Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104743 articles
Browse latest View live

DID You Miss Agness Masogange Killer and Hot Photos? These are The New Ones for Men Only...

$
0
0

 DID You Miss Agness Masogange Killer and Hot Photos? These are The New Ones for Men Only...



PHOTOs!! Who was calling ZARI ‘Cucu’? She is still the s*xiest pregnant woman in East Africa

$
0
0



PHOTOs!! Who was calling ZARI ‘Cucu’? She is still the s*xiest pregnant woman in EA

Nuh Mziwanda Atimkia Kuishi Kwao..Hakai Tena Kwa Shilole...Shilole Afunguka Sababu ...

$
0
0
Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani umemfanya msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda kuondoka nyumbani kwa mpenzi ambaye ni msanii,Shilole ili kumpisha mpenzi wake afunge kwani hawajafunga ndoa.

Shilole ameyazungumza hayo wakati akizungumza na Clouds Fm,ratiba yake nzima ya mapishi kwenye mwezi Mtukufu na kusema kuwa mwezi huu wa Ramadhani ameacha kufanya vitu vyote vya starehe na ndiyo maana hata mpenzi wake Nuh ameondoka nyumbani kwake ili asiharibu funga yake.

‘’Nuh ameondoka nyumbani kwangu amerudi kwao ili asiharibu funga yangu,’’alisema Shilole

Nora: Bongo Movie Wamesharibu Sanaa ya Uigizaji Tanzania...Huwezi Kaa na Wazazi Wako Ukaangalia Movie Wataharibu Hali ya Hewa tu

$
0
0
MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amedai kuwa ‘Bongo Movies’ wameharibu sanaa ya  uigizaji hapa Tanzania. Nora amefunguka hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa lokesheni wakishuti movie.

"Naipenda kazi yangu na ninaiheshim sanaaaaa hii ndo sanaa ilionikuza mpaka leo na bado nakua nayo Mungu afungue heri zake lol tunajua kukomaaa ila nais Mungu ndo ameandika.

Nitatumia kipaji changu akili yangu kuwatumikia Watanzania pale palipokua apajaenda sawa nawaakikishia hiii kitu imewabeba wooooootee kiasi kwamba utatamani kumwita mama yako mnakaa mnajifunza kitu unakaa na baba yako mnaangalia sio kama movie nyingi zilizopo hukai na wazazi wako mkaangalia mana unajua wataharibu tuuuuu ila hii sio movie manaa bongo movie wamesharibu sanaa ya uigizaji tanzania," Nora ameandika.

Una maoni gani juu ya mtazamo huu wa Nora?

Wema Sepetu, Sabuni Utakayoogea ndio Utakayonukia

$
0
0
Kwako Wema I. Sepetu ninakuandikia maneno haya, uyashike, uyakumbuke siku zote za maisha yako na kuyasimamia ili uweze kufika katika kilele cha mafanikio ambacho weengi hutamani kufika lakini wanaishia kupiga mbizi kwenye Kokoto.

Dunia nzima kwa sasa kumekuwa na mlolongo mkuubwa sana wa wasanii na hata watu wanaoishi kiujanja ujanja ili kufanikisha malengo yao kimaisha.

Kumekuwa na mlolongo mkuubwa sana wa vijana ambao wanaingia kwenye tasnia ya sanaa pasipo kuwa na Elimu wala weredi wa Sanaa hio, lakini goal lao kuu lipo katika kuusaka umaarufu na kuwa na majina makubwa.

Ukichungulia kwenye boti ya wasanii wa filamu utakutana na lundo la vijana kwa wazee ambao wamechumpa huko ili wapate shavu na siku moja wawe miongoni mwa nyota katika medani hio.

Ukija kwenye sanaa ya uimbaji, utakutana na lundo la Vijana kwa wazee, na wote hawa wanatamani siku 1 magazeti yapambwe na habari zao.

Kundi kuubwa la vijana wa kike kwa kiume wamekunja madaftari na kuachana nayo pia kuipa elimu Kisogo na kujikita katika sanaa. Imefika hatua kijana anatiririka mistari ya wimbo katika mtihani wake wa mwisho wa kidato cha 4... Hii yote ni katika kuusaka umaarufu ambao ndio lengo kuubwa kwa mlio wengi wenu.

Mifano ipo mingi. Ila kwa leo nataka nikupe shubiri na ujikaze umeze tu maana ndio itakayokuponya.
na kama ukikaidi basi ukae ukijuwa ipo siku utakwenda ogelea baharini na kopo.

Rekodi zinaonesha Wema ulipata kuwa Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kufanikiwa kukwea pipa mpaka Warsaw Poland kwenda kuliwakilisha Taifa la Tanzania katika kinyang'anyiro cha Miss World.

Ushindi wako haukuwa msafi kama Sanda kwani kuna utata ulijitokeza kati yako na mwanadada Jokate ambae kuna kundi la watu mpaka sasa hawataki kuamini kuwa ulimgaragaza kihalali Mrembo huyo.

Nikitafakari zaidi naona kuwa Wema si Miss Tanzania wa kwanza au wa mwisho ktk Taifa hili. Ni dhahiri shahiri kuwa kuna Mamiss walitangulia kabla yako na kuna wengine walifuata baada yako lakini wanaishi maisha ya heshima na taadhima. Wanaitumikia jamii na kufanya kazi zao halali na zenye kuwapatia mapato halali.

Mifano miwili tu kwanza nianze na Mama ya Mama HOYCE TEMU na pia nimtaje ANGELA DAMAS ambao wamesimama imara na kufanya mambo makubwa katika jamii na pia wamekuwa wakikusanya na kujiingizia mapato halal.

wanasema starehe ya Mbwa ni kuukalia mkia wake lakini Wema wewe tangu ulipokuwa Miss mwaka 2006 mpaka hivi sasa umekuwa ni mtu wa kuusaka umaarufu kupitia kila njia ambayo unaona itasaidia kukubakiza midomoni mwa watu. Umekuwa ni mtu wa kucheza na vyombo vya habari ili uweze kulibakiza jina lako on top...

Kwa hili umefanikiwa mno, umefanikiwa jina lako kudumu katika midomo ya watu, umefanikiwa jina lako kudumu kwenye baadhi ya vipindi vya Redio na Runinga, na kama hio haitoshi Mama nakupongeza kwa kufanikiwa kulidumisha jina lako kwenye vichwa vya habari vya Magazeti, japo kwa akili ya kikubwa ni wazi kuwa hapa unamaliza kuni kwa kuchemsha mawe.

Lakini je watu uliowalenga walijadili jina lako wana tija yoyote ama wana faida yoyote wanakupatia?
Au hivyo vipindi vya redio na runinga vinavyotumia jina lako kusukuma siku je vinawalenga watu wenye tija katika jamii ambao wanaweza wakakuunganisha na taasisi fulani au NGO ili uweze kuanza kufanya makusanyo halali ya pesa?

Hebu tafakari kwa mapana je hayo magazeti ya marangi rangi ambayo kila Alfajiri yanaibuka na habari kukuhusu wewe je yanasomwa na watu makini au je yamewekwa kwenye kundi gani katika jamii?

Sitaki kuchuma dhambi kwa kujiaminisha kuwa eti wewe ni msichana mreembo sana so utabakia on top for the rest of your life.

Macho yangu yalipata kumuona Aminata Juma mwishoni mwa miaka ya 90 akisoma Sekondari ya Jangwani na kisha Zanaki.

Aminata alikuwa Mashalaah alieumbika katika kila Idara na akili ya Darasani pia, aliposimama Aminata basi Kajala hakuthubutu kusogea na mara zote aliishia kulekule jeshini Jitegemee.

Alipofungua kinywa chake Aminata na kuongea Lugha yoyote ile iwe Lugha mama ya Taifa ama iwe Lugha ile ya kigeni basi Amina Chifupa hakuthubutu hata kupiga chafya...

Sitaki na sintoruhusu kuaminishwa kuwa wewe Wema ni mzuri zaidi ya aliepata kuwa Msomi wa Chuo Kikuu kitivo cha Sheria Sylvia Bahame ambae alipata pia kuwa Miss Tanzania mwaka 2003, huko ni sawa na kumfunika Nyuki kwa tenga.

Sifa unazozisaka sasa na umaarufu unaoufurahia sio kitu cha msingi kwa mtu makini. Kumbuka umesha jidharirisha saana ili mradi tu jina lako libaki midomoni mwa watu. Familia yako imeshajadiliwa saana na wewe umelifurahia hilo ili mradi tu ubaki on top.

Wenzio wakaenda mbaali zaidi na kumdhalilisha mpaka Mama yako kwa kubandika picha kwenye mitandao akiwa mtupu.

Najuwa huu ni mfumo mlionao wasanii wa leo kwa kupenda kutokelezea kwenye headlines katika Media tofauti ati mkiamini kuwa ndio mnauza na mtadumu milele...lakini mwamuzi wa kweli anaeweza kukudumisha juu milele ni bidii katika kazi yako halal.

Wema wewe tangu umejikita kwenye tasnia ya maigizo huna movie hata 1 ambayo unaweza kuitaja kuwa ni bora na ipo kwenye viwango vya ubora kwa baadhi tu ya sinema za hapa Afrika ya Mashariki.

Wema wewe huwezi kujifananisha na wasanii wa Luninga kutoka hapo Kenya, lets say wasanii walioshiriki katika tamthiria ya Sumu la Penzi.

Kama hio haitoshi Wema wewe huna kipaji cha kuigiza kumzidi msanii yeyote wa kike katika tamthiria ya Siri ya Mtungi.
Hivyo ni wazi kuwa huna

Tofauti na mkia wa Mbuzi...haustiri uchi na wala haufukuzi Nzi.

Jipange sasa;

Hakuna binadamu vigeugeu katika hii Dunia kama wabongo. Na kuna harufu ya wabongo kukuchoka Mama kwa skendo zako za kujitengenezea ili ubaki ukijadiliwa bila faida.

Alikuwepo MR NICE;
Nadhani unakumbuka ni jinsi gani alishika na kubamba jamii.
Lakini leo hii anakesha Corner Bar akiomba (200) mia mbili ili acheze pool table.

Alikuwepo SINTA;
Eskimo huyu alitamba katika maigizo ya Runinga, lakini zake zilipopita zilikwenda na hazikurudi na hazitorudi ng'o.

Pakawepo na JUMA KASIMU maarufu kama JUMA NATURE;
Yaani aliishika Bongo kiasi kwamba chochote alichokiimba kilibamba.

INSPEKTA HAROUN na RAY C;
Hakika walitamba mno, lakini leo hii wabongo wamewachoka na kuwaona kama kopo la chooni. Kwa kifupi wamepotea kama harufu ya ushuzzi.

Sasa Mama jitathmini upya, maana painukapo leo basi patainama Kesho, je kwa miaka takriban 10 ambapo umedumu midomoni mwa watu kwa series yenye episode nyiingi za kujitengenezea wewe mwenyewe je umepata faida ipi? Au ndio yaleyale ukipenda vitamu basi utahalalisha vya haramu.

Alinena Gang Chomba "If you don't change your self, changes will change you".

THINK BIG!

Shifta/JF

Kifo cha Tajiri Mtoto Jimmy Chazuo Gumzo Mjini

$
0
0
Kifo cha huyu kijana mdogo (21) aliyekuwa milionare ,kimezua gumzo ya aina yake uko instagram siku ya leo. Hakika msiba wake umewateka watu wengi mno ikiwemo mastaa wa bongo movie na bongo fleva, baadhi ya mastaa walioguswa na msiba huo ni jokate, diva, ommy dimpoz,wema sepetu, martin kadinda, young dee, bob junior na mastaa wengine kibao bila kumsahau baba angu mdogo LEMUTUZ nae aliguswa kama kawaida yake.

Chanzo cha kifo chake inasemekana ni ajali ya gari aliyoipata uko maeneo ya mbezi beach akiwa ndani ya gari lake la kifahar aina Mercedes benz , R.I.P JIMMY japokuwa sikujui

MWENYE KUJUA WASIFU WA MAREHEMU PLEASEEEE ,maana sio kwa kuvunja rekodi kiasi kile, alikuwa anafanya ishu gani mpaka awe maarufu sana especially baada ya kifo chake? maana mbea mie apa nimefeli, matajir wenzie akina lemutuz mje mtupe wasifu wa marehemu. R.IP aiseh, umeenda ukiwa mdogo sana...

Nape Amshambulia Freeman Mbowe........Amtaka AJIUZULU Maana Amekiabisha Chama Kwa Hukumu Aliyopewa.

$
0
0
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kujiuzulu uenyekiti kwa kile alichosema amekiaibisha chama kwa hukumu aliyopewa hivi karibuni.

Mbowe alihukumiwa hivi karibuni kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kutiwa hatiani na mahakama mkoani Kilimanjaro kwa kosa la kumpiga Msimamizi wa Uchaguzi mwaka 2010.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Karumwa, wilayani Nyang’hwale mkoani Geita, Nape alisema miongoni mwa sifa za kiongozi, ni kuzuia hasira na kuwa na kifua kigumu.

Alisema kwa kulinda heshima yake na ya chama chake, Mbowe anapaswa kujiuzulu.

“Jana (juzi) Mahakama ya Hai mkoani Kilimanjaro ilitoa hukumu ya kumfunga jela mwaka mmoja Mbowe au alipe faini ya Sh milioni moja. Yeye na chama chake waliamua kulipa faini ili asiende jela,” alisema Nape.

Akisisitiza kuwa alichofanya Mbowe ni aibu, Nape alisema, “mtu mzima ukiwa umejifunga taulo na mtoto akaja kuichukua hutakiwi kumkimbiza mtoto badala yake unatakiwa kuchutama.

“Ukiamua kumkimbiza mtoto na wewe unaonekana akili yako kama mtoto. Yeye ni kiongozi wa chama, alitakiwa kuonesha uwezo wake kama kiongozi, kutumia hekima na busara dhidi ya msimamizi huyo wa uchaguzi badala ya kumpiga hadharani.”

Nape alishutumu siasa za vurugu sanjari na kutumia vijana kwa maslahi ya viongozi wa juu. Alitaja Chadema kwamba kimejijenga kwenye misingi ya ubabe jambo alilotakavijana kuwa macho na kujihadhari na maandamano.

Michepuko Embu Ooneeni Huruma Ndoa za Wenzenu..Someni Hapa Jinsi ya Kuandika Meseji Kwa Jamaa yako ili Hata ikisomwa na Mkewe Isiwe Shida

$
0
0
Embu hli suala liangaliwe vizuri ili kutosababisha matatizo ktk ndoa za watu.Jana nimetoka kazini, nikakatext ka mchepuko ka kitambo kidogo.

Mimi: Mambo vipi!
Mchepuko: Poa tu mpenzi wangu.

Aisee nikashtuka nikaidelete sms haraka. Nikajiuliza vipi kama ingepokelewa na mke wangu.

Jamani michepuko ifike mahala mjue kabisa tuko na familia zetu, lakini pia tunawajali. Chondechonde msilainishe sms. Andikeni sms ngumu ngumu., ili hata ikisomwa kwa bahati mbaya na wake zetu wasilete shida.

Mfano:
Mimi: Mambo vipi!
Mchepuko: Poa tu we kizibo, uko poa.
Mimi: We bweg*e nini, niko poa. Umekula
Mchepuko: Nile umenipa hela , f*la nini?

Namna hiyo tuendelee dumisha ndoa. Tunawajali sana michepuko.

Asanteni

Wamembaka Mke Wangu, Nimeona Niachane Nae tu'.....Soma Stori hii Utajifunza Kitu

$
0
0

Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.

Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.

Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."

Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.

Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.

Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.

Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.

Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.

Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.

Tulikotoka na mwanamke huyu:-

Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)

Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.

Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.

Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaño yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.

Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.

Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.

Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.

Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.

Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.

Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.

By Nevile pablo-JF

Baada ya Kushambuliwa kwa Kumpa Break Nuh Mziwanda, Shilole Ajibu Mapigo

$
0
0
Baada ya Shilole kutangaza kumpa break mwenzi wake Nuh Mziwanda kwa muda wa mwezi huu mzima, wakitarajia kuendeleza malavi davi yao baada ya kipindi hiki kitakatifu kupita, baadhi ya  mashabiki ambao wanajinasibu kuijua dini  wamekuwa wakimshambulia Shilole kwa maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa kitendo cha kutaka kumrudia tena Miziwanda  bila ndoa sio sawa kwa upande wa dini na wengine kwenda mabli zaidi na kudai hata kazi yake ya sanaa ambayo humfanya kukata maouno pia haifai, kitendo ambacho kimepelekea Shilole kujibu mapigo kwa kuandika jina lake kamili na kusema ni Mungu pekee ndio anamjua na sio binadamu.

“Zuwena Mohamed bint Yusuph anaeyenijua ni Mungu pekee na si binaadam” –Shilole ambaye jina lake ni Zuwena Mohammed alindika hayo mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.

Jamaniu tuacheni kuwanyooshea kidole watu wakati vingiune vinakusonta wewe.

Mzee wa Ubuyu

Green Guard Wampa Kichapo Kizito Mgombea Urais wa CCM Aliyetaka Kutibua Mkutano wa Lowassa

$
0
0
Harakati za makada wa CCM wanaowania urais kusaka wadhamini mkoani zinaendelea kukumbwa na vituko baada ya wanamgambo wa chama hicho, maarufu kama Green Guards, kumshushia mkong’oto Dk Mussa Muzamill Kalokola aliyeingilia mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya mgombea mwingine.

Tukio hilo lililotokea juzi, ni mwendelezo wa matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mchakato huo, yakiwamo ya wanachama kutaka kuchana fomu za mgombea baada ya kunyimwa ‘posho’ na kada mwingine kukosa wadhamini na kulazimika kuomba chakula cha mchana kutoka kwa mkuu wa wilaya.

Katika tukio la Tanga, Dk Kalokola, ambaye pia anadaiwa kushawishi wanachama wasimdhamini mgombea mwingine wa urais, Bernard Membe, alidaiwa kuvamia mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kutaka kulazimisha apewe kipaza sauti kwa ajili ya kuomba wanachama wamdhamini, kitu ambacho viongozi wa CCM wa wilaya hawakukubaliana nacho na alipoendelea kung’ang’ania ndipo Green Guards walipoamriwa wamuondoe eneo hilo.

Picha za video za tukio hilo ambazo zimesambazwa mitandaoni zinawaonyesha vijana hao wa Green Guards wakimsomba mzobemzobe mgombea huyo, kumuangusha kwa kumpiga ngwala na mkoba wake wenye stika ya fomu za mgombea urais, ukionekana kuzagaa chini.

Alipoulizwa  kuhusu mkasa huo, Dk Kalokola alikiri kupigwa katika tukio hilo lilitokea mchana Jumatano ya Juni 17, 2015 alipofika kwenye ofisi za CCM za Wilaya ya Tanga Mjini, siku ambayo mgombea huyo anadai alipangiwa na katibu wa wilaya.

Dk Kalokola alisema baada ya kukabidhiwa fomu za kuomba kuteuliwa na CCM Julai 15 mwaka huu mkoni Dodoma, alikwenda mkoani Tanga ili kupata wadhamini.

“Tulielekezwa kuwa makatibu wa CCM wa mikoa ndiyo watakaotutafutia wadhamini siyo sisi tutafute hivyo mimi tarehe 16 nilikwenda ofisi za CCM kuripoti kwa katibu wa Mkoa,” alisema.

Hata hivyo, alisema hakuweza kuonana na Katibu huyo baada ya kuambiwa kuwa hayupo na amemwachia majukumu hayo katibu wa CCM wa Wilaya ya Tanga Mjini.

Alisema siku hiyo alikuta wagombea wawili waliofika ofisi hizo wakitaka kupewa wadhamini ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali.

“Hawakutaka hata kunisikiliza shida yangu. Mimi nikaamua kutoa taarifa makao makuu ya CCM,” alisema.

Hata hivyo, baadaye saa 12:00 jioni alipigiwa simu na katibu wa CCM wilaya hiyo ya Tanga, akielezwa kuwa aende siku inayofuata asubuhi yaani Alhamisi.

“Nilienda pale nikasaini kitabu nikawaeleza kuwa mimi jana (juzi) nilikuwa na kesi ya kupinga Katiba jijini Dar es Salaam kwa hiyo ningeomba nipate wadhamini siku hiyo hiyo ili nisafiri,”alisema Dk Kalokola ambaye amefungua kesi akitaka Mahakama Kuu itangaze kuufuta mchakato wa kupata Katiba mpya kinyume cha utashi wa chama hicho tawala ambacho kinajisifu kwa kufanikisha mchakato huo.

Dk Kalokola, ambaye wakati anachukua fomu pia aliiponda CCM akidai inaiba sera za wapinzani, alisema siku iliyofuata alikubaliwa na kutakiwa kurejea saa 6:00 mchana.

“Nilipofika nikakutana na vijana wa Green Gurd wakiwa mlangoni, wakanipiga ngwala wakiniambia huu ni mkutano wa Lowasa, nikawaambia kuwa mimi nakwenda kumuona Katibu nina ahadi naye,” alisema.

“Wakaendelea kunipiga lakini kinachonisikitisha vijana hawa wamekuwa wakija nyumbani kwangu kuniomba msaada, hata sare walizovaa niliwanunulia mimi… sasa cha kushangaza wagombea wako 37 kama kila mgombea mmoja siku moja katika kila mkoa tutamaliza lini zoezi hili?” alihoji.

Alisema kutokana na kipigo hicho, hajaweza kupata wadhamini kwenye mkoa huo ambao alipanga kuanzia kutafuta wadhamini.

“Kesho (leo) ndiyo nitaanza tena baada ya kutoka mahakamani juzi (Alhamisi). Hadi sasa sijapata wadhamini hata kwenye mkoa mmoja,”alisema.

Dk Kalokola alisema tukio hilo mbali ya kulitolea taarifa makao makuu ya CCM, pia ameliripoti kituo cha Polisi cha Chumbageni.

Lakini katibu mwenezi wa CCM wa Wilaya ya Tanga, Lupakishyo Kapange alisema kuwa alilazimika kuwaamuru Green Guard wamuondoe kwa sababu mtangazania huyo alikuwa aking’ang’ania kupewa kipaza sauti ili azungumze katika mkutano uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya Lowassa.

“Alikuja hadi nilipokuwa nikitangaza, akataka kuninyang’anya kipaza sauti, nilipomuomba afuate taratibu za kuandaliwa mkutano wake kwa sababu huu ulikuwa wa mtangazania mwingine, hakutaka kunielewa akang’ang’ania nikaamua kuwaita Green Guards wa CCM hapa Tanga wamuondoe,” alisema Kapange.

Katibu wa CCM wa wilaya, Lucia Mwilu alisema Dk Kaloloka, ambaye ni mkazi wa Tanga, alifika ofisini kwa mara ya kwanza Juni 15 wakati wa mapokezi ya Membe na alikuwa akiwazuia wanachama waliokuwa wakitaka kumdhamini mgombea huyo.

“Nilimwita na kumuomba afuate taratibu zilizopo kwenye fomu za wagombea urais, lakini nikakubaliana naye tukutane Juni 16 mchana ili anipe fomu zake hatimaye niweze kumuandalia taratibu za kudhaminiwa. Hakufanya hivyo badala yake akamvamia katibu mwenezi,” alisema Mwilu.

Alifafanua  kuwa tukio la kumondoa Dk Kalokola lilitokea saa 7:50 mchana wakati wanachama wa CCM wakimsubiri Lowassa nje ya jengo la chama hicho la mkoa wa Tanga, lakini waziri huyo mkuu wa zamani na timu yake aliwasili Tanga saa 12:00 jioni.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi wa mkoa, Zubery Mwombeji alisema Dk Kalokola alitaka kutumia jukwaa la Lowassa kuwapata wadhamni, wakati ni kinyume na taratibu za CCM.

Alisema baada ya hapo alikwenda kituo cha polisi kuomba aruhusiwe kutumia jukwaa hilo, lakini ofisa upelelezi alimtaka aende kuonana na viongozi wa CCM Kwa sababu suala hilo haliko chini ya polisi.

Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kusitikishwa kwao na kitendo cha kada huyo kushambuliwa, lakini wamesema baadhi yao walimsihi Dk Kalokola afuate taratibu lakini hakutaka kuwasikiliza.

Taarifa za Mwigizaji JB Kugombea UBUNGE Jimbo la Kinondoni....JB Aongea na Kusema Haya Hapa

$
0
0
Staa mkubwa wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ amekanausha taarifa za kutaka kugombea ubunge jimbo la kinondoni ambazo zimekuwa zikienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

JB ameeleza kuwa japo watu mbali mbali wamekuwa wakimfuata na kumtaka agombee yeye amekuwa akiwashukuru na kuwaeleza kuwa anaipenda sana kazi yake ya uigizaji.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram aliyaeleza hayo akiwa anatolea ufafanuzi kile ‘mrekebishatabia’ alichokiandika kwenye mtandao huo.

@mrekebishatabia,  Na mimi nimezisikia habari hizo eti nataka kugombea k,ndoni. si za kweli ingawa kuna kundi kubwa lilinifata na kunishawishi nigombee lakini niliwajibu nashukuru kwa kunifikiria lakini nafurahia kazi ya uigizaji kuliko kazi nyingine...

Awali ‘mrekebishatabia’ alitoa orodha ya wasanii wanasemekana kuwania ubunge ambapo aliandika;

Kwa mujibu wa jamiiforums hawa ndo wasanii wanaowania kugombea Ubunge 2015
1. Prof Jay- Mikumi
2. Dude- Tabora Mjini
3. JB- Kinondoni
4. Soggy doggy- Segerea
5. Steve Nyerere - Kinondoni
6. Afande Sele- Morogoro Mjini
7. Dokii- Kilosa Morogoro
8. King majuto- Tanga Mjini
9. Shilole- Igunga
10. Kalapina- Kinondoni
11. Baba Levo (haijawekwa wazi)
12. Juma chikoka-Ilala
13. Kingwendu- hajaweka wazi jimbo
14. Wema sepetu- Singida
Mwingine nani??? Mambo yanaelekea yatachanganya hapo baadae. Kila la heri wasanii wote.

Maskin Timu yetu ya Taifa Wenyewe Tunaipenda lakini....Yatuabisha Tena Nyumbani Mbele ya Waganda...God Help us

$
0
0
Maskin timu yetu ya Taifa wenyewe tunaipenda lakini mpira unatutosa hivhivi yan! Juzi tu mashabiki wamewafata mazoezini nakuwazomea na kuwapiga mawe kwa ajili ya wiki iliyopita ilipigwa 3-0 na Misri. Sasa Usiku wa jana mechi imeisha  imepigwa tena na Uganda the cranes bao 3-0. dah lkn tutafanyaje sasa ndio timu yetu tuendelee kuonyesha uzalendo wa kuipenda tuuuu maana ndio cha kwetu.
Japo inauma si eti jaman sijui tatzo nini maskini!

Lowassa Avunja Record Tena, Elfu 58 Wamdhamini Iringa....

$
0
0


Ni katika Safari ya matumaini...!!!

Tulidhania Singida record yake ya wadhamini elfu 22, isingevunjwa, ila Moshi wakavunja kwa wadhamini 33 elfu, siku moja baadae, rekodi ya Moshi ikavunjwa na Mbeya kwa kupata wadhamini 53 elfu...!!!

Jana Iringa, wameweka rekodi mpya ya kutisha, wadhamini 58 elfu...!!!!

Kama hujui kusoma, picha huoni...!? Kama kipofu, huwezi kusoma pia, SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, si unasikia CCM ikichanja mbuga na Lowassa...!!! Chagua Lowassa 2015...!!!

Tuhuma zote dhidi yake zimegonga mwamba kwani ni propaganda na uzushi, kwani Vyombo vyote halali vya Dola....👇👇👇👇👇👇

PCCB, COURTS, DPP, POLICE, TUME YA MAADILI YA VIONGOZI YA UMMA na KAMATI YA MAADILI YA CCM.... hajawahi kutuhumiwa achia mbali kushtakiwa ktk maisha yake ya utumishi...!!!

Pia anapendwa na makundi yoooooote....Waalimu na wafanyakazi, wafugaji, wakulima, wavuvi, masheikh, maaskofu, wakristo, waislam, bodaboda, machinga, UVCCM, BAVICHA, UWT, Umoja wa Wanawake CCM, CCM NEC, Wafanyabiashara wakubwa, wasio na dini, Albinos etc etc...!!

So we made our hearts and minds, we go with Lowassa 2015...!!!

Walioiba mali ya umma jiandaeni...!! Mnajua shughuli ya Lowassa...!!!

CCM thru LOWASSA 2015 ndio chaguo sahihi...!!!

Kocha wa Taifa Stars Maart Nooij na Benchi Lake Lote La Ufundi Watimuliwa Kazi

$
0
0
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku wa kuamkia leo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.

Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.

2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.

3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Tarehe 21 Juni 2015

$
0
0
















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumapili  ya  Tarehe 21 Juni  2015

Mwanamuziki Davido Aipeperusha Bendera ya Tanzania Kwenye Mtandao..Unajua ni Kwanini ? Soma Hapa

$
0
0
Kuna vitu vimeendelea mitandaoni kwa muda mrefu, labda wakati mwingine mitandao ya kijamii huwa haina taarifa za ukweli kuhusu ukweli wa ishu zenyewe.

Staa wa muziki toka Nigeria, Davido aliwahi kuingia kwenye headlines baada ya kuweka post ambazo watu walihisi kwamba jamaa hakuwa na furaha na ushindi wa Diamond Platnumz kupata Tuzo tatu South Africa na pia Idris kuibuka na Ushindi wa BBAHotshots mwaka 2014.

Davido kaweka post hii dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wake @Instagram, ameweka bendera ya Tanzania alafu hajaandika chochote zaidi ya kuweka alama ya love !!

Mkwasa Apawe Mikoba ya Nooij Kuiokoa Timu ya Taifa Stars iliyochoka Kama Mbwa Koko

$
0
0
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfukuza kazi kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mart Nooij pamoja na benchi zima la ufundi la Stars baada ya kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Uganda kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Kufuatia kutimuliwa kwa kocha na benchi zima la ufundi la Stars, kitu pekee kinachotakiwa kufanyika ni kumkabidhi kocha mzawa majukumu ya kukinoa kikosi hicho ambacho kwa sasa kimepoteza mwelekeo kutokana na vipigo vya mfululizo

Charles Boniface Mkwasa ni kocha ambaye anauwezo wa kuichukua timu ya Taifa kwa kipindi hiki cha mpito ambacho tunafikiri nini cha kufanya juu ya haya yote ambayo yametokea. Licha ya makocha wengi hapa nchini kuwa na leseni za ukocha za daraja A, Mkwasa ni kocha ambaye yupo kwenye kazi hiyo kwa muda mrefu akifanya kazi tofauti na makocha wengine ambao wana leseni kama yake lakini wameziweka ndani bila ya kuzifanyia kazi.

Mkwasa ambye kwasasa ni kocha msaidizi wa Yanga chini ya Mholanzi Hans van Pluijm, anauelewa mkubwa wa wachezaji wa Tanzania kuanzia namna ya uchezaji wao na mazingira halisi ya soka la bongo kwa mapana yake. Amesha kutana nao kwenye timu mbalimbali wakati timu yake ilipocheza dhidi ya timu hizo kwenye mechi za ligi akiwa kama kocha.

Lakini tunatakiwa tuelewe kwamba, Mkwasa siyo nabii hivyo hawezi kuyabadili haya yanayotokea hii leo kwa siku moja. Anahitaji muda wa kutosha na ushirikiano mkubwa kutoka TFF na wadau wengine wa soka ili kuweza kupata kile ambacho watu wengi wamekuwa wakikitamani lakini mwisho wa yote wamekuwa wakiishia kwenye maumivu.

Tumekuwa na makocha wengi wa kigeni ‘wazungu’ lakini bado hatujafika popote wala hata nusu ya pale tunapopataka, nikisema hivyo sina maana nawabeza makocha wa kigeni waliowahi kuinoa Stars. Ila naangalia kama walifikia malengo ambayo tumekuwa tukitaka kuyaona kwenye soka letu la Tanzania, kama nao wamekuwa wanakuja wanalipwa mamilioni ya fedha lakini bado wameshindwa kutupeleka pale tunapopataka basi sioni ulazima wa wao kuja.

Kumwamini kocha mzawa na kumpa timu sio dhambi wala si ujinga, kama atapata ushirikiano wa kutosha kama wanaopewa makocha wa kizungu naamini mzawa anaweza akatusaidia kuliko hata hawa makocha wa kigeni ambao kila kukicha wanaichukua timu hakuna wanachokifanya mwisho wa siku tunaishia kuwatimu na kuwalipa pesa nyingi wanatokomea na kuiacha timu ikiwa kwenye hali mbaya.

Mwarobaini wa taizo letu sio makocha wa kigeni hapo naomba tuelewane, hata kama tutamchukua Sir Alex Ferguson, Jose Mourinho, au Pep Guadiola bado tatizo litabaki palepale kwasababu tatizo letu sisi sio kocha. Tatizo linalolitafuna soka la Tanzania ni mfumo wazungu wao wanaita ‘system’, hapa ndipo imelala mizizi ya matatizo yote yanayolitafuna soka la bongo.

Sasa inabidi kuichimbua mizizi hiyo ili siku moja na sisi tufurahie matunda ya soka kama nchi nyingine ndogo za Afrika ambazo zimethubutu lakini sisi kila kukicha bado tunapiga mark time palepale. Mfano mzuri ni Botswana hawa jamaa waliopata umaarufu kwa ngoma ya ‘makhirikhiri’ walishiriki michuano ya AFCON sisi tukiwa watazamaji kwenye TV zetu. Nchi nyingine ni Burkina Faso wale ambao Erasto Nyoni aliwafunga goli wakiwa kwao baada ya kutoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam, nao pia walifuzu kucheza AFCON sisi tukawa watazamaji tu.

Sasa ifike wakati tujifunze kukubali vyetu, hebu tumpe huyu mzalendo hii timu wakati sisi tukiangalia tunaanzia wapi kuichimba hii mizizi yetu ya mfumo mbovu ambao unalitesa na kuligaragza soka letu kila kukicha. Ninaposema timu apewe Mkwasa sio kwamba nampigia debe la hasha, ila ukiangalia kwa makocha wazalendo waliopo hapa Tanzania wenye leseni kama ya Mkwasa na wanafanya kazi basi utaungana na mimi kuomba timu hii apewe Mkwasa mbali ya kuwa na leseni ya daraja la juu.

Mfano mzuri ni yule kocha wa timu ya wanawake ‘Twiga Stars’ Rogasian Kaijage, ameweza kuivusha na kuipeleka kwenye michuano ya All Africa Game itakayopigwa Congo Brazzaville. Angalia mazingira anayofanyia kazi, wachezaji alionao na ushirikiano anaopewa kwenye ile timu hapo utajua kuwa hata hawa wazalendo wanajua ila basi sisi tuna kasumba ya kuwadharau na kutukuza hao makocha tunaowaamini kuwa watatufikisha tunapotaka.

Kwasasa Stars ipo kwenye wakati mgumu sana hasa wachezaji wake wanaokipiga kwenye timu hiyo, wameshapoteza mechi tano mfululizo na hiyo inawaondolea hali ya kujiamini pindi wawapo uwanjani. Wakishatanguliwa kufungwa wanakata tamaa wakijua yaliyowakuta kwenye mchezo uliopita yanajiudia tena kwenye mchezo ambao wanacheza kwa wakati huo. Ukijumlisha na mashabiki wao kuwazomea hapo ndio mambo yanakuwa magumu kwao kwani wanakuwa wanacheza kwa presha ya kutaka kuwaridhisha mashabiki.

Endapo tutampa timu Mkwasa, basi tumuache afanye kile ambacho anaona ni sawa kwa yeye kukifanya kwa wakati huo. Tusimpe presha kubwa bali tumuamini, tumpe ushirikiano na kuheshimu yale yote atakayokuwa akiyafanya kwenye kikosi hicho akiamini yataleta mafanikio. Kweli tupo kwenye wakati mgumu lakini tunatakiwa kuwa wavumilivu kwenye hili hasa kwa kipindi hiki cha mpito tulichopo wakati huu

Davido Achezea Akili za Watanzania.kwa Kuwatubeep Kwa Bendera..Ugomvi wa WEMA SEPETU na Diamond Platnumz ni Faida Kwake TUZO za MTV 2015

$
0
0
Ukitaka kujua kuna watu hawana kazi ya kufanya utaangalia tofauti ya comment za kwenye post ya Davido kwenye instagram. Kawaida huwa anapata comment 100 hadi 200. Lakini post hii ambayo aliyoweka picha ya bendera ya Tanzania imepata zaidi ya comment 2600 ndani ya masaa 4.

Ukiangalia comment zimejaa za wa Tanzania waki-comment ujinga kumpa support na wachache wakiongea vitu vya msingi. Hapa ni hivi, kuna kundi la watu wanaongoza kampeni za kumpigia kura Davido kwenye vipengele vya MTV Awards ambapo Davido yupo na Diamond...Kisa cha Watu kumpigia Kura Davido Kinatokana na Ugomvi wa Diamond na Wema Sepetu Ambao walikuwa ni Wapenzi zamani...Wema Sepetu na Team yake ndio vinara wa kuwashawishi watu wampigie kura Davido Badala ya Diamond..

Sasa inavyoonekana Davido alipata hizo taarifa na kutumia advantage kwa ku-post bendera ya Tanzania na kuweka alama ya love. Basi kawateka wote wasio na kazi wanaanza kupoteza muda wao. Wengine wanasema Davido ka-show love tu kwa Tanzania. Anaanzaje kutoa love bila sababu ya msingi.

Ishu za kitaifa tuache team zisizokuwa na msingi na tutumie bundle zetu vizuri kama sio kujifunza mambo ya msingi basi kuwa support ndugu zetu wanaotuwakilisha sio strangers. Hizi ni baadhi ya comments na nyingine ni nzuri ila nyingine utashangaa kama kweli hawa ni watanzania au wahamiaji tu.



Winger mpya wa Man United ajiweka karibu na ex wa Chris Brown, Karrueche Tran

$
0
0
Memphis Depay si jina geni hasa kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United. Ni mchezaji mpya aliyesajiliwa majira haya ya joto hivi.

Mchezaji huyo ameonekana akiwa karibu na aliyekuwa mpenzi wake na Chris Brown, Karrueche Tran. Wameonekana kwenye picha waliyopiga pamoja walipokutana huko Miami.

Depay anatarajiwa kujiunga rasmi na timu yake mpya mapema mwezi ujao.

Kupitia Instagram, mchezaji huyo alipost picha hiyo na Karruache na hakuandika caption yoyote. Mashabiki wengi wameonekana kuipenda japo wamemuonya juu ya Chris Brown.
Viewing all 104743 articles
Browse latest View live




Latest Images