Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Baba aua Binti yake, Amzika Nyumbani Kwake

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake na kumyonga kwa kutumia kanga.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na kumzika.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.

Alisema baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga shingoni.

Kwa taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo, maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe.

Raza aibukia sakata la Escrow .....Ataka SUKI kuwaangukia wahisani

$
0
0
MJUMBE wa Baraza la Wawakilishi na Mbunge wa Uzini, Zanzibar, Mohamed Raza, amesema ataishauri Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUKI), kuwaandikia barua wahisani ili kuwaeleza namna sakata la Tegeta Escrow lisivyowahusu Wazanzibari.

Alisema amefikia uamuzi huo ili kushawishi wahisani waendelee kutoa misaada yao kama kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Raza alisema sakata hilo limewaathiri wananchi wa Zanzibar kutokana na kunyimwa misaada na wahisani.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanapaswa kuwaandikia barua wahisani na kuwaeleza ukweli.

 "Sakata la Tegeta Escrow limewaathiri Wazanzibari kwa kunyimwa misaada wakati hawahusiki…hakuna kiongozi hata mmoja aliyetajwa kwenye kashfa hii.

"Nitalizungumza hili kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi ili viongozi wetu waweze kuwaandikia barua wahisani ya kuwaelezea jambo ambalo linaweza kusaidia kupata misaada," alisema Raza.

Alisema kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, Serikali imeshindwa kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoahidi katika awamu iliyopita, hali ambayo inaweza kusababisha kukwamisha maendeleo.

"Mwaka 1995 wakati wa uongozi wa Rais mstaafu Dk. Salmin Amour (Komandoo), wahisani walitunyima misaada kwa madai ya kuwapo kwa migongano, lakini Tanzania ilishindwa kututetea badala yake walituambia hawawezi kutusaidia kwa sababu wahisani walikataa," alisema.

Akizungumzia suala la rushwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Raza alisema kuna baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka Bara wanapita kwa wanachama wao na kutoa rushwa ili waweze kuchaguliwa kuwania urais.

"Ninawaambia wanachama wa CCM wachukue fedha zao, lakini wasiwachague kwenye mkutano mkuu," alisema.

Alisema wananchi ndio wenye mamlaka ya kuwachagua viongozi wao siyo wana CCM peke yake.

Kuhusu utawala wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Raza alisema amejitahidi kuleta maendeleo na kwamba anapaswa kuongezewa muda ili amalizie alipoishia.

"Ningekuwa na uwezo ningemwambia Dk. Shein aendelee na awamu nyingine ili amalizie utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyoanzisha," alisema.

Mapenzi Au Pesa: Wolper Atoboa Anachoshobokea

$
0
0
Hapa na Pale: Kufuatia kuibuka kwa mabishano juu ya nini kinamata kwenye mahusiano kati ya ufundi wa mapenzi au pesa, watu mablimbali wamekuwa wakifunguka mitazamo yao juu swala hili.Staa mrembo wa Bongo Movies, Jackline Wolper naye amefunguka kuwa yeye ni team pesa.

Kupitia ukurasa wake mtandaoni Wolper aliandika kuwa japo anapenda ufundi kidogo lakini yeye anapenda pesa na kuelezakuwa yeye mwenyewe ni fundi.

“Me team chapaaaa ufundi nashobokea kwa mbaliiii siuzimii sana maana me mwenyewe fundi seremala chaaaaaa”-Wolper aliandika mala baada ya kuweka picha ya kanga iliyoandikwa maneno ‘Mapenzi Pesa, Ufundi Peleja Veta'.

Wewe je upo team gani? funguka

Mzee wa Ubuyu

Alikiba asema vurugu zilizotokea Afrika Kusini zimesababisha video ya ‘Chekecha’ ichelewe, awaomba msamaha mashabiki

$
0
0
Staa wa muziki Alikiba amesema kuwa video shooting ya wimbo wake ‘Chekecha’ ambayo imepangwa kufanyika Afrika Kusini, imechelewa kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia) zilizoibuka hivi karibuni nchini humo.

Tayari tulikuwa tumeplan kila kitu unajua kunakuwa kuna zile dancing, choreographer wangu alikuwa ameshacreate kila kitu amewatumia dancers wa South Africa, lakini kilichotufelisha ni hii Xenophobia iliyokuwa imetokea,” alisema Alikiba kupitia Ubaoni ya E-Fm. “Vile vile unajua vifaa kule wanakuwa wanaazima kwahiyo imekuwa ni sheria ambayo imepitishwa hairuhusiwi kufanya hivyo mpaka patulie.”

Hata hivyo Alikiba amesema mipango yote inaenda vizuri na siku si nyingi atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kulipa deni la video alilonalo kwa mashabiki wake.

Kwahiyo tumefanya tena opportunity nyingine tumepata tayari namshukuru Mungu tumeshapanga kila kitu.

Kwa kuonesha kuwa anawajali na kuwaheshimu mashabiki, King Kiba hakusita kuwaomba msamaha kwa kuchelewa kufanya video ya ‘Chekecha’, wimbo ambao una karibia kufikisha miezi mitatu toka ulipoachiwa mwishoni mwa February.

Mimi nataka kuchukua nafasi hii kukuomba samahani, mafans wangu wote na wapenzi wa muziki, najitahidi sana lakini sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake.”

Aunty Ezekiel: Sinta Mzika Wema, Familia ya Wema Yacharuka yasema Heri Kajala Kuliko Aunty

$
0
0
‘Nikifa usije kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki au majirani wakaapishana kwa maneno hayo, walitafutwa wazee wenye hekima ili kuondoa laana hiyo.

Sasa, hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo sababu, Ijumaa Wikienda lina kila kitu!

AUNT BILA KUUMA MANENO

Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.

KIASA CHA KAULI

Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.

 MSIKIE AUNT ‘LAIVU’

Ijumaa wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?

Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.

“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.

 AANZA KUFUNGUKA

”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.

 ILIKUWA UTANI, IYOBO ATAJWA

“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,” alisema Aunt.

 FAMILIA YAWEKA KIKAO

Kufuatia vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni familia ya  Wema inadaiwa kuweka kikao na kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia kuwa, urafiki wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini hautadumu kwa sababu ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.

Chanzo makini kutoka katika familia ya Wema kimelipenyezea ubuyu Ijumaa Wikienda ambapo kilitiririka:

“Mama Wema kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema kwa sasa hataki tena kumwona mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu ni mnafiki.

 MAAZIMIO YA KIKAO YAFIKA KWA WEMA

“Maneno hayo ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa Wema, akawaelewa na kusema hana haja tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee nini maana hakuna anachomsaidia.”

 AUNT TENA, AMWANIKA WEMA SASA

Aunt alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema na jinsi staa huyo alivyoyapokea, alisema:

 “Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.

“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.

“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.

“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao.

 WEMA AZIDI KUCHAMBULIWA

“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”

 WEMA NAYE ATEMA NENO

Baada ya Ijumaa Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:

“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.

“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”

Aunt  ‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema akiamini Aunt  ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu wake hao.
Chanzo:Global publishers

Wastara Amuanika Mbaya Wake..Kumbe Kisa ni Kuolewa na Marehemu Sajuki

$
0
0
Baada ya kipindi kirefu cha tetesi ya staa wa filamu Wastara kuhofia maisha yake, akihisi upo mpango wa kumuangamiza kwa njia mbalimbali ikiwepo ajali, staa huyo amesema tetesi hizo ni kweli na amekwishazitolea ripoti polisi.

Msanii huyo amekiri kupitia eNewz kuwa, ni kweli yupo katika tishio la maisha yake, mhusika mkubwa wa hilo akiwa mwanaume ambaye alikuwa na mahusiano yake wa zamani ambaye hawana maelewano mazuri naye.
Wastara amesema kuwa, amekuwa na historia ya mahusiano mabovu na mtu huyo na kupelekea kuachana naye, na kitendo cha yeye kuolewa na marehemu Sajuki kikiwa sababu ya kuamsha ugomvi upya, na hapa anaeleza mwenyewe mambo yalivyoanza na kujikuta katika hali hiyo na vilevile hatua alizochukua, Wastara.
Wastara amesema kuwa, mwanaume huyo amekwishamtamkia wazi kuwa anahusika na moja ya ajali iliyomkumba, akitumia mambo ambayo ameyaita ya kiswahili kutaka kumuangamiza, jambo ambalo amekwishalitolea ripoti polisi takriban miaka 5 iliyopita.
Staa huyo amesema kuwa, chochote ambacho kitampata kwa mujibu wa maelezo aliyotoa kwa mwanausalama kutokana na vitisho vya bwana huyo, moja kwa moja vitakuwa vimemuweka hatiani, akisisitiza kuwa ana imani kuwa maisha yake yanasonga kwa mipango ya Mungu ambayo mwanadamu hawezi kuvuruga.

Shilole Ajitetea, Adai Amesikitishwa na Mtu aliyezoom na Kumpiga zile picha Mali zake zikininginia...

$
0
0
Baada ya picha chafu za Shilole kusambaa mtandaoni hadi kupelekea BASATA kumuandikia barua ya onyo, muimbaji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ amevunja ukimya.

Shilole amesema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati akitumbuiza Ubelgiji hivi karibuni, kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.

Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.

“Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion .” Alisema Shishi kupitia 255 ya Clouds Fm.

Ameongeza kuwa amesikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.

Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.

Kuhusu kama amepokea barua ya kuitwa kujieleza kutoka BASATA, Shishi amesema kuwa hajapokea barua hiyo kwasababu bado yuko Ubelgiji.

Maoni:Unamshauri Nini Aunt Ezekiel Kuhusu Ugomvi na Wema?

$
0
0
Kwa kuangalia historia ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ni zaidi ya marafiki ambao walikuwa maswahiba walioshibana kiasi kwamba hakuna mtu anaeweza kujua kama leo watakuwa maadui. Na urafiki huu ulikomaa zaidi pale Madame Wema alipokuwa amerudiana na Diamond Platinumz kiasi kwamba hata safari za nje za Wema na Diamond na Aunt nae alikuwa anasafiri na hatukujua alikuwa anasafiri kwa gharama ya nani.

Kwa ukaribu huu wa Wema na Diamond kulimfanya Dogo wetu Moses Iyobo kupata bahati ya mtende kilaini kwa dada yetu Aunt Ezekiel ambaye walianza mapenzi chini chini na kuficha kila walipoulizwa kama wana uhusiano ila alikataa, ila mwisho ya yote yalikuja julikana baada ya Aunt Ezekiel kupata ujauzito.

Sasa ikawa hawana jinsi lazima waweke wazi. Hatujui kama Madame Wema au Diamond alitumika kupiga pande kwa hawa wapenzi wawili ama la ila chanzo ni yeye kuwa na ukaribu na Diamond na Aunt Ezekiel ndo kukampa mwanya Moses Iyobo nae kuwa na uhusiano na Aunt Ezekiel.

Sasa leo kuna kamtihani kamemkuta Aunt Ezekiel kwa kuwa Madame Wema ameachana na Diamond Platinumz, na kuachana kwao kumetengeneza mgongano mpaka kupelekea kuwa na Team Diamond& Zari na Team Wema. Kwa kuangalia kwa umakini zaidi Aunt Ezekiel anakaribia kupata mtoto na Moses Iyobo na Upande mwingine bado yuko na Uswahiba na Wema Sepetu.

Aunt Ezekiel anapata mtihani kwa kulazimishwa na Wema kuwa bado awe kwenye Team Wema wakati yeye tayari ana usiano na Moses Iyobo ambaye ni Dancer wa Diamond na ukiangalia kwa umakini kila itakavyokuwa lazima Moses ndo anauhusika na kila kitu kwa huduma za Aunt Ezekiel.

Sasa ukiangalia kwa mbali kuna ugomvi wa chini chini kati ya Wema na Aunt Ezekiel ikisemekana kama Wema hataki Aunt Ezekiel amsapoti Diamond ila naamini Aunt Ezekiel anafanya ivi kwa mapenzi ya mpenzi wake Moses Iyobo.

Ukiwa kama wewe mdau unaweza mshauri nini Aunt Ezekiel;

1- Aaache kumsaport Diamond kwa kulinda urafiki wake na Wema?

2- Aache kumsaport Wema ali ajenge uhusiano zaidi na Moses Iyobo na kwa faida ya mtoto wao?

3- Au afanya uamuzi gani kwa hawa wahasimu wawili ili aweke mambo sawa kwa pande zote mbili.

Tumshauri dada yetu please bila matusi.

By Abatmwe on JF

Majambazi Wakamatwa Wakitaka Kuiba Katika Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori-Dar

$
0
0
Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar.

Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.

Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar.


Wema Sepetu And Aunty Ezekiel End Their Hostility And Become Friends Again.

$
0
0
Since last week there have been constant news about Wema Sepetu and Aunty Ezekiel's friendship coming to an end.

Even yesterday some newspapers, and blogs had news of the two celebs swearing not to bury each other when they die.

But according to reports yesterday evening Wema and Aunty ended their enmity which was growing to dangerous heights.

One of their close friend called Junaithar arranged a meeting for the two to reconcile and they agreed. They even ate and drink together and these are pics when the two met.

Junaithar is the one who made sure VJ penny and Wema forgot their hostility and became best friends again.

Mtangazaji Fredwaa Anapotea Ajitatmini Upya Pale Clouds, Pesa si Kila Kitu

$
0
0
Licha ya kwamba mimi si msikilizaji sana wa clouds fm ila tangu enzi za Masoud kipanya, Phina Mango na Hando nimekuwa ni msikilizaji wa kipindi cha power breakfast.

Sasa shida yangu ni huyu kijana Ferdwaa ambaye nikiri wazi ninamkubali sana na wakati yupo RFA nilikuwa sikosi kipindi chake cha asubuhi na vodacom lakini tangu ameamia clouds fm ni kwamba amefunikwa haswaa na Pj na Hando na hata msikilizaji huwezi kubaini kama Ferdwaa naye yupo.

Ushauri wangu kwa clouds media mnauwa talent ya Fredwaa yule Jamaa ana uwezo wa kuhost kipindi peke yake lakini kwa sasa pale mmekosea Hando na Pj wanambana, najua Boss Ruge unasoma hapa mbunieni kipindi chake Fredwaa mnauwa kipaji chake.

By Matola-JF

Yanga Yafanya Maamuzi Magumu ..Yawatema Hawa Wachezaji Saba

$
0
0
BENCHI la ufundi la Yanga chini ya Mdachi, Hans van Der Pluijm, limedaiwa kufanya maamuzi magumu ambayo kwa namna moja au nyingine, yatawashangaza wadau wengi wa klabu hiyo.

Imedaiwa kuwa kocha huyo ambaye ameiongoza Yanga msimu huu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, amependekeza wachezaji saba kuondolewa kutokana na mchango yao finyu msimu mzima, akiwemo mchezaji mkongwe wa klabu hiyo, Jerry Tegete na Danny Mrwanda aliyetua katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akitokea Polisi Moro.

Habari za kuaminika kutoka Yanga zinasema kuwa mbali na Tegete na Mrwanda, nyota wengine ambao wamepitiwa na panga la kocha huyo mwenye msimamo mkali ni Nizar Khalfan, Rajab Zahir, Hussein Javu, Edward Charles na Hassan Dilunga.
Habari zinasema kuwa walio na mikataba watatolewa kwa mkopo, ambao ni Dilunga na Edward

“Kwa hali hiyo wachezaji hao hatutakuwanao tena msimu ujao kutokana na kocha kapendezeka waachwe waende wakatafute maisha sehemu nyingine ili nafasi zao tuweze kusajili wengine wenye uwezo na sifa za kuwa Yanga.

“Anataka msimu ujao kikosi chake kiwe chenye wachezaji wa ushindani ambao wataisaidia Yanga kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu na ile ya kimataifa, hivyo baada ya tathmini yake ya msimu uliomalizika, ameona nyota hao  hawatakuwa na msaada, ndiyo maana amewependekeza waondoke zao,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa juu ya jambo hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema kuwa si muda wa kuzungumzia suala hilo na kwamba muda ukifika wataweka wazi kila kitu.“Tuvumiliane katika hili, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Tiboroha.Alipotafutwa Tegete jana mchana alijibu kwa kifupi: “Mimi sijazipata hizo taarifa (za kutemwa).” Kisha akakata simu.

Download Wimbo Mpya wa Mkali wa Chorus Bongo G-Nako Wara Wara wa Weusi -Sichezi Mbali

$
0
0
Mkali wa Chorus Bongo G-Nako Wara Wara wa Kundi la Weusi Sasa Ameamua Kuja Kivyake Bila Kumshirikisha Mtu yoyote na Kuangusha Bonge la Wimbo....Sikiliza ama Download Hapa Kupitia Rubega.com


Picha: Siku Mashetani Yangu Yakinipanda Nitawambia Kitu-Kitale

$
0
0
Hii ni moja ya picha iliyosabisha mafuriko ya COMMENTS na LIKES  mtandaoni. Hawa ni mastaa wa hapa Bongo, Kitale ‘mkudesimba’ na Vj Penny.

Kitale alibandika picha hii kwenye ukurasa wake na kuiandikia “Kuna siku mashetani yng yakinikalia vibaya nitawambia kitu” kisha kum- tag penny na kumalizia naneno haya….UfundiPelekaVeta ….MapenziAuPesa.

Mashbiki wengi walishusha komenti za kumtaka Kitale awambie hicho kitu, huku wengine wasimshauri achukue mrembo penny kwani watatengeneza bonge la COUPLE.

Kiufupi kila mtu aliandika lake lakini hadi sasa Kitale hakujibu komenti hata za mashabiki hao, tuendelee kuisubili hiyo siku mashetani yake yakimpanda.

Mzee wa Ubuyu

Mume wa Zari Ivan Anaswa Kwa Shosti wa Zari Ambaye ni Model Maarufu Uganda

$
0
0
Kampala, Uganda
Habari kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba aliyekuwa mume wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kunasa penzi la shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo aitwaye Stella Nankya, Ijumaa Wikienda limetonywa.

Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.

Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.

“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti moja la nchini Uganda.

Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.

Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.

Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:

“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”

Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.

Wastara: Hakuna na Mwanamke ‘Used’ Kama Hafai Kwako Kuna Mtu Kwake Huyo Mdada ni Malkia

$
0
0
Utamuacha Mwanamke fulani kwa kashfa zote na kejeli za kila namna kwamba hafai na haoleki ILA Mwanaume yule atamchukua na kudate nae na pengine atamuoa na wataishi kwa furaha na kuzaa watoto,atasahau hata kama uliwahi kuwa Boy wake na kashfa zako...Kapata Perfect Match yake....Mwanamke fulani ataachwa na wewe utakutana nae na kumpokea,na pengine utamuoa na kuishi kwa amani. Umepata Perfect match yako..Hii inaitwa Love Circle...

Hakuna Mwanaume wala Mwanamke 2nd hand/Used kwamba hafai...Kama hafai kwako kuna mtu kwake huyo mdada ni Malkia...Kama hafai kwako,kuna mdada anamtamani amfanye awe mfalme wake..

Binadamu hana Mshale wa kuonyesha kilomita ngapi katembea au ana listi ya watu mia ngapi!
Kuna watu wametumika kwelikweli,shusha engine mara 6 na kumwaga oil nyeusi,ila wameolewa na kutulizwa ndani..Wewe unayejiona mpya mpya unanukia Nylon bado unamanga manga...Haijalishi wewe ni Mpya au Used,when ur perfect match arrives, everything else about Past will be history!

By Wastara on Instagram

Picha: Diamond amfanyia shopping mwanaye mtarajiwa Uingereza

$
0
0
Diamond Platnumz anajivunia kuwa baba mtarajiwa, ndio maana ameanza mapema kumuandalia mazingira mazuri mwanaye mtarajiwa kwa kumnunulia vitu mbalimbali na kushare na followers wake wa kwenye mitandao ya kijamii.
“Anything for my little angel…” ndio maneno aliyoandika kwenye picha hii.
Muimbaji huyo wa ‘Nasema Nawe’ amabye weekend iliyopita alikuwa na show jijini London, ameshare picha akifanya shopping ya vifaa vya mtoto wanayemtarajia kumpata na Zari The Bosslady.
mondi shopping5
Zari naye alishare picha zingine za Diamond Facebook:
mondi shopping2
“Current situation in London…… damn he thinks ‘she’ should have more than one”-Zari
mondi shopping3
“The excitement tho”– Zari

Photos: Faiza Ally Spends Good Time With Her Alleged New Millionaire Boyfriend In Dubai

$
0
0
After staying lonely for months following her separation wit baby daddy and Mbeya Mjini member of Parliament Sugu Joseph Mbilinyi, finally actress Faiza Ally is in a relationship again. Faiza has been in Dubai since last week and sources say that she is there to see her new boyfriend who is said to be a millionaire.

"Faiza is in Dubai to see her millionaire boyfriend she got recently" the source told Swahiliworldplanet

We tried to reach the controversial celeb and when asked about it she said that it is true she is with her new man in Dubai but she denied her boyfriend being a millionaire, she also said that their relationship isn't serious yet so when it becomes mature everyone will know all about him.

Anyhow, congrats to them and we pray for you Faiza and your boo..............

Source:Swahili Planet

Hajui Kama Nimeoa, Penzi Limenoga Nataka Kusema Ukweli Lakini Sujui Nianzie Wapi

$
0
0
Sijawahi kuwa mzinzi tangu nimeoa miaka 5 iliyopita. Hadi hivi karibuni nilipoanzisha uhusiano na binti mmoja..

Tulifahamiana kikazi, yeye yupo idara ya uhasibu. Huja kazini kwangu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya transaction mbalimbali.

Tukazoeana na kuwa wapenzi. Kiukweli mambo yalienda haraka haraka sana na aliingia mazima mazima kiasi kwamba hata kila nilipotaka kumwambia ukweli najikuta nashindwa maana alikua resi ile mbaya.

Ikawa ni mahaba niue, kila tukitoka kazini tupo wote sehemu, weekend tutaenda cinema, beach etc. Yaani ghafla bin vuu anaongelea ndoa. Kila siku ya Mungu lazima agusie ndoa itakua vipi.

Wakati mwingine anaingia Google kusearch magauni ya harusi na viatu na maids wake watavaa nini siku hiyo. yaani nabaki mdomo wazi maana moyoni najua nimeshaoa siku nyingi.

Kila akianzisha hizo story za magauni najitutumua sasa nianze kumwelewesha kwamba nimeoa basi hunikata kauli haraka na kuendelea kusema mambo ya ndoa yetu kwamba napendelea ukumbi gani ndo mzuri.

Sasa tuna miezi miwili ameanza kuongelea suala la kupata mtoto ananiuliza kuwa naonaje akibeba mimba kabisa tufunge ndoa wakati ana mimba. Basi humjibu kuwa tusubiri kwanza asibebe kabisa mimba, nikijibu hivyo anakua mkali anauliza "hiyo mimba unaibeba wewe au mimi?" Mimi nabaki kimya.

Kwa kweli namuonea huruma kwa mawazo aliyonayo, mimi niliingia kwenye huu uhusiano kubadilisha mboga tu and I thought it would be a temporary thing. Kiuchumi yupo vizuri balaa simpati hata kwa dawa.
Ukifika alipopanga thamani za vitu alizonazo ndani ni za gharama sana, na nyumba ni ya kisasa, ana miradi mingi mbali na kazi na alinipeleka anapojenga nyuma ni kama imeisha bado ukuta tu wa nje.

Tatizo pekee ninaloliona ni kuwa huyu binti time is ticking very fast against her age, yupo kwenye mid 30s; somewhere between 30-36 years. Hivyo anadhani amechelewa.

Anasema amepoteza muda mwingi kwenye relationship iliyopita iliyochukua 7 years na jamaa akaoa mtu mwingine na kumuacha yeye, hivyo anasema hataki tena long relationship. Ameshaniunganisha na ndugu kibao. Kila wiki natambulishwa kwa ndugu mpya.

Wakuu, naona huruma Kubreak hii news kuwa nilishaoa. Ingawa nampenda moyoni lakini pia nimechoka maisha ya digi digi ninayoishi maana nikiwa home kwangu usiku lazima anipigie simu na anaongea zaidi ya nusu saa na hapo tumetoka kuonana jioni. Basi najifanya naenda dukani kwa mangi kununua kitu na kupiga stori ili wife asishtuke kuwa naenda kuongea na simu.

I think wengi mnajua maisha ya Ku,cheat yalivyo magumu ni utumwa, ni jela ya nje.

Wakuu nianzeje kumwambia ukweli anielewe? Au nitume mtu mwingine ndo amwambie kama anampa umbea vile?

I need to get out of this mess maana wife somehow ameanza kushtukia mwenendo wangu.

Please, advise

Huyu House Girl Anaelekea Kuvunja Ndoa yangu Sasa

$
0
0
Nipo kwenye lindi la mawazo kuhusu housegirl wetu ambae nilimpa mimba kwa bahati mbaya. Mimi nina mke na familia yangu huyu binti sasa anataka nimfanyie kitu mbaya maana mimba hataki kuitoa na kuondoka kagoma na muda unazidi kwenda mwishowe itaanza kuonekana

Sasa hivi anashinda kwenye TV tu na remote kazi hataki kufanya yote tisa, kumi sasa juzi Jumamosi usiku katumwa kazi na wife unaambiwa kamfanyia wife kiburi kisichosemekana katumwa akalete kitu dukani akakataa live akaambiwa akapike akakataa, akaanza kuongea kwa mafumbo huku akienda chumbani mimi nilikua bar kwenye mambo yangu.

Mdogo wangu wa kike ndio akazifanya zile kazi nyumba imekua very tense bomu linaweza kulipuka any time wife anamwandalia pesa zake aweze kuondoka maana kwa mawazo ya wife anadhani kwa kuwa hatujamlipa mshahara miezi mitatu mfululizo ndio maana analeta kiburi kumbe ni mimba.

Sijui niongee na Chale akodi wavuta bangi! Wakuu kati yenu kuna mwenye jawabu ya hili tatizo? Hivi kwanini huyu binti ananifanyia hivi!? Kwanini asikubali kupokea hela akaondoka, kila nachomwambia hataki, anasema eti nitamwacha, sasa Mimi simtaki tena, kwa nn tunalazimishana?

Wanaume wapo kibao why me? Wangapi wametoa mimba hawajafa? Mke wangu mwenyewe alishika mimba huku tuna mtoto mchanga wa miezi sita mbona aliitoa na hakufa? Sasa yeye ni nani hasa asitoe, mi naona nikodi wahuni tufanye elimination method.

Wadau nyumba inaungua naomba kwa imani zenu wote mniombee naahidi sirudii tena nikipona na janga hili maana wife wangu hanaga mchezo kabisa na mambo ya uzinzi msg tu ya simu alitaka kuniacha huko nyuma.Kuna mganga anaeweza kubadilisha matokeo ya tatizo kama hili?

By Navin-govind-JF
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images