Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

PAUL MAKONDA Awa LULU Kinondoni, Wapinzani Wake Wabaki Midomo Wazi

$
0
0
Mtakumbuka kuwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais Jakaya Kikwete afanye uteuzi wa wakuu wa wilaya ambapo katika uteuzi huo, Paul Makonda Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa CCM akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wilaya yenye pilika na vurugu nyingi hapa Tanzania. Wengi walibeza uteuzi huo na wengine wakihoji uwezo wa Makonda mpaka kukabidhiwa wilaya kubwa ya Kinondoni. Viongozi wa vyama vya Upinzani hususan Henry Kilewo wa CHADEMA alianzisha mada humu kwa lengo la kumtisha Makonda kuwa anaingia kwenye wilaya ambayo itakuwa maji shingo kwake.

Kelele za wapinzani dhidi ya makonda zimetokana na jinsi alivyokuwa mahiri alipoteuliwa kuwa mbunge wa bunge maalum la Katiba. Hakika Makonda alionesha ukomavu mkubwa na alitoa michango yenye tija kwa taifa. Aidha, wengine walimbeza Makonda kutokana na msimamo wake wa kumpinga Edward Lowasa pale anapotumia fedha nyingi kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa. Sambamba na hilo, wengine wamemchukia Makonda kwa kuweka bayana msimamo wake wa kutokubaliana na midahalo iliyokuwa inaandaliwa na iliyokuwa tume ya mabadiliko ya Katiba chini ya Joseph Warioba. Tena ilifika wakati Paul Makonda alisingiziwa kuwa amempiga Warioba ilhali ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemnusuru kipigo kutoka kwa wahuni wa CHADEMA ambao waliandaliwa kuvuruga mdahalo huo ili ionekane kuwa ni CCM ndio waliovuruga.

Akiwa amekaa madarakani chini ya miezi miwili tu, Makonda ameonesha kuwa ni mchapa kazi na jasiri mkubwa katika kushughulikia kero zinazowakabili wana Kinondoni. Makonda ameonekana kuwa ni mfanya maamuzi sahihi. Mathalan, ameamua kuwa katika hospitali za Manispaa ya Kinondoni hasa Mwananyamala, Kuwe na Dawati la Polisi ambalo watashughulikia huduma za PF 3 ambazo kabla ya hapo, majeruhi walikuwa wanatakiwa kwenda kwanza kituo cha polisi kupata huduma hiyo kabla ya kwenda hospitali.

Aidha, Hivi karibuni, Paul Makonda ameunda Kamati kushughulikia ujenzi mbovu wa barabara za manispaa ya Kinondoni. Mtakumbuka kuwa Kinondoni inaongoza kwa kuwa na barabara za lami zinazojengwa na kuharibika ndani ya muda mfupi. Barabara za kutoka Kinondoni Biafra hadi Bestbite Namanga, barabara ya Hubert Kairuki na barabara ya Mwanyamala Hospitali ni mfano wa barabara ambazo zimejengwa na kuharibika ndani ya miezi sita tu tangu kukamilika ujenzi.

Kwa haya machache, hata akina Hemry Kilewo ambao walimshambulia kabla hajaaapishwa, leo wamebaki midomo wazi na wamebaki kumshangilia na kumpigia makofu. Hata humu jf, zile mada zilizokuwa zinaanzishwa na BAVICHA za kumshambulia Makonda zimepungua. Hakika Makonda umeonesha mfano mzuri kwa vijana wa hapa nchini. Endelea kuwajibika kwani wana Kinondoni wana imani na wewe.


Hatimaye Mwigizaji SHAMSA FORD Atoboa Kuwa Nay ndio “EndlessLove” Wake

$
0
0
Staa mrembo wa Bongo Movies Shamsa Ford ambae siku za hivi karibuni alikanusha waziwazi alipokuwa akihojiwa na vy mbo mablimbali vya habari juu ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi wa Staa Nay wa Mitego hatimaye jana kupitia ukurasa wake mtandaoni alibandikaa picha yake pamoja na ya Nay ankuandika maneno ya kimahada yaliyosomeka “Miss u so much my endlesslove.”

Kitendo ambacho kinathibitisha kuwa wawili hawa wapo kwenye penzi moto moto

Siku za hivi baribuni zilisambaa picha za wawili hawo wakiwa wanadendeka wadaku wakahisi wa wili hawo wanatoka lakini Shamsa alijitokeza na kusema kuwa hao wapo kwenye project ambayo itatoka hivi karibuni na kusisitiza Nay ni binamu  yake.

Nadhani hapa sasa anataka tuamni kale kamsemo ka binamuu……

Picha za Instagram za watoto wa afisa wa polisi wa Kenya wakila bata na ndege ya jeshi hilo zazua utata!

$
0
0
Picha zilizowekwa Instagram za wasichana wakiwa wamekaa pembeni ya ndege ya polisi iliyokuwa itumike kuwabeba maofisa wa Recce kwenda kukabiliana na shambulio la Garissa zimezua utata nchini Kenya.

Picha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Instagram ya Ndanu Munene Mbithi, anayesemekana kuwa binti wa polisi wa anga wa Kenya, Kamanda Rogers Mbithi.

Picha hizo zinamuonesha Ndanu akiwa na msichana mwingine kwenye matukio tofauti, moja ikiwa ni wiki 10 zilizopita na nyingine wiki 62 zilizopita.

Picha mbili zimeandikiwa maelezo, “Mombasa ni raha tu.” Na nyingine ya msichana akiwa ndani ya ndege hiyo iliyoweka 27 zilizopita imeandikiwa, “Hi Mombasa. #birthdayweekend.”

Akaunti hiyo ya Instagram iliyounganishwa na Twitter na Facebook kwa jina la Ndanu Mbithi imefutwa jana tangia picha hizo ziwekwe hadharani.

Wakenya wenye hasira jana walihoji kuhusiana na matumizi mabaya ya ndege za polisi na kwanini akaunti hizo zilifutwa.

Weekend iliyopita ilibainika kuwa ndege hiyo ya Cessna iliyokuwa iwapeleke makomando wa kikosi cha Recce hadi kwenye chuo kikuu cha Garissa hakupatikana kwakuwa ilikuwa imeenda Mombasa kwa safari binafsi bila ruhusa wa IGP.

IG Joseph Boinet amethibitisha kupokea ripoti inayothibitisha kuwa ndege hiyo haikuwepo kwakuwa ilikuwa Mombasa kupeleka watu. Ndege hiyo iliondoka Nairobi April 2 saa 1.30 asubuhi ikiwa ni masaa mawili baada ya shambulio la kigaidi kwenye chuo kikuu Garissa.

Ndege hiyo ilidaiwa kukodishwa na maafisa wa juu wa polisi kwa mfanyabiashara wa Nairobi kwa maelekezo kutoka kwa Mbithi kwenda kumchukua mke wa mtoto wake.

Afrika Kusini hakukaliki, raia wa kigeni washambuliwa, baadhi wauawa, Malawi kuwaondoa watu wake

$
0
0
Vurugu kubwa zilizoenda sambamba na uporaji mali, zimeibuka jana usiku kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambapo raia wa kigeni wamelengwa.

Baadhi ya watu wameuawa na maelfu kukimbia makazi yao kufuatia kuendelea kwa mashambulio hayo.

Makundi makubwa ya raia wa Afrika Kusini yalikuwa yakizunguka kwenye maduka mbalimbali yanayomilikiwa na wageni na kupora mali. Fujo hizo zinaendelea katika maeneo mbalimbali ya Durban.

Maduka mengi yamechomwa moto licha ya polisi kuongeza nguvu ya ulinzi.

Mwamvita Makamba ni miongoni mwa raia wa kigeni walioathirika na fujo hizo ambapo gari yake ilipigwa risasi.

Wakati huo serikali ya Malawi jana ilisema kuwa itawasaidia raia wake kuondoka nchini humo. Zaidi ya raia 360 wa Malawi wamepoteza makazi yao na kila kitu.

Mrembo Agness Masogange Atimuliwa Sauz Afrika..Kisa Kizima Hichi Hapa

$
0
0
HABARI ikufikie kuwa muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald ‘Masogange’ anadaiwa kutimuliwa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ na sasa amekuwa akionekana Bongo akirandaranda mitaani.

TUJIUNGE JOHANNESBURG
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho Masogange ni rafiki yake aliyeko maeneo ya Midland jijini Johannesburg, Sauzi, staa huyo alitimuliwa na mwenye nyumba baada ya kodi ya pango kwisha na kutakiwa kulipa jambo ambalo lilimshinda.

Ilisemekana kwamba mwanaume aliyekuwa akimpa jeuri aliyetajwa kwa jina maarufu la Said 2010 ambaye ni mfanyabiashara, Mbongo aishie jijini humo alimtosa hivyo bidada akarejea Bongo kinyemela.

KUMBE CHANZO NI TUNDA
Habari nzito zilidai kwamba chanzo cha jamaa huyo ‘kumfungia vioo’ Masogange ni baada ya kunasa kwenye penzi la muuza nyago mwingine wa video za wasanii wa Kibongo aliyetajwa kwa jina maarufu la Tunda.

Ilidaiwa kwamba zile mbwembwe za Masogange za kujitundika mitandaoni zilifika mwisho baada ya Said kuhamia kwa Tunda, mtoto mweupe mwenye sura ya mvuto ambaye anaonekana kwenye video za nyimbo za akina Matonya, TID ‘Mnyama’, Christian Bella na wengine wengi.Ilizidi kunyetishwa kwamba, awali, Tunda alikuwa Bongo lakini jamaa huyo alimtumia tiketi ya ndege na sasa anatanua naye Bondeni kwa Madiba.

UGOMVI
Ubuyu uliendelea kumwagwa kwamba, hivi karibuni Masogange na Tunda waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku wakitukanana mitandaoni bila kuanika sababu ya bifu lao.

“Kama ulikuwa unamfuatilia Masogange wiki mbili hivi zilizopita, utagundua kuna mtu alikuwa anagombana naye. Si mwingine ni huyo Tunda ambaye amemdatisha jamaa hadi akasahau kama kuna Masogange.
“Wewe fikiria, Masogange siyo mtu wa kutua Bongo kimyakimya bila kutupia picha kwenye Instagram ili kuwarusha roho wenzake. Siyo kwamba hawezi, sasa hivi yupo juu ya mawe ndiyo maana anajificha,” kilisema chanzo hicho.

SUALA LA URAIA
Chanzo hicho kilipotonywa kuwa mwaka jana Masogange alitamba kuukwaa uraia wa Sauzi na kuukana wa Bongo kilisema:“Mimi nimeishi hapa South Africa (Sauzi) zaidi ya miaka mitano. Nilishaomba uraia miaka kibao sijapata hadi leo, huyo Masogange ni nani wampe uraia kwa siku mbili? Hizo fiksi tu. Kama aliomba sawa lakini hawezi kupewa uraia kirahisirahisi. Kuna process (taratibu) ndefu hadi mtu apate uraia.

MASOGANGE ATAKWENDA TENA SAUZI?
Chanzo hicho kilizidi kudadavua kuwa siyo kwamba Masogange hatakwenda tena Sauzi kwa sababu ana watu na marafiki kibao nchini humo lakini kwa sasa hana maskani ya kufikia baada ya kutimuliwa.“Anaweza kwenda any time (muda wowote) lakini mpaka awe na uhakika na pa kufikia,” kiliongeza chanzo hicho.

Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Masogange, alipopatikana alisomewa kila kitu ‘eituzedi’ ambapo aliomba chondechonde isiandikwe kwamba ametimuliwa bali yupo Bongo kwa ajili ya mapumziko.
“Jamani si kweli, waambie wahariri nipo huku (Bongo) kwa ajili ya mapumziko tu,” alisema Masogange kwa kifupi.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka juzi Masogange alikamatwa Sauzi kwa msala wa madawa ya kulevya ambapo alihukumiwa kisha akalipa faini na kurejea Bongo kabla ya baadaye kutangaza kupata uraia nchini humo.
GPL

Mke wa Mwanamuziki SHETTA Adai Talaka, Kisa Rose Ndauka

$
0
0
Siku chache baada ya habari ya staa wa Bongo Fleva , Nurdin Bilal ‘Shetta’ kudaiwa kulala chumba kimoja na staa wa Bongo Movies, Rose Ndauka kuandikwa gazetini, mkewe Neila Yusuf ameshindwa kuvumilia na kudai talaka yake, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Shetta na Rose waliripotiwa na “gazeti pendwa”moja kuwa walilala katika chumba kimoja katika Hoteli ya Kingway iliyopo mkoani Morogoro walipokuwa wamekwenda kwenye mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya gazeti hilo kusambaa mtaani na mke wa Shetta kufikishiwa nakala yake na wapenda ‘ubuyu’, kilinuka ile mbaya nyumbani kwa Mbongo Fleva huyo, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke aliamua kudai talaka yake.

Mke huyo wa Shetta ambaye wamebahatika kupata mtoto mmoja na msanii huyo (Kayla) alimjia juu mumewe na kutaka amwambie ukweli wa habari hiyo jambo lililoleta tafrani hadi kufikia hatua ya kutimka nyumbani hadi wazazi wa pande zote mbili wakalazimika kuweka vikao vya usuluhishi.

Licha ya jitihada hizo kutoka kwa wazazi, bado mama Kayla alikataa kusuluhishwa na kudai hasira zake zitashuka mara atakapokutana na Rose uso kwa uso.“Kilinuka kiasi cha mke wa Shetta kufungasha virago huku akisisitiza kwamba kabla ya kuondoka mazima atahakikisha anamfungia kazi Rose ili aweze kumweleza kinaga ubaga juu ya ilikuwaje akapindua na mumewe chumba kimoja,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa  Rose na kuulizwa kama amepata taarifa za kutafutwa na mke wa Shetta na kuhusu kuhusishwa na tukio hilo ambapo alijibu kuwa hajapata taarifa.“Mimi sijapata hizo taarifa, kama ananitafuta mimi nipo tu maana sijafanya kosa lolote. Kama nilivyosema awali, kweli nilisafiri na Shetta kwenda Morogoro na tulilala hoteli moja lakini vyumba tofauti, Shetta namheshimu siwezi kufanya naye jambo kama hilo,” alisema Rose.

 Shetta  kwa upande wake  alipotafutwa ili kujua ukweli wa tukio hilo ambapo alikiri kumtokea na kuwashushia lawama wambeya.“Ni kweli mke wangu amekerwa sana na habari zile, kuna wambeya ndiyo wamemjaza maneno kiasi cha kuleta tafrani hadi wazazi kuingilia kati ingawa mimi naamini haya ni mambo ya kifamilia tu ambayo mke wangu atayaelewa na yataisha tu.

Mke wangu ni muelewa sana, nampenda na ananipenda, hii hali ni ya kawaida kwa wanandoa ila kwa kuwa mimi ni msanii mke wangu atajua tu kuwa watu wanaongea sana juu yetu,” alisema Shetta.

GPL

WEMA SEPETU na PENNY Waingia ‘Chimbo’ Wasema 'Hatutaki Tena Kushabikia Mambo ya Diamond na Zari Hayatuhusu'

$
0
0
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema  Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona habari za mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zarinah Hassan zinapamba moto kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la project.

Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga kazi badala ya kupoteza muda.

Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki tena kushabikia mambo ya Zari na Diamond kwa sababu hayatuhusu,” alisema.

Zitto Kabwe: Sitaki kulumbana na CHADEMA, Nawaheshimu Sana na Siasa za Chuki zimepitwa na Wakati

$
0
0
Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hawezi kulumbana na viongozi wa chama chake cha zamani cha Chadema kwa kuwa anachofanya sasa ni kutafuta wanachama wa chama chake kipya.

Zitto alisema hayo juzi mjini Morogoro wakati wa mkutano wa ziara ya uzinduzi wa chama hicho uliofanyika katika kiwanja cha ndege mjini hapa.

Akihutubia huku akishangiliwa na wananchi, Zitto aliwataka kumpima na kumchuja yeye kwa matendo yake na kwamba kwa sasa jitihada zake amezielekeza mikoani kupata wanachama.

Nimekuwa nikisikia maneno maneno mengi kutoka kwa viongozi wangu wa zamani lakini nawaheshimu na sitoweza kuwajibu kwani siasa za chuki kwa sasa zimepitwa na wakati, ninachofanya ni kukijenga chama,”alisema Zitto.

Kiongozi huyo alisema Morogoro ni moja ya mkoa unayoifanya nchi kukosa maendeleo kutokana na viwanda vingi kubinafsishwa na hivyo kutokuwa na faida kwa wananchi.

Morogoro ni mkoa wa sita katika kuchangia pato la Taifa na takribani Sh2.2 trilioni zimekuwa zikipatikana kwa ajili ya maendeleo ya watu wa mkoa huo,” alisema Zitto.

Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira aliwataka wanawake nchini kuacha kushiriki siasa za vurugu na malumbano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mghwira alisema ni vyema wakaangalia namna gani nchi inakua kiuchumi na watoto na vijana wanapata elimu iliyo bora ambayo itawafanya kufanya kazi kwa uzalendo.

Aliwataka wananchi kuwa na taratibu za kuwakumbuka mashujaa wa Taifa hasa kwa mambo mema na mzuri waliyoyafanya wakati wa uhai wao.

Mpaka sasa chama hicho cha ACT kimefanya mikutano yake ya uzinduzi katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa na Morogoro na Dodoma .

Nape awajibu wanaoishinikiza CCM itoe ratiba ya uchaguzi

$
0
0
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema chama hicho hakitaendeshwa kwa mashinikizo ya watu wanaotaka kitangaze haraka ratiba ya uteuzi wa wagombea wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Kauli ya Nape imekuja baada ya baadhi ya makada wa chama hicho kuhoji inakuwaje CCM kinachelewa kutoa ratiba ya mchakato wa uchaguzi, wakati muda unasonga.

Aprili 6 mwaka huu, akaunti ya mtandao wa Twitter iliyosajiliwa kwa jina la Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), Hamis Kagasheki, ulihoji “CCM ni chama cha wanachama wote. Hii ni Aprili hakuna ratiba au utaratibu wa wanachama kumpata mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama. Kulikoni?”

Kagasheki mwenyewe hakupatikana kuzungumzia ujumbe huo, baada ya simu yake ya mkononi kuuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe wa simu hakujibu.

Mbali na Kagasheki, makada kadhaa wa chama hicho pia wamekuwa wakihoji mantiki ya chama hicho kuzuia watu wasitangaze nia kabla ya wakati.

Majibu ya Nape
Nape alisema vikao vya chama ndivyo vitakavyoamua mchakato huo uanze lini, lakini CCM haina historia ya kuwahi wala kuchelewa.
 
CCM mara nyingi huandaa ratiba yake kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec). Hao wanaotaka kuharakisha mambo wajaribu kupitia mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010, CCM ilitangaza uteuzi muda gani. Kwanini safari hii wanatia presha?” alihoji.

Mapema mwezi uliopita Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa alipozungumza na wajumbe wa halmashauri ya Jimbo la Same Magharibi wakati akishiriki na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, alisema uteuzi wa wagombea wa udiwani, ubunge na Urais utafanyika Juni.

Lakini Nape juzi alisema hata hiyo Juni iliyotangazwa awali na Kinana haijapitishwa na chama, hivyo bado tarehe rasmi ya uteuzi haijatolewa.

Mwaka 2010, ratiba ya uteuzi wa wagombea katika chama hicho tawala ilitangazwa mwanzoni mwa Juni na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa

Please Help, My Husband Is Drinking My Menstrual Blood + Urine

$
0
0
Greetings Admin, please don't disclose my identity.

Am a 30 year old lady within Warri and am married to a rich man who runs most of the big shops in town. I have been with this man for the past 3 years now but I have a big problem that needs serious help.

My husband from the time he came back from Tanzania last year he started drinking my menstrual blood and urine, he told me that I should remind him every time when am attending so that I should let him suck the blood.

The first day he did this it was on a night when he wanted to have s£x with me and discovered that I was on my periods, he told me not to worry coz that's what he wanted.

I really need help dont know what to do coz every time he does that I usually feel dizzy and sleepy. Ive been wanting to tell my friends but am scared I suspect my hubby is using me into rituals what can I do coz I dont want to lose him..he helps my family.

This is K-Lyinn Boutique in Dubai….Money Talks

$
0
0
This is K-Lyinn Boutique in Dubai….Money Talks
She is Really The number one Boss Lady in East and Central Africa.
Any Comment ?



Photos: Zari Shows off Her Million Dollar Bed with HER sons on It

$
0
0
She Captioned the Pic as Below:
I Thank you God everyday..... Been kicked out of ma bed tonight that it's warm n cozy.... Love you soldiers-ZARI

ZITTO: Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Ushirikiano wa vyama

$
0
0
Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Ushirikiano wa vyama

Kumekuwa na shauku ya wananchi kwa sisi kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo yetu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo ...wa uchumi unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa

1 tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu ALLIANCE na Msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba.

2 tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi.

3 hatuna shida na Tupo tayari kushirikiana na chama chochote kilicho tayari kushirikiana na sisi ikiwemo UKAWA ili kuunganisha nguvu kuitoa CCM kwa malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.

ACT Wazalendo haijatoa kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu. Bali tumeweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano. Tupo tayari kwa UMOJA. UMOJA ni moja ya misingi mikuu 10 ya chama Chetu na Umoja ni nguvu.
Tupo tayari

Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo

UNCONFIRMED:Kauli ya Al-Shabaab Kuhusu Kuishambulia Tanzania

$
0
0
Taarifa kutoka redio YARAT FM ya Somalia leo saa mbili asubuhi kwenye kipindi cha MAKHAR TWALLIB:

Mkuu wa kikundi cha Al - Shabaab leo asubuhi wakati akihojiwa juu ya taarifa zilizoenea kwamba wana mpango wa kuvamia Tanzania amesema haya yafuatayo;

Kamwe hawajawahi kufikiria kushambulia, Tanzania Kwa sababu hawana sababu ya kufanya
hivo!

Amesema kwamba mbali ya kuzingatia kuwa, Tanzania kuna waislam wengi, bali pia wanajua na kutambua msaada wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1995 alipotoa msaada wa tani 500,000 za Mahindi kipindi nchi hiyo ina janga la njaa. Hivyo hawawezi kulipa unyama huo kwa marehemu baba wa taifa.

Pia kiongozi huyo aliongeza kuwa Tanzania haijapeleka jeshi lake Somalia yenyewe nchi kama nchi, tofauti na Kenya na Uganda.

Wanajeshi wachache Watanzania walioko Somalia ni katika jeshi la AU, na sio Kwa amri ya Tanzania.

Kiongozi huyo pia katoa pole katika muda wa siku mbili ambao Watanzania hususani wanachuo waliokuwa katika hali ya sintofahamu na pia vyombo vya usalama ambavyo vililazimika kuimarisha ulinzi katika sehemu nyeti mbalimbali.

Kiongozi huyo kamaliza kwa kusema kwamba wao wanazingatia msemo wa Quran kwamba, "Fight those who fight you, spare those who don't fight you''

Kutoka Mogadishu ni mimi,

Professor kilaza

Hali ya Mke wa Mwanamuziki Mabeste Yazidi Kuwa Mbaya..Mabeste Afunguka Yote na Kuomba Msaada wa Hali na Mali

$
0
0
Mwanamuziki Mabeste amefunguka kirefu juu ya ugonjwa unao msumbua Mkewe toka Ajifungue mwaka 2013 mpaka sasa ...Inasikitisha sana jisomee mwenyewe hapo chini :

"Hii ni kwa waTanzania wenzangu, ndugu zangu na fans wote wa Mabeste!! Watu husema mficha maradhi kifo humuumbua!! Mke wangu anaumwa mda mref tangia ana ujauzito wa mtoto wetu (kendrick) alikua akisumbuliwa na moyo unakua unamuuma, pumzi zinabana! Na alikua anazimia zimia mara kwa mara! Hospital wakasema itakua ni ujauzito unamsumbua!! Na alikua akipimwa pressure inakua low! Mungu alimlinda akajifungua salama mwez wa 7/2013!

 Lakini ile hali ilizidi kuendelea hata baada ya kujifungua!! Anabanwa pumz, nguvu zinamuishia, moyo unamuenda mbio hata kupelekea kupoteza faham mara kwa mara!! Alikua sometimes anakaa sawa kwa mda mchache kama three weeks ama two kisha inajirudia! Hospital wakawa wanampa bed rest na matibabu kiasi!! Mimi ni mkristo mwenye imani na MUNGU! So nikawa nampeleka hospital na kanisani kufanya maombi! Tumefanya hivyo kwa mda mrefu! Ilibidi niache kaz zangu kipindi ambacho nilitoa (NISHAURI Audio from Am Records) na hata wakat nimepishana na Management yangu ya zamani (Bhits) hata pale wife alikua mgonjwa na studio nilikua sijaenda kwa mda wa miezi mitatu! Nilikua home tu nauguza! kabla ya mapishano kutokea!

 Na hata ile day nimeenda na wife kwa interview XXL pale pia wife alikua mgonjwa ila alijikaza tu! So kuumwa kwa wife kumefanya nisimame hadi kazi zangu! Ndo maana hata baada ya mapishano btn mm na bhits hamkuendelea kumsikia Mabeste! Niliendelea kuuguza kipindi chote cha 2013 mpaka mwaka jana mwishoni 2014!! Ambapo wife alipata nafuu kwa kiasi ambacho nilidhani yamekwisha sasa naeza rudi kazini! January 2015 nikatangaza kurudi rasmi mzigoni na nikaachia (USIWE BUBU) nilipanga ku fight niachie Usiwe bubu video February, bahati mbaya hali ya wife ikajirudia na ikawa mbaya zaidi ya mwanzo...so ikanibid nitangaze tena rasmi kusimama kazi zangu ili fans wangu msije mkanichukulia vbaya!

Wife wangu kwa sasa ni bado ni mgonjwa sana anahitaji usimamiz wa karibu zaidi haswa kutoka kwangu! Nimempeleka agha khan hosp...akafanyiwa vipimo, wakani hamishia muhimbili kwa ajili ya Ct Scan, ili waangalie kwa ubongo kama una uvimbe au damu imevujia! after CT SCAN ma Dr. Wame suggest apimwe M.R.I kwa vile ana symptoms zote za mtu anayekaribia kupata (STROKE) vile vile imegundulika pia psychological ameshakua affected kutokana na stress za mda mrefu, too much thinking etc. So ameshakua affected hadi imekuja physically anakua anakakamaa mwili! Kiukweli she went through a very hard time kwa kuumwa na mawazo zaidi maana tangu amzae mwanetu Kendrick hajapata malezi ya mama! Vile haezi m take care vizuri wkt yeye anaumwa! Kwa sasa bado Tunaendelea na vipimo na matibabu mpaka atakapo maliza vipimo na kupatiwa matibabu! Tatizo nililo nalo!! Nimekaa home mda mrefu sana miaka miwili na nusu sasa bila kufanya kazi kwa ajili ya kuuguza! Maana hali ya wife nilikua siwez kumuacha na mschana wa kazi au mdogo wangu ambao naishi nao coz hawaezi mhandle wife incase lolote likitokea! Na mda wote huo nimekua niko nae kwa ukaribu sana hata kama natoka issue ya muhim na yy yuko sawa kias basi atajikaza tuta toka wote! Hiii imepelekea Mabeste kutoskika kimziki! Kusimama kwa biashara zangu,kumaliza pesa zangu zote Bank!! Maana ilikua pesa zinatumika bila kuingia! Kwa matibabu na basic needs za daily life! Coz nna wadogo zangu pia nawalea! Hapa nilipofikia naomba msaada wenu ili niweze kumtibia my wife! Coz bado anahitaji kuendelea na matibabu na vipimo! Naamini MUNGU mwema Atamponya lakini kwa sasa Nimekwama kuendeleza matibabu vile for two years na nusu nilikua natumia pesa tu bila kuingiza! So kwa yeyote atakaye guswa Tgo pesa 0715032472 jina la usajiri William V. NGOWI 

SPECIAL THANKS TO
@nchakalih @vanessamdee @manecky_amrec
@bobmanecky @officialbriantz @likudaz @clowtz @djmafuvu @adamjuma ( Aj) @adolphghika @castolocavana @kennedyEATV
na kama kuna nilie msahau thanks saaana kwa support yenu hadi hapa nilipofikia MUNGU AWABARIKI"


Watu 9 wakamatwa Msikitini wakiwa na vifaa vya mlipuko, Sare za Jeshi, Majambia na vifaa vya Kuficha Nyuso

$
0
0
Watu 9 wamekamatwa wakiwa wamejifungia kwenye msikiti wa Soni Morogoro wakiwa na vifaa vya milipuko hatari! Watu hao ni watanzania 

Katika purukushani hizo polisi mmoja amenusurika kuuawa baada ya kukatwa na jambia shingoni.


Kajala Awaongoza Mastaa Kumtuliza Wema

$
0
0
Kufuatia kauli ya Wema Sepetu ya hivi karibuni kuwa hawezi kupata mtoto wa kumzaa, mastaa wa fani mbalimbali wamejitokeza kumtuliza moyo, wakiongozwa na hasimu wake wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema hana sababu ya kukata tamaa, kwani bado ni mdogo.

Akizungumza na na gazeti la Risasi Mchanganyiko baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia tatizo alilonalo.

“Namuombea sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini,  roho inaniuma sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge. Na watu waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na kumtunza kama wake.

“Naomba achukue mfano wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa watoto, natumia mguu wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila kitu kasoro mtoto, atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa kwake na hapo machungu, huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa kwake,” alisema Wastara Juma.

Wengine waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha ambaye alisema;

“Mtoto siyo mwisho wa maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto na wanaishi kwa amani kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo ishu kubwa kihivyo, watu waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina mpango wa kuwa na mtoto.”

Dawa ni Kuacha Ngono, Mayai ya Kware Hayatibu UKIMWI

$
0
0
Hivi karibuni nilikuwa Dar es salaam kwa likizo fupi, nikashangaa mtaani kwetu, msiniulize maeneo gani, nilikuta wakaazi wengi waliokuwa wakifuga kuku wa mayai au wa nyama wamebadili biashara na sasa wanafuga ndege aina ya Kware na wanauza mayai yake kam njugu.

Nilipodadisi niliambiwa yanatumiwa na waathirika wa ugnjwa wa UKIMWI maana wameambiwa na wataalmu wetu kwamba mayai ya Kware yanatibu UKIMWI.

Nilishangaa zaidi kusiki eti dozi yake ni mayai matano kwa siku kila siku na baada ya kutumia kwa miezi mitatu mgonjwa anapona kabisa. Si hivyo tu nikasikia madai mengine kwamba hayo mayai ya Kware yanatibu pia ugonjwa wa Kansa.

Napenda kuwausia Watanzania wenzangu kwamba dawa ni kuacha ngono, mayai ya Kware hayatibu UKIMWI

Wanawake wa Stahili Hii, Wanakera Mno

$
0
0
Mwanamke nimemtongoza kanikubalia, nikamuomba mzigo kanibania, alafu muda mwingi anaokutana na mimi anakifanya ana haraka muda mwingi utamsikia akisema 'nataka kuondoka lakini nina haraka' as if mmekutana bahati mbaya.

Basi unapozidi kumbembeleza, we unaongea naye ye yuko busy anachat kwa text na watu wengine na ninapojitahdi kutaka kugundua anachat na nani, ndivyo simu yake anaiweka mbali na upeo wa macho yangu.

Mara nyingi mimi ndo wa kwanza kumshtua kene simu kila siku, nisipofanya hivo siku inapita na ninapomuulza kama ananipenda anajibu ananipenda. Naomba mnisaidie huyu binti ananipenda kweli? Au yupo kimaslah zaidi?

Ushauri kwa mabinti kama mwanaume huwezi kumpenda au haujakidhi vigezo vyako, mtose siku ileile ya kwanza sio kukubal Kinafiki.

Ukweli wa Taarifa zinazoenea Kuwa Mwanamuziki HUSSEIN MACHOZI Amefariki Dunia Huu Hapa

$
0
0
Hizi Habari zinazoenea Kuwa Hussein Machoz amefariki sio za Kweli Hussein amekanusha....
Taarifa za Kizushi zimefanya mama yake mzazi akazimia na Dada yake kukimbizwa Hospitali kwa Mshtuko.... PINGA USAMBAZAJI WA HABARI KIPUUZI BILA KUTHIBITISHA....

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images