Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Viashiria vya Uwezekano wa Kuahirishwa Kwa Uchaguzi Mkuu 2015, Rais Kikwete asiongezewe muda wa Urais - Peter Mziray

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Tanzania Peter Kuga Mziray amesema mwenendo wa Tume ya Uchaguzi kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura hauridhishi na unatoa viashiaria vya uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Tanzania Peter Kuga Mziray amesema mwenendo wa Tume ya Uchaguzi kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura hauridhishi na unatoa viashiaria vya uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba na kuwaongezea muda viongozi waliopo akiwemo Rais Kikwete.
Mziray amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika suala la uboreshaji wa daftari la wapiga kura na upigaji kura ya maoni imeshindwa kufanya kazi yake na hivyo inatakiwa kuachia ngazi mara moja.

Mziray ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha APPT-Maendeleo amesema hayo jana wakati akiwa katika kipindi cha HOT MIX cha EATV ambapo amedai kuwa tume hiyo ilijua tangu zamani kuwa kufikia mwaka huu daftari lilipaswa kuwa limeboreshwa lakini lakini cha kushangaza hadi sasa kazi ya uboreshaji haina matumaini yoyote kama itamalizika kwa wakati.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume, mwezi wa nane mwaka huu ni kipindi cha wagombea kuanza kuchua fomu za urais, sasa itamaliza kazi hiyo lini? Inasema mwezi wa saba lakini hiyo haiwezekani, hii inaweza kuwa ni janja ya kuwaongezea viongozi waliopo muda kwa njia ya kuahirisha uchaguzi” amesema Peter Mziray.

Amesema Baraza la Vyama vya Siasa na chama chake cha APPT – Maendeleo haviko tayari kuona Rais Kikwete akiongezewa muda, jambo la msingi ni viongozi wote wa tume kujiuzulu nafasi zao kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi yao kwa wakati.

Kuhusu hatma ya katiba mpya, amesema kuwa ni vyema serikali ifanyie marekebisho katiba iliyopo ya mwaka 1977 katika maeneo ambayo Kituo cha Demokrasia na Rais Kikwete walikubaliana ambayo ni pamoja na kuwepo tume huru ya Uchaguzi, Matokeo ya uchaguzi wa Rais kupingwa mahakamani na kuwepo kwa mgombea huru .

Toa Maoni yako Hapa Chini

Shamsa: Sijutii Kuachana na Mume Wangu, Nimepitia Mateso Mengi

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford amesema kamwe hatajutia kitendo cha kuachana na  mumewe, Dickson.

Akiongea na gazeti la Amani Shamsa alisema kuwa kipindi chote  wakati yupo kwenye uhusiano na mumewe huyo waliefunga naye ndo ya kimilia alikuwa akiteseka  na kupata shuruba nyingi japo hakuwa tayari kuziweka hadharani.

“Sijutii kuachana na mume wangu, nimepitia mateso mengi, sikotayari kurudi japokuwa nina motto naye” Shamsa alisema.

Kwa sasa inadaiwa Shamsa anatoka na Staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ambaye  naye aliachana na mchumba wake ,Siwema hivi karubuni.

Kajala Atamani Kumlipa Wema Mil.13 Zake ili Kuepuka Masimango ya Kila Siku

$
0
0
Staa  mrembo  wa Bongo Movies, Kajala Masanja  kwa mara ya kwanza  ameibuka  na kutoa ya moyoni kuwa anatamani kulipa shilingi milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake  Wema Sepetu kama faini ili asiende jela miaka saba.

Akizungumza na gazeti la Amani, Kajala  alisema  kuwa huwa anaumia sana kila anapokumbuka kuwa alipewa kiasi hicho chapesa ingawa uwezo wa kulipa anao.

Huwa  nateseka  sana kila ninapokumbuka kuwa nilitolewa 13 japokuwa naaamini alitoka kwa mmoja,kinachoniuma muhusika anaiongelea  kila siku tena kwa mabaya,” alisema Kajala

Toa maoni yako Hapa chini

Faiza Asaka wa Kumpa Penzi, Wanaume Kazi Kwenu

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies,  Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ ametoa kali baada ya kusema kuwa ana hamu ya kumpata mwanaume mwingine wa kumpa raha lakini mpaka sasa hajapata.

Akizungumza na  gazeti la Ijumaa juzikati, Faiza alisema tangu alipoachana na Mheshimiwa Sugu, aliona bora ajitulize lakini sasa anajiona kuna kitu anakikosa na wa kumpa kitu hicho ni mwanaume.

Niseme tu kwamba tangu niachane na Sugu sijakutana na mwanaume mwingine, hebu ‘imagine’ ni muda gani? Sasa nimeshindwa kuvumilia, natafuta wa kunipa raha maana kuna hali flani ikinijia nakuwa kama chizi, swali ni je, nani mwanaume sahihi wa kunipa ‘zawadi’ hiyo? Hapo ndipo mtihani ulipo,” alisema Faiza.

Udaku Specially blog


Toa Maoni yako Hapa Chini

Nuhu Mziwanda na Shilole ni Sikio Lisilo Sikia Dawa..Wachafua Tena watu kwa Picha Zao Chafu mtandaoni

$
0
0
LEO kupitia kwenye kwenye mtandao ule maarufu wa picha nchini, msanii Nuhu mziwanda a.k.a mume mtarajiwa wa mwanadada Shilole ameweke picha hiyo hapo juu ambayo imezua utata mkubwa sana kwa wadau wachache walioiona picha hiyo kwenye mtandao, kabla haijafutwa. Wengi wao wamehoji,
 je kuna umuhimu gani wa kutupia mambo mazito kama hayo kwenye mitandao ya kijamii??

Picha hiyo ilikuwa na maandishi yanayosema

“I’m just hold it tight, my favorite thing on her boy”

Kwanza kabisa kingereza kibovu,  pili picha chafuuu machoni kwa watoto wadogo mtandaoni, why? Why? Why?

Nini maoni yako mdau juu ya picha kama hizi toka kwa wasanii ambao ndio kioo cha jamii?

Udaku Specially blog

Kama Una Kipaji cha Utangazaji wa Redio hii Hapa Kutoka Kwa Millard Ayo inakuhusu

$
0
0
Millard Ayo Ameandika Hivi Katika Ukurasa Wake wa Facebook:

"Najua nina watu wangu wanapenda sana utangazaji.... unapenda kukionesha kipaji chako mbele ya mtu wako ‪#‎millardayo‬ ?!! unaweza kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa UFASAHA? ungependa siku moja uwe sehemu ya timu ya #MillardAyo kwenye ‪#‎Radio‬ na ‪#‎TV‬ ? kaa karibu yangu siku sio nyingi nitakupa njia za kunifikia, usiache kumtag mtu unaeamini anakipaji cha utangazaji wa Radio na TV. ‪#‎TZA‬ ‪#‎POWER101‬ ‪#‎BASE‬'

Udaku Specially blog


Toa Maoni Yako Hapa Chini

Aunt Ezekiel Alia Mimba Kumkosesha 'Madili ya Pesa'

$
0
0
Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel, amesema kwamba anatamani kujifungua, kwani amechoshwa na mimba yake, kwa sababu imemfanya ashindwe kupata kazi ya kucheza filamu nyingine.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana, msanii huyo alisema kuwa mialiko ya kucheza filamu imekata na sasa haingizi kipato chochote, badala yake pesa inatoka, hali ambayo inamfanya atamani ajifungue ili aondokane na adha hiyo.

Siyo siri nimechoshwa na hii mimba, natamani hata leo nijifungue, kwani sipati tena tenda za kwenda kuigiza ambazo huwa zinaniingizia pesa ya kujikimu na sijui lini nitajifungua,” alisema msanii huyo.

Aunt Ezekiel, ambaye aliigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu ya Chozi la Mwanjaa, alisema kwamba anatambua ujauzito ni baraka na kuna watu wanatamani kupata mimba na hawapati, lakini wakati mwingine ni kama adhabu

Udaku Specially Blog


Toa Maoni Yako hapa Chini

Mtanzania Anayetuhumiwa kwa Ugaidi wa Kuuwa Wanafunzi 148 Garissa Kenya Kizimbani

$
0
0
Dar/Dodoma/Nairobi. Mtanzania anayedaiwa kuhusika katika shambulizi la kigaidi lililoua watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa – Kenya, Rashid Charles Mberesero, jana alifikishwa mahakamani na kuwekwa kizuizini kwa mwezi mmoja wakati polisi wakiendelea kukusanya ushahidi dhidi yake.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia anafahamika kwa jina la Rehani Dida alirejeshwa Nairobi kutoka Garissa alikopelekwa awali kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kukiri kujihusisha na kundi la Al- Shabaab.

Mahakama jijini Nairobi ilisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ambaye hakutakiwa kujibu tuhuma hizo na wenzake wanne watalazimika kuwa chini ya uchunguzi mkali wa polisi kwa kipindi cha mwezi mmoja na baadaye wanaweza kusomewa mashtaka ya kuhusika katika shambulizi hilo lililoua watu hao, wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Haikufahamika mara moja sababu za kuamuliwa kuwekwa kizuizini kwa muda huo mbali ya taarifa kueleza kuwa ‘watashikiliwa na polisi tena katika kituo cha siri’.

Mwendesha Mashtaka, Daniel Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mtanzania huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano, alikuwa amepanga safari ya kuelekea Somalia kwa ajili ya kujiunga na makundi ya kigaidi.

Watuhumiwa hao ni kati ya 14 waliotiwa mbaroni hivi karibuni baada ya shambulizi hilo la kigaidi.

Mahakama hiyo pia imewaamuru washukiwa wengine kuendelea kushikiliwa na polisi kwa muda wa siku tano hadi 15.

Awali, Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa polisi walikuwa wakifuatilia kwa karibu uhusiano baina ya wale waliofanya shambulizi hilo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki hoteli mjini Garissa. Inasemekana kuwa watu waliotekeleza shambulio hilo walikuwa wamelala katika hoteli hiyo.


Toa Maoni yako Hapa Chini

Mgomo wa Madereva wa Magari Wasababisha Taabu Kubwa kwa Wasafiri, Angalia Picha Mbali Mbali Hapa

$
0
0
Mgomo  wa  Madereva  umeanza  rasmi  leo  katika  maeneo  mbalimbali   nchini kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali.

Sababu  kubwa  ya  madereva  hao  kugoma  ni  kuishinikiza  serikali  kuweka  mfumo  mzuri  wa  ajira  na  kupinga  kanuni  inayowataka  kurudia  kusoma  katika  chuo  cha  taifa  cha  usafirishaji,NIT  kila  leseni  zao  zinapokwisha  muda. 

Madereva  hao  wanadai  malalamiko  yao  makubwa  ni  kitendo  cha  Serikali  kuongeza  kifungu  kidogo  katika  sheria  mpya  ya  mwaka  2015  namba 31  inayowataka  madereva  wote  wenye  leseni  za  madaraja  E,C1,C2,C3  na  C kurudi  darasani  kila  baada  ya  miaka  mitatu  kuongeza  utaalamu  katika  fani  hiyo  ya  udereva  ili  kupunguza  ajali  za  mara  kwa  mara  zinazotokea. 
 

Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungu huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.

Mgomo Wa Madereva: Serikali Yakubali Kufuta Agizo la Kuwataka Madereva Kwenda kusoma ili Kumaliza Mgomo

$
0
0
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.

Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.

Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.

Attention: Ukioa Mke Msomi Mwenye Kazi Nzuri, Jua Sio Kila Mara Utapewa Mapenzi

$
0
0
Wanawake walioenda shule wakapata kazi ni shida utasikia "leo nimechoka kazi zilikuwa nyingi, niache nilale kidogo" imetoka hiyo, tena utasikia "niache nilale kesho nina presentation" ishatoka hapo kama ndo hamu ilikuzidi, utakoma.

Usiombe ukawa na hamu, yani utatamani uchepuke, kutana na asiye na kazi sasa, kila mda kakutegeshea, unatupia mawe utakavyo, labda zile siku za utaalamu wao.

Jamani wanawake wasomi badilikeni

REVEALED: CHADEMA Yapanga Kupenyeza Mamluki ACT - Wazalendo!

$
0
0
Baada ya Zitto kutoa kauli kwa vyombo vya habari kuwa, kuna zaidi ya wabunge 50 kutoka vyama vya CCM na CHADEMA watakao hamia ACT, CHADEMA kupitia kitengo chake cha intelijensia kimetangaza upelelezi rasmi ili kuweza kuwavumbua wabunge hao wasaliti wa chama na mamluki wengine!

Aidha, maofisa hao katika kitengo hicho cha intelijensia cha CHADEMA wameeleza wazi kuwa wanaifanya kazi hiyo kwa usahihi na umakini mkubwa ili kuhakikisha taarifa watakazokusanya ni za kweli huku wakielezea mkakati wao wa kupenyeza watu wao ndani ya ACT kwa ajili ya taarifa zaidi!

My take,

Kwa hali hii, nadhani CHADEMA imeanza kusahau jukumu lake la msingi la kufanya siasa na kujenga chama, badala yake nguvu nyingi zaidi imeelekezwa kwenye kusaka hao wanaoitwa 'wasaliti'!

Mbona CCM ina watu wanatofautiana kimtazamo lakini maisha ya siasa yanaenda kama kawaida na hatusikii majina majina kama wasaliti?

Sakata la Gwajima: Serikali Inapoamua Kukumaliza Baada ya Kuchanganya Dini na Siasa

$
0
0
Ishu ya Gwajima ni kama ndio imeanza upya baada ya kutakiwa kuleta nyaraka kumi muhimu, zikiwemo returns za hesabu zake za kanisa, bodi ya wadhamini, hati ya usajili wa kanisa, namba ya utambulisho, jumla ya makanisa yake, mali anazimiliki nk 

Kwa juu juu ni rahisi kuona hili ni jambo jepesi lakini kiuhalisia huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa enzi za gwajima. Kila nyaraka atakayoleta itachambuliwa kwa vigezo vyote na kwakweli nyingi ya nyaraka hizo (kama zitakuwepo) zitakuwa na mushkeli

Na mushkeli utakaotokea kwenye kila nyaraka utaangaliwa kwa jicho la kisheria na adhabu zake, hii ni msiba kwa yoyote yule ambaye anafanyiwa ukaguzi na serikali, yataibuka mengi mengi ambayo hayajulikani, kuanzia mamlaka ya mapato, vyeti na usajili, uhamiaji, taratibu za kuendesha kanisa nk nk

Pamoja na kashfa zake nyingi lakini hii ishu ni ya kisiasa zaidi, na hii inatokana kuweka wazi msimamo wake bila woga wa kuwaunga mkono watu wawili muhimu kwenye uchaguzi mkuu ujao Lowassa na Dr Slaa, hawa wawili hawa ni homa mbaya kwa ccm kwasasa, yeyote atakayefanikiwa kuchukua madaraka ni kiama kwa ccm, japo El yupo ccm

Gwajima anaponzwa na kujiamini kulikopitiliza na kuchanganya na siasa za makundi, hawatamuacha hadi wahakikishe wamemmaliza kabisa

TANESCO Yatangaza Mgawo wa Umeme wa Siku Tisa Kutokana na Upungufu wa Nishati hiyo Katika Gridi ya Taifa

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza mgawo wa umeme kwa siku tisa katika baadhi ya maeneo kutokana na upungufu wa nishati hiyo katika Gridi ya Taifa.

Hali hiyo imetokana na maombi ya Kampuni ya Pan African Energy (PAT) inayosimamia uzalishaji wa gesi asilia Songosongo kusimamisha uzalishaji kwa nyakati tofauti ili kufanya matengenezo na kubadilisha baadhi ya vifaa kwenye mitambo yake.

Taarifa ya shirika hilo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana ilisema shughuli hiyo itafanyika kwa siku tofauti kati ya Aprili 6 na Mei 10.

“Hivyo Shirika linawatangazia wateja wake waliounganishwa kwenye mfumo wa gridi ya Taifa kwamba kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo kutokana na matengenezo hayo yanayofanyika kila mwaka,” ilisema.

Tanesco inategemea gesi hiyo kuendesha mitambo yake ya Ubungo 1, Ubungo 2 na Tegeta yenye uwezo wa kufua megawati 245 na kuendesha mitambo mingine ya umeme ya Songas yenye uwezo wa megawati 180.

Taarifa hiyo ilisema pamoja na kutumia vyanzo vingine vya kufua umeme kama maji na mafuta, katika kukabiliana na matengenezo hayo, ukosefu huo wa gesi utaathiri ufuaji wa umeme kwa siku tisa. Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema upungufu huo kwa kila siku utagawanywa kidogokidogo kwenye mikoa iliyopo kwenye gridi na hautaathiri upatikanaji wa umeme kwa mkoa mzima.

Akizungumzia mgawo huo, Meneja wa Mawasiliano Tanesco, Adrian Severin alisema ukiondoa tatizo hilo la ukarabati wa miundombinu ya gesi, shirika lake halina tatizo la kuilazimisha nchi kuingia katika mgawo kwa sasa.

Pia, aliitaja mikoa ambayo haitaathiriwa na mgawo huo kuwa ni Kagera, Ruvuma, Kigoma, Lindi, Mtwara na Wilaya ya Loliondo, Arusha.

CHANZO: Mwananchi

Wema Sepetu Afunguka Kwa Mapana na Marefu Kuhusu Siri ya Utajiri Wake

$
0
0
Live abetter life wengi wetu tumekuwa watu wa kulalamika maisha magumu, hakuna kazi na muda mwingine tunatupa lawama kwa Mungu kwanini amekuumba masikini.

Lakini bila kufikilia kwanini uzaliwe masikini na ukubali kufa masikini? ajira ziko nyingi sana lakini sababu ni ipi wewe ukose? elimu? rushwa? juhudi? au kukata tamaa? Je tangu umeamka leo umfanya kitu gani cha maana cha kukuingizia pesa? 

Iam sure kama upo Kijiweni, Kitandani au umejiachia sehemu ya starehe unapiga picha then unalalamika maisha magumu amka jitume pesa unayo tumia kuweka bando na kusoma umbea.

Uliwahi piga mahesabu kwa week unatumia shilingi ngapi kuweka vocha katika simu yako? na hiyo pesa ukiijumlisha kwa mwezi ni shilingi ngapi? Iam sure ni pesa ambayo inaweza kuwa mtaji wa biashara au mwanzo wa kulipia ada ukasome kozi furani ili uongeze juudi.

Hao matajiri wanaotutengenezea simu na vocha wote walianza na 0 now wako nusu number usilalamike maisha magumu wakati huna juudi yoyote uliyo fanya live a better life tumia vocha yako vizuri je ungependa kuwa kana Wema Sepetu.

Basi jifunze kujaribu kwani hta yeye alijaribu kuwa Miss na hakuwa na mategemeo ya kushinda but leo hii amekuwa tamanio la wengi, always try and never give up hata mimi sikutegemea kama leo hii ningekuwa kipenzi cha wengi but nilijaribu na nikafika.

Usiogope always try # Live abetter life# Be Wema fanya Wema

Diamond Afunguka Kiroho Mbaya Kinachomfanya Ampende Zari, Akanusha Kugombana na Fela

$
0
0
Wakati akihojiwa na Clouds Fm kipindi cha leo Tena alipoulizwa anachopenda zaidi kwa Zari ni kitu gani?

Alifunguka kuwa anachopenda ni tabia ya Zari ya kujielewa. Akaendelea kufunguka Zari anajua kutofautisha maisha yao halisi na maisha ya instagram. Kwani baada ya maisha ya instagram ya mapichapicha anajua kuwekeza kwa ajili ya kesho na ni mshauri wake wa mipango ya kimaendeleo.

Pia anasema anazimia ngozi yake Zari Ile mbaya.

Kasema mtarajie mtoto na atakuja kwenye social media kuwaomba mmchagulie Jina siku zikifika maana huyu ni mtoto wa kitaifa.

Amekataa katakata kusema kati ya Zari na Wema nani anayaweza zaidi licha ya kubananishwa sana na watangazaji.

Pia alitumia nafasi hiyo kukanusha uvumi kuwa kagombana na Fela baada ya kumshauri Fela awanunulie gari Yamoto kwani kasema Yamoto wanajengewa kila mtu nyumba yake kitu ambacho ni kikubwa kuliko gari. So huo uvumi ni wa uongo.

Pia alikanusha kuwa na nyama ya kusindika (beef) na Ommy Dimpoz.

Nb: Mimi nimependa hiyo spirit ya Zari muda wa kazi mnapiga kazi, muda wa mapenzi mapenzi na muda wa kuuza sura mnauza sura.

Ukweli Kuhusu Uvumi Ulionea Juu ya 'Ndoa' ya Zari na Diamond Huu Hapa

$
0
0

Kama wewe ni mmoja kati ya watu waliochukizwa au kuumizwa na taarifa kuhusu ndoa ya mastaa wawili wanao make headline kwa sasa, zarinah hassan aka zari pamoja na mpenzi wake diamond platnumz, taarifa ikufikie kuwa uvumi huo haukuwa kweli, diamond na zari "HAWAJAFUNGA NDOA"

Uvumi huo ulienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, mara baada ya mastaa hao kupiga picha wakiwa wamevaa mavazi ya harusi na kuzitundika kwenye mitandao ya kijamii. 

Taarifa zinasema picha hizo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kuitangaza shoo kubwa ya super star kutoka uganda, ZARINAH HASSAN . Show hiyo inayotambulika kwa jina la CIROC ALL WHITE PARTY ambayo itafanyika kwenye ukumbi mkubwa pale MLIMANI CITY mei moja. 

Zile picha walipiga kwa ajili ya kuitangaza show hiyo kubwa inayotabiriwa kuvunja record kwa kuhudhuriwa na mastaa pamoja na watu mbali mbali mashuhuli.

Mtoto wa Mwisho wa Rais Kikwete Ataka Ubunge B’moyo, Atamba ana Uwezo wa Kuongoza

$
0
0
Makada wawili wa CCM wilayani Bagamoyo,  wameonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo kupambana na mbunge wa sasa, Dk Shukuru Kawambwa.

Makada hao ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Dunda, Yusufu Mrisho Kikwete ambaye ni kitinda mimba wa familia ya Rais Jakaya Kikwete na Abdursharrif Zahoro ambaye  ni mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi  CCM wilayani humo.

Wakati  makada hao wakitangaza nia hiyo  juzi, tayari  mbunge wa jimbo hilo Dk Shukuru Kawambwa  alikwisha tangaza nia ya kutaka kutetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Naye Yusuph Kikwete alisema  ana matumaini makubwa ya kushinda kwa kuwa, amekuwa akiungwa mkono na makundi mbalimbali, wakiwamo vijana ambao wamekuwa wakimshawishi kugombea nafasi hiyo.

 “Ni kweli kuna makundi mengi, yamekuwa yakinishawishi kuingia katika kinyang’anyiro na baada ya kutafakari sana na kujipima kama ilivyo kwa wanasiasa wengine, nimeona siwezi kukataa ushawishi huo, maana kuna watu wameona uwezo wangu  wa kiuongozi,” alisema.

Tishio la ugaidi SAUT - Mwanza: Wanafunzi na Mhadhili watimka huku mtihani ukiendelea

$
0
0
Kutoka chuo kikuu cha SAUT Mwanza, wanafunzi wa shahada ya uzamili katika biashara MBA, walikuwa na mtihani ghafla akaingia kijana wa wa Kisomali, watu wote mbio kila mtu akipitia upenyo ajuao yeye.

Purukushani kwa kwenda mbele, Mhadhili mbio, wanafunzi mbio.Kumbe yule kijana ni mwanafunzi pia ila alikosea Darasa.

Toa Maoni yako Hapa chini

Zitto Kabwe Aanza Vizuri ACT Wazalendo, Afanya Mkutano wa Kwanza Songea, Watu Wafurika Kumsikiliza

$
0
0
Picha Kiongozi wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Z.Kabwe akihutubia umati mkubwa wa wana Songea waliohudhuria kumsikiliza,ikiwa ni ziara yake ya kwanza toka ang'atuke katika chama cha CHADEMA.
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images