Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

JUAN MATA AWAANDIKIA CHELSEA BARUA YA KUWAAGA MARA BAADA YA KUJIUNGA MAN U-VERY TOUCHING

0
0
On the completion of his transfer from Chelsea FC, Juan Mata took out time to write a letter to everyone associated with Chelsea. And yes, this is very emotional indeed. Get ready to board the feels train (an overused but appropriate phrase).

Juan Mata: “Hi everyone, As you can imagine this is a very important day in my life, and with these lines I would like to express the memories and emotions that come to me as I write. This letter is written from my heart, and first of all I would like to say that I will never forget all the affection given to me by the Chelsea fans. From the very first day until the last. With your support and affection I have grown up as a player and I have had an amazing time both on and off the pitch. I will always feel the gratitude towards you. Always. No words are enough to give back all the things I have received. There has been plenty of good moments: the FA Cup, my first trophy as a Blue; the immense happiness of winning titles for the first time in the club’s history, such as that magical Champions League night in Munich and the Europa League… On the other hand, I have experienced some complicated situations from a personal point of view, mainly during the last six months. Every message I got through the social media, every nice word you have said to me on the street, and of course, your support in the stadium, has made me feel incredibly proud of the Chelsea fans; you deserve a team like the one you’ve got, with so many fantastic players. I won’t forget the faith you put in me when I was given the player of the year award the last two seasons. I feel really proud and I will never forget those nights. Thank you so much for the way you have treated me, you have been unbelievable. I hope you understand that after going through a complicated and, for me, new situation in the last few months, I believe this is the best choice in order to carry on with my football career and to keep enjoying this sport. Before last summer, my intention was to stay here for a long time; as long as the club wanted me to, and to keep winning trophies for Chelsea FC. This is how happy I was in the club and in the city. However, as you all know, things changed after the preseason. From feeling like an important player, I started to experience some difficult situations and I felt unable to help the team to the extent that I wanted and was used to. Obviously, I fully respect the circumstances. Football is a team sport and it’s not easy to play regularly in such a good squad. In sports you may win or lose, but the most important thing is to give everything. I hope you know and feel that I have always done so. In every game, in every training session, without exception. I have always tried my best for the club. I would like to emphasise the affection, admiration and respect that I’ve had for my former team mates since the first day. I want to thank the captains for their help and understanding at all times. They made me feel comfortable when I arrived and they have supported me throughout the difficult times this season. I thank all my former team mates for these two and a half years and I wish them the best, personally and professionally, for the future. Of course I have been closer to some of them, but the most important thing is that my years in Chelsea have left me with great friends. Friends forever, football rivalries aside. I also want to highlight the day-to-day job of every member of the Chelsea staff: medical team, kit men, staff at Cobham and Stamford Bridge, media and marketing department, Chelsea TV team… All of them are very important in making this club a great one. Thank you for your treatment and your efforts to make the life of the players easier. Furthermore, thanks to every manager I have had the pleasure to work with during my time here. They have all been a big help for my progression as a player. I have always respected their decisions, whatever they were; they made me more mature and a stronger person. You learn from everything, and certain situations make you think about other team mates who are coping with similar situations more regularly. Thank you Andre for giving me the opportunity to join Chelsea FC. Without your support, none of this would have happened. To Robbie and Rafa, for their unlimited trust in me. And to Jose, for making me a stronger player, because in difficult moments, I have learnt to remain positive and to keep working hard. Lastly, I want to thank the Club, and in particular its owner, Roman Abramovich, for trusting me and making an important investment when signing me. Also for their understanding regarding my situation over the last months. I’m very glad to have been part of the squad that made his and our dream come true: winning the Champions League on that unforgettable night in Munich. Additionally, my years in Chelsea have been profitable for the club, which I’m very pleased about. I want to make clear that the stage that now comes to an end has been extremely important for me, personally and professionally. Although many of you, like myself, never thought this moment would come, this is football and a new chapter is about to begin. I would have liked to say good bye to all of you in the stadium, or in a press conference, but it has not been possible. I’m sure, i will be able to do it in the future, because is what you deserve. Evidently, today is a day of mixed feelings, remembering the past and looking forward to the future and what it has to bring. I look forward to being happy and to enjoy what I like the most: play football. I will never forget my time in Chelsea and the affection I take with me, I will keep forever. I wish you the best. A big hug to all of you. THANK YOU so much, Juan.”

DK.KIGWANGALLA HATARINI KUVULIWA UANACHAMA CCM

0
0
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla yuko hatarini kuvuliwa uanachama wa chama hicho, hatua ambayo endapo itachukuliwa itasababisha apoteze nafasi yake ya ubunge.

Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari umemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana jioni zinasema baada ya vikao hivyo vilivyofanyika Januari 11 mwaka huu, imeazimiwa kuwa suala la Dk Kigwangalla pamoja na madiwani watano wilayani humo lipelekwe katika ngazi ya CCM mkoa na baadaye taifa.

Dk Kigwangalla jana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema: “Hata mimi nimesikia taarifa hizo, isipokuwa sijapewa taarifa rasmi. Ila nafahamu kwamba vikao vya chama vilikuwepo na mimi niliitwa ila kama ambavyo nimeshasema siwezi kuhudhuria”.

Gazeti hili lilimtafuta Mbunge huyo machachari kutokana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mitandao ya Facebook na Tweeter akieleza kuhusu taarifa za kuwapo mpango wa kumfukuza uanachama.

Kupitia mitandao hiyo Dk Kigangwalla aliandika: “Nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu’ hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. “

Mbunge huyo aliongeza: “Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang’anywe kadi ya uanachama wa CCM. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa Nzega.”

Mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa CCM wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha CCM wilayani humo.

“Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no’, basi sina haja ya kuendelea kupambana,” aliongeza.

Aliendelea: “Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako”.

Kauli ya CCM Nzega

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega, Amos Kanuda alikiri Dk Kigwangwalla kujadiliwa katika vikao vya chama vya wilaya, ikiwamo Kamati ya Siasa.

NAJ AFUNGUKA MENGI KUHUSU MR. BLUE ASEMA HAJUTII KUTOLEWA BIKRA NA KABAISA HUYO

0
0
Mwanamuziki Naj ambae kwa sasa anaishi Uingereza ameelezea story nzima ya mahusiano kati yake na mr. Blue yaliyodumu kwa muda kidogo kabla ya kuchana mwaka jana mwanzoni. Naj anasema Blue ndo alikua boy wake wa kwanza na ndo aliyemtoa bikra.

Naj anafunguka kwamba hakua anajua kama kipindi yuko na Kabaiser kwamba alikua na mademu wengine   wawili. Anasema Blue alikua mpole kwake na mstaarabu na wala hajutii kukutana nae maishani na kumfanya awe mwanamme wa kwanza kumvulia chu.....Naj ambae kwa sasa yupo masomoni uingereza alisema mahusiano yao yalikua magumu kutokana na umbali waliokua nao na mambo flan ambayo alisema ni ya kiprivate na hawez kuyaweka hadharani

BREAKING NEWS:MADERAVA WA MALORI TABORA WAFUNGA BARABARA KISA WENZAO WATATU WALIO UAWA

0
0
Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inasema malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kukatwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
IMG-20140126-WA0003Mbali na malori kuna mabus ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambalo wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au Rpc  afike,huku wakidai hilo limekua ni tatizo sugu eneo hilo kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
IMG-20140126-WA0006Eneo hili linaitwa laziba lipo katikati ya mji wa Laziba na Nzega,ni kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana  saa 3 usiku.

PROFESA BAREGU AFICHUA SIRI YA USALITI CHADEMA

0
0
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu. 

Alisema kitendo cha wanachama na viongozi kunyoosheana vidole vya usaliti kinakiangusha chama na kwamba Chadema kimefeli katika mambo matatu, ambayo ndiyo yanapaswa kuwa msingi wa chama na kama yangezingatiwa mapema, hoja ya usaliti isingezungumzwa leo.

Aliyataja mambo hayo yanayozalisha hoja nzito ya usaliti iliyosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kuvuliwa uanachama kuwa ni kusikilizana, kuvumiliana na kuaminiana.

“Kukosekana kwa mambo hayo ndio kiini cha kuibuka kwa hoja ya usaliti, hatua hii ni mbaya katika maendeleo ya chama kinachojijengea uaminifu kwa wananchi,” alisema.

Alisema kuendelea kwa hali ya kushutumiana ndani ya chama kunasaidia kukitafuna na ipo siku Chadema haitakuwa na mtu msafi, kwani wote wataitana wasaliti.

“Chadema ni chama kizuri cha siasa, lakini kimefeli kabisa katika kuyadhibiti mambo hayo matatu muhimu, nadhani hili ni tatizo kubwa linalokiandama chama hiki.

“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati chama hakitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.

Akizungumzia mgogoro wa hivi karibuni ndani ya chama hicho uliosababisha Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo kuvuliwa uanachama, huku Zitto Kabwe akikimbilia mahakamani, Profesa Baregu alisema hayo ni madhara ya kutotumia hekima na kukosekana kwa busara ya kumaliza tofauti kwa mazungumzo.

“Kama hamsikilizani wala kuaminiana, lazima athari ziwepo, tena kubwa tu, kwa sababu matukio ya namna hiyo yanakuwa endelevu, leo kashutumiwa huyu ni msaliti, huwezi kujua mwingine atashutumiwa lini …na mvurugano uliotokea hivi karibuni ndio uhalisia wa kile nilichokisema hapo awali, kwamba ndani ya Chadema kumekosekana utamaduni wa kumaliza tofauti kwa mazungumzo, kwa ujumla watu hawavumiliani wala kusikilizana,” alisema Profesa Baregu.

Aidha alitahadharisha kwa kusema, usaliti utakidhoofisha chama kwa kiasi kikubwa, ambapo alikitolea mfano Chama cha NCCR-Mageuzi, ambacho kilikumbwa na mazingira kama hayo na mwisho wake kikaparaganyika ovyo kwa sababu kila mtu alijikuta anatazamwa kuwa msaliti. 

Wakati huo huo, imebainika kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini haijatoa mwongozo wowote juu ya barua iliyoandikiwa na Mwigamba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha. Mwigamba aliitaka ofisi hiyo iingilie kati suala la kunyofolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama hicho.

Inaelezwa kuwa Mwigamba alifikia hatua ya kuandika barua hiyo kabla hajavuliwa uanachama, ambapo alifanya hivyo baada ya kutokea sintofahamu baina ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na wafuasi wanaomuunga mkono Mbowe.

Akithibitisha madai hayo, Mwigamba alisema ni kweli kuwa alimwandikia barua Msajili, ambayo ilikuwa ikihoji ukiukwaji wa katiba ya chama pamoja na kuondolewa kwa kipingele cha ukomo wa muda wa uongozi, hata hivyo mpaka sasa hajapatiwa majibu.

Alisema mara baada ya kuandika barua hiyo, Msajili aliwaandikia Chadema ili kupata ufafanuzi wa madai hayo, ambapo walijibu kuwa walisambaza waraka kwa makatibu wa chama hicho wa mikoa ili kupata uungwaji mkono kabla ya kukiondoa.

Hata hivyo, Mwigamba alilalamikia hatua hiyo kwa madai kuwa inakiuka katiba na utaratibu wa chama hicho na kwamba barua iliyosainiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Shaibu Akwilombe, Julai 13, 2006, kwenda kwa makatibu hao ilikuwa ikiwaarifu kuwa yanapelekwa mapendekezo ya ziada.

Kwamba waunge mkono pendekezo kuwa Katibu Mkuu na manaibu wawili wateuliwe na Mwenyekiti, wasipigiwe kura na majina yao yapelekwe Baraza Kuu kwa ajili ya kupiga kura kuchagua mmoja.

“Katiba ya mwaka 2006 isomeke pia kiongozi anaweza kuchaguliwa tena na ndiyo walileta mapendekezo na mwanzo mpaka mwisho wa barua ilikuwa inaongelea mapendekezo tu. Msajili alinitumia nakala ya majibu yao ili nitoe maelezo ya ziada, ambayo pia nilishafanya hivyo tangu Desemba 30 mwaka jana,” alisema Mwigamba.

Alisema kuwa katika majibu ya Chadema ya Desemba mwaka jana kwa Msajili, yalionesha wazi kwamba Mwigamba alishavuliwa uanachama wa chama hicho, wakati alikuwa bado hajafukuzwa, ambapo walidai kwamba kipengele hicho kilifanyiwa marekebisho.

“Nilimweleza Msajili kuwa katiba ya Chadema, inataka mapendekezo ya katiba yapelekwe kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, siku 30 kabla ya mkutano huo, ukizingatia kikao cha Mkutano Mkuu kilifanyika Agosti 13, 2006 na kufanya mabadiliko ya Katiba Julai 13, mwaka huo huo ndiyo iliandikwa barua, sasa hata kama barua ingesafirishwa kwa ndege ama kwa usafiri wowote lazima zingeanza kupokelewa kuanzia Julai 14 mpaka 16, hapo tayari siku zimepungua, si 30 tena,” alisema Mwigamba.

Alisema kuwa waraka huo uliosambazwa kwa wajumbe ulitakiwa kuwafikia siku 30 kabla na kwamba haukueleza iwapo mapendekezo hayo yaliandaliwa na Baraza Kuu ambalo linatoa mapendekezo kwa Mkutano Mkuu au la!

Alisema waraka huo, ambao alibahatika kuuona, ulikuwa hauna uzito unaostaili, kwani ulikuwa sawa na barua ya uchumba ambayo ni tofauti na cheti cha ndoa unachoweza kupeleka ushahidi Mahakamani.

Anasema wakati barua ya Akwilombe ikisambazwa ilikuwa pamoja na rasimu, ambapo yeye (Mwigamba) akiwa mmoja wa Makatibu wa Wilaya hakuona nakala yake.

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ili kupata ufafanuzi, hata hivyo hakuweza kupatikana, kutokana na kuwa katika vikao, huku simu yake ya kiganjani ikiwa haipatikani. 

Alipotafutwa Msemaji wa Chadema, Tumaini Mkene, alishindwa kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa, ambapo alisema suala hilo lilishazungumzwa katika mkutano wa waandishi wa habari na majibu yake yanajitosheleza.

TOBA:ETI HUYU NDIO MWANAMKE MWENYE MWILI WENYE THAMANI KUBWA KULIKO WANAWAKE WOTE DUNIA

0
0
 Her name is Amanda Lepore, a transsexual who has been tagged as 'the most expensive body on earth'.

The 46 years old blonde had a sex change operation from male to female when she was 19, and ever since then, she has gone under the knife for all sorts of extreme plastic surgery procedures.

The busty party-girl has had three breast augmentations, butt implants, multiple nips and tucks, lip injections, fillers, nose job, forehead life, botox and had her hairline lowered; she even had her bottom ribs broken to achieve a smaller waist and a perfect hourglass statistics of 38-22-38.
Speaking on her sex change procedure, she described it as the most painful procedure she has ever done.

She has however refused to disclose just how much she has spent in total on all her procedures, responding instead with "There is a reason I am labelled 'The Most Expensive Body On Earth'".



SITTA"UWOGA NI ADUI MBAYA SANA WA MAENDELEO NA HAKI"

0
0
Waziri wa tanzania Samwel Sitta amewasihi vijana kutokuwa waoga, kwani "UWOGA NI ADUI MBAYA SANA WA MAENDELEO NA HAKI" hivyo kila mwananchi ana haki ya kufurahia rasilimali za nchi, ambazo kuna baadhi ya viongozi wanataka kuhodhi madaraka kwa namna yeyote ili waendelee kuchumia matumbo yao. 

Akamalizia kwa kusema, yuko tayari "KUBEBA TOCHI ALIYOIACHA MWALIMU NYERERE". Vijana walilipuka kwa shwange na makelele, kongamano hilo alikuwepo waziri mwingine wa tanzania Dr Harrison Mwakyembe na viongozi wengine waandamizi wa serikali na viongozi wa dini pia.

Haya banah, tutashuhudia mengi sana mwaka huu 2014, hoja hii ya Sitta inafanana na ile ya Kamanda makini Lema "HAKUNA DHAMBI MBAYA NA KUBWA DUNIANI KAMA WOGA".

Yangu macho tu

ZURII FASHION & BEAUT BOUTIQUE KUNA STOCK MPYA KWA AJILI YENU

0
0
Wale wateja wetu wa Plus Size tumesikia kilio chenu na sasa Zurii Fashion & Beauty Boutique kuna Stock Mpya kwa ajili yenu Plus Size ladies (wale mlio jaliwa neema hahaha). Size 14-20 sasa zinaptikana ZuRii. Kuna Nguo nzuri sana na quality nzuri sana za kazini, kanisani na za mitoko.
Size ndogo 8-12 pia zipo.
 Tuko Sinza Legho, nyuma ya Rombo Green View Hotel, Dar Es Saalm. Whatsapp au tupigie +255659189769 kwa maelezo zaidi. Karibuni sana.
LOOK GOOD, FEEL GOOD with ZuRii.








Follow us on Instagram @zuriiboutique
Like our page on facebook Zurii Fashion Boutique

UNAKUTANA NA PICHA HII YA MPENZI WAKO AMEIPOST INSTAGRAM, ..!!?? UTALIA, UTACHEKA, UTANUNA AU ..??

0
0
Kuna hatari sana siku hizi kwenye haya mapozi ya upigaji picha, haswa zile ambazo ni kwaajili ya kupost kwenye mitandao..huyu sijui alikuwa anafikiria nini na kupost hii picha Intagram

NYOKA MKUBWA AINA YA CHATU AKUTWA AMEKUFA NDANI YA BONETI YA GARI NDOGO. CHEKI PICHA ZAIDI

0
0


Joka kubwa aina ya chatu la kutwa limekufa ndani ya bonneti ya gari ndogo, joka hilo lilikufa ndani ya boneti kwasababu ya kuungua kutokana na joto kali la engine.,,kuweni makini mnapo fungua bonet za magari unaweza kuta hajafa akakugonga...

KIGOGO WA WEMA NOMA SANA..AMNASA RAFIKI WA WEMA KULIPA KISASI

0
0
Tatoo ya Clement Mgongoni Mwa Naima
Stori: Imelda Mtema
NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).

“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.

NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.

“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.

“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.

“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.

WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.

“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.

UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.

Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).

“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.

WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.

Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.

“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.

NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.

“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.

“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu. 

Chanzo:Global Publishers

ASKARI MAGEREZA WADAIWA KUUWA MFUNGWA

0
0
Msemaji wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omary Mtiga
Askari Magereza wanane, wamefikishwa mahakamani wilayani Mafia mkoani Pwani kwa tuhuma za mauaji ya mfungwa.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa Wilaya ya Mafia, Hassan Makube, ilidaiwa kuwa, Desemba 19 mwaka jana, askari hao walimuua Basiri Makungu aliyekuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kilombero, lililopo kwenye wilaya hiyo. Askari waliofikishwa mahakamani hapo walitajwa kuwa ni Sajenti Sadick na wenzake ambao walifunguliwa kesi namba 1/2014.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja walimuua Makungu, baada ya kumshambulia kwa kipigo mwishoni mwa mwaka jana.

Kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu, pamoja na kesi ya mauaji kutokuwa na dhamana, watuhumiwa hao walirudishwa rumande hadi Februari 7 mwaka huu.

Akizungumzia tukio hilo, ofisa wa juu wa Jeshi la Magereza, Menrad Tesha alisema kuwa, jeshi hilo linafahamu taarifa za askari hao kushtakiwa kwa makosa hayo, lakini akasema suala hilo halipo chini yao. Tesha alipohojiwa kuhusu mustakabali wa ajira za askari hao na iwapo wanashtakiwa kama raia au wafungwa alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa sasa.

“Siwezi kuzungumzia ajira zao hapa, huu siyo utendaji unaotakiwa, kila kitu kina taratibu zake, hivyo siwezi kulizungumzia hilo,” alisema Tesha.

Alieleza kuwa askari anapotuhumiwa kwa makosa yoyote suala lake huachwa mikononi mwa vyombo vinavyostahili, ili kuwachukulia hatua.

“Hivi sasa wale ni watuhumiwa, kwa hiyo mimi kuliongelea siyo sahihi. Kama kuna kitu ungetaka kufahamu, basi nakushauri mfuate mkuu wa gereza kule walipo sasa (Mafia), atakueleza kila unachotaka kufahamu kuhusu askari hao kwani bado wapo huko,” alisema Tesha.

Matukio ya Askari Magereza kuua wafungwa

Februari mwaka jana ilidaiwa kuwa Willfred Mallya mwenye namba 315 aliyefungwa mwaka 2003 katika katika Gereza la Kisongo mjini Arusha aliuawa kutokana na kipigo cha Askari Magereza.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omary Mtiga licha ya kukiri kutokea kwa kifo cha mfungwa huyo, alikanusha kuwa kilitokana na kipigo cha askari hao akisema kifo chake kilikuwa ni cha kawaida.

Desemba mwaka 2010, askari wanne wa jeshi hilo waliokuwa wakifanya kazi katika Gereza la Lilungu mkoani Mtwara, walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji ya mfungwa.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Abdulhaman Mohamed mbele ya Hakimu Stepheni Mbungu.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Oktoba 31, mwaka 2010 watuhumiwa hao kwa pamoja walimuua mfungwa aliyekuwa na namba 215, Kasimu Kumchaya.

PICHA MBALI MBALI ZA MAKAMANDA WA CHADEMA WAKIWA KATIKA HELKOPTA..

0
0
Makamanda wakiwa ndani ya Helkopta kuelekea katika Operesheni Pamoja Daima, Kilelema.

MCHUMBA WA MTU AAGA ANAKWENDA KWA BIBI YAKE MGONJWA KUMBE ANAENDA KUUZA MWILI WAKE..AKAMATWA

0
0
Stori: Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili.

Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.

Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.

OFM NOMA: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa mikononi mwa OFM na Polisi.


Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.

Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.

Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.

“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.

OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.

Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.

Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.

PENNY: DIAMOND KAMA CHIZICHIZI VILE!

0
0
Stori: Imelda Mtema na Erick Evarist
MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa sifa ya aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni kama chizichizi lakini kwa undani zaidi ni mtu makini.

Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.
“Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali,” alisema Penny na kuongeza:

“Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani.”
Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.


Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana’, akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani. 
GPL

BONGE LA NYAU AMEIKANA ACCOUNT YA INSTAGRAM INAYOCHONGANISHA BEEF KATI YA DIAMOND NA ALI KIBA

0
0
Jumapili ya jana ilikua jumapili mbaya sana kwa msanii Diamond kwani ni kama vile karibu watu wote waliojiunga instagram walimuona mtu mbaya kwake. Ishu ilianza ivi, kupitia akaunti moja huko Instagram inayotumia jina la TeamKiba iliandika ujumbe unaosemekana umeandikwa na Diammond ukisema "Unajua kua kuna watu hawataki kabisa kukubali kua mimi ni zaidi yao kuanzia mziki wangu mpaka maisha yangu, mtu anaulizwa twitter hivi mkiamua kufanya nyimbo na Diamond hamuoni kwamba itapendeza sanaa. Et never eve haiwezi kutokea mimi kuimba na Diamond, badala angekubali apate kick nimrudishe katika mziki analeta dharau wakati anipati kimziki wala kipesa. Muziki wake hauna tena soko nasikia sasa hivi kajiunga na taasisi ya mkopo inaitwa FAIDIKA NA PRIDE kakopeshwa kujenga nyumba. Sitaki kua mnafiki ni Ali Kiba"

Mwandishi wetu wa Ngama Media aliendelea kufatilia picha linaendaje na baada ya mda mfupi akaunti hiyo iliendelea kupost ujumbe mwingine kwa njia ya picha unaodaiwa kua umetolewa katika page ya Rafiki mkubwa wa AliKiba anaefahamika kwa jina la Bonge la Nyau ukisema "Hivi huyo msanii Domo Diamond anamtaka kitu gani msanii Ali kiba? Tokea juzi amekua akimzungumzia katika media kwa wale mliofatilia katika interview yake baada ya kusamehewa na kituo cha chanel ten aliropoka maneno haya kuhusu Ali Kiba kujiunga Pride akakopeshwa ndio tatizo? Kuna matajiri kibao humu mjini wana maisha mazuri kwa ajili ya mikopo. Zote chuki Diamond kama na wewe unataka mikopo si ukajiunge?? Sio kumpiga majungu mwenzio watu kibao wamejiunga na mikopo washapata inawasaidia. Kama na wewe unataka tena usisusumbuke bofya hapa http://pri*****tanzania.wapka.mobi (tumeficha adress hiyo kwa sababu ni ya matapeli) utapatiwa mkopo na sio kumponda mwenzio.

Sasa movie linaanza hapaaaa, kupitia akaunti ya Bonge la nyau instagram, Bongo la nyau alikana kuandika ujumbe huo hapo juu na hichi ndo alichokisema " Jaman haya mambo yanayoendelea mm yanazidi kunisangaza cz napigowa simu sana na kutumiwa msg kwamba nimepost msg ya kumponda diamond kwa kusema alimponda ali kiba before... dah kweli nishai inshu iko iv iyo account hapo juu ilikuwa yangu miezi mitatu iliyopita bt kuna matapeli wa pride walinizidi ujanja wakai haki na kuchange password mpaka email ikawa chini yao wananisumbua sana cz wanapokea deal zangu zote wanawatapeli watu, watu wakijua wanawasiliana na bonge la nyau nshapokea cm ya kulaumiwa sana mpaka kutaka kupelekwa police kwaajiri ya matapeli hao cz iyo account ilikuwa kuwa kubwa sana na ina fans zangu wengi wanaojua kuwa ni mm uyo bt sio ivyo leo wamekuja na utapeli mwingine wa kuwachonganisha diamond na ali kiba ili kutangaza mambo yao ya pride sio poa kabisa cz wananiharibia mm naonekana naingilia mambo yasiyonihusu kabisa siwezi kukaa kuponda msanii mwenzangu yoyote wala kumuongelea kwa mabaya..... iyo sio peg yangu na siitumii so kama utamuitaji bonge la nyau hapatikani kwa page iyo ntwawapostia page yangu nnayatumia, hao ni matapeli wa pride wanaowaibia watu cz hata ukisoma story vizuri wameingia mambo ya kujengewa nyumba na pride akajidai eti mbona na mm bonge la nyau nimejenga kwa mkopa wa pride no no no no me sijajenga kwa pride na still niko kwa mama yangu ni uzushi tuu wa kutaka pride i kik kwa kupitia majina ya wasanii.."

Baada ya uchunguzi wetu uliofanya na mwandishi wetu kutoka Ngama Media tuligundua kweli kua akaunti ya Bonge la nyau ipo hacked na ndo ilitumiwa na matapeli kuchochea bifu hilo hapo juu.

Utapeli uliokua ukitumika katika akaunti feki kwa kutumia wasanii majina ya wasanii mbalimbalindo uliotumika na hapa katika bifu hili la Ali Kiba na Diamond. Matapeli hawa hujifanya wanatoa mikopo ya hadi zaidi ya milioni 20 kwa kujisajili kwa sh 80,000 tu. Sasa ukijidanganya ukatuma hiyo hela jua kua ndo umeshatapeliwa na hela yako haitarudi na hata ukiwapigia kwa namba uliyowatumia hela hutawapata. 

Ukweli ni kwamba hakuna mikopo inayotolea mtandaoni bila ya dhamana na bila ya kuandikishiana mikataba sasa chunga sana usije ukaibiwa. Mwandishi wetu kutoka Bongoclan ataendelea kuwaletea habari zaidi kuusu bifu il na tunapanga kuwatafuta wasanii Diaamond na Alikiba ili waelezee upande wao.

ANGALIA PICHA NA VIDEO JINSI JAY Z NA BEYONCE WALIVYOPAWISHA TUZO ZA GRAMMY NA WIMBO WAO WA DRUNK IN LOVE

0
0
Jay Z and Beyonce put on a showstopping performance as they opened the 2014 Grammy Awards on Sunday night performing hit song, Drunk In Love. Beyonce wore a black thong, glittering bra and sheer bodysuit while Jay Z looked dapper in a suit. Definitely one of the best performances of the night. See more photos and video of their performance

ANGALIA VIDEO HAPA:

PROF LIPUMBA AKOSOA UTEUZI WA WAZIRI WA FEDHA SAADA SALUMU

0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya. Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara. 

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita. 

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti. 

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi. 

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

Alisema kutokana na hali hiyo, uamuzi wa Serikali wa kuwaondoa mawaziri mizigo hautafanikiwa kwa sababu waziri huyo anaweza kuongeza mzigo mwingine kwa nchi.

“Mawaziri mizigo, wanaisababishia Serikali kuwa na viongozi mizigo, hivyo basi tunapaswa kuwa makini kwa kupinga kuongozwa na viongozi mizigo, kwa sababu wanaweza kutuletea matatizo,” alibainisha. 

Akitolea mfano katika kipindi ambacho Waziri wa Fedha anapaswa kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali, ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, mchakato wa Bunge maalumu la Katiba, vitambulisho vya uraia na mambo mengine ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji fedha. 

Alisema kutokana na hali hiyo, waziri huyo anapaswa kusimamia matumizi ya fedha katika shughuli mbalimbali zikiwemo za halmashauri na safari za Rais, ambapo katika kipindi hiki cha robo mwaka, safari zake za nje zimemaliza bajeti yake ya mwaka mzima. 

Alisema kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alipaswa kumchagua mtu makini mwenye sifa stahiki kukalia nafasi hiyo, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa kufuata taratibu za kisheria. 

Alisema chama hicho hakina mashaka na uteuzi wake, lakini wana mashaka na chuo alichosoma na kupata shahada ya kwanza na ya pili.

WAZIRI AJIBU 
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza. Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.

“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland. “Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.

Source: Mtanzania JUMATATU, JANUARI 27, 2014

UKWELI KUHUSU PICHA YA DAVIDO NA MSICHANA ANAYESEMEKANI NI MBONGO WAKIWA KITANDANI.

0
0
Wiki hii yote kumekuepo na picha iliyosambaa mtandaoni ikimwonyesha msanii Davido akiwa kitandani na msichana anayesemekana ni mbongo. Ki ukweli mimi kama admin wa Bongoclan nimeiona katika Blog nyingi sana siwezi zikumbuka zote.

Baada ya kuiona picha hiyo nlijiuliza maswali mengi sana moja ni kujua kama kweli mdada huyo ni mbongo au watu wanazusha tu, hiki ndo kilichoandikwa katika moja ya blog zilizoandika story hiyo. "Msanii maarufu wa muziki wakizazi kipya ajulikane kwajina la davido tika nchini Nigeria anaetamba na kibao chake cha SKELEWU,hivi ndivyo alivyo pigwa picha na mwana dada huyu anaedaiwa kuwa mwigizajiwa bongo wakiwa katika pozi la mahaba alivyokuja Bongo."

Katika uchunguzi uliofanya na Bongoclantz.com umebaini kua story hiyo ni feki, na wala mdada yule si mbongo kama watu walivyozusha.  Ukweli kuhusu story hiyo ni kua mdada huyo ni raia wa Nigeria na story hii ilikua ni ya mwaka jana mwezi wa tatu. Unaweza soma baadhi ya story hizo kwa kubonyeza link zifuatazo LINK1,LINK2, LINK3 kama utazisoma vizuri na kutazama tarehe za story hizo utagundua kua story zote hizo ni za mwaka jana mwezi wa tatu.

Davido alivyotafutwa hiyo mwaka jana baada ya picha hizo kusambaa mtandaoni alisema kua hamjui na wala hajawahi kumwona mwanamke huyo na anashindwa kuelewa ilikuaje hadi akaingia katika chumba chake na jinsi picha hiyo ilivyosambaa. 

Skendo hii ya kusambaa kwa picha za Davido akiwa na mwanamke kitandani na picha kusambaa mtandaoni si ya mara ya kwanza kwani kuna mdada mwingine alishapiga picha na kuzisambaza mtandaoni. Picha hizo zilimwonyesha mdada huyo akiwa na Davido kitandani

MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA USIKU HUU MJINI MOSHI

0
0
Mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed, ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD,amefariki Dunia usiku huu  katika hospitali ya KCMC mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro alikokuwa amepelekwa kwa matibabu. MCD ambaye alikuwa na bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band na Kurudi tena Twanga Pepeta amepatwa na mauti hayo usiku huu, Taarifa za kifo cha MCD zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Hassani Rehani.

Tutazidi kupeana taarifa za msiba huu kwa kadri  zitakavyokuwa zikitufikia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images