Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Habari zaidi Kuhusu Watu 9 Waliokamatwa Msikitini na Silaha, Milipuko, Majambia na Bendera ya Al Shaabab Morogoro

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limekamata watu 9 wakiwa na silaha za kulipua na nguo za jeshi la wananchi wakiwa wamejifungia katika msikiti wa Suni Kidatu wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema tukio la kukamatwa kwa watu hao limekuja kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu ambapo jambazi mmoja aliruka katika bajaji na kisha kumjeruhi askari shingoni ambapo wananchi wenye hasira kali walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza jambazi huyo akiwa na silaha na kisha kumchoma .

Kamanda Paul amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliongeza nguvu ya askari ambapo walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wakiwa katika msikiti wa Suni Kidatu na baada ya kupekuliwa wamekutwa na vifaa vya milipuko nguo za kijeshi la wananchi wanaendelea kuwashikilia watuhumiwa na kuna taarifa kuwa watuhumiwa hao walijiandaa kufanya tukio la uhalifu .

Aidha kamanda paul amewashukuru wananchi wa ruhembe kidatu wilayani kilomeroa mbao wametoa ushikiano kufanikisha kukamtw akwa watuhumiwa hao.

Huwezi Amini Ajali za Barabarani Zaua WATU 969 Ndani ya Siku 102

$
0
0
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiungana na Watanzania kuomboleza vifo vya watu 19 walioteketea katika ajali ya basi lililoungua moto baada ya kugongana na lori juzi mjini Morogoro, imefahamika kuwa, ajali za barabarani zimegharimu maisha ya watu 969 kati ya Januari Mosi na Aprili 12 mwaka huu.

Aidha, watu 2,500 wamejeruhiwa katika kipindi hicho, wengine wakisababishiwa ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizo. Hii ina maana kwamba, kwa wastani, watu 10 walipoteza maisha katika ajali za barabarani kila siku kati ya Januari na Aprili 12 mwaka huu, ilhali waliojeruhiwa ni wastani wa watu 25 katika muda kama huo.

Hayo yalibainishwa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mohammed Mpinga aliyesema hayo yametokea katika ajali za barabarani 2,224 za kati ya Januari na mwanzoni mwa Aprili.

Alisema watu 866 walikufa na wengine 2,363 kujeruhiwa kati ya Januari na Machi, wakati wengine 103 wamepoteza maisha na 138 kujeruhiwa kati ya Machi 11 na Aprili 12 mwaka huu.

Alisema katika ajali zote hizi chanzo kikubwa ni mwendokasi wa madereva bila kuzingatia alama na michoro ya barabarani na abiria kushabikia mwendo kasi na kumtetea dereva pindi anapofanya makosa.

“Dereva akifanya makosa akikamatwa abiria wanachangia kumlipia faini dereva jambo ambalo linawapa madereva kiburi wakiamini akifanya makosa abiria wanamsaidia,” alisema Mpinga.

Aliongeza kuwa kwa upande mwingine wamiliki wa vyombo vya usafiri wanachangia ajali kwani wamekuwa wakiwadhibiti na kuwaamrisha madereva wao kwenda mwendo kasi na pale anapokosea anamlipia faini jambo ambalo linapelekea kutokea kwa ajali zinazopoteza maisha ya watu wengi na kuwaachia wengine vilema vya maisha.

Alisema pia tabia binafsi za madereva kuendesha kwa ubabe barabarani pindi wanapokutana na magari madogo, kitendo alichosema si sahihi kisheria na linaweza kusababisha ajali hivyo ni vyema kila mmoja kumheshimu mwenzake na kufuata sheria.

Pia alisema jambo lingine linalosababisha ajali za barabarani ni matumizi ya dawa za kulevya na ulevi mambo ambayo humfanya dereva kuchoka na matokeo yake kusababisha ajali.

Aidha aliwataka madereva kuwa na tahadhari wanapoendesha hususani vipindi vya mvua, akiwahimiza kuwa waangalifu na kuzingatia michoro na alama za barabarani na abiria kutoa taarifa za madereva wanaokwenda kinyume na sheria za barabarani. JK atuma salamu Wakati Mpinga akianika takwimu hizo,

Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe kuomboleza vifo vya watu 19 na wengine 11 waliojeruhiwa katika ajali ya basi na lori iliyotokea mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Msimba kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Mbeya, kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha abiria hao 18 kuungua vibaya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua vibaya.

“Huu ni msiba mkubwa kwa Taifa, hivyo nakutumia salamu zangu za rambirambi, na kupitia kwako naomba salamu zangu za rambirambi na pole nyingi ziwafikie pia wanafamilia, ndugu na jamaa waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo.

Namuomba Mola awape moyo wa uvumilivu na subira watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo mbaya.

Vilevile namuomba Mola awawezeshe majeruhi wote wa ajali hiyo kupona haraka, ili warejee katika hali yao ya kawaida na kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao,” aliongeza kusema Rais Kikwete.

Majibu ya DNA Test Aliyoifanya NAY WA MITEGO Kubaini Kama Mtoto Aliyezaa na SIWEMA ni Wake Ama Laa Yametoka..Majibu Haya Hapa

$
0
0
Baada ya utata mzito kutawala kwenye vyombo vya habari juu ya uhalali wa mtoto wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mzazi mwenzake Siwema Edson, hatimaye kipimo cha vinasaba (DNA) kimetoka na kumaliza ubishi kwamba mtoto huyo aitwaye Curtis ni damu halisi ya msanii huyo.

Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana, waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.

Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na sakata hilo.

“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.

“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi tena.

“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.

Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazi.

Mkwara wa Gwajima kwa Polisi wazaa matunda.....Mahojiano Yasitishwa Kusubiri Uamuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

$
0
0
Hoja za kisheria alizowasilisha Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu kutakiwa kuwasilisha nyaraka 10 za utajiri na usajili wa kanisa lake polisi zimezaa matunda.

Sasa, agizo la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam la kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka hizo leo limesitishwa kusubiri utatuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.

Wakili John Mallya anayemtetea Askofu Gwajima alimweleza mwandishi jana usiku kuwa baada ya makubaliano na polisi mteja wake leo hatafika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kama ilivyokuwa imepangwa mpaka hoja hizo za kisheria zitakapotolewa uamuzi.

Alhamisi iliyopita, polisi ilimtaka Gwajima kuwasilisha vielelezo hivyo, lakini hatua hiyo ilipingwa na kiongozi huyo akieleza kuwa hatapeleka nyaraka yoyote iwapo jeshi hilo halitajibu barua aliyoliandikia kutaka liombe vitu hivyo kwa maandishi.

Nyaraka zilizotakiwa kuwasilishwa polisi ni hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la Wadhamini (Baraza la Kiroho), idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia na nyaraka za helikopta ya kanisa.

Nyaraka nyingine ni; muundo wa uongozi wa kanisa, waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za kanisa, nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari na kuambatana na mtu anayepiga picha za video kanisani hapo.

Siwezi kuwasilisha kwa mdomo kwa kuwa hizi si mali za Gwajima… ni mali ya taasisi na si vitu vyake binafsi,” alisema wakili huyo.

Katika barua yake kwa polisi, Wakili Mallya alisema: “Tunaiomba Polisi kumwandikia rasmi mteja wetu kimaandishi nyaraka mnazozihitaji na vifungu vya sheria vinavyotumika na polisi kutaka nyaraka hizo… tutashukuru kupata hati hiyo.”

Kauli ya Kova
Mapema alipoulizwa kuhusu kitakachotokea leo, Kamanda Kova alisema: “Suala la Mchungaji Gwajima kwenda na vielelezo alivyoagizwa na Polisi siwezi kulizungumzia hadi hapo itakapotokea hakuja navyo ndipo nitakapotoa tamko langu la mwisho.

Nitazungumziaje hili? Si hadi itokee hakuja na vielelezo na kama akija navyo halafu mimi nimeongea tofauti, nimeona italeta malumbano kati yangu na yeye na mimi sitaki ifikie huko.

Kuna mambo mengi ya kufanya hivyo nitalitolea tamko la mwisho kwa waandishi wa habari kuhusu mchungaji Gwajima kama itatokea hivyo ili tuendelee na mambo mengine.”
 
Kwa msisitizo zaidi
Mallya alisema nchi inaongozwa kwa sheria, hivyo kila kitu kinatakiwa kiwe cha kisheria na kwamba wameiandikia polisi kuitaka waombe nyaraka hizo kimaandishi na kuonyesha vifungu vya sheria vinavyowaongoza kuziomba badala ya kusema kwa mdomo kwa sababu vitu hivyo ni vya kanisa na siyo vya Gwajima peke yake.

Askofu Gwajima alihojiwa na Polisi, Kanda ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kumtolea maneno makali Polycarp Kardinali Pengo baada ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kutoa tamko lililotofautiana na la viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu suala la Katiba.

WEMA SEPETU: Kumuimba Msichana Uliyeachana naye ni USHAMBA wa Mapenzi

$
0
0
Staa wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.

Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.

Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo, ambao wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

Here is why VERA SIDIKA is Being Roasted on Social Media

$
0
0

Vera Sidika shared this photo of former Miss Tanzania, K-Lynn, who had just walked down the aisle with her old lover, Renigald Mengi, a Tanzanian tycoon.

This did not go down well with her fans who felt that she was supporting relationships between young girls and older men.


Do you think Vera has a point?

Mwanaume Kutoka Uganda Alie Wahi Kutoka Kimapenzi na Zari Afungu, Adai Zari Alichoropoa Mimba zake Mbili

$
0
0
Hasira ya kibuti? Ubuyu kutoka nyumba ya jirani, Kampala nchini Uganda unaeleza kuwa mwanaume Farouk Sempala aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameibuka na madai mazito kuwa mwanamama huyo alichoropoa mimba zake zaidi ya mbili.

TUJIUNGE UGANDA
Katika mahojiano maalum na Gazeti la Red Pepper la nchini humo hivi karibuni, Sempala alifunguka kuwa alishtushwa na habari kuwa mwanadada huyo alikutana na Diamond kwenye ndege na kuanza projekti ambayo matokeo yake ni mimba.

MIMBA ZAIDI YA 2
Jamaa huyo alidai kuwa, wakati akiwa kwenye mapenzi na Zari baada ya mwanamama huyo kutengana na mumewe, Ivan Semwanga, alitoa mimba zake zaidi ya mbili hivyo anaamini kuwa hata hiyo ya Diamond anaweza kuichoropoa.Sempala alisema kuwa katika kipindi cha mapenzi yao, walikuwa hawatumii kinga hivyo Zari alikuwa akinasa mimba lakini akawa anachoropoa.

AANIKA SIRI ZA NDANI
“Tulifanya ngono laivu tena mara nyingi tu bila kinga.
“Katika kufanya hivyo nilimpa mimba siyo mara moja wala mbili lakini alikuwa akizichoropoa.
“Kamwe Zari hakunipenda. Alichotaka ni kumuonesha tu Ivan (aliyekuwa mume wa Zari) kwamba alikuwa amepata mwanaume mwenye misuli,” alianika siri zao Sempala katika gazeti hilo.

AMECHUKUA HATUA GANI?
Alipoulizwa juu ya hatua alizochukua au anazotarajia kuzichukua kwa Zari, Sempala alisema hakuna hatua atakayochukua lakini ameamua kusema juu ya uchoropoaji huo wa mimba akiwa na wasiwasi kuwa huenda hata hiyo ya Diamond ataichoropoa hivyo achukue tahadhari.

GUMZO
Habari kutoka kwa chanzo chetu chenye maskani yake Chuo Kikuu cha Kampala (Kiu) nchini Uganda kililitonya Amani kwamba, baada ya habari hiyo kuingia mitaani iligeuka gumzo kubwa huku wengi wakieleza kuwa huenda Sempala ameamua kumchafua Zari kwa sababu mwanamama huyo alimpiga kibuti cha kihistoria.
“Yaani gumzo hapa Kampala ni habari hiyo ambayo imetoka kwa ukubwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti.
“Unajua huyu Sempala bado kiroho kinamuuma. Kinachoonekana anatapatapa kwa sababu Zari alimpiga kibuti kibaya na cha ghafla kisha akanasa kwa Diamond,” kilisema chanzo hicho.


SEMPALA ACHUKIA UHUSIANO WA ZARI, DIAMOND
Kati ya watu wa mwanzo walioponda uhusiano wa Zari na Diamond ni Sempala ambaye alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema kwamba hapendezwi kabisa na pea ya wawili hao.
Habari zilieleza kwamba Sempala ambaye anasifika kwa dili za mjini, anaonekana kutokuwa katika hali ya kawaida tangu alipopigwa chini na Zari mwaka jana hivyo kuchukuliwa kama anasema chochote kutokana na kuchanganyikiwa.

ZARI YUPO SAUZI
Juhudi za kumpata Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akitarajia kupata wa nne, aliyeko nchini Afrika Kusini ’Sauzi’ ili kusikia upande wake juu ya sakata hilo, ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.
Diamond alipotafutwa na kunyetishiwa ishu hiyo alisema kuwa hana la kusema na hawezi kushindana na midomo ya watu.

Linah: Wasanii wa Bongo Wakiweka Picha Mtandaoni na Kuvaa Kama hivi Wanapondwa ila Picha Kama Hiyo Akiweka Rihanna Wanamsifia

$
0
0
Msanii Linah anasema wasanii wa bongo wakiweka picha kwenye mitandao ya jamii wanapondwa,picha hiyo hiyo akiweka Rihanna anasifiwa kisha akamalizia kwa kusema Tusupport wa nyumbani.

Wewe unalipi la kushauri hapa?

Bongo Fuse:Bikira wa Kisukuma Afunguka Ugomvi wake na Lemutuz, Umaarufu Wake Mitandaoni na Sheria Mpya ya Mitandao

$
0
0
Seth de  Jesus Giovanni Aka Bikira wa Kisukuma Kama Anavyofahamika kwenye ukurasa wa Instagram Amefunguka mengi kuhusu umaarufu wake alionae mitandaoni, Ugomvi alionao na Super staa Lemutuz pamoja na Sheria ya Mitandaoni Tusiandikiae Mate 

Bongo Fuse TV inakuletea Mahojiano Hapa chini:

Amanda Awa Mbogo Baada ya Kuambiwa Anatumia ARV

$
0
0
Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.

Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.

Akizungumza na mwandishi wetu, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.

“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.

Kajala Masanja Aibiwa Nguo ya Ndani Kiuchawi......Aikuta Nje Ikiwa Imelowa Damu

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amepatwa na dhahama ya aina yake baada ya kuibiwa nguo yake ya ndani kimazingara kisha kuikuta nje ikiwa imeloa damu.

Kwa mujibu wa Gpl , mara nyingi Kajala ana kawaida ya kufua na kuzianika nguo hizo ndani lakini katika mazingira ya kutatanisha moja ilipotea na kila alipofanya jitihada za kuitafuta, hakuiona.

Baada ya nguo hiyo kutooneka ghafla, Kajala alichanganyikiwa sababu nyumbani kwake hakuna hata panya ambaye anaweza kuibeba pengine na kuitupa sehemu nyingine.

Habari  zinaarifu kuwa baada ya kulitafuta ‘kufuri’ hilo kwa muda mrefu bila mafanikio, alikuja kulikuta kwenye ndoo tupu ya maji tena ikiwa imetobolewa huku ikiwa imetapakaa damu.

Zitto Kabwe Ni Balaaa!!! Hizi ni Picha 10 za Mkutano wa ACT Mkoani Tabora.......Watu Walijaa kupita maelezo

$
0
0
Kiongozi  Mkuu  wa  Chama  cha  ACT-Wazalendo  akiwahutubia  mamia  ya  Wananchi  Mkoani  Tabora  Jana. 









Sakata la Emmanuel Mbasha Kubaka: Daktari Atoa Ushahidi Mahakamani, Asema Vipimo Havikuonyesha Dalili yoyote ya Msichana Huyo Kubakwa

$
0
0
Shahidi wa nne katika kesi ya tuhuma za ubakaji inayomkabili Emmanuel Mbasha, mume wa mwanamuziki wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, jana alidai mahakamani kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili mlalamikaji.

Hayo yalidaiwa na daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, ambaye alimfanyia vipimo msichana huyo.

Daktari huyo alidai katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba vipimo alivyomfanyia msichana huyo anayedaiwa kubakwa na Mbasha, havikuonyesha kitu chochote.

Dk. Migole alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa alili ya kufanyiwa vipimo.

Alidai kwamba binti huyo alipofika hospitalini hapo, alimfanyia kwanza vipimo vya macho kisha kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, ambavyo hutolewa bure.

Dk. Migole  alidai kwamba baada ya kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, akiwa na baadhi ya ndugu wa familia yake, hakwenda bali aliingia mitini na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.

Alidai baada ya kufanyiwa hivyo, vipimo hivyo  vilionyesha kuwa hakuna kitu chochote alichofanyiwa, kwa maana ya kubakwa au kuingiliwa na mwanamume katika mwili wake na kuwajazia fomu aina ya PF3 kwa kile alichokiona.

Binti huyo hakuonekana kuwa na ujauzito, maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na wala mbegu za kiume katika sehemu za siri,” alidai daktari huyo.

Hata hivyo, baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Flora  Mujaya, hawakuweza kusikiliza ushahidi mwingine kutokana na taarifa za msiba wa hakimu mwenzao, zilizofika mahakamani hapo.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri Aprili 20, mwaka huu.

Mbasha anadaiwa kuwa Mei 23 na 25, mwaka jana, alimbaka binti  mwenye umri wa miaka 17, ambaye anadaiwa ni shemeji yake  huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Dereva Wa Bajaji Asimulia Jinsi Magaidi 10 Walivyonaswa Morogoro Wakiwa Na Silaha Msikitini............Imamu Awakana 'Magaidi' Hao

$
0
0
Dereva  wa bajaji, Alphonce Maurus, aliyebeba watu wanaodhaniwa kuwa watuhumiwa wa ugaidi, Kidatu wilayani Kilombero, ameweka hadharani namna alivyomfahamu mmoja wao.

Amesema mtuhumiwa ambaye aliuawa na wananchi baada ya kumjeruhi polisi, Hamad Makwendo, alijihusisha na mchezo wa kareti na masuala ya dini ya Kiislamu.

Dereva huyo huyo aliwaeleza waandishi wa habari waliofuatilia taarifa za kina za tukio hilo jana kwamba Makwendo alikuwa hana kazi maalumu ya kumwingizia kipato.

Maurus alitoa taarifa hizo katika kata ya  Chikago, Kidatu wilayani Kilombero ambapo watu 11 walikamatwa na polisi  msikitini wakiwa na silaha, milipuko na sare za jeshi.

Alisema siku ya tukio, saa tatu usiku, akiwa katika  eneo lake la kufanyia kazi, walitokea watu 11 ambapo watano pamoja na mwenyeji ambaye ni marehemu, walipanda katika bajaji yake na wengine sita walipanda katika bajaji ya mwenzie.

Alisema watu hao walitaka kufikishwa katika msikiti wa Suni na kwamba wakati wote wa safari, mwenyeji wao ndiye alikuwa akizungumza lugha ya Kiswahili huku wenzake wakisikiliza bila kujibu kitu.

‘’Tuliwafikisha hadi eneo walilotaka na kisha tuligeuza na yule mwenyeji wao, ambapo tulipofika manyasini tulisimamishwa na polisi wakitaka kujua tumetoka wapi na tunakwenda wapi.

Yule mwenyeji alishuka na kuanza kukimbia jambo lililofanya askari kuanza kumkimbiza huku na sisi tukifuatilia nyuma,’’ alisema.

Alisema Makwendo alipofika mbele alimkata polisi mmoja na jambia  na ndipo polisi walifanikiwa kumpiga risasi na wakamchukua na  walimchukua na kumpandisha katika gari lao.

Maurus alisema wananchi walifika katika eneo hilo na kuzingira gari hilo na kumshusha mtu huyo huku wakitishia kuchoma moto gari la polisi.

Akizungumzia  mwonekano wa watu hao, dereva huyo alisema walivalia mavazi ya jamii ya Kihindi, maarufu kama Punjabi, huku umri wao ukionekana kati ya miaka 20 na 25 tofauti na mwenyeji wao alieyonekana na umri wa takribani zaidi ya miaka 30.

 Kwa upande wake, askari aliyejeruhiwa, Koplo Nasoro Dabi, ambaye amelazwa katika zahanati ya Polisi Mkoa wa Morogoro, alisema siku ya tukio, akiwa na askari wenzake walisimamisha bajaji aliyopanda Makwendo.

Alisema baada ya bajaji hiyo kusimama, mtuhumiwa huyo alikimbia, hali iliyoashiria kuwa ni mhalifu hivyo kuwalazimu askari watatu, akiwemo yeye kumfukuza.

‘’Wakati tukimkimbiza, nilikuwa mbele na kwamba tulipofika katika giza alichomoa jambia na kunishambulia. Askari wenzangu waliokuwa nyuma yangu walifyatua risasi na zingine kupiga juu hali iliyosababisha wananchi wengi kujitokeza kumpiga na kumchoma moto,’’ alisema.

Alisema wakati tukio hilo likiendelea askari wengine walifanya mawasiliano na Mkuu wa  Kituo cha Ruhembe kwa ajili ya kuwaongezea nguvu.

Naye Mganga Mkuu  Zahanati ya Polisi Morogoro, Mrakibu Thomas Kawala, alisema walimpokea askari huyo anaendelea na matibabu.

Kawala alisema  askari huyo alifika zahanati hapo akiwa na maumivu makali  lakini kwa sasa anaendelea vyema na matibabu.

Mmoja wa Kiongozi wa Msikiti  wa Masjid Salah Al – Fajih , Mohamed Manze, alisema wakiwa viongozi na waumini, hawakuwa na taarifa zozote za ujio wa watuhumiwa hao na kwamba katika msikiti huo wako vijana wanne ambao huwa wanalala na kujisomea hapo.

Alisema siku ya  tukio watuhumiwa hao walifika msikitini hapo saa nne ambapo ibada ya mwisho ilikwishafanyika na waumini kutawanyika, ambapo walikuwa wamebakia vijana hao peke yao.

Manze alisema  walitumia mwanya huo kuingia na kujihifadhi bila taarifa zozote kwa uongozi wa msikiti, jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu za msikiti huo.

Hata hivyo, alisema wakiwa waumini wa msikiti huo, hawakupendezwa na suala hilo kwa kuwa limewachafua na kuwaharibia sifa na kwamba Makwendo hakuwa muumini wao.

Alisema hawana nasaba na kikundi chochote kinachojihusisha na uhalifu  na kwamba wanalaani vibaya watu wanaotumia dini katika masuala hayo ya uhalifu.

MBOWE: Jakaya Kikwete Akijiongezea Muda Hatutakubali, Nchi itawaka Moto

$
0
0
Kupitia taarifa ya habari ya ITV mbowe anasema hatutakubali kikwete aongezewe muda eti kwa sababu daftari la wapiga kura bado.akasisitiza lazima nchi itawaka moto..

Je una maoni Gani Kuhusu Kauli hiyo ya Mbowe?

Nimemfumania Mke Wangu Akifanya Mapenzi na Baba Mkwe Wake Nifanyaje?

$
0
0

Sio rahisi kuamini nashangaa, sina amani maishani mwangu baada ya kukuta mke wangu anafanya uzinzi na baba mkwe wake ambae ni Baba yangu Mzazi. Kwakweli nilishitshwa kuona hali kama hii, hakika ndio muda wa kiama huu nimeshindwa mpaka sasa nichukue hatua gani Hapa nilipo ...

Naombeni ushauri wa Kufanya Katika Hali Kama Hii 

2 Tanzanians killed in South Africa on Anti-Foreigners Attacks

$
0
0

Two Tanzanians living in South Africa have been killed in what has been linked with the ongoing xenophobic violence that rocked the country recently.

News of the deaths came as the minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Bernard Membe, announced from Oman that Tanzania had begun evacuating its nationals from Yemen that has been engulfed in a bloody war between government forces and rebels.

In South Africa, a representative of Tanzanians living in the country told The Citizen yesterday, that the two met their deaths in the anti-foreigners attacks that have left another five people from other countries dead and thousands displaced in the city of Durban.

Mr Bonka Kuseleka, a representative of the Tanzanians, named the deceased as Rashid Jumanne, a cigarette peddler who died on Tuesday in Stenga, a suburb in Durban and one Athumani alias China Mapepe, who died on Wednesday in the largest city in the South African province of KwaZulu-Natal.

According to Mr Kuseleka, Rashid was shot dead by unknown gunmen while peddling his merchandise while Athumani, a detainee at Westville correctional facility was stabbed to death by fellow inmates.

“As I speak to you now we are on a peaceful march with some locals in Durban to condemn these brutal killings but so far we have lost two Tanzanians here,” he told The Citizen by phone from Durban.

Familia Yaweka Wazi Jinsi kifo Cha Secky wa Lulu Michael Kilivyotokea...Ukweli Huu Hapa

$
0
0
Familia ya marehemu Lusekelo Samson Mwandenga 'Seky' imeweka wazi chanzo cha kifo cha marehemu baada ya kuzagaa habari mitandaoni kuhusu chanzo cha kifo chake kuwa Lulu Michael Amehusika..

Familia hiyo imeeleza kuwa marehemu aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake kisha akapelekwa hospitali na baadaye kufariki dunia akiwa hospitali.

Enzi za uhai wake, marehemu alikuwa mdau mkubwa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, hivyo msiba wake umegusa tasnia hiyo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Secky mahali pema peponi. AMEN.


Breaking News:Polisi Wenye Silaha za Moto Waizingira Nyumba ya Askofu Gwajima Huko Sala Sala Muda Huu

$
0
0
Kinachoendelea Muda huu nyumbani kwa Gwajima ni Polisi wenye silaha za moto wameizingira nyumba ya Gwajima ..Habari tulizozipata ni kuwa Jana Gwajima Alitakiwa aripoti Polisi na Kupeleka Hati za Mali alizo agizwa lakini hakufanya hivyo ..Hivyo muda huu Polisi wako kwake kwa ajili ya kumkamata lakini Mpaka sasa Gwajima amejifungia Ndani na Polisi Wameshindwa kuingia Ndani Kwa ajili ya Kumkamata.....

Tutaendelea kuwapa Kinachojiri....

Lemutuz Asikitishwa na Kifo cha Ghafla cha Rafiki Yake Super Bilionea Seky

$
0
0
Live at my Office downtown Dar Tancot House 2nd FL kazi kama kawa maana Mwanaume ni kazi kwanza ninasikitika sana kutangaza kifo cha gafla cha rafiki yangu wa karibu sana Super Bilionea Seky.

I am speechless Wiki mbili nzima zilizopita mara kwa mara tumekutana Mliman City na Tripple 7 Club mara ya mwisho tulikuwa wote Jumamosi iliyopita mke wake alikuwa anaumwa sana tukaenda wote Baraka Plaza tuka kaa masaa mengi kumsubiria mke wake na leo asubuhi saa tatu.

Tumeongea sana kwenye simu kuhusu viwanjani leo akaniahidi kunipigia back in One Hour twende wapi leo 1 hour ago nimepigiwa Simu kuwa amefariki ghafla Ohh my God bado I am speechless.

Ninamuombea sana mke wake na watoto katika hiki kipindi kigumu sana kwao this one really hurts Binadam tunapita tu hapa Duniani we are just weak creatures of God.

I cry for U Seky a great human being Mungu amuweke mahali pema peponi, please people lets pray for my friand
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images