala Morogoro, ilikuwa ni hoteli moja lakini kila mtu alilala chumba chake, siwezi kujihusisha na hayo mambo, mimi nina familia,” alisema msanii huyo ambaye pia aliwahi kutamba na kibao cha Kerewa, alichomshirikisha Diamond.

Kwa upande wake, Rose Ndauka alipoulizwa kuhusu suala hilo, kwanza alishtuka na kuuliza zilikopatikana habari hizo kabla ya kukiri ukweli kuwa alipanda gari la Shetta na wote kulala hoteli moja mjini Morogoro, lakini kila mtu na chumba chake.

“Halafu nisingependa kuandikwa andikwa kila siku kwa mambo hayo, unajua kama mimi nina mtu wangu? Andikeni halafu tutaonana mahakamani, maana naona lengo lenu ni kuniharibia,” alisema Rose
GPL

TOA MAONI YAKO HAPA

Kova: Ole Wenu Wafuasi wa Gwajima

0
0
Kamanda Kova amewaonya vikali wafuasi wa Gwajima kuandamana Leo kuelekea makao makuu ya polisi ambapo mch. Gwajima Leo atahojiwa.

Onyo hilo linakuja baada ya mchungaji Gwajima kuwaambia wafuasi wake wakati wa ibada ya pasaka kumsindikiza makao makuu atakapoenda kuhojiwa.

My take;
Gwajima bora uwazuie wafuasi wako kwani watakula kichapo kikali Kova huwa hatanii waulize wanabawacha

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Zitto Kabwe: Wabunge zaidi 50 wa vyama Mbalimbali Kujiunga na ACT-Wazalendo

0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo , Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na Chama chake kipya cha "ACT", wakiwemo wa CCM na Chadema.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Diamond: Rais Anajuwa Mambo Mengi Kuliko Mimi Kwenye Muziki

0
0
Kijana huyu akihojiwa na Gadina wa Radio Efm kwenye kipindi cha Ubaoni amesema,Rais amempigia simu juzi na kumuliza saizi ya koti analovaa ili amletee zawadi kutoka Marekani.

Pili amesema wakiongeaga na Rais huwa Rais anajuwa mambo mengi ya muziki huko Amerika kuliko yeye.

Nimejiuliza hivi ni kweli Rais JK anaweza kufanya hivyo ukizingatia majukumu mazito yanayomkabili juu ya taifa na wananchi wake?

Ni kweli Rais JK anajuwa mambo ya burudani na vinavyojiri kwenye ulimwengu wa muziki kuliko Diamond?

Au kijana baada ya kupewa nafasi na Mh. Rais ameanza kujisahau na kuhisi ni saizi yake?

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Vanessa Mdee ndio msanii bora wa kike kwa sasa, Jide kakabidhi kijiti rasmi

0
0
Tukubali tukatae ila msanii wa kike Vanessa Mdee ndiyo queen wa R&B na music wa kizazi kipya East Africa kwa sasa.

Amefanikiwa kuondoa utawala wa Lady Jaydee kwa muda mrefu.

Kwa sasa ndiyo msanii anayepata airplay kuliko wasanii wote East Africa kwenye channel za kimataifa na wimbo wake hatari sana "nobody but me".

Mwana muziki huyu ambae ni mwanasheria kitaaluma music wake na uimbaji wake una standards za kimataifa unaweza kupenya popote

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Mtabiri abaini mambo mazito kwenye maisha ya Lady Jaydee mwaka huu

0
0
Kwa Lady Jaydee, mwaka 2015 utakuwa wenye mafanikio makubwa, ndoa mpya, stress kiasi na magonjwa lukuki, kwa mujibu wa mtabiri!

Mtabiri huyo alialikwa na Lady Jaydee kwenye kipindi chake, Diary ya Lady Jaydee ambapo alidai kuwa mwaka huu muimbaji huyo atapata pesa nyingi kupitia muziki wake lakini kiafya akitabiriwa homa nyingi na kukifiria kifo mara kwa mara.

“Kuna vitu vitaisha mwaka huu ambavyo itabidi uache,” mtabiri huyo alimweleza Jide. “KAwanza hii ni possibility you need to avoid, kuna wakati hali ya kifo itakupa stress sana, unaweza ukasema maisha yangu yatakuaje?

“Usifikirie hivyo, utakuwa unafikiria kifo, utafikiria baada ya kifo nini kinaendelea, utakuwa unafikiria siku nikifa nitaenda peponi au nitaenda motoni, kwahiyo kifo kitakuja kwako lakini usifikirie, kwamba ukiumwa tu kidogo haa nitakufa, no hufi, because ningeona kifo kwenye utabiri wako wa mwaka 2015! Mwaka huu utaumwa kidogo, utaumwa magonjwa, afya yako itakuwa weak sana, kama ungeolewa ingekuwa kama kinga ya kwa mwaka huu, lakini mwaka huu utakuwa na furaha sana kwa sababu ya pesa, kwahiyo kama utakuwa na pesa basi utaishi muda mrefu.

Pia alitabiriwa kufanya vizuri kimuziki ndani ya mwaka 2015-2016 na pia kuolewa na mwanaume maarufu na tajiri.
~Bongo5

Udaku Specially Blog

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Zitto Kabwe Asema Kitendo Cha kuitwa MSALITI Ni Mbinu Zinazotumika Kumuua Mwanasiasa wa Upinzani

0
0
Kiongozi  wa  chama  cha  ACT-Tanzania,Zitto Kabwe  amesema  kuitwa  msaliti  ni  mbinu  zinazotumika 'kumuua' mwanasiasa  wa  upinzani  nchini.

Amesema  mwanasiasa  wa  upinzani  akitakiwa  kuuawa  kisiasa  si  jambo  geni  kusikia  anatuhumiwa  kutumika  na  Usalama  wa  Taifa  au  Pandikizi  la  Chama  cha  Mapinduzi, CCM.

Akizungumza  na  wahariri  wa  vyombo  vya  habari   jijini  Dae  es  Salaam  juzi,Zitto  alisema  kauli  kama  hiyo  ilitumika  kumshusha  kisiasa  mjumbe  wa  kamati  kuu  ya  CHADEMA, Mabere Marando  na  Mwenyekiti  wa  NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

"Si  jambo  jipya, mmesahau  kwamba  Mbatia  aliitwa  pandikizi,leo  Mbatia  yuko  wapi,si  yuko  meza  moja  na  UKAWA?

"Mmesahau  baada  ya  serikali  ya  Umoja  wa  kitaifa  juzi  tu  hapa  kwamba CUF  waliitwa  CCM-B, mmesahau  kwamba  CUF  waliitwa  mashoga, leo  kiko  wapi?

"Mmesahau  Marando  aliitwa  pandikizi, tena  dhidi  ya  Mrema(Mwenyekiti  wa  TLP),leo  Marando  ni  shujaa  na  Mrema  tunamtukana.Hizi ni  siasa  tu  na  zitaendelea  tu," alisema

Aidha  alisema  kuna  watu  wengine  wataibuka  baadaye  nao  wataanza  kulaumiwa, kama  Mwalimu Nyerere  alivyosema.....Ukishakula  Nyama  ya Mtu  Huachi.

Kutokana  na  hali  hiyo  alisema, walioitwa  wasaliti  wametoka  huko  walikokuwa  na  watasikika  wasaliti  wengine  wanaibuka  kwa  sababu  siasa  iko  hivyo..

"Juzi  nimemsikia  Halima Mdee  anasema  mimi  siyo ACT,ninyi  mliwahi  kuandika  kama  Halima  ni  ACT,hiyo  maana  yake  nini,inamaanisha  kuna  presha  anapigwa  huko.

"Angalau  Shibuda  ni  mtu  ambaye  haeleweki  misimamo  yake  ni  nini, lakini  hivi  ni  vitu  vya  kawaida,"alisema.

Akizungumzia  kutumiwa  na  vyombo  vya  usalama,Zitto  alisema  yeye  kama  kiongozi  hawezi  kuacha  kuwasiliana  na  watu  wa  usalama  wa  Taifa.

"Huwezi  kuwa  kiongozi  wa  chama  kikubwa  kinachojiandaa  kushika  dola  usiwe  na  uhusiano  na  Mkuu  wa  Jeshi  la  Polisi,Mkuu  wa  jeshi  la  wananchi  au Mkuu  wa  Usalama  wa  Taifa,utakuwa  ni  kiongozi  wa  ajabu  sana." Alisema

Licha ya Kukatazwa Mgomo wa Madereva wa Mabasi Waanza Rasmi Ubungo

0
0
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba katika stendi ya Ubungo jijini Dar es Salaam kuna mgomo wa madereva waendeshayo mabasi yaendayo mikoani. Mgomo huo umeanza leo kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali. Taarifa zaidi pamoja na picha vitawajia hivi punde.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Askofu Gwajima Awaacha Waumini Wake Njia Panda...

0
0
MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaacha waumini wake njia panda kufuatia kauli yake ya kuwataka wamsindikize Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati jijini Dar, jana alipokwenda kuhojiwa huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwa ametoa tamko la kuzuia waumini hao kukusanyika kituoni hapo.

Gwajima aliyetoa kauli hiyo kwa waumini wake katika ibada ya Jumapili iliyopita kanisani kwake, Kawe jijini Dar, alitarajiwa kufika kituoni hapo kujibu tuhuma za kumtusi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo.

Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao, juzi jijini Dar, baadhi ya waumini wa Gwajima walisema wanashindwa kufanya uamuzi wa kumsindikiza kiongozi huyo kwani jeshi la polisi limesema halitaruhusu mtu kumsindikiza.

“Kusema kweli tumebaki njia panda maana mchungaji amesema twende tumsindikize lakini Kova naye kasema jeshi la polisi litatumia nguvu kuwatawanya watu ambao watakaidi amri hiyo ya jeshi la polisi,” alisema muumini mmoja huku waumini wenzake wakiunga mkono.

Wakati Gwajima alipowataka waumini wake wamsindikize kituoni hapo, Kova alisisitiza kuwa kiongozi huyo wa dini anatakiwa kufika kituoni hapo akiwa na mwanasheria wake pamoja na watu wachache tu wa karibu hivyo kuwafanya waumini wengi wa kanisa la Gwajima kubaki njia panda.

Kupitia video inayomuonesha Gwajima akimtupia maneno makali Pengo, mchungaji huyo wa Ufufuo na Uzima alimtuhumu Pengo kuwa amewasaliti maaskofu wenzake waliotoa tamko la kuipigia kura ya ‘Hapana’ Katiba Inayopendekezwa kwa kile walichodai haikukidhi matakwa ya wananchi.

Askari JKT auawa akisaidiana na Polisi kukabili majambazi

0
0
WATU wawili akiwemo jambazi mmoja na askari mwanafunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamekufa na wengine kunusurika kuuawa katika tukio lililotokea juzi, mjini Mafinga mkoani Iringa wakati majambazi wakirushiana risasi na askari wa Jeshi la Polisi.

Risasi hizo zilipigwa wakati Polisi hao wakijaribu kuokoa fedha za mfanyabiashara Salama Semwaiko zilizoporwa na majambazi wawili waliotumia pikipiki wakati wakifanya uporaji huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mfanyabiashara huyo aliporwa fedha hizo juzi majira ya saa 2.45 asubuhi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda kwenye biashara zake.

Tukio hilo la kusikitisha lililovuta hisia za watu wengi na kufanya baadhi kuzimia wengine kukimbia hovyo na kujifungia ndani kwa ajili ya kuokoa maisha yao lilitokea katika eneo la Kinyanambo B, nje kidogo ya mji wa Mafinga.

Kamanda Mungi alisema; “mfanyabiashara huyo akiwa katika gari lake akielekea kwenye biashara zake mjini Mafinga, mfanyabiashara huyo alisimamishwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa koti jeusi na baada ya kusimama alimtolea silaha na kumtaka atoe fedha na vitu vyote vya thamani alivyokuwa navyo .”

“Baada ya kuona hana msaada mfanyabiashara huyo alijikuta akilazimika kutoa Sh 700,000 alizokuwa nazo, simu ya mkononi na baadaye ilitokea pikipiki ambayo haikufahamika namba za usajili na kumpakia mtu huyo na kuanza kukimbilia eneo la Kinyanambo,” alisema.

Alisema mara baada ya majambazi hao kutoweka, Jeshi la Polisi lilipewa taarifa na kuwahi eneo la tukio na kwa kushirikiana na wananchi walianza kuwakimbiza majambazi hao na ndipo majibizano ya risasi yalipoanza.

Katika hekaheka hiyo, Kamanda Mungi alisema Said Ngudi (25) ambaye ni askari wa JKT Makutupora, Dodoma alipigwa risasi na kufa papo hapo wakati akisaidia kupambana na majambazi hao.

Toa maoni Yako Hapa chini

Picha:Hichi Ndicho Kinaendelea Ubungo, Polisi Walazimika Kutumia Mabomu Kuwatawanya na Kutuliza Vurugu Zinazofanywa na Abiria

0
0
Habari  zilizotufikia zinaarifu Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kufuatia mgomo wa madereva.



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Kamanda wa Mkoa wa Arusha Akanusha Uvumi Ulionea Mitandaoni ya Gaidi Aiyevaa Baibui Kukamatwa na Bomu Mkononi Arusha

0
0
Kamanda wa Mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa mwanaume mmoja aliyevalia vazi la baibui akiwa na bomu mkoani humo

TOA MAONI YAKO HAPA

Alazimishwa Kula Mahindi Mabichi Gunia zima Hadi Yaishe Baada ya Kukutwa Akiiba Mahindi Hayo Shambani

0
0
Jamaa huyu (pichani) alazimishwa kula mahindi mabichi baada ya kukutwa akiiba mahindi hayo shambani huko Bukoba mkoani Kagera. Wamiliki wa shamba hilo baada ya kumkuta akiiba mahindi aliyojaza kwenye gunia, walimuamuru kukaa chini na kuyala yakiwa mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo alikubaliana nacho kwa kuogopa kipondo.
Unaonaje adhabu hii aliyopewa jamaa huyu? inatosha au ulipenda apewe adhabu gani?
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images