Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Video ya Interview ya Wema Sepetu Kuhusu Mtoto na Diamond, Mimba ya Zari na Alivyotoa Mimba

$
0
0
'Kukosa mtoto wakwangu inaniuma naishia kupenda watoto wa watu'- Wema

Hii  ni Part iv  ya Wema Sepetu aliyofanya katika kipindi cha Take One na Zamaradi , kafunguka mambo mengi na kumuongelea Zari .

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne Ya Tarehe 23 Juni 2015

$
0
0





















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumanne  Ya  Tarehe  23  Juni 2015

Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) lamteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti mpya

$
0
0
Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limemteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti Mpya wa muda.

Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.

Wema:Jamani Nikiwa Bungeni Sitaongea Hivyo na Kuropoka Kama Wengi Wanavyodai

$
0
0
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalumu Singida,amesema anafurahishwa na kitendo cha mashabiki wake kumwigiza sauti akiwa bungeni kwa  kuwa wameonyesha kumkubali kabla hajafika ‘Mjengoni’.

Alisema sauti hiyo inayomuigiza alitumiwa kupitia simu yake na haikumkwaza zaidi ya kufurahia  kwamba watu wengi wanakubali awe bungeni.


  • “Nafurahi kwa kuwa wengi wameshanipeleka bungeni wakati mimi ndiyo kwanza nipo katika harakati  za kuomba kuchaguliwa kupitia umoja wa wanawake Singida , lakini nafurahia kwa kuwa inaonyesha wengi wananikubali,  ila nikipitishwa kuwawakilisha wana Singida bungeni sitaongea kama walivyonirekodi katika sauti hiyo,” alisema Wema kwa furaha.


Aunty Ezekiel: Sipendi Mwanangu Awe Mwigizaji Nataka Asome Sana

$
0
0
Staa wa Bongo Movie,Aunty Ezekiel amefunguka kuwa hapendi mtoto wake aliyejifungua hivi karibuni aitwaye Cookie,awe mwigizaji wa filamu kama yeye.

Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa atakachofanya kama mzazi anataka mtoto wake asome na kama akiwa mwigizaji basi iwe kama kazi yake ya ziada siyo anayoitegemea kwenye maisha yake.


  • ‘’Binafsi sipendi mwanangu awe mwigizaji kama mimi,na siyo lazima kama mimi mama yake niwe mwigizaji na yeye awe hivyo kuna kazi nyingi ila ninachotaka asome sana na kama atataka kuwa msanii basi iwe kazi yake ya pili siyo aitegeeme katika maisha yake,’alisema Aunty.



  • ‘’Hata mimi pamoja na kwamba ni mwigizaji lakini siitegemei sana kazi hiyo nina kazi zingine nafanya,’’aliongezea Aunty.

Diamond Asitisha Kupokea Maombi ya collabo za Wasanii wa Nigeria

$
0
0
Diamond Platnumz sasa ni ‘hotcake’ kiasi cha kuwafanya wasanii wengi wa Afrika kutamani kufanya naye collabo, lakini kwa uamuzi mpya alioupitisha wasanii wa Nigeria ambao hawajafanikiwa kufanya nae wataikosa nafasi hiyo.

Platnumz ambaye Jumamosi iliyopita pamoja na msanii wa Afrika Kusini, Donald wameshoot video ya collabo yao mpya, amesema kwa sasa amefunga milango ya kupokea collabo za wasanii wa Nigeria. Hii inamaanisha zile collabo za wasanii wanaomuomba yeye afanye nao.


  • “Sababu ya kusimamisha kwa sasa isiwe too much too much “ amesema Diamond kupitia 255 ya Clouds Fm. “ kwasababu mwanzo tulikuwa tunafanya collabo na watu kwasababu ya kutafuta tobo la kuingia Nigeria, tumeishaingia vizuri Nigeria tunakubalika tunafahamika na nyimbo zetu zinafanya vizuri hata tukitoa nyimbo ambazo tunatoa wenyewe tu zinahit, mfano kama Nasema Nawe navyokwambia sasa hivi inafanya vizuri Nigeria, so inakuwa haina maana kila mtu akushirikishe shirikishe unakuwa hauna umuhimu, zimebaki tu baadhi ya collabo za ambazo za wasanii wanaofanya vizuri zitatoka baadae lakini sio kwasasa hivi kwani tumezisimamisha, kwani tumekuwa tukiombwa sana sana sana na wasanii wa Kinigeria kufanya collabo tumesimamisha.”


Diamond ameongeza kuwa collabo ya mwisho kutoka Nigeria ni ile ya Kcee na yeye iliyotoka hivi karibuni, ambayo wanatarajia kuifanyia video nchini Afrika Kusini.


  • “katika nyimbo ambazo tumeshirikishwa itakuwa ya mwisho hii tumefanya na Kcee kwa sasa ambayo kuanzia kesho tunaanza kushoot video yake ambayo inafanyika hapa hapa South Africa, ilitakiwa tushoot Mozambique lakini kwasababu nina issue za kifamilia hapa South Africa imeshindikana kwenda Mozambique imebidi nimwambie inabidi tushoot hapa hapa.”


Hata hivyo Diamond amesema miongoni mwa wasanii wengine wa Afrika ambao wametuma maombi ya kufanya naye collabo ni pamoja na Ferré Gola pamoja na kundi la Too Fan la Togo.

Steve Nyerere: Kero za Kinondoni zimenifanya nigombee Ubunge

$
0
0
Msanii wa filamu za Kibongo,Steve Mengere’Nyerere’ hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea ubunge kupitia jimbo la Kinondoni.

Aidha Steve alisema kuwa Kinondoni ndipo alipozaliwa na kukulia na anajua changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo ambazo ni wakati wa mvua wananchi hukubwa na mafuriko lakini hakuna kiongozi aliyeweza kutatua tatizo hilo.

Pia aliongeza kuwa mikopo midogo midogo kwa kina mama na ajira kwa vijana,ongezeko la ada mashuleni ,kero ya uchafu ,tiba kwa akina mama wajamzito ambapo kwa sasa hivi mama mjamazito mzazi anapoenda kujifungua anaambiwa aende na pamba, mkasi n.k, vitanda kuwa vichache kwenye wodi zote. Gari la wagonjwa ni mmoja tu.

Nape: CCM itashinda tu hata kwa goli la mkono

$
0
0
CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani hapa.

Neno “bao la mkono” hutumiwa kama goli lililofungwa kwa kuupiga mpira kwa mkono kinyume cha taratibu za mpira, lakini hukubaliwa kwa kuwa mwamuzi anakuwa hajaona kitendo hicho.

“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape.

Nape, aliye kwenye ziara ya katibu mkuu wa CCM, aliwataka wananchi wa Sengerema kusubiri ushindi wa chama hicho na kuwakumbusha kuwa wanapaswa kuiweka CCM kuanzia udiwani mpaka ubunge kwa nafasi ya urais tayari kuna uhakika.

Katika mkutano huo, Nape alisema ana uhakika CCM itashinda baada ya kushuhudia mwitikio wa Watanzania tangu alipoanza kuongozana na Kinana katika ziara zake za kuizunguka nchi na kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao.

Amebainisha kuwa amejifunza na kujiridhisha kuwa chama chake bado kinapendwa miongoni mwa wapigakura waliofikiwa tofauti na vyama vya upinzani.

“Tumefika maeneo mengi ambayo upinzani haujafika. Huko tuna hazina kubwa ya wanachama. Hakuna namna Ukawa wanaweza kuingia Ikulu mwaka huu,” alisisitiza.

Wapinzani waja juu
Kauli hiyo ya Nape ilipingwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani waliosema kuwa mtendaji huyo anamaanisha kuwa CCM itaiba kura.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakutaka kabisa kuzungumzia kauli ya Nape zaidi ya kusema watakutana Oktoba.

“Kwa bahati mbaya kauli za Nape siwezi kuzijibu. Kauli za Nape zichukue kama zilivyo, ingekuwa ni (katibu mkuu wa CCM, Abdulraham) Kinana, ningemjibu lakini ajue kuwa tutakutana Oktoba,” alisema Dk Slaa alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo.

Naibu mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema kauli ya Nape inamaanisha kuwa CCM itaiba kura kwani kwa kawaida bao la mkono ni bao haramu.

“Kauli hiyo inaonyesha dhahiri kuwa wataiba kura na kwa sababu katiba yetu ni mbovu matokeo yake yatatangazwa kama yalivyo… hiyo ndiyo maana ya bao la mkono,” alisema.

Kambaya alisema hata hivyo CCM isijiaminishe kwa lolote kwani hivi sasa wananchi wamebadilika kimtazamo kutokana na matatizo mengi yanayoiandama nchi kama vile afya, elimu duni na migogoro ya ardhi.

“Lakini CCM wajue kuwa kutatokea machafuko makubwa iwapo wamejipanga kuingia Ikulu kwa njia hiyo ya bao la mkono. Kauli ya Nape ni ya kidikteta na inaonyesha dhahiri kuwa wamejikita kwenye utawala wa mabavu,” alisema.

Kadhalika Kambaya alisema CUF imeshajipanga na kuhakikisha inaziba mianya yoyote ya wizi wa kura kuanzia kwenye Daftari la Wapigakura hadi katika ujanja wa kuwapigisha kura marehemu, askari na wanajeshi kama inavyodaiwa kufanyika Zanzibar.

Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema Nape anatoa maneno ya kuvutia kwake kama njia ya kuwakatisha tamaa wapinzani na wanachama, hata hivyo alimuonya kuwa siasa za sasa hazitabiriki kwa njia hiyo.

“Lakini ajue kuwa mambo yanabadilika. Anaweza kushangaa mambo yakawa mengine, sasa hivi wananchi wana mwamko mkubwa na wanabadilika,” alisema.

Alisema CCM haina haja ya kujitapa kwa sasa wakati bado haijapata mgombea kwani huenda wakapata ambaye wananchi hawatamuunga mkono hata kidogo.

“Bado CCM wana makundi jambo ambalo kwao ni udhaifu. Lakini pia lazima wajue kuwa wakati wa mchujo utakapofika, wale watakaokatwa hawatafurahia kuachwa na hapo kuna sababu za wapinzani kushinda,”alisema.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wakati Nape anabishana kwenye majukwaa, NCCR inaendelea kupiga kazi.

“Badala ya kujadili hoja za msingi zenye manufaa kwa wananchi yeye anajadili CCM kupiga bao?” alihoji Mbatia.

Akijibu hoja ya Nape, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikaria alisema kauli ya kada huyo imekaa kisiasa na si kiuhalisia kwani ni kawaida kwa chama cha siasa kujiaminisha kuwa kitashika dola.

“Unajua chama chochote hata kiwe kidogo lazima kikiri kuwa kitashika dola ili mradi ilani yao inakubalika na unakubaliwa na wananchi kwa sababu chama chochote nia yake ni kuingia ikulu,” alisema.

Alisema hata vyama vidogo kama TLP hukiri ushindi kwa kusema kuwa vinataka kuingia ikulu kwa sababu chama hakiwezi kukiri mbele ya wananchi kuwa hakitashinda.

"I Get Kichefuchefu When I Hear Diamond Platnumz' Name."...Ali Kiba

$
0
0
Ali Kiba says he deserved all awards he scooped at the recently concluded Kili Music Awards 2015 contrary to what some people say that he didn't deserve all 5 awards including entertainer of the year.

 Kiba said he had all criteria to win and he is now well prepared to fight with anyone who thinks he is the real King of Bongofleva

And when the paparazzi mentioned Diamond Platnumz name Kiba didn't look impressed at all and quickly he said he gets nausea(kichefuchefu) whenever and wherever he hears Diamond's name

"Bro. I don't want to hear that name(Diamond), I get nausea(kichefuchefu), you know when I quit the game for a sometime I was just reviewing it but no one managed to be on my chair, and I decided to have a great comeback and from now there is no looking back" said Ali Kiba

He added by saying "I don't mean there isn't best artist like me, don't understand me badly, there are best artists but not that young man(Diamond), music is more than fanfare(mbwembwe), I'm working and I mean it now. If he believes he is fit, works  will give the truth but not childish dramas "

Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi aliyoifungua Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ dhidi ya mkewe wa zamani

$
0
0
Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi aliyoifungua Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ dhidi ya mkewe wa zamani ikitokea Mahakamani Manzese Dar es salaam kuhusu mke wake wa zamani.

Taarifa inasema Mahakama ya Manzese imeamuru Mbunge Joseph Mbilinyi akabidhiwe mtoto wao kutokana na kesi aliyoifungua dhidi ya mke wake huyu akidai anamuharibu mtoto.

Hii habari imekuja siku kadhaa tu baada ya TUZO ZA KILI 2015 ambapo mke huyu wa zamani aliingia kwenye headlines kutokana na vazi alilokuwa amevaa.

Baada ya Sugu Kushinda Kesi,Faiza Asema Bora Kufa Kuliko Kumuona Sasha Akilelewa na Mama Mwingine

$
0
0
Baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi mahakamani ya kutaka apewe amlee mtoto wake aitwaye Sasha,aliyekuwa mzazi mwanzake,Faiza Ally amefunguka kuwa ni bora kufa kuliko kumuona mtoto wake akilelewa na mama mwingine wakati yeye yupo hai.

Sugu alimfikisha mahamakani mzazi mwenziye kwa madai kuwa ameshindwa kumlea mtoto wao kwa kuwa mama huyo si mwadilifu.

Faiza ameandika hivi kupitia Akaunti ya Instagram:

Sielewi joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonya mtoto wangu- mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana – na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili- sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana !

Sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili- mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu- nina ndoto na mwanangu nyingi sana – nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea- naona uchungu sana kupelekea mahakani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .

Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe- ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamia na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba Sasha.

Sifurahishwi na uadui wa team za mitandaoni lakini sina nguvu ya kuzuia – Alikiba

$
0
0
Alikiba amekiri kutofurahishwa na uhasama unaondelea kati ya mashabiki wake na mashabiki wa Diamond Platnumz kwenye mitandao ya kijamii japo amesema hana uwezo wa kuzuia hali hiyo.


  • “Unajua sisi ni vioo vya jamii na tunapendwa na watu wengi sasa unapoona mambo yanatokea kama hivyo huwezi kufanya chochote na mimi siwezi kuingilia suala lolote la mashabiki,” Alikiba amekiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.



  • “Lakini kiukweli sifurahishwi nalo kama kuna uwezekano wangeacha tu. Kiukweli tusupport vya kwetu ili tuwende kwenda mbele.”

Mjamzito Afanyiwa Ukatili wa Kutisha: Alifika Hospitali Akiwa na Uchungu, Wauguzi Wakamfukuza.......Dakika Chache Baadae Akajifungulia Bafuni

$
0
0
MJAMZITO aliyefahamika kwa jina la Rotha Bujiku, amejifungulia bafuni karibu na zahanati ya kijiji baada ya kudaiwa kufukuzwa na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo, kwa maelezo kuwa anajifungua kila mwaka.

Tukio hilo lilitokea wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu majira ya saa 2 asubuhi baada ya mjamzito huyo kufika katika zahanati hiyo kwa lengo la kupata huduma ya kujifungulia kwa wataalamu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililovuta umati wa watu, mjamzito huyo alikataliwa kupokewa na muuguzi wa zamu aliyetajwa kwa jina la Constansia John.

Ilielezwa kuwa muuguzi huyo alikataa kumpokea kwa madai kuwa mjamzito huyo alishapewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa akajifungue katika hospitali ya wilaya ya Maswa kwani amekuwa akizaa watoto kwa mfululizo.

Inaelezwa kwamba, wakati Rotha akiugulia maumivu ya uchungu, muuguzi huyo alimpigia simu ya mkononi Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Leticia Kachumi kumjulisha hali hiyo na alipofika alitaka mjamzito huyo aondoke katika eneo hilo na atafute usafiri ili aweze kufika katika hospitali ya wilaya kama alivyoelekezwa katika siku za nyuma.

“Leticia alipofika hapo zahanati baada ya kupigiwa simu na Constansia, licha ya kumuona anaendelea kulalamika kutokana na uchungu alimwamuru aondoke eneo hilo mara moja na atafute usafiri wa kumfikisha hospitali ya wilaya iliyoko umbali wa kilomita 36, kwani walishamweleza kuwa amekuwa akizaa mfululizo na hiyo ni mimba ya kumi na moja,” alisema shuhuda, Kundi Mageni.

Kutokana na hali hiyo, mjamzito huyo alilazimika kuondoka zahanati hapo bila msaada wowote na baada kufika karibu na nyumba iliyoko na zahanati hiyo, alikwenda katika bafu la nyumba ya jirani ambalo halina sakafu na kujifungulia humo na baadaye kusaidiwa na wasamaria wema waliosikia sauti ya mtoto.

“Kwa kweli huyu mama amejifungulia katika mazingira machafu na hatarishi kwa afya yake na mtoto aliyemzaa. Kwa kweli hili ni tukio la kusikitisha. Huwezi kuamini wauuguzi hao ambao ni wanawake kumtendea mwenzao ukatili wa kiasi hiki,” alisema Pili Kidesela, Diwani wa kata ya Shishiyu (CCM).

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Jonathan Budenu aliyefika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo, alisema kitendo kilichofanywa na wauguzi hao ni kinyume cha maadili ya kazi yao na hivyo ni lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote waliohusika.

Mwingine ajifungulia kichakani
Wakati hayo yakitokea Maswa, mkoani Arusha binti mwenye umri wa miaka 17 alijikuta akijifungulia kichakani baada ya kuzidiwa uchungu wakati akisubiri kuombewa kwenye mkutano wa dini uliofanyika Viwanja vya Magereza, Kisongo nje kidogo na Jiji la Arusha.

Anna Ngitoria, mkazi wa Endurimeti, wilayani Arumeru, alikuwa miongoni mwa mamia ya wakazi wa Arusha, Kilimanjaro na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja huo wa magereza kwa ajili ya kile kilichodaiwa kuwa ni maombi yaliyoandaliwa na kituo kimoja cha redio cha jijini Arusha, Radio Safina.

Kwa kawaida uongozi wa kituo hicho huandaa makongamano ya kila mwezi kwenye uwanja huo wa Kisongo na kujumuisha mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni wanawake na wasichana ambao hupendelea kuhudhuria maombezi hayo kwa matarajio tofauti.

Mikusanyiko ya maombi ya ‘Radio Safina’ imekuwa ikikusanya watu wengi mithili ya ‘Kikombe cha Babu,’ ambacho nacho kilivuma sana miaka mitatu iliyopita na tukio la msichana huyo kujifungua katika moja ya matukio hayo kimezua hisia tofauti mjini hapa.

Akizungumza katika hospitali ya Mount Meru ambapo amelazwa kwa sasa, binti huyo, Anna amekiri kuwa alijifungua kabla ya wakati kwa sababu alikuwa na ujauzito wa miezi saba tu.

Mtoto wake njiti sasa anahudumiwa katika wodi maalumu iliyopo hospitalini hapo na wauguzi wanasema anaendelea vizuri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 24 Juni 2015

$
0
0



















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumatano  ya  Tarehe  24  Juni  2015

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limemteua Charles Boniface Mkwassa, kuwa kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania(Taifa Stars)

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.

“Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.

Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.

Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana.

TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.

Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki.

Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.

Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.

Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.

Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi.

Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”

Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.

U15 Yaingia  Kambini
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.

Kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.

U15 ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.

NB: Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.

Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Sauti Sol waonesha mfano kwa kum-support Diamond kwenye tuzo za MTV MAMA 2015

$
0
0
Kundi la Sauti Sol kutoka Kenya ambalo linaiwakilisha Afrika Mashariki kwenye BET Awards 2015 zinazotarajiwa kutolewa Jumapili hii June 28 nchini Marekani, wameonesha mfano unaopaswa kuigwa na wasanii pamoja na mashabiki wa muziki wa Tanzania kuwaunga mkono wasanii wetu wanaowania tuzo za kimataifa.

Kupitia akaunti yao ya Instagram Sauti Sol wameutambua uwakilishi wa Diamond katika tuzo za BET za mwaka jana, na kumpigia kampeni ya kupigiwa kura kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 ambapo anawania tuzo tatu.

“Mwaka jana ni @diamondplatnumz ndiye aliyetuwakilisha nchini Marekani kwenye #BETAwards2014 This year we’re so humbled to be the ones representing African music at @bet_intl @bet_africa #Betawards2015 on 28th June at the Nokia Theatre, LA. Shukran sana kwa sapoti aliyetuonyesha. Je, wamkubali? Haiya basi, check link kwenye bio ya @wcb_wasafi kisha umpigie kura #BestMale As many times as you possibly can, ni wakati wa Afrika mashariki”

Endelea kuwapigia kura Diamond na Vanessa wanaoiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu. Diamond anashindania vipengele vitatu, Best Male, Best Collaboration na Best Live. Vee Money anawania kipengele kimoja cha Best Female.

Ingia hapa uweze kuwapigia kura mara nyingi uwezevyo.

Watanzania tuungane kuwapigia kura wasanii wote wanaotajwa kuwania tuzo za kimataifa ili kusaidia kuukuza muziki wa nyumbani.

Sugu ashinda kesi dhidi ya mama mtoto wake Faiza, mahakama yaamua apewe mtoto

$
0
0
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshinda kesi aliyomfungulia aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto wake wa kike aitwaye Sasha.

Kwa mujibu wa maelezo ya Faiza kupitia akaunti yake ya Instagram, mahakama imetoa hukumu ambayo ni mtoto achukuliwe na kulelewa na baba yake mzazi.

Sugu alimshitaki Faiza kwa madai kuwa hana maadili na ana hofia kuwa atamharibu mtoto wao, hivyo alitaka kumchukua mtoto kutoka kwa mama yake aishi naye.


Hiki ndicho amekiandika Faiza baada ya hukumu kutolewa:
“Sielewi Joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonywa mtoto wangu,mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana, na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili.

"Sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana ! sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili.

"Mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu.
 
"Nina ndoto na mwanangu nyingi sana , nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea.

"Naona uchungu sana kupelekwa mahakamani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .
 
"Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamie na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba sasha …..”

Menejiment ya Ali Kiba, yaiba Nyimbo za Diamond na kuziuza iTunes..Meneja wa Diamond Platnumz Awachoma iTunes

$
0
0
Wakuu nimeona instagram meneja wa Diamond anaeitwa Salaam akilalamika wizi unaofanywa na menejiment ya King Kiba kuuza nyimbo za Diamond kwenye mtandao wa iTunes bila makubaliano yoyote.

Rockstar ndio kampuni inayomsimamia Kiba na ndio inauza nyimbo za Diamond kwa wizi.



@iTunes the company below as #Rockstar4000 
who act as they have license to sell the songs
of my artist diamond platnumz on @iTunes they
are THIEVES. They don't have any contract or
any relationship with us this is Unacceptable to
let companies sell
contents of the Artists without any agreement
both sides. PLEASE
REPOST Wizi kwa Wasanii wetu HAUKUBALIKI.
Naomba hii Kampuni
ya Rockstar4000 iachane na Wizi wake wa kuuza
kazi za @ diamondplatnumz hatuna makubaliano
yoyote na kampuni yako kuuza Nyimbo za
diamondplatnumz Tutakutana Mahakamani.
Uvumilivu umetushinda.

NUHU MZIWANDA Awaka Elimu yake na Matokea yake ya Form 4 Hadharani..'Ninavyokosea Kiingereza sio Kwamba Napenda, ni Shule Hamna’

$
0
0
Huwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye maisha.

Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole.

Nuhu ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki’

‘Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh



Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia.... ‘Kupata Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa, ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza sio kwamba napenda, ni shule hamna

Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule.

Mange Kimambi Aonyesha Uzalendo..Ampigia Kura Diamond Platnumz MTV Awards na Kisha Kusema Haya

$
0
0
Guys, acheni haya mambo jamani…. Mnaenda too far with this jamani… Tunajiaibisha sana watanzania… Busy kwenye ma insta page ya wanaigeria. English zeneyewe hamjui mnaishia kuchambwa na wanaigeria…

Yani tunazidi onekana mabolizozo….. Jamani kweli mnaenda kujipendekeza kwa wanaigeria hivyo..AIBUUUU

Kuweni wazalendo jamani. Diamond hayuko huko kama Diamond ,He is there carrying our flag. Yuko hapo kama Diamond from Tanzania.

Jamani naomba msome hapo pameandikwaje chini ya jina la Diamond? TANZANIA…

Hivi Diamond kaua mtoto wa nani mpaka tuko tayari kuididmiza nchi yetu sababu yake??? Yani huwezi kudharau maujinga yake ukampigia kura sababu ya Tanzania.AIBUUU

You know what, naipenda Tanzania kwanza so no matter Diamond kafanya nini nimemvotia Diamond mpaka vidole vimeumaaaa….

Na kesho nikiamika namvotiaaa…Bado sijamvotia Davido aiseeeeee…..Sio kwamba simkubali ila sio mbele ya mtanzania mwenzangu…

Hivi Diamond kuna alofanya kubwa sana mpaka tumchukie hivi jamani??? Its true dogo anazingua kishenzi ila sio kiasi cha kumchukia hivi….

Mie naomba tumvotie then awards zikiisha turudi kumchukia……hahahaha. Tena na swaumu itakuwa imekwisha na posti zake na Zari zinaanza tena…hahahahahhahaa.. I enjoy hating on those 2….hahhahahhahahahhahahaah ah……

Ila kusema ukweli sina chuki serious hivyo na Diamond kha!!! Mpaka nikamvotie mnaigeria jamani….Na kwenye best collabo nimepiga kura pia mpaka vidole vimeota suguuuuuuuu…..Hahahaha…

Haya twende na wewe kampigie kura Diamond…… Akishachukua hizo awards ndo turudi kwenye team zetu for now tuungane plsssss….

Yani jamani ni ujingaaaaa, hivi unajua siamini hii kitu ya Diamond, Zari na Wema imekuwa bonge la issue hivi…Dah…..

Im sure management yake watamrekebisha baada ya haya majanga yaliyotokea lately…Ila pls mvotieni..

Source: U-Turn
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images